Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (11)

Kwenye mkutano uliopita, tulifanya ushirika juu ya kipengele cha tisa cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi: “Kuwasiliana kwa usahihi, kutoa, na kutekeleza mipango mbalimbali ya kazi ya nyumba ya Mungu kulingana na mahitaji yake, ukitoa mwongozo, usimamizi, na himizo, na kukagua na kufuatilia hali ya utekelezaji wake.” Tulifanya ushirika juu ya majukumu ambayo viongozi na wafanyakazi sharti wafanikishe na kazi ambayo ni lazima wafanye, na vilevile tulichanganua baadhi ya tabia za viongozi wa uongo. Ingawa hatukufanya ushirika juu ya mambo mahususi ya namna viongozi na wafanyakazi wanavyopaswa kutekeleza kila mojawapo ya mipangilio ya kazi, tulifanya ushirika juu ya mambo mahususi ya kanuni za utekelezaji wa mipango hiyo, na vilevile kile ambacho viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya. Je, mumeweza kupata ufafanuzi maalum zaidi na sahihi wa kazi ambayo viongozi na wafanyakazi wanastahili kuifanya kupitia katika ushirika wetu juu ya kipengele cha tisa? Je, sasa mko wazi kuhusu ni kazi ipi ambayo viongozi na wafanyakazi wanastahili kufanya? Jambo la muhimu kwao ni kutekeleza kazi kulingana na matakwa ya Mungu na mipango ya kazi ya nyumba Yake. Hilo ndilo linalohitajika kimsingi. Sasa, sote tunaelewa. Kazi ambayo kiongozi au mfanyakazi lazima afanye ndani ya nyumba ya Mungu, na majukumu yake ni yapi, yote yamefanyiwa ushirika kwa mahususi sana katika kipengee cha tisa. Ni pana kimsingi. Mawanda ya majukumu yao hayajawekewa mipaka, na kazi ambayo wanapaswa kufanya, pamoja na jinsi ambavyo wanapaswa kuifanya, vyote vimetajwa kwa uwazi pia. Kama mtu bado hajui jinsi ya kufanya kazi halisi sasa baada ya kutajwa kwa dhahiri, hilo ni tatizo la mtu huyo kuwa na ubora duni wa tabia. Yeye ni aina ya kiongozi wa uongo asiyeweza kufanya kazi. Kuna aina nyingine ya kiongozi wa uongo ambaye hupanga kazi kulingana na mawazo na fikira zake tu, na yeye huwatumia watu bila mpangilio, akisababisha kisa cha wapishi wengi sana. Mbali na kazi hiyo kutofanywa vizuri—yeye pia huiharibu kabisa, na kuiacha bila namna ya kuendelea. Viongozi wa uongo hawatawahi kutekeleza mipango ya kazi, sembuse kufanya kazi halisi. Wao hufanya tu kazi wanayoipenda, wakitilia mkazo ile kazi ya mambo ya jumla; wanapofanya kazi, wao hujua tu jinsi ya kutoa amri na kupaza sauti kubwa wakisema kauli za kuvutia na mafundisho yasiyo na maana. Kamwe wao hawafuatilii kazi, wala hawajali iwapo imekuwa ya ufanisi. Hii ni aina moja ya kiongozi wa uongo. Kwa ufupi, iwe kwamba mtu hawezi kufanya kazi halisi au hafanyi kazi halisi kama kiongozi—hata hali iweje—kama hawezi kufanikisha majukumu ya viongozi na wafanyakazi au kufanya kazi ya agizo la Mungu, na kama hawezi kutimiza vipengele mbalimbali vya kazi vilivyopangwa na nyumba ya Mungu, basi yeye ni kiongozi wa uongo.

Sasa, kupitia katika ushirika wetu juu ya majukumu tisa ya viongozi na wafanyakazi na ufichuzi wetu wa namna mbalimbali ambazo viongozi wa uongo hujionyesha, je, mmepata maarifa na ufahamu wa msingi wa jinsi ya kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi? (Ndiyo.) Je, hivyo basi mnaiona kazi ya nyumba ya Mungu ikiwa rahisi kufanya? Je, mahitaji ya mwanadamu ni ya juu? Je, ni yenye kuzidi? (Si ya juu; yote ni mahitaji tunayoweza kutimiza.) Je, kuna viongozi na wafanyakazi ambao husema, “Kuna vipengele vingi sana na aina nyingi sana za kazi ambazo nyumba ya Mungu inatuhitaji tufanye. Kadiri kiongozi anavyokuwa juu, ndivyo mawanda ya kazi yake yanavyoongezeka, na ndivyo anavyowajibikia vipengele vingi zaidi vya kazi. Kufanya kazi hiyo vizuri na kuona ikitekelezwa kulingana na mahitaji ya Aliye juu—tunaweza kufa kwa ajili ya uchovu, sivyo?” Je, kuna yeyote aliyeanguka kwa kufanya kazi yoyote ya kuonekana, kwa sababu ya kila kipengele cha kazi hadi mahali inapostahili kuwa? (Hapana.) Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwa mgonjwa kwa ajili ya uchovu? Je, kuna mtu yeyote ambaye ana shughuli nyingi sana kiasi kwamba hana muda wa kula au kulala? (Hapana.) Wengine wanaweza kusema, “Unamaanisha nini ukisema hapana? Kuna watu ambao huchoka wanapofanya kazi za kanisa, kwa kuwa wao hufanua kwa muda mrefu bila kuweza kula kwa ratiba ya kawaida, au kufanya kazi na kupumzika kwa njia iliyodhibitiwa, wakifanya kazi na kupumzika kwa usawa. Wanaishia kuwa wangonjwa kutokana na uchovu.” Je, mumewahi kusikia kuhusu jambo kama hili likitokea? (Hapana.) Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuhisi namna fulani baada ya kusikia kipengele cha tisa na kuona yaliyomo katika vipengele mbalimbali vya kazi katika nyumba ya Mungu, na vilevile viwango vyake vinavyohitajika kwa viongozi na wafanyakazi katika kufanya kazi hii maalum, akihisi woga na hofu? Je, yeye huhisi, “Si rahisi kuwa kiongozi au mfanyakazi. Bila mwili kuwa sana, ubora mzuri wa tabia, moyo mpana, na nguvu na uwezo uzidio uwezo wa binadamu, ni nani angeweza kufanya kazi hiyo vizuri?” Je, kuna yeyote ambaye amwewahi kuwa na wazo hili? Je, ni wazo halali? (Hapana.) Je, ni kitu gani kinachofanya lisiwe halali? Kwanza, wanapokuwa wakifanya kazi ya nyumba ya Mungu, bila kujali cheo chao ni kipi, na kama jukumu lao ni pana au ni la kipengele kimoja cha kazi, viongozi na wafanyakazi lazima angalau wafanye kazi yao ya msingi vizuri, pamoja na kazi moja au mbili za ziada, kwa kiwango cha juu zaidi. Hata kama wamepewa kazi pana, hilo halimaanishi kwamba wanapaswa kutoa ufuatiliaji au mwelekeo wa upana. Ni sharti walenge kuchukua jukumu la kazi muhimu zaidi, au kushughulikia kwa wakati mmoja udhaifu katika kazi fulani. Baadhi ya watu wanaweza kuwa na nguvu nyingi, wana hisia kali ya uwajibikaji, na ubora mzuri wa tabia, na wanaweza kufanya kazi mbalimbali za aina tofautitofauti, lakini kazi yao kuu kimsingi inahusisha kazi moja au mbili tu. Kwa kazi nyingine, wanahitaji tu kuuliza baadaye, waulize kuihusu, na wajaribu kuielewa, na watatue tu matatizo wanapoyagundua. Hiyo ni sehemu ya kazi hiyo. Sehemu nyingine ni kwamba hata kama wanashughulikia vipengele kadhaa vya kazi kwa wakati mmoja, wanahitaji tu wasimamizi wakuu kufanya kazi hizo. Kila wanachofanya ni kusimamia kazi mbalimbali, waziangalie, na kuzielekeza; kazi kuu wanayopaswa kufanya wenyewe bado ni kazi moja. Na, je, mtu anaweza kuchoka kwa kufanya kipengele kimoja cha kazi? (Hapana.) Ikiwa ubora wa tabia wa mtu unatosha na akili yake ni inayobadilika, atapanga kazi ipasavyo kulingana na jinsi muda unavyotengwa na jinsi ya kuifanya iwe na ufanisi. Hatakuwa namna iliyovurugika isiyopangwa, bila njia ya kuendelea mbele. Hawezi kuonekana kuwa mwenye shughuli nyingi—atafanya kazi kulingana na utaratibu uliowekwa—lakini kazi hiyo haitakosa kuwa na ufanisi, na italeta matokeo mazuri. Huyo ni mtu aliye na ubora mzuri wa tabia, anayejua namna ya kutengawafanyakazi na muda wa kazi jinsi inavyostahili. Watu ambao hawana ubora wa tabia au walio na ubora duni wa tabia ni shida, bila kujali kazi yoyote wanayofanya. Wao huwa na shughuli nyingi sana kila siku, lakini kinachowashughulisha, wao wenyewe hawawezi kusema kwa kweli. Hawana ratiba, hawafikirii kuhusu wakati; wanaamka mapema sana na kulala wakiwa wamechelewa; Hawawezi kula katika wakati wa kawaida—lakini kulingana na ufanisi wa kazi, hawafanyi kazi halisi hata kidogo. Je, si hiki ni kisa cha mtu mwenye ubora duni wa tabiaupita kiasi? (Ndiyo.) Mtu wa aina hii huonekana kuwa na shughuli nyingi kila siku bila kupumzika, lakini hawezi kufikia kilele cha kazi, wala hawezi kutofautisha mambo yaliyo ya dharura na kile kinachoweza kungoja, na hana ufanisi katika kutatua matatizo. Hili linapunguza kasi ya kazi. Yeye ana hamu kubwa sana moyoni, na hupata vidonda mdomoni. Hata katika visa hivi, hata hivyo, haanguki kutokana na uchovu. Watu wenye ubora duni wa tabia wanaweza kufanya kazi zaidi ya saa nane kwa siku, lakini ufanisi wa kazi yao ni duni zaidi kuliko ule wa watu walio na ubora mzuri wa tabia. Kwa hivyo, ni lazima wajishughulishe, sivyo? Wanapaswa kujishughulisha—hawawezi kupata matokeo, hata wanapokuwa na shughuli nyingi; wasipoendelea kujishughulisha na shughuli nyingi, kazi inapooza. Huyu ni mtu mwenye ubora duni wa tabia sana kiasi kwamba hana uwezo wa kuwa na uwezo wa kufanya kazi au kuikabili. Zaidi ya hayo, kuna vipengele vingi katika kazi ya nyumba ya Mungu, na mahitaji ni makali kwa namna fulani kulingana na wafanyakazi na wakati. Kwa watu wengi, wanapokuwa na shughuli nyingi kiasi, huwa ni kwa ajili ya kujitahidi kufikia ubora na kupata matokeo mazuri, kwa kuwa kazi ya nyumba ya Mungu iko tofauti na ile ya biashara na viwanda vya ulimwengu usioamini: Hizo huhitaji faida za kiuchumi, ilhali sisi tunasisitiza matokeo ya kazi. Lakini kwa kuwa watu wengi ni wenye ubora duni wa tabia, wasio na maadili wasio na ufanisi kupita kiasi katika kazi yao, inawachukua muda mwingi zaidi kupata matokeo. Je, wengi wenu sasa hamna mawazo hasi kuhusu majukumu ya viongozi na wafanyakazi? Jambo moja ni hakika: Viongozi na wafanyakazi hawataanguka kwa ajili ya uchovu kwa kufanya kazi kulingana na mahitaji ya nyumba ya Mungu. Zaidi ya mambo haya ya nje na yasiyo na upendeleo, kuna jambo lingine unaloweza kuwa na uhakika nalo: Kama mtu amejitwika mzigo na ni mwenye ubora wa tabia fulani—na asiyepuuza ukweli kwamba kuna kazi ya Roho Mtakatifu—basi, kukiwa na matatizo ambayo hawezi kuwaza kuhusu au kutabiri, na akiwa na mambo ambayo hajawahi kuyapitia hapo awali na hana uzoefu nayo, Roho Mtakatifu atampa kumbusho za kila mara, akimtia nuru na kumsaidia wakati wowote. Kazi ya kanisa haitegemei kabisa uwezo, nguvu, na mizigo ya kibinadamu inayopaswa kufanywa—sehemu yake lazima itegemee kazi na uongozi wa Roho Mtakatifu, namna watu wengi walivyopitia. Kwa hivyo, namna yoyote ambavyo mtu anaiangalia, kutimiza majukumu yake ni jambo ambalo kiongozi au mfanyakazi lazima afanikishe. Hilo si hitaji la ziada kwao. Wasioamini wanapofanya kazi duniani, wao hutenda kulingana na msingi wa ubora wa tabia yao binafsi. Kufanya wajibu katika nyumba ya Mungu ni tofauti: Mtu hafanyi tu kwa msingi wa ubora wake wa tabia—lazima pia ategemee ufahamu wake wa kanuni za ukweli kama anatarajia kupata matokeo. Wakati mwingine, ni lazima pia asaidiane na kushirikiana kwa upatano kama anataka kufanya wajibu wake vizuri. Wengine wanaweza kuuliza, “Je, kufanya kazi katika nyumba ya Mungu kunatuhitaji ‘kupinda mgongo na kujitahidi kufanya kila tuwezalo mpaka siku yetu ya kufa’? ‘Viunzi vya hariri vya majira ya kuchipua hufuma hadi wafe’—je, tunahitaji kufikia hilo? Je, nyumba ya Mungu itakamilika tu tunapokufa kwa uchovu?” Je, hili ndilo ambalo Mungu anataka kutoka kwa mwanadamu? (Hapana.) Ushirika wetu kuhusu mahitaji ya majukumu ya viongozi na wafanyakazi unakusudiwa tu kuwapa watu uwazi na ufahamu kuhusu jinsi ya kushirikiana na kazi ya Mungu kulingana na kanuni za ukweli na mbinu za kazi ambazo Anahitaji, ili kazi Yake iweze kuendelea kwa utaratibu na ufanisi, na ili maneno na kazi Yake viweze kupata matokeo bora zaidi ndani ya watu Wake wateule. Kipengele kimoja cha hili ni kuhusu kukuza na kueneza kazi; kingine ni kuhusu kuyafanya maneno na kazi ya Mungu yapate matokeo ambayo yanapaswa kuleta ndani ya wale ambao wanamfuata. Haya ni majukumu ya viongozi na wafanyakazi, na kile ambacho wanapaswa kufanikisha katika kazi yao.

Kipengele cha Kumi: Kulinda vizuri na kutenga kwa busara vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu (vitabu, vifaa mbalimbali, nafaka, na kadhalika), na kufanya ukaguzi, matengenezo, na ukarabati wa mara kwa mara ili kupunguza uharibifu na hasara; pia kuzuia watu waovu wasivimiliki

Leo, tutasonga mbele kufanya ushirika kuhusu kipengele cha kumi cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi: “Kinga kikamilifu na kutenga kwa busara vifaa mbalimbali vya nyumba ya Mungu (vitabu, vifaa mbalimbali, nafaka, na vinginevyo) na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, matengenezo, na kukarabati kupunguza uharibifu na hasara; vilevile, kuzuia watu waovu wasivimiliki”. Kipengele cha tisa ni sharti pana kiasi kwa viongozi na wafanyakazi. Kipengele cha kumi ni sehemu nyingine ya kazi, moja ambayo ndani yake kuna sharti bayana la majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Sehemu hii ya kazi inahusisha vifaa ambavyo ni mali ya nyumba ya Mungu, baadhi yake vinanunuliwa kugharimia mahitaji muhimu ya maisha ya watu wanaotekeleza majukumu yao muda wote, na wengine ambapo vyombo, nyenzo, na kadhalika ambavyo vinanunuliwa kwa kazi ya kueneza injili. Kuna vitabu pia vya maneno ya Mungu na baadhi vitu kama vile vinahusisha kuingia katika uzima kwa ndugu na dada, na kwamba vinastahili kuwekwa na nyumba ya Mungu. Hizi ni bidhaa ambazo zinahusisha imani ya watu kwa Mungu. Aina tatu, kwa jumla: vitu vya lazima vya uzima, vitu vya lazima vya kazi, na vitu vya lazima vya imani kwa Mungu. Iwe vitu vinanunuliwa na nyumba ya Mungu au kutolewa na ndugu na dada, mara tu wanapomiliki nyumba ya Mungu, wanahusika na suala la uongozi na utengaji wa nyenzo na viongozi na wafanyakazi. Ingawa hii kazi haionekani kuwa ya maana ukitaza kwa nje ukilinganisha na desturi ya kanisani, kazi ya usimamizi na utaalamu, na wala sio kitu kinachohitaji kuwa kwa ajenda, bado ni kazi ya maana ambayo viongozi na wafanyakazi wanastahili kuifanya. Vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu vinahusika kwa kazi, maisha, masomo, na vitu hivi vyote vya watumishi kufanya wajibu, kwa hivyo ulinzi na utengaji wa busara ni vya maana sana na sharti visikose kutiliwa maanani

Ulinzi Sahihi

Kama viongozi na wafanyakazi, kilicho cha muhimu zaidi ya kufanya vizuri kazi ya usimamizi wa kanisa na kufanya maisha ya kanisa kuwa mazuri ni kufanya kazi ya kueneza injili vizuri, na pia kazi mbalimbali husika. La ziada, nyenzo mbalimbali za nyumba ya Mungu zinastahili kupewa usimamizi unaofaa. Vitu hivi vinastahili kulindwa vizuri; usiruhusu vipate ukungu au vivamiwe na vijidudu, na usiruhusu watu wavimiliki kana kwamba ni mali yao ya binafsi. Nyumba ya Mungu pia ina masharti bayana na hatua za jinsi viongozi na wafanyakazi wanastahili kufanya kazi yao vizuri. Wanastahili kuanza kwa kukagua iwapo watumishi wanaosimamia hivi vitu wanafaa, ni watu wa kuwajibika, na iwapo wanajua jinsi ya kuvisimamia, na iwapo wanaweza kutimiza kwa uangalifu majukumu yao—iwapo vitu hivi vitawekwa salama kwa usimamizi wao. Kwa kuhifadhi nafaka, kwa mfano, je, hiyo sehemu wanapozihifadhi katika msimu wa mvua—wakati hali ya anga iko na unyevu na kuna mvua nyingi—unyevunyevu? Je, watu wanaosimamia hii wanaikagua kwa wakati? Nafaka ikipata unyevunyevu, je, wanaitoa nje kukauka? Je, wanasimamia mambo haya kwa uangalifu kana kwamba ni wao wanaomiliki? Je, wanao ubinadamu wa aina hiyo? Je, wanao uaminifu wa aina hiyo? Wanastahili kuanza kwa kufanya ukaguzi wa watu wanaosimamia hivi vitu, kuona ubinadamu wao ni wa aina gani na iwapo wana dhamiri na ni wenye maadili. Iwapo mtu anaonekana kuwa mwenye ubinadamu, na mwenye ukarimu, na wengine wanasimulia mema kumhusu, lakini wewe bado haujui iwapo wanafaa kusimamia vitu vya nyumba ya Mungu, ni kipi kinastahili kufanywa? Ni lazima ufuatilie, upeleleze vitu na uangalie. Ni lazima uulize baada ya vitu baada ya muda mchache kuona iwapo mtunzaji amekuwa akitimiza majukumu yake. Kuhusu nafaka, kwa mfano, tatizo kuu ni unyevu. Mtunzaji anastahili kukagua iwapo ghala ya nafaka lina unyevunyevu na iwapo kuna uwezekano wa wadudu katika nafaka, na wanastahili kutafuta mtu anayejua kuhusu mambo kama hayo, kushauriana naye na kupata kuelewa kuhusu ni desturi zipi zinazoweza kuhakikisha kwamba nafaka hazitapata unyevu na kumea ukungu au kuvamiwa na wadudu. Mara wanapohifadhi nafaka, wanafaa kuangalia ghala, au kufungua dirisha ili hewa iingie. Hiyo itakuwa kutimiza majukumu yao. Iwapo mtunzaji atachukua hatua ya kufanya haya mambo pasipo kuukumwa au kukumbushwa, basi wao ni wa kuaminika, jambo ambalo linaondoa hofu. Je, vipi kuhusu watu wanaotunza vifaa aina mbalimbali, basi, je, wanastahiki kwa kazi? Bado hujui; ni lazima uwaangalie, pia. Jinsi gani vifaa vingi—vifaa vya umeme, samani, vituo, na kadhalika—vinalindwa iwapo haviko kwa matumizi ya kawaida. Je, mtunzaji anaviangalia na kuvitengeneza? Je, wao hufanya ukaguzi wa vifaa vya umeme, kuvitia umeme and kuviwasha? Kwa kuuliza, unaweza kuarifiwa kwamba mtunzaji wa hivi vitu anafanya hivi mara kwa mara. Vitu hivyo vinaweza kuwa havitumiki, lakini havina vumbi, kumaanisha kwamba aghalabu mtu huja kuvitunza—utaona kwamba mtunzaji ako sawa, kwamba wanatimiza majukumu yao. Hivyo basi unaweza kuwa na hakikisho. Kuna pia vitabu ya maneno ya Mungu. Kila mojawapo wa hivyo si rahisi kupata, na isitoshe, vitabu vya maneno ya Mungu ni vya maana zaidi kwa kila muumini kuliko kitu chochote—zaidi ya nafaka, vifaa vya umeme, au kitu chochote. Hivyo, kwa kuwa na hivi vitu vyote, ni kwa manufaa zaidi kupata mtu anayefaa kuvisimamia na pahali panapofaa kuvihifadhi. Upitishaji wa hewa stahiki, uangalizi na ukaguzi ni muhimu, pia, hawawezi kuacha vitabu vipate unyevunyevu au majimaji, au kuliwa na panya. Vitu hivi vyote vinastahili kuchungwa. Vivyo hivyo, wale wanaosimamia vitu hivyo wanastahili wale wanaofaa kwa kazi hiyo. Ni lazina uangalie hili, pia. Iwapo walinzi ni wazembe, wavivu, wasiojali, baadhi ya vitu vitaharibiwa, iwapo sio kupitia unyevunyevu na ukungu, basi kupitia wadudu. Hizi zote ni hasara, zinazosababishwa na ukosefu wa usimamizi na ukaguzi kwa upande wa viongozi na wafanyakazi. Iwapo walinzi watalinda vitu hivi ipasavyo, hili jukumu la viongozi na wafanyakazi limetimizwa. Iwe vitu hivi ni vikubwa na vidogo, na iwe vinatumika mara kwa mara au la, bora viwe katika kundi la vitu vinavyomilikiwa na nyumba ya Mungu, linastahili kupangwa ili mtu aweze kulisimamia. Kitu kinastahili kuwa salama, haijalishi aina yake na popote kilipowekwa, na inastahili kuhakikishwa kwamba hakuna kamwe lolote linaloharibika. Hiyo ndiyo kuwa kuaminika na kuwajibika. Iwapo anayesimamia vitu anapatikana kwamba hastahili, je, ni nini kinachostahili kufanywa? Upangaji wa wajibu wao unastahili kurekebishwa mara moja, na mtu mwingine kupatikana kuwabadilisha. Baadhi ya watu, kwa mfano, ni wazururaji wasio na kazi, wanye upendo wa kula lakini bali sio wa kufanya kazi, huku hawawajibiki. Wanachukulia vitu vya kanisa kimzaha, kana kwamba ni mali ya umma, wakifikiria kwamba ni sawa bora visipotee. Iwe vitu hivi vina ukungu au vimevamiwa na wadudu, au iwe chochote kimeharibiwa na, wao hawajali wala kuuliza. Unapowauliza, wanasema wamemaliza kuvitazama, na kila kitu kiko sawa. Kwa kweli, hawajaenda kuvitazama kwa muda mrefu. Kisha siku moja mtu anapopata kwamba nafaka imepatwa na ukungu na nyaya za vifaa zimeliwa na panya, na hata vitabu ya maneno ya Mungu vimekuwa na unyevunyevu mwingi kiasi kwamba maandishi yaliyomo hayaonekani na hayako wazi. Kuchunguza kuhusu vitu hivi pekee wakati huo—je, huko si kuchelewa? (Ndiyo, madhara yameshafanyika.) Haya ndiyo matokeo ya usimamizi usiofaa, Je, basi ni ukweli kuwa mtu anayesimamia hafai? Je, ni ukweli kwamba ni watu upungufu wa ubinadamu na wapotovu? (Ndivyo.) Wasioamini wangemwita mtu wa aina hii mpotovu; tuseme nini? Kwamba ubinadamu wa mtu huyu ni mbaya, kwamba hana uaminifu. Hawawezi hata kamwe kutimiza hilo jukumu dogo; hawawezi hata kamwe kufanya kitu ambacho mtu anayejitahidi, aliye na chembe ya dhamiri na ubinadamu, anaweza kufanya. Je, bado yeye an imani katika Mungu? Hata wasioamini wanaamini, “Fanya uwezavyo ili ushughulikie kwa uaminifu chochote kile watu wengine wamekukabidhi”-mtu huyu hata hatoshelezi kiwango kadiri cha uadilfu cha wasioamini, hivyo hawastahili kuhudumu kama mwanachama wa watumishi wa uongozi wa vitu. Watu wasiofaa sharti washughulikiwe upesi, na wanaofaa kuchukua nafasi zao wapatikane. Iwapo huna imani na watumishi wa uongozi wa vitu, na huna muda wa kuchunguza wewe mwenyewe, au huwezi kufuatilia mambo na kuangalia kwa sababu za kueleza hali ya mambo, ni lipi la kufanya hapa? Unaweza kumshurutisha anayelinda vitu aandike hakikisho, akisema kwamba iwapo kuna uharibifu wa vitu anavyosimamia, atagharimia, au kwamba yuko tayari kukubali adhabu kutoka kwa nyumba ya Mungu. Ni sharti isuluhishwe kulingana na mfumo wa usimamizi. Iwapo kiongozi au mfanyakazi anaweza kufanya kazi yao kufikia cheo hiki, watakuwa wanatimiza majukumu yao.

Kitu chochote cha nyumba ya Mungu, kiwe kikubwa au kidogo, ghali au rahisi, kiwe au kisiwe cha matumizi kwako, iwapo utafanywa kuvisimamia, basi ni jukumu lako. Hii kazi iko chini ya eneo la majukumu ya viongozi na wafanyakazi, kwa hivyo unafaa kutafuta mtu anayestahili na mahali pahali panapofaa ili kitunzwe ifaavyo. Usiruhusu vitu vya nyumba ya Mungu kuharibiwa. Kwa ulinzi wa vitabu vya maneno ya Mungu, kwa mfano—mara tu kiongozi au mfanyakazi anapotayarisha watumishi wanaofaa, wanapaswa kuuliza baadaye mara kwa mara: “Vitabu vingi vimetolewa karibuni, lakini usiwe mzembe, hata ingawa kuna vichache vimebaki. Kwa kuweka vitabu, jambo kuu na kutoruhusu vipate unyevu au kuharibiwa na jua, na kutoruhusu vikanyagwe na kukunjwa kiasi cha kupoteza umbo.” Ni sharti waulizie na kudadisi mara kwa mara. Iwapo vitabu vipya vimekuja, ni sharti waulize ni jinsi gani vinatunzwa vizuri; iwapo vyote vitatosha katika mahali pa mwanzo, na visipotoshea, iwapo mahali pengine pamepatikana pa kuviweka, na vipi hapo mahali pako, iwapo ni salama na kavu; iwapo vitabu vimewekwa vizuri; na iwapo kuna wasiwasi kuhusu panya, iwapo kuna haja ya kuweka paka. Mambo haya yote ndiyo ambayo viongozi na wafanyakazi sharti wafanye, na wajibu wao wanaopaswa kutimiza. Hii kazi inaonekana kwa kiasi fulani kuwa isiyo ya maana, lakini hii, pia, ni mojawapo ya kazi ambazo viongozi na wafanyakazi wanastahili kufanya kila siku. Usiishushe hadhi—ni sharti ichukuliwe kwa uzito. Vitu hivyo vinaweza kuwa mali ya umma na kutomilikiwa na mtu binafsi, lakini ni sharti vitunzwe vizuri; bila kujali iwapo vitakuwa vya matumizi kwako baadaye, na bila kujali iwapo ni vyako vya kutumia, kuvitunza vizuri ni jukumu lako, jambo ambalo liko chini yako, na hufai kutafuta sababu au kisingizio ili kuepuka na kulipuuza. Bora tu kitu ni jukumu lako, ni kitu unachofaa kusimamia, kazi unayofaa kufanya. Kwa yote yaliyomo, unastahili kudadisi na ujaribu kuelewa vitu au ushiriki mwenyewe. Kama una muda wa kwenda kwenye eneo na uangalie wewe mwenyewe, hilo litakuwa bora zaidi bila shaka. Lakini iwapo mazingira na hali ya mambo hairuhusu hilo, au iwapo una shughuli nyingi na kazi, unastahili bado kudadisi na kuuliza kwa wakati, katika juhudi la kuzuia vitu vya nyumba ya Mungu kuharibika au kupata hasara kwa njia yoyote. Kufanya hivi kunamaanisha kwamba umetimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi.

Utengaji wa busara

Kuhusiana na vifaa vya nyumba ya Mungu, kuna sehemu nyingine muhimu ya kazi zaidi ya kuvilinda: kuvitenga kwa busara. Vitu hivi vyote ni vya matumizi ya watu—vyote ni vitu muhimu—kwa hivyo lengo kuu katika kuvilinda ni ili vitumike kwa busara. Kabla ya kuviweka vitu hivi kwa matumizi ya busara, ni jukumu la viongozi na wafanyakazi kuvitenga kwa busara. Utengaji wa busara ni nini? Nyumba ya Mungu ina kanuni na masharti yanayozingatiwa kujua ni nani atakayepewa kuvitumia. Kusudi kuu ya hivi vitu, iwapo vitatolewa na ndugu na dada au kununuliwa na nyumba ya Mungu, sio kuvihodhi kwa misaada au kama sadaka kwa kazi ya ustawi; badala yake, ni vya matumizi ya ndugu na dada wote wanaofanya kazi muda wote. Hivyo basi, jinsi vinavyopaswa kutengwa—kanuni zinazotumika kuvitenga—ni jukumu lingine ambalo viongozi na wafanyakazi wanastahili kulitimiza kwa uendeshaji wa vifaa katika nyumba ya Mungu. Tumetaja hapa utengaji wa busara; hapa, kuwa “busara” ni kanuni inayohitajika katika nyumba ya Mungu.

I. Kutenga Vitabu vya Maneno ya Mungu kwa Busara

Tutaanza na vitabu vya maneno ya Mungu. Kila wakati vitabu vipya vinapotolewa, nyumba ya Mungu ina matakwa na masharti kwa njia ya kanuni kuhusu ni nani anayestahili kupewa hivyo vitabu. Katika kanisa, kuna watu ambao husoma maneno ya Mungu na wale ambao hawasomi, kuna watu wanaopenda ukweli na wasiopenda ukweli, na kuna watu wanaotekeleza wajibu wao na wasiotekeleza wajibu wao—utofautishaji unafaa kufanywa kati ya aina hizi za watu. Kuna pia vitabu maalum kwenye kundi la vitabu vya kiada—sarufi, kamusi, na vitabu vingine vya matumizi. Hivi vyote vinastahili kusambazwa kulingana hasa na kanuni. Ni sharti vipeanwe kwa wale wanaovihitaji, wala sio wale wasiovihitaji. Alafu kuna vitabu vya matumizi vinavyochapishwa kwa idadi ya chini—iwapo hivi vinatolewa kwa mtu-ni kipi kinachohitajika kwa mtu huyo? Unaweza kuvisoma, lakini usiviharibu; usiviache nje au kurarua karatasi kutoka kwenye hivyo vitabu bila mpango. Na vinastahili kurudishwa mahali vilipotolewa mwanzoni unapomaliza kuvisoma. Kuhusu na vitabu vya imani kwa Mungu, viongozi na wafanyakazi wanastahili kuvisambaza kulingana hasa na utaratibu wa kazi kwenye nyumba ya Mungu, na wanastahili kuruhusu watu wateule wa Mungu kuelewa kanuni, pia, na kutenda kulingana na kanuni.

II. Kutenga Vifaa vya Aina Mbalimbali kwa Busara

Kinachofuata ni jinsi ya kutenga aina mbalimbali ya vifaa. Hii ni kazi muhimu kiasi. Utengaji wa aina mbalimbali ya vifaa ni vyenye shuruti kidogo. Vifaa kama hivyo ni pamoja na vifaa vya umeme, na pia vyombo vinavyohitajika kwenye taaluma mbalimbali. Viongozi na wafanyakazi wanapozambaza vitu hivi, yafaa kuwe na kanuni zinazozingatiwa, pia. Kwa wale wanaopewa, ni sharti wawe ni watu wanaoweza kuendesha vifaa vivyo kwa uzoefu na kufanya matumizi sahihi na yenye busara. Iwapo mtu ni mwanafunzi au hajui kabisa jinsi ya kutumia kitu, hafai kupewa kitu hicho. Hii inazingatiwa sana sana vifaa vya umeme vya bei ghali kama vifaa vya kupiga picha na kompyuta za bei ghali, vile vile vifaa vya kurekodi, vifaa vya picha au vifaa vinavyohitajika utoaji wa video—hata kidogo, chombo hiki kisipeanwe kwa mtu yule ili kuzuia uharibifu. Viongozi na wafanyakazi yafaa wahakikishe kwamba wale wanaotumia chombo cha aina ile, mwanzo, wanafaa kuthamini mtambo, na pili, wana uwezo wa kutengeneza ipasavyo. Baadhi ya mashine, kwa mfano, ni lazima kwa masharti kipewe mapumziko ya dakika kumi baada ya matumizi ya masaa mawili ili kipoe. Pasipo kupoa, itaharibu mashine na kufupisha muda wa manufaa yake. Watu wanaothamini mashine wataitumia kwa akali kulingana na tahadhari za matengenezo; watazifuata wao wenyewe, bila wewe kuwaambia, na watakuwa waangalifu zaidi bado ukiwasihi. Watu kama hao wana haki kutumia mashine; wanafaa kwa matumizi ya vitu vya bei ghali kwa sababu wanafahamu jinsi ya kuthamini mashine, na wanazingatia kwa uzito zaidi matengenezo na tahadhari za ukarabati wa vitu hivyo. Watu kama hao, wanaoweza kutunza mashine na kuzitumia kwa njia ya kawaida ndio wanaofaa zaidi kwa utengajii na usambazaji wa mashine za kiwango cha juu. Viongozi na wafanyakazi wanastahili kuchunguza kwa makini kwa mujibu huu. Iwapo kuna kompyuta ya teknolojia ya hali ya juu na inatolewa kwa matumizi kwa yeyote yule anayeomba kwa kueleza haja nayo, je, kuna kanuni? (Hapana.) Ni lipi lisilo sahihi kuhusu hilo? Kwa viongozi na wafanyakazi, wanaohusika kwa usambazaji na utengaji wa vitu kama hivi, kinachofaa kuzingatiwa ni ustadi wa taaluma wa mtu anayewajibika na kazi hiyo; sehemu nyingine ni kuwa, ni lazima wazingatie kiasi cha upendo wa mashine aliyonao mtu yule, iwapo wanao ubinadamu, iwapo wanathamini mashine wanapozitumia. Iwapo mtu huyo hajui kutunza mashine na hana uzoefu na ujuzi wa kitaaluma, na anataka tu kucheza na mashine kwa sababu ya upekuzi, basi anapasa kuzuiwa na kukatazwa kutumia. Hawastahili kutumia na kutunza mashine za kiwango cha juu. Inatosha kuwapa wanaofanya kazi za kawaida mashine za kawaida. Wale wanaojua taaluma; walio na ubinadamu mzuri; na wanajua jinsi ya kutumia, kutunza na kuthamini mashine wanaweza kutumia vitu vya kiwango vya juu, kwa sababu wana ujuzi kwa taaluma na wana uwezo kutumia mashine za viwango vya juu. Ukimpa mtu mpumbavu au mshenzi kitu cha kiwango cha juu atumie, ataharibu mashine kwa siku chache. Wengine hawataweza kutumia, na haitakuwa rahisi kutengeneza. Hili halikwamishi tu kazi ya kanisa bali pia linaharibu vifaa kwenye nyumba ya Mungu. Kinachojitokeza hapa ni kipi? Kwamba watu kama hao hawafai kutumia mashine nzuri. Mashine nzuri sharti zipewe kwa watu wenye ubinadamu, ambao wana ufahamu wa kitaaluma, wazitumie. Inatosha kwa wale wasio na ustadi kwa taaluma na walio na wenye ubinadamu duni kutumia vitu vya kawaida. Je, utengaji wa vitu jinsi hii ni wa busara? (Ndiyo.)

Kuhusiana na kila aina ya mali ghafi, watu tofauti wanazo njia tofauti za kuzichukulia. Baadhi ya watu hununua kompyuta ya teknolojia ya hali ya juu, na baada ya miaka miwili ya matumizi, bado inaonekana mpya; hakuna kamwe alama za vidole zionekanazo kwenye kioo, na kicharazio daima ni kisafi, bila doa la vumbi. Kompyuta ya mezani ni nadhifu na yenye kuvutia, pia, na vilivyohifadhiwa kwenye kompyuta vyote viko kwa utaratibu na wazi. Mtu akimwambia kuwa ni vibaya kwa kioo kikitumika kwa muda mrefu, atauliza papo hapo ni jinsi gani ya kutunza kioo hicho—njia yoyote ile ambayo ni bora zaidi, hiyo ndiyo atakayofanya. Iwapo mtu atamwambia kwamba kompyuta inahitaji kupumzika baada ya matumizi ya muda mrefu, kwamba itafanya kazi vibaya zaidi iwapo itapata joto, hivyo basi kuathiri urefu wa maisha ya mashine, basi anapotambua kwamba amekuwa akiitumia kompyuta yake kwa zaidi ya masaa mawili, atasimamisha mara moja ili kuiruhusu itulie. Ikitulia polepole kwa sababu hali ya hewa ni ya joto, ataweka pepeo na kuipulizia. Anaihudumia mashine kwa uangalifu maalum kana kwamba ni mwanawe. Ni mwangalifu na mwenye tahadhari hasa anapoiweka ndani ya mfuko wake, na anapoiweka kwenye meza, anasafisha sehemu ya juu ya meza na kuiweka mashine inavyostahili. Je, huu sio ushupavu wake? (Ndiyo.) Watu kama hao hawapendi tu mashine—wanapoona wengine wakiharibu na kusababisha madahara kwenye mashine, hawastahimili. Watu kama hao wanastahili kutumia mashine nzuri. Baadhi ya watu walio na hela pia watanunua kompyuta za hali ya juu, wasizozipenda hata kidogo mara tu wanapozifikisha nyumbani. Hawazisafishi, haijalishi kiwango cha vumbi kwenye kompyuta, na wanazichafua sana. Wengine watatumia mashine kwa miaka miwili, na bado itaonekana mpya; watu hawa wanatumia mashine kwa miezi miwili, na inaonekana kana kwamba imetumika kwa miaka kumi. Ukiwaeleza kuwa mashine zinahitaji utunzaji, watasema, “Nini maana ya kutunza kitu hicho? Mashine zinatoa huduma kwa watu, kwa huduma kwa watu. Ikiharibika, nunua tu mpya!” Hivyo basi, mashine inaharibika chini ya miezi sita kwa sababu ya matumizi yasiyofaa. Unafikiria nini kuhusu hawa watu? Je, wanastahili kutumia mashine za hadhi ya juu? (Hapana.) Haijalishi uzuri wa kompyuta wanazonunua, hawafikirii kuzitunza, bali kuzirusha na kuziweka ovyo ovyo. Baadhi ya kompyuta zao zina mikwaruzo, zingine zimeharibiwa na maji; zingine zinaanguka chini na kuvunjika. Wanazitumia kwa fujo. Kuna kitu kinachokosa katika ubinadamu wa watu hawa. Mko tayari kutenga mashine nzuri kwa matumizi kwa watu kama hao? (Hapana.) Baadhi ya watu huvaa miwani na vioo vyao kila mara huwa visafi sana, ilihali vioo vya watu wengine vina sehemu za nje chafu, na ukoko na alama za vidole na vinginevyo. Ni jinsi gani hata wanaweza kuvitumia vikiwa katika hali hii? Wale wanaotunza miwani zao wanajali wanapoziweka chini; hawataruhusu kamwe vioo kugusa sehemu ya juu ya meza au kitu chochote, wala kuruhusu vioo kukwaruzwa au kuwa na michubuko. Vioo ni muhimu sana hasa kwa walio na changamoto ya kuona karibu— utazitumia vipi iwapo umekwaruza vioo? Baadhi ya watu ni wenye fujo kwa miwani yao, na vioo vyao vinatiwa ukungu baada ya kuivaa kwa muda mfupi tu. Hawawezi kuona chochote kwa wazi wanapoivaa—watakuwa bora zaidi bila kuitumia. Hata hivyo wanafikiria ni sawa kuendelea kuvaa zilivyo, kana kwamba haina maana. Nakanganywa na hili: Je, lengo lao la kuvaa miwani si ni ili waweze kuona vitu kwa dhahiri zaidi? Ni nini wachoweza kuona waziwazi, vioo vyao vikiwa vimekwaruzwa? Je, watu hawa si ni wenye fujo? Fujo, kweli. Kuna ukosefu wa kitu katika ubinadamu wa watu wenye fujo iliozidi—hawajui jinsi ya kutunza vitu, sembuse kufikiria kuvipenda.

Linapokuja suala la vyombo muhimu kwa nyumba ya Mungu, je, jukumu la viongozi na wafanyakazi ni lipi? Unapotenga chombo kama hiki, kinafaa kupewa watu wanaostahili. Wale wanaotumia vyombo vya hadhi ya juu ni sharti wawe watu wanaojua jinsi ya kutunza vitu. Watakitunza, watakiangalia, na kukidumisha; kikiwa katika umiliki wao, utakuwa na uhakika kwamba hawakiharibu au kuteketeza kwa makusudi au kutokana na hali ya kujijenga yenyewe, isipokuwa kupitia muda mfupi wa uzembe au ukosefu wa ishara ya maarifa yajulikanayo na wote. Watu kama hawa wanaweza kutumia chombo hiki; wanaweza kupewa vyombo vizuri vya hali ya juu. Kwa wale ambao kwa asili ni wenye fujo katika matumizi ya vitu, itafaa kuwapa vifaa vya kawaida kutumia. Vile vile, msimamizi wa vyombo na vifaa vile wana wajibu wa kuweka ushahidi wa matumizi: ni nani amechukua kitu kipi na atakitumia kwa muda gani, au ni kifaa kipi kimetengwa kwa matumizi ya mtu fulani, ambaye, kinapoharibika, anafaa kulipia kulingana na thamani yake. Washiriki wote ni sharti waweke alama kwa vitu hivi, ili kwamba mambo ni ya haki na busara kwa kila mtu. Mashine na vyombo vinastahili kutunzwa vyema, kwa vyovote vile bila kujali iwapo matumizi yake ni ya muda mfupi au mrefu; mtumiaji ni sharti ajifunze kuvitumia ipasavyo, na vinapokuwa na hitilafu, vinastahili kukarabatiwa papo hapo. Ni bora zaidi, kazi hii ikifanywa kwa uangalifu. Hali ikitokea ambapo utawala wa Shetani unawakamata watu, basi jukumu kuu la viongozi na wafanyakazi ni kuvikabidhi vyombo na vifaa muhimu kwa watu wa kuaminika na kutegemewa. Mara tu wanapovituma, wanafaa kumshauri mtu, wakimwambia, “Hivi ni vitu kutoka kwa nyumba ya Mungu vya wewe kutumia kutekeleza wajibu wako. Havipaswi kuchezewa. Unastahili kuvitumia kwa busara and kuvitunza vyema. Usiviharibu. Kwa maana vyombo na vifaa hivi vinahitajika kwa utendaji wa wajibu, iwapo kuna madhara kwavyo, fidia inastahili kulipwa kulingana na thamani ya vitu hivi. Iwapo kazi itacheleweshwa kwa sababu ya uharibifu wa vyombo, hilo ni jambo zito, kumaanisha kuwa kuna usumbufu na uharibifu kwa kifaa. Hivyo basi, ni sharti ujue jinsi ya kutumia ipasavyo aina mbalimbali za vyombo na vifaa kwa kufanya majukumu, bila shaka ni sharti kutoharibu rasilimali ya nyumba ya Mungu. Hakikisha umekumbuka kanuni hizi: matumizi ya busara, na ukaguzi wa mara kwa mara, ukarabati na matengenezo—kitu kinapokuwa na hitilafu, toa ripoti mara moja na uombe ukarabati”. Ili kufanya kazi hii vyema, kwa upande mmoja, viongozi na wafanyakazi ni sharti, wajue kanuni za utengaji na matumizi; sehemu nyingine ni kwamba wanastahili wawezeshe watumiaji kujua jinsi ya kutekeleza matengenezo na matunzo, na iwapo hitilafu inatokea, jinsi ya kutekeleza ukarabati na kadhalika. Haya ni maarifa ya kiwango cha kawaida ambayo watu wanastahili kuelewa na kumiliki linapokuja suala la kutunza na kutumia aina mbalimbali ya vyombo na vifaa.

Viongozi na wafanyakazi wanastahili kutenga kwa busara vyombo mbalimbali vya nyumba ya Mungu. Iwapo, kwa mfano, mtumishi anahitaji kompyuta iliyo na vipengele muhimu kiasi, unastahili kumpa moja wapo ya hizo. Iwapo atasema moja haitoshi, ni sharti umuulize kwa nini, na uchunguze ili uone ikiwa anachosema ni cha kweli. Usikubali tu kutenda kulingana na ombi lake na kumpa kompyuta anazoziomba, ukimpa mbili anaposema moja haitoshi, ukimpa tatu anaposema mbili hazitoshi. Je, hautakuwa unasambaza kompyuta kana kwamba ni vidude? Je, hili halitakuwa uzembe? Unastahili kwanza kuchunguza hali na ufanye uamuzi kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu. Ni sharti uidhinishe kikamilifu si kiholela maombi yote, ikitukia kwamba baadhi ya watu wanaomba tu wakisingizia kutekeleza majibu. Vile vile, baadhi ya watu wanaofanya kazi muhimu wanaweza kuhitaji kompyuta ya teknolojia ya hali ya juu, lakini kompyuta zao binafsi zina mpango wa hadhi ya chini. Viongozi na wafanyakazi ni sharti wachunguze, pia, na kutenga vifaa kwa busara. Utoaji wa kompyuta unastahili kuamuliwa kulingana na hali ya kazi na mahitaji ya hadhi ya kompyuta. Iwapo mtu ni kiongozi au mfanyakazi wa kawaida na hajishughulishi na ufundi wa kompyuta au kazi ya utengenezaji wa video, na anatumia kompyuta pekee kufanya mambo kama kwenda mtandaoni, kutafuta zana, na kupiga simu, na hahitaji mengi hususani vitu maalum vya kompyuta, basi anaweza kutumia kompyuta ya kawaida. Baadhi ya wakongwe wanajua tu jinsi ya kufanya vitendo rahisi kama kuchapisha, kwenda mtandaoni, na kupiga simu lakini mara tu wanapokuwa viongozi au wafanyakazi, wanapewa kompyuta za teknolojia ya hali ya juu. Je, hili ni la busara? Je, hawatafuti upendeleo maalum? Je, hawafurahii faida za vyeo? (Ndiyo.) Je, matumizi ya aina hii ya vyombo vya daraja la juu, hadhi ya juu ni yapi? Vinastahili kutolewa kwa watumishi husika na watumishi weledi. Havistahili kulinganishwa na cheo cha mtu. Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wanaamini kimakosa kwamba wanastahili kufurahia haki za upendeleo za matumizi ya vitu kadhaa katika nyumba ya Mungu. Je, hii ni kanuni katika nyumba ya Mungu? Hapana. Mara tu watu wanapokuwa viongozi na wafanyakazi, kwa upesi wanapewa kompyuta za teknolojia ya hali ya juu, rununu, na vipokea sauti vinanyobanwa kwa kichwa, wanapewa aina kadhaa za vyombo vya hadhi ya juu. Je, matokeo yake ni yapi? Je, haya yanafanywa kufikia matokeo bora kazini? Je, watu hao hawafurahishwi na tamaa ya mwili? Je unatumia kompyuta hii ya teknolojia ya hali ya juu kufanya nini? Je, hamfanyi mikusanyiko ya mtandaoni na kuhubiri maneno na mafundisho? Je, unajua kuziweka video mtandaoni au unaweza kutengeneza video? Je, unajua kutengeneza usalama wa mtandao au unaweza kuunda tovuti? Je, unajua weledi kwa nyanja hizi? Iwapo hauna, ni kwa matumizi yapi unahitaji kompyuta ya hadhi hii? Je, hili sio jambo la kuudhi la kufanya? (Ndivyo.) Iwapo una hela zako, hakuna wa kujali ni kompyuta ngapi unanununa, na hakuna yeyote atakayekuingilia haijalishi ni za hadhi ya juu gani. Sasa tunazungumzia jinsi vifaa vya nyumba ya Mungu vinastahili kutengwa kwa busara. Je, kwa “busara” kuna maana gani? Wakati viongozi na wafanyakazi wanatumia hivi vyombo vya kiwango cha juu vya nyumba ya Mungu, je, hili linazingatiwa kama kutumika kwa “busara”? (Hapana.) Hawajui taaluma au jinsi ya kufanya lolote. Je, kuwa na kompyuta ya teknolojia ya hali ya juu kunawafanya wakuwe wa kiwango cha juu? Kwa nini wanatangaza? Nyumba ya Mungu haina haki za upendeleo wa matumizi na utengaji wa vifaa kwa viongozi na wafanyakazi; hawana upendeleo maalum, ni hii kamwe sio kanuni ya busara ya utengaji kwa nyumba ya Mungu—haina busara kamwe. Mtu anaweza kununua vitu hivi mwenyewe akiwa na uwezo wa kufanya hivyo; iwapo hawana uwezo kufanya hivyo, na wanahitaji kupewa na nyumba ya Mungu, basi inatosha wao kutumia vile vya kawaida. Hii ni haki na busara. Wale wanaojuwa kwa kweli kutumia vyombo hivi vyenye kiwango cha juu ni wale watumishi wenye taaluma wanaohusika katika hii kazi, kwa hivyo nyumba ya Mungu inastahili kuwapatia hivi vyombo. Hizi ni baadhi ya kanuni ambazo viongozi na wafanyakazi wanastahili kuelewa na kufahamu kuhusu utengaji wa vitu kwa nyumba ya Mungu. Angalia kwa makini tena, kulingana na kanuni hizi, kuona iwapo vitu hivi havijagawiwa kwa busara pahali popote. Iwapo ni hivyo, fanya hima urekebishe. Baada ya baadhi ya watu kuwa viongozi au wafanyakazi, wanaona kuwa hakuna yeyote katika nyumba ya Mungu anayewarairai, kwamba hakuna anayewapatia vifaa vya kiwango cha juu, na kwamba bado wanavalia zao, mavazi kuukuu, bado wanatumia kompyuta zao ndogo kuukuu, na kwamba nyumba ya Mungu bado haijawapa kile kizuri. Basi, wanaenda kwa wanaohusika na fedha na kuomba kununuliwa kompyuta mpya. Je, hii ni busara? (Hapana.) Wanasema, “Iwapo hutanipatia, sitatekeleza wajibu wangu—nitatafuta fursa ya kufanya nyumba ya Mungu ininunulie kompyuta yenye teknolojia ya hali ya juu, ya kisasa, ya kufanya haraka!” Ni wakakamavu sana—hakuna kitu ambacho hawatajaribu kukifanya. Baada ya watu hawa kuwa viongozi, wanaifanya nyumba ya Mungu ni kama yao, wakiwaza, “Pesa za nyumba ya Mungu ni zangu, pia—Nitazitumia nipendavyo”. Hili ni jambo ambalo wapinga Kristo wana uwezo wa kulifanya.

III. Kutenga kwa Busara Ugavi na Vyakula Mbalimbali vya Kila Siku

Sasa tumekamilisha kuzungumzia kuhusu utengaji wa busara wa vitu ni vifaa mbalimbali. Kinachofuata, tutazungumzia vitu vya matumizi ya kila siku, kwa mfano: nafaka, mboga na vyakula vilivyokaushwa, vile vile viambato vya kupika, vyakula mbalimbali vya ziada na kadhalika. Vitu hivi havifai tu kulindwa kwa busara, lakini pia kutengwa kwa busara. Basi, vitu vinawezaje kugawiwa kwa busara? Nyumba ya Mungu ina vipimo vya vyakula, na wale wanaosimamia vitu hivi wanastahili kuvitenga kwa busara kwa kuzingatia vikali vipimo hivyo. Hawastahili kuwapa wale wa karibu nao vyakula vingi vizuri. Kwa mfano, iwapo mchele wenye ladha na ulio bora unanunuliwa, au iwapo matunda kiasi au nyama inanunuliwa mara chache, na unagawa kiasi kikubwa cha hivi kwa yeyote unayeelewana naye, au uwagawie vitu vyote vizuri, huku unatuma vibovu kwa wengine—je, hii linazingatiwa kama utengaji wa busara? (Hapana.) Je, ni jinsi gani “busara” inaweza kupimwa hapa, basi? Je, ni njia gani ya kutengwa vitu inayoweza kuzingatiwa kuwa yenye busara? Hata utengaji, kulingana na kanuni na vipimo vinavyohitajika kwamba nyumba ya Mungu ina masharti ya vyakula, kutolewa kwa kiasi kinachostahili kutolewa. Iwapo unahisi kwamba uko na uhusiano wa karibu na mtu, unaweza kumpa sehemu yako. Usiwe mkarimu na vitu vya wengine, na usitumie vitu vya nyumba ya Mungu kuonyesha ukarimu kwa watu wengine; iwapo unataka kuwa mkarimu, fanya hivyo ukitumia vitu vyako. Ukarimu si kanuni katika nyumba ya Mungu—kanuni ya nyumba ya Mungu ni utengaji wa busara. Usambazaji wa mahitaji muhimu ya maisha ya kila siku na vyakula mbalimbali inapaswa kufanywa kulingana na vipimo vilivyowekwa na nyumba ya Mungu, si kiholela. Kwa kawaida, viongozi na wafanyakazi wanaweza kusimamia na kuona iwapo watu wanaowajibika na usambazaji wa hivyo vitu wana nia nzuri, iwapo usambazaji ni wa busara, iwapo usambazaji unafanywa kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu, jinsi idadi kubwa ya watu wanaeleza ilivyo, iwapo wana malalamiko, na iwapo kila mtu ameshughulikiwa. Ni kitu kipi kinachostahili kufanywa iwapo vitu vitakuwa nadra wakati mwingine. Je, ni vyema kwa viongozi na wafanyakazi kuviweka na kuvila wenyewe? Baadhi yao wanaweza kusema, “Viongozi na wafanyakazi wana vyeo na hadhi kubwa zaidi, na kawaida wao ndio wanaozungumza zaidi nasi, hili linawanya kukauka midomo. Iwapo kuna kitu chochote kizuri, acha tuwaachie wale.” Je, ni vyema kutenga vitu kwa njia hii? (Hapana; vitu vinastahili kuachiwa wale walio na mahitaji kwa kweli.) Iwapo kuna uhaba wa baadhi ya bidhaa za huduma za afya za bei ghali, vinapaswa kutengwaje? Vinastahili kutengewa wale wanaojitumia kwa ajili ya Mungu kwa miaka mingi na wamefanya mchango. Watu hawa ni dhaifu kiafya kutokana na umri wao, lakini bado ni waangalifu kwa utendaji wa majukumu yao, na ndugu na dada wamenufaika pakubwa kutoka kwao. Watu hawa wanahitaji kudumisha na kutunza miili yao kidogo, na ni haki kwamba waruhusiwe kula na kutumia bidhaa za huduma za afya. Kusiwe na yeyote wa kupigania ruzuku haba. Hivi ndivyo viongozi na wafanyakazi sharti wagawe hivi vitu. Je, hii ni busara? (Ndiyo.) Je, watu wengi watakuwa na pingamizi kwa utengaji kama huu? Kuna yeyote anayesema, “Ingawa mimi si mzee hivyo, lakini nina kazi nyingi ya kufanya—Ninafanya kazi zaidi ya masaa nane kila siku. Kazi yangu inaweza kuwa isiyo na ufanisi sana, na ninaweza kuwa sijaifanya kwa miaka mingi, lakini afya yangu sio nzuri sana wakati mwingine, pia. Kwa nini hakuna anayenijali? Wakati kuna mambo mazuri, haijawahi kuwa zamu yangu kuyapata, lakini kukiwa na kazi ya kufanya, kila mara ni mimi ninayetafutwa”? Je, mtu kama huyu anastahili kutengewa sehemu fulani? Kwa sababu ana ujasiri wa kuomba, mwachie kidogo—je, hili ni la busara? Mungekubali kufanya hivyo? (Hapana.) Ingekuwa ni mimi, ningekubali. Kwa nini kusumbuliwa kuhusu mambo kama hayo? Watu hawaishi maisha yao kwa raha; hawaishi kula, kunywa na kujifurahisha. Kwa nini kupigania vitu hivi? Iwapo mtu anataka kupigania na hali yao kiasi inafaa, basi mwache afurahie hivyo vitu kidogo. Atakuwa ameonyeshwa upendeleo maalum, lakini wewe hutakuwa umepoteza; hakuna haja ya kusumbuliwa. Basi, tuseme kwamba mtu angesema, “Kwa nini usinipe kiasi? Afya yangu si njema, pia; iwapo nitapata kula kitu kizuri, nitaweza, kulingana na kuimarika kwa afya yangu, kufanya kazi zaidi na kutia bidii katika kazi ya Mungu, na kazi yangu itakuwa na ufanisi mwingi.” Kwa sababu amefanya ombi hili, usimwaibishe kwa kukataa ombi lake, msambazie kiasi. Watu wengine hawastahili kusumbuliwa kuhusu hili, kuwa mwenye ukarimu zaidi kiasi. Je, maisha yako yasingeendelea kama yalivyokuwa hapo awali bila hivyo vitu? Yale ambayo Mungu anapa watu sio haba; ni mengi na tele—hakuna haja ya kupigania vitu. Iwapo kuna kitu maalum na hakuna anayehisi kwamba anakihitaji au kwamba anahitaji kujifurahisha, basi mtu wa aina yoyote ambaye wengi wanakubali ndiye anayestahili kupewa kula. Tunasisitiza ubinadamu na busara kwa utengaji wa vitu. Wale wanaopokea vitu hivi, wanastahili kuvikubali kutoka kwa Mungu na kumshukuru kwa neema Yake. Wengine hawafai kuvipigania. Iwapo utapigania, wewe huna busara, unasababisha usumbufu kwa makusudi, na unakosea. Hivi ndivyo hali maalum kama hiyo inavyopaswa kushughulikiwa. Kuna kanuni za kushughulikia hali maalum na vilevile za kawaida; hazipaswi kuchukuliwa bila mpangilio, sembuse kwa msingi wa mahitataji ya uhusiano wa binadamu. Wakati vitu hivi vinagawiwa kwa busara, viongozi na wafanyakazi wametimiza wajibu wao.

Katika kugawa riziki na chakula cha kila siku, viongozi na wafanyakazi wanapaswa pia kufanya hivyo kulingana na hali halisi, idadi halisi ya watu, na kiasi halisi kinachohitajika, ili kuvigawanya kwa njia ya busara ya kweli kwa lengo la kutoviruhusu viharibiwe au kupata hasara. Hili ni jukumu ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kutimiza. Wakati mwingine, wanapokuwa hawana maarifa ya hali maalum, wanaweza kugawa vitu fulani kulingana na kanuni ya msingi, na kutambua baadaye, kupitia maoni ya kila mtu na ufuatiliaji unaofuatia, kwamba mgao haukuwa wa busara, kwamba ulikuwa umefungwa kidogo na kanuni. Katika hali hiyo, ni lazima wafanye vyema wakati ujao, ili kuepuka kujirudia kwa tatizo hilo na kupunguza upotevu na hasara. Huko ni kutimiza majukumu yao. Bila shaka, ili kuepuka kuwepo kwa uharibifu na upotevu, ni lazima, kwa sehemu fulani, wafanye ushauriano zaidi wanapogawa vitu; ni lazima pia wazingatie kanuni kikamilifu. Hili ni jambo la lazima. Usitoe vitu bila ubaguzi, ukose kuwapa wale wanaohitaji kwa kweli, kutowapa wale wanaofanya wajibu wao kwa dhati, walio na uhalisi wa ukweli, lakini uwape hasa wale wanaojipendekeza ambao hawana ufahamu wa kiroho. Je, kufanya hivyo ni kutenda kulingana na kanuni? (Hapana). Je kufanya hivyo si kupuuza kabisa? Kutotenda kulingana na kanuni si kutimiza majukumu ya mtu. Kutimiza majukumu ya mtu kunarejelea nini? Si kufanya mambo kwa njia isiyo ya dhati na kufuata kanuni, na haitimizwi kwa kuchukua mfululizo wa hatua zilizowekwa—badala yake, huku ni kutenda kwa kuzingatia kwa ukali kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu, huku ukihakikisha kuwa hakuna viza vya upotevu au uharibifu vinavyotokea kwa kitu chochote cha nyumba ya Mungu. Huku ndiko kutimiza jukumu lako kwa kweli. Kwa mfano, katika kisa cha kuwapa mayai watu watano, unapaswa kumpa kila mtu moja kwa siku, na kuwapa kila baada ya siku kumi, kwa hivyo utakuwa hasa umetoa hamsini. Unapasa kutoa kwa namna hii, kwa sehemu, kwa sababu ni idadi ndogo na ni rahisi kushughulikia; zaidi ya hayo, ni kiwango sahihi kabisa kwa wao kula. Kutenda kwa namna hii, kulingana na viwango na vipimo vinavyohitajika na nyumba ya Mungu, ni sawa kabisa—ni kutenda kulingana na kanuni. Iwapo kiongozi au mfanyakazi, akihofia usumbufu, aliwapa mayai ya siku mia moja kwa wakati moja—mayai mia tano—je, hilo lingefaa? Niambie, je, ni rahisi kusafirisha na kutunza mayai hamsini, au mia tano? (Hamsini). Idadi ndogo ni rahisi kusafirisha na kutunza. Watu wengine hutuma mayai ya siku mia moja, na matokeo yake, mengine huvunjika njiani, na mengine hupondwa yanapobebwa mahali yanapopelekwa. Yanapovunjika kidogo kidogo, sehemu fulani hupata uharibifu. Kuongezea kwa hili, watu wanapoona mayai mengi yametolewa, watayaharibu kwa urahisi, na hivyo hawatakuwa na mayai ya kula kabla ya siku ya shehena inayofuata. Hivyo, wakati mayai haya yamevunjwa na kupata uharibufu, je, si ni uzembe wa viongozi na wafanyakazi unaosababisha hilo? (Hasa.) Ikiwa wataagiza zaidi, unaweza kuwapa? Kulingana na kanuni, huwezi kuwapa zaidi kabla ya tarehe iliyowekwa, lakini watahisi huzuni wakati hawana chochote cha kula. Ni nini kinachopasa kufanywa hapa? Hili linahitaji mgao wa busara. Unapogawa vitu hivi, viongozi na wafanyakazi lazima wazingatie kanuni za mgao wa busara na kiwango kinachohitajika na nyumba ya Mungu, kuvitoa kwa wakati na mara kwa mara. Zaidi ya hapo, lazima wawe wa kuelewa haraka kama kumekuwa na visa vya upotevu, iwapo kumekuwa na maombi ya kurudiwa au maombi ya vitu vilivyo adimu kutokana na upotevu, na iwapo kumekuwa na visa vya upotevu kwa vitu vilivyotolewa ambavyo watu hawakuvipenda. Nyama na mboga, kwa mfano, vyote viwili vinatolewa, na watu wengi wanapendelea nyama, hivyo wanaweza kuila kwa siku tatu au tano, na mboga huachwa. Mboga hazihifadhiki vizuri; baadhi yake huharibika na kuoza baada ya muda, na hivyo wanaishiwa kabla ya bechi linalofuata kutolewa. Mtu yeyote anaweza kutuma maombi upya kuuliza zaidi. Je, vingine zaidi vinapasa kupeanwa katika kisa hiki? Ni jambo la busara kuwapa zaidi? (Hapana.) Watu wengine watakula nyama na mayai kwa ujanja, na kula mboga zote wanazozipenda huku wakitoa sababu na visingizio vya kila aina ili wasile mboga wasizozipenda. Mboga zikichuchuka na kuwa njano na kuwa mbaya, wanasema haziliki na wanaishia kuwalisha nguruwe na kuku, au kuzitupa, na kuagiza zaidi. Viongozi na wafanyakazi wanapokumbana na jambo hili, watalishughulikia vipi? Wakisema, “Nitakupa zaidi wakati mwingine, unavyoona kwamba haitoshi—Nitakupa zaidi, kwa sababu nyinyi hula sana,” je, hii ni njia sahihi ya kulishughulikia? Si huo ni upofu? (Ndiyo) Inakuwaje kwamba wao ni vipofu? (Hawaelewi ni kitu gani kinachoendelea: Sababu kuu ya chakula ambacho walikitoa kutowatosha ni kwamba walikibadhiri.) Wanakimbilia hitimisho bila kuelewa kinachoendelea kweli. Kuna chakula cha kutosha cha kuliwa katika sehemu nyingi ambazo zimetolewa kulingana na vipimo ya nyumba ya Mungu. Kwa nini hakitoshi katika eneo hilo pekee? Je, hilo linahitaji uchunguzi maalum? Lazima waende kwenye eneo la kazi na waulize kwa uangalifu na kwa undani juu ya hali hiyo, ili waone kinachoendelea. Mwishowe, kupitia uchunguzi na ufahamu, wanaona kuwa mpishi mahali hapo ni mtu mbaya na asiye na maadili mema, aliyewalisha kuku chakula cha watu, akipoteza chakula cha nyumba ya Mungu kimakusudi. Ni mwenye kuchagua sana kile anachokula, na anapenda kula tu chakula kitamu. Hatakula mboga wakati hakuna nyama, na wakati iko, hawatakula hata tofu. Anapopata mayai anayala katika kila mlo. Anachagua chakula kitamu pekee na hali mboga yoyote ya kawaida wala hajali ikiwa itaharibika. Uelewa umemwonyesha mpishi kuwa mtu mbaya—hivi anapaswa kuongezewa kiwango wakati ujao mgao unapotolewa? (Hapana) Je, si kumpa zaidi ndiyo kila kitu? Je, tatizo hili litashughulikiwa vipi pindi tu linapogunduliwa? Mbadilishe mara moja; mbadilishe na mtu mwenye ubinadamu kiasi ili achukue wajibu huo. Gundua na kulitatua tatizo hilo mara moja, na kuwaondoa watu wabaya kama hao, tufaha zilizooza kama hizo. Baadhi ya watu wanaweza kuuliza, “Kwa kuwa hapiki tena, itakuwa sawa akiwalisha kuku?” (Hapana) Akiwalisha kuku, kuku hawatataga mayai; akiwalisha nguruwe, nguruwe watakonda. Halitakuwa jambo la busara kumfanya alishe chochote. Watu kama hao lazima wafukuzwe—hawastahili kufanya kazi katika nyumba ya Mungu. Matatizo mengine yakipatikana wakati wa kugawa vifaa vya nyumba ya Mungu yanapaswa pia kutatuliwa kwa haraka. Lengo la kutatua matatizo haya ni lipi? Ni kupunguza upotevu na uharibifu unaotokana na vitu vya maada vya nyumba ya Mungu. Wengine wanaweza kuuliza, “Ili kutatua matatizo hayo, inabidi mtu aende kuchunguza jikoni. Je, si Umesema kwamba viongozi na wafanyakazi hawaruhusiwi kuingia jikoni? Kwa nini wanaruhusiwa sasa?” Hayo ni masuala mawili tofauti. Sikusema kwamba hawaruhusiwi kwenda—huo ulikuwa uchanganuzi wa viongozi na wafanyakazi kutojua jinsi ya kufanya kazi, wakizurura ovyo na kuzungukazunguka kwa uzembe, wakijifurahisha katika faida ya hadhi, siku zote wakienda jikoni kutafuta vitu vizuri vya kula. Kwa sasa wanaenda jikoni kutatua matatizo sio kutafuta vitu vizuri vya kula. Nenda unapopaswa kwenda na usiende wakati hupaswi kwenda. Viongozi na wafanyakazi wana kazi nyingi ya kufanya, na hii ni mojawapo ya kazi zao, ambayo matatizo yake yanaweza kujulikana tu kwa kuingia katika kina cha jikoni na kupata ufahamu wa maelezo. Mpishi akigunduliwa kuwa hafai, atafukuzwa kazi mara moja na nafasi yake ichukuliwe na mtu anayefaa. Kufanya hivyo kunahakikisha kwamba vitu vilivyotolewa na nyumba ya Mungu havijabadhiriwa na kuharibiwa. Hata hivyo Ninasema, sharti la viongozi na wafanyakazi ni kwamba watimize wajibu wao—ikiwa ni jambo unalopaswa kuhangaikia na kufanya, basi lazima ulihangaikie na kulifanya. Ni lazima uangalie kwa macho yako na utumie masikio yako kusikiliza kwa makini kile ambacho kila aina ya mtu anachosema—na bila shaka, lazima pia ujifunze moyoni kuwa na maoni, mawazo, na utambuzi kuhusu mambo ya kila namna; jambo lingine muhimu ni kutilia maanani kanuni zinazotakiwa kufuatwa na nyumba ya Mungu, na kutobadilika kutoka kwazo wakati wowote. Kazi yoyote unayofanya, lazima kwanza uelewe kanuni na masharti yanayotakiwa na nyumba ya Mungu; kabla hujaanza kazi, lazima ujiulize mara chache zaidi maswali kama vile: Je, ninaelewa vizuri kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu? Je, hili linapaswa kufanywaje, ndiyo liwe limefanywa kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu? Linapaswa kufanywaje ili lilingane na kanuni za hali maalum? Linapaswa kushughulikiwaje katika hali ya kawaida? Ni lazima kabisa ujiulize maswali haya zaidi na mengine kama haya kabla ya kuanza kazi, na uombe zaidi mbele za Mungu. Sehemu moja ni kujichunguza; sehemu nyingine ni kukubali uchunguzi wa Mungu. Kufanya hivyo ni jambo la msaada kwa msaada kwa viongozi na watenda kazi katika kufanya makosa machache na kukengeuka kidogo katika kazi yao, kupunguza upotevu wa vitu vya maada vya nyumba ya Mungu na kupunguza hasara ya nyumba ya Mungu zaidi. Kilicho muhimu zaidi ni kwamba kufanya hivyo kunashikilia majukumu ya viongozi na wafanyakazi na kunatimiza majukumu hayo. Hiki ndicho ambacho viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya. Hili ndilo sharti kwa viongozi na wafanyakazi. Kuchunga na kugawa vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu si kazi tata. Kwa upande mmoja, ni suala la viongozi na wafanyakazi wenyewe kufahamu kanuni; sehemu nyingine ni kwamba viongozi na wafanyakazi lazima wafanye ushirika juu ya kanuni hizi zaidi kwa watu wanaohusika na kusimamia vitu mbalimbali vya maada, kufuatilia mambo zaidi na kujaribu kuelewa mambo zaidi na kuchunguza zaidi kuhusu hali ya usimamizi, wakati wote wakifanya ushirika zaidi na wasimamizi wa kugawa vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu ili kuwapa ufahamu zaidi juu ya kanuni hizi. Bila shaka, viongozi na wafanyakazi lazima pia waendelee kudadisi na kuuliza kuhusu jinsi watu hao wanavyogawa na kutoa vitu, na kama kuna hali yoyote maalum—kwa mfano, kama wasimamizi wanagawa vitu kulingana na kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu katika majira tofauti, kwa nyakati tofauti, na katika hali ambapo watu wa aina mbalimbali wana mahitaji tofautitofauti. Lengo la kufanya hivyo ni kuwezesha vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu vifanya kazi zake kwa ufanisi na kutumika kwa busara kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo na kulindwa katika utunzaji ulio bora zaidi kwa matengenezo bora zaidi. Hili ni jukumu la viongozi na wafanyakazi.

Kusimamia Nyenzo za Nyumba ya Mungu Vizuri Ni Wajibu wa Watu Wote Wateule wa Mungu

Kwa kuwa mmeelewa majukumu ya viongozi na wafanyakazi, je, mmeelewa pia kanuni ambazo kila ndugu na dada anapaswa kushika ushughulikiaji wao wa mali ya maada ya nyumba ya Mungu? Huenda ninyi si viongozi, lakini bado lazima mtimize jukumu la usimamizi. Hii ni haki ya watu wateule wa Mungu. Pia, kuhusiana na vitu kadhaa vya kimaada vya nyumba ya Mungu—kama vitabu na vyombo vya kila aina, chakula, vinywaji, na vitu vya kila siku; na kadhalika—lazima kila mtu avichukulie kwa upendo na uangalifu. Kila mtu anapaswa kufanya uchunguzi, marekebisho na utunzaji wa mara kwa mara wa vitu mbalimbali anavyotumia, na anapaswa kuvitumia kwa busara—usiache viharibike na kupotea bure vikiwa mikononi mwako, au kuvitupa bila mpangilio. Wengine husema, “Kitu hiki si changu, hata hivyo. Sikukinunua kwa pesa zangu. Nyumba ya Mungu ilinipa—ni mali ya umma. Sihitaji kujali kinapotengenezwa na kurekebishwa, au ni wapi kinapohifadhiwa. Siwezi kukibeba kila mahali kana kwamba nimekiteka nyara.” Je, mawazo kama haya ni ya busara? Je, si ni yenye ubinafsi na yasiyo na ubinadamu? (Ndiyo.) Basi, ni kanuni zipi zinazopaswa kufuatwa katika matumizi ya mali ya nyumba ya Mungu? Ikiwa umepewa kitu fulani kwa ajili ya matumizi yako, basi ni wajibu wako kukitunza na kukirekebisha wakati unapokitumia. Ni wewe unayekiwajibikia kikamilifu; bila kusihiwa au kusimamiwa na mtu mwingine, unapaswa kukitunza, kukithamini, na kukilinda kana kwamba ni mali yako binafsi. Huko ndiko kuwa na ubinadamu. Unapaswa kuzingatia hali ya kitu unapopewa, wakati huruhusiwi kukitumia tena au wakati ambapo umemaliza kukitumia, unapaswa kukirudisha kwa mhifadhi wake kikiwa katika hali kamili ambayo hakijaharibika na katika hali yake ya awali. Hii inaitwa kuwa na busara; hili ni jambo linalopaswa kuwepo katika ubinadamu. Unasema kwamba unamwamini Mungu, kwamba una dhamiri na mantiki, kwamba unapenda ukweli, unaufuatilia, na unatii, lakini ikiwa huna hata ubinadamu mdogo zaidi unaopaswa kuwa nao katika kuitendea mali ya maada, unawezaje hata kuzungumzia kupenda ukweli au kuutenda? Je, hilo si jambo tupu sana? Ikiwa huwezi hata kutimiza wajibu unaopaswa kutimiza katika kuichukulia mali ya maada, hilo linamaanisha kwamba ubinadamu wako si mzuri—“kukosa ubinadamu” ni njia ya kawaida ya kusema hivyo. Zaidi ya hayo, namna unavyotumia vitu vyako mwenyewe, iwe wewe si makini au uko makini katika kuvitendea, hiyo ni haki yako. Hakuna atakayeingilia kati. Lakini nyumba ya Mungu ina kanuni za matumizi ya vitu vyake. Kanuni hizi zote zinategemea dhamiri na busara, na ingawa huenda zisifikie kilele cha ukweli, angalau zinafuata viwango vya ubinadamu. Kama huwezi hata kufikia kiwango hiki cha ubinadamu, kama huwezi hata kuvichukulia na kuvitumia vyombo na vifaa ambavyo nyumba ya Mungu imekupa, basi kama unaweza kuelewa ukweli na kuingia katika ukweli kwa hakika ni tatizo—linahitaji kutiliwa shaka. Kwa hivyo, linapokuja suala la jinsi unavyoshughulikia vitu hivi, una haki ya kuvitumia, na kwa kawaida pia una jukumu la kuvirekebisha, kuviunda, na kuvitunza. Lazima uchukulie mambo haya kwa uzito. Kama wewe, kama wasemavyo wasioamini, unasema, “Si changu, hata hivyo. Sikukinunua kwa pesa zangu. Kitu cha umma kikivunjika, kitavunjika—nunua kipya tu, au kirekebishe, hali ikiwa mbaya zaidi. Hata hivyo, si kama nimepoteza.” Kama hivyo ndivyo unavyofikiri, hilo ni tatizo—uko hatarini. Huna tabia njema, na moyo wako hauko mahali pazuri. Kutumia vitu vyako mwenyewe kwa uangalifu, lakini uvichukulie vitu vya nyumba ya Mungu kama visivyo muhimu, kutojali kuvithamini—je, huyo si mtu ambaye moyo wake hauko mahali pazuri? Je, Mungu anapenda watu ambao mioyo yao haiko mahali pazuri? (Hapana.) Hebu Niambie, je, si Mungu huwachunguza watu ambao mioyo yao haiko mahali pazuri? (Ndiyo.) Mungu huwachunguza wale ambao mioyo yao iko mahali pazuri na wale ambao mioyo yao haiko mahali pazuri kwa usawa. Unapokubali uchunguzi wa Mungu, ni kitu gani kinachopaswa kufanyika ukigundua kuwa unafikiri kwa namna hiyo? Usijali? Acha bila kudhibitiwa? Usijali kuhusu hilo? “Kile ninachofikiri ni shughuli yangu. Wewe ni nani uingilie kati? Ukiniruhusu nitumie kitu, basi nina haki ya kukitumia—na kwa vyovyote vile, itakuwa sawa nisipoivunja mashine. Kwa nini unatoa madai makubwa na mengi sana?” Je, hii ni njia nzuri ya kuwaza? (Hapana.) Ni “kukosa ubinadamu.” Ukiwa na mawazo kama hayo, lazima ukubali uchunguzi wa Mungu na useme, “Mungu, nina tabia potovu, na ubinadamu wangu ni duni. Nilikuwa nikifikiri kwamba nilikuwa muungwana na mwenye heshima, kwamba nilikuwa na hadhi; nisingefikiria kitu hiki kidogo kingenifunua: Nina tamaa za ubinafsi; moyo wangu hauko mahali pazuri; Nina malengo yangu madogo. Niko tayari kukubali uchunguzi Wako na nidhamu Yako, na niko tayari kujigeuza.” Lazima uombe na utubu mbele za Mungu, na umruhusu Akuchunguze. Ukiwa umekubali uchunguzi Wake, unapaswa kujigeuzaje? Utasema, “Ilikuwa ni kinyume cha maadili kufikiri kama nilivyofikiri hapo awali—hayo ndiyo mawazo ya wasioamini, ya wasio na imani. Siwezi kufikiri hivyo tena. Sipaswi kuchukua njia hiyo. Mimi ni muumini katika Mungu; ninahitaji kuwa mtu mwenye ubinadamu na heshima, ninahitaji kufanya mambo ambayo Mungu anapenda. Ninahitaji kubadilisha njia yangu ya kutumia vifaa na mashine katika siku zijazo. Lazima niviache vipumzike wakati vinapopaswa kupumzika, nivitengeneze inavyopasa, na nivitunze inavyopasa. Lazima nivisafishe mara kwa mara, na niangalie mara kwa mara vipengele vyake mbalimbali ili kuhakikisha matumizi yake ya kawaida. Nami nitavisafisha mara moja nitakapomaliza kuvitumia, na kuvirudisha katika ulinzi, ili nisiwaruhusu watu wasiohusika kuviingilia.” Na kisha, utakapotumia mashine tena katika siku zijazo, utakuwa mwangalifu na makini sana. Maoni yako yatakuwa yakibadilika kila mara, na njia zako zitaboreka, ukigeuka kutoka kwa mawazo na vitendo vyako vya ubinafsi na vinavyostahili dharau vya awali kuelekea hisia ya uwajibikaji, akili ya kujali mambo, na akili ya kuchukua jukumu. Mabadiliko katika mawazo yako ni mwanzo wa kujigeuza kwa kweli. Yanakuwa mabadiliko katika njia zako unapofanya mawazo na fikira zako ziwe halisi katika utendaji wako. Ni wakati inapofikia kiwango hiki ndipo Mungu anaona kwamba wewe unageuka na kutubu kweli; mageuzi na mabadiliko haya unayofanya yatakubalika kwa Mungu kweli. Huku ni kutenda ukweli. Ni jambo gani la msingi zaidi ambalo mtu lazima awe nalo katika kutenda ukweli? Dhamiri na busara ambazo watu wanapaswa kuwa nazo. Na, je, mtu mwenye ubinafsi na mwenye kustahili dharau ana dhamiri na busara? (Hapana.) Huenda mkajua kama suala la mafundisho kwamba hamwezi kuacha vitu vya nyumba ya Mungu vikiwa vimelala, au kuviharibu na kuvipoteza, au kutoviwajibikia—lakini mtazamo wako ukoje moyoni na mawazoni mwako? “Kuna maana gani ya kujali kuhusu mambo hayo? Jambo hilo hata si langu.” Mawazo kama hayo yataiongoza tabia yako, na, je, fundisho unalolijua litakuwa na manufaa yoyote basi? Hapana—litakuwa tu fundisho ambalo halina faida yoyote. Ni pale tu mawazo na mitazamo yako itakapobadilika, na uwe umegeuka na kutubu mbele za Mungu, ndipo tabia zako na matendo yako ya vitendo yatakapoanza kubadilika. Hapo ndipo kile unachoishi kwa kudhihirisha kitaanza kuwa na ubinadamu; hapo ndipo utakapoanza kuingia katika uhalisi wa ukweli. Jambo dogo kama hilo huufunua ubinadamu wa mtu, na pia hufunua kama mtu huyo hakika anapenda ukweli.

Kusimamia vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu ni jukumu ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kutimiza, na kila mmoja wa watu wateule wa Mungu anapaswa kwa pamoja kutoa usimamizi, msaada, na ushirikiano wa hali ya juu kabisa. Huu ni wajibu wa kila mtu. Watu wateule wa Mungu wanapaswa kuwa kielelezo. Wanapaswa kuanza na wao wenyewe—ni pale tu wanapofanya kazi nzuri wenyewe ndipo wanapostahili kuwasimamia wengine, na kutathmini kama kile ambacho wengine wanafanya kinafaa na kinapatana na kanuni. Hili ni jambo linalomhusisha kila mmoja, jambo hilo dogo linafichua ubinadamu wa watu, na vilevile na mtazamo wao kuelekea ukweli. Viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya kazi hii vizuri na kwa nguvu nyingi, kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu, na kila ndugu na dada wa kawaida anapaswa pia kulishughulikia jambo hili kwa ukali na tahadhari. Lazima ujichunguze mara kwa mara, uchunguze kama kuna matatizo katika ubinadamu wako na mawazo yako, na ni mtazamo wa aina gani ulio nao. Unapogundua kuwa kuna tatizo na mtazamo wako na mawazo yako, unapaswa kuomba haraka na ujigeuzena unaposimamia au kutumia vitu vya nyumba ya Mungu, unapaswa kujitahidi kwa kiasi fulani usikemewe na dhamiri yako wala kupungukiwa kuhusu Mungu, na kwa kiasi fulani kuheshimiwa na wengine na kuwafanya wakubali kile unachofanya, na kusema kwamba una ubinadamu, ambao unaonekana na wote. Jambo kuu ni kwa watu kuzingatia kanuni wanapofanya hili. Huu ndio wajibu ambao watu wanapaswa kutimiza, jambo ambalo mshiriki yeyote wa nyumba ya Mungu anapaswa kutimiza. Si jukumu la viongozi na wafanyakazi tu.

Je, sasa unaelewa zaidi kuhusu kipengee cha kumi cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi? Baada ya kuelewa kanuni, watu wanapaswa kuwa makini zaidi na waangalifu sana katika kufanya kazi hii, na wanapaswa kuishughulikia kwa bidii zaidi, na wasiwe wavivu—kisha wataweza kupunguza uharibifu na upotevu wa vitu vya maada vya nyumba ya Mungu, na kuvizuia kuchukuliwa na watu waovu. Hili linapaswa kuwa la kufikiwa. Kwa nini ninasema ni rahisi kufanikisha? Haya ni mambo ambayo maisha ya kila siku ya kila mtu nyumbani yanaweza kugusia. Ni rahisi kuwa makini katika kusimamia vitu vya nyumbani kwako mwenyewe, kwa hivyo ukilinda vitu vya nyumba ya Mungu kana kwamba ni vyako mwenyewe, kulingana na mahitaji ya nyumba Yake, uvitenge kwa busara, na uweze kupunguza uharibifu na upotevu, na usiwaruhusu watu waovu wavimiliki, basi utakuwa unatimiza jukumu la viongozi na wafanyakazi. Kazi hii inaonekana kwa asili yake kuwa kazi ya jumla. Kwa nini tunaiita kazi ya jumla? Inahusisha usimamizi wa vitu vya maada. Visimamie na uvigawe vizuri, na utakuwa unatimiza jukumu lako. Pia, kanuni ya kazi hii ni rahisi sana—inahusisha kanuni moja tu, na haihusishi ukweli mgumu. Mradi tu mtu ana mzigo na nia sahihi, anaweza kufanya kazi hii vizuri bila kuhitaji kuelewa ukweli mwingi sana, na bila kuhitaji ukweli mwingi afanyiwe ushirika nao. Kwa hivyo, kazi hii ni kazi moja, na ni kazi ya mambo ya jumla. Ni kazi ambayo ni rahisi kwa viongozi na wafanyakazi kufanya. Mradi tu wewe ni mwenye bidii kiasi, unauliza maswali zaidi, unafanya udadisi zaidi, ujishughulishe zaidi, na uwe na nia sahihi, unaweza kuifanya. Sio ngumu hata kidogo. Tumemaliza ushirika wetu kuhusu kipengele cha kumi cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Ni rahisi hivyo.

Mtazamo na Udhihirisho wa Viongozi wa Uwongo Kuhusiana na Nyenzo za Nyumba ya Mungu

Sasa kwa kuwa umeelewa jukumu hili la viongozi na wafanyakazi, kuhusu hilo, tutaendelea kuchanganua dhihirisho ambalo viongozi wa uongo huonyesha wanapofanya kazi hii, na mambo wanayofanya ambayo yanamaanisha kuwa wanaweza kutambuliwa kama viongozi wa uongo. Kwanza, viongozi wa uongo wanapofanya kazi hii, hawawezi kulinda vitu mbalimbali ipasavyo. Ulinzi ni kipengele cha kwanza cha kazi muhimu linapokuja suala la vitu vya maada vya kila aina. Viongozi wa uongo ni wavurugaji katika kila kitu wanachofanya; pamoja na kuzama kwenye kinamisi linapokuja suala la ukweli na kanuni mbalimbali zinazouhusisha, pia ni fujo linapokuja suala la kulinda vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu. Hawajui ni watu wa aina gani wa kuwatafuta ili kuvisimamia au jinsi vinavyopaswa kulindwa. Hawana malengo sahihi na mipango maalum, wala hatua za kina za kufanya kazi hii. Ikiwa kuna mtu aliye tayari kuchukua shida, vitu hivi vinaweza kulindwa; ikiwa hayupo, kiongozi wa uongo huacha vitu hivi viwekwe kando kwa njia ya kawaida. Hawapati mtu anayefaa kuvilinda au mahali pazuri pa kuvihifadhi, na sembuse hawafanyi ushirika juu ya kanuni mahususi za kuvilinda. Wakati huo huo, hawafanyi mipango yoyote ya kuwekwa, kutengenezwa, na kutengenezwa kwa vitu hivi vya maada katika siku zijazo. Baadhi ya viongozi wa uongo hata hawajui kabisa kuhusu ni vitu gani vilivyomo katika nyumba ya Mungu—hawajali kuhusu na hawaulizi kuhusu hili. Tuseme kwamba nyumba ya Mungu imechapisha vitabu vipya vya maneno ya Mungu, kwa mfano. Ni vitabu vingapi vilivyobaki baada ya kusambazwa, ni nani amepangwa kuvihifadhi, jinsi vinavyohifadhiwa, na kama vinahifadhiwa mahali pazuri—kiongozi wa uongo hatajua lolote kati ya mambo haya, wala hatauliza au kufanya uchunguzi kuvihusu. Kwa nini hatauliza? Anafikiri kwamba kulinda vitu vya maada vya nyumba ya Mungu ni jambo dogo, kwamba yeye ni kiongozi, mtu anayefanya mambo muhimu, ambaye huhubiri pekee. Hajali hata kidogo “mambo haya madogo,” lakini yeye huyatoa ili yafanywe na watu ambao hawaelewi chochote, na hajali kama yamefanywa vizuri au vibaya. Kwa hivyo, hachukui kazi ya kulinda vitu vya maada vya nyumba ya Mungu kwa uzito hata kidogo. Hii ni sababu moja. Nyingine ni kwamba baadhi ya viongozi wa uongo wamechanganyikiwa—akili zao zimevurugika. Hawana mawazo ya kawaida au ufahamu wa kulinda vitu, na hawana utaratibu au njia ya jinsi ya kulinda vitu vya nyumba ya Mungu. Hivyo, hawajui ni vitu vingapi kati ya hivi vimeharibika, na hawajui kama kuna matukio ya upotevu, pia. Wakati baadhi ya vitu vinachukuliwa na watu waovu, kiongozi wa uongo anasema, “Waache—hata hivyo, kila kitu kiko mikononi mwa Mungu.” Baadhi ya vitu muhimu hutumiwa na watu binafsi bila idhini ya mtu yeyote; watu hao huchukua vitu hivi, na wengine hawawezi kuvitumia katika kazi zao, na hakuna mtu anayethubutu kuviomba. Kiongozi wa uongo anasema, “Hakuna shida kubwa. Nunua tu kipya. Alichukua kitu hicho, kwa hivyo mwache akitumie kwanza. Ni kitu tu—ni sawa bila kujali ni nani anayekitumia. Ikiwa hakitumii kwa busara, hiyo ni kati yake na Mungu. Hakuna haja ya sisi kuingilia kati.” Tazama jinsi anavyohubiri fundisho kuu la “kushughulikia” suala hilo, akigeuza masuala makubwa kuwa madogo na kuyafanya madogo yasiwe kitu. Viongozi wa uongo hawatimizi majukumu yao yoyote linapokuja suala la kulinda vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu. Hawajali au kuuliza kuvihusu, na hawatatui au kushughulikia matatizo yoyote. Hata Aliye juu akiichunguza kazi yao, wanazungumza tu kwa kukwepa ili kumpa majibu yasiyoridhisha, na yanaishia hapo.

Baadhi ya ndugu hununua vifaa, nguo, na dawa kwa ajili ya matumizi ya nyumba ya Mungu, na kiongozi wa uongo anapoona vitu hivyo, yeye huvichunguza na kujichukulia nguo nzuri, viatu, na mifuko, na kuwaruhusu wengine kuchukua vitu vilivyobaki ambavyo wao wenyewe hawahitaji. Baradhuli wanaowaongoza wanapoona hili, wanasema, “Kiongozi wetu amechagua anachotaka—sasa, ni zamu yetu. Tukimaliza, tutavitupa vitu visivyo na thamani vilivyoachwa kwa ndugu na dada walio chini yetu.” Yeyote anayeangukiwa na vitu hivi, huyo ndiye anayevimiliki, na vitu vilivyobaki ambavyo hakuna mtu anayependa vinatupwa kando, na hakuna anayevilinda. Na kwa hivyo, vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu kwa kutaja tu vina nafasi za kulindwa, lakini kwa kweli, havilindwi hata kidogo—sehemu hizo ni mahali pa kutupa tu, bila mtu yeyote kuzisimamia. Wanatupa vitu mahali fulani na kuviache virundikane. Kuna nguo, viatu na soksi, dawa, na vifaa vya elektroniki, pamoja na bidhaa za kila siku na vyombo vya jikoni—ni mchanganyiko, wenye kila aina ya takataka ndani yake, na hata chakula cha watu na chakula cha mbwa huchanganywa. Ukiuliza ni nani anayesimamia vitu hivi na kama wao huvipanga; au kama kuna maagizo kuhusiana na vitu hivi, na jinsi vinavyohitaji kulindwa; au, ikiwa vitu hivi havihitajiki kwa kazi ya nyumba ya Mungu, kama ndugu na dada wanavihitaji—hakuna anayejua majibu. Ni jambo la kawaida kabisa kwa ndugu na dada kutojua, lakini viongozi na wafanyakazi pia hawana majibu ya maswali yoyote kati ya haya—wanakwepa kabisa kujumikia mambo haya, wakisema ama “Sijui,” au “Mtu anashughulikia hilo,” na hivyo kukupuuza wewe, na kuidanganya nyumba ya Mungu. Hili husababisha matatizo haya kutotatuliwa. Si vigumu kwa viongozi na wafanyakazi kupata watu wanaofaa wasimamie vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu, sivyo? Viongozi wa uongo hawafanyi hata kazi rahisi ya kumtafuta mtu mwaminifu wa kulinda vitu hivi ipasavyo, kuweka kumbukumbu nzuri na kuviweka katika mpangilio mzuri. Wao hufanya nini basi? Ndugu na dada wanapotoa nguo au mahitaji ya kila siku kwa ajili ya nyumba ya Mungu, na viongozi wa uongo wanapoona vitu hivi, wanawazunguka, kama kundi la mbwa mwitu wenye njaa wakila nyama pamoja. Wanajaribu mavazi yoyote yanayowafaa, wakirudia rudia, wakijichagulia vitu bila kikomo. Nyumba ya Mungu inaponunua mashine za aina tofauti na vifaa muhimu na vya gharama kubwa, wanakimbilia kujichagulia vilivyo vizuri kwanza. Kwa nini wanachagua vile vizuri? Wanafikiri kwamba kama kiongozi au mfanyakazi, wana haki za matumizi ya kibinafsi ya vitu vya nyumba ya Mungu. Chochote ambacho nyumba ya Mungu inatoa nacho, huwa wanachagua vitu bora kwanza. Hivi ndivyo wanavyoshughulikia vitu vya nyumba ya Mungu. Je, ni kufanya kazi? Je, hii si dhihirisho la viongozi wa uongo? Linapokuja suala la vitu vyenye tarehe za kuharibika—kwa mfano chakula na dawa—viongozi wa uongo hawajali. Hawatafuti wafanyakazi wanaofaa ili wasimamie, wala hawawaambii wafanyakazi, “Baadhi ya vitu hivi vina tarehe za kuharibika, kwa hivyo viweke kwenye rekodi mara moja. Harakisha kuvigawa kwa ndugu na dada kabla ya tarehe za mwisho wa matumizi, ili vitumike kwa busara—usingoje viharibike; usiache vipotee.” Viongozi wa uongo hawafanyi mambo haya kamwe. Kitu kinapoharibika, wanakitupa tu. Viongozi na wafanyakazi wanapofanya kazi katika nyumba ya Mungu, kwa uwazi kabisa, wanapaswa kuwa wasimamizi wa nyumba ya Mungu. Jambo la kwanza wanalopaswa kufanya ni kulinda kwa busara vitu vya nyumba ya Mungu, kuvilinda kwa uthabiti na kufanya uchunguzi sahihi katika suala hili. Hili pia ni jambo la msingi katika kazi ya nyumba ya Mungu, lakini viongozi wa uongo hawawezi hata kufanya kazi ya msingi kama hii. Je, wamechanganyikiwa, ni wenye ubora duni wa tabia, na wapumbavu—au je, mioyo yao haiko mahali pazuri? Ikiwa ni wapumbavu na waliochanganyikiwa, wanajuaje kujichagulia vitu vizuri? Kwa nini hawaachi vitu vyao wenyewe au kuwapa watu wengine kwa kawaida? Kwa nini hawaharibu au kuhasiri vitu vyao wenyewe? Na kwa nini huu ndio mtazamo wao kuelekea vitu vya nyumba ya Mungu? Ni wazi kwamba hawana maadili, na mioyo yao haiko mahali pazuri. Mara tu viongozi na wafanyakazi wanapopata hadhi, na kukutana na mawanda mapana ya kazi ya nyumba ya Mungu, wanapata fursa ya upendeleo ya kupata vitu mbalimbali vya kimwili na mali ya umma ya nyumba ya Mungu, na wao ndio wenye habari zaidi kuhusu vitu hivi. Na bado wanavipuuza, hawavilindi ipasavyo, na wanamruhusu mtu yeyote kuvitumia na kuvichukua, wanamruhusu yeyote aliye tayari kuvijali afanye hivyo, na ikiwa mtu hayuko tayari kuvijali na hana uwajibikaji, hajali, na hata akigundua kuwa mtu ana tatizo, hawalitatui. Hawa ni viongozi wa uongo. Katika hatua hii, tumehitimisha kwamba viongozi wa uongo, mbali na kuwa wenya ubora duni wa tabia na wasiobeba mzigo, pia mioyo yao iko mahali pabaya, na ni wenye tabia mbaya. Kwa kuwa viongozi hawa ni wenye ubora duni wa tabia na hawana uwezo wa kuelewa, kufanya kwao kazi mbaya katika kazi inayohusisha ukweli na kuingia katika uzima kunaeleweka. Na kwa kuwa wao ni wenye ubora duni wa tabia na hawana uwezo wa kufanya kazi, kufanya kwao kazi mbaya katika kazi inayohusisha utawala pia ni jambo ambalo linaweza kuvumiliwa. Lakini kutoweza kwao kufanya kazi inayohusisha kusimamia vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu—ambayo ndiyo kazi ndogo na rahisi zaidi—kunaonyesha jambo fulani kwa uwazi zaidi: Kwa baadhi ya viongozi wa uongo, tatizo lao si rahisi kama kuwa na ubora duni wa tabia na kutobeba mzigo, hata zaidi ni tabia yao duni na ubinadamu duni. Kupitia ushirika wetu kuhusu jukumu la kumi la viongozi na wafanyakazi, dhihirisho lingine la viongozi wa uongo limefunuliwa: Si tu kwamba ni watu wenye ubora duni wa tabia, wasiobeba mzigo, na wanaojishughulisha na starehe za kimwili—pia ni watu wenye tabia duni, na mioyo yao haiko mahali pazuri. Vitu visivyo vyao, hawavijali—hata hayawalindi. Umefanywa kuwa msimamizi wa nyumba ya Mungu, na bado unauuma mkono unaokulisha na huyalindi maslahi ya nyumba ya Mungu huku mkiishi kwa kuyategemea; unavitupa vitu vya nyumba ya Mungu pembeni, kana kwamba ni vya watu wa nje, na huvilindi, na unafikiri si jambo kubwa. Huku si kushindwa kutimiza majukumu yako—ni tatizo la ubinadamu wako, ni ukosefu mkubwa wa maadili! Kulinda vitu wanavyopaswa kuvilinda kwa namna mbaya, au kutovilinda, kunaonyesha kwamba viongozi wa uongo hawana ubinadamu, na kwamba mioyo yao haiko mahali pazuri. Hawawezi hata kulinda vitu vya nyumba ya Mungu vizuri, kwa hivyo ikiwa wangevigawa, je, wanaweza kufanya hivyo kwa busara? Wanashindwa hata kutenda kulingana na kanuni. Wanaona vitu vya nyumba ya Mungu vikitupwa ovyo, kuharibiwa, na kupotezwa, bila mtu yeyote mzuri wa kuvisimamia, na wanajua vizuri sana mioyoni mwao kwamba kufanya hivyo si sawa—lakini bado, hawashughulikii jambo hili. Hilo ni moyo wa mtu kuwa mahali pabaya. Je, wale watu wachafu, ambao mioyo yao iko mahali pabaya, wanaweza kutenga vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu kwa busara? Hawana uwezo wa kufanya hivyo—ukiwaachia wagawe vitu hivyo, watafanya mambo ambayo hayana maadili zaidi.

Katika shamba moja la kanisa linalofuga mbwa, mtu anayejukumikia kuwafuga anawajali sana watoto wa mbwa waliozaliwa. Alihofu kwamba watoto wa mbwa hawangeweza kupata lishe waliyohitaji, kwa hiyo aliomba mayai ya ogani ili mbwa wale. Kiongozi wa uwongo pale alitia sahihi ombi hilo mara moja; hakuwaza jinsi mayai ya ogani yalivyo haba. Hakuna hata ya kutosha watu kula, basi kwa nini awape mbwa? Je, hii si njia ya kipumbavu ya kushugulikia jambo hili? Je, tabia ya namna hii ya kiongozi huyo wa uwongo ni ipi? Je, inapaswa kuainishwaje? Je, utendaji huu wa kiongozi huyo wa uwongo sio wa kipumbavu? Anachokisema yule kiongozi wa uwongo wakati wote, kila anapoufungua mdomo wake, ni mafundisho yanayolingana na mapendeleo ya watu, lakini kwa kweli, haelewi hata kidogo kanuni za ukweli, basi jambo linapotendeka, wanalisogea na kulishughulikia kulingana na mawazo, mapendeleo, na matakwa ya binafsi ya binadamu—na hatimaye anakamilisha kufanya jambo kama hili la kuudhi kama vile kuwalisha mbwa mayai ya ogani. Je, ugawaji wa namna hii wa vitu vya nyumba ya Mungu na kiongozi huyo wa uwongo unazingatiwa kuwa kwa busara (Hapana.) Je, kwa nini hawezi kutimiza ugawaji wa busara? Kwa juujuu, inaonekana kiongozi huyo wa uwongo alikuwa anaingilia kati, anawajibika, na anafuatilia hata jambo hili dogo sana, na alikuwa na sababu kubwa na msingi wa kuunga mkono ombi hili—lakini, je, alikuwa akitenda kulingana na kanuni? Je, alikuwa akitenda kufuatana na kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu? Hapana. Kwa hiyo, kwa kuangalia asili ya hiki kitendo chake, ni tendo jema ama tendo ovu? Je ni timilisho la jukumu lake ama kutowajibika? Ni kutowajibika—ni kukosa msimamo, ni kufanya mambo maovu kwa kutojali! Kwa sababu ya jambo hili, je, unaona nini kuwa kiini cha ubinadamu wa kiongozi huyu wa uwongo? Je, sio ufahamu uliopotoshwa na kutumia kanuni bila kufikiri? Kile anachosema kwa kila pumzi ni mafundisho sahihi, na kinaonekana kana kwamba hakuna hata kifungu kisicho sahihi ndani yake, lakini kwa kweli, yamepotoshwa. Mtu kama huyo anajifanya wa kiroho na ana ufahamu uliopotoka—yeye ni mtu asiye na thamani anayekosa ufahamu wa kiroho. Tumetaja hivi punde kwamba ubinadamu wa viongozi wa uwongo ni kwamba wana hulka duni na mioyo yao iko mahali pabaya. Wanakosa kanuni inapofika wakati wa kugawa vitu vya nyumba ya Mungu, na wanavigawa bila kufikiri, jambo linaloonyesha kwamba viongozi wa uwongo wamepotoshwa katika ufahamu wao na kutumia kanuni bila kufikiri, na kwamba hawana maadili katika matendo yao—wanatenda tu bila kufikiri na bila mpango maalum. Viongozi wa uwongo wanaonekana kwa nje kuwa wakarimu na wema sana, huku kwa kweli huu ni ukarimu na wema wa uwongo. Kwa mfano, mbwa jike alipozaa watoto wa mbwa, mtunza mbwa alisema anapaswa kuwapa mbwa blanketi jipya lililotengewa watu. Kisha mtu fulani akasema, “Itasikitisha kuwapa mbwa blanketi jipya—itakuwa vyema zaidi kuwapa ndugu na dada badala yake, na kuwapa wanyama blanketi kuukuu tunayobadilisha.” Je, unaonaje kuhusu pendekezo hili? Kugawa vitu vipya kwa watu na vitu vya zamani kwa wanyama ni jambo la busara kabisa. Hii ndiyo kanuni; huu ni ugawaji wa busara. Je, viongozi wa uwongo wanashughulikia mambo kama haya vipi wanapokumbana nayo? Baada ya kusikia hili, kiongozi wa uwongo pale alitafakari: “Wanyama hawapati kamwe kutumia vitu vipya. Kila wakati wanatumia wakati vitu vya zamani, vitu vichafu. Sisi watu daima tunapata kutumia vitu vipya. Maneno ya Mungu yamesema kwamba wakati mwingine sisi si wazuri hata kama nguruwe au mbwa. Kwa hiyo, msipigane na nguruwe na mbwa juu ya vitu. Huko ni kukosa ubinadamu.” na hivyo, anaishia kuwapa blanketi mpya wanyama hao. Watu kule huenda hawakupoteza kwa kutumia ya zamani, lakini jinsi jambo hili lilivyoshughulikiwa linatoa mfano kweli wa suala hilo. Je, kiongozi wa uwongo alihusika kivipi katika jambo hili? Je, mnaweza kusema kwamba watu wa kawaida wanaweza kulifanya jambo kama hilo? (Hapana.) Je, ni watu wa namna gani, basi, wangeruhusu mambo yafikie hatua hii wakilishughulikia jambo hili? (Watu wa kipumbavu ambao hawana akili ama fikira za watu wa kawaida.) Majibu haya yote ni sahihi—watu hao hawana maana kabisa. Watu wa kawaida wanapokumbana na jambo kama hili, wanajua jinsi ya kulishughulikia kwa busara, lakini viongozi wa uwongo, wanaojifanya kuwa wa kiroho wenye ufahamu uliopotoka hawajui jinsi ya kulishughulikia. Namna yao ya kulishughulikia jambo hilo pia inaonekana kuwa na msingi, na pia inaonekana kubaliana na kanuni za nyumba ya Mungu, na inaungwa mkono na sababu nyingi zenye uthibitisho wa busara—lakini wanatoka katika sehemu hiyo kuisikia bila kujua wacheke au walie, ni jambo la kuchekesha sana. Inakuwaje kwamba hawawezi hata kuelewa mantiki rahisi na dhahiri? Je, wanaishiaje kulishughulikia kwa njia potovu hivyo? Linakera sana. Ukiwafanya watende kama wasimamizi, watawafanya mbwa wawakamate panya, paka walinde nyumba, na nguruwe vitandani—kila kitu kitavurugika. Je, viongozi wa uwongo wanaweza kugawa kwa busara vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu? (Hapana.) Ni watu wa aina tofauti, waliovurugika, na wapumbavu. Kando na wale viongozi wa uwongo wenye ufahamu uliopotoka hasa na mioyo yao mahali pasipostahili, wengi wa viongozi wa uwongo pia hufanya machafuko na mchanganyiko wa aina hii ya kazi, ingawa wana ubora wa tabia kiasi na hawajapotoshwa katika ufahamu wao. Hawawezi hata kutimiza majukumu madogo zaidi wanayopaswa kutimiza. Kwa hivyo, unapowauliza kuhusu kazi hii, jibu lao huwa ni lile lile kila mara: “Fulani-na-fulani anaifanya kazi hiyo. Fulani-na-fulani anajua. Ukiwa na maswali yoyote, itabidi niende nimuulize fulani-na-fulani.” Na huo utakuwa mwisho wa kusikia juu ya kazi hiyo. Huu ndio udhihirisho ambao viongozi wa uwongo huonyesha wanapofanya kazi hii.

Linapokuja suala la kazi ya kugawa vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu, viongozi wa uwongo hawawezi tu kufanya hivi kulingana na kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu, pia wanaruhusu hisia zao binafsi, mapendeleo, na tamaa zao nyingi, pamoja na ufahamu wao binafsi kuchanganyika katika hili. Wanafanya mchanganyiko na machafuko ya kazi hii, bila kanuni za kuzungumzia hata kidogo. Kwa hivyo, kiongozi wa uwongo anaposimamia vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu, mara nyingi hutukia, katika hali ambapo hakuna mtu anayejua kinachoendelea, kwamba vitu vinaharibiwa, vinatumiwa vibaya bila sababu, au kwamba vitu vinapotea na idadi hazilingani. Vitu vingine vinachukuliwa na watu binafsi kwa matumizi yao binafsi, bila wao kunukuu au kuripoti hili. Viongozi wa uwongo hawawezi hata kusimamia sehemu rahisi kama hii ya mambo ya jumla kufanya vizuri. Wanafanya machafuko katika kazi hii, lakini bado wanahisi kuwa watulivu, wakifikiri kwamba wamefanya kazi nyingi. Viongozi wa uwongo kamwe hawafanyi ukaguzi wa mara kwa mara, matengenezo, na utunzaji wa vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu; moyoni, hawajali hata kidogo kuhusu vitu hivi. Tuseme kwamba uwaulize, “Je, kuna mtu yeyote anayeshughulikia matengenezo na utunzaji wa vifaa hivi? Je, kumekuwepo na visa vya uharibifu katika kupata vipuri wakati wa kuvitengeneza? Au kwa mtu yeyote aliyetumia fedha kupita kiasi au kutapeliwa? Je, kuna mtu yeyote aliyewajibishwa baada ya matukio hayo? Je, kuna yeyote aliyetozwa faini au kupewa onyo?” Viongozi wa uwongo hawawezi kujua wala kujali lolote kati ya haya. Iwe pesa zilitumiwa kinyume cha sheria kununua vitu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iwe kuna yeyote ameteuliwa kusimamia vitu hivyo baada ya kununuliwa, kama vitu vilivyonunuliwa vinafaa na kama vinaweza kutumiwa kwa njia inayofaa, na, ikiwa sivyo, kama vilirudishwa au kubadilishwa ndani ya muda uliowekwa—hawajui lolote kati ya hayo. Ni wajinga sana—hawajui chochote. Kitu pekee ambacho viongozi wa uwongo wanawaza kuhusu ni jinsi ya kuhubiri mafundisho kwenye mikutano kuwafanya watu wawatukuze; hawana uwezo wa kufanya kazi linapofikia suala maalum la usimamizi wa vitu, wala hawana mtazamo wowote kuhusu jambo hili. Hawajui kwamba hii ni kazi wanayopaswa kuwa wanafanya, wala hawajui jinsi ya kuifanya. Maoni ambayo viongozi wa uwongo wanachukua juu ya vitu vya nyumba ya Mungu ni kwamba ni vya kila mtu, kwa hivyo yeyote ambaye angependa kutumia kitu anaweza kufanya hivyo, na yeyote anayehitaji kitu anaweza kukichukua au aombe kutoka kwa watu wa ngazi ya juu—kwamba hii ni haki ya kila mtu, na kwamba vitu vya nyumba ya Mungu havipaswi kuwa chini ya usimamizi au udhibiti wa mtu binafsi. Kwa hivyo, mtu akivunja au kupoteza mashine, hawajali, na mtu akiomba kununua kitu, hawajali ikiwa ni ghali au nafuu. Ukweli ni kwamba nyumba ya Mungu ina kanuni kuhusiana na mambo haya. Maadamu viongozi na wafanyakazi wanatimiza majukumu yao na wanafanya uhakiki ufaao kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu, hasara na uharibifu huo wote unaweza kuepukwa. Hata hivyo viongozi wa uwongo hawafanyi kazi hii rahisi ambayo inaweza kuzuia hasara. Je, si wanakula tu chakula cha nyumba ya Mungu bure? Je, si wanadoea bure? Je, huu si udhihirisho maalum wa “uwongo” wa viongozi wa uwongo? Je, mtawashughulikia vipi viongozi kama hao, mkikutana na mmoja? (Kwa kumtimua.) Kumtimua tu, na hakuna lolote zaidi? Je, hamfai kumfundisha jambo moja au mawili? “Mashine hiyo iliwekwa hapo, na ikapata unyevunyevu, na hakuna mtu aliyeiangalia kwa siku kadhaa. Haijulikani ikiwa umeme bado unafanya kazi, au ikiwa panya wametafuna nyaya. Kwa nini hujishughulishi na vitu hivi? Kompyuta ninayotumia imeharibika na inahitaji irekebishwe. Itachelewesha kazi ikiwa haitarekebishwa. Lakini nimetuma ombi kwako mara nyingi kwa ajili ya hiyo, kwa nini hujazingatia? Unajishughulisha na nini bila kufikiri siku nzima, kama kuku aliyekatwa kichwa? Wakati kiongozi kama wewe anategemewa kufanya kazi, unachelewesha kazi yote, na mashine na vitu vyote vinaharibiwa kwa mkono wako. Hutunzi au husimamii vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu. Hustahili kuwa kiongozi—Fanya upesi na ujiuzulu!” Je, ni sawa kumkaripia namna hii? (Ndiyo.) Je, ni kitu gani kinachomilikiwa na mtu anayethubutu kuwakaripia viongozi na wafanyakazi? Lazima kwanza awe jasiri, na lazima awe na hisia ya haki. Wengine wanaweza kusema, “Singethubutu kuwakaripia viongozi na wafanyakazi. Ni maofisa, na mimi ni askari tu, nafasi yangu ni ya chini sana kuliko yao. Wana ukweli na wanaweza kuhubiri mahubiri. Sina uwezo wa kitu chochote, na siko katika nafasi ya karipiakuwakaripia.” Je, haya si mantiki ya mshenzi? (Ndiyo.) Kwa hivyo, je, mngewezaje kumkaripia kiongozi wa aina hii, basi? “Ikiwa unaweza kufanya kazi hii, basi jaribu uwezavyo kuifanya, na uifanye kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu. Chochote unachopanga ili tufanye, tutatii. Lakini kama hujaribu uwezavyo kufanya kazi hii, usipoifanya kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu, hutawahi kutufanya tukusikilize! Zaidi ya hayo, ikiwa hufanyi kazi yoyote ya kweli, tuna haki ya kukutoa kwenye nafasi yako na kukuondoa! Jidhuru, ikiwa unataka kumdhuru mtu—usijaribu kutudhuru sisi sote.” Je, mngethubutu kuwakaripia namna hii (Ndiyo.) Unasema hivyo sasa, je, mngeweza kweli, wakati utakapofika kufanya hivyo? Kwa ujumla, Pamoja na mambo yanayogusa kanuni za kweli na mambo muhimu, hamthubutu kuzungumza kwa kawaida, kwa kuhofia kwamba ukosefu wa ufahamu, na uwazi katika kuzungumza, kunaweza kumaanisha kwamba mnatoa tu hukumu kwa viongozi na wafanyakazi na kusababisha usumbufu. Lakini mnapaswa kuwa na uwezo wa kufahamu suala la kusimamia vitu vya maada; mnapaswa mjifunze ufahamu katika jambo hili na mpate kufahamu kanuni zake.

Kulikuwa na mtu ambaye alikuwa akisimamia mavazi katika timu ya utengenezaji filamu. Alikuwa mtundu katika matendo yake, na kila mara akibadhiri vitu vya nyumba ya Mungu kisirisiri. Alipotoka katika timu ya utengenezaji filamu, alichukua baadhi ya vitu, na ukaguzi wa baadaye wa akaunti ulionyesha kwamba pesa nyingi alizopokea hazikuwa sawa. Zaidi ya hayo, ingawa hakuwa akifanya kazi, alikuwa na pesa, na pia alikuwa amenunua vitu vingi vya hali ya juu. Watu wengi walikuwa wamembembeleza alipokuwa katika timu ya utengenezaji filamu, na wote walitaka wawe na uhusiano mzuri na yeye, ili walipohitaji nguo, wangetakiwa tu kuomba, naye angewapa. Ikiwa mtu alikuwa na uhusiano mbaya naye, hata hangempa nguo ambazo alipaswa kupata. Hili ni tatizo gani? Ni tatizo na ufanyakazi wa usimamizi. Sehemu yake ni kwamba alikuwa akibadhiri vitu hivi yeye mwenyewe; sehemu nyingine ilikuwa kwamba hakugawa vitu vya nyumba ya Mungu kulingana na kanuni, lakini badala yake alifuata hisia zake, mapenzi yake mwenyewe, na mahusiano yake. Kwa mujibu wa kanuni, mtu huyu alipaswa atakaswe. Hili lilikuwa tatizo dhahiri. Kiongozi wa uwongo hakufanya hivyo tu, bali alimchukulia kuwa mtu mwema na akampangia kwenda mahali pengine afanye wajibu wake. Je, huku hakukuwa kuongeza kosa? Una maoni gani kuhusu jinsi kazi hii ilivyofanywa? Je, ililingana na kanuni? Je, kiongozi huyu alitimiza majukumu ambayo viongozi na wafanyakazi walipaswa kutimiza? (Hapana.) Tukiweka kando kwa sasa ni faida gani ambayo kiongozi angeweza kupata kwa kumshughulikia mtu huyo kwa njia hii—kuamua tu kutoka kwa jinsi alivyolishughulikia jambo hilo, asili ya jambo hili ilikuwa gani? Ilikuwa ni ile ya kumhifadhi mtu mwovu kulingana na hisia, na sio kumshughulikia kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu. Kwa hiyyo, ili kuunganisha hilo na kipengele cha kumi cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi, ni kosa gani ambalo kiongozi na mfanyakazi wa aina hii anafanya katika kushughulikia vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu? Je, kiongozi huyu alitimiza majukumu yake? Je, kushughulikia kwake kwa jambo hilo kulitegemea kulinda vitu vya nyumba ya Mungu? Hakika haikuwa hivyo. Hakuchukulia kwa uzito vitu vya nyumba ya Mungu, hata akapuuza akiruhusu vitu hivi viharibiwe au kuchukuliwa na mtu mwovu. Je, hivyo ndivyo angeishughulikia ikiwa vitu vyake mwenyewe vingeharibiwa au kuchukuliwa mikononi mwa watu wengine? Hapana—basi angewaza juu ya kulipiza kisasi na fidia. Kwa hivyo, kwa nini hakushughulikia vitu vya nyumba ya Mungu kwa njia hiyo? Hata alisema, “Anaweza kuchukua vitu vichache, akipenda—hachukui kiasi hicho. Anaweza kubadhiri vitu hivi kidogo, akipenda—ni nani asiye na tamaa kidogo ya kufanya hivyo? Kiasi kidogo anachobadhiri kina umuhimu gani? Si kana kwamba wengine wanapata kidogo.” Huu ni mtazamo wa aina gani? Je, huu ndio mtazamo ambao viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuwa nao kuhusu vitu vya nyumba ya Mungu? (Hapana.) Si wanauma mkono unaowalisha? Na mwishowe walitoa mantiki gani? “Mwacheni abadhiri vitu hivyo—hakuna haja ya sisi kupatanisha hesabu hizi naye. Je, fedha na vitu hivyo vidogo vinajumlisha nini? Wapinga Kristo wanabadhiri zaidi ya hiyo. Ubadhirifu wake wa vitu hivyo ni kati yake na Mungu—ni shughuli yake jinsi atakavyotoa hesabu mbele za Mungu, wakati utakapofika. Hilo halina uhusiano wowote nasi.” Je, ni mawazo na hisia gani mnapata baada kumsikia kiongozi akisema jambo kama hilo? Yeyote aliye na hisia zozote za haki, mwenye ufahamu mdogo wa dhamiri, angelia kindani akisikia maneno haya, na angehisi kuvunjika moyo na kusikitishwa, hata kama angekuwa mfuasi wa kawaida tu, sembuse kama angekuwa kiongozi au mfanyakazi! Kiongozi wa uwongo wa aina hii anafurahia neema na ulinzi wa Mungu sana, na ukweli Wake mwingi sana, lakini bado ana mtazamo wa aina hii wa kutojali kuhusu vitu vya nyumba Yake. Je, ana ubinadamu? Je, anafaa kuwa kiongozi au mfanyakazi? (Hapana.) Mara tu mtu kama huyo ametimuliwa, je, anastahili kuwa kiongozi au mfanyakazi katika wakati ujao? (Hapana—ubinadamu wake ni duni.) Je, ubinadamu wake duni unajidhihirikaje? (Katika kutotetea kwake masilahi ya nyumba ya Mungu.) Je, ni tendo gani maalum ambalo kwalo hatetei masilahi ya nyumba ya Mungu? Ni nini kiini cha udhihirisho huu maalum? Mioyo ya watu kama hawa haiko mahali panapostahili na ni wenye tabia duni; wanazungumza vizuri sana, lakini hawafanyi chochote cha kweli. Watu kama hao kamwe wasiwe viongozi na wafanyakazi. Wale ambao mioyo yao haiko mahali panapostahili si wapenda ukweli, bali wananuia tu kujinufaisha wao wenyewe; wale ambao mioyo yao haiko mahali panapostahili hawafikirii kamwe kuhusu watu wateule wa Mungu, na hawatetei kamwe kazi ya kanisa au masihali ya nyumba ya Mungu.

Jambo la kwanza la msingi ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya ni kuweka ulinzi ufaao juu ya vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu, wafanye ukaguzi ipasavyo na walinde nyumba ya Mungu, bila kuruhusu vitu vyovyote viharibiwe, vipotezwe, au vichukuliwe na watu waovu. Hiki ndicho kiwango cha chini wanachopaswa kufanya. Mara tu unapochaguliwa kama kiongozi au mfanyakazi, nyumba ya Mungu inakutazama wewe kama mtumishi Wake: Wewe ni wa tabaka la uwongozi, na wajibu unaobeba ni mzito kuliko ule wa wengine. Una jukumu kubwa. Ndiyo maana kila mtazamo wako, kila tendo lako, kila mpango wako wa kushughulikia masuala, na kila mbinu yako ya kutatua matatizo, yote yanahusisha masihali ya nyumba ya Mungu. Usipozingatia hata masilahi ya nyumba ya Mungu au kuyatia moyoni, hustahili kuwa mtumishi wa nyumba Yake. Je, huyu ni mtu wa aina gani? Kwa nini hafai kuwa mtumishi wa nyumba ya Mungu? Miongoni mwa viongozi wa uwongo, kuna wengine ambao si wenye ubora duni wa tabia tu—tatizo lao kubwa ni kwamba hawabebi mzigo wowote; hawajui jinsi ya kufanya kazi, lakini hawatafuti ukweli, na hawana uwezo wa kutimiza hata majukumu madogo ambayo mtumishi anapaswa kutimiza. Hawana dhamiri wala busara. Hii ni kwa sababu mioyo yao haiko mahali panapostahili, wana tabia duni, na ni wabinafsi na waovu; hawaitetei kazi ya kanisa hata kidogo, lakini mara nyingi wanaharibu na kusaliti masilahi ya kanisa, wakipata fadhila za watu na kudumisha uhusiano wao na watu wengine kwa gharama ya kuyadhuru masihali ya kanisa. Wanaruhusu vitu vya maada vya nyumba ya Mungu, kuvunjwa, kuharibiwa, kupotea, au hata kuchukuliwa mikononi mwa watu waovu, na hawajali kuhusu hili hata kidogo, au kuhisi hata kidogo kuwa na deni au hatia kuhusu hili. Kwa hivyo, linapokuja suala la kuwachagua viongozi na wafanyakazi, tukitazama hili kutoka kwa taswira ya ubinadamu, ni jambo gani la msingi zaidi wanalopaswa kuwa nalo? Ni lazima wawe na dhamiri na hisia ya haki, na nia zao zinapaswa kuwa zinazofaa. Ubinadamu wao lazima kwanza upite kipimo. Haijalishi ni uwezo kiasi gani wa kazi walio nao, au kiwango gani cha ubora wa tabia walicho nacho, watu wa aina hiyo watafikia kiwango kama watumishi ikiwa watatumika kama wasimamizi. Angalau, wataweza kutetea masilahi ya nyumba ya Mungu na masilahi ya kawaida ya ndugu na dada. Hawatayasaliti kabisa masilahi ya ndugu na dada, wala yale ya nyumba ya Mungu. Wakati masilahi ya nyumba ya Mungu na ndugu na dada yanapokaribia kupata madhara au uharibifu, watakuwa wamelifikiria kabla, na watakuwa wa kwanza kusonga mbele na kuwalinda, hata kama kufanya hivyo kutaathiri usalama wao wenyewe, au kuwahitaji walipe gharama au kuteseka. Yote haaya ni mambo ambayo watu wenye dhamiri na busara wanaweza kufanya. Viongozi na wafanyakazi wengine wa uwongo hukimbilia kutafuta mahali salama pa kujificha wanapokabiliwa na hali hatari, lakini wakiwa na vitu muhimu vya nyumba ya Mungu—vitabu vya maneno ya Mungu, simu za mkononi, kompyuta, na kadhalika—hawavijali wala kuviulizia. Ikiwa wangekuwa na wasiwasi kuhusu jinsi kukamatwa kwao kungeathiri uhalisi wa kazi ya kanisa, wangeweza kuwatuma wengine wayashughulikie mambo haya—lakini viongozi hawa wa uwongo wanajificha tu kwa ajili ya usalama wao wenyewe. Wana hofu ya kufa, na ili kuhakikisha usalama wao wenyewe, hawafanyi wawezavyo. Kwa hivyo kuna matukio mengi ambapo uzembe wa viongozi wa uwongo, kutotenda, na kutowajibika kunasababisha vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu na matoleo kwa Mungu kuporwa na kuchukuliwa na joka kuu jekundu wakati hali hatari zinapotokea, jambo ambalo husababisha hasara kubwa. Wakati hali hizo zimetokea tu kanisani, wazo la kwanza la viongozi na wafanyakazi linapaswa kuwa kuweka vifaa na vitu vya maada vya nyumba ya Mungu mahali panapostahili, ili kuvikabidhi kwa watu wanaofaa kwa ajili ya usimamizi; joka kuu jekundu lazima lisiruhusiwe kabisa kuvichukua. Lakini viongozi wa uwongo hawawazii mambo kama hayo kamwe; hawaweki masilahi ya nyumba ya Mungu kwanza, badala yake wao huweka usalama wao binafsi kwanza. Kushindwa kwa viongozi wa uwongo kufanya kazi ya kweli mara nyingi husababisha vitu mbalimbali muhimu vya nyumba ya Mungu kupata hasara au uharibifu. Je, huu si uzembe mkubwa katika jukumu kwa upande wa viongozi wa uwongo? (Ndiyo).

Kuhusu kipengele cha kumi cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi, ni dhihirisho gani kuu la viongozi wa uwongo tunalolifichua? Mtazamo wa viongozi wa uwongo kuelekea vitu vya maada vya nyumba ya Mungu ni wa kutojali na kutojali; hawafuati kanuni, bali wanagawa vitu hivyo bila mpangilio, kwa kuzingatia mawazo na mapendeleo yao wenyewe. Wanaposimamia mambo, vitu vya nyumba ya Mungu mara nyingi huathiriwa na uharibifu na upotevu mkubwa au mdogo, ambao husababisha hasara kwa kazi ya nyumba ya Mungu. Hili ndilo dhihirisho kuu la viongozi wa uwongo. Viongozi wa uwongo hawawezi hata kushughulikia kazi hii moja, rahisi ya mambo ya jumla; hawawezi hata kufanya hivyo au kufanya vizuri—wanaweza kufanya nini, basi? Kwa hivyo, unapoona watu kama hao wanatenda kama viongozi, unaweza (pl) kukagua na kusimamia kazi zao. Ikiwa watafanya fujo katika sehemu hii moja ya kazi ya mambo ya jumla, bila kufanya hata kile wanachoweza, na bila kutafuta watu wengine wanaofaa kufanya kazi hiyo wanapokosa muda, basi viongozi kama hao wanapaswa kufukuzwa na kuondolewa kwenye nafasi zao mara moja. Nyumba ya Mungu haitawatumia kamwe. Je, hili linafaa? (Ndiyo.) Kwa nini? Mtu ambaye moyo wake hauko mahali panapostahili, ambaye ufahamu wake umepotoshwa, na ambaye anatenda tu kulingana na hisia zake na tamaa zake za ubinafsi, za msingi na tamaa, si wa kuaminika. Je, mtu asiyeaminika anaweza kufanya kazi gani vizuri? Je, ni wajibu gani wanaoweza kufanya vizuri? Je, wana uwezo wa kufanya kazi kwa uaminifu? (Hapana.)

Kupitia ushirika wa leo kwenye kipengele cha kumi cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi, je, sijaweka wazi kanuni na viwango vingine vinavyohitajika kwa viongozi na wafanyakazi? Kinachohusika hapa si swala la ubora wa tabia, wala sio swali la uwezo wa kufanya kazi, bali ni swali la ubinadamu. Chunguza watu wanaohudumu kama viongozi na wafanyakazi, au wale ambao kanisa linawasitawisha, na uone kama kuna wowote miongoni mwao ambao wana ubinadamu duni na ambao mioyo yao haiko mahali panapostahili, ambao ubinadamu wao ni sawa na ule wa viongozi wa uwongo waliogawanywa katika kipengele cha kumi. Ikiwa kweli utapata viongozi na wafanyakazi kama hao, unapaswa kuwafukuza, na ni sharti ukumbuke kamwe kutowachagua watu wa aina hiyo kama viongozi, na kamwe kutowasitawisha watu wa aina hiyo kuwa viongozi na wafanyakazi. Ikiwa watu wengine hawaelewi ubora wa ubinadamu wa watu hao na wawachague, waripoti mara moja. Usiwape nafasi ya kuwa viongozi na wafanyakazi. Watu hao hawawi viongozi na wafanyakazi kufanya kazi ya kweli, bali kuharibu kazi ya kanisa. Ikiwa watakuwa viongozi, vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu vitaharibika tu baada ya hili. Je, mko radhi kuyaona matokeo kama haya? (Hapana.) Kwa hivyo, je, mnapaswa kuwatendeaje watu kama hao, basi? Ikiwa kwa sasa wanahudumu kama viongozi, waripoti na muwaondoe kwenye nyadhifa zao. Kama hawajachaguliwa, basi mwambie kila mtu: “Mtu huyu si mzuri. Msimchague, chochote mtakachofanya; kitakuwa na madhara kwa kanisa”. Na kama watu wamehadaiwa na kupotoshwa katika kuwachagua, lazima mjulishe kila mtu mara moja: “Tulifanya jambo baya leo. Tulimchagua mtu mwenye ubinadamu duni, ambaye moyo wake uko mahali pasipostahili, kama kiongozi wetu. Sasa kwa kuwa tumefanya hivi, masihali ya nyumba ya Mungu yatapata hasara na madhara. Tunapaswa tuwaondoe kutoka nyadhifa zao mara moja, ili kulinda maslahi na vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu zisiharibiwe. Hatupaswi tuwaache wafanikiwe na mpango wao.” Je, hili ni jambo linalofaa kufanywa? (Ndiyo.)

Wale walioteuliwa kama viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuwa na ubora wa tabia na uwezo wa kufanya kazi; sasa pia kuna mahitaji ya ubora wa ubinadamu wao. Mnasemaje, je, ndivyo hali ilivyo kwamba watu wengi hawatimizi vigezo vya kuwa viongozi na wafanyakazi? Ni lipi kati ya haya matatu ndilo muhimu zaidi? (Ubinadamu.) Na pili? (Uwezo wa kazi.) Baada ya hapo? (Kama wana ubora wa tabia au la.) Utaratibu huo ni sahihi kabisa. Unapochagua viongozi wakati ujao, wapime kulingana na utaratibu huu. Watu wangine husema, “Kuna tatizo na utaratibu huu. Tuseme kwamba ubinadamu unakuja kwanza, na kuna baadhi ya watu ambao wana ubinadamu lakini wenye ubora duni wa tabia, na ikiwa watachaguliwa kama viongozi, hawataweza kufanya kazi yoyote ya kweli—je, bado ni sawa kuzingatia ubinadamu wa watu wakati huo?” Ubinadamu wa watu ni wa muhimu sana, na ni jambo la kwanza unalopaswa kuangalia, lakini si jambo pekee la kuzingatia unapochagua viongozi na wafanyakazi. Ikiwa ubinadamu wa mtu unafikia kiwango, kinachofuata angalia uwezo wake wa kufanya kazi. Iwapo hana uwezo wa kufanya kazi, na hawezi kufanya kazi yoyote ya kweli, unaweza kumwomba afanye kazi isiyozidi uwezo wake. Iwapo ana ubinadamu mzuri, na ana uwezo wa kubeba kazi na anajaribu awezavyo kuifanya vyema, na ni mtu mwenye kuaminika, na nyumba ya Mungu haina haja ya kuwa na shaka kumtumia, na anaadilisha, anasaidia, na ni wa msaada kwa akina ndugu na dada wengi kabisa, basi anafikia kiwango kinachohitajika. Ikiwa ana ubora duni wa tabia na hana uwezo wa kufanya kazi, au ikiwa ni wastani tu kulingana na uwezo wake wa kufanya kazi, mwelekeze afanye kazi rahisi au kazi moja. Ikiwa ana ubora mzuri wa tabia na uwezo mkubwa wa kufanya kazi, anaweza kufanya kazi fulani muhimu au kazi kadhaa tofauti. Je, huwezi hata kupanga matayarisho ya namna hii? Ikiwa ana ubinadamu duni na moyo wake hauko mahali panapostahili, basi haijalishi uwezo wake wa kufanya kazi ni mkubwa kiasi gani, je, ataweza kufanya kazi hiyo vizuri? (Hapana.) Iwapo angesimamia kampuni au wafanyakazi wachache, kuna uwezekano hilo lisiwe tatizo—lakini ni masuala yapi yanayoweza kutokea iwapo angeombwa asimamie vitu mbalimbali vya maada vya nyumba ya Mungu? Kwanza, hangesimamia kabisa vitu hivyo au kuyashughulikia mambo kulingana na kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu. Moyo wake hauko mahali panapostahili, hapendi ukweli, na hakuna chochote ila hila ndani ya moyo wake, si kitu isipokuwa dhana na mawazo maovu, hivyo kila anapotenda, anafanya hivyo kulingana na mapendeleo yake mwenyewe, na kwa kuzingatia masilahi yake mwenyewe, si kwa kuzingatia kanuni za ukweli, wala kwa haki. Anazingatia tu kile anachopoteza au kupata, na hafikirii kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu—na hivyo amekusudiwa kushindwa katika kazi ya viongozi na wafanyakazi. Je, hili limeamuliwa na nini? Linaamuliwa na ubora wa ubinadamu wake; halijaamuliwa na uwezo wake wa kufanya kazi. Na kwa hivyo, unapopima kama mtu fulani ni mwema au duni, na kama anafikia viwango vya nyumba ya Mungu kwa ajili ya uteuzi wa viongozi na wafanyakazi, kwanza angalia ubinadamu wake: Ikiwa ubinadamu wake ni wa kutegemewa na unafikia kiwango kinachostahili, kinachofuata fikiria kama ana uwezo wa kufanya kazi na ana mzigo; kisha zingatia vipengele vingine.

Hiki ni kipengele cha kumi cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Hii ni zaidi au chini ya kile kilichochambuliwa katika kipengele cha kumi cha maonyesho mbalimbali ya viongozi wa uwongo. Mtu anaweza kuona katika mtazamo na maonyesho ambayo viongozi wa uwongo wanashughulikia vitu vya maada vya nyumba ya Mungu, kwamba wengi wao hawana dhamiri na busara, kwamba wao wana ubinadamu duni sana na hawawajibiki—unaweza kusema mioyo yao iko mahali pasipostahili. Je, sasa hatuna ushahidi mmoja zaidi ambao unaweza kutumika kuamua kwamba mtu fulani ni kiongozi wa uwongo? Viongozi wengine wa uwongo hawawezi kufanya kazi kwa sababu wana ubora duni wa tabia, na kwa sababu wao ni vipofu na hawana ufahamu kuhusu mambo. Wengine hawafanyi kazi ya kweli kwa kuwa mioyo yao haiko pahali panapostahili, na wapo kwa ajili ya manufaa yao pekee—hawatetei masihali ya nyumba ya Mungu, na hawajali ikiwa watu wateule wa Mungu wanaishi au kufa. Kila aina ya kiongozi wa uwongo lazima atimuliwe na aondolewe haraka iwezekanavyo, ili kuzuia kucheleweshwa kwa kazi ya nyumba ya Mungu na madhara kwa watu Wake wateule.

Mei 1, 2021

Iliyotangulia: Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (6)

Inayofuata: Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (21)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp