Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (21)

Jinsi ya Kuwatofautisha Wapinga Kristo na Watu Wenye Tabia ya Wapinga Kristo

Kuwatofautisha kwa Msingi wa Mitazamo Yao Kuelekea Ukweli

Leo tutaendelea kushiriki juu ya majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Kabla ya kuanza rasmi ushirika, hebu tupitie mojawapo ya mada kuhusu wapinga Kristo ambayo ilifanyiwa ushirika hapo awali: jinsi ya kuwatofautisha watu wenye tabia ya mpinga Kristo na wale wenye kiini cha mpinga Kristo, na tofauti kati ya watu wa aina hizi mbili ni zipi. Kwanza, tutashiriki juu ya jinsi ya kuwatambua wapinga Kristo; hili si jambo gumu sana. Kwanza kabisa, unapaswa kuona waziwazi ni udhihirisho upi bainifu ambao wale walio wapinga Kristo huonyesha, ili uweze kumtambua mpinga Kristo halisi kwa muda mfupi, ukiamua kwamba kwa hakika yeye si mtu aliye na tabia ya mpinga Kristo pekee au mtu anayetembea katika njia ya mpinga Kristo. Kwa njia hii, utakuwa na utambuzi kuhusu wapinga Kristo na hutapotoshwa, kutegwa, na kudhibitiwa nao tena. Sasa jambo la muhimu zaidi ni kuweza kutofautisha tofauti dhahiri kati ya watu wenye kiini cha asili ya mpinga Kristo na wale wenye tabia ya mpinga Kristo. Ili kuwatambua watu wa aina hizi mbili, ni lazima kwanza mfahamu sifa zao kuu. Watu wengine hufahamu tu udhihirisho wa upotovu wa wapinga Kristo katika maisha ya kila siku, kama vile tabia zao za kupenda hadhi na kupenda kuwakaripia wengine, lakini hawawezi kutambua kiini cha asili cha wapinga Kristo. Je, hili linafaa? (Hapana.) Pia kuna wale wanaosema kwamba udhihirisho unaojitokeza zaidi wa wapinga Kristo ni kiburi na majivuno yao, na huwaainisha watu wote wenye kiburi na majivuno kama wapinga Kristo. Je, hili ni sahihi? (Hapana.) Kwa nini si sahihi? Kwa sababu kiburi na majivuno sio udhihirisho unaojitokeza zaidi wa wapinga Kristo; ni tabia potovu zinazoshirikiwa na wanadamu wote waliopotoka. Kila mtu ana tabia ya kiburi na majivuno, kwa hivyo kuwaainisha watu wote wenye kiburi na majivuno kama wapinga Kristo ni kosa kubwa. Basi, ni udhihirisho upi ndio udihirisho wa msingi wa wapinga Kristo, unaoweza kufanya tofauti za kiini kati ya wapinga Kristo na watu wenye tabia ya mpinga Kristo kuwa wazi kwa kwa tazamo la haraka, na kumwezesha mtu kutambua kwamba viini vya watu wa aina hizi mbili ni tofauti, na kwamba watu kama hao wanapaswa kutendewa tofauti? Katika nyanja fulani, kama vile matendo, mwenendo, na tabia, je, watu wa aina hizi mbili wanafanana? (Ndiyo.) Ikiwa hamtazami kwa makini, hamtofautishi kwa uzito, au hamna ufahamu sahihi na utambuzi wa tabia na kiini cha watu wa aina hizi mbili mioyoni mwenu, ni rahisi sana kuwatendea kana kwamba walikuwa wa aina moja. Mnaweza hata kumchukulia kimakosa mpinga Kristo kama mtu mwenye tabia ya mpinga Kristo na kinyume chake, yaani, ni rahisi kufanya hukumu potovu za aina hii. Basi, ni sifa na tofauti zipi kuu kati ya watu wa aina hizi mbili zinazoweza kumruhusu mtu kutofautisha kwa ushahidi thabiti nani ni mpinga Kristo na nani ni mtu mwenye tabia ya mpinga Kristo? Hampaswi kuwa wageni kwa mada hii, kwa hivyo hebu tusikie mawazo yenu. (Nyanja moja inayotumika kutofautisha kati ya wapinga Kristo na watu wenye tabia ya mpinga Kristo ni kupitia mtazamo wao kuelekea ukweli; nyingine ni kupitia ubinadamu wao. Katika mtazamo wao kuelekea ukweli, wapinga Kristo huuchukia ukweli na hawaukubali kabisa. Haijalishi wametenda matendo mangapi maovu yanayosababisha vurugu na usumbufu, na haijalishi jinsi mnavyoshiriki nao au kuwapogoa, hawakubali hilo na wanakataa katakata kutubu. Watu wenye tabia ya mpinga Kristo wanaweza pia kufanya mambo mabaya wasipoelewa ukweli au kufahamu kanuni, lakini wanapopogolewa, wanaweza kuukubali ukweli, kujitafakari na kujijua wenyewe, na wanaweza kuhisi majuto na kutubu. Kwa mtazamo wa mwelekeo wao kuelekea ukweli, kiini cha wapinga Kristo ni kwamba wanauchukia ukweli, huku watu wenye tabia ya mpinga Kristo wanaweza kuukubali ukweli. Kwa mtazamo wa ubinadamu wao, wapinga Kristo ni watu waovu wasio na hisia ya dhamiri au hawajui aibu, ilhali watu wenye tabia ya mpinga Kristo wana dhamiri na hisia ya aibu.) Mmetaja sifa mbili; je, maudhui haya yalifanyiwa ushirika hapo awali? Je, hizi zinachukuliwa kuwa sifa dhahiri? (Ndiyo.) Mitazamo ya wapinga Kristo na watu wenye tabia ya mpinga Kristo kuelekea ukweli ni tofauti kabisa. Hili ni jambo muhimu sana, na ni udhihirisho wenye sifa dhahiri. Wapinga Kristo wanauchukia ukweli na hawaukubali kabisa. Afadhali wafe kuliko kukubali kwamba maneno ya Mungu ni ukweli. Haijalishi jinsi mnavyoshiriki kuhusu ukweli, wao hupinga na kuuchukia ndani yao. Wanaweza hata kuwatukana kwa ndani, kuwadhihaki, na kuwadharau, wakiwatendea kwa dharau. Wapinga Kristo wana uhasama na ukweli; hii ni sifa dhahiri. Na sifa za watu wenye tabia ya mpinga Kristo ni zipi? Ili kuwa sahihi na wasio na upendeleo, watu wenye tabia ya mpinga Kristo lakini walio na dhamiri na busara kiasi wanaweza kubadilisha mawazo yao na kuukubali ukweli kupitia wengine wanaoshiriki ukweli nao. Wakipogolewa, wanaweza pia kutii. Yaani, maadamu watu wenye tabia ya mpinga Kristo wanamwamini Mungu kwa dhati, wengi wao wanaweza kuukubali ukweli kwa viwango tofauti. Kwa muhtasari, watu wenye tabia ya mpinga Kristo wanaweza kuukubali ukweli na kutii kupitia njia kama vile kusoma maneno ya Mungu wenyewe, kukubali nidhamu na nuru ya Mungu, au upogoaji, usaidizi, na utegemezo kutoka kwa ndugu na dada. Hii ni sifa dhahiri. Wapinga Kristo, hata hivyo, ni tofauti. Haijalishi ni nani anayeshiriki ukweli, wao hawasikilizi wala kutii. Wana mtazamo mmoja tu: Afadhali wafe kuliko kuukubali ukweli. Haijalishi jinsi mnavyowapogoa, haina maana. Hata mkishiriki ukweli kwa uwazi iwezekanavyo, hawaupokei; hata wanaupinga na kuuchukia kwa ndani. Je, mtu mwenye tabia kama hiyo anayeuchukia ukweli anaweza kumtii Mungu? La hasha. Kwa hivyo, wapinga Kristo ni maadui wa Mungu, na wao ni watu wasioweza kuokolewa.

Kuwatofautisha Kwa Msingi wa Ubinadamu Wao

Muda mfupi uliopita, ninyi pia mlitaja sifa nyingine ya kuwatofautisha wapinga Kristo na watu wenye tabia ya mpinga Kristo, ambayo ni kwa mtazamo wa ubinadamu. Nani angependa kushiriki zaidi kuhusu sifa hii? (Wapinga Kristo wana ubinadamu mwovu hasa; wanaweza kuwakandamiza na kuwatesa watu, na haijalishi wametenda uovu kiasi gani, hawajui kutubu.) Hiyo ni kweli, sifa kuu ya wapinga Kristo ni ubinadamu wao mwovu, kutokuwa na aibu kwao, na ukosefu wao wa dhamiri na busara. Haijalishi wametenda matendo mangapi maovu kanisani au wamesababisha uharibifu kiasi gani kwa kazi ya kanisa, hawafikiri ni aibu, wala hawajioni kama wenye dhambi. Iwe nyumba ya Mungu inawafichua au ndugu na dada wanawapogoa, wao hawatingishiki, na hawahisi kulaumiwa au kuhuzunika. Huu ni udhihirisho wa wapinga Kristo kwa upande wa ubinadamu. Sifa zao kuu ni ukosefu wa dhamiri na busara, na ukosefu wa aibu, na tabia ya kishenzi kupita kiasi. Mtu yeyote anayegusa maslahi yao huhukumiwa na kuteswa nao, na wana hamu kubwa hasa ya kulipiza kisasi, hawamsazi yeyote, hata jamaa zao wenyewe. Hivi ndivyo wapinga Kristo walivyo washenzi. Kwa upande mwingine, watu wenye tabia ya mpinga Kristo, bila kujali ni upotovu kiasi gani wanaofichua, si lazima wawe watu waovu. Haijalishi wana mapungufu au kasoro gani katika ubinadamu wao, ni makosa gani wanayoweza kufanya, au ni katika nyanja zipi wanaweza kushindwa na kujikwaa, wanaweza kujitafakari na kujifunza mafunzo baadaye. Wanapokabiliwa na kupogolewa, wanaweza kukubali makosa yao na kuhisi majuto; na ndugu na dada wanapowakosoa au kuwafichua—ingawa wanaweza kujaribu kujitetea kidogo na kutokuwa tayari kukubali wakati huo—kwa kweli tayari wanakuwa wamelikubali kosa lao mioyoni mwao na wametii. Hili linathibitisha kwamba bado wanaweza kuukubali ukweli na wanaweza kuokolewa. Wanapofanya makosa au kukumbana na matatizo yoyote, dhamiri na busara zao bado zinaweza kufanya kazi; wanatambua, sio wenye ganzi na wasio na hisia, au wakaidi na wanaokataa kukubali mambo. Zaidi ya hayo, ingawa watu wa aina hii wana tabia ya mpinga Kristo, wao ni wenye huruma kiasi na wema kiasi. Wanapokumbana na mambo mbalimbali, sifa wanazoonyesha kwa upande wa ubinadamu zinaweza kuelezewa—kwa njia inayofaa zaidi na rahisi kueleweka—kama wenye busara kiasi. Wakipogolewa vikali, kwa kiwango cha juu wanaweza kuhisi uchungu kidogo mioyoni mwao, lakini ukilitazama kutokana na udhihirisho wa ubinadamu wao, inaweza kuonekana bado wanajua aibu, kwamba dhamiri yao inaweza kuwahukumu, na kwamba busara yao inaweza kuwa na athari fulani ya kuzuia. Wakileta hasara kwa maslahi ya nyumba ya Mungu au kuwadhuru ndugu na dada wowote, daima wanasumbuka moyoni na wanahisi kwamba wamemkosea Mungu. Watu wenye tabia ya mpinga Kristo hufunua udhihirisho huu kwa viwango tofauti. Hata kama hawafanyi marekebisho mara moja au kufanya chaguo sahihi na kutenda kwa usahihi baada ya mambo kutokea, watu hawa bado wana hisia ya utambuzi mioyoni mwao. Dhamiri yao huwashtaki; wanajua wamekosea na hawapaswi kutenda hivyo tena, na pia wanahisi kwamba wao si watu wema—kwa njia isiyo dhahiri, wote wanaweza kuwa na hisia hizi. Zaidi ya hayo, baada ya muda, hali yao itageuka, na watakuwa na toba ya kweli. Watahisi majuto makubwa, wakijutia kwamba hawakufanya chaguo sahihi au kutenda kwa usahihi hapo awali. Udhihirisho huu hasa ndio udhihirisho wa kawaida na wa kawaida zaidi wa wanadamu waliopotoka. Hata hivyo, wale walio wapinga Kristo ni wa kipekee; sio wanadamu bali ni mashetani. Haijalishi ni muda gani unapita baada ya wao kutenda uovu au dhambi, hawana majuto hata kidogo; wanabaki kuwa wakaidi na wenye kung'ang'ania kufanya mambo hadi mwisho. Watu wenye tabia ya mpinga Kristo wanaweza kutii wanapokumbana na upogoaji wa kawaida. Wanapokabiliwa na upogoaji mkali, wanaweza kujitetea, kukana mambo, na kukataa kulikubali wakati huo, lakini baadaye wanaweza kujitafakari na kujijua wenyewe, na kuhisi majuto na kutubu. Hata kama mtu anawadhihaki na kuwahukumu kuwa hawana ubinadamu, wanaweza kuhisi maumivu mioyoni mwao lakini hawatapinga au kumchukulia mtu huyo kama adui. Wanaweza pia kumwelewa mtu yule mwingine, wakiwaza, “Ninapaswa kujilaumu mwenyewe kwa kufanya kosa hilo; jinsi wengine wanavyonitendea, hilo halipiti kiasi.” Udhihirisho huu hujifunua kwa viwango tofauti katika watu tofauti. Kwa muhtasari, haya ndiyo madhihirisho ya kawaida na ya asili ya watu wenye tabia ya mpinga Kristo, watu wenye tabia potovu, na hapa ndipo wanapotofautiana waziwazi na wapinga Kristo. Kupitia udhihirisho tofauti wa hali hizi mbili, inakuwa wazi mara moja ni watu gani hasa walio watu waovu na wapinga Kristo, na ni watu gani walio na tabia ya mpinga Kristo tu lakini si watu waovu.

Kuwatofautisha Kwa Msingi wa Kama Wanatubu Kweli au Hawatubu

Vipengele viwili vya tofauti kati ya wapinga Kristo na watu wenye tabia ya mpinga Kristo zimetajwa hivi punde: Kipengele cha kwanza ni mtazamo wao kuelekea ukweli; mtazamo wa watu kuelekea ukweli ni mtazamo wao kuelekea Mungu. Katika kipengele hiki, kuna tofauti ya wazi kati ya watu wa aina hizi mbili. Pili, kwa upande wa ubinadamu, watu wa aina hizi mbili pia wana tofauti ya wazi ya kiini. Sifa hizi mbili ni dhahiri sana; wao ni watu wa aina tofauti kabisa. Mbali na tofauti hizi mbili, kipengele kingine ni iwapo kuna udhihirisho wowote wa toba baada ya kutenda uovu. Kwa upande wa wale walio wapinga Kristo, haijalishi ni matendo gani maovu wanayotenda—iwe wanawatesa watu, wanaanzisha falme zinazojitegemea, wanashindana na Mungu kwa ajili ya hadhi, wanaiba sadaka, au kitu kingine chochote—hata wakifichuliwa moja kwa moja, hawayakubali matendo haya. Ikiwa hawayakubali, wanaweza kutubu? Afadhali wafe kuliko kutubu. Hawakubali ukweli wa matendo yao maovu. Hata wakitambua kwamba ufichuzi huo ni sahihi kabisa, wao hupinga na kuukataa. Hawatajitafakari kamwe iwapo wako kwenye njia isiyo sahihi au kusema, “Nimehukumiwa kuwa mpinga Kristo. Hili ni hatari sana, na ninahitaji kutubu.” Hawana kabisa mawazo ya aina hii akilini mwao. Ubinadamu wao hauna sifa hizi. Kwa hivyo, wapinga Kristo wana sifa dhahiri: Haijalishi wanamwamini Mungu kwa miaka mingapi, hawaupokei ukweli hata kidogo na hawaonyeshi mabadiliko ya kweli. Wanapoanza kumwamini Mungu kwa mara ya kwanza, wanapenda kujitokeza miongoni mwa umati, kushindania mamlaka na faida, kuwatesa watu, na kuunda vikundi na kuligawanya kanisa. Lengo lao katika kujaribu kushikilia mamlaka ni kulitegemea kanisa na kuanzisha ufalme unaojitegemea. Baada ya miaka mitatu hadi mitano ya kuamini, unapowaona tena, bado wanaonyesha udhihirisho na sifa hizi zilezile bila mabadiliko yoyote. Hata baada ya miaka minane au kumi, wanabaki vilevile. Watu wengine husema, “Labda watabadilika baada ya miaka 20 ya kuamini!” Je, wanaweza kubadilika? (Hapana.) Hawatabadilika. Wanaonyesha udhihirisho huu huu iwe wanashirikiana na watu wachache au na walio wengi, iwe wanafanya wajibu wa kawaida au wanatenda kama viongozi au wafanyakazi. Hawatubu kamwe wala kurudi nyuma, wakiendelea katika njia ileile hadi mwisho. Hawatatubu kamwe. Hivi ndivyo wapinga Kristo walivyo. Kwa upande wa watu wenye tabia ya mpinga Kristo, hata kama wengine si watu waovu, wao pia wana tabia potovu. Wanafunua kiburi, udanganyifu, ubinafsi, udhalili, na aina nyingine za upotovu. Wanaonyesha pia ubinadamu duni. Wanapoanza kumwamini Mungu kwa mara ya kwanza, wao pia wanataka kushindania umaarufu na faida, kujitokeza ili kupata sifa za watu, na wana tamaa ya makuu na matamanio ya kuwa viongozi na kushikilia mamlaka. Udhihirisho huu upo kwa viwango tofauti katika wanadamu waliopotoka na sio tofauti sana na ule wa wapinga Kristo. Hata hivyo, katika mchakato wa kumwamini Mungu, wanaelewa baadhi ya kweli kwa kupitia hukumu na ufichuzi wa maneno ya Mungu, na wanafunua tabia hizi potovu kwa uchache zaidi na zaidi. Kwa nini tabia hizi potovu hufunuliwa kwa uchache zaidi na zaidi? Ni kwa sababu baada ya kuelewa ukweli, wanatambua kwamba mwenendo na udhihirisho huu ni ufichuzi wa tabia potovu. Ni wakati huu tu ndipo dhamiri yao inapata utambuzi, na wanaona kwamba wamepotoka sana na kwa kweli wanakosa mfano wa mwanadamu. Kisha wanakuwa tayari kufuatilia ukweli na kufikiria jinsi ya kutupa mbali tabia hizi potovu, na jinsi wanavyoweza kujiweka huru kutoka kwa utumwa wa tabia hizo potovu, na kuwa mtu anayefuatilia na kutenda ukweli. Huu ni udhihirisho gani? Je, si huku ni kutubu hatua kwa hatua? (Ndiyo.) Katika mchakato wa kupitia kazi ya Mungu, wanagundua matatizo yao wenyewe, wanatambua tabia zao potovu, na kuelewa hali zao mbalimbali. Pia wanakuja kukijua kiini cha ubinadamu wao, na dhamiri yao inapata utambuzi unaoongezeka; wanahisi zaidi na zaidi kwamba wamepotoka sana na hawafai kutumiwa na Mungu na kwamba wamepata chuki ya Mungu, na wanajichukia kwa ndani. Bila kujua, hatua kwa hatua, wanatubu ndani kabisa ya mioyo yao, na kwa toba hii, mabadiliko madogo hutokea, mabadiliko madogo ambayo yanaweza kuonekana katika mwenendo wao. Kwa mfano, hapo awali, mtu alipofichua matatizo yao, wangehisi uchungu, kughadhibika kwa aibu, na kujaribu kujieleza na kujitetea, wakifanya kila juhudi kupata visingizio na sababu mbalimbali za kujitetea. Kwa njia ya upitiaji unaoendelea, hata hivyo, wanakuja kutambua kwamba mwenendo huu si sahihi na wanaanza kurekebisha hali na mwenendo huu, wakifanya kazi kwa bidii kukubali maoni sahihi, wakijitahidi kwa ushirikiano wenye upatanifu na wengine. Mambo yanapowapata, wanajifunza kutafuta na kushiriki na wengine, na wanajifunza kuwasiliana kutoka moyoni na kupatana kwa amani na wengine. Je, haya ni madhihirisho ya toba? (Ndiyo.) Baada ya kumwamini Mungu, hatua kwa hatua, wanapata ufahamu wa kweli wa baadhi ya tabia, mwenendo na udhihirisho wa mpinga Kristo ambao wanafichua. Kisha, hatua kwa hatua wanatupa mbali tabia zao potovu, na wanaweza kuacha njia zao za awali zisizo sahihi za kuishi, na kuacha kufuatilia umaarufu na hadhi, na wanaweza kutenda, kujiendesha, na kufanya wajibu wao kulingana na kanuni za ukweli. Mabadiliko kama haya hufikiwaje? Je, hufikiwa kupitia kuukubali ukweli na kujibadilisha na kutubu bila kukoma? (Ndiyo.) Mambo haya yote hufikiwa katika mchakato wa toba endelevu. Hatimaye, hali yao hakika inaimarika, kimo chao pia kinakua kadiri upitiaji wao unavyoongezeka, na mambo yanapowapata, wanaweza kujitafakari. Iwe wanakumbana na vikwazo au kushindwa, au wanapogolewa, wanayaleta mambo haya mbele za Mungu na kumwomba Yeye, na wanaweza pia kuhusisha, kuchanganua, na kuielewa hali yao potovu wanaposoma maneno ya Mungu. Ingawa bado wanaweza kufichua upotovu na kuwa na mawazo yasiyo sahihi mambo yanapowapata, wanaweza kujitafakari na kujiasi wenyewe. Maadamu wanatambua masuala haya, wanaweza kuutafuta ukweli bila kuacha ili kuyatatua na kutenda toba. Ingawa maendeleo haya ni ya polepole sana na matokeo ni madogo, wanabadilika ndani kabisa ya mioyo yao bila kuacha. Watu wa aina hii daima hudumisha mtazamo na hali ya bidii, chanya, na ya kujisukuma ya kugeuka na kujirejea na kutubu. Ingawa wakati mwingine wanashindana na wengine kwa ajili ya umaarufu na hadhi na kufichua baadhi ya udhihirisho na matendo ya wapinga Kristo kwa viwango tofauti, baada ya kupitia upogoaji, hukumu, na maadibisho, au nidhamu ya Mungu, tabia hizi potovu hutupwa mbali na kugeuzwa kwa viwango tofauti. Chanzo kikuu cha kufikiwa kwa matokea haya ni kwamba watu wa aina hii wanaweza, ndani ya mioyo yao, kutafakari na kuelewa tabia zao potovu na njia zisizo sahihi walizozichukua, na wanaweza kugeuka. Ingawa mabadiliko, ukuaji, na faida kutokana na kurejea kwao ni vidogo sana, na maendeleo ni ya polepole sana, kiasi kwamba wao wenyewe wanaweza hata kukosa kutambua, baada ya miaka mitatu hadi mitano ya upitiaji kama huo, wanaweza kuhisi mabadiliko fulani ndani yao, na wale walio karibu nao wanaweza pia kuyaona. Kwa vyovyote vile, kuna tofauti kati ya watu kama hao walio na tabia ya mpinga Kristo na wale walio wapinga Kristo. Sifa kuu katika suala hili ni ipi? (Watu wenye tabia ya mpinga Kristo wanaweza kutubu.) Wanapofanya kitu kibaya, wanapotenda dhambi, au kukumbana na upogoaji, hukumu na maadibisho, kurudi au kufundishwa nidhamu, wanaweza kutubu. Hata wanapotambua kwamba wamekosea au wamefanya kosa, wanaweza kujitafakari na kuwa na mtazamo wa kugeuka na kutubu ndani ya mioyo yao. Hii ni tofauti bainifu inayowatenganisha kabisa watu wenye tabia ya mpinga Kristo na wapinga Kristo.

Muhtasari wa Tofauti Kati ya Wapinga Kristo na Watu Wenye Tabia ya Wapinga Kristo.

Wapinga Kristo ni Mashetani walio hai. Inaweza kusemwa kwamba wanaishi kama Mashetani; wao ni ibilisi na Mashetani ambao watu wanaweza kuwaona. Basi, hebu tufanye muhtasari wa tofauti za kiini kati ya wapinga Kristo na watu wenye tabia ya wapinga Kristo. Kipengele kimoja ni mtazamo wao kuelekea ukweli. Wapinga Kristo hawakubali ukweli kabisa. Ingawa wanaweza kukiri kwa maneno kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, na vitu chanya, na maneno ambayo ni ya manufaa kwa watu, na kigezo cha vitu vyote chanya, na kwamba watu wanapaswa kuyakubali, kutii, na kuyatenda—ingawa wanaweza kusema haya yote—hawawezi kabisa kuyatenda maneno ya Mungu. Kwa nini hawayatendi? Kwa sababu hawakubali ukweli mioyoni mwao. Wao husema kwa midomo yao kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, lakini kwa nia tofauti kabisa: Wanasema hivi ili kuficha ukweli kwamba hawakubali ukweli na ili kuwapotosha watu. Kwa sababu tu wapinga Kristo wanaweza kusema maneno na mafundisho, haimaanishi kwamba wanakiri mioyoni mwao kuwa maneno ya Mungu ni ukweli. Hawawezi kuutenda ukweli kwa sababu kimsingi hawakubali ukweli wa maneno ya Mungu mioyoni mwao; hawana nia ya kukubali ukweli na kuutenda ukweli ili kuingia katika uhakika wa ukweli. Kwa upande mwingine, watu wenye tabia ya wapinga Kristo si lazima wawe wapinga Kristo. Baadhi yao wanaweza, kwa viwango tofauti, kukubali na kuutii ukweli, na vitu chanya, na maneno sahihi—hii ni tofauti moja. Watu wenye kiini cha wapinga Kristo wana uhasama na ukweli, na kuutelekeza, lakini baadhi ya watu wenye tabia ya wapinga Kristo wanaweza kukubali na kuutenda ukweli. Kupitia kusoma maneno ya Mungu, na kupitia miaka kadhaa ya kuipitia kazi ya Mungu, mtazamo wao kuelekea ukweli unaweza kubadilika kiasi fulani. Wanahisi kutoka ndani ya mioyo yao kwamba ingawa hawawezi kuutenda, ukweli ni mzuri na ni sahihi. Ni kwamba tu hawapendi ukweli au hawapendezwi nao sana, kwa hivyo kuutenda kunahitaji juhudi na mapambano. Kwa hivyo, watu wenye tabia ya wapinga Kristo lakini wenye dhamiri na busara kiasi wanaweza kukubali ukweli kwa viwango tofauti. Angalau, kutoka ndani ya mioyo yao, hawaupingi wala hawachukizwi na ukweli, na hawako kinyume nao. Watu wengi wako katika hali ya aina hii na wanaonyesha udhihirisho wa aina hii kuelekea ukweli. Njia hii ya kuwaeleza watu kama hao si kuwapamba wala kuwakashifu. Hili ni jambo lisilo na upendeleo, sivyo? (Ndiyo.) Kipengele kingine ni kuwatofautisha kwa mtazamo wa ubinadamu, yaani, kutofautisha kwa kuzingatia dhamiri, busara, na wema au uovu wa ubinadamu wao. Yeyote aliye na ubinadamu mwovu, asiyekubali ukweli, na aliye kinyume na ukweli hasa, bila shaka ni asiyeamini au mpinga Kristo. Watu wengine hawapendi ukweli hasa na hawapendezwi nao. Wengine wanaposhiriki ukweli, wao husinzia na kukosa uchangamfu. Hata hivyo, watu wa aina hii hawana ubinadamu mwovu na hawawatesi wengine. Ukishiriki kuhusu nia za Mungu, kanuni za ukweli, au sheria za nyumba ya Mungu, wanaweza kusikiliza na wako radhi kuukubali ukweli na kuufuatilia, lakini si lazima waweze kuutenda ukweli. Wakiwa viongozi, huenda wasiweze kukuongoza kuelewa ukweli au kukuleta mbele za Mungu, lakini hawatakukandamiza kamwe. Huu ndio ubinadamu wa watu wenye tabia ya wapinga Kristo. Kwa vyovyote vile, ubinadamu wa watu wenye tabia ya wapinga Kristo si mwovu kiasi hicho; wanaweza kukubali ukweli kwa viwango tofauti. Kinyume chake, wapinga Kristo si tu kwamba hawana dhamiri na busara bali pia wana ubinadamu mwovu mno. Watu wenye tabia ya wapinga Kristo wana hisia ya dhamiri, na busara kiasi, na wanaweza kushughulikia mambo fulani kwa busara. Kwa mfano, kuhusu jinsi ya kuchagua na upande gani wa kuchukua katika kushughulikia mahitaji ya nyumba ya Mungu, katika kuwatendea watu mbalimbali kanisani, na katika kushughulikia mambo chanya na hasi, wanaweza kutofautisha haya na mambo mengine kama hayo na, hatimaye, wanaweza kufanya chaguo sahihi kulingana na dhamiri zao. Watu wa aina hii hawana ubinadamu mwovu kama huo na ni wema wa moyo kwa kiasi. Kuna tofauti nyingine, ambayo tumeishiriki punde tu, ambayo ni kwamba kuna baadhi ya watu wenye tabia ya wapinga Kristo ambao wanaweza kukubali ukweli, na wanapokosea, wanaweza kujitafakari na kuwa na moyo wa toba. Kinyume chake, wapinga Kristo hawaonyeshi kabisa dhihirisho hizi mbili. Wao ni wagumu na hawabadiliki kwa sababu wako kinyume na ukweli, hawakubali ukweli, na wana ubinadamu mwovu mno. Haiwezekani kwa watu wa aina hii kugeuka na kufikia toba. Iwapo mtu anaweza kutubu kweli inategemea hasa iwapo ana dhamiri na busara, na mtazamo wake kuelekea ukweli. Watu wenye tabia ya wapinga Kristo, kwa sababu hawana ubinadamu mwovu, wana dhamiri na busara kiasi, na wanaweza kukubali baadhi ya kweli kwa viwango tofauti, wana uwezekano wa kugeuka. Wanapofanya makosa au kutenda, dhambi wanaweza kutubu baada ya kupogolewa. Hili huamua kwamba watu wenye tabia ya wapinga Kristo wana tumaini la kuokolewa, ilhali wapinga Kristo hawawezi kuokolewa; wao ni wa aina ya ibilisi na Shetani. Tofauti za kiini kati ya wapinga Kristo na watu wenye tabia ya wapinga Kristo ni sifa hizi kadhaa. Je, muhtasari huu hauna upendeleo? (Ndiyo.) Kuhusu sifa hizi kadhaa za wapinga Kristo, udhihirisho wa kina tulioushiriki hauna upendeleo na unalingana na ukweli, bila kipengele chochote cha kuwakashifu. Watu wateule wa Mungu wote wamekumbana na kushuhudia hili; hivi ndivyo wapinga Kristo walivyo. Kuhusu watu wenye tabia ya wapinga Kristo, pia tumefichua udhihirisho mbalimbali, ambao wote unaonekana na watu na unapatana na ukweli, bila kuupamba.

Watu wenye tabia ya wapinga Kristo wana mapungufu na kasoro nyingi katika ubinadamu wao, na pia hufunua tabia mbalimbali potovu kwa viwango tofauti. Tabia hizi potovu zina udhihirisho bainifu ulio wazi katika kila mtu. Kwa mfano, watu wengine ni wenye kiburi hasa, wengine ni wenye hila na wadanganyifu hasa, wengine ni wagumu hasa, wengine ni wavivu hasa, na kadhalika. Maonyesho haya ni udhihirisho wa watu wenye tabia ya wapinga Kristo, na ni sifa bainifu za ubinadamu wa watu kama hao. Ingawa watu hawa wana wema kiasi mioyoni mwao—kwa maneno ya kawaida, wana moyo mwema kiasi—wanapokumbana na mambo, wanaona waziwazi kwamba maslahi ya nyumba ya Mungu yanadhuriwa, lakini kwa sababu wanaogopa kuwaudhi wengine, wao huwa kama kobe anayejificha kwenye gamba lake, wakiishi kwa kufuata falsafa ya Shetani na hawako radhi kushikilia kanuni za ukweli. Ingawa ndani kabisa wanahisi kwamba hawapaswi kutenda hivi na kwamba wanamkosea Mungu kwa kutenda hivi, bado hawawezi kujizuia ila kuchagua kuwa watu wanaotaka kuwafurahisha wengine. Kwa nini iko hivi? Kwa sababu wanaamini kwamba ili kuishi na kuendelea kuishi, ni lazima wategemee falsafa ya Shetani, na ni kwa njia hii tu ndiyo wanaweza kujilinda. Kwa hivyo, wanachagua kuwa watu wanaotaka kuwafurahisha wengine na hawatendi ukweli. Mioyoni mwao wanahisi kwamba kwa kutenda hivi, hawana dhamiri na wamekosa ubinadamu; wao si wanadamu na ni wabaya kuliko mbwa mlinzi. Hata hivyo, baada ya kujilaumu, wanapokabiliwa na hali nyingine, bado hawatubu na bado wanatenda vivyo hivyo. Daima wao ni dhaifu na daima wana hisia hatia. Hili linathibitisha nini? Linathibitisha kwamba ingawa watu wenye tabia ya wapinga Kristo si wapinga Kristo wenyewe, ubinadamu wao kwa kweli una matatizo na mapungufu, kwa hivyo hakika wao hufunua upotovu mwingi. Ukiangalia udhihirisho wa jumla wa mtu kama huyo, yeye ni mtu aliyepotoshwa kwa kina na Shetani asiyebadilika hata kidogo; yeye ndiye hasa kile ambacho Mungu hurejelea kama uzao wa Shetani. Watu wenye tabia ya wapinga Kristo ni bora kuliko wapinga Kristo kwa njia gani? Ili kuwa sahihi, ingawa watu walio na tabia ya wapinga Kristo lakini si kiini cha wapinga Kristo hufunua tabia mbalimbali potovu za Shetani, wao si watu waovu kamwe. Hali yao ni kama inavyosemwa kwa kawaida kuhusu jinsi mtu si mwenye hila na mwovu wala si mtu mwema; ni kwamba tu wanamwamini Mungu kwa dhati, wako radhi kutubu, na wanaweza kukubali ukweli baada ya kupogolewa, wakiwa na utii kiasi. Ingawa wao si watu waovu na bado wana tumaini la kuokolewa na Mungu, wako mbali sana na kiwango cha kumcha Mungu na kuepuka maovu ambacho Mungu ananena kukihusu! Watu wengine humwamini Mungu kwa miaka mitatu hadi mitano na huwa na mabadiliko na maendeleo kiasi. Watu wengine humwamini Mungu kwa miaka minane hadi kumi na hawana maendeleo yoyote. Watu wengine hata wamemwamini Mungu kwa miaka 20 bila mabadiliko yoyote makubwa; bado wako vilevile kama walivyokuwa hapo awali. Wanashikilia mawazo yao kwa ukaidi. Ni kwamba tu, kwa sababu wamesikia maneno ya Mungu na wanazuiliwa na sheria na kanuni mbalimbali za nyumba ya Mungu, hawajafanya makosa makubwa, hawajatenda matendo maovu yanayosababisha hasara kubwa kwa nyumba ya Mungu, na hawajasababisha maafa makubwa. Watu wenye tabia ya wapinga Kristo hakika hawawezi kuokolewa wote na Mungu mwishowe. Wengi wao labda ni watendaji huduma, na baadhi yao hakika wataondolewa. Kwa vyovyote vile, ingawa wao si watu waovu, wao ni watu wenye ubinadamu duni. Matokeo na hatima zao hakika hazitakuwa sawa. Yote inategemea iwapo wanaweza kukubali ukweli na jinsi wanavyochagua njia zao. Watu wengine husema, “Maneno Yako yanapingana. Je, Hukusema kwamba watu hawa wanaweza kugeuka na kutubu?” Ninachomaanisha ni kwamba watu hawa, katika mazingira fulani na katika mazingira tofauti, wanaweza kukubali ukweli kwa viwango tofauti. “Viwango tofauti” inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba watu wengine huwa na mabadiliko kidogo baada ya kumwamini Mungu kwa miaka mitatu hadi mitano, na mabadiliko makubwa baada ya miaka 10 hadi 20. Watu wengine humwamini Mungu kwa miaka 10 hadi 20 na bado wako vilevile kama walivyoanza kuamini, daima wakipiga kelele, “Ni lazima nitubu, ni lazima niulipe upendo wa Mungu!” lakini kwa kweli hawana mabadiliko. Ni kwa sababu tu wana hisia ya dhamiri ndiyo maana wana hamu hii mioyoni mwao na wako radhi kugeuka na kutubu. Hata hivyo, kuwa radhi, si sawa na kuweza kuutenda ukweli, wala si sawa na kuingia katika uhalisi. Kuwa radhi ni kutoupinga ukweli tu, kutochukizwa nao, na kutoukashifu ukweli waziwazi, kutomhukumu, kumshutumu, au kumkufuru Mungu waziwazi—ni udhihirisho huu tu. Lakini haimaanishi kuweza kutii na kukubali na kuutenda ukweli kweli, wala haimaanishi kuweza kuuasi mwili na tamaa za mtu mwenyewe. Je, huu si ukweli usio na upendeleo? (Ndiyo.) Ndivyo ilivyo hasa. Kuwa na dhamiri na busara kiasi na moyo wa kutubu kiasi katika ubinadamu wa mtu haimaanisha kwamba hana tabia potovu. Watu wenye tabia ya wapinga Kristo ni tofauti kimsingi na wapinga Kristo, lakini hii haimaanishi wao ni watu wanaoweza kukubali na kuutii ukweli. Wala haimaanishi kwamba wao ni watu wenye uhakika wa ukweli, au kwamba wao ni watu ambao Mungu anawapenda. Kuna tofauti za kiini kati ya vipengele hivi viwili; viwili hivi ni tofauti kabisa. Watu wenye tabia ya wapinga Kristo hakika ni bora zaidi kwa upande wa ubinadamu, mtazamo wao kuelekea ukweli, na kiwango chao cha toba wakilinganishwa na wapinga Kristo. Hata hivyo, kiwango ambacho Mungu huwapima watu hakitegemei jinsi wanavyotofautiana na wapinga Kristo; hiki si kiwango. Mungu hupima ubinadamu wa mtu, iwapo ana dhamiri na busara, iwapo anapenda na kuukubali ukweli, iwapo anatenda wajibu wake kwa uaminifu, iwapo anamtii Mungu, na iwapo anaweza kupata ukweli na kufikia wokovu. Hivi ndivyo viwango ambavyo Mungu huwapima watu. Mungu ametoa mahitaji mbalimbali kwa wale walio na tabia ya wapinga Kristo. Mungu hutumia mahitaji haya kuwapima watu wenye tabia ya wapinga Kristo kwa kusudi la kuwaokoa. Baada ya kusikia ikielezwa hivi, mnaelewa, sivyo? Kwanza, ni lazima mwelewe wazi kwamba haijalishi mna tabia ya wapinga Kristo kiasi gani, maadamu mnaweza kukubali ukweli, ninyi si wapinga Kristo. Ingawa ninyi si wapinga Kristo, haimaanishi ninyi ni watu wanaomtii Mungu. Kutochukizwa na ukweli wala kutokuwa kinyume nao hakumaanishi ninyi ni watu wanaotenda na kuutii ukweli. Kuwa na dhamiri na busara kiasi, kuwa na moyo mwema kwa kiasi, na kuwa na ubinadamu bora kuliko wapinga Kristo si lazima kumaanishe ninyi ni watu wema. Kiwango cha kupima iwapo mtu ni mwema au mbaya hakitegemei ubinadamu wa wapinga Kristo. Haijalishi wapinga Kristo wanafanya mambo mabaya mangapi, hawakiri kamwe wala hawatubu, bali wanaendelea kutenda vivyo hivyo; hawageuki nyuma kamwe, na wanampinga Mungu hadi mwisho. Ingawa watu wengine wenye tabia ya wapinga Kristo wanataka kugeuka na kutubu kwa dhati, kugeuka kidogo hakumaanishi wana toba ya kweli. Kuwa na azma ya kutubu hakumaanishi kuweza kuelewa ukweli, kupata ukweli, na kupata uzima.

Watu wengine husema, “Mimi si mpinga Kristo, kwa hivyo mimi ni bora kuliko wapinga Kristo na sijapotoshwa kwa kina kama wao.” Je, maneno haya ni sahihi? Je, huu ni uelewa potovu? (Ndiyo.) Watu wenye tabia ya wapinga Kristo ni sawa na wapinga Kristo katika tabia yao potovu, lakini kiini chao cha asili ni tofauti. Fikirieni—je, kauli hii ni sahihi? (Ndiyo.) Basi, elezeni. (Watu wenye tabia ya wapinga Kristo wana tabia potovu kama tu wapinga Kristo. Wote wana tabia za kiburi na ovu, na wote hufuatilia hadhi. Hata hivyo, kiini chao cha ubinadamu ni tofauti. Watu wenye tabia ya wapinga Kristo wana hisia kiasi ya dhamiri, na wanaweza kukubali ukweli kwa viwango tofauti. Hawachukizwi na ukweli na hawauchukii ukweli. Kwa upande mwingine, watu wenye kiini cha wapinga Kristo wana kiini cha ubinadamu chenye kudhuru. Hawana hisia ya dhamiri, na wanachukizwa na ukweli na wanauchukia ukweli. Hawatawahi kutubu.) Wote wana tabia potovu, kwa nini basi Mungu huwaainisha watu wenye kiini cha wapinga Kristo kama wapinga Kristo na kama maadui Zake? (Ni hasa kwa kuzingatia mtazamo wao kuelekea ukweli. Wapinga Kristo wanachukizwa na ukweli na wanauchukia ukweli, na kuuchukia ukweli kwa kweli ni kumchukia Mungu.) Kitu kingine chochote? (Kiini cha wapinga Kristo ni kile cha ibilisi.) Je, watu ambao kiini chao ni kile cha ibilisi wana tumaini lolote la kuokolewa? (La.) Watu hawa hawakubali ukweli hata kidogo na hawawezi kuokolewa. Ikizingatiwa kwamba watu wa aina hizi zote mbili wana tabia potovu, tofauti ni ipi kati ya wale wanaoweza kuokolewa na wale wasioweza kuokolewa? Kwa upande wa tabia zao potovu pekee, watu wa aina hizi mbili ni sawa, kwa nini basi wapinga Kristo hawawezi kuokolewa, huku watu wenye tabia ya wapinga Kristo lakini si kiini cha wapinga Kristo wana tumaini hafifu la kuokolewa? (Watu wenye tabia ya wapinga Kristo si kama wapinga Kristo, ambao wana uhasama mkubwa na ukweli na vitu chanya. Ingawa hawapendi ukweli hasa, hawachukizwi na ukweli na wanaweza kuukubali kwa viwango tofauti, wakibadilika kidogo kidogo. Zaidi ya hayo, ubinadamu wao una hisia kiasi ya dhamiri, tofauti na wapinga Kristo wasio na hisia ya aibu.) Tumaini la kuokolewa liko hapa; hii ndiyo tofauti ya kiini. Tukihukumu kutokana na kiini cha wapinga Kristo, watu wa aina hii hawawezi kuokolewa na hawana tumaini la kuokolewa. Hata kama unataka kuwaokoa, huwezi; hawawezi kubadilika. Wao si watu wa aina ya kawaida wenye tabia potovu ya Shetani, bali ni watu wa aina yenye kiini cha uzima cha ibilisi na Shetani. Watu wa aina hii hawawezi kuokolewa kabisa. Kinyume chake, kiini cha watu wa kawaida wenye tabia potovu ni nini? Wana tabia potovu tu; hata hivyo, wana kiasi fulani cha dhamiri na busara, na wanaweza kukubali baadhi ya kweli. Hii inamaanisha kwamba ukweli unaweza kuwa na athari fulani kwa watu hawa, na kuwapa tumaini la kuokolewa. Ni watu wa aina hii ndio Mungu huwaokoa. Wapinga Kristo hawawezi kuokolewa kabisa, lakini, je, watu wenye tabia ya wapinga Kristo wanaweza kuokolewa? (Ndiyo.) Tukisema kwamba wanaweza kuokolewa, hii si kauli ya uhakika. Tunaweza kusema tu wana tumaini la kuokolewa—hii ni kauli ya uhakika zaidi. Hatimaye, iwapo mtu anaweza kuokolewa inategemea mtu binafsi. Inategemea iwapo anaweza kukubali ukweli kwa hakika, kuutenda ukweli, na kuutii ukweli. Kwa hivyo, inaweza kusemwa tu kwamba watu wa aina hii wana tumaini la kuokolewa. Kwa nini basi wapinga Kristo hawana tumaini la kuokolewa? Kwa sababu wao ni wapinga Kristo; asili yao ni ile ya Shetani. Wana uhasama na ukweli, wanamchukia Mungu, na hawakubali ukweli hata kidogo. Je, Mungu bado anaweza kuwaokoa? (La.) Mungu huwaokoa wanadamu wapotovu, sio Shetani na ibilisi. Mungu huwaokoa wale wanaoukubali ukweli, sio masalia wanaouchukia ukweli. Je, hili linaeleweka wazi? (Ndiyo.) Tunashiriki hivi ili kuepuka watu wengine kuwa na uelewa potovu. Baada ya kutofautisha kati ya wapinga Kristo na watu wenye tabia ya wapinga Kristo, watu wengine hufikiri kwamba wao si wapinga Kristo na hii inamaanisha wako mahali salama, kwamba wamejipatia kimbilio kweli na hakika hawataondolewa, kutimuliwa, au kuondoshwa katika siku zijazo. Je, huu ni uelewa potovu? Kuwa na tumaini la kuokolewa hakumaanishi mtu ataokolewa. Tumaini hili bado linahitaji watu waende na kulishika. Mtazamo wako kuelekea ukweli ni tofauti na ule wa wapinga Kristo. Huchukizwi na ukweli, au ubinadamu wako ni bora kidogo kuliko ule wa wapinga Kristo; una hisia kiasi ya dhamiri, ni mwema wa moyo kwa kiasi, huwaumizi wengine, unajua kutubu unapofanya kitu kibaya, na unaweza kugeuka. Kuwa na sifa hizi chache tu kunamaanisha una masharti ya msingi ya kukubali ukweli, kuutenda ukweli, na kufikia kuokolewa. Lakini kutokuwa mpinga Kristo hakumaanishi utaokolewa. Wewe si wapinga Kristo, lakini bado wewe ni mwanadamu mpotovu. Je, wanadamu wote wapotovu wanaweza kuokolewa? Si lazima. Hata kama mtu si mpinga Kristo au mtu mwovu, maadamu hafuatilii ukweli, bado hawezi kuokolewa. Mungu anawaokoa watu kupitia wao kukubali na kufuatilia ukweli. Tabia potovu za watu zina uhasama na Mungu. Maadamu tabia potovu zipo ndani ya mtu, bado anaweza kumwasi Mungu, kukaidi Mungu, kumsaliti Mungu, na kadhalika. Kwa hivyo, anahitaji kukubali hukumu, kuadibu, majaribu, na usafishaji wa maneno ya Mungu; anahitaji ruzuku na uongozi wa maneno ya Mungu, upogoaji, adabu, na adhabu ya Mungu, na kadhalika—hakuna hata kazi moja kati ya hizi anazofanya Mungu inayoweza kukosekana. Kwa hivyo, ili kufikia kuokolewa, kwa upande mmoja, kazi ya Mungu inahitajika, na kwa kuongezea, watu wanahitaji kuwa na azma ya kushirikiana. Wanahitaji kuweza kuvumilia ugumu na kulipa gharama, kuingia katika uhakika wa ukweli baada ya kuelewa ukweli, na kadhalika. Hii ndiyo njia pekee ya kupata wokovu wa Mungu wa siku za mwisho, na kupokea baraka adimu ya ajabu sana ya kukamilishwa na Mungu mwenye mwili, kwa msingi wa kuelewa ukweli. Ni rahisi hivyo. Sawa, acha tumalizie ushirika kuhusu mada hii hapa.

Kipengele cha Kumi na Tatu: Kuwalinda Watu Wateule wa MunguWasisumbuliwe, Kupotoshwa, Kudhibitiwa, na Kudhuriwa Vibaya Sana na Wapinga Kristo, na Kuwawezesha Watambue Wapinga Kristo na Kuwatelekeza Kutoka Mioyoni Mwao

Kazi Kadhaa Ambazo Viongozi na Wafanyakazi Ni Lazima Wafanye Baada ya Kutambua Kuwa Wapinga Kristo Wanalisumbua Kanisa

Kufuatia, tutashiriki juu ya mada kuu. Ushirika wetu kuhusu jukumu la kumi na mbili la viongozi na wafanyakazi umekamilika. Katika ushirika huu, tutajadili kuhusu jukumu la kumi na tatu: “Kuwalinda watu wateule wa Mungu wasisumbuliwe, kupotoshwa, kudhibitiwa, na kudhuriwa vibaya sana na wapinga Kristo, na kuwawezesha watambue wapinga Kristo na kuwatelekeza kutoka mioyoni mwao.” Jukumu la kumi na tatu linahusisha mada ya jinsi viongozi na wafanyakazi wanavyopaswa kuwatendea wapinga Kristo. Wapinga Kristo wanapotokea kanisani, viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya kazi gani? Kwanza, jukumu hili linasema kwamba wakati wa kutatua matatizo kama hayo, viongozi na wafanyakazi wanahitaji kujitokeza ili kuwalinda ndugu dhidi ya usumbufu, upotoshaji, udhibiti, na madhara mabaya sana ya wapinga Kristo. Hii ndiyo kazi ya kwanza wanayopaswa kufanya. Kuhusu jinsi wapinga Kristo wanavyowasumbua, kuwapotosha, kuwadhibiti, na kuwadhuru vibaya sana watu wateule wa Mungu, mengi yameshirikiwa kuhusu hili hapo awali, kwa hivyo maudhui haya hayatakuwa mada kuu ya ushirika wa leo. Leo, tutazingatia ni majukumu gani ambayo viongozi na wafanyakazi lazima watimize na ni kazi gani ambayo lazima wafanye wanapokabiliana na tabia na matendo haya ya wapinga Kristo ili kuwalinda watu wateule wa Mungu dhidi ya madhara. Kwanza, viongozi na wafanyakazi ni lazima wawakinge watu wateule wa Mungu dhidi ya usumbufu, upotoshaji, udhibiti, na madhara mabaya sana ya wapinga Kristo—hili ni mojawapo ya majukumu ya viongozi na wafanyakazi. “Mojawapo ya majukumu” inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba miongoni mwa kazi nyingi wanazofanya viongozi na wafanyakazi, kuwalinda watu wateule wa Mungu ili waweze kuishi maisha ya kawaida ya kanisa bila usumbufu na madhara makubwa ya wapinga Kristo ni kazi muhimu. Pia ni kazi isiyoepukika ambayo hawawezi kukwepa wajibu wao. Viongozi na wafanyakazi wanapaswa kulipa umuhimu jambo hili na wasilipuuze. Kudumisha utendaji wa kawaida wa maisha ya kanisa ni kazi muhimu sana na ndiyo kazi ya kwanza kabisa miongoni mwa kazi zote za kanisa. Hili pia ni jukumu la viongozi na wafanyakazi. Kazi ya msingi ya viongozi na wafanyakazi ni kuwaongoza watu wateule wa Mungu kuingia katika uhakika wa ukweli. Mashetani, wapinga Kristo, wanapokuja kuwasumbua na kuwapotosha watu, na kushindana na Mungu kwa ajili ya watu Wake wateule, viongozi na wafanyakazi wanapaswa kusimama ili kuwafichua wapinga Kristo ili watu wateule wa Mungu waweze kuwatambua, na kuwafanya wapinga Kristo wafichue maumbo yao ya kweli, na kisha kuwaondoa kanisani. Hili ni kuzuia watu wateule wa Mungu wasidhibitiwe na kudhuriwa vibaya sana na wapinga Kristo. Hili ndilo jukumu ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kutimiza wanapofanya kazi ya kanisa. Basi kuzuia mambo haya kunamaanisha nini? Yanapaswa kuzuiwaje? Neno “kuzuia” kwa maana halisi linamaanisha kukomesha kitu kisitokee kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo. Jambo la msingi hapa ni nini? Kukomesha matukio yasitokee ndiko kunakotimiza uzuiaji. Katika kushughulikia matukio ya wapinga Kristo, kazi ya msingi ya viongozi na wafanyakazi ni kuwazuia wapinga Kristo wasiwasumbue, wasiwapotoshe, wasiwadhibiti, na wasiwadhuru vibaya sana watu wateule wa Mungu kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo. Ni lazima wawalinde watu wateule wa Mungu dhidi ya madhara ya wapinga Kristo kadiri iwezekanavyo. Hii ndiyo kazi muhimu ambayo viongozi na wafanyakazi wanahitaji kufanya, na hiki ndicho tunachohitaji kushiriki kwa uwazi kuhusu jukumu la kumi na tatu. Basi, watu wateule wa Mungu wanaweza kulindwaje? Kwa kukomesha matendo haya maovu yanayofanywa na wapinga Kristo yasitokee. Kuna njia na mbinu nyingi za kuwazuia, kama vile kufichua, kupogoa, kuchanganua, na kuzuia. Kuna nini kingine? (Kutimua.) Hiyo ndiyo hatua ya mwisho. Wakati ndugu bado hawana utambuzi na hawajui kwamba mtu fulani ni mpinga Kristo, lakini viongozi na wafanyakazi tayari wamemtambua kuwa ni mpinga Kristo, wakimtimua moja kwa moja, wale wasio na utambuzi wanaweza kuwa na mawazo na hukumu, na wengine wanaweza kukwazika. Katika hali kama hizi, viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya kazi gani? Nimetaja nini hivi punde? (Kufichua, kupogoa, kuchanganua, na kuzuia.) Je, ninyi mna mbinu zozote nzuri za kuwazuia wapinga Kristo wasitende maovu? Je, kuwafuatilia ni mbinu nzuri? Je, inahesabiwa kama njia na mbinu yenye ufanisi inayolingana na kanuni? (Ndiyo.) Njia ifaayo ya kuwatendea wapinga Kristo ni ipi? Je, hukumu, kuadibu, majaribu, na usafishaji vinaweza kuwa na athari kwa wapinga Kristo? (La.) Kwa nini la? (Wapinga Kristo hawakubali ukweli; wako kinyume nao.) Wapinga Kristo wako kinyume na ukweli na hawaukubali, kwa hivyo kutumia majaribu, usafishaji, hukumu, na kuadibu ili kuwashughulikia wapinga Kristo si jambo linalofaa. Zaidi ya hayo, Mungu hafanyi kazi hii juu yao. Wazo hili halifai, kwa hivyo bila shaka mbinu hii haitafanya kazi. Basi ni mbinu gani hasa inayofaa? Watu wengi ambao wameteseka sana kutokana na madhara ya wapinga Kristo huwachukia sana na wanaamini kwamba wapinga Kristo wanapaswa kuhukumiwa, kulaaniwa, na kufichuliwa hadharani. Wanafikiri kwamba wapinga Kristo wanapaswa kulazimishwa wakiri makosa yao na waungame dhambi zao waziwazi kanisani na waaibishwe kabisa. Je, ninyi mnafikiri kutumia mbinu hizi kungefaa? (La.) Tukizingatia kiini cha wapinga Kristo, kuchukua hatua kama hizo kwa kweli hakuwezi kuwa kupita kiasi—jinsi maibilisi wanavyotendewa ni sawa; inaweza kufanywa kwa urahisi kama kuponda mdudu. Kwa hivyo kusudi la viongozi na wafanyakazi kufanya hivi linaonekana kuwa halali na sahihi sana, lakini, je, kuna masuala yoyote na mbinu hizi? Je, kazi hii iko ndani ya upeo wa majukumu ya viongozi na wafanyakazi? Je, kufanya mambo kwa njia hii kunalingana na kanuni au la? (Hakulingani.) Ni wazi, hakulingani na kanuni. Kanuni zinatoka wapi? (Kutoka kwa maneno ya Mungu.) Sahihi. Ingawa walengwa wa matendo kama hayo ni wapinga Kristo—maibilisi—mbinu zinapaswa pia kulingana na kanuni na mahitaji ya Mungu, kwa sababu katika kufanya kazi hii viongozi na wafanyakazi wanatimiza majukumu yao, si kushughulikia mambo ya familia au masuala ya kibinafsi.

I. Kufichua

Kuwashughulikia wapinga Kristo na kuwazuia wasitende maovu na kuwapotosha na kuwadhuru watu wateule wa Mungu ni jukumu la viongozi na wafanyakazi. Kusudi ni kuwalinda watu wateule wa Mungu dhidi ya madhara, si kumtesa mtu yeyote au kuchukua fursa ya kumlipiza kisasi mtu yeyote, na bila shaka si kufanya kampeni dhidi ya mtu yeyote. Kwa hivyo, ni kazi zipi ambazo viongozi na wafanyakazi wanahitaji kufanya ili kuwazuia wapinga Kristo wasitende maovu kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo? Ya kwanza ni kuwafichua. Kusudi la kufichua ni nini? (Kuwasaidia watu kukuza utambuzi.) Sahihi. Ni kuwasaidia watu wateule wa Mungu watambue kiini cha wapinga Kristo, ili waweze kujiweka mbali na wapinga Kristo mioyoni mwao na wasipotoshwe nao, na ili—wapinga Kristo wanapojaribu kuwapotosha na kuwadhibiti—waweze kuwakataa kikamilifu, badala ya kuwaruhusu wapinga Kristo wawapotoshe na kuwachezea. Basi, je, kuwafichua ni muhimu? (Ndiyo.) Kuwafichua ni muhimu sana, lakini ni lazima uwafichue kwa usahihi. Basi, unapaswa kuwafichuaje? Msingi wa kufichua kwako unapaswa kuwa nini? Je, ni sawa kuwaita majina kiholela? Je, ni sawa kuwalaani kwa namna ya kutojali bila msingi? (La.) Basi unapaswa kuwafichuaje kwa usahihi ili kufikia lengo la kuwalinda watu wateule wa Mungu? (Kwa upande mmoja, ni lazima tuwafichue bila upendeleo na kwa ukweli kulingana na ukweli wa matendo yao maovu. Zaidi ya hayo, ni lazima tuwatambue na kuwachanganua kulingana na maneno ya Mungu.) Kauli hizi mbili ni sahihi kabisa; vipengele vyote viwili ni vya lazima. Kwa upande mmoja, lazima kuwe na ushahidi wa kweli. Ni lazima uhukumu na uainishe kiini chao kulingana na maneno yenye makosa, matendo, na mawazo na maoni ya kipuuzi yaliyofunuliwa na wapinga Kristo. Jambo muhimu zaidi, hata hivyo, ni kuwatambua na kuwachanganua kulingana na maneno ya Mungu. Unapaswa kurejelea maneno yapi ya Mungu? Ni maneno yapi yaliyo ya moja kwa moja na makali zaidi? (Maneno yanayowafichua wapinga Kristo.) Sahihi; ni lazima utafute maneno fulani yanayowafichua wapinga Kristo ili kuwafichua na kufanya ulinganisho ipasavyo na bila upendeleo, ukihakikisha usahihi kamili. Ndugu wataelewa baada ya kusikia hili; watakuwa na utambuzi mara moja kumwelekea mtu anayehusika, na watajilinda dhidi yake. Wakiwa na utambuzi mioyoni mwao, watahisi kuchukizwa na mtu huyu: “Kwa hivyo, yeye ni mpinga Kristo kweli! Alinisaidia hapo awali na hata akanifanyia hisani. Nilidhani alikuwa mtu mwema. Kupitia uchanganuzi na ushirika huu, unafiki wake na udhihirisho wake wa kiini wa upinga Kristo umefichuliwa, na kumsaidia kila mtu kuona kwamba mtu huyu ni hatari. Maneno ya Mungu yamemfunua kwa usahihi sana! Yeye si mtu mwema. Anasema mambo mazuri na inaonekana hakuna matatizo katika matendo yake, lakini kwa kufichua kiini chake, sasa ni dhahiri kwamba yeye ni mpinga Kristo kweli.” Tukihukumu kutokana na mabadiliko ya mawazo ya watu, viongozi na wafanyakazi wanapofanya kazi ya kuwafichua wapinga Kristo, wanawazuia wapinga Kristo wasiwapotoshe na kuwasumbua watu wateule wa Mungu kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo. Bila shaka, wanatimiza pia jukumu la kuwalinda watu wateule wa Mungu dhidi ya udhibiti na madhara makubwa ya wapinga Kristo. Wanafanya mojawapo ya kazi zao kwa njia ya vitendo. Kazi hii ni ipi? Kuwafichua wapinga Kristo. Kazi ya kuwafichua wapinga Kristo ni mojawapo ya kazi ambazo viongozi na wafanyakazi lazima wafanye ili kuwalinda watu wateule wa Mungu. Kuhusu kazi mbalimbali ambazo viongozi na wafanyakazi lazima wafanye, hatutazipanga kulingana na ukubwa au matokeo yake; hebu kwanza tushiriki juu ya kazi ya “kufichua.” Kufichua kiini cha asili cha wapinga Kristo kunajumuisha kufichua nia, makusudi, na matokeo ya matendo yao maovu ya daima yanayovuruga na kusumbua kazi ya kanisa; kufichua jinsi wapinga Kristo, wanapotumika kama viongozi na wafanyakazi, hawafanyi kazi yoyote halisi ya kanisa hata kidogo na wanapuuza kuingia katika uzima kwa watu wateule wa Mungu; kufichua sura mbaya ya wapinga Kristo kama watu wasiojijua wenyewe hata kidogo, kamwe hawatendi ukweli, na huzungumza tu maneno na mafundisho ili kuwapotosha watu; na kufichua maneno na matendo yao tofauti mbele ya watu na nyuma ya migongo yao. Kufichua kabisa vipengele hivi kunaonyesha umbo la kweli la wapinga Kristo kama Mashetani na maibilisi waovu. Hii ni kazi muhimu ambayo viongozi na wafanyakazi lazima wafanye. Basi, viongozi na wafanyakazi wanahitaji kuwa na nini ili waifanye kazi hii? Kwanza kabisa, wanahitaji kuwa na hisia fulani ya mzigo, sivyo? (Ndiyo.) Viongozi na wafanyakazi wanapobeba jukumu hili, mara nyingi wao huwaza, “Mtu huyo ni mpinga Kristo. Baadhi ya ndugu mara nyingi humwendea wakiwa na maswali, wakijisogeza karibu naye kila mara na kuwa na uhusiano mzuri naye. Wakiwa wamepotoshwa na mtu huyu, watu wengi hasa wanamwabudu. Nini kifanyike kuhusu hili?” Wao huja mbele za Mungu kuomba na mara nyingi hutafuta kwa makusudi maneno ya Mungu yanayowafichua wapinga Kristo, wakijitayarisha na ukweli katika jambo hili. Kisha wanamwomba Mungu atayarishe wakati unaofaa au wao wenyewe hutafuta wakati na fursa inayofaa ili kushiriki na ndugu kuhusu jambo hili. Wanalichukulia hili kama mzigo wao na kazi muhimu wanayohitaji kuifanya baadaye. Wanajitayarisha, wanatafuta, na wanamwomba Mungu kila mara ili awape mwongozo; daima wako katika hali ya akili na hali ya namna hii. Huku ndiko kunakoitwa kuwa na hisia ya mzigo. Baada ya kujitayarisha na mzigo kama huo kwa muda fulani, ni lazima wasubiri hadi hali ziwe zinazofaa. Angalau, ni lazima wasubiri hadi watu wawili au watatu wawe na utambuzi wa kweli wa mpinga Kristo kabla ya kuanza kumfichua. Wakiamua kwamba mtu fulani anaonekana kuwa mpinga Kristo kulingana na hisia zao pekee, lakini hawawezi kung’amua kama mtu huyo kwa kweli ni mpinga Kristo au la, basi hawapaswi kutenda kwa pupa. Kwa ufupi, wanapofanya kazi hii, hakika watakuwa na nuru na mwongozo wa Mungu. Hii ndiyo maana ya kufanya kazi halisi na kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi.

II. Kupogoa

Baada ya kazi ya kuwafichua wapinga Kristo kutekelezwa, ingawa ndugu wanapata utambuzi kiasi, kabla ya wapinga Kristo kufichuliwa kikamilifu, bila shaka wao hufanya mambo zaidi ya kuwapotosha na kuwasumbua ndugu, na kusababisha watu wengi zaidi kuwaabudu, kuwasifu, na kuwafuata. Hili huwachelewesha sana watu wateule wa Mungu wasiingie katika njia sahihi ya kumwamini Mungu, likizuia kuingia kwao katika uzima na kusababisha madhara makubwa. Basi, kazi ya pili ambayo viongozi na wafanyakazi ni lazima waifanye, ni kwamba wapinga Kristo wanapowapotosha na kuwasumbua ndugu, au maneno na matendo yao yanapokiuka kanuni za ukweli waziwazi, viongozi na wafanyakazi ni lazima wakamate ushahidi na wajitokeze upesi ili kuwapogoa, na kufichua matendo yao maovu kulingana na maneno ya Mungu, ili ndugu waweze kutambua na kuona waziwazi sura ya kweli ya wapinga Kristo. Hili ni jukumu lisiloweza kuepukika la kuwalinda watu wateule wa Mungu na kulinda kazi ya nyumba ya Mungu. Viongozi na wafanyakazi hawapaswi kukaa tu bila kufanya chochote au kufumbia macho; wanapaswa kuchukua fursa upesi, kubainisha matukio, na kujitokeza ili kuwapogoa wapinga Kristo, wakifichua kwa usahihi matendo yao, tamaa zao za makuu, matamanio, na kiini chao. Bila shaka, ni muhimu pia kuainisha kwa usahihi zaidi ni mtu wa aina gani wapinga Kristo walivyo, ili ndugu waweze kuona hili waziwazi, ili wapinga Kristo wenyewe walijue, na ili wapinga Kristo wafahamu kwamba si kila mtu hana utambuzi kuwahusu na anaweza kudanganywa nao—kwamba angalau baadhi ya watu wanaweza kung’amua matendo na tabia zao na kuona waziwazi tamaa zao za makuu na matamanio yaliyofichika, pamoja na kiini chao. Kusudi la kuwapogoa wapinga Kristo, bila shaka, si kufichua tu kiini chao kupitia maneno. Jambo muhimu zaidi, ni nini? (Kwa upande mmoja, ni kuwasaidia ndugu kukuza utambuzi, na pia kuzuia matendo maovu ya wapinga Kristo.) Sahihi. Ni kuwazuia, ili wanapofanya mambo yanayowapotosha na kuwasumbua watu, wawe na kizuizi fulani na wahisi hofu kiasi; kuwafanya wawe chini ya masharti, wawe na vizuizi fulani, na wasithubutu kutenda bila kujali; kuwajulisha kwamba mbali na nyumba ya Mungu na ukweli, huku ukweli ukiwa na mamlaka, pia ina amri za utawala, na kwamba haiwezekani kutenda kidhalimu na kwa kutojali kimakusudi katika nyumba ya Mungu, kudhuru masilahi ya nyumba ya Mungu, na kuwadhuru watu wateule wa Mungu; na pia kuwajulisha kwamba watawajibishwa kwa kutenda makosa ya kutojali yanayosumbua kazi ya kanisa na kudhuru kuingia katika uzima kwa watu wateule wa Mungu. Huku wakiwapogoa wapinga Kristo upesi, viongozi na wafanyakazi ni lazima pia wasimame ili kuwafichua, wakiwasaidia watu kukuza utambuzi na kuona waziwazi tamaa za makuu, matamanio, dhamira, na makusudi ya wapinga Kristo. Hili pia, bila shaka, ni kuwalinda watu wateule wa Mungu na kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu. Haya yote ni mambo ambayo viongozi na wafanyakazi lazima wayazingatie, na iko ndani ya upeo wa majukumu yao kufanya kazi hii; hawawezi kuipuuza au kuifanya bila uangalifu. Ikiwa viongozi na wafanyakazi watagundua wapinga Kristo kanisani, wanapaswa kuwa macho kila wakati kuhusu maneno na matendo yao na maoni potofu wanayoyaeneza kwa siri, na ni lazima watekeleze kuwapogoa na kuwafichua. Hii ni mojawapo ya kazi za viongozi na wafanyakazi ili kuwalinda watu wateule wa Mungu wasisumbuliwe na kudhuriwa na wapinga Kristo.

III. Kuchanganua

Kazi inayofuata kwa viongozi na wafanyakazi ni ipi? Ni kuchanganua. Kuchanganua karibu kufanane na kufichua, lakini kuna tofauti katika kiwango. Linapokuja suala la kuchanganua, si kufichua tu ukweli, hali halisi, au usuli; kunahusisha suala la uainishaji, yaani, kunahusisha tabia ya wapinga Kristo, suala hili la kiini, la msingi. Changanua mtazamo wao kumwelekea Mungu, ukweli, wajibu wao, na kazi ya nyumba ya Mungu, pamoja na nia, dhamira, na kusudi la kueneza kwao maoni potofu—sababu za wao kufanya hivi—na utambue kiini chao ni nini hasa kupitia mawazo, maoni, maneno, matendo yao, na tabia na udhihirisho wanaoufunua. Haya yanapaswa kulinganishwa na maneno ya Mungu na kuelezwa ili ndugu waweze kupata ufahamu wa kina zaidi wa wapinga Kristo na kuona waziwazi kwa mtazamo wa vitendo kwa nini hasa wapinga Kristo walio mbele yao wanasema na kufanya mambo haya, mtazamo wa Mungu kwa watu kama hao ni upi, na jinsi Anavyowaainisha. Bila shaka, viongozi na wafanyakazi wanapaswa pia kuwaambia ndugu wajiweke mbali na wapinga Kristo na kuwakataa, na pia kuwa macho dhidi ya kupotoshwa na matendo, tabia, maneno, na maoni ya wapinga Kristo ili kuepuka kumwelewa Mungu visivyo, kujihadhari dhidi ya Mungu, kujiweka mbali na Mungu, kumkataa Mungu, na hata kumhukumu na kumshutumu Mungu mioyoni kama wapinga Kristo wanavyofanya. Kusudi la kuchanganua, kama kazi nyingine kama vile kufichua na kupogoa, ni kuwazuia wapinga Kristo wasiwapotoshe, wasiwasumbue, na wasiwadhuru watu wateule wa Mungu. Ni kuwalinda watu wateule wa Mungu wasidhuriwe vibaya sana na wapinga Kristo na wasikengeuke kutoka kwa njia sahihi ya kumwamini Mungu. Watu wateule wa Mungu wanapoona waziwazi ukweli na hali halisi kuhusu jinsi wapinga Kristo wanavyolisumbua kanisa na kuona waziwazi kiini cha wapinga Kristo, hawataweza tena kupotoshwa na kudhibitiwa nao. Hata kama baadhi ya watu waliochanganyikiwa na watu wapumbavu bado wanawastaajabu na kuwaabudu ndani yao na kushirikiana nao na kuwakaribia, wapinga Kristo hawawezi tena kusababisha masuala makubwa. Watafanya tu mambo kadhaa kwa watu wapumbavu, bila kuathiri kuingia katika uzima kwa wale wanaoamini kwa dhati katika Mungu hata kidogo, na hivyo, hawataweza kusumbua na kuvuruga kazi ya kanisa. Kufikia kiwango hiki ndicho viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuweza kutimiza. Yaani, ni lazima wahakikishe kwamba wale wanaoamini kwa dhati katika Mungu na wanafanya wajibu wao kwa hiari na wale wanaopenda ukweli wanaweza kuishi maisha ya kawaida ya kanisa na kutimiza wajibu wao. Wakati huo huo, ni lazima pia waweze kuhakikisha kwamba watu hawa wanaweza kujilinda dhidi ya upotoshaji na usumbufu wa wapinga Kristo, na kuwakataa wapinga Kristo. Huku ni kukomesha utendaji maovu na usumbufu wa wapinga Kristo kwa kiwango kikubwa zaidi, na kufikia kikamilifu athari ya kuwalinda watu wateule wa Mungu. Bila shaka, haijalishi jinsi unavyofanya kazi yako kwa ufanisi na jinsi unavyozungumza kwa kina, bila kuepukika kutakuwa na baadhi ya watu wapumbavu, watu wenye ubora duni wa tabia, na watu waliochanganyikiwa ambao hawawezi kuwakataa wapinga Kristo na bado watawaheshimu na kuwachukulia kwa heshima mioyoni mwao. Hata hivyo, watu wengi watakuwa wamefikia kiwango ambapo wanaweza kuwakataa wapinga Kristo. Ikiwa viongozi na wafanyakazi wanaweza kutimiza hili, watakuwa tayari wamewalinda watu wateule wa Mungu kwa kiwango kikubwa zaidi, wakitimiza kikamilifu matokeo yaliyotarajiwa. Kuhusu wajinga hao ambao hawawezi kuelewa ukweli haijalishi jinsi unavyoshirikiwa, ikiwa bado wanaweza kutumika kidogo, wanapaswa kupewa uangalifu na msaada kiasi, pamoja na upendo zaidi, subira, na uvumilivu. Huku ni kufanya kila kitu ambacho mtu anapaswa kufanya, na kufanya kazi kwa njia hii ni kufuata kanuni. Je, kuna viongozi na wafanyakazi wengi wanaoweza kufikia kiwango hiki? (La.) Kwa hivyo, ni lazima juhudi kubwa zaidi ifanywe; ni lazima uwalinde watu wateule wa Mungu bila kuchoka na kwa kiwango kikubwa zaidi. “Kwa kiwango kikubwa zaidi” inamaanisha nini? Inamaanisha kufanya kila liwezekanalo kushiriki kanuni za ukweli unazozielewa, kuwasilisha ushahidi ambao tayari umepatikana—udhihirisho mbalimbali wa matendo maovu ya wapinga Kristo—ukiyahusisha na maneno ya Mungu yanayowafichua wapinga Kristo, na kushiriki na kuyachanganua. Hili ni ili kwamba ndugu waweze kuona hali halisi, ya kweli waziwazi, watambue na waone waziwazi kiini cha wapinga Kristo, na wajue mtazamo wa Mungu kuwaelekea wapinga Kristo. Hii ni kazi muhimu ambayo viongozi na wafanyakazi ni lazima waifanye.

IV. Kuweka Masharti

Ni kazi gani inayofuata ambayo viongozi na wafanyakazi lazima wafanye? Ni kuzuia. Kazi hii ya “kuzuia” ni rahisi kutekeleza; inahusisha kuchukua hatua fulani maalum ili kufikia matokeo ya kizuizi. Kwa mfano, wapinga Kristo daima huzungumza maneno na mafundisho, daima hujikweza, wakati mwingine huwadharau wengine, mara nyingi hushuhudia kuhusu mateso waliyovumilia na michango waliyoitoa katika nyumba ya Mungu wakati wa mikutano, na kujishuhudia bila aibu, wakizungumza kuhusu jinsi wengine wanavyowastaajabu, jinsi walivyo bora kuliko wengine, jinsi walivyo wa kipekee, na kadhalika. Viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya kila wawezalo kuzuia matendo mbalimbali maovu ya wapinga Kristo yanayowapotosha na kuwadhibiti watu wateule wa Mungu, badala ya kuwaachilia kila mara. Wanapaswa kutilia masharti muda wao wa kuzungumza na mada wanazojadili. Zaidi ya hayo, kuhusu matendo ya wapinga Kristo hadharani na faraghani, kama vile kutumia hisani ndogo kuwavuta watu upande wao, kuchochea fitina, kueneza mawazo na maneno hasi, na kadhalika, viongozi na wafanyakazi hawapaswi kutenda kana kwamba wao ni viziwi au vipofu. Wanapaswa kufahamu upesi matendo ya wapinga Kristo; punde tu wanapogundua tabia zinazowapotosha na kuwasumbua wengine, wanapaswa kufichua na kuchanganua tabia hizi upesi na kuwawekea wapinga Kristo vizuizi, wasiwaruhusu kuzunguka wakiwapotosha watu na kuisumbua kazi ya kanisa. Je, hii ni mojawapo ya kazi muhimu ambazo viongozi na wafanyakazi wanahitaji kufanya? (Ndiyo.) Je, unaweza kuzuia matendo maovu ya wapinga Kristo kwa kuwapogoa, kuwafichua, na kuwachanganua tu? (La.) Huwezi kuwazuia kwa njia hii kwa sababu wao ni Mashetani na maibilisi waovu. Maadamu mikono na miguu yao haijafungwa, na vinywa vyao havijazibwa, wataeneza maoni potofu na kuzungumza maneno ya kishetani yanayowasumbua watu. Viongozi na wafanyakazi ni lazima wachukue hatua upesi ili kuwazuia; hasa wanapoeneza maoni potofu ili kuwapotosha na kuwasumbua watu, viongozi na wafanyakazi ni lazima wawakatishe na kuwakomesha kwa wakati unaofaa. Ni lazima pia wawawezeshe watu wateule wa Mungu wawe na utambuzi na waione sura ya kweli ya wapinga Kristo waziwazi. Hii ndiyo kazi halisi ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya.

V. Ufuatiliaji

Baada ya kuwazuia wapinga Kristo, kinachofuata ni kuwafuatilia. Angalia ni nani wapinga Kristo wamempotosha na ni maoni potofu na maneno gani ya kishetani wameyaeneza kwa siri, chunguza kama wanaunga mkono joka kubwa jekundu na wanatenda kwa ushirikiano nalo, kama wameungana na ulimwengu wa kidini, kama wanafanya mbinu za siri na washiriki wa magenge yao, kama wanaweza kusaliti habari fulani muhimu kuhusu nyumba ya Mungu, na kadhalika. Hili pia ni jukumu ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kutimiza. Kabla ya matendo ya wapinga Kristo kufichuliwa, viongozi na wafanyakazi hawapaswi “kujitolea kikamilifu kusoma vitabu vya wenye hekima na kutozingatia mambo ya nje,” bali wanapaswa kuwa werevu kama nyoka. Punde tu viongozi na wafanyakazi wanapogundua kwamba mtu fulani ni mpinga Kristo, ikiwa wakati bado haujafika wa kumwondoa au kumtimua mtu huyo, ni lazima wamfuatilie kwa karibu ili kumzuia asiendelee kutenda maovu, wakihakikisha kwamba maneno na matendo yake yanafuatiliwa na watu wateule wa Mungu. Kwa sababu wapinga Kristo wanapenda mamlaka na kujenga uhusiano na watu wenye nguvu, viongozi na wafanyakazi wanapaswa kutazama kwa makini ni nani ambaye wapinga Kristo wanashirikiana naye kila mara kwa siri na kama wanawasiliana na watu wa kidini. Baadhi ya wapinga Kristo mara nyingi hushirikiana na wachungaji na wazee wa kidini, na wengine hata hushirikiana na watu kutoka Idara ya Kazi ya Muungano wa Pamoja. Matukio kama haya yanapotokea, viongozi na wafanyakazi hawapaswi kufumbia macho jambo hili, bali wanapaswa kuwa macho dhidi ya wapinga Kristo na kuwa waangalifu. Ikiwa mpinga Kristo ataona kwamba mbinu zake za kuwapotosha na kuwavuta watu upande wake hazifanyi kazi katika nyumba ya Mungu na kwamba matendo yake maovu yamefichuliwa, na anajua kwamba hatakuwa na mwisho mwema, huwezi kutabiri kile anachoweza kufanya au kiwango ambacho uovu wake unaweza kufikia. Kwa hivyo, punde tu unapokuwa na uhakika moyoni mwako kwamba mtu fulani ni mpinga Kristo, ni lazima umfuatilie kwa karibu na kumtazama bila kulegea. Hili ni jukumu lako. Lengo la kufanya hivi ni nini? Ni kuwalinda watu wateule wa Mungu, na kukomesha, kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo, wapinga Kristo wasitende matendo haramu dhidi ya kanisa na ndugu ili kuwadhuru akina ndugu. Baadhi ya wapinga Kristo daima huulizia kuhusu sadaka: “Ni nani anayesimamia pesa za nyumba ya Mungu? Ni nani anayeweka hesabu? Je, hesabu zinawekwa kwa usahihi? Je, inawezekana kuna ubadhirifu unaoendelea? Pesa za kanisa zinawekwa wapi? Je, mambo haya hayapaswi kutangazwa hadharani, na kumpa kila mtu haki ya kuyajua? Nyumba ya Mungu ina mali ngapi? Nani ametoa sadaka nyingi zaidi? Kwa nini sijui mambo haya?” Maneno yao yanafanya ionekane kana kwamba wanajali kuhusu mambo ya kifedha ya nyumba ya Mungu, lakini kwa kweli, wana nia tofauti. Hakuna mpinga Kristo hata mmoja asiyetamani pesa. Basi viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya nini katika hali kama hizi? Kwanza, unapaswa kusimamia sadaka ipasavyo, ukiwakabidhi watu wanaotegemewa kwa ajili ya ulinzi, na hupaswi kabisa kuwaacha wapinga Kristo wafanikiwe katika kutimiza malengo yao—hupaswi kuchanganyikiwa kuhusu jambo hili. Punde tu hali ya aina hii inapotokea, unapaswa kutambua: “Kuna jambo lisilo sawa. Mpinga Kristo anakaribia kufanya kitu. Pesa za kanisa zinalengwa nao. Wanaweza kuwa wanapanga kuungana na joka kubwa jekundu ili kuzipangia njama na kuzitwaa pesa za kanisa. Lazima tuihamishe mara moja!” Kwa upande mmoja, huwezi kuwaacha wapinga Kristo wajue ni nani anayesimamia fedha za nyumba ya Mungu. Zaidi ya hayo, ikiwa watu wanaosimamia pesa wanahisi kuna hatari ya usalama, pesa na watu wanaozisimamia ni lazima wahamishwe haraka. Je, hili si jambo ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kulijali, na kazi wanayopaswa kuifanya? (Ndiyo.) Kinyume chake, viongozi wapumbavu huwasikia wapinga Kristo wakisema mambo haya na bado wanawaza, “Mtu huyu anabeba mzigo na anajua kuonyesha kujali kuhusu pesa za nyumba ya Mungu, kwa hivyo tumpe jukumu fulani na tumwache asaidie katika uwekaji hesabu.” Kwa kufanya hivi, je, hawajakuwa akina Yuda? (Ndiyo.) Siyo tu kwamba wameshindwa kulinda sadaka, bali hata wamezisaliiti kwa wapinga Kristo, na kwa kweli wamekuwa akina Yuda. Mnawaonaje viongozi na wafanyakazi hawa? Je, wao si watu waovu? Je, wao si maibilisi? Siyo tu kwamba wameshindwa kutimiza majukumu yao, bali pia wamewakabidhi sadaka za Mungu na ndugu kwa wapinga Kristo. Kwa hivyo, katika maeneo ambapo kuna wapinga Kristo, punde tu viongozi na wafanyakazi wanapogundua dalili zozote za hili, ni lazima waanzishe uchunguzi na wafanye kazi fulani mahususi, ambapo kazi ya “ufuatiliaji” ni ya lazima.

Kazi ya ufuatiliaji inayofanywa na viongozi na wafanyakazi si kuhusu kufanya ujasusi au shughuli zozote za upelelezi; ni kutimiza tu jukumu lako, kujali zaidi, kuchunguza kwa makini zaidi, na kuona kile ambacho wapinga Kristo wanafanya na kile wanachokusudia kufanya. Ukigundua dalili zozote za wao kutenda maovu na kulisumbua kanisa, ni lazima uchukue hatua za kulikabili hilo haraka iwezekanavyo; huwezi kabisa kuwaruhusu wafanikiwe. Huku ni kukomesha, kwa kiwango kikubwa zaidi, matukio ya wapinga Kristo kuisumbua kazi ya kanisa yasitokee. Kwa kawaida, hili pia hulinda vyema zaidi kazi ya kanisa na kuwalinda watu wateule wa Mungu. Huu ni udhihirisho wa viongozi na wafanyakazi wanaotimiza majukumu yao. Ufuatiliaji haumaanishi kupanga watu wachache watende kama maajenti wa siri, na kuwafanya wawafuate, kuwafuatilia kwa nyuma, na kuwapeleleza watu kama majasusi, au kupekua nyumba zao na kutumia mbinu kali za kuwahoji. Nyumba ya Mungu haijihusishi na shughuli kama hizo. Hata hivyo, ni lazima uelewe upesi hali ya wapinga Kristo. Unaweza kuulizia kuhusu hali yao ya hivi karibuni kwa kuzungumza na wanafamilia wao au ndugu wanaoweza kuwatambua au wanaowafahamu. Je, hizi zote si mbinu na njia za kufanya kazi hii? Ikiwa viongozi na wafanyakazi watafanya kazi zilizo ndani ya upeo wa majukumu yao na zinazoambatana na kanuni zinazohitajika na Mungu, wanatimiza majukumu yao. Kusudi la viongozi na wafanyakazi kutimiza majukumu yao ni nini? Ni ili ufanye yote uwezayo ili kuwazuia wapinga Kristo wasisababishe vurugu na usumbufu kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo, na hivyo kuwazuia wapinga Kristo wasiwadhuru watu wateule wa Mungu na kusaliti masilahi ya nyumba ya Mungu. Hili ni jukumu la viongozi na wafanyakazi. Je, huku hakukomeshi kutokea kwa matukio ya wapinga Kristo kwa kiwango kikubwa zaidi? Je, viongozi na wafanyakazi wanaochukua hatua hizi hawafanyi yote yanayowezekana? (Ndiyo.) Je, ni vigumu kufanya hivi? (La.) Si vigumu; hili ni jambo ambalo wale wanaoelewa ukweli wanaweza kulitimiza. Watu wanapaswa kufanya kila wawezalo kutimiza kile wanachoweza; mengine wamwachie Mungu ayafanye, Aonyeshe mamlaka Yake na kupanga, na kuongoza. Hili ndilo jambo ambalo hatuna wasiwasi nalo hata kidogo. Mungu yu pamoja nasi. Siyo tu tuna Mungu mioyoni mwetu, bali pia tuna imani ya kweli. Huu si msaada wa kiroho; kwa kweli, Mungu yuko kwa siri, na Yeye yupo kando ya watu, daima yupo pamoja nao. Wakati wowote watu wanapofanya jambo lolote au kutekeleza wajibu wowote, Yeye anatazama; Yeye yupo ili kukusaidia wakati na mahali popote, akikuhifadhi na kukulinda. Kile ambacho watu wanapaswa kufanya ni kufanya kila wawezalo kutimiza kile wanachopaswa. Maadamu unafahamu, unahisi moyoni mwako, unaona katika maneno ya Mungu, unakumbushwa na watu walio karibu nawe, au unapewa ishara yoyote au dalili na Mungu inayokupa habari—kwamba hili ni jambo unalopaswa kufanya, kwamba hili ni agizo la Mungu kwako—basi unapaswa kutimiza wajibu wako na si kukaa tu bila kufanya kitu au kutazama ukiwa pembeni. Wewe si roboti; una akili na mawazo. Jambo linapotokea, unajua kabisa unachopaswa kufanya, na bila shaka una hisia na ufahamu. Basi tumia hisia na ufahamu huu katika hali halisi, uishi kwa kuyadhihirisha na kuyageuza kuwa matendo yako, na kwa njia hii, utakuwa umetimiza wajibu wako. Kwa mambo unayoweza kufahamu, unapaswa kutenda kulingana na kanuni za ukweli unazozielewa. Kwa njia hii, unafanya kila uwezalo na unajitahidi kabisa kutimiza wajibu wako. Kama kiongozi au mfanyakazi, unapofanya juhudi yako yote, yaani, unapokomesha matendo maovu ya wapinga Kristo yasitokee kwa kiwango kikubwa zaidi, Mungu ataridhika kwamba unaweza kutenda kwa njia hii. Kwa nini Mungu ataridhika? Mungu atatoa uamuzi kuhusu viongozi na wafanyakazi kama hao: Wanatimiza majukumu yao na wanafanya juhudi zao zote kutekeleza kazi halisi ya jukumu lao. Je, hiki ni kibali cha Mungu? (Ndiyo.)

VI. Kutimua

Jukumu la kumi na tatu la viongozi na wafanyakazi linajumuisha kazi mahususi wanazopaswa kutekeleza, ambazo tuliorodhesha kadhaa: Ni lazima watende wawafichue, wawapogoe, wawachanganue, wawazuie, na kuwafuatilia wapinga Kristo. Ushirika kuhusu kanuni hizi za msingi umekamilika. Bila kujali matendo mahususi ambayo viongozi na wafanyakazi huchukua katika hali maalum, kanuni za kuwashughulikia wapinga Kristo hazibadiliki. Zaidi ya hayo, kusudi kuu la kazi hizi ni kuwalinda watu wateule wa Mungu. Tuseme kwamba watu wateule wa Mungu tayari wamemtambua mtu kwa kauli moja kama mpinga Kristo na wametambua na kung'amua kabisa kwamba mpinga Kristo daima anatafuta kuwapotosha na kuwadhibiti watu; wanajua kwamba kwa kuwepo kwa mpinga Kristo, hakuwezi kuwa na siku nzuri au maisha mazuri ya kanisa, na kila mtu anadai kwa kauli moja kwamba mpinga Kristo aondolewe kanisani. Katika hali hizi, baadhi ya viongozi na wafanyakazi bado wanatetea kumwacha mpinga Kristo abaki ili atumike kama mafunzo ya kutenda kufichua, kupogoa, kuchanganua, kuzuia, na kufuatilia wapinga Kristo—je, bado kuna haja ya kupitia michakato hii? Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wanaweza kusema, “Tusipopitia michakato hii, si nitakuwa ninapuuza majukumu yangu? Ni kupitia tu michakato hii ndiko kunakoangazia jukumu langu kama kiongozi. Ni lazima nitekeleze kazi hii. Iwe ndugu wanakubali au la, ni lazima kwanza nimwache mpinga Kristo abaki. Kwanza nitamfichua, kisha nitampogoa na kumchanganua, na kuwaruhusu ndugu wathibitishe zaidi kwamba yeye ni mpinga Kristo. Baada ya makubaliano ya kauli moja, ndipo tutamwondoa au kumtimua. Je, hili halitakuwa na ufanisi zaidi?” Matokeo yake, katika kipindi hiki, mpinga Kristo anaanza kueneza mawazo ya kuwapotosha watu na kuvuruga kazi ya kanisa tena, akisababisha hofu miongoni mwa kila mtu, huku wengine wakikataa hata kuja kwenye mikutano. Ili kuonyesha azimio lao na kuthibitisha kwamba hawapuuzi majukumu yao, viongozi na wafanyakazi hawa hufuata tu utaratibu kwa juu juu na kuichelewesha kazi. Matokeo yake, wanapitia njia nyingi zisizo za lazima, wanavuruga utaratibu wa maisha ya kanisa, na kupoteza wakati wa thamani wa watu wateule wa Mungu katika kufuatilia ukweli, na baadaye ndipo wanamwondoa mpinga Kristo. Je, mbinu hii inakubalika? (La.) Ina kosa gani? (Ni kufuata tu kanuni na kufanya mambo kijuujuu.) Kusudi la viongozi na wafanyakazi kufanya kazi hizi ni lipi? (Kuwalinda watu wateule wa Mungu.) Kwa hivyo, ikiwa baadhi ya watu bado hawajamtambua mpinga Kristo na bado wameshikamana na yeye sana, na viongozi na wafanyakazi wanapoamua kumtimua mpinga Kristo kutoka kanisani, baadhi ya watu wanakasirika, wakisema kwamba nyumba ya Mungu haina upendo au haki kwa watu, haina kanuni katika jinsi inavyofanya mambo, na kadhalika, na hata baadhi ya watu waliochanganyikiwa wanapotoshwa na kushawishiwa na mpinga Kristo na wanataka kumfuata nje ya kanisa, ni kitu gani kinachopaswa kufanyika katika hali hii? Wakati huu, viongozi na wafanyakazi wanahitaji kufanya kazi fulani muhimu, kama vile kutekeleza kumpogoa mpinga Kristo na kutumia maneno ya Mungu kumfichua na kumchanganua ili ndugu waweze kujifunza masomo kivitendo na hatimaye wamtambue mpinga Kristo. Siku moja, wanasema, “Mtu huyu anachukiza sana. Kwa kweli yeye ni mtu mwovu na mpinga Kristo. Hebu tumwondoe haraka!” Hii si sauti ya mtu mmoja tu bali ni sauti ya ndugu wengi. Katika hali hii, je, bado kuna haja ya kufanya kazi ya kumzuia na kumsimamia mpinga Kristo? Hapana, mtimueni tu moja kwa moja. Viongozi na wafanyakazi wanaofikia kiwango hiki katika kazi yao wamepata matokeo ya kuwalinda watu wateule wa Mungu dhidi ya madhara ya wapinga Kristo. Hili linathibitisha nini? Kwa upande mmoja, linathibitisha kwamba ndugu wa kanisa hili wana utambuzi, ubora wa tabia, na hisia ya haki. Kwa upande mwingine, inaweza kuwa kwamba viongozi na wafanyakazi wana uwezo wa kufanya kazi halisi, au kwamba matendo ya mpinga Kristo huyu yako wazi sana, ubinadamu wake ni mbaya sana na mwovu sana, na kuamsha hasira ya umma, na yeye mwenyewe alijifungia njia mapema, akiwaepushia viongozi na wafanyakazi sehemu kubwa ya mchakato wa kumshughulikia. Je, hili haliokoi juhudi nyingi? Katika hali kama hiyo, kumwondoa au kumtimua ni jambo jema, sivyo? Zaidi ya hayo, kazi ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya ni pana na haihusu tu kazi hii moja. Je, unafikiri kwamba kumtimua mpinga Kristo ndio mwisho wake? Kwamba umefanikisha kila kitu kikamilifu? Sivyo hata kidogo! Una kazi nyingine ya kufanya. Kando na kuwashughulikia wapinga Kristo na kuwalinda watu wateule wa Mungu dhidi ya madhara yao, viongozi na wafanyakazi pia wana jukumu la kuwaongoza watu wateule wa Mungu kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, kuwaongoza kutatua tabia zao potovu, na kuwaongoza kutatua tabia yao ya mpinga Kristo, miongoni mwa kazi nyingine nyingi muhimu. Hata hivyo, mpinga Kristo akitokea wakati wa kufanya kazi hizi, basi kumshughulikia mpinga Kristo kunakuwa kipaumbele cha juu. Ni lazima kwanza wamfichue na kumshughulikia mpinga Kristo, na pia washiriki kuhusu vipengele vingine vya ukweli. Usumbufu wa mpinga Kristo ukitokea na ikawa vigumu sana kwa kazi nyingine kuendelea, huku kazi hiyo ikikabiliwa na kizuizi na mwingilio na mpinga Kristo akiathiri sana ukuaji wa uzima wa ndugu, utaratibu wa maisha ya kanisa, na mazingira ya kutekeleza wajibu, basi bila shaka ni muhimu kwanza kushughulikia janga hili kubwa na chanzo cha maafa. Ni baada tu ya mpinga Kristo kuondolewa na kushughulikiwa ndipo kazi nyingine inaweza kuendelea kawaida na kwa utaratibu. Kwa hivyo, mpinga Kristo akitokea kanisani na ndugu wakamtambua haraka ndani ya muda mfupi na kusema kwa kauli moja, “Nenda zako, mpinga Kristo!” je, hili halitawaepushia viongozi na wafanyakazi juhudi nyingi? Je, hupaswi kufurahi kwa siri? Unaweza kusema, “Nilikuwa na wasiwasi kwamba singeweza kumzuia mpinga Kristo huyu, ibilisi huyu. Pia nilikuwa na wasiwasi kwamba baadhi ya ndugu wangepotoshwa na kudhuriwa vibaya sana na yeye, na kwamba kimo changu mwenyewe kilikuwa kidogo sana nisiweze kufichua kiini cha mpinga Kristo, kuchanganua mambo haya kikamilifu, na kutatua tatizo hili.” Sasa, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Kwa kauli hii moja kutoka kwa ndugu, suala hilo linatatuliwa, na “mzigo” wa viongozi na wafanyakazi unaondolewa. Jambo hili ni zuri ajabu! Unapaswa kumshukuru Mungu; hii ni neema ya Mungu! Mambo ya aina hii huenda yakatokea kanisani, kwa sababu mengi yamejadiliwa kuhusu mada ya kuwafichua wapinga Kristo, na kwa sababu ndugu si duni sana ikilinganishwa na viongozi na wafanyakazi, kama unavyoweza kudhani. Chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, wao pia wana uwezo kiasi wa kuelewa ukweli na kutatua matatizo kwa kujitegemea. Wanapoungana kupiga kura na kumtimua mpinga Kristo, ni jambo jema, ni ishara nzuri! Viongozi na wafanyakazi hawahitaji kuhisi huzuni, kukata tamaa, au kuwa hasi kuhusu hili. Baada ya kuondoa vizuizi hivi vya wapinga Kristo, kila hatua ya kazi inayofuata bado inasalia kuwa jaribu kali kwa viongozi na wafanyakazi. Kila kazi wanayohitaji kufanya inahusisha majukumu yao na masuala yanayohusu ubora wa tabia na uwezo wao wa kazi.

Udhihirisho Ambao Viongozi wa Uwongo Huonyesha Wakati Wapinga Kristo Wanasababisha Usumbufu

Tumemaliza ushirika kuhusu jukumu la kumi na tatu la viongozi na wafanyakazi: “Kuwalinda watu wateule wa Mungu wasisumbuliwe, kupotoshwa, kudhibitiwa, na kudhuriwa vibaya sana na wapinga Kristo, na kuwawezesha watambue wapinga Kristo na kuwatelekeza kutoka mioyoni mwao.” Basi, tutachanganua na kufichua udhihirisho wa aina ya watu wasioweza kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi—viongozi wa uwongo—kwa kuwalinganisha na kazi ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kutimiza. Katika kufanya kazi hii, kuna kazi nyingi ambazo viongozi na wafanyakazi wanahitaji kufanya, zikiwahitaji kuwa na ubora fulani wa tabia, kuwa wasikivu, makini, wenye bidii, wawajibikaji, wenye kujali mzigo wa Mungu, kuwa na moyo wa upendo unaowalinda watu wateule wa Mungu, na kadhalika. Ni kwa kuwa na sifa hizi tu ndiyo wanaweza kutimiza majukumu na wajibu wao. Viongozi wa uwongo, hata hivyo, ni kinyume kabisa na hili; wanakosa sifa hizi katika ubinadamu wao. Wanaweza kuwa na ubora fulani wa tabia, wakiwa na uwezo wa kuelewa ukweli na kuwatambua wapinga Kristo, au wanaweza kuwa na ubora duni kiasi wa tabia, wakiweza angalau kuwatambua baadhi ya wapinga Kristo walio dhahiri wanaotenda maovu mengi hata kama hawawezi kung’amua kikamilifu kiini cha asili cha wapinga Kristo; au, ubora wao wa tabia unaweza kuwa duni sana kiasi kwamba hawawezi kutambua au kung’amua tofauti kati ya wale walio na kiini cha wapinga Kristo na wale walio na tabia ya mpinga Kristo. Kwa vyovyote vile, viongozi wa uwongo huonyesha dhihirisho hizi mbili: Moja ni kwamba hawafanyi kazi halisi; nyingine ni kwamba wanajihusisha tu na kazi ya juu juu, ya mambo ya jumla, huku wakiwa hawawezi kabisa kutatua matatizo halisi au kufanya kazi halisi. Katika kazi inayohusiana na jukumu la kumi na tatu, dhihirisho hizi mbili bainifu wa viongozi wa uwongo zinabaki kuwa dhahiri. Basi, tutashiriki kuhusu ni udhihirisho gani hasa walio nao.

I. Kutowafichua na Kuwashughulikia Wapinga Kristo kwa Hofu ya Kuwaudhi

Wapinga Kristo wanapowasumbua, kuwapotosha, kuwadhibiti, au kuwadhuru vibaya sana watu wateule wa Mungu, udhihirisho wa kwanza wa viongozi wa uwongo ni kutotenda. Kutotenda kunamaanisha nini? Kunamaanisha kutofanya kazi halisi. Kuna sababu za kutofanya kazi halisi, hasa hofu ya kuwaudhi watu na ukosefu wa ujasiri wa kuzingatia kanuni. Baada ya kuwa viongozi, watu hawa huanza kuonyesha mamlaka yao, wakiwaza, “Sasa nina hadhi, na mimi ni kiongozi wa kanisa. Lazima nisimamie chakula, mavazi, makazi, na usafiri wa ndugu; lazima nitambue kama kile ambacho ndugu wanasema kinalingana na ukweli na kinapatana na adabu za watakatifu. Lazima nione kama wao ni waaminifu kwa Mungu, kama maisha yao ya kiroho ni ya kawaida, kama wanafanya maombi ya asubibi na jioni, kama mikutano yao ya kawaida ni ya kawaida—lazima nisimamie haya yote.” Viongozi wa uwongo wanajali tu masuala haya. Kwa upande wa taratibu, wanaonekana kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi, lakini masuala muhimu ya kanuni yanapotokea, au hata wapinga Kristo wanapotokea, viongozi wa uwongo hujificha gizani bila kutoa sauti, ambapo wao hunyamaza na kujifanya kuwa hawajui na hawawezi kuona chochote. Haijalishi ni maoni yapi ya uwongo ambayo wapinga Kristo wanaeneza, wao hujifanya hawasikii. Wapinga Kristo wanapowasumbua, kuwapotosha, na kuwadhibiti watu wateule wa Mungu, wao pia hujifanya kuwa hawajui, kana kwamba habari hizi zote hupotea zinapowafikia. Wao hujifanya hawawezi kuwatambua wapinga Kristo ambao hata ndugu wa kawaida wanaweza kuwatambua, wakisema, “Siwezi kuwang’amua. Itakuwaje nikimtimua mtu asiyefaa? Itakuwaje nikiwakosea ndugu? Kando na hilo, nyumba ya Mungu bado inahitaji watu wa kutumikia!” Wakitumia visingizio vya kila aina kukwepa majukumu ya viongozi na wafanyakazi, wao huepuka kuwashughulikia wapinga Kristo na hawawalindi ndugu dhidi ya madhara ya wapinga Kristo. Hata baadhi ya viongozi wa uwongo husema, “Nikiwafichua wapinga Kristo kila wakati, itakuwaje wakiwachochea ndugu wanishambulie? Basi hakuna atakayenipigia kura katika uchaguzi ujao, na sitaweza kuwa kiongozi tena. Ushawishi wangu si wenye nguvu kama wao!” Ili kulinda hadhi na usalama wao binafsi, viongozi wa uwongo hawatimizi kabisa jukumu lao la kuwalinda watu wateule wa Mungu, wala hawawazuii wapinga Kristo kuwadhuru ndugu kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo. Wao hutenda kama mtu anayetaka kuwafurahisha wengine na kama mwoga, huku wakati huo huo wakiwa watu wabinafsi na wenye kudharauliwa. Hawawalindi ndugu bali wanafikiria kwa makini sana jinsi ya kujilinda wenyewe. Linapokuja suala la kuwashughulikia wapinga Kristo au kuwapogoa na kuwafichua ili ndugu waweze kupata utambuzi, wao huogopa sana, wakiwa na wasiwasi wa kupoteza hadhi yao, na wanahisi kwamba kufanya hivyo ni hasara kwao. Wao hupuuza kabisa masilahi ya watu wateule wa Mungu, wakizingatia tu masilahi yao wenyewe, sifa, usalama wa kibinafsi, na usalama wa familia zao, wakihofia kwamba kuwaudhi wapinga Kristo kimakosa kunaweza kuwafanya wawe na uadui mkali na kusababisha kulipiza kisasi. Kiongozi wa uwongo wa aina hii kwa kweli ana ubora fulani wa tabia. Kwa ubora wa tabia na ufahamu wao, wanajua kikamilifu ni nani walio wapinga Kristo, lakini tatizo liko katika hofu yao ya kuwaudhi wapinga Kristo. Wakiiona tabia katili ya wapinga Kristo, wao hawathubutu kuwaudhi. Ili kujilinda wenyewe, hata hivyo, wao hawasiti kutoa kafara masilahi ya nyumba ya Mungu na ya watu wateule wa Mungu; wao hutazama bila kujali huku ndugu wakikabidhiwa kwa wapinga Kristo, wakiwaruhusu wapinga Kristo kuwapotosha, kuwadhibiti, na kuwadhuru vibaya sana wapendavyo. Viongozi wa uwongo mara kwa mara huwaambia tu kwa siri kwa baadhi ya watu wasio na uovu walio na ubinadamu mzuri ambao hawahatarishi usalama wao, “Mtu huyo ni mpinga Kristo. Anawapotosha wengine. Yeye si mtu mwema.” Hata hivyo, mbele ya ndugu wote na mbele ya wapinga Kristo, wao hawathubutu kamwe kumwambia mpinga Kristo “hapana” hata mara moja. Hawana ujasiri kamwe wa kufichua matendo yoyote maovu au kiini cha wapinga Kristo. Hata wakati wa mikutano, wapinga Kristo wanapotawala mazungumzo na kuongea kwa saa moja au masaa mawili, wao hawathubutu kutoa sauti. Wapinga Kristo wakipiga meza na kuwakodolea watu macho, wao hawathubutu hata kupumua kwa sauti kubwa. Katika mawana ya kazi yao, wale walio na kimo kidogo, wale walio na ubinadamu waoga, na wale wanaotaka kufuatilia ukweli lakini bado hawajapata utambuzi huhisi kufadhaika kwa sababu hakuna viongozi au wafanyakazi wanaoweza kujitokeza kufichua na kutambua matendo maovu ya wapinga Kristo. Wao hutazama bila uwezo wa kufanya chochote huku wapinga Kristo wakitenda kidhalimu kanisani, wakitenda wapendavyo na kuvuruga maisha ya kanisa, bila njia yoyote ya kuwapinga. Viongozi wa uwongo, wakati huo huo, hawafanyi kazi yoyote halisi na hawatatui matatizo halisi kwa ajili ya watu wateule wa Mungu. Ndugu wanapoanguka katika matatizo, mbali na viongozi wa uwongo kushindwa kufichua na kuzuia matendo maovu ya wapinga Kristo, wao hata hawathubutu kusema neno moja la haki. Hata kama dhamiri yao inahisi kitu na kuwahukumu kidogo, na wanamwaga machozi machache katika maombi kwa Mungu faraghani, siku inayofuata wakati wa mkutano, wanapowaona wapinga Kristo wakitoa matamshi yasiyowajibika kuhusu kazi ya nyumba ya Mungu na kuihukumu kiholela, hata kumhukumu Mungu isivyo moja kwa moja na kueneza mawazo kumhusu Mungu, wanapuuza hilo licha ya kujua ni makosa. Hata wanapowaona wapinga Kristo wakibadhiri matoleo, wao huchukua mtazamo wa kulipuuza. Hawawafichui au kuwazuia wapinga Kristo hata kidogo, na bado hawahisi hata lawama kidogo mioyoni mwao—huu ni ukosefu mkubwa wa uwajibikaji! Mtu yeyote aliye na hisia fulani ya dhamiri, hata akihisi nguvu zake ni dhaifu sana, anapaswa kuungana na akina ndugu walio na kimo na utambuzi kiasi ili kushiriki kuhusu jambo hili na kujadili jinsi ya kuwashughulikia wapinga Kristo. Lakini viongozi wa uwongo wanakosa azimio na ujasiri kama huo, na hata zaidi, wanakosa hisia kama hiyo ya uwajibikaji. Wao hata huwaambia akina ndugu, “Wapinga Kristo ni wakatili sana. Tukiwaudhi, wataturipoti kwa serikali, na kisha hakuna hata mmoja wetu atakayeweza kumwamini Mungu. Wapinga Kristo wanajua maeneo ya mikutano ya kanisa, kwa hivyo hatuwezi kuwachokoza.” Hii ni tabia mbaya kabisa ya kuweka silaha chini na kujisalimisha kwa wapinga Kristo, ya kuafikiana na Shetani na kumwomba rehema.

Kando na kujilinda wenyewe, viongozi wa uwongo hawafanyi kazi yoyote ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya, kama vile kuwalinda watu wateule wa Mungu na kuwasaidia kupata utambuzi dhidi ya wapinga Kristo, na hawatimizi majukumu yoyote kabisa, na bado wanataka ndugu wawachague kama viongozi kila wakati. Baada ya kumaliza muhula mmoja, wanataka kuchaguliwa kwa muhula unaofuata. Je, huku si kukosa aibu na kutoweza kuokolewa? Je, watu kama hao wanastahili kuwa viongozi? (La.) Nyumba ya Mungu inakukabidhi wewe kundi la kondoo, lakini wanyama wa mwituni wanapokuja, wakati muhimu, wewe unajilinda tu na unalikabidhi kundi hilo kwa wanyama wa porini. Unatenda kama mwoga, ukitafuta kimbilio, mahali salama, pa kujificha. Na matokeo yake, kundi linadhurika—baadhi ya kondoo wanaumwa hadi kufa, na wengine wanapotea. Tuseme kwamba kiongozi anawaona wapinga Kristo wakivuruga kazi ya kanisa bila kujali na kuwapotosha na kuwadhibiti watu wateule wa Mungu, na bado anachukua mtazamo wa kulipuuza tu ili kulinda taswira, hadhi, na maisha yake, na kuhakikisha usalama wake mwenyewe. Watu wengi wateule wa Mungu kwa hivyo wanapotoshwa, wanahisi kutokuwa na msaada, na wanakuwa hasi na dhaifu; wengine hata wanatekwa na wapinga Kristo, na wengine hawataki kutekeleza wajibu wao. Na bado kiongozi huyu hahisi chochote anapoona usumbufu unaosababishwa na wapinga Kristo; dhamiri yake haihisi lawama. Je, kiongozi au mfanyakazi wa aina hii ana ubinadamu wowote? Kwa ajili ya kufikia lengo lao la kujihifadhi, hawasiti kuwakabidhi watu wateule wa Mungu kwa wapinga Kristo na kuwaruhusu wapinga Kristo kuwapotosha, kuwadhuru vibaya sana, na kuwaharibu. Huyu ni kiongozi wa aina gani? (Kiongozi wa uwongo.) Je, huyu si kibaraka wa Shetani? Kwa kweli yuko upande gani? Ingawa anaainishwa kama kiongozi wa uwongo, kiini cha suala hili kinaweza kuwa kibaya zaidi kuliko kile cha kuwa kiongozi wa uwongo. Kina asili ya kuwasaliti akina ndugu, kama vile watu wale wanaokamatwa na kuteswa na kuwa Mayuda, wakiwakabidhi ndugu kwa joka kuu jekundu ili wadhuriwe vibaya sana. Kwa hivyo, asili ya kiongozi wa uwongo anayewakabidhi watu wateule wa Mungu kwa wapinga Kristo ni ipi? Je, viongozi wa uwongo kama hao si waovu mno? Ikilinganishwa na wapinga Kristo, viongozi hawa wa uwongo hawaonekani kwa nje kuwa na nia ya kupinga ukweli. Wanaonekana kuweza kushiriki baadhi ya ukweli, kuwa na uwezo kiasi wa kuelewa, na kuweza kutenda ukweli kidogo, na baadhi yao wanaweza hata kuvumilia ugumu na kulipa gharama. Na bado, nyumba ya Mungu inapowakabidhi kundi la kondoo la Mungu, na watu waovu na ibilisi wanapotokea, hawatumii maisha yao wenyewe kufanya kila wawezalo kuwalinda watu wateule wa Mungu. Badala yake, wanafanya kila wawezalo kujilinda wenyewe, wakiwasukuma ndugu mbele ili watende kama ngao ya kinga ili kupata usalama na masilahi yao wenyewe. Watu hawa ni wa kudharauliwa na wabinafsi walioje! Kwa juu juu, ubinadamu wao unaonekana kutokuwa na masuala makubwa. Wana upendo kwa watu, wanaweza kuwasaidia wengine, wako tayari kulipa gharama na wanaweza kuvumilia ugumu wowote wanapotekeleza wajibu wao. Hata hivyo, wapinga Kristo wanapotokea, wanafanya kitu kisichotarajiwa na kisichoeleweka: Haijalishi jinsi wapinga Kristo wanavyowapotosha watu wateule wa Mungu au kuvuruga maisha ya kanisa, hawafanyi chochote, na haijalishi ni watu wangapi wanaoshambuliwa, kutengwa, au kudhuriwa na wapinga Kristo, wao hupuuza. Kwa kufanya hivyo, viongozi hawa wanawakabidhi kabisa watu wateule wa Mungu chini ya udhibiti wa wapinga Kristo, wakiwaruhusu wapinga Kristo wawapotoshe na kuwadhuru vibaya sana wapendavyo, huku viongozi hawa wenyewe hawafanyi kazi yoyote kabisa. Wapinga Kristo wanapoondolewa na tatizo kutatuliwa, viongozi hawa kisha hujitokeza kushiriki kuhusu kujijua kwao, kuhusu jinsi walivyokuwa dhaifu, waoga, wenye hofu, wabinafsi, na wadanganyifu, na kwamba hawakuwa waaminifu, hawakuwalinda watu wateule wa Mungu vizuri, na walimvunja moyo Mungu na ndugu. Wanaonekana wenye majuto sana; wanaonekana kuwa wamegeuka na kuwa na uwezo wa kutubu. Hata hivyo, wapinga Kristo wanapotokea tena, wao huwasukuma ndugu kwa wapinga Kristo kama walivyofanya wakati uliopita, na kujitafutia mahali salama pa kujificha. Ingawa wao wenyewe hawajapotoshwa au kudhuriwa na wapinga Kristo, wamepuuza majukumu yao na wamesaliti agizo la Mungu, na mtazamo wao kwa wajibu wao, mtazamo wao kwa watu wateule wa Mungu, na nafsi zao za kweli zimefichuliwa kabisa. Kila wakati wapinga Kristo wanapotokea, wao hawachagui kusimama upande wa Mungu na kupigana na wapinga Kristo hadi mwisho, na hawasemi kile kinachopaswa kusemwa hata kidogo au kufanya kazi inayopaswa kufanywa hata kidogo ili kuwalinda watu wateule wa Mungu na hivyo kuhisi amani katika dhamiri zao, na hata kidogo hawatimizi majukumu ya viongozi ili kuridhisha nia za Mungu. Chaguzi na matendo yote ya viongozi hawa wa uwongo ni kwa ajili ya kulinda hadhi yao wenyewe isidhuriwe. Hawajali kuhusu maisha au kifo cha watu wateule wa Mungu. Kwao kila kitu kiko sawa mradi sifa, masilahi, na hadhi yao wenyewe haiharibiwi. Ni nani anayewafichua wapinga Kristo, nani anayewatimua wapinga Kristo, jinsi wapinga Kristo wanavyopaswa kushughulikiwa—ni kana kwamba mambo haya hayawahusu; hawajali wala hawaingilii. Wapinga Kristo wanapovuruga maisha ya kanisa, kuwadhuru watu wateule wa Mungu, na kuwasingizia na kuwatesa wale wanaofuatilia ukweli, wao hupuuza. Mambo haya hayana maana kwao; yote yako sawa kwao, maadamu hadhi yao haiko hatarini. Mnaonaje kuhusu watu wa aina hii? Kawaida, ubinadamu wao hauonekani kuwa mbaya, na wanaonekana kuweza kufanya kazi fulani. Wanapokabiliwa na upogoaji, wanaonekana kuweza kujijua na kuwa na moyo wenye majuto kiasi. Hata hivyo, wanapokutana na wapinga Kristo wanaovuruga kanisa, wanapoteza kabisa busara yao, hawana hisia ya haki, na wanakosa hata ujasiri wa kupigana dhidi ya wapinga Kristo. Wanapowaona ibilisi na Mashetani, wao hulegeza msimamo; wanapowaona watu waovu wakisababisha usumbufu, wao huwaepuka. Tukihukumu kutokana na mtazamo wao kwa watu waovu na wapinga Kristo, ni njia gani hasa wanayoifuata? Je, si hili linaonyesha waziwazi suala lao? (Ndiyo.) Mtu wa aina hii anaweza kutoonekana kuwa mpinga Kristo kwa juu juu, lakini mtazamo anaouonyesha kwa matendo na tabia za watu waovu na wapinga Kristo ndiyo hasa tabia ya wapinga Kristo, na asili ya hili ni mbaya sana. Inaweza kusemwa kwamba ni asili ya kutelekeza majukumu yao na kuwasaliti watu wateule wa Mungu. Je, si asili hii ni mbaya sana? Je, wanaonyesha uaminifu wowote kwa kazi ya kanisa na agizo la Mungu? Je, wana hata chembe ya mtazamo wa uwajibikaji? Haijalishi ni lini wanakabidhiwa agizo au kazi, kanuni yao ni kuepuka kuwaudhi watu na kujilinda wenyewe. Hiki ndicho kiwango chao cha juu zaidi cha kujiendesha na kanuni yao ya kufanya mambo, na hili halitabadilika kamwe. Hebu tuweke kando kwa sasa swali la kama watu kama hao wanaweza kuokolewa—tukihukumu tu kwa upande wa kazi ya kuwashughulikia wapinga Kristo, je, viongozi hawa wa uwongo wanastahili kukubali agizo la Mungu? Je, wanastahili kuwa viongozi na wafanyakazi? (La.) Watu hawa hawastahili kuwa viongozi na wafanyakazi. Hii ni kwa sababu hawana dhamiri na busara, na hawastahili kuchukua kazi ya uongozi wa kanisa; hawawazuii wapinga Kristo, kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo, kuwadhuru watu wateule wa Mungu, na pia hawafanyi kila wawezalo kutimiza jukumu hili au kufanya kazi hii vizuri ili kuwalinda watu wateule wa Mungu—si kwamba wana ubora duni wa tabia na hawawezi kufanya hivi, bali ni kwamba hawafanyi tu. Kwa hivyo, tukilitazama kutokana na mtazamo huu, watu wanaoogopa kuwaudhi wengine hawastahili kabisa kuwa viongozi na wafanyakazi. Je, si kuna viongozi na wafanyakazi wengi wa aina hii? (Ndiyo.) Wakati ambapo hakujatokea jambo, wanakimbia huku na kule kwa shauku kuliko mtu mwingine yeyote; wana shughuli nyingi kiasi kwamba hawachani hata nywele zao au kuosha nyuso zao, wakionekana kufikia kiwango cha kiroho sana. Lakini wapinga Kristo wanapotokea, wao hutoweka; wanatafuta visingizio vya kila aina ili kukwepa, na hawashughuliki na wapinga Kristo. Asili ya tabia hii ni ipi? Ni kukosa uaminifu katika utendaji wa wajibu wao na kutokuwa wa kuaminika. Katika wakati muhimu, wanaweza hata kumsaliti Mungu na kusimama upande wa Shetani, wakiipa kisogo huku kazi ya kanisa ikivurugwa na kuharibiwa na watu waovu na wapinga Kristo. Hawana hata manufaa kama mbwa mlinzi. Hii ni aina ya kiongozi wa uwongo.

II. Kutoweza Kuwatambua Wapinga Kristo

Kuna aina nyingine ya viongozi wa uwongo: Wapinga Kristo wanapotokea, hawawezi kutambua wana tabia na kiini gani, kile wanachodhihirisha na kufunua, wanasababisha usumbufu wa aina gani kwa akina ndugu, ni kauli, mawazo, mitazamo, na tabia zipi zinaweza kuwapotosha na kuwasumbua akina ndugu, ni mbinu zipi ambazo wapinga Kristo hutumia kuwadhibiti watu, akina ndugu wanaweza kupotoshwa, kudhibitiwa, na kudhuriwa vibaya sana katika hali gani, na kadhalika—haya yote ni masuala ambayo viongozi wa uwongo hawawezi kutambua. Wapinga Kristo huwapotosha akina ndugu; wao na akina ndugu waliopotoshwa hujitenga na kanisa ili kufanya mikutano yao wenyewe na kuunda falme huru. Hawakubali uongozi wa nyumba ya Mungu, hawakubali mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu, na hawatii mipango au maelekezo yoyote kutoka kwa nyumba ya Mungu, sembuse kutii matakwa yoyote ya Mungu kwa watu. Lakini matendo yote kama hayo ya wapinga Kristo ya kuwapotosha watu wateule wa Mungu hayachukuliwi kama matatizo na viongozi wa uwongo. Hawawezi kuona tatizo katika hali hizi, na zaidi ya hayo hawawezi kuona jinsi maneno, matendo, mawazo, na mitazamo ya wapinga Kristo inavyowasumbua, kuwapotosha, na kuwadhuru watu. Hawawezi kuona athari hizi hasi na hawajui jinsi ya kuzitambua. Baadhi ya akina ndugu wa kawaida, kwa sababu ya kuona na kusikia mengi, wanaweza kuwa na utambuzi, hisia, na mwamko kiasi, lakini viongozi wa uwongo hawawezi kung’amua mambo haya. Hata mtu anapodokeza kwamba fulani anafanya mambo fulani ya kuwapotosha watu na kuunda makundi kwa siri, viongozi wa uwongo bado huzuia, wakisema, “Hatuwezi kueneza kauli hizi. Msisababishe usumbufu. Wao wana uhusiano mzuri—kuna ubaya gani wakifanya ushirika pamoja? Tunahitaji kuwapa watu uhuru!” Bado hawawezi kung'amua hili. Ikiwa hawawezi kung’amua mambo, wangeweza kuchunguza na kutafuta, na kufanya ushirika na akina ndugu wanaoelewa ukweli na walio na utambuzi kiasi. Hata hivyo, viongozi wa uwongo ni wenye kujihesabia haki sana. Akina ndugu wanapowakumbusha, hawakubali, wakiwaza, “Wewe ndiwe kiongozi au ni mimi? Kwa kuwa nilichaguliwa kuwa kiongozi, ni lazima ninaelewa ukweli kuliko mtu wa kawaida. Vinginevyo, kwa nini nichaguliwe mimi badala ya mtu mwingine? Hii inathibitisha kwamba mimi ni bora kuwaliko ninyi nyote. Bila kujali kama mimi ni mkubwa au mdogo kuwaliko ninyi, ubora wa tabia yangu bila shaka ni mzuri kuliko wenu. Mpinga Kristo anapotokea, ninapaswa kuwa wa kwanza kumtambua. Ninyi mkimtambua kwanza, sitakubali. Tutasubiri hadi mimi nimtambue kabla ya kufanya chochote!” Matokeo yake, mpinga Kristo hueneza uzushi na makosa mengi miongoni mwa akina ndugu, anapinga waziwazi mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu, na kulipinga na kulishambulia waziwazi kanisa, nyumba ya Mungu, na mipango ya kazi kutoka kwa Aliye juu. Mpinga Kristo hata huwavuta akina ndugu waziwazi upande wake ili washiriki katika mikutano ya kipekee ambapo washiriki humsikiliza tu mpinga Kristo mwenyewe akihubiri na kukubali uongozi wake. Hata wale walio na ubora duni zaidi wa tabia kanisani wanaweza kuona kwamba mtu huyu ni mpinga Kristo. Ni katika hali kama hiyo tu ndipo viongozi wa uwongo hukubali: “Lo, yeye ni mpinga Kristo! Imekuwaje nimegundua hili sasa hivi tu? La, kwa kweli niligundua hapo awali, lakini sikusema chochote kwa sababu niliogopa akina ndugu walikuwa na kimo kidogo na walikosa utambuzi.” Hata wao hubuni uwongo maridadi. Ni wazi kwamba ni kwa sababu wao wenyewe wamekufa ganzi, ni wapumbavu, wana ubora duni wa tabia, na hawawezi kutambua mpinga Kristo ndiyo maana wanawaacha akina ndugu wapate madhara mengi sana kutoka kwao. Badala ya kuhisi hatia, wanawalaumu akina ndugu kwa kuongea upuuzi, kueneza uvumi usio na msingi, kutoelewa watu, na kadhalika. Huyu ni kiongozi wa aina gani? Je, hajachanganyikiwa kabisa? Kiongozi kama huyo kimsingi hana uwezo wa kujitwika kazi ya kanisa. Kwa nje, mara nyingi yeye hula na kunywa maneno ya Mungu, huomba, huhudhuria mikutano, husikiliza mahubiri, huandika maelezo ya kiroho, na kuandika makala za ushuhuda, akionekana kuweka juhudi nyingi, lakini matatizo yanapotokea, hawezi kuyatatua, hawezi kutafuta ukweli kulingana na maneno ya Mungu, na bila shaka hawezi kuwatambua wapinga Kristo kwa kuzingatia maneno ya Mungu. Viongozi wa uwongo kwa kawaida wanaweza kuhubiri kwa saa moja au masaa mawili, na wanapofanya ushirika juu ya maneno ya Mungu na upitiaji wao wenyewe wanaweza kuongea bila kukoma, lakini wapinga Kristo wanapoeneza uzushi na kauli za uwongo, wakiwapotosha akina ndugu na kuisumbua kazi ya kanisa, hawana la kusema na hawafanyi kazi yoyote kabisa. Sio tu kwamba wanashindwa kuweka hatua zozote za kuzuia au kuwaongoza akina ndugu kutambua uzushi na kauli za uwongo za wapinga Kristo, lakini hata wanapoona vurugu na usumbufu unaosababishwa na wapinga Kristo, hawawafichui au kuwachanganua, wala hawawapogoi wapinga Kristo; hawafanyi kazi yoyote kabisa. Tatizo la watu kama hawa ni lipi? (Ubora wao wa tabia ni duni sana.) Licha ya ubora wao duni wa tabia, bado wanajisifu kwamba wao ni watu wa kiroho, viongozi wazuri, na wale wanaofuatilia ukweli na kupenda maneno ya Mungu, na wanasema bila aibu kwamba wameacha starehe za familia na za kimwili ili kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Kwa kweli, wao ni viongozi halisi wa uwongo wasiowajibika, wasio na dhamiri na busara, na waliokufa ganzi na wapumbavu kwa kiwango cha juu—wao ni Mafarisayo halisi, wanafiki. Wanajua tu jinsi ya kuhubiri mafundisho na kupiga kelele wakitaja kauli mbiu. Watu wanapowauliza maswali, wanaweza kutoa mbubujiko wa nadharia nyingi ili kuwapotosha, lakini kwa uhalisi, hawawezi kueleza kanuni za ukweli kwa uwazi hata kidogo. Hata hivyo, wanajiona kuwa na uwezo wa kufahamu na kuelewa ukweli. Mioyoni mwao, wanajua wazi kwamba watu wanapotafuta suluhu za matatizo kutoka kwao, hawawezi kutoa majibu yanayolingana na ukweli, lakini bado wanajifanya kuwa viongozi wazuri na watu wa kiroho. Je, si huku ni kukosa aibu kiasi? (Ndiyo.) Viongozi wengi wa uwongo wana sifa moja na tatizo moja: kutokuwa na chembe ya aibu. Wanafikiri kwamba kuwa na hadhi na cheo cha kiongozi na kuweza kuzungumzia nadharia za kiroho kunawafanya wawe watu wa kiroho. Wanatumia muda mwingi kuliko wengine kula na kunywa maneno ya Mungu, kusikiliza mahubiri, na kutazama video kutoka kwa nyumba ya Mungu, na kufanya ushirika zaidi na wengine kuhusu maneno ya Mungu, kwa hivyo wanaamini kwamba wanaweza kufanya kazi ya viongozi na wafanyakazi na kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Lakini ukweli ni kwamba suala kubwa la wapinga Kristo kuwapotosha na kuwasumbua watu wateule wa Mungu bila aibu linapotokea, wao hutazama tu lakini hawana uwezo wa kufanya chochote, na hawajui ni sehemu zipi za maneno ya Mungu za kutumia ili kuwaelekezea na kuwachanganua wapinga Kristo, ili akina ndugu wapate utambuzi, wawakatae wapinga Kristo kutoka mioyoni mwao, na kuepuka kupotoshwa na kudhibitiwa na wao. Ingawa wakati mwingine wanahisi wasiwasi kidogo ndani, bado wanafikiri kwamba wamemwamini Mungu kwa muda mrefu na wamesikiliza mahubiri mengi, na kwamba wanaelewa ukweli kuliko mtu wa kawaida na wanaweza kuongea kwa ufasaha. Mara nyingi wao hujisifu: “Mimi ni wa kiroho. Ninaweza kuhubiri. Ingawa siwezi kutatua tatizo la wapinga Kristo kuwapotosha na kuwasumbua watu wateule wa Mungu, na siwezi kuyahusisha maneno ya Mungu na wapinga Kristo na kuwatambua, nimefanya kazi ninayopaswa kufanya na kusema ninachopaswa kusema. Mradi akina ndugu wanaweza kuelewa, hiyo inatosha!” Kuhusu matokeo ya mwisho ni yapi, iwapo watu wateule wa Mungu wamelindwa, wao hawana uhakika kuhusu hili mioyoni mwao. Pia wanadhani wao ni werevu na wanajifanya kutatua matatizo, lakini mwishowe, wanazungumza tu maneno na mafundisho mengi bila kutatua masuala hayo. Hawawezi kushiriki ukweli ili kuwafichua na kuwachanganua wapinga Kristo. Badala yake, wao hutoa tu maneno na mafundisho ili kujihalalisha na kujitetea, wakizungumza kwa saa moja au masaa mawili na kuwaacha watu wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, na hata mambo waliyoyaelewa hapo awali yakiwa yametiwa ukungu. Wanashindwa kuwaokoa akina ndugu kutokana na upotoshaji wa wapinga Kristo, na pia wanashindwa kuwawezesha kuwatambua wapinga Kristo na kuwakataa kutoka mioyoni mwao—kamwe hawafikii matokeo ya kuwalinda akina ndugu. Hata kama wanaweza kuona tokeo hili, bado wanadai utambulisho wa kiongozi na hawajinyenyekezi ili kutafuta ukweli na wengine, au kuripoti tatizo kwa ngazi za juu ili kutafuta suluhu. Je, watu kama hao si wahuni? Wewe si kitu, lakini bado unajifanya. Unajifanya kwa ajili ya nini? Kwa kuwa huwezi kuwa kiongozi, unapaswa kujiuzulu na uende ukajifanyie kwingineko. Hupaswi kuwadhuru watu wateule wa Mungu! Unapokuwa ukijifanya, wapinga Kristo huchukua fursa ya kufanya mambo mengi maovu yanayowasumbua na kuwadhibiti watu, wakiwapotosha na kuwadhuru wengi! Nani ataliwajibikia hili? Nyumba ya Mungu itadai uwajibikaji kwa hili!

Baadhi ya viongozi na wafanyakazi hawafanyi kazi yoyote halisi wanaposhughulikia matukio ya wapinga Kristo, na pia hawawezi kuwatambua wapinga Kristo. Katika kipindi ambacho wapinga Kristo wanawapotosha na kuwadhibiti akina ndugu, hawajawahi kamwe kufichua kwa kweli matendo maovu na kiini cha wapinga Kristo, wala hawawezi kuvieleza kwa uwazi. Baadaye, baadhi ya watu wateule wa Mungu wenye utambuzi huwafichua na kuwafukuza wapinga Kristo, na viongozi hawa wa uwongo huhisi kwamba ni mafanikio yao wenyewe. Baada ya wapinga Kristo kufukuzwa, wao hufanya muhtasari na kuzungumza mafundisho fulani: “Tazameni, wapinga Kristo wanapozungumza na kutenda, maisha ya kanisa huwa si ya kawaida, watu husumbuliwa, na hupata hasara katika maisha yao. Ili kuepuka madhara ya wapinga Kristo, ni lazima tutambue matendo, maneno, ubinadamu, kiini, na kadhalika, vya wapinga Kristo—tunapaswa kuyaelewa mambo haya yote. Mungu anaruhusu kuonekana kwa wapinga Kristo kanisani, akiwaruhusu wafanye mambo na kufichua ubaya wao wenyewe, akiwafunua wapinga Kristo, ili tuweze kujiandaa na ukweli, tukue katika utambuzi, na kuongeza kimo chetu haraka iwezekanavyo—nia za Mungu zimo katika hili! Sasa tumewatambua wapinga Kristo na hatuzuiliwi tena nao; kila mtu anaweza kuwakataa. Hili ni jambo linalostahili kusherehekewa!” Mwishowe, viongozi wa uwongo huzungumza kwa sauti rasmi na kutoa muhtasari wao, wakizungumza kana kwamba wamefanya kazi nyingi halisi, wamelipa gharama kubwa, na wamefanya jukumu muhimu katika kuwafukuza wapinga Kristo. Je, huku si kukosa aibu kiasi? Bila shaka, tangu mwanzo hadi mwisho, hawakuweza kutambua mpinga Kristo ni nini; hawaelewi jinsi wapinga Kristo wanavyowapotosha watu, kile wapinga Kristo wanachowafanyia watu wateule wa Mungu, au kiini cha tabia ya wapinga Kristo ni kipi, lakini wanajifanya kana kwamba wamefanya kazi nyingi. Ni dhahiri kwamba ni akina ndugu waliowatambua wapinga Kristo na kuwafukuza kutoka kanisani; ni dhahiri kwamba viongozi wa uwongo hawakufanya jukumu ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya au kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi, lakini bado wanafanya muhtasari na kujipatia sifa, kana kwamba walikuwa wamepanga kila kitu tangu zamani na sasa wanawaambia akina ndugu kwamba matendo yao yamezaa matunda na kufanikiwa kabisa. Je, huku si kukosa aibu? Kwa nini unazungumza kwa sauti ya uafisa namna hiyo? Hufanyi kazi yoyote halisi na bado unazungumza kama afisa. Wewe ni afisa wa joka kuu jekundu? Je, watu kama hao si Wafarisayo? (Ndiyo.) Wanajua tu jinsi ya kupiga kelele wakitaja kauli mbiu na kuhubiri mafundisho. Mambo yanapotokea, si tu kwamba wanashindwa kuyashughulikia ipasavyo, lakini pia hawana njia ya utendaji. Wao huzungumza tu upuuzi na kutumia kanuni bila kufikiri; kimsingi hawawezi kutatua matatizo yoyote. Baada ya mambo kupita, wao hutenda kana kwamba hakuna kilichotokea, wanajifanya kuwa watu wema, na kujipatia sifa bila soni kabisa. Watu hawa ni Mafarisayo haswa. Wanaweza tu kuhubiri mafundisho, kupiga kelele wakitaja kauli mbiu, kuweka juhudi kiasi, na kuvumilia ugumu kiasi, na hawawezi kufanya kazi yoyote halisi, lakini bado wanajifanya kuwa watu wa kiroho. Wao ni Mafarisayo. Hiki ndicho kiini cha aina hii ya viongozi wa uwongo. Wanaweza kuhubiri mafundisho mengi sana mbele ya kila mtu, kwa nini basi hawawezi kuwafichua na kuwashughulikia wapinga Kristo? Wanaweza kuhubiri kwa saa kadhaa mfululizo na wana ufasaha mkuu, kwa nini basi, wanapokabiliwa na matatizo halisi—hasa wanapokabiliwa na matendo maovu ya wapinga Kristo—hawawezi kuyashughulikia, wakionekana wamepigwa na butwaa? Sababu ya hili ni ipi? Ni kwa sababu ubora wao wa tabia ni duni sana. Duni kiasi gani? Hawana ufahamu wa kiroho. Wana elimu na akili, ni werevu sana katika kushughulikia mambo ya nje, na wana uelewa kiasi wa sheria. Hata hivyo, inapokuja kwa mambo ya kumwamini Mungu, mambo ya kiroho, na masuala mbalimbali muhimu, hawawezi kutambua na hawawezi kung’amua chochote, wala hawawezi kupata kanuni zozote za ukweli. Wakati hakuna matatizo, wanakaa kwa utulivu kama mvuvi anayesubiri vuo lake, lakini masuala yanapotokea, wanatenda kama vikaragosi, kama sisimizi kwenye sufuria la moto, wakifunua sura ya kusikitisha. Wakati mwingine wanatenda kwa uzito na umakini mkubwa. Wasipokuwa makini, wanaonekana wa kawaida, lakini wanapokuwa makini, kwa kweli hilo huwafanya watu wacheke. Hii ni kwa sababu wanapokuwa makini, hawazungumzi chochote isipokuwa mambo ya uwongo na maneno yasiyo na ufahamu wa kiroho, yote yakiwa ni maoni ya mtu asiye na ujuzi. Hata hivyo, wanadumisha sura ya makini isiyo na hisia—je, hili si la kuchekesha? Mtu akiuliza maswali muhimu ili wayajibu, wao huchanganyikiwa na kukosa la kusema, wakionekana walioaibika sana. Kuna viongozi wengi wa uwongo kama hawa. Dhihirisho lao kuu ni ubora duni wa tabia na ukosefu wa ufahamu wa kiroho; wao ni watu waliochanganyikiwa. Inamaanisha nini kukosa ufahamu wa kiroho? Inapokuja kwa mambo ya kiroho na mambo yanayohusisha ukweli, ni kama wanajaribu kutafsiri Kigiriki cha kale—hawakielewi kabisa. Hata hivyo, bado wao hujifanya, wakisema, “Mimi ni wa kiroho. Nimemwamini Mungu kwa muda mrefu. Ninaelewa kweli nyingi. Ninyi ni waumini wapya, mmeanza tu kumwamini Mungu na hamwelewi ukweli. Hamtegemeki.” Wao daima hujiona kuwa wamemwamini Mungu kwa muda mrefu na wanaelewa ukweli. Watu kama hawa ni wa kuchukiza na wa kuchekesha. Hili linahitimisha ushirika juu ya dhihirisho za viongozi wa uwongo kama hawa.

III. Kuwa kama Mwavuli wa Kuwakinga Wapinga Kristo

Kuna aina nyingine ya viongozi wa uwongo ambao wanachukiza hata zaidi. Sio tu kwamba wanashindwa kuwafichua wapinga Kristo, lakini pia wanakuwa kama mwavuli wa kuwakinga wapinga Kristo, wakitumia usaidizi wa upendo kama kisingizio cha kuyadekeza matendo maovu ya wapinga Kristo yanayosumbua kazi ya kanisa. Haijalishi ni kauli ngapi za uwongo ambazo wapinga Kristo hueneza ili kuwapotosha watu, mbali na viongozi hawa wa uwongo kutozipinga au kuzifichua, wao pia huwapa fursa wapinga Kristo kueleza mitazamo yao na kuzungumza kwa uhuru. Bila kujali ni aina gani za usumbufu, upotoshaji, au madhara ambayo watu wateule wa Mungu hupitia, wao hawajali. Hata watu wengine wanapodokeza: “Watu hawa ni wapinga Kristo. Wao ni wale wanaopaswa kuzuiwa na nyumba ya Mungu; hawapaswi kuendelezwa au kukuzwa, na bila shaka hawapaswi kulindwa. Wamewadhuru akina ndugu vya kutosha. Ni wakati wa kuwawajibisha na kuwafichua na kuwashughulikia kikamilifu,” viongozi wa uwongo hujitokeza kuwatetea wapinga Kristo. Wakizingatia mambo kama umri wa wapinga Kristo, miaka ambayo wamemwamini Mungu, na michango ya awali, wanatumia visingizio mbalimbali kuwatetea na kuwalinda. Viongozi wa ngazi za juu wanapoenda kukagua kazi au kuwashughulikia wapinga Kristo, viongozi wa uwongo huwazuia akina ndugu kuripoti ukweli wa matendo maovu ya wapinga Kristo kwa walio katika ngazi za juu. Hata wanachukua hatua za kulifunga kanisa ili viongozi wa ngazi za juu wasijue kuhusu wapinga Kristo wanaolisumbua kanisa, na pia huwazuia akina ndugu wenye utambuzi kuwafichua wapinga Kristo. Bila kujali ni visingizio gani ambavyo viongozi wa uwongo hutumia au ni madhumuni gani waliyo nayo ya kuwa kama mwavuli wa kuwakinga wapinga Kristo, kwa kufanya hivyo, hatimaye wanalinda maslahi ya wapinga Kristo huku wakisaliti maslahi ya kanisa na watu wateule wa Mungu. Wanatumia visingizio mbalimbali kuwalinda wapinga Kristo, kama vile “wapinga Kristo pia wanamwamini Mungu na wana haki ya kuzungumza katika nyumba ya Mungu” na “wamewahi kufanya wajibu hatari hapo awali; nyumba ya Mungu inapaswa kuzingatia michango yao ya zamani.” Wanawazuia akina ndugu kuwatambua wapinga Kristo na hawawaruhusu viongozi wa ngazi za juu kujifunza kuhusu matendo yao mbalimbali maovu, huku, wakati huo huo wao wenyewe hawawafichui na bila shaka hawawapogoi wapinga Kristo. Wapinga Kristo hawa wanaweza kuwa wanafamilia wao, marafiki wa karibu, au, hata zaidi, watu wanaowaabudu na ambao wanapata ugumu kuwaachilia. Bila kujali hali, maadamu wanajua kwamba watu hawa ni wapinga Kristo na bado wanatetea matendo yao maovu, wakiwaambia wengine wawachukulie kwa upendo, na hata kutumia njia mbalimbali kuwapa wapinga Kristo fursa za kueneza kauli mbalimbali za uwongo ili kuwapotosha na kuwasumbua watu wateule wa Mungu, dhihirisho hizi zinaonyesha kwamba wanakuwa kama miavuli ya kuwakinga wapinga Kristo. Baadhi ya viongozi wa uwongo wanaweza kuwa wamefanya kazi halisi kiasi katika maeneo mengine, lakini inapokuja suala la kuwashughulikia wapinga Kristo, hawawashughulikii kulingana na matakwa ya nyumba ya Mungu. Zaidi ya hayo, hawatimizi majukumu ya viongozi na wafanyakazi kama inavyotakiwa na nyumba ya Mungu—hawawakomeshi wapinga Kristo kueneza mawazo, hisia hasi, uzushi, na kauli za uwongo kwa kiwango kikubwa zaidi ili kuwapotosha watu kanisani. Badala yake, mara nyingi wao hutetea mafundisho ya kupotosha yanayoonekana kuwa ya kweli yanayosemwa na wapinga Kristo, pamoja na kauli na matamshi yao ambayo yanatokana na maarifa au falsafa ya Shetani, kama mambo chanya. Haya yote ni dhihirisho lao la kuwa kama miavuli ya kuwakinga wapinga Kristo. Bila shaka, pia kuna baadhi ya viongozi wa uwongo ambao hawawashughulikii wapinga Kristo kwa sababu wanathamini ushawishi wao katika jamii. Wanasema, “Akina ndugu wengi wanatoka katika tabaka la chini la jamii na hawana ushawishi. Ingawa mtu huyu ni mpinga Kristo mwenye ubinadamu mwovu, ana mamlaka na ushawishi duniani na ana uwezo. Akina ndugu au kanisa linapokabiliwa na hatari, je, hatuhitaji mtu wa kuogofya kujitokeza na kutulinda? Kwa hivyo, hebu tufumbie macho makosa yao na tusiwe wakali sana kuhusu hilo.” Viongozi wa uwongo wako tayari kuwa kama miavuli ya kuwakinga wapinga Kristo ili wapinga Kristo wawatetee na kuwaunga mkono—viongozi wa uwongo wanaweza kufanya hata jambo hili. Pia kuna baadhi ya viongozi wa uwongo walio na mtazamo potovu. Wao husema, “Baadhi ya wapinga Kristo wana hadhi na ushawishi katika jamii; wana heshima. Kanisa letu lina watu wawili kama hao. Ingawa wao ni wapinga Kristo, tukiwaondoa, watu watafikiri kwamba kanisa letu halina watu wenye uwezo, na wale walio miongoni mwa makundi ya kidini watatudharau. Tunahitaji kuwaweka kwa ajili ya maonyesho. Kwa hivyo, watu hawa wawili ni hazina za kanisa letu; hakuna anayeweza kuwatambua au kuwaondoa. Lazima walindwe.” Haya ni mantiki ya aina gani? Wanawachukulia wapinga Kristo kama watu wenye talanta, kwa hivyo wanawalinda. Je, viongozi hawa wa uwongo si waovu? (Ndiyo.) Bila kujali hali, maadamu viongozi na wafanyakazi wanawaruhusu wapinga Kristo kufanya chochote wanachotaka kanisani na kusumbua kazi ya kanisa, wao ni viongozi na wafanyakazi wa uwongo. Bila kujali jinsi wapinga Kristo na watu waovu wanavyoeneza kauli za uwongo, ni watu wangapi wanapotoshwa, jinsi wanavyoshambulia na kuwatenga watu chanya, na wanawadhuru watu wangapi wateule wa Mungu, viongozi wa uwongo hupuuza na kujifanya viziwi—mradi tu wanaweza kujihifadhi wenyewe, hilo linawatosha. Hili ndilo dhihirisho kuu la viongozi wa uwongo. Haijalishi wapinga Kristo wanasema au wanafanya nini, viongozi wa uwongo hawawafichui, kuwachanganua, au kuwazuia ili akina ndugu waweze kuwatambua na kuwakataa. Badala yake, wanawalea wapinga Kristo kama wanyama wao wa kufugwa, wanawahudumia na kuwalinda kama waheshimiwa, wanawafungulia njia, na kuwatengenezea fursa mbalimbali za wao kujionyesha. Ni maslahi ya nani yanayotolewa kafara huku wakiwaacha wapinga Kristo wafurahie uhuru wao kikamilifu? (Maslahi ya watu wateule wa Mungu.) Si tu kwamba viongozi wa uwongo wanashindwa kuwalinda watu wateule wa Mungu, lakini pia wanawaruhusu wapinga Kristo wachukue usukani kanisani, wakiwafanya akina ndugu wawatumikie wapinga Kristo kama ng’ombe na farasi, kama watumwa, wakiwafanya wafuate maagizo ya wapinga Kristo, wakubali matamshi na mawazo na mitazamo yao ya uwongo, wakubali udhibiti wao, na hata kukubali madhara makubwa wanayoyafanya, na kadhalika. Hii ndiyo kazi ambayo viongozi wa uwongo hufanya. Je, wanawazuia wapinga Kristo kuwadhuru vibaya sana watu wateule wa Mungu kwa kiwango kikubwa? Je, wametimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi? Je, wamefanya kazi ya kuwalinda watu wateule wa Mungu? (Hapana.) Kwa ufupi, bila kujali sababu ni ipi, kiongozi yeyote anayewafungulia njia wapinga Kristo ili wafanye wapendavyo bila kufanya kazi yoyote ni kiongozi wa uwongo. Kwa nini Ninasema wao ni viongozi wa uwongo? Kwa sababu wapinga Kristo wanapowapotosha na kuwadhibiti watu wateule wa Mungu, wanawaacha akina ndugu wateseke mno kutokana na madhara mbalimbali ya wapinga Kristo, wakisaliti agizo walilopewa na Mungu. Nyumba ya Mungu iliwakabidhi kondoo wa Mungu, watu wateule wa Mungu, kwako, na wewe hukutimiza jukumu lako. Hustahili kujitwika agizo la Mungu! Bila kujali sababu au uhalali wowote unaoweza kuwa nao, ikiwa wakati wa uongozi wako ulitenda kama mwavuli wa kuwakinga wapinga Kristo, na kuwasababisha akina ndugu wateseke mno kutokana na usumbufu, upotoshaji, udhibiti, na madhara makubwa ya wapinga Kristo, basi wewe ni mwenye dhambi wa enzi zote. Sababu ya hili ni, si kwamba huwezi kuwatambua wapinga Kristo au kung’amua kiini chao—unajua wazi moyoni mwako kwamba wapinga Kristo ni Mashetani na ibilisi, lakini huwaruhusu watu wateule wa Mungu wawafichue na kuwatambua. Badala yake, unawaacha akina ndugu wawasikilize, kuwakubali, na kuwatii. Hii ni kinyume kabisa na ukweli. Je, hili halikufanyi uwe mwenye dhambi wa enzi zote? (Ndiyo.) Mbali na wewe kushindwa kuwalinda wale wanaofanya wajibu wao kwa dhati na kufuatilia ukweli, pia uliwaendeleza wapinga Kristo hadi nafasi za viongozi na wafanyakazi, ukiwalea kama wanyama wa kufugwa na kuwafanya akina ndugu watii maagizo yao. Nyumba ya Mungu haikuwakabidhi watu wateule wa Mungu kwako wawatumikie wapinga Kristo kama watumwa au kama watumwa wako, bali ili uwaongoze watu wateule wa Mungu kupigana dhidi ya Shetani na wapinga Kristo na kuwatambua na kuwakataa wapinga Kristo, na kuwawezesha watu wateule wa Mungu kuishi maisha ya kawaida ya kanisa, kufanya wajibu wao kwa kawaida, kuingia katika uhalisi wa ukweli, na kumtii na kumshuhudia Mungu chini ya uongozi wa Mungu. Ikiwa huwezi hata kutimiza wajibu huu, je, unastahili kuitwa mwanadamu? Na bado unataka kuwalinda wapinga Kristo. Je, wapinga Kristo ni mababu zako au kipenzi chako? Hata kama una uhusiano wa damu nao, unapaswa kuzingatia kanuni za ukweli na kuipa haki kipaumbele mbele ya familia. Unapaswa kuhisi ni wajibu wako kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi—kuwafichua, kuwatambua, na kuwakataa wapinga Kristo, na kufanya kila uwezalo kuwalinda akina ndugu kwa nguvu zako zote, ili kuwazuia wasidhuriwe na wapinga Kristo. Huku ni kufanya wajibu wako kwa uaminifu na kukamilisha agizo la Mungu; ni kwa kufanya hivi tu ndiyo unaweza kuitwa kiongozi au mfanyakazi anayefikia kiwango kinachostahili. Ikiwa unashindwa kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi na kwa hiari unakuwa kama mwavuli wa kuwakinga wapinga Kristo, unaweza kuwa nini kingine isipokuwa mwenye dhambi wa enzi zote? Hili linahitimisha ushirika juu ya viongozi wa uwongo wanaotenda kama miavuli ya kuwakinga wapinga Kristo. Ni wazi kwamba, kuwaweka watu kama hao miongoni mwa viongozi wa uwongo si dhuluma hata kidogo; hili ni mojawapo ya dhihirisho za viongozi halisi wa uwongo.

IV. Kutojali au Kuuliza Kuhusu Watu Ambao Wamepotoshwa na Wapinga Kristo

Kuna udhihirisho mwingine wa viongozi wa uwongo ambao unakasirisha hata zaidi. Baadhi ya viongozi wa uwongo wanaweza kuwapambanua wapinga Kristo kwa kiwango fulani wakati wa mwingiliano wao lakini hushindwa kuwashughulikia papo hapo. Pia wao hushindwa kufichua na kuchanganua papo hapo matendo maovu na kiini cha wapinga Kristo kupitia tabia zao mbalimbali, wakiwawezesha ndugu na dada kuwatambua na kuwakataa wapinga Kristo. Hili tayari linahesabika kama kutotimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Baadhi ya ndugu na dada wanapopotoshwa na kuwafuata wapinga Kristo, viongozi hawa wa uwongo hubaki bila kujali, kana kwamba jambo hilo haliwahusu. Zaidi ya hayo, hawasikii kujilaumu au kujishutumu kokote mioyoni mwao. Hawahisi kwamba wamemkosea Mungu au ndugu na dada. Badala yake, mara nyingi wao husema kauli hii “maarufu”: “Watu hawa walipotoshwa na wapinga Kristo. Wanastahili jambo hilo! Ni kosa lao kwa kukosa utambuzi. Hata kama hawangewafuata wapinga Kristo, bado wangekuwa walengwa wa kuondolewa na nyumba ya Mungu.” Mbali na viongozi hawa wa uwongo kutojilaumu au kuhisi hatia baada ya ndugu na dada kupotoshwa na wapinga Kristo, wao pia lakini hata zaidi hawatafakari au kutubu. Badala yake, wao husema mambo ya kikatili, wakidai kwamba ndugu na dada hawa walistahili kupotoshwa na wapinga Kristo. Ni jambo lipi linaloweza kuonekana kutoka katika maneno haya? Je, watu hawa wana ubinadamu wowote? (La.) Ukosefu wao wa ubinadamu ni hakika. Basi kwa nini wanasema mambo haya? (Ili kukwepa kujukumika.) Kwanza, ni kukwepa kujukumika, kuwapotosha na kuwazima watu hisia. Wao huamini: “Watu hao walipotoshwa na wapinga Kristo kwa sababu wanakosa utambuzi, jambo ambalo halinihusu mimi. Hawakufuatilia ukweli, kwa hivyo walistahili kupotoshwa!” “Walistahili” linamaanisha nini? Linamaanisha watu hawa wanapaswa kupotoshwa na kudhibitiwa na wapinga Kristo, na wanapaswa kudhuriwa vibaya sana na wapinga Kristo—matendo yoyote wanayopokea kutoka kwa wapinga Kristo, wanastahili kuyapitia; wanastahili kuwafuata wapinga Kristo. Dokezo ni kwamba watu hawa hawapaswi kumfuata Mungu bali wanapaswa kuwafuata wapinga Kristo, kwamba kumfuata Mungu lilikuwa kosa upande wao, na Mungu kuwachagua lilikuwa kosa pia, na kwamba ingawa wameingia katika nyumba ya Mungu, kuongozwa kwao na wapinga Kristo kulikuwa jambo lisiloepukika. Je, si hivi ndivyo viongozi wa uwongo wanavyodokeza? Mbali na kuwakashifu ndugu na dada, bali wao pia wanamkufuru Mungu. Je, watu kama hao si wenye kuchukiza? (Ndiyo.) Wanachukiza mno! Mbali na kukwepa kujukumika na kufunika ukweli wa mambo kwamba hawakuwalinda ndugu na dada, hata wanawashambulia, wakisema kwamba watu hawa walistahili kupotoshwa na wapinga Kristo na kwamba hawastahili kumwamini Mungu na kupokea wokovu wa Mungu. Kauli hii moja hufichua jinsi tabia yao ilivyo duni! Ingawa hawakusumbua, kuwapotosha, au kuwakandamiza ndugu na dada moja kwa moja kama wapinga Kristo, mtazamo wao kwa ndugu na dada, kwa agizo la Mungu, na kwa kundi walilokabidhiwa na nyumba ya Mungu unaonyesha jinsi wasivyo na huruma na wakatili kwa kweli! Hakuna anayekubali kazi ya Mungu kwa urahisi; inajumuisha kujitolea na ushirikiano wa wale wanaohubiri injili. Hili hugharimu nguvu kazi na rasilimali nyingi, na, hata zaidi, damu ya moyo wa Mungu imo ndani yake. Ni Mungu anayepanga watu, matukio, vitu, na mazingira mbalimbali ili kuwaleta watu mbele Yake. Viongozi wa uwongo hawatilii maanani lolote kati ya haya. Haijalishi ni nani anayepotoshwa na wapinga Kristo, wao hulipuuzilia mbali kwa msemo mmoja tu: “Wanastahili jambo hili!” Kwa kufanya hivyo, wanafanya bidii yote ya kila mtu aliyehusika na damu ya moyo wa Mungu kupotea bure, na kuipoteza yote. “Wanastahili” linamaanisha nini? Linamaanisha, “Ni nani aliyewaambia muwahubirie injili? Hawastahili kumwamini Mungu. Kuwahubiria injili lilikuwa kosa. Nani aliyewaambia wawafuate wapinga Kristo? Ingawa sikufanya kazi yoyote halisi, pia sikuwafanya wawafuate wapinga Kristo. Walisisitiza kufanya hilo wenyewe; walistahili kuwafuata wapinga Kristo!” Mtu kama huyu ana ubinadamu wa aina gani? Je, ana moyo wowote? Yeye ni mnyama mkatili, mbaya kuliko mbwa mlinzi, na bado yeye ni kiongozi? Hastahili! Ni lazima muwe na utambuzi: Mkiona kwamba watu kama hao wanakosa dhamiri na busara na wana moyo usio na huruma, ni lazima msiwachague kama viongozi. Msipumbazike! Sio tu kwamba wanashindwa kufanya kila liwezekanalo ili kufidia hasara na kuwarejesha wale waliopotoshwa na wapinga Kristo, bali pia wao husema mambo ya kikatili—wana nia mbaya sana! Tatizo la mtu wa aina hii ni zito zaidi kiasili kuliko lile la kiongozi wa uwongo wa kawaida. Ingawa hawezi kuchukuliwa kama mpinga Kristo, kulingana na udhihirisho wake, ni wazi hana ubinadamu na hastahili kuwa kiongozi au mfanyakazi. Yeye ni kikaragosi kibovu tu, kisicho na shukrani! Hajui agizo la Mungu ni nini, wala hana ufahamu wowote wa kazi anayopaswa kufanya. Halishughulikii kwa dhamiri na busara; hastahili kuwa kiongozi wa watu wateule wa Mungu na hastahili kukubali agizo la Mungu. Hasa, viongozi wa uwongo hawana upendo kwa watu wateule wa Mungu. Ndugu na dada wanapopotoshwa, wao hata huwaongezea chumvi kwenye kidonda, wakisema mambo kama “Walistahili jambo hilo,” bila kuonyesha huruma yoyote. Mtu kama huyo, akimwona mtu amepatwa na bahati mbaya au matatizo, hatamsaidia bali atamwongezea chumvi kwenye kidonda. Dhamiri yake haitahisi kujilaumu kokote, na ataendelea kuwa kiongozi jinsi alivyokuwa daima. Je, huku si kukosa aibu? (Ndiyo.) Bila kuwataja ndugu na dada, hata kama mtu mwema asiyeamini anadhuriwa vibaya sana na maibilisi, kama muumini katika Mungu na kama kiumbe aliyeumbwa, yeyote aliye na ubinadamu wa kawaida angehisi huruma; moyo wake unapaswa kuhisi uchungu zaidi kiasi gani wakati ni ndugu na dada—wale wanaomwamini Mungu kwa dhati—wanaopotoshwa na kudhuriwa na wapinga Kristo. Viongozi hawa wa uwongo hawafanyi kazi halisi wapinga Kristo wanapokuwa wakitenda maovu na kuwadhuru watu wateule wa Mungu. Hawafichui wala kuchanganua matendo maovu na kiini cha wapinga Kristo, achilia mbali kuwa na mzigo wa kuwasaidia ndugu na dada kupata utambuzi wa wapinga Kristo na kuwakataa kutoka mioyoni mwao. Hawahisi hisia yoyote ya uwajibikaji kwa jambo hili. Hata watu wengine wanapopotoshwa na wapinga Kristo, wao hutoa tu kauli baridi, isiyo na hisia, “Wanastahili jambo hilo.” Inakasirisha kweli! Ili kukwepa kujukumika, kujihifadhi, kuwapotosha na kuwazima hisia watu wengi zaidi, na kuepuka kushutumiwa na Mungu, wanasema mambo ya kikatili. Je, si hili ni jambo la kuchukiza? (Ndiyo.) Haijalishi mnasema nini, hamkutimiza majukumu yenu, na hamkuifanya kazi yenu ipasavyo—huu ni udhihirisho wa viongozi wa uwongo; hamwezi kuyakana mambo haya haijalishi mnajaribu kiasi gani. Ninyi ni viongozi wa uwongo.

Mbali na baadhi ya viongozi wa uwongo kuwa na moyo usio na huruma, bila hisia, na bila kuwajibika baada ya baadhi ya ndugu na dada kupotoshwa na wapinga Kristo, wakisema kwamba watu hawa walistahili kupotoshwa, lakini hata mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu inapotaka kwamba watimize wajibu wao wa kuwarejesha wale walio na ubinadamu mzuri kiasi na tumaini la kurejeshwa miongoni mwao kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo, viongozi hawa wa uwongo bado hawafanyi kazi yoyote halisi. Hata watu wengine wanapoomba kurudi kanisani, wao hubaki kuwa wasiojali na wenye dharau, wasiyachukulii maisha ya watu kama kitu cha thamani zaidi. Wanashindwa kuwarejesha ndugu na dada hao waliopotoshwa kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo. Hawawezi kutimiza jukumu hili, na hawafanyi juhudi zozote kulitimiza. Ingawa mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu inataka mara kwa mara kazi hii ifanywe vizuri, viongozi wa uwongo hawatingishiki, hawachukui hatua yoyote wala kufanya kazi yoyote. Matokeo yake, baadhi ya watu waliopotoshwa na wapinga Kristo na waliotengwa au kuondolewa bado hawawezi kurudi katika nyumba ya Mungu na hawajaanza tena maisha ya kawaida ya kanisa. Bila shaka, baadhi ya watu kwa kweli hawafikii masharti ya kurejeshwa na nyumba ya Mungu katika nyanja mbalimbali, lakini kuna wengine ambao wanaweza kurejeshwa. Ikiwa, kupitia msaada wa upendo na uungwaji mkono wa subira, wanaweza kuuelewa ukweli, kuwatambua, na kuwakataa wapinga Kristo, wanaweza kurejeshwa. Hata hivyo, kwa sababu viongozi na wafanyakazi hawafanyi kazi halisi, hawatekelezi mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu, na hawayachukulii maisha ya watu hawa kama muhimu, baadhi ya watu bado wameachwa wakizurura nje. Viongozi na wafanyakazi hawa huipuuza mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu wakitumia visingizio mbalimbali. Hata wanawapuuza ndugu na dada hao wanaotaka kurudi kanisani na wanafikia masharti ya kanisa ya kukubaliwa. Wao huja na visingizio vya kila aina, wakisema kwamba watu hawa wana ubinadamu mbaya, wanakabiliwa na hatari za kiusalama, wanapenda kujipamba, wanafurahia anasa za kimwili, wanapenda hadhi, na kadhalika. Wakitumia visingizio na sababu hizi za kubuni, wao hukataa kuwaruhusu warudi kanisani. Watu hawa wamepotoshwa na wanadhibitiwa na wapinga Kristo, lakini kupotea kwao hakuwahangaishi viongozi wa uwongo. Hawana hisia yoyote ya wajibu wala hisia yoyote ya dhamiri. Labda wanafikiri kuwarejesha watu hawa ni vigumu au ni hatari, au labda hawako tayari na hawakubaliani nao ndani kabisa. Kwa vyovyote vile, kwa sababu mbalimbali, hawatekelezi kabisa mpango huu wa kazi wa nyumba ya Mungu. Huu ndio udhihirisho wa viongozi wa uwongo kama hao. Sio tu kwamba wanashindwa kushirikiana kikamilifu na kutimiza majukumu yao kuhusu kazi yoyote waliyopewa na Mungu au nyumba ya Mungu, lakini mtu anapofichua kutowajibikia majukumu yao, wao hujitetea, wakisema mambo yanayokwepa majukumu yao na kujihalalisha ili kufunika ukweli wa kutowajibikia majukumu kwao. Je, viongozi wa uwongo kama hao si ni wenye kuchukiza zaidi? (Ndiyo.) Kwa muhtasari, viongozi hawa wa uwongo pia ni wasiojali wanaposhughulika na wapinga Kristo wanaowadhuru vibaya sana watu wateule wa Mungu, na hawafanyi kazi yoyote halisi. Wao hupuuza kila undani wa kazi hii unaohitajika na nyumba ya Mungu. Hawako tayari kuvumilia ugumu au kulipa gharama, wakipendelea tu kufanya wapendavyo na kutenda jinsi wanavyotaka—wakifanya kidogo wakijisikia, na kutofanya chochote wasipojisikia. Wanaipuuza kabisa mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu, wanapuuza wajibu na majukumu waliyokabidhiwa na nyumba ya Mungu, na hasa wanapuuza nia na matakwa ya Mungu. Watu hawa hawana ubinadamu wala dhamiri; wao ni kama maiti zinazotembea tu. Je, mngethubutu kulikabidhi jambo hili kuu la maisha yenu ya kufuatilia wokovu katika kumwamini Mungu kwa watu wasio na ubinadamu? (La.) Hata kama hawatakukabidhi kwa wapinga Kristo, je, watafanya kila wawezalo kupigana dhidi ya wapinga Kristo wanapowapotosha na kuwadhuru vibaya sana watu wateule wa Mungu? La, hawatafanya hivyo, kwa sababu watu kama hao ni wanyama wakatili wasiowajibika. Wao hutumikia kama viongozi ili tu kujipatia manufaa wenyewe.

Wakati mwingine viongozi wa uwongo huonyesha kuwajali ndugu na dada; huwauliza kama kuna chochote wanachohitaji, jinsi wanavyoendelea kuhusu chakula na malazi, na kadhalika. Wao hutilia maanani sana linapokuja suala la mambo yanayohusiana na maisha ya kila siku, lakini linapokuja suala la mambo yanayohusisha agizo la Mungu, uzima na mauti ya ndugu na dada, na kanuni za ukweli, wao hubaki bila kujali na hawafanyi chochote bila kujali ni nani anayewauliza. Wanajali tu anasa za kimwili za watu, chakula, mavazi, makao, usafiri, au manufaa ya kimwili, na wanashughulikia tu mambo kama hayo. Watu wengine husema, “Maneno Yako yanakinzana. Je, si Ulisema kwamna wana moyo usio na huruma? Je, mtu mwenye moyo usio na huruma angekuwa tayari kuwafanyia wengine mambo haya?” Je, mtu mwenye moyo usio na huruma angekuwa na moyo mwema kiasi cha kuwafanyia kila mtu mambo haya? (La.) Kwa kweli, baadhi ya watu wenye mioyo isiyo na huruma wangefanya mambo haya, na kuna sababu mbili za hili. Moja ni kwamba, wanapokuwa wakimfanyia kila mtu jambo, wao huwa pia wakijifanyia wenyewe, na wananufaika kutokana na hili. Ikiwa hawawezi kupata manufaa yoyote kutokana na kufanya jambo, tazameni muone kama bado watalifanya—watabadilisha mtazamo wao mara moja na kuacha. Zaidi ya hayo, wanatumia pesa za nani kufanya mambo haya na kutafuta manufaa kwa kila mtu? Ni nyumba ya Mungu ndiyo inayogharamia. Wao ni wajuzi wa kutumia rasilimali za nyumba ya Mungu kwa ukarimu wa kujionyesha. Watakasoaje kufanya mambo haya wakati wao binafsi wanapata manufaa? Wanapokuwa wakitafuta manufaa kwa ajili ya kila mtu, kwa kweli wao huwa wakijifanyia mambo wenyewe. Hawana moyo mwema kiasi cha kutafuta manufaa kwa ajili ya kila mtu mwingine! Ikiwa kweli wangekuwa wakitafuta manufaa kwa ajili ya kila mtu, hawangepaswa kuwa na nia zozote za ubinafsi, na wangepaswa kushughulikia mambo kulingana na kanuni za nyumba ya Mungu. Hata hivyo, wao badala yake daima hujitafutia manufaa wenyewe, na hawafikirii hata kidogo kuhusu kuingia katika uzima kwa watu wateule wa Mungu. Zaidi ya hayo, wanamfanyia kila mtu mwingine mambo ili watu wawaheshimu na kusema, “Mtu huyu hututafutia manufaa na anajitahidi kulinda maslahi yetu. Tukikosa chochote, tunapaswa kumwomba akishughulikie. Akiwepo, hatutatendewa vibaya.” Wanafanya mambo haya ili kila mtu awashukuru. Kwa kutenda kwa njia hii, wanapata umaarufu na faida, kwa hivyo kwa nini wasifanye mambo haya? Ikiwa wangetafuta manufaa kwa ajili ya kila mtu, lakini hakuna aliyejua ni wao waliofanya, na kila mtu akamshukuru Mungu, na hakuna aliyehisi kuwa na shukrani kwao, je, bado wangefanya hivyo? Hakika hawangekuwa na moyo wa kufanya hivyo; sura zao halisi zingefichuliwa. Watu kama hawa wanapofanya chochote, kiini cha asili yao hufichuliwa kikamilifu. Kwa hivyo, wapinga Kristo wanapolisumbua kanisa, kamwe hawatafanya kazi yoyote halisi ili kuwalinda watu wateule wa Mungu.

Hivi punde kwamba baada ya watu wateule wa Mungu kupata upotoshaji, udhibiti, na madhara ya wapinga Kristo, viongozi wa uwongo bado hulifumbia macho jambo hilo. Hawafikirii njia yoyote ya kuwarejesha watu wateule wa Mungu, wala hawatekelezi wajibu na majukumu yao. Wanazingatia tu hisia na maslahi yao wenyewe. Hawatimizi majukumu yao na hawajiwajibishi; badala yake, wanakwepa majukumu yao na kuyaepuka. Na hata wanawahukumu watu wateule wa Mungu baada ya kupotoshwa na kudhibitiwa na wapinga Kristo, wakisema kwamba hawaamini kwa dhati katika Mungu, ili kukwepa jukumu lao wenyewe, bila kuhisi kuchomwa katika dhamiri. Viongozi hawa wa uwongo ndio wanaochukiza zaidi. Aina tofauti za udhihirisho wa viongozi wa uwongo ambazo tumejadili zote ni za kuchukiza sana, lakini mtu wa aina hii ya mwisho hana ubinadamu kabisa. Mtu wa aina hii ni mnyama mkatili, mnyama mwenye mavazi ya kibinadamu; hawezi kuchukuliwa kama sehemu ya wanadamu, bali anapaswa kuainishwa miongoni mwa wanyama. Kwa nini hatimizi majukumu yake? Kwa sababu hana ubinadamu, hana dhamiri wala busara. Majukumu, wajibu, upendo, subira, huruma, kuwalinda ndugu na dada—hakuna hata kimoja cha vitu hivi kilicho moyoni mwake; hana sifa hizi. Kutokuwa na sifa hizi katika ubinadamu wake ni sawa na kutokuwa na ubinadamu. Huu ndio udhihirisho wa aina ya nne ya kiongozi wa uwongo.

Hizi ni takriban aina nne za udhihirisho wa viongozi wa uwongo ambazo zinahitaji kufichuliwa ndani ya jukumu la kumi na tatu la viongozi na wafanyakazi. Bila shaka, kuna baadhi ya udhihirisho mwingine unaofanana na huu, lakini aina hizi nne kimsingi tayari zinaweza kuwakilisha udhihirisho mbalimbali wa viongozi wa uwongo katika kutekeleza kazi hii, pamoja na kiini cha ubinadamu wao. Haijalishi tunagawanya udhihirisho wao katika vikundi vingapi, dhihirisho mbili zinazojulikana za viongozi wa uwongo zinaweza, kwa vyovyote vile, bado kupatikana ndani ya vikundi hivi vinne: Mojawapo ni kutofanya kazi halisi, na nyingine ni kutoweza kufanya kazi halisi. Hizi ndizo dhihirisho mbili zinazojulikana zaidi wa viongozi wa uwongo. Bila kujali ubinadamu na ubora wa tabia wa viongozi wa uwongo ukoje, na bila kujali jinsi wanavyouchukulia ukweli, kwa vyovyote vile, dhihirisho hizi mbili zimo ndani ya vikundi hivi vinne. Huu ndio mwisho wa maudhui kuhusu kuwafichua viongozi wa uwongo katika ushirika wetu wa leo kuhusu jukumu la kumi na tatu la viongozi na wafanyakazi.

Nyongeza: Kujibu Maswali

Je, mna maswali yoyote? (Mungu, nataka kuuliza swali. Mwanzoni mwa mkutano, Mungu alituuliza kuna tofauti gani kati ya watu wenye tabia ya wapinga Kristo na wapinga Kristo halisi, na sifa za kawaida za kiini cha wapinga Kristo ni zipi. Wakati huo, tulihisi akili zetu zikiwa tupu, na baada ya kutafakari kwa muda, tuliweza tu kufikiria maneno na mafundisho rahisi sana. Mungu amekuwa akishiriki ukweli kuhusu kuwafichua wapinga Kristo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, lakini tunaweza tu kuelewa na kutenda sehemu yake ndogo sana. Sababu moja ya hili ni kwamba hatujaweka juhudi katika ukweli huu, na nyingine ni kwamba tumekutana na wapinga Kristo wachache kiasi na hatujafikia kuelewa ukweli huu kwa kuuhusisha na hali halisi. Kwa hivyo, hata sasa hatuna kuingia kokote katika ukweli huu, hatuna utambuzi mwingi wa wapinga Kristo, na kuna udhihirisho mwingi wa tabia ya wapinga Kristo ndani yetu ambao hatujautambua bado. Nataka kuuliza jinsi ya kutatua tatizo hili.) Kwa kipengele chochote cha ukweli, ni lazima uwe na uzoefu halisi na maarifa ya upitiaji, ili maneno ya ukweli yaandikwe moyoni mwako. Mchakato wa kupata ukweli daima huwa namna hii. Mambo unayoweza kukumbuka ni yale uliyoyapata kupitia uzoefu wako; hizo ndizo athari za kina zaidi. Kwa hivyo, tulipokuwa tukishiriki juu ya mada ya wapinga Kristo leo, Niliwaongoza mpitie maudhui haya kwanza. Mliweza kukumbuka baadhi yake. Kati ya mambo mliyoweza kukumbuka, baadhi yake ni ya kinadharia kwenu, lakini kwa kawaida kuna baadhi ya udhihirisho wa wapinga Kristo ambao mnaweza kulinganisha zaidi au kidogo na maisha halisi—kila mtu lazima apitie hilo kwa njia hii. Hali ya kawaida kwa watu ni kwamba haijalishi wanaonekana kuelewa vizuri kiasi gani wanaposikiliza mahubiri, wanaelewa tu kinadharia na kwa upande wa mafundisho, na hawana maarifa ya ukweli. Ni wakati upi ndio mtu anaweza kuuelewa ukweli? Ni pale tu anapokuwa amepitia mambo haya ndipo anaweza kuwa na maarifa ya vitendo. Bila kupitia hali halisi, hakuna anayeweza kupata maarifa. Na kwa hivyo, tulipokuwa tukishiriki juu ya mada ya wapinga Kristo leo, ilikuwa muhimu kufanya mapitio ya haraka na kuwapa kumbusho rahisi. Baada ya hili, bila kujali kama tulishiriki kuhusu majukumu ya viongozi na wafanyakazi au udhihirisho mbalimbali wa viongozi wa uwongo, angalau haingekuwa tupu kwenu, basi. Hata hivyo, bado mnahitaji kujionea wenyewe udhihirisho mbalimbali wa wapinga Kristo. Watu wengine husema, “Ikiwa Mungu hatapanga watu, matukio, na vitu halisi, tunaweza kupata wapi fursa ya kuona? Hatuwezi kuwatafuta wapinga Kristo sisi wenyewe, sivyo?” Hamhitaji kuwatafuta. Suluhisho rahisi zaidi ni kwamba mnapokutana na wapinga Kristo, jaribuni kadiri ya uwezo wenu kuwalinganisha na maneno ya Mungu. Linganisheni ufunuo wao wa nje, kauli, matendo, na tabia, pamoja na mawazo na mitazamo yao, na hata njia yao ya kujiendesha na kushughulika na ulimwengu, mtindo wao wa maisha, na kadhalika—yaani, walinganisheni na dhihirisho kumi na tano za wapinga Kristo ambazo zimejadiliwa. Walinganisheni wengi wao kadiri mwezavyo. Hivi ndivyo ufahamu wa watu ulivyo: Hawawezi kukumbuka mengi kutoka kwa kumbukumbu kwa sababu kumbukumbu ya mwanadamu ni finyu. Watu wanaweza kuzungumza kwa ufasaha juu ya mambo ambayo wameyapata kwa kweli kupitia uzoefu wa moja kwa moja. Haijalishi wanasema mengi kiasi gani, haitegemei kumbukumbu bali uzoefu na kile ambacho wamepitia. Mambo haya waliyojifunza yako karibu zaidi na ukweli na kile ambacho ni kweli kihalisi—haya ni mambo ambayo watu wamevuna kupitia uzoefu. Kando na hayo, mambo yanayopatana na mawazo na dhana za kibinadamu na mambo ambayo ni ya msingi wa maarifa hayapatani na ukweli, haijalishi yamechukua nafasi kubwa akilini mwako kwa miaka mingapi baada ya kuingia mara ya kwanza. Unapouelewa ukweli kwa hakika, mambo haya yataondolewa na kutupiliwa mbali. Hata hivyo, mambo yale yaliyo karibu na ukweli na yanayopatana na ukweli, ambayo umeyavuna kupitia uzoefu, ndiyo yenye thamani. Bila kujali kama mmeelewa kikamilifu maswali Niliyowauliza leo, hakika kuna sehemu ya mada ya kuwatambua wapinga Kristo ambayo mnaweza kuielewa, kwa sababu nyote mmepitia upotoshaji na usumbufu fulani kutoka kwa wapinga Kristo. Hili limewapa utambuzi kiasi, na mnapokutana na wapinga Kristo wakitenda maovu na kusumbua kazi ya kanisa, ukweli huu unaweza kuanza kufanya kazi ndani yenu. Maneno haya huanza kufanya kazi tu mnapokutana na mazingira halisi. Ikiwa hujapitia upotoshaji wa wapinga Kristo na unawazia tu matendo yao akilini mwako, hili halina maana. Haijalishi mawazo yako ni mazuri kiasi gani, haitamaanisha kwamba utaweza kuwatambua. Ni wakati tu wa kukabili mazingira halisi ndipo watu huwa na mwitikio kiasili, wakitumia mawazo na mitazamo yao wenyewe, baadhi ya nadharia walizojifunza, na baadhi ya mafundisho, mbinu, na njia walizojifunza, ili kukabiliana na kushughulikia mambo haya, na hatimaye kufanya chaguzi mbalimbali. Lakini kabla ya watu kukumbana na hali hizi, tayari ni vizuri sana ikiwa wana ufahamu ulio wazi na taswira iliyo wazi ya nadharia mbalimbali. Watu wengine husema, “Kuna umuhimu gani Wewe kusema mengi kabla hatujakutana na wapinga Kristo?” Kuna umuhimu. Je, maneno yanayowafichua wapinga Kristo hayajachapishwa katika kitabu? Je, maneno hayo ni kitu ambacho mnaweza kupitia kikamilifu na kukiona waziwazi kwa siku moja au mbili? La. Kusudi la kuyachapisha katika kitabu hicho ni kuwaokoa ninyi na kuwaruhusu myasome maneno haya mara kwa mara, na kuuelewa ukweli huu, na pia kusoma maneno ya Mungu na kupokea ugavi wa uzima mnapokutana na hali mbalimbali katika siku zijazo—iwe ni tukio la mpinga Kristo, matatizo katika kubadilisha tabia yako mwenyewe, au kitu kingine chochote. Maneno ya Mungu katika kitabu hiki ndiyo chanzo cha wewe kupitia na kushughulikia mambo haya na kuingia katika vipengele hivi vya ukweli. Kiasi unachoweza kuelewa unaposikiliza mahubiri hakiwakilishi kiasi cha uhalisi ulio nao. Ikiwa huwezi kufumbua au kukumbuka kitu kwa wakati mmoja, haimaanishi hutakipitia kamwe au hutafikia kukielewa kamwe katika siku zijazo. Kwa muhtasari, ni lazima muelewe kwamba ni mambo ambayo watu hupata kupitia uzoefu tu na kuyafahamu kulingana na maneno ya Mungu ndiyo yanayohusiana na ukweli. Mambo ambayo watu hukumbuka na mambo wanayoyaelewa akilini mwao mara nyingi hayahusiani na ukweli; ni ya kimafundisho tu. Ni mambo gani ndiyo yaliyo muhimu zaidi linapokuja suala la ukweli? Mambo muhimu zaidi ni uzoefu na kuingia. Kwa kipengele chochote cha ukweli, watu wanapokipitia kihalisi, mavuno yao ya mwisho ni matunda ya ukweli na njia ya wao kuokoka. Kwa hivyo, kutokumbuka si tatizo.

Kama Ningeanza kujadili mada kuu moja kwa moja mwanzoni mwa mkutano, je, mngeweza kuitikia kwa wakati kweli? Kwa hivyo, ilinibidi Nitumie mbinu fulani, na kwanza kuwauliza, “Je, mnakumbuka tofauti kati ya watu wenye kiini cha wapinga Kristo na watu wenye tabia ya wapinga Kristo?” Kusudi Langu la kuuliza swali hili kwanza halikuwa kuwaacha mkiwa mmepigwa na butwaa au kuwaanika, bali ili kuwapa kumbusho. Kisha, tulifanya mapitio, na baadhi ya watu wakakumbuka polepole: “Tumeshiriki hapo awali kuhusu jinsi wapinga Kristo wanavyouchukulia ukweli, na jinsi ubinadamu wa wapinga Kristo ulivyo.” Baadhi ya maudhui kuhusu wapinga Kristo tayari yameacha athari ya kina kwenu; maudhui haya yanasubiri kutumiwa na wewe unapopitia mambo kama hayo, ili yawe mwongozo na mwelekeo kwa ajili ya utendaji wako. Lakini kuna maudhui mengi zaidi ambayo hukupata athari yoyote kwayo baada ya kuyasikia kwa mara ya kwanza. Maudhui haya pia yanahitaji kupitiwa. Unapopitia uzoefu huu na kisha kula na kunywa, na kuomba kwa kusoma maneno haya, utapata hata zaidi. Iwe ni maudhui ambayo una athari kwayo au la, baada ya kupitia mambo haya, yote yatachanganyika pamoja. Mafundisho uliyoyakumbuka yatakuwa uelewa wako wa vitendo na mavuno yako baada ya kuyapitia. Kuhusu maudhui ambayo hukupata athari yoyote kwayo, baada ya kuyapitia mara moja, unaweza kupata athari kiasi, lakini yatakuwa tu maarifa ya kihisia. Maarifa haya ya kihisia yanaweza tu kubaki katika kiwango cha mafundisho. Yanasubiri wewe upitie mambo kama hayo tena, na katika hatua hiyo yatakuongoza, kukupa mwelekeo, na kukupa njia ya utendaji. Kupitia maneno ya Mungu na kupitia ukweli ni mchakato wa aina hii. Je, ni aibu kwamba hamkujua jinsi ya kujibu swali Nililouliza? Si aibu. Mkininiuliza Mimi swali bila kutarajia, Mimi pia itanibidi nilitafakari papo hapo, Nikizingatia swali linamaanisha nini na linahusisha vipengele vipi vya ukweli. Ubongo na akili ya mwanadamu hufanya kazi hivi—vinahitaji muda wa kujibu. Hata kama ni kitu unachokifahamu sana, ikiwa hujakutana nacho kwa miaka mingi, bado utahitaji muda wa kuitikia unapokutana nacho tena ghafla. Haijalishi umepitia kitu kwa kina kiasi gani, ukikutana nacho tena baada ya siku nyingi au miaka mingi, bado utahitaji muda wa kujibu—isitoshe, uelewa wenu wa mada ya wapinga Kristo uko tu katika kiwango cha maneno na mafundisho, bado hamwezi çkulilinganisha na wapinga Kristo mnaokutana nao katika maisha halisi, na inaweza kusemwa kwamba kimsingi bado hamwezi kuwatambua wapinga Kristo. Kwa hivyo, ukweli huu unawasubiri ninyi muupitie kivitendo—hapo ndipo mnaweza kuthibitisha uhalisi na usahihi wa maneno ya Mungu. Kwa mfano, hapo awali tulishiriki kwamba wapinga Kristo ni wasiotubu kwa uthabiti. Tuseme kwamba ulikariri hili na unasema, “Mungu alisema kwamba wapinga Kristo ni wasiotubu kwa uthabiti. Watamwasi Mungu na kupingana na Yeye hadi mwisho. Hawakubali ukweli na hawakubali kamwe kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, bila kujali chochote. Wao wako kinyume na ukweli.” Ni kimafundisho tu kwamba unaelewa, unakubali, au una athari ya kauli hii; ni maarifa ya kihisia tu. Ndani kabisa ya moyo wako, unahisi kwamba kauli hii ni sahihi, lakini ni maneno gani mahususi ambayo wapinga Kristo husema, ni tabia zipi potovu wanazofichua, na ni asili gani inayowaongoza, na kadhalika, vinavyohusiana na kupatana na maneno ya Mungu yanayowafichua wapinga Kristo? Ni yapi kati ya hayo yanayoweza kuonyesha kwamba ufichuzi wa Mungu ni wa kweli? Hili linakuhitaji ukutane na mpinga Kristo ana kwa ana, au kusikia kutoka kwa mashahidi kuhusu matendo na maneno ya mpinga Kristo, na mwishowe, unagundua, “Maneno ya Mungu ni ya vitendo sana, ni sahihi kabisa. Mtu huyu ameainishwa kama mpinga Kristo mara kadhaa na pia ametimuliwa mara kadhaa. Ingawa bado hajafukuzwa au kuondolewa, udhihirisho na ufichuzi wake unaonyesha kwamba hakubali ukweli kabisa, hatubu kwa uthabiti, na sio tu kwamba ana tabia ya wapinga Kristo bali pia ana kiini cha asili cha wapinga Kristo—yeye ni mpinga Kristo hasa.” Na siku moja, mtu huyu anapofukuzwa, unathibitisha moyoni mwako: “Maneno ya Mungu ni sahihi sana! Watu wenye tabia ya wapinga Kristo wanaweza kubadilika, lakini wale wenye kiini cha wapinga Kristo hawatabadilika.” Maneno haya yanakita mizizi moyoni mwako. Siyo tu kumbukumbu au athari kiasi, wala si aina tu ya maarifa ya kihisia. Badala yake, unaelewa na kuyakubali maneno ya Mungu kwa undani: “Mpinga Kristo hatabadilika; atampinga Mungu hadi mwisho. Si ajabu Mungu hawaokoi; si ajabu Mungu hafanyi kazi kwa watu kama hao. Si ajabu kwamba kamwe hawana nuru au mwangaza wanapotekeleza wajibu wao na hawaonyeshi ukuaji wowote—wameazimia kufuata njia yao wenyewe. Huyu kweli ni mpinga Kristo!” Unapothibitisha usahihi wa maneno ya Mungu, unawaza moyoni mwako: “Maneno ya Mungu ni ukweli kwa hakika. Maneno haya ni sahihi. Amina!” Inamaanisha nini wewe unaposema Amina? Inamaanisha kwamba kupitia uzoefu wako, umefikia kuelewa kwamba maneno ya Mungu ndiyo kigezo cha kupima vitu vyote, kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, na kwamba hata wakati enzi hii na binadamu hawa vitakapopita, maneno ya Mungu hayatapita. Kwa nini hayatapita? Kwa sababu haijalishi ni lini, kiini cha wapinga Kristo hakitabadilika kamwe, na maneno ya Mungu yanayofichua kiini cha wapinga Kristo hayatabadilika kamwe. Ingawa enzi hii itapita, ingawa wanadamu hawa potovu watapita, maneno haya ya Mungu daima yatakuwa ukweli wa mambo—hakuna anayeweza kulikana hili. Hili ndilo neno la Mungu! Unapohisi kwamba maneno ya Mungu yanalingana na kuhusiana na mambo ya hakika unayoyaona na kukutana nayo, na moyo wako unapata uthibitisho, na si tu hisia kwamba maneno ya Mungu lazima yawe sahihi au kwamba maneno ya Mungu hayana makosa, na badala yake umeona na umeyapitia wewe mwenyewe, basi kwa kawaida utasema Amina kwa maneno ya Mungu. Wakati huo, Nikiuliza tena, “Udhihirisho wa watu wenye kiini cha wapinga Kristo ni upi?” uelewa wako wa ndani utaonekana mara moja. Hutakuwa na athari tu, msemo uliokaririwa, au aina ya ufahamu au maarifa ya kihisia. Utasema mara moja, “Wapinga Kristo hawakubali ukweli kabisa na hawatubu kwa uthabiti!” Ingawa huenda kauli hii isiwe na muundo mwingi wa kimantiki, ingawa inasemwa ghafla, na watu hawataielewa mwanzoni, wewe unajua inamaanisha nini kwa sababu umeipitia na umeiona kwa macho yako mwenyewe. Wapinga Kristo ni vitu viovu namna hiyo—hawatatubu kamwe. Maneno haya yanahitaji kupitiwa; yeyote asiyeyapitia hatapata chochote.

Oktoba 2, 2021

Inayofuata: Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (1)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp