Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (4)
Kipengele cha Tano: Kudumisha ufahamu wa sasa na uelewa wa hali na maendeleo ya kila kipengele cha kazi, na kuweza kusuluhisha matatizo mara moja, kurekebisha mikengeuko, na kurekebisha kasoro katika kazi ili iendelee sambamba
Ushirika wa leo unahusu jukumu la tano la viongozi na wafanyakazi: “Kudumisha ufahamu wa sasa na uelewa wa hali na maendeleo ya kila kipengele cha kazi, na kuweza kusuluhisha matatizo mara moja, kurekebisha mikengeuko, na kurekebisha kasoro katika kazi ili iendelee sambamba.” Tutazingatia jukumu hili ili kuchanganua dhihirisho mbalimbali za viongozi wa uongo, ili tuone kama viongozi wa uongo wanatimiza majukumu yao katika kazi hii, na iwapo wanashikilia imara wajibu wao na kutekeleza kazi vizuri.
Viongozi wa Uongo Hujiingiza Katika Starehe na Hawajishughulishi Sana na Mashinani ili Kuielewa Kazi.
Jukumu la tano la viongozi na wafanyakazi linataja kwanza “Kudumisha ufahamu wa sasa na uelewa wa hali na maendeleo ya kila kipengele cha kazi.” “ Hali na maendeleo ya kila kipengele cha kazi” inarejelea nini? Inarejelea jinsi hali ya sasa ya kipengele fulani cha kazi ilivyo. Viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuelewa nini hapa? Kwa mfano: Ni kazi gani mahususi ambazo wafanyakazi wanafanya, ni shughuli gani wanazoshughulika nazo, kama shughuli hizi ni muhimu, kama ni kazi muhimu na za maana, jinsi wafanyakazi hawa wanavyofanya kazi kwa ufanisi, kama kazi hiyo inaendelea vizuri, kama idadi ya wafanyakazi inalingana na kiwango cha kazi, kama kila mtu amepewa kazi za kutosha, kama kuna visa vyovyote vya wafanyakazi wengi sana kupewa kazi fulani—ambapo kuna wafanyakazi wengi sana kwa kazi ndogo sana, na watu wengi hawana kitu cha kufanya—au visa ambapo kiwango cha kazi ni kikubwa sana lakini wafanyakazi ni wachache sana, na msimamizi anakosa kuelekeza kwa ufanisi, na kusababisha ufanisi mdogo wa kazi na maendeleo ya polepole. Hizi zote ni hali ambazo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuelewa. Zaidi ya hayo, wakati wa kutekeleza kila kipengele cha kazi, iwe kwamba mtu yeyote anasababisha usumbufu au hujuma, iwe kuna mtu yeyote anayezuia maendeleo au kudhoofisha, iwe kuna aina yoyote ya kuingilia au uzembe unaotokea—haya pia ni mambo ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuelewa. Kwa hivyo wanapataje ufahamu wa masuala haya? Baadhi ya viongozi wanaweza kupiga simu mara kwa mara kuuliza, “Je, ninyi mna shughuli nyingi sasa hivi?” Wakisikia upande mwingine ukisema wana shughuli nyingi sana, wanaweza kujibu kwa kusema, “Sawa, mradi tu ninyi mna shughuli nyingi, nimetulia.” Unaonaje kuhusu njia hii ya kufanya kazi? Unaonaje kuhusu swali hili? Je, hili ni swali muhimu la lazima kuuliza? Hii ni tabia ya kazi ya viongozi wa uongo—wanafanya tu mambo kwa njia isiyo ya dhati. Wanaridhika na kufanya kazi kiasi ya juu juu ili kutuliza dhamiri zao kidogo lakini hawazingatii kufanya kazi halisi, sembuse kwenda mashinani, kwa kila timu, kuelewa hali ya sasa ya kazi. Kwa mfano, iwapo mipango ya wafanyakazi inafaa, jinsi kazi inavyofanywa, kama matatizo yoyote yametokea—masuala haya halisi hayachunguzwi na viongozi wa uongo, ambao badala yake hutafuta mahali pasipojulikana pa kula, kunywa, na kujifurahisha bila kuvumilia ukali wa upepo au jua. Wanatuma barua tu au wamwambia mtu aulize kwa niaba yao mara kwa mara, wakifikiri kwamba huku ni kufanya kazi yao. Zaidi ya hayo, huenda ndugu wasiwaone kwa siku kumi au nusu ya mwezi. Ndugu wanapoulizwa, “Kiongozi wenu anashughulikia nini? Je, anafanya kazi halisi? Je, anawapa mwongozo na kutatua matatizo?” wanajibu, “Hata usiseme, hatujamwona kiongozi wetu kwa mwezi mmoja. Tangu mkutano wa mwisho aliotufanyia, hajawahi kuja tena, na sasa tuna matatizo mengi bila mtu wa kutusaidia kuyatatua. Hakuna njia nyingine; msimamizi wa kikundi chetu na ndugu wanapaswa kuja pamoja kuomba na kutafuta kanuni, kujadili na kushirikiana pamoja katika kazi hiyo. Kiongozi hafai hapa; sasa hatuna kiongozi.” Kiongozi huyu anafanya kazi yake vizuri kiasi gani? Aliye juu anamwuliza kiongozi huyu, “Baada ya filamu ya mwisho kukamilika, je, ulipokea maandishi yoyote mpya ya filamu? Unarekodi nini kwa wakati huu? Kazi hiyo inaendeleaje?” Kiongozi anajibu, “Sijui. Baada ya filamu ya mwisho, nilikuwa na mkutano mmoja nao, baada ya hapo wote walikuwa na nguvu, hawakuwa hasi, na hawakuwa na matatizo yoyote. Hatujakutana tangu wakati huo. Kama unataka kujua hali yao ya sasa, ninaweza kupiga simu nikuulizie.” “Kwa nini hukupiga simu ili uelewe hali hiyo mapema?” “Kwa sababu nimekuwa na shughuli nyingi sana, nikihudhuria mikutano kila mahali. Si zamu yao bado. Nitaweza kuelewa hali hiyo tu nitakapokutana nao wakati ujao.” Huu ndio mtazamo wao kuhusu kazi ya kanisa. Kisha Aliye juu anasema, “Hufahamu hali ya sasa au matatizo yaliyopo katika kazi ya utengenezaji wa filamu, hivyo, je, maendeleo ya kazi ya injili yakoje? Ni kazi ya injili ya nchi gani imeenea vyema zaidi, iliyo bora zaidi? Ni watu wa nchi gani walio na ubora mzuri zaidi wa tabia kwa ulinganisho na wanaelewa haraka? Ni nchi gani iliyo na maisha bora ya kanisa?” “Ah, nilikuwa nimelenga tu mikutano, nilisahau kuuliza kuhusu mambo haya.” “Basi, katika timu ya injili, ni watu wangapi wanaoweza kushuhudia? Ni watu wangapi wanakuzwa ili washuhudie? Nani anawajibika na anafuatilia kazi ya kanisa na maisha ya kanisa katika nchi gani? Ni nani anayenyunyizia na kuchunga? Je, waumini wapya wa kanisa kutoka nchi mbalimbali wameanza kuishi maisha ya kanisa? Je, dhana na mawazo yao yametatuliwa kabisa? Ni watu wangapi wamejikita katika njia ya kweli, hawapotezwi tena na watu wa kidini? Baada ya kumwamini Mungu kwa mwaka mmoja au miwili, ni wangapi wanaoweza kufanya wajibu wao? Je, unaelewa na kushika mambo haya? Matatizo yanapotokea katika kazi, ni nani anayeweza kuyatatua? Je, unajua katika timu ya injili, ni kundi gani au watu wapi binafsi wanaowajibika kwa kazi yao na wana matokeo halisi?” “Sijui. Kama unataka kujua, ninaweza kukuuliza. Kama huna haraka, nitauliza nitakapopata muda; bado nina shughuli nyingi!” Je, kiongozi huyu amefanya kazi yoyote halisi? (Hapana.) Anasema “Sijui” kuhusu kila kitu; anauliza tu kuhusu mambo wakati anapoulizwa, kwa hivyo anajishughulisha na nini? Haijalishi anaenda kwenye timu gani kwa ajili ya mikutano au kuangalia kazi, anashindwa kutambua matatizo katika kazi na hajui jinsi ya kuyatatua. Ikiwa huwezi kung’amua hali na tabia za watu mbalimbali kwa wakati mmoja, basi, je, hupaswi angalau kufuatilia, kuelewa, na kufahamu masuala yaliyopo katika kazi, ni kazi ipi inayofanywa kwa sasa, na imefikia hatua gani? Hata hivyo, viongozi wa uongo hawawezi hata kufanya hivi; je, wao si vipofu? Hata wakienda kwenye timu mbalimbali kanisani kufuatilia na kuangalia kazi, hawaelewi hali halisi hata kidogo, hawawezi kutambua matatizo muhimu, na hata wakiona matatizo fulani, hawawezi kuyatatua.
Kulikuwa na timu ya utengenezaji wa filamu iliyokuwa ikijiandaa kupiga picha za filamu yenye changamoto kubwa ya aina ambayo hawakuwa wamewahi kujaribu hapo awali. Kiongozi wao hakujua kama walikuwa wanafaa kushughulikia maandishi haya ya filamu, kama mwelekezi na timu nzima walikuwa na uwezo wa kukamilisha kazi hii—hakujua hali hizi. Alisema tu, “Mmechukua maandishi mapya ya filamu. Nendeni mkapige picha, basi. Nitawaunga mkono na kufuatilia. Fanyeni kila muwezalo, na matatizo yanapotokea, mwombeni Mungu na muyatatue kulingana na maneno ya Mungu.” Kisha akaondoka. Kiongozi huyu hakuweza kuona au kutambua matatizo yoyote yaliyokuwepo; je, kazi inaweza kufanywa vizuri namna hii? Baada ya timu ya utengenezaji wa filamu kupokea maandishi haya ya filamu, mwelekezi na wana-timu mara nyingi wangechambua mtiririko wa hadithi na kujadili mavazi na fremu za picha, lakini hawakujua jinsi ya kupiga picha filamu hiyo; hawakuweza kuanza rasmi utengezaji wa filamu hiyo. Je, hii si hali iliyopo? Je, haya si matatizo yaliyopo? Je, haya si masuala ambayo kiongozi anapaswa kutatua? Kiongozi alishinda kila siku katika mikutano, hakuna matatizo halisi yaliyotatuliwa baada ya siku nyingi za mikutano, na bado upigaji picha haukuweza kuendelea kama kawaida. Je, kiongozi huyo alikuwa na athari yoyote? (Hapana.) Alipiga kelele tu akitaja kauli mbiu ili kuongeza ari: “Hatuwezi kuzembea, hatuwezi kuinyonya nyumba ya Mungu bure!” Hata aliwakaripia watu: “Nyinyi watu hamna dhamiri, mnainyonya nyumba ya Mungu bila hisia yoyote ya utambuzi—hamna aibu?” Baada ya yeye kusema haya, dhamiri ya kila mtu ilihisi kulaumiwa kidogo: “Ndiyo, kazi inaendelea polepole sana, na bado tunapata milo yetu mitatu kwa siku namna hii—je, si huu ni unyonyaji? Hatujafanya kazi yoyote kweli. Basi, ni nani atakayeyatatua matatizo haya yanayotokea katika kazi? Hatuwezi kuyatatua kwa hivyo tunamuuliza kiongozi, lakini kiongozi anatuambia tuombe tu kwa bidii, tusome maneno ya Mungu, na tushirikiane kwa amani, bila kushiriki jinsi matatizo haya yanavyopaswa kutatuliwa.” Kiongozi huyo alifanya mikutano mahali pa kazi kila siku, lakini matatizo haya hayakuweza kutatuliwa. Baada ya muda, imani ya baadhi ya watu ilikuwa baridi, na hali zao zikawa za kukata tamaa kwa sababu hawakuona njia ya kusonga mbele na hawakujua jinsi ya kuendelea na upigaji picha wa filamu. Waliweka matumaini yao yote katika kiongozi, wakitumaini kwamba angeweza kutatua matatizo halisi, lakini ole wao, kiongozi huyu alikuwa kama kipofu, hakujifunza taaluma hiyo wala hakufanya ushirika, majadiliano, wala kutafuta kutoka kwa wale walioielewa. Mara nyingi angeshikilia kitabu cha maneno ya Mungu na kusema, “Ninasoma maneno ya Mungu kwa ajili ya ibada ya kiroho. Ninajiandaa na ukweli. Mtu yeyote asinisumbue, nina shughuli nyingi!” Hatimaye, matatizo zaidi na zaidi yaliongezeka, yakisababisha kazi hiyo kuwa katika hali ya kupooza kiasi, lakini kiongozi huyo wa uongo bado alifikiri alikuwa akifanya kazi nzuri. Kwa nini ilikuwa hivyo? Aliamini kwamba kwa kuwa alikuwa amefanya mikutano, kuuliza kuhusu hali ya kazi, alitambua matatizo, alishiriki maneno ya Mungu, alionyesha hali za watu, na kila mtu alikuwa amejiweka wazi kulinganishwa na hali hizi na kuazimia kufanya wajibu wake vizuri, basi jukumu lake kama kiongozi lilikuwa limetimizwa, na alikuwa amefanya kila kitu ambacho kingetarajiwa kutoka kwake—ikiwa kazi mahususi zinazohusiana na vipengele vya kitaaluma hazingeweza kusimamiwa vizuri, hilo halikumhusu kiongozi. Kiongozi huyu ni wa aina gani? Kazi ya kanisa ilikuwa imeanguka katika hali ya kupooza kiasi, lakini hakuwa na wasiwasi au kufadhaika hata kidogo. Kama Aliye juu Hangeuliza au kuhimiza, angeendelea tu kujivuta, bila kutaja kamwe kilichokuwa kikiendelea chini yake, bila kutatua matatizo yoyote. Je, kiongozi kama huyo alikuwa ametimiza majukumu yake ya uongozi? (Hapana.) Kwa hivyo, alizungumzia nini siku nzima katika mikutano? Alibwabwaja kwa uzembe, akihubiri mafundisho na kusema kauli mbiu tu. Kiongozi hakutatua matatizo halisi katika kazi, hakutatua hali za watu za uzembe na hasi, na hakujua jinsi ya kutatua masuala katika kazi ya watu kulingana na kanuni za ukweli. Matokeo yake, mradi mzima ulisimama na hakuna maendeleo yaliyoonekana kwa muda mrefu. Hata hivyo kiongozi hakuwa na wasiwasi hata kidogo. Je, huu si udhihirisho wa viongozi wa uongo kutofanya kazi halisi? Kiini cha dhihirisho hili la viongozi wa uongo ni nini? Je, huku si kupuuza wajibu kwa kiasi kikubwa? Kupuuza kazi ya mtu, kushindwa kutimiza majukumu yake—hiki ndicho hasa viongozi wa uongo wanachofanya. Unakaa kwenye eneo la kazi ili tu kufanya mambo kwa njia isiyo ya dhati, bila kutatua matatizo halisi. Unakaa kwenye eneo la kazi ili tu kuwadanganya watu; bila kufanya kazi yoyote halisi, hata kama ungekaa hapo wakati wote, haingefanikisha chochote. Matatizo mbalimbali hutokea katika kazi na katika mambo ya kitaaluma, baadhi yake ambayo unaweza kuyatatua lakini huyatatui—huku tayari ni kupuuza wajibu kwa kiasi kikubwa. Zaidi ya hayo, wewe ni kipofu machoni mwako na akilini mwako: Wakati mwingine unapogundua matatizo, huwezi kung’amua kiini chake. Huwezi kuyatatua, lakini unajifanya kuwa na uwezo wa kuyashughulikia, ukistahimili tu huku ukikataa kushiriki au kutafuta ushauri kutoka kwa wale wanaoelewa ukweli, na hamripoti au kutafuta kutoka kwa Aliye juu pia. Kwa nini iko hivyo? Je, unaogopa kupogolewa? Unaogopa kwamba Aliye juu atajua ukweli kukuhusu na kukutimua? Je, huku si kuzingatia hadhi bila kuitetea kazi ya nyumba ya Mungu hata kidogo? Ukiwa na mawazo ya aina hii, unawezaje kufanya wajibu wako vizuri?
Haijalishi kiongozi au mfanyakazi anafanya kazi gani muhimu, na asili ya kazi hii ni gani, kipaumbele chake kikuu ni kuelewa na kufahamu jinsi kazi inavyoendelea. Lazima awe pale yeye mwenyewe kufuatilia mambo na kuuliza maswali, kupata taarifa zake moja kwa moja. Hapaswi kutegemea tu uvumi au kusikiliza ripoti za watu wengine. Badala yake, lazima aangalie kwa macho yake mwenyewe hali ya wafanyakazi na jinsi kazi inavyoendelea, na kuelewa ni matatizo yapi yaliyopo, kama maeneo yoyote yanapingana na mahitaji ya Aliye juu, iwapo kuna ukiukwaji wa kanuni, kama kuna usumbufu wowote au ukatizaji, kama kuna ukosefu wa vifaa muhimu au vifaa vya kufundishia vinavyohusiana na kazi ya kitaalamu—lazima wajue mambo haya kila wakati. Haijalishi wasikiliza ripoti ngapi, au ni kiasi gani wanachopata kutokana na uvumi, hakuna hata moja kati ya haya yanayoshinda kuwepo mtu binafsi; ni jambo sahihi zaidi na la kuaminika kwake kuona mambo kwa macho yake mwenyewe. Mara tu anapofahamu vipengele vyote vya hali hiyo, atakuwa na ufahamu mzuri wa kile kinachoendelea. Hasa lazima awe na ufahamu wa wazi na sahihi kuhusu ni nani mwenye sifa nzuri na anayestahili kukuzwa, kwani hili pekee ndilo linalowaruhusu kuwakuza na kuwatumia watu kwa usahihi, jambo ambalo ni muhimu iwapo viongozi na wafanyakazi watafanya kazi yao vizuri. Viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuwa na njia na kanuni za kukuza na kuwafundisha watu wenye ubora mzuri wa tabia. Zaidi ya hayo, wanapaswa kuwa na ufahamu na uelewa wa matatizo na magumu ya aina mbalimbali yaliyopo katika kazi ya kanisa, na kujua jinsi ya kuyatatua, na pia wanapaswa kuwa na mawazo na mapendekezo yao kuhusu jinsi kazi inavyopaswa kuendelea, au matarajio yake ya baadaye. Kama wanaweza kuzungumza kwa uwazi kuhusu mambo kama hayo wakiwa wamefumba macho, bila shaka au tashwishi yoyote, basi kazi itakuwa rahisi zaidi kutekeleza. Na kwa kufanya kazi kwa njia hii, kiongozi atakuwa akitimiza majukumu yake, sivyo? Lazima awe na ufahamu mzuri wa jinsi ya kutatua masuala yaliyotajwa hapo juu katika kazi, na lazima mara nyingi atafakari mambo haya. Anapokumbana na matatizo, lazima ashiriki na kujadili mambo haya na kila mtu, akitafuta ukweli ili atatue masuala hayo. Kwa kufanya kazi halisi huku akiwa amesimama kidete kwa njia hii, hakutakuwa na matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa. Je, viongozi wa uongo hufanya hivi? (Hapana.) Viongozi wa uongo wanajua tu kujifanya na kuwadanganya watu, wakijifanya kana kwamba wanaelewa mambo ambayo hawaelewi kwa kweli, hawawezi kutatua matatizo yoyote halisi na kujishughulisha na mambo yasiyo na maana. Wanapoulizwa wamekuwa wakishughulikia nini, wanasema, “Mahali petu pa kuishi hapakuwa na mito michache, na timu ya utengenezaji wa filamu ilikosa na kipande cha kitambaa cha kutengeneza mavazi, kwa hivyo nilienda kununua kiasi. Wakati mwingine tuliishiwa na viungo jikoni, na mpishi hangeweza kuondoka, kwa hivyo ilinibidi nitoke niende kununua, na nilinunua mifuko michache ya unga njiani. Mambo haya yote ilinibidi nifanye mwenyewe.” Kwa kweli wamekuwa na shughuli nyingi. Je, hawapuuzi kazi zao wanazostahili kufanya? Hawajali hata kidogo au kubeba mzigo hata kidogo linapokuja suala la kazi inayoangukia katika wigo wa majukumu yao kama viongozi, wakitafuta tu kuboronga. Tatizo la ubora wa tabia yao wenyewe kuwa duni sana na wao kuwa vipofu machoni na akilini ni kubwa sana, lakini pia hawabebi mzigo wowote na hujiingiza katika starehe, mara nyingi wakishinda siku kadhaa katika sehemu ya starehe. Mtu anapopata tatizo na kuwatafuta ili apate suluhisho, hawapatikani, na hakuna anayejua wanachofanya hasa. Wanadhibiti muda wao wenyewe. Juma hili, wanafanya mkutano kwa ajili ya timu moja asubuhi moja, wanapumzika alasiri, na kisha jioni, wanawakusanya watu wanaosimamia mambo ya jumla ili kujadili masuala. Juma linalofuata, wanafanya mkutano kwa ajili ya wale wanaosimamia mambo ya nje, wakiuliza kwa juu juu, “Je, kuna matatizo yoyote? Je, mumesoma neno la Mungu katika kipindi hiki? Je, mumezuiliwa au kusumbuliwa katika mawasiliano yenu na wasioamini?” Na baada ya kuuliza maswali haya machache, wanamalizia hapo. Kufumba na kufumbua, mwezi mmoja unapita. Wamefanya kazi gani? Ingawa walifanya mikutano kwa kila timu kwa zamu, hawakujua chochote kuhusu hali ya kazi ya timu yoyote, wala hawakujifunza au kuuliza kuihusu, sembuse kujiunga na kazi au kuielekeza katika kila timu. Hawakushiriki, hawakufuatilia, au kutoa maelekezo kuhusu kazi hiyo, lakini kulikuwa na mambo machache waliyofanya kwa wakati: kula kwa wakati, kulala kwa wakati, na kufanya mikutano kwa wakati. Maisha yao ni ya kawaida kabisa, wanajitunza vizuri wao wenyewe, lakini utendaji wao wa kazi haujafikia kiwango kinachohitajika.
Baadhi ya viongozi hawatimizi majukumu ya viongozi na wafanyakazi hata kidogo, hawafanyi kazi muhimu ya kanisa lakini badala yake huzingatia tu mambo ya jumla yasiyo na maana. Wao hubobea katika usimamizi wa jikoni, wakiuliza kila mara, “Tunakula nini leo? Je, tuna mayai yoyote? Nyama imebaki kiasi gani? Tukiwa nje, nitaenda kununua kiasi.” Wanaona kazi ya jikoni kuwa muhimu sana, wakizurura jikoni bila sababu, wakifikiria kula samaki zaidi kila mara, nyama zaidi, kufurahia zaidi, kula chakula bila wasiwasi wowote. Wakati watu katika kila timu wana shughuli nyingi wakifanya kazi, wakizingatia kufanya majukumu yao vizuri, viongozi hawa wanazingatia tu kula vizuri, kuishi maisha ya starehe. Tangu wawe viongozi, sio tu kwamba hawajakuwa wakiijali kazi ya kanisa na kuepuka juhudi zozote ngumu, lakini pia wamejitunza ili wanenepe na kuwa wenye mashavu ya waridi. Wanafanya nini kila siku? Wanashughulika na mambo ya jumla, mambo mengine madogo, hawajafanya kazi yoyote halisi vizuri au kutatua matatizo yoyote halisi. Lakini hawahisi majuto mioyoni mwao. Viongozi wote wa uongo hawafanyi kazi muhimu ya kanisa, wala hawasuluhishi matatizo yoyote halisi. Baada ya kuwa viongozi, wanawaza, “Ninahitaji tu kupata watu wachache wa kufanya kazi mahususi, na kisha sihitaji kuifanya mwenyewe.” Wanaamini kwamba mara tu watakapowapanga wasimamizi kwa kila kazi, wao wenyewe hawana chochote cha kufanya. Wanaamini huku ndiko kufanya kazi ya uongozi, na kisha wana haki ya kufurahia faida za hadhi yao. Hawashiriki katika kazi yoyote halisi, hawafuatilii au kutoa mwelekeo, na hawafanyi uchunguzi au utafiti ili kutatua matatizo. Je, wanatimiza majukumu ya kiongozi? Je, kazi ya kanisa inaweza kufanywa vizuri kwa njia hii? Aliye juu Anapowauliza kuhusu jinsi kazi inavyoendelea, wanasema, “Kazi yote ya kanisa inaendelea kwa kawaida. Kila kipengele cha kazi kina msimamizi anayekishughulikia.” Wakiulizwa zaidi kuhusu kama kuna matatizo yoyote katika kazi, wanajibu, “Sijui. Labda hakuna matatizo yoyote!” Huu ndio mtazamo wa viongozi wa uongo kwa kazi yao. Kama kiongozi, unaonyesha kutowajibika kabisa kwa kazi uliyopewa; yote imekabidhiwa kwa wengine, bila ufuatiliaji, maswali, au usaidizi katika kutatua matatizo kutoka upande wako—unakaa tu pale kama msimamizi wa kazi asiye na shughuli. Je, huku si kutowajibika katika jukumu lako? Je, hutendi kama afisa? Je, si huku ni kotofanya kazi yoyote mahususi, kutofuatilia kazi, kutotatua matatizo halisi—je, viongozi wa aina hii si mapambo tu? Je, wao si viongozi wa uongo? Huu ndio mfano halisi wa kiongozi wa uongo. Kazi ya kiongozi wa uongo ni kutapatapa na kutoa maagizo bila kushiriki au kufuatilia kazi, wala kutafuta au kutambua matatizo katika kazi. Hata matatizo yanapogunduliwa, hayatatui. Anatenda tu kama msimamizi asiyefanya kazi yeye mwenyewe, akifikiri kwamba huko ni kufanya kazi. Lakini kuongoza kwa namna hii hakuwapi wasiwasi wowote; wanaishi kwa raha kila siku, na ni wachangamfu wakati wote. Inakuwaje bado wanaweza kutabasamu? Nimegundua ukweli: Watu kama hao hawana haya kabisa. Hawafanyi kazi yoyote halisi kama viongozi, wanapanga watu wachache tu wafanye kazi na wanaona imetosha. Huwaoni kamwe mahali pa kazi; hawana habari yoyote kuhusu maendeleo au matokeo ya kazi ya kanisa, lakini bado wanafikiri wana uwezo na wanafikia kiwango kinachohitajika kama kiongozi. Huu ni mfano halisi wa kiongozi wa uongo, hafanyi kazi halisi hata kidogo. Viongozi wa uongo hawabebi mzigo wa kazi ya kanisa, hawahangaiki au kuwa na wasiwasi bila kujali ni matatizo mangapi yanatokea; wanaridhika na kufanya mambo ya jumla na kisha wanafikiri wamefanya kazi halisi. Haijalishi namna Aliye juu anavyowafichua viongozi wa uongo, hawahisi vibaya ndani, wala hawajioni wakiwa katika kufichuliwa; hawajitafakari au kutubu. Je, si watu kama hao hawana dhamiri na mantiki? Je, mtu aliye na dhamiri na mantiki anaweza kuichukulia kazi ya kanisa namna hii kweli? Hakika hawezi.
Kwa jumla, watu wenye dhamiri na mantiki kidogo, wakisikia ufichuzi wa dhihirisho mbalimbali ya viongozi wa uongo na kujiweka kama vielelezo vya kulinganisha na maelezo haya, wataweza kuona, kwa kiasi kikubwa au kidogo, kwamba kuna kitu kutoka kwao wenyewe katika maelezo haya. Nyuso zao zitashtuka, watakosa utulivu, mioyo yao itakuwa na wasiwasi, wakihisi kuwa na deni kwa Mungu, na wataamua kwa siri: “Hapo awali, nilijishughulisha na starehe za mwili, sikufanya kazi yangu vizuri, sikutimiza majukumu yangu, sikufanya kazi halisi, nilikuwa asiyejua nilipoulizwa, siku zote nilitaka kukwepa, na siku zote nilijifanya, nikihofu kwamba punde tu wengine wangeona kile kilichokuwa kikiendelea kwangu, sifa na hadhi yangu ingepotea, na ningeipoteza nafasi ya kiongozi niliyoshikilia. Ni sasa tu ndipo ninaona kwamba tabia kama hiyo ni ya aibu na haiwezi kuendelea. Lazima niwe mwenye bidii zaidi katika kuchukua hatua, na kuweka juhudi. Nikiendelea kushindwa kufanya vizuri, hilo litakuwa jambo lisilosameheka—dhamiri yangu ingenilaumu!” Viongozi wa uongo kama hawa bado wana ubinadamu na dhamiri fulani; angalau, dhamiri yao ina ufahamu. Baada ya kusikia kufichua Kwangu, wanajiona kwa maneno haya na kuhisi wasiwasi; wanatafakari: “Kwa kweli sijafanya kazi yoyote halisi, au kutatua matatizo yoyote halisi. Sistahili agizo la Mungu au cheo cha kiongozi. Nifanye nini, basi? Lazima nirekebishe mambo; kuanzia sasa, lazima nitie bidii na kutatua matatizo halisi, nishiriki katika kila kazi maalum, niepuke kukwepa, niepuke kujifanya, na kufanya mambo kwa kiwango kamili cha uwezo wangu. Mungu huchunguza mioyo ya watu na mawazo ya ndani kabisa, Mungu anajua kipimo cha kweli cha kila mtu; bila kujali kama ninafanya mambo vizuri au vibaya, kuyafanya kwa moyo wote ndiyo muhimu zaidi. Iwapo siwezi hata kufanya hivi, je, bado naweza kuitwa mwanadamu?” Kuweza kujitafakari kwa njia hii kunaitwa kuwa na dhamiri. Watu wasio na dhamiri, haijalishi unavyowafichua, hawaoni haya au kuhisi mioyo yao ikipiga; wanaendelea tu kufanya chochote wanachotaka. Hata wakijiona katika kile ambacho Mungu amefichua, hawajali kuhusu hilo: “Si kama nilitajwa kwa jina,” wao huwaza. “Kwa nini niogope? Ubora wa tabia yangu ni mzuri, nina kipaji; nyumba ya Mungu haiwezi kuendelea bila mimi! Kuna nini nisipofanya kazi yoyote halisi? Siifanyi mimi mwenyewe, lakini mimi humwambia mtu mwingine aifanye, kwa hivyo inafanywa tu, sivyo? Kwa vyovyote vile, kila kazi ambayo unaniambia nifanye, mimi hukufanyia, haijalishi ni nani ninayempangia aifanye. Ubora wa tabia yangu ni mzuri, kwa hivyo mimi hufanya kazi kwa busara. Katika siku zijazo, nitaendelea kuboronga na kufurahia maisha kama ninavyotaka.” Haijalishi jinsi ninavyochanganua au kufichua viongozi wa uongo kwa kutofanya kazi halisi, watu wanaohusika wanabaki vile vile, wasiojali kabisa: “Waache wengine wafikirie wanachotaka, na wanichukulie wanavyotaka kunichukulia—mimi sitaifanya kabisa!” Je, viongozi hao wa uongo wana dhamiri? (Hapana.) Hii ni mara ya nne ambayo tumeshiriki juu ya kufichua udhihirisho mbalimbali wa viongozi wa uongo, na kila Ninapowafichua watu kama hao, wale wenye dhamiri kidogo hukosa amani kabisa, wakihisi kutokuwa salama kwa kutofanya kazi yao vizuri, na wanaazimia kutubu kwa siri haraka na kubadilika. Wakati huo huo, wale wasio na dhamiri hawana haya kabisa; hawahisi chochote. Bila kujali jinsi Ninavyoshiriki, wao huendelea kuishi maisha yao kama kawaida, wakifurahia maisha wanavyotaka. Unapowauliza, “Baadhi ya watu wanawajibikia kazi ya injili, wengine kazi ya tafsiri, na wengine kazi ya utengenezaji wa filamu—ni kazi gani mahususi unayowajibikia?” wanasema: “Ingawa sijafanya kazi yoyote mahususi, mimi husimamia kila kitu. Ninawaandalia mikutano.” Ukimuuliza, “Unafanya mikutano mingapi kwa mwezi?” atajibu: “Angalau, mkutano mmoja mkubwa kwa mwezi, na mkutano mdogo kila baada ya majuma mawili.” Na ukimuuliza, “Mbali na kufanya mikutano, ni kazi gani mahususi ambayo umefanya?” Atajibu: “Mikutano imenifanya niwe na shughuli nyingi, ni kazi gani mahususi ninayoweza kufanya? Zaidi ya hayo, wigo ninaosimamia ni mpana sana, sina muda wa kazi mahusui.” Viongozi hawa wa uongo wanahisi kwamba wako sahihi kabisa—kwamba wao ni viongozi imara na thabiti! Haijalishi wamefichuliwa na kupogolewa namna gani, hawakasirishwi hata kidogo na hilo. Kama Ningeambiwa nifanye kazi mahususi, kama vile kuwapikia watu watano, lakini nilikuwa Nimetayarisha tu chakula cha kutosha watu wanne pekee, Ningehisi vibaya kwa kutotengeneza chakula cha kutosha, na Ningehisi hatia kwa kutomlisha kila mtu vizuri. Kisha Ningewaza jinsi ya kufidia jambo hilo, kuhakikisha Ninahesabu kwa usahihi wakati ujao ili kila mtu apate chakula cha kutosha. Na ikiwa mtu angesema kwamba chakula kina chumvi nyingi, Ningehisi vibaya pia. Ningeuliza ni chakula gani kilikuwa na chumvi nyingi, kisha Ningewauliza wengine kama viungo vilikuwa sahihi. Ingawa ni vigumu kumfurahisha kila mtu, bado lazima Nijaribu kila namna ili kufanya vizuri kile Ninachotarajiwa kufanya. Huku kunaitwa kutimiza majukumu ya mtu; haya ndiyo mantiki ambayo watu wanapaswa kuwa nayo. Wewe lazima utimize majukumu yako kila wakati; bila kujali ni kazi ipi, lazima ushiriki mwenyewe. Mtu yeyote akitoa maoni tofauti—bila kujali ni nani—na ugundue kwamba wewe hauko sahihi na unahisi vibaya baada ya kuisikia, basi ni lazima ufanye marekebisho na kufanya kile unachofanya kwa dhati katika siku zijazo, ukikifanya vizuri hata kama inamaanisha kuvumilia ugumu fulani. Viongozi wa uongo hawana hisia hii, kwa hivyo hawavumilii ugumu wowote hata kidogo. Baada ya kusikia ukweli huu kuhusu kufichuliwa kwa viongozi wa uongo, hawahisi chochote hata kidogo, bado wanafurahia chakula chao, wanalala fofofo, na kufurahia maisha, wakiwa na hali ile ile ya furaha kila siku, na bila hisia ya kubeba mzigo mzito mabegani mwao, au maumivu ya hatia mioyoni mwao. Hawa ni watu wa aina gani? Watu kama hawa wana tatizo na tabia zao: Hawana dhamiri, hawana mantiki, na wana tabia duni. Licha ya kufichua dhihirisho mbalimbali za viongozi wa uongo kwa muda mrefu—kutoka katika mtazamo chanya, kukimu na kushiriki, na kutoka katika mtazamo hasi, kuzifichua na kuzichanganua—sehemu ya viongozi wa uongo bado hawawezi kutambua masuala yao wenyewe, wala hawajawahi kukusudia kutafakari na kutubu. Kusingekuwa na usimamizi na msukumo wowote kutoka kwa Aliye juu, bado wangeboronga kazi yao kadri wawezavyo, bila kubadilisha mkondo hata kidogo. Haijalishi Ninavyowafichua, bado wanakaa hapo bila kujali na bila kukumbuka. Je, si wao ni wasio na aibu kabisa? Watu wa aina hii hawafai kuwa viongozi au wafanyakazi; ni wenye tabia duni sana hivi kwamba hawana aibu! Kwa watu wa kawaida, hata kumsikia tu mtu akitaja mapungufu yao, kasoro, au chochote kisichofaa au kinyume na kanuni kuhusu kile walichofanya—bila kujali kufichuliwa mahususi—ingekuwa vigumu kwao kuvumilia, na wangehisi kukasirika na kudhalilishwa, na wangefikiria jinsi ya kubadilika na kujirekebisha. Wakati huo huo, viongozi hawa wa uongo huharibu kazi yao kabisa na bado wanaishi na moyo safi bila hatia, bila kuhisi wasiwasi au dukuduku, na kubaki bila kukumbuka kabisa bila kujali jinsi wanavyofichuliwa—hata wao huenda katika sehemu za kujificha na kutafuta starehe, na huwa hawapo wanapotakiwa kuwa. Kwa kweli hawana aibu!
Kiongozi wa kanisa lazima angalau awe na dhamiri na mantiki, na pia aelewe ukweli fulani—ni hapo tu ndipo anapoweza kuhisi mzigo. Je, udhihirisho wa kuhisi mzigo ni upi? Akiwaona watu fulani wakiwa hasi, wengine wakiwa na uelewa potovu, wengine wakipoteza mali za nyumba ya Mungu, wengine wakifanya kazi zao kwa njia isiyo ya dhati, wengine hawafanyi kazi ipasavyo wanapofanya wajibu wao, wengine wakisema maneno ya ajabu kila wakati lakini hawafanyi kazi halisi…, kugundua kuwa matatizo mengi yapo ndani ya kanisa na yanahitaji kutatuliwa, kuona kazi nyingi ikisalia bila kufanywa, hii inawafanya wajihisi mzigo. Tangu anapoanza kuwa kiongozi, inahisi kama kuna moto unaowaka ndani yake kila mara; akigundua tatizo na hawezi kulitatua, anakuwa na wahaka na wasiwasi, hawezi kula au kulala. Wakati wa mikutano, wakati watu wengine wanaripoti matatizo katika kazi zao ambayo kiongozi huyu hawezi kuyang’amua na kuyatatua mara moja, kiongozi hakati tamaa; anahisi kwamba lazima atatue tatizo hili. Baada ya kuomba na kutafuta, na kulifikiria kwa siku mbili, mara tu anapojua jinsi ya kulitatua, yeye hulitatua tatizo haraka. Baada ya kutatua suala hilo, yeye hutazama vipengele vingine vya kazi haraka na kugundua tatizo lingine la watu wengi sana kuhusika katika kazi iliyohitaji kupunguzwa kwa wafanyakazi. Kisha yeye huita mkutano haraka, kupata taswira kamili ya hali hiyo, kupunguza wafanyakazi, na kupanga mipango inayofaa, na hivyo tatizo hutatuliwa. Haijalishi ni kazi gani wanayokagua, viongozi wanaobeba mzigo wataweza kutambua matatizo kila wakati. Kwa matatizo yoyote yanayohusiana na ujuzi wa kitaaluma, au ambayo yanapingana na kanuni, wataweza kuyatambua, kuuliza kuyahusu, na kuyaelewa, na wanapogundua tatizo, wao hulitatua haraka. Viongozi na wafanyakazi wenye akili hutatua matatizo yanayohusiana na kazi ya kanisa, ujuzi wa kitaaluma, na kanuni za ukweli. Hawazingatii mambo madogo katika maisha ya kila siku. Wanaangalia kila kipengele cha kazi ya kueneza injili ambayo Mungu aliagiza. Wanauliza kuhusu na kukagua matatizo yoyote ambayo wanaweza kuyaona au kugundua. Ikiwa hawawezi kutatua tatizo wenyewe wakati huo, basi wao hukutana na viongozi wengine na wafanyakazi, kufanya ushirika nao, kutafuta kanuni za ukweli, na kufikiria kuhusu njia za kulitatua. Wakikumbana na tatizo kubwa ambalo hawawezi kulitatua, basi wao hutafuta upesi kutoka kwa Aliye juu, na kumruhusu Aliye juu Alishughulikie na kulitatua. Viongozi na wafanyakazi kama hawa ni watu wenye kanuni katika matendo yao. Haijalishi kuna matatizo gani, mradi tu wameyaona, hawatayaacha; wanasisitiza kuelewa kikamilifu matatizo haya na kisha kuyatatua moja baada ya lingine. Hata kama hayajatatuliwa kikamilifu, kuna uhakika kwamba matatizo haya hayatatokea tena. Huku ni kufanya wajibu wa mtu kwa moyo wake wote, nguvu zake, na akili yake yote, akitimiza kikamilifu majukumu yake. Hao viongozi na wafanyakazi wa uongo ambao hawafanyi kazi halisi au kuzingatia kutatua matatizo halisi hawawezi kugundua matatizo yaliyo mbele yao na hawajui ni kazi gani inayopaswa kufanywa. Mradi tu wanaona kwamba akina ndugu wanajishughulisha wakifanya wajibu wao, wanaridhika kikamilifu, wakihisi kwamba haya ni matokeo ya kazi yao halisi; wanafikiri kwamba vipengele vyote vya kazi ni vizuri sana na kwamba hakuna mengi ya wao kufanya binafsi au matatizo yoyote ya kutatua, kwa hivyo wao huzingatia kufurahia faida za hadhi yao. Daima wao hutaka kujionyesha na kujisifu miongoni mwa akina ndugu. Kila wanapowaona akina ndugu, wao husema, “Kuwa muumini mzuri. Fanya wajibu wako vizuri. Usifanye mambo kwa moyo usio wa dhati. Ukiwa mtukutu au usababishe matatizo, nitakutimua!” Wanajua tu kuonyesha hadhi yao na kuwakaripia watu. Wakati wa mikutano wao huwa wanauliza ni matatizo gani yaliyopo katika kazi na kuuliza kama wale walio chini yao wana matatizo yoyote, lakini wengine wanapoeleza shida na matatizo yao, hawawezi kuyatatua. Licha ya haya, wao bado wanafurahi, na bado wanaendelea kuishi na moyo safi. Akina ndugu wasipoleta shida au matatizo yoyote, wanahisi kwamba wanafanya kazi yao vizuri sana, wakiwa wanaridhika. Wanafikiri kwamba kuuliza kuhusu kazi ndiyo kazi waliyopewa kufanya, na matatizo yanapotokea na Aliye juu Afuatilie na kuona kwamba ni jukumu la kiongozi huyo, anaduwazwa. Wengine huweka shida na matatizo ya kazi iliyo mbele yao, lakini bado wanalalamika kuhusu kwa nini hawatafuti ukweli ili kuyatatua. Wasipotatua matatizo halisi wao wenyewe, wao hupisha jukumu kwa wasimamizi walio chini yao, wakiwakemea vikali wale wanaofanya kazi maalum. Karipio hili huwasaidia kupunguza hasira zao, na hata wanaamini kwa dhamiri safi kwamba wanafanya kazi halisi. Hawajawahi kuhisi wasiwasi au wahaka kuhusu kutoweza kugundua au kutatua matatizo, wala kutoweza kula au kulala vizuri kwa sababu ya jambo hili—hawajawahi kupitia shida ya aina hii.
Kila Ninapotembelea kanisa la shambani, Mimi hutatua matatizo fulani. Kila Ninapoenda, si kwa sababu nilipata tatizo fulani maalum la kushughulikia; ni kuwa na muda wa ziada tu wa kuzunguka na kuona jinsi kazi ya timu mbalimbali kanisani inavyoendelea, na jinsi hali za watu katika kila timu zilivyo. Mimi huwakusanya wasimamizi kwa ajili ya mazungumzo, Ninawauliza ni kazi gani ambayo wamekuwa wakifanya katika kipindi hiki, na ni matatizo gani yaliyopo, Mimi huwaruhusu waibue masuala fulani, kisha Ninashiriki nao kuhusu jinsi ya kuyatatua. Ninapofanya ushirika nao, Ninaweza pia kugundua matatizo mapya. Tatizo la aina moja ni yale yanayohusiana na jinsi viongozi na wafanyakazi wanavyofanya kazi zao; lingine ni matatizo katika kazi ndani ya mawanda wa majukumu yao. Zaidi ya hayo, pia Ninawasaidia na kuwaongoza juu ya jinsi ya kufanya kazi maalum, jinsi ya kutekeleza kazi, ni kazi gani wanayopasa kufanya, na kisha kufuatilia wakati ujao, Nikiwauliza jinsi kazi Niliyowapa wakati uliopita inavyoendelea. Usimamizi, uhimizaji, na ufuatiliaji kama huo ni muhimu. Ingawa hili halifanyiki kwa shangwe, nderemo na kupiga kelele, kutumia vipaza sauti kutoa matangazo yoyote, kazi na majukumu haya mahususi huwasilishwa na kutekelezwa kupitia baadhi ya viongozi na wafanyakazi wanaoweza kufanya kazi halisi. Hivyo, kazi ya kila timu inakuwa na utaratibu na kuendelea, ufanisi wa kazi huboreshwa, na matokeo huwa bora zaidi. Mwishowe, kila mtu katika kila timu anaweza kushikilia wajibu wake mwenyewe, akijua kile anachopaswa kufanya na jinsi ya kukifanya. Angalau, kila mtu anatekeleza wajibu wake anaostahili kutekeleza, wote wana kazi zao, na kile wanachofanya kinafanywa kulingana na mahitaji ya nyumba ya Mungu na pia kinaweza kufanywa kulingana na kanuni. Je, huku si kupata matokeo fulani? Je, viongozi wa uongo wanajua jinsi ya kufanya kazi kwa njia hii? Viongozi wa uongo wangetafakari: “Kwa hivyo, hivi ndivyo Aliye juu Anavyofanya kazi: kuwaita watu wengine pamoja kupiga gumzo, kila mtu akiandika maelezo katika kitabu kidogo, na baada ya maelezo kuandikwa, kazi ya Aliye juu imekamilika. Ikiwa hivi ndivyo kazi inavyofanywa na Aliye juu, basi tutaifanya vivyo hivyo.” Hivyo, viongozi wa uongo huiga kwa njia hii. Wanaiga mwonekano, lakini mwishowe, hawafanyi kazi yoyote halisi, hawatekelezi kazi yoyote waliyoambiwa kufanya, wakipumzika tu bila kuzungumza chochote. Wakati mwingine, Mimi pia huenda kwenye mashamba ya mboga na nyumba za kuhifadhia mimea ili kuona jinsi miche inavyokua, au kujua ni mizunguko mingapi ya mimea inayoweza kupandwa kwenye nyumba za kuhifadhia mimea wakati wa msimu wa baridi, na ni mara ngapi inapaswa kunyunyiziwa. Kazi hizi, ziwe kubwa au ndogo, zote zinahusisha masuala ya kiufundi yanayohusiana na kilimo cha mboga, na mradi tu mtu anazifanya kwa bidii, anaweza kuzitimiza. Viongozi wa uongo huonyesha wapi uongo wao hasa? Kinachojulikana zaidi ni kutofanya kazi halisi; wanafanya tu kazi fulani zinazowafanya waonekane wazuri na kisha wanaona zimeshafanyika, na kisha wanaanza kufurahia faida za hadhi yao. Haijalishi wanafanya kazi ya aina hii kiasi gani, je, inamaanisha kwamba wanafanya kazi halisi? Viongozi wengi wa uongo wanaelewa ukweli kwa njia isiyo safi, wakielewa tu maneno na mafundisho fulani, ambayo inafanya iwe vigumu sana kufanya kazi halisi vizuri. Sehemu fulani ya viongozi wa uongo hawawezi hata kutatua masuala yanayohusiana na mambo ya jumla; ni wazi kwamba wana ubora duni wa tabia na hawana uelewa wa kiroho. Hakuna maana kabisa katika kuwastawisha. Baadhi ya viongozi wa uongo wana ubora mzuri kiasi wa tabia, lakini hawafanyi kazi halisi, na wao hujishughulisha na starehe za kimwili. Watu wanaojishughulisha na starehe za kimwili si tofauti sana na nguruwe. Nguruwe hushinda siku nzima wakilala na kula. Hawafanyi chochote. Hata hivyo, baada ya mwaka mmoja wa kazi ngumu ya kuwalisha, wakati familia nzima inakula nyama ya nguruwe mwishoni mwa mwaka, wanaweza kusemwa kuwa walikuwa wa huduma. Ikiwa kiongozi wa uongo anafugwa kama nguruwe, akila na kunywa bure mara tatu kila siku, ananenepa na kuwa na nguvu, lakini hafanyi kazi yoyote halisi na ni mnyang’anyi, je, kumtunza kumekuwa bure? Je, kumekuwa na manufaa yoyote? Wanaweza tu kutumika kama foili na wanapaswa kuondolewa. Kwa kweli, ni bora kufuga nguruwe kuliko kiongozi wa uongo. Viongozi wa uongo wanaweza kuwa na cheo cha “kiongozi,” wanaweza kuchukua nafasi hii, kula vizuri mara tatu kwa siku, kufurahia neema nyingi za Mungu, kukua wanene na wenye rangi nzuri kutokana na kula kote mwishoni mwa mwaka—lakini, je, vipi kuhusu kazi? Angalia yote yaliyotimizwa katika kazi yako mwaka huu: Je, umepata matokeo katika eneo lolote la kazi mwaka huu? Ni kazi gani halisi uliyofanya? Nyumba ya Mungu haiulizi kwamba ufanye kila kazi kikamilifu, lakini lazima ufanye kazi muhimu vizuri—kazi ya injili, kwa mfano, au kazi ya utengenezaji wa filamu, kazi ya maandishi, na kadhalika. Hizi zote lazima zizae matunda. Katika hali ya kawaida, kazi nyingi zinapaswa kutoa matokeo na mafanikio baada ya miezi mitatu hadi mitano; ikiwa hakuna mafanikio baada ya mwaka, basi hili ni tatizo kubwa. Ndani ya mawanda ya jukumu lako, ni kazi gani ambayo imezaa matunda zaidi? Ni ipi ambayo wewe umelipia gharama kubwa zaidi na kuteseka zaidi juu yake kwa mwaka mzima? Wasilisha mafanikio haya, na utafakari kama umepata mafanikio yoyote ya thamani kutoka katika mwaka mzima wa kufurahia neema ya Mungu; unapaswa kuwa na ufahamu wazi wa hili moyoni mwako. Ulikuwa unafanya nini ulipokuwa ukila chakula cha nyumba ya Mungu na kufurahia neema ya Mungu kwa muda huu wote? Je, umefanikisha chochote? Ikiwa hujafanikisha chochote, basi unaboronga tu; wewe hakika ni kiongozi wa uongo. Je, viongozi kama hao wanapaswa kutimuliwa na kuondolewa? (Ndiyo.) Je, unaweza kuwatambua viongozi wa uongo kama hao unapokutana nao? Je, unaweza kuona kwamba wao ni viongozi wa uongo, wakiboronga tu ili kupata tiketi ya mlo wa bure? Wanakula hadi midomo yao iwe na mafuta lakini hawaonekani kuwa na wasiwasi au wahaka kuhusu kazi, hawashiriki au kuuliza kuhusu kazi yoyote maalum. Hata wakiuliza, ni kwa sababu fulani; wanafanya hivyo tu wakati ambapo Aliye juu Anawashinikiza kuhusu matokeo, la sivyo hawangejisumbua. Daima wanajishughulisha na starehe, mara nyingi wakitazama filamu au vipindi vya runinga. Wanagawa kazi na wakati kila mtu mwingine anajishughulisha akifanya wajibu wake, wanapumzika na kujifurahisha wenyewe. Kukiwa na tatizo na ujaribu kuwatafuta ili walishughulikie, hawaonekani, lakini hawachelewi kula. Na baada ya kula, kila mtu anaporudi kazini, yeye huenda kupumzika zaidi. Ukimwuliza, “Kwa nini usitoke nje uangalie kazi? Kila mtu anasubiri mwongozo wako, anasubiri mipangilio yako!” Anasema: “Kwa nini mnisubiri mimi? Nyinyi nyote mnaweza kufanya hivyo, nyote mnajua jinsi ya kufanya kazi hiyo—si ni sawa tu na wakati ambapo sipo? Siwezi kupumzika kwa muda?” “Je, huko ni kupumzika? Wewe unatazama tu filamu!” “Ninajifunza ujuzi wa kitaaluma, ninajifunza jinsi filamu zinavyopigwa picha.” Hata anabuni visingizio. Anatazama filamu moja baada ya nyingine, na kila mtu anapopumzika usiku, yeye pia anapumzika. Kila siku, anaboronga hivi, lakini hili litaendelea hadi lini? Kila mtu anamwona kama mwenye kusumbua, anamfanya kila mtu ahisi vibaya, na hatimaye, hakuna anayemjali. Hebu Niambie, kiongozi kama huyu asipokuwa usukani, je, kazi bado inaweza kuendelea? Bila yeye, je, dunia itaacha kuzunguka? (Inaendelea kuzunguka.) Basi, anapaswa kufichuliwa ili kila mtu aweze kuona kwamba hashughulikii kazi zinazofaa na kwamba hakuna anayepaswa kuzuiwa na yeye. Viongozi wa uongo kama hao ambao hawashughulikii kazi zinazofaa lazima wafichuliwe na kuchanganuliwa ili kila mtu awatambue, kisha watimuliwe wasimame kando! Je, mnaweza kuwatambua viongozi wa uongo kama hao mnapokutana nao? Bila viongozi wa uongo, je, nyote mtahisi kama mabaharia wasiokuwa na nahodha? Je, mtakamilisha kazi na kutimiza kazi kwa kujitegemea? Kama hamtaweza kufanya hivyo, basi mko hatarini. Kukabiliana na viongozi wa uongo wa aina hii, ambao hawafanyi kazi yao ipasavyo, hawaongozi kwa mfano, na hushinda wakikaa kimya wakipiga gumzo mtandaoni—je, mtakuwa na utambuzi katika hali ya aina hii? Je, mtashawishiwa nao pia kushiriki katika mazungumzo yasiyo na maana na kuchelewesha wajibu wenu? Je, bado mnaweza kuwafuata viongozi wa uongo kama hao? (Hapana.)
Baadhi ya viongozi wa uongo ni walafi na wavivu, wakipendelea starehe kuliko kazi ngumu. Hawataki kufanya kazi wala kuwa na wasiwasi, wanakwepa juhudi na uwajibikaji, wanataka tu kujifurahisha. Wanapenda kula na kucheza, na ni wavivu hasa. Kulikuwa na kiongozi mmoja wa uongo ambaye angeamka asubuhi tu baada ya kila mtu kumaliza kula, na usiku, bado angekuwa wakitazama tamthilia za TV huku kila mtu mwingine akipumzika. Ndugu anayehusika na kupikia hakuweza kuvumilia tena na akamkosoa. Je, mnafikiri kwamba angemsikiliza mpishi? (Hapana.) Tuseme kiongozi au mfanyakazi angemkaripia, akisema, “Wewe unapasa kuwa na bidii zaidi; kazi inayohitaji kufanywa lazima ifanywe. Kama kiongozi, lazima utimize majukumu yenu bila kujali kazi unayofanya ni ipi; lazima uhakikishe kwamba hakuna matatizo katika kazi hiyo. Sasa kwa kuwa tatizo limepatikana, na wewe haupo kulitatua, hili linaathiri kazi. Ukifanya kazi hivi kila mara, je, huku si kuchelewesha kazi ya kanisa? Je, naweza kubeba jukumu hili?” Je, angesikiliza hili? Hakuna ukakika. Kwa viongozi hao wa uongo, kundi linalofanya maamuzi linapaswa kuwafukuza kazi mara moja na kuwapangia kazi nyingine, likiwaacha wafanye chochote wanachoweza kufanya. Ikiwa ni wazembe, wanaotaka kukaa tu popote wanapoenda, hawawezi kufanya chochote, basi wawafukuze bila kuwaruhusu kufanya wajibu wowote. Hawastahili kufanya wajibu; si wanadamu, hawana dhamiri na akili ya ubinadamu wa kawaida, hawana haya. Kwa viongozi hao wa uongo, ambao ni wazembe, punde wanapong’amuliwa, wanapaswa kutimuliwa kazi moja kwa moja; hakuna haja ya kujaribu kuwahimiza, na hawapaswi kupewa fursa zozote za kupitia uchunguzi, wala si lazima kushiriki ukweli na wao. Je, hawajasikia ukweli wa kutosha? Kama wangepogolewa, je, wangeweza kubadilika? Hawangeweza. Mtu akiwa na ubora duni wa tabia, wakati mwingine ana maoni ya kipuuzi, au anashindwa kuona taswira kamili kwa sababu ya ujinga, lakini ni mwenye bidii, hubeba mzigo, na si mvivu, basi mtu kama huyo, licha ya kupotoka katika kufanya wajibu wake, anaweza kutubu anapokabiliwa na kupogolewa. Angalau, anajua majukumu ya kiongozi na anajua anachopaswa kufanya, ana dhamiri na hisia ya uwajibikaji, na ana moyo. Hata hivyo, wale ambao ni wavivu, wanapendelea faraja kuliko kazi ngumu, na hawajabeba mzigo, hawawezi kubadilika. Hakuna mzigo mioyoni mwao; haijalishi ni nani anayewapogoa, haina maana. Baadhi ya watu husema, “Basi, ikiwa hukumu, kuadibu, majaribu, na usafishaji wa Mungu ungewajia, je, vingebadilisha suala lao la kutobeba mzigo?” Hili haliwezi kubadilishwa; linaamuliwa na asili ya mtu, kama vile ambavyo mbwa hawezi kubadilisha tabia yake ya kula uchafu. Kila unapomwona mtu ambaye ni mvivu na asiyebeba mzigo na pia anahudumu kama kiongozi, unaweza kuwa na uhakika kwamba yeye ni kiongozi wa uongo. Wengine wanaweza kusema, “Unawezaje kumwita kiongozi wa uongo? Ana ubora mzuri wa tabia, ni mwerevu, anaweza kuona mambo, na anaweza kubuni mipango. Katika ulimwengu, alisimamia biashara, alihudumu kama Mkurugenzi Mkuu; ana ujuzi, uzoefu, na ana hekima ya kidunia!” Je, sifa hizi zinaweza kutatua tatizo lake la kuwa mvivu na kukosa kubeba mzigo? (Hapana.)
Ni aina gani ya udhihirisho na sifa ambazo wale ambao ni wavivu kupita kiasi huonyesha? Kwanza, katika chochote wanachofanya, wao huwakifanyi kwa dhati, wao huzunguka huku na kule, huenda kwa mwendo wa starehe, na hupumzika na kuahirisha inapowezekana. Pili, hawazingatii kazi ya kanisa hata kidogo. Kwao, yeyote anayependa kuwa na wasiwasi kuhusu mambo kama hayo anaweza kufanya hivyo. Hawatajali. Wanapohangaika kuhusu jambo fulani, ni kwa ajili ya umaarufu, faida, na hadhi yao—kilicho muhimu kwao ni kwamba wanaweza kufurahia faida za hadhi. Tatu, wanaepuka ugumu katika kazi yao; hawawezi kukubali kazi yao kuwa ya kuchosha hata kidogo, kuudhiwa sana hili likifanyika, na hawawezi kuvumilia ugumu au kulipa gharama. Nne, hawawezi kuvumilia katika kazi yoyote wanayofanya, kila mara wakikata tamaa katikati na hawawezi kufanya mambo hadi yakamilike. Wakiwa katika hali nzuri kwa muda, wanaweza kufanya kazi fulani kwa ajili ya kujifurahisha, lakini ikiwa kitu kinahitaji kujitolea kwa muda mrefu, na kinawafanya wawe na shughuli nyingi, kinahitaji kufikira sana, na kuchosha miili yao, baada ya muda wataanza kunung’unika. Kwa mfano, baadhi ya viongozi wanasimamia kazi ya kanisa, na wao huiona ikiwa mpya na ya kusisimua mwanzoni. Wao huwa motisha sana katika ushirika wao wa ukweli na wanapoona akina ndugu wana matatizo, wanaweza kuwasaidia na kuyatatua. Lakini, baada ya kuendelea kwa muda, wanaanza kuona kazi ya uongozi kuwa ngumu sana, na wanakuwa hasi—wanatamani kubadili kazi ili wafanye ile iliyo rahisi, na hawako tayari kuvumilia magumu. Watu kama hao hawana uvumilivu. Tano, sifa nyingine inayowatofautisha watu wavivu ni kutotaka kwao kufanya kazi halisi. Mara tu miili yao inapoteseka, wanakuja na visingizio vya kukwepa na kuiacha kazi yao, au kuikabidhi kwa mtu mwingine. Na mtu huyo anapomaliza kazi, bila aibu wao huvuna thawabu wenyewe. Hizi ndizo sifa tano kuu za watu wavivu. Mnapaswa kuangalia ili muone kama kuna watu wavivu kama hao miongoni mwa viongozi na wafanyakazi makanisani. Ukimpata mmoja, anapaswa kutimuliwa mara moja. Je, watu wavivu wanaweza kufanya kazi nzuri kama viongozi? Haijalishi wana ubora upi wa tabia au ubora wa ubinadamu wao, kama wao ni wavivu, hawataweza kufanya kazi yao vizuri, na watachelewesha kazi na mambo muhimu. Kazi ya kanisa yenye pande nyingi; kila kipengele chake kinahusisha kazi nyingi za kina na inahitaji ushirika kuhusu ukweli ili kutatua matatizo ili ifanywe vizuri. Kwa hivyo, viongozi na wafanyakazi lazima wawe na bidii—lazima wafanye mazungumzo mengi na kazi nyingi kila siku ili kuhakikisha ufanisi wa kazi. Wakizungumza au kufanya kiasi kidogo sana, hakutakuwa na matokeo. Kwa hivyo, ikiwa kiongozi au mfanyakazi ni mtu mvivu, hakika ni kiongozi wa uongo na hawezi kufanya kazi halisi. Watu wavivu hawafanyi kazi halisi, sembuse kwenda wenyewe kwenye maeneo ya kazi, na hawako tayari kutatua matatizo au kujihusisha na kazi yoyote maalum. Hawana uelewa au ufahamu wowote wa matatizo katika kazi yoyote. Wana fikiria za juu juu tu, zisizoeleweka vichwani mwao kutokana na kusikiliza kile ambacho wengine wamesema, na wanaboronga kwa kuhubiri mafundisho kidogo tu. Je, mnaweza kumtambua kiongozi wa aina hii? Je, mnaweza kujua kwamba yeye ni viongozi wa uongo? (Kwa kiwango fulani.) Watu wavivu ni wazembe katika wajibu wowote wanaofanya. Haijalishi wajibu wao ni upi, hawana uvumilivu, wanafanya kazi kwa manung’uniko, na wanalalamika kila wanapopitia magumu fulani, wakimwaga malalamiko yasiyoisha. Wanamtukana yeyote anayewakosoa au kuwapogoa, kama mwanamke mwenye ulimi mkali anayewatukana watu mitaani, kila mara akitaka kuweka hasira zake juu ya wengine, na hataki kufanya wajibu wake. Inaonyeshaje kwamba hawataki kufanya wajibu wao? Inaonyesha kwamba hawabebi mzigo, hawataki kuchukua jukumu, na ni watu wavivu. Hawataki kuteseka kwa shida au kulipa gharama. Hii inatumika hasa kwa viongozi na wafanyakazi: Ikiwa hawabebi mzigo, je, wanaweza kutimiza majukumu ya viongozi na wafanyakazi? Hawawezi kabisa.
Viongozi wa Uwongo Hawafuatilii Wala Kutoa Mwelekeo Kuhusu Kazi
Tumejadili hivi punde kipengele hiki cha jukumu la tano la viongozi na wafanyakazi: “kudumisha ufahamu na uelewa wa hali ya kila kipengele cha kazi.” Kwa kujadili kipengele hiki, tulifichua baadhi ya maonyesho maalum ya viongozi bandia, pamoja na utu na tabia zao. Sasa, hebu tuangalie “kudumisha ufahamu na uelewa wa maendeleo ya kila kipengele cha kazi.” Bila shaka, maendeleo ya kazi yana uhusiano kwa kiasi fulani na hali ya kazi, uhusiano huo ni wa karibu mno. Ikiwa mtu hawezi kudumisha ufahamu na uelewa wa hali ya kipengele cha kazi, basi vile vile hawezi kudumisha ufahamu na uelewa wa maendeleo ya kazi. Kwa mfano, jinsi maendeleo ya kazi yalivyo, yameendelea kufikia hatua gani, hali za watu wanaohusika ni zipi, iwapo kuna matatizo yoyote na nyanja za kitaaluma, iwapo kuna sehemu yoyote ya kazi ambayo haikidhi mahitaji ya nyumba ya Mungu, matokeo yaliyopatikana ni ya aina gani, kama watu wowote wanaofanya kazi wasio na ujuzi sana katika nyanja za kitaaluma za kazi wanajifunza, ni nani anayeandaa mafundisho, wanachofundishwa ni kitu gani, wanajifunza vipi, na kadhalika—masuala haya maalum yote yanahusiana na maendeleo. Kwa mfano, je, kazi ya kutunga nyimbo za dini si ni muhimu sana? Kwa wimbo mmoja, kuanzia uteuzi wa kwanza wa vifungu muhimu vya maneno ya Mungu hadi kukamilika kwa utunzi, ni kazi gani maalum zinazohitaji kufanywa katika mchakato huu? Kwanza, ni muhimu kuchagua vifungu muhimu vya maneno ya Mungu vinavyofaa kuwa nyimbo za dini, na lazima pia viwe na urefu unaofaa. Hatua ya pili inahusisha kutafakari ni mtindo upi wa wimbo unaofaa kwa kifungu hicho ili kiwe cha kupendeza na cha kufurahisha kuimba. Kisha, watu wanaofaa wa kuimba wimbo lazima wapatikane. Je, hizi si kazi maalum? (Ndiyo.) Baada ya wimbo kutungwa, kiongozi wa uongo hawezi kuuliza kabisa kama muundo ni bora au mtindo unafaa. Mtunzi, anapogundua ukosefu wa usimamizi, binafsi huhisi unatosha na huendelea kuurekodi. Kifungu cha maneno ya Mungu ambacho kila mtu alikuwa anatarajia kigeuzwe kuwa wimbo hatimaye huwekwa kwenye muziki na kufanywa wimbo, lakini wengi wanaona bado kina dosari wanapoimba. Ni tatizo lipi linalojitokeza? Wimbo uliotungwa haukufikia kiwango kinachostahili: Ulirekodiwa licha ya kukosa mdundo na mvuto. Kiongozi wa uongo, baada ya kuusikia, anauliza, “Ni nani aliyetunga wimbo huu? Kwa nini ulirekodiwa?” Kufikia wakati wanapouliza swali hili, angalau mwezi mmoja tayari umepita. Katika mwezi huo, je, kiongozi hangepaswa kufuatilia na kuelewa haraka maendeleo ya kazi hii? Kwa mfano, utunzi wa wimbo ulikuwa unaendeleaje? Je, lahani msingi liliamuliwa? Je, ulikuwa na mdundo? Je, mdundo na mtindo wa wimbo huu ulilingana na maneno ya Mungu? Je, watu binafsi wenye uzoefu unaofaa walisaidia kwa mwongozo? Baada ya kuutunga, je, wimbo huu ungeweza kuimbwa na watu wengi kote? Ungekuwa na athari gani? Je, tuni yake ilizingatiwa kuwa nzuri? Kiongozi wa uongo alishindwa kufuatilia mambo kama haya kwa ujumla. Na ana sababu ya kutofuatilia: “Sielewi utunzi wa nyimbo za dini. Ninawezaje kufuatilia jambo ambalo silielewi? Haiwezekani.” Je, hii ni sababu halali? (Hapana.) Siyo sababu halali; kwa hivyo, je, mtu ambaye hajui kutunga nyimbo za dini bado anaweza kufuatilia? (Ndiyo.) Anapaswa kufuatiliaje? (Anaweza kushirikiana na akina ndugu na dada, na kuukagua wimbo na mdundo kulingana na kanuni ili kuona kama unafaa; anaweza kufuatilia kazi kwa vitendo, badala ya kupuuza jukumu lao.) Sifa kuu ya kazi ya viongozi wa uongo ni kuongea ovyo kuhusu mafundisho na kurudia kauli mbiu mithili ya kasuku. Baada ya kutoa maagizo yao, wanapuuza tu jambo hilo. Hawaulizi maswali kuhusu maendeleo yanayofuata ya kazi hiyo; hawaulizi kama matatizo yoyote, upotofu, au matatizo yamejitokeza. Wanaona kazi yao imekamilika mara tu wanapoigawa kazi. Kwa kweli, kama kiongozi, baada ya kupanga kazi, lazima ufuatilie maendeleo ya kazi. Hata kama hujui taaluma ya kazi hiyo—hata kama huna ujuzi wowote kuihusu—unaweza kupata njia ya kutekeleza kazi yako. Unaweza kupata mtu anayeielewa kweli, anayefahamu taaluma husika, kufanya uchunguzi na kutoa mapendekezo. Kutokana na mapendekezo watakayotoa unaweza kutambua kanuni zinazofaa, na hivyo utakuwa na uwezo wa kufuatilia kazi hiyo. Iwe unaifahamu au unaielewa taaluma husika au la, angalau wewe lazima usimamie kazi hiyo, uifuatilie, na ufanye uchunguzi na uulize maswali kila mara kuhusu maendeleo yake. Lazima uendelee kuelewa mambo kama hayo; hili ni jukumu lako, ni moja ya sehemu ya kazi yako. Kutofuatilia kazi, kutofanya chochote zaidi mara tu imepeanwa, kupuuza majukumu yako—hivi ndivyo viongozi wa uongo wanavyofanya mambo. Kutofuatilia au kutoa mwelekeo kuhusu kazi, kutouliza au kutatua masuala yanayojitokeza, na kutoelewa maendeleo au ufanisi wa kazi—hizi pia ni dalili za viongozi wa uongo.
Viongozi wa Uwongo Hawafanyi Kazi Halisi, Jambo Linalochelewesha Maendeleo ya Kazi
Kwa sababu viongozi wa uongo hawajifunzi kuhusu maendeleo ya kazi, na kwa sababu hawawezi kutambua kwa haraka—sembuse kutatua—matatizo yanayojitokeza ndani yake, hili mara nyingi husababisha kucheleweshwa kwa mara kwa mara. Katika kazi fulani, kwa sababu watu hawaelewi kanuni na hakuna mtu anayefaa wa kuwajibikia au kuisimamia, wale wanaofanya kazi mara nyingi huwa katika hali ya mtazamo hasi, uzembe, na kusubiri, jambo ambalo huathiri vibaya maendeleo ya kazi. Kama viongozi wangetimiza majukumu yao—kama wangesimamia kazi, kuisukuma mbele, kuikagua, na kupata mtu anayeelewa taaluma hiyo kutoa mwongozo, basi kazi ingekuwa imeendelea kwa haraka badala ya kukumbwa na ucheleweshaji wa mara kwa mara. Kwa viongozi, basi, ni muhimu kufahamu na kuelewa hali ya kazi. Bila shaka, pia ni muhimu sana kwa viongozi kufahamu na kuelewa jinsi kazi inavyoendelea, kwani maendeleo yanahusiana na ufanisi wa kazi na matokeo yanayokusudiwa kufikiwa. Ikiwa viongozi na wafanyakazi hawaelewi jinsi kazi ya kanisa inavyoendelea, na hawafuatilii au kusimamia mambo, basi bila shaka maendeleo ya kazi ya kanisa yataenda polepole. Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi wanaofanya majukumu wana tabia za kilaghai sana, hawana hisia ya ubebaji mzigo, na mara nyingi wao huwa na mtazamo hasi, wazembe, na wavivu. Ikiwa hakuna mtu mwenye hisia ya ubebaji wa mzigo na uwezo wa kazi anayechukua jukumu la kazi kwa njia thabiti, akijifunza kuhusu maendeleo ya kazi kwa wakati unaofaa, na kuwaongoza, kuwasimamia, kuwaadhibu, na kuwarekebisha wafanyakazi wanaofanya majukumu, basi bila shaka, kiwango cha ufanisi wa kazi kitapungua sana na matokeo ya kazi yatakuwa duni sana. Ikiwa viongozi na wafanyakazi hawawezi hata kuona hili kwa uwazi, ni wapumbavu na vipofu. Na kwa hivyo, viongozi na wafanyakazi lazima waangalie haraka, wafuatilie, na kuelewa maendeleo ya kazi, wachunguze ni matatizo gani waliyo nayo watu wanaofanya majukumu yanayohitaji kutatuliwa, na kuelewa ni matatizo gani yanaopaswa kutatuliwa ili kufikia matokeo bora. Mambo haya yote ni muhimu sana, mtu anayechukua jukumu la kiongozi lazima awe wazi kuhusu mambo haya. Ili kutenda wajibu wako vizuri, hupaswi kuwa kama kiongozi wa uongo, ambaye hufanya kazi isiyokamilika kisha anafikiri ametimiza wajibu wake vizuri. Viongozi wa uongo ni wazembe na wapuuzi katika kazi yao, hawana hisia ya uwajibikaji, hawasuluhishi matatizo yanapojitokeza, na haijalishi ni kazi gani wanayofanya, wanaipitia tu juujuu na kuifanya kwa uzembe; wao husema tu maneno ya kujigamba, kutoa mafundisho na mazungumzo matupu, na kufuata tu taratibu kazini bila uhalisi. Kwa ujumla, hii ndiyo hali ya jinsi viongozi wa uongo wanavyofanya kazi. Ingawa, ikilinganishwa na wapinga Kristo, viongozi wa uongo hawafanyi chochote kibaya waziwazi na hawafanyi uovu wa wazi wala hawaufanyi kwa makusudi, ukizingatia ufanisi wa kazi zao, ni sawa kuwaelezea kama watu wazembe, kama wasiobeba mzigo, kama wasiowajibika na wasio na uaminifu kwa wajibu wao.
Tumeshiriki hivi punde kuhusu viongozi wa uongo kutofanya kazi halisi, na kutofahamu na kuelewa maendeleo ya kila kipengele cha kazi. Kuhusu matatizo na ugumu unaotokea katika kazi ya kanisa, pia ni kweli kwamba viongozi wa uongo wanavipuuza kabisa au wanatoa mafundisho machache tu na kuiga kauli mbiu ili kuvitupa pembeni. Kuhusiana na mambo yote ya kazi, mtu hatawahi kuwaona wakija mahali pa kazi wenyewe kujaribu kuelewa na kufuatilia kazi. Mtu hatawaona wakishiriki ukweli ili kutatua matatizo pale, na zaidi hatawaona wakiongoza na kusimamia kazi kibinafsi, kuzuia kasoro na upotovu kutokea. Huu ndio udhihirisho ulio wazi zaidi wa njia ya hali ya uzembe ambayo vingozi wa uongo wanvyofanya kazi. Ingawa viongozi wa uongo, tofauti na wapinga Kristo, hawakusudii kuharibu au kutatiza kazi ya kanisa, wala hawafanyi maovu mbalimbali na kuanzisha falme zao huru, tabia zao mbalimbali za kizembe husababisha vikwazo vikubwa kwa kazi ya kanisa, kiasi kwamba matatizo mbalimbali yanaendelea kutokea bila mwisho na hayatatuliwi. Hili linaathiri kwa uzito maendeleo ya kila kipengele cha kazi ya kanisa, na huathiri kuingia katika uzima kwa watu wateule wa Mungu. Je, viongozi hao wa uongo hawapaswi kuondolewa? Viongozi wa uongo hawawezi kufanya kazi halisi—chochote wanachofanya huanza kwa nguvu lakini kinakoma mwishoni. Jukumu wanalochukua ni kama la kuanzisha hafla: Wanaimba kwa kurudia kauli mbiu na kuhubiri mafundisho, na wanapowapa wengine kazi hiyo na kupanga atakayeiwajibikia, wanaona wanamaliza nayo. Wanafananishwa na vipaza sauti vinavyosikika vinavyopatikana maeneo ya vijijini nchini China – huu ndio upeo wa jukumu wanalochukua. Wanafanya kazi ndogo tu ya mwanzo; kwa kazi iliyobaki, hawapo kabisa. Kuhusu maswali maalum kama vile jinsi kila kipengele cha kazi kinavyokwenda, ikiwa kinalingana na kanuni, na ikiwa kina ufanisi—hawajui majibu. Hawashirikiani kwa undani na watu wa kawaida na kutembelea mahali pa kazi ili kufahamu na kuelewa maendeleo na maelezo ya kila kipengele cha kazi. Kwa hivyo, viongozi wa uongo huenda hawakusudi kusababisha usumbufu na misukosuko, au kufanya maovu mbalimbali wakati wa uongozi wao, lakini, kwa kweli, wanalemaza kazi, wao huchelewesha maendeleo ya kila kitu cha kazi ya kanisa, na kufanya iwe vigumu kwa watu wateule wa Mungu kutekeleza majukumu yao vizuri na kupata kuingia katika uzima. Kwa kufanya kazi kwa namna hii, wangewezaje kuwaongoza watu wateule wa Mungu kwenye njia sahihi ya imani kwa Mungu? Hili linaonyesha kwamba viongozi wa uongo hawafanyi kazi yoyote halisi. Wanashindwa kufuatilia kazi ambayo wanapaswa kuwajibikia au kutoa mwongozo na usimamizi kuishusu ili kuhakikisha kwamba kazi ya kanisa inaendelea kawaida; wanashindwa kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa ya viongozi na wafanyakazi, na wanashindwa kutimiza uaminifu au wajibu wao. Hili linathibitisha kwamba viongozi wa uongo sio waaminifu katika jinsi wanavyofanya majukumu yao, kwamba ni wa kipuuzi tu; wanawadanganya watu wateule wa Mungu na Mungu Mwenyewe, na wanaathiri na kuzuia utekelezaji wa mapenzi Yake. Ukweli huu unaonekana kwa wote. Huenda ikawa kwamba kiongozi wa uongo hana uwezo wa kufanya kazi hiyo; huenda pia ikawa wanapuuza kazi yao na kwa makusudi. Vyovyote vile, ukweli unabaki kwamba wanaiharibu kazi ya kanisa. Hakuna maendeleo yoyote yanayofanywa katika kila kipengele cha kazi ya kanisa, na matatizo yaliyokusanywa yanabaki bila kutatuliwa kwa muda mrefu. Hili haliathiri tu kuenea kwa kazi ya injili, bali pia linazuia kwa uzito kuingia katika uzima kwa watu wateule wa Mungu. Mambo haya ya kweli yanatosha kuonyesha kwamba mbali na viongozi wa uongo kutoweza kufanya kazi halisi, wao pia wanakuwa vikwazo kwa kazi ya kueneza injili, na vizuizi kwa utekelezaji wa mapenzi ya Mungu kanisani.
Viongozi wa uongo hawafanyi kazi halisi na hawawezi kutatua matatizo ya kweli. Licha ya kuchelewesha maendeleo ya kazi na kuathiri matokeo yake, pia linasababisha hasara kubwa kwa kazi ya kanisa, kubadhiri rasilimali watu, rasilimali za kimwili, na vilevile rasilimali za kifedha. Kwa hivyo, viongozi wa uongo wanapaswa kufidia hasara za kiuchumi. Baadhi ya watu husema, “Ikiwa viongozi na wafanyakazi wanapaswa kulipa fidia kwa hasara zinazosababishwa na kutofanya kazi yao vizuri, basi hakuna atakayetaka kuwa kiongozi au mfanyakazi.” Watu kama hao wasio na wajibu hawastahili kuwa viongozi au wafanyakazi. Wale wasio na dhamiri au mantiki ni watu waovu—je, si ni balaa ikiwa watu waovu wanataka kuwa viongozi na wafanyakazi? Kwa kuwa kazi nyingi ya nyumba ya Mungu inahusisha gharama za kiuchumi, je, si ni lazima kuzipigia hesabu gharama hizo? Je, sadaka ya Mungu ni kitu ambacho watu wanaweza kutumia vibaya na kutupilia mbali kwa hiari yao? Viongozi na wafanyakazi wana haki gani ya kupoteza sadaka za Mungu? Kuleta hasara ya kiuchumi lazima kufidiwe; hili ni jambo la kawaida na la haki, na hakuna mtu aliye na uwezo wa kupinga. Kwa mfano, iwapo kuna kazi ambayo inaweza kukamilika kwa mwezi mmoja na mtu mmoja. Ikiwa inachukua miezi sita kufanya kazi hii, je, matumizi ya miezi mitano iliyobaki hayasababishi hasara? Acha niwape mfano kuhusu kuhubiri injili. Iwapo mtu yuko tayari kuchunguza njia ya kweli na huenda angeweza kushawishiwa ndani ya mwezi mmoja tu, baada ya hapo anaingia kanisani na kuendelea kupokea unyunyizaji na riziki, na ndani ya miezi sita anaweza kuweka msingi. Lakini mtazamo wa mtu anayehubiri injili kuelekea jambo hili ni wa kutojali na kuzembea, na viongozi na wafanyakazi pia wanapuuza majukumu yao, na mwishowe ikachukua nusu mwaka kumshawishi mtu huyo, je, nusu mwaka huo hautakuwa hasara kwa maisha yao? Ikiwa watakutana na majanga makubwa na bado hawajaweka msingi katika njia ya kweli, watakuwa hatarini, na, je, watu hao hawatakuwa wamewakatisha tamaa basi? Hasara kama hiyo haiwezi kupimwa kwa pesa au vitu vya kimwili. Ikiwa uelewa wa mtu huyo wa ukweli utasitishwa kwa nusu mwaka, na acheleweshwe kuweka msingi na kuanza kufanya wajibu wake kwa nusu mwaka, nani atajukumikia hili? Je, viongozi na wafanyakazi wanaweza kumudu kubeba jukumu hili? Hakuna anayeweza kumudu kubeba jukumu la kuchelewesha uzima wa mtu. Kwa kuwa hakuna anayeweza kumudu kubeba jukumu hili, ni nini kinachofaa kwa viongozi na wafanyakazi kufanya? Maneno manne: Jitolee kwa ukamilifu. Jitolee kwa ukamilifu kabisa kufanya nini hasa? Kutimiza majukumu yako mwenyewe, kufanya kila kitu uonacho mwenyewe, kufikiria akilini mwako, na kufanikisha kwa ubora wako mwenyewe. Huku ndiko kujitolea kwa ukamilifu, huku ni kuwa mwaminifu na mwenye kuwajibika, na hili ndilo jukumu ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kutimiza. Baadhi ya viongozi na wafanyakazi hawachukulii kuhubiri injili kuwa jambo la muhimu. Wanafikiri, “Kondoo wa Mungu watasikia sauti ya Mungu. Yeyote anayechunguza na kukubali atabarikiwa; yeyote asiyechunguza na kutokubali hatabarikiwa, na anastahili kufa katika janga!” Viongozi wa uongo hawaonyeshi hali ya kujali kabisa nia za Mungu, na hawabebi mzigo wowote wa kazi ya injili; pia hawajukumikii wageni ambao wameingia tu kanisani, na hawachukui uzima wa watu wateule wa Mungu kwa uzito—wao daima huzingatia kujifurahisha katika manufaa ya hadhi zao. Haijalishi ni watu wangapi wanachunguza njia ya kweli, hawana wasiwasi hata kidogo, wakiwa na mtazamo wa kupita tu na mambo, wakifanya mithili ya mfalme au afisa aliyestaafu. Haijalishi jinsi kazi ilivyo muhimu au ya dharura, hawataonekana kwenye eneo la tukio, wala hawatauliza na kuelewa hali ya kazi, au kufuatilia kazi na kutatua matatizo. Wanapanga tu kazi na kudhani kwamba kazi yao imekamilika kabisa, na wanaamini kwamba huku ndiko kufanya kazi. Je, huku si kuwa na tabia ya kupuuza? Je, huku si kuwadanganya wale walio juu yao na chini yao? Je, viongozi na wafanyakazi kama hao wanafaa kutumiwa na Mungu? Je, sio kama maafisa wa lile joka kubwa jekundu? Wanafikiri, “Kuwa kiongozi au mfanyakazi ni sawa na kushikilia ofisi, na mtu anapaswa kufurahia manufaa ya hadhi hiyo. Kushikilia ofisi hunipa haki hii, kunaniepusha kuwepo katika kila jambo. Ikiwa kila wakati ningekuwepo mahali pa tukio, nikifuatilia kazi na kuelewa hali ilivyo, lingekuwa jambo la kuchosha lililoje, ni jambo la kudhalilisha kiasi gani! Siwezi kukubali uchovu wa aina hii!” Huu ndio utendakazi wa viongozi na wafanyakazi wa uongo, wanaojali tu kutamani faraja na kufurahia manufaa ya hadhi bila kufanya kazi yoyote halisi, na wakikosa dhamiri au mantiki. Vidudu hao wanapaswa kuondolewa, na hata wakichukuliwa adhabu, wanastahili! Baadhi ya viongozi na wafanyakazi, licha ya miaka mingi ya kufanya kazi ya kanisa, hawajui jinsi ya kuhubiri injili, wala hata kutoa ushuhuda. Ukiwaambia washiriki kuhusu ukweli wote juu ya maono ya kazi ya Mungu kwa wapokeaji watarajiwa wa injili, hawana uwezo. Wakiulizwa, “Je, umewahi kujitahidi ili kujisatiti na ukweli wa maono?” viongozi wa uongo hutafakari, “Kwa nini niweke juhudi kama hizo? Kwa hadhi yangu ya juu, hiyo kazi si yangu; kuna wengine wengi wa kuifanya.” Nieleze, ni viumbe wa aina gani hawa? Wamekuwa wakifanya kazi ya kanisa kwa miaka mingi, bado hawajui jinsi ya kuhubiri injili. Na linapokuja suala la ushuhuda, lazima wamtafute mhubiri wa injili awafanyie. Kama, kiongozi au mfanyakazi, huwezi kuhubiri injili, kushuhudia, au kufanya ushirika na watu kuhusu ukweli juu ya maono, unaweza kufanya nini? Je, majukumu yako ni yapi? Je, umeyatimiza? Je, unaishi kwa kuhimili tu kile ulicho nacho tayari? Ni nini ulicho nacho? Ni nani aliyekuidhinisha kuishi kwa kutegemea kile ulicho nacho tayari? Baadhi ya wasimamizi wa timu za injili hawajawahi hata kuwaona na kuwasikiliza watu wengine wakihubiri injili. Hawana haja ya kusikiliza; hawataki kusumbuliwa, wanaona ni jambo la kusumbua, na hawana subira. Wao ni viongozi, kwani hamjui—maafisa, si vingine—kwa hivyo hawafanyi kazi hizi maalum; wanawatafuta akina ndugu na dada wazifanye. Iwapo baadhi ya wafanyakazi wa injili wanakutana na mtu wa hadhi ya juu, ambaye hufanya mambo yote kwa dhati, na ambaye anatamani kuelewa baadhi ya ukweli maalum kuhusu maono. Wafanyakazi wa injili hawawezi kushiriki kwa uwazi kikamilifu, kwa hivyo wanawaomba viongozi wao wafanye hivyo. Viongozi hujikuta kwamba hawana la kusema, na hata wao huamua kutoa visingizio, wakisema, “Sijawahi kufanya kazi hii mwenyewe. Nyinyi nendeni mkafanye; Nitawaunga mkono. Matatizo yoyote yatajitokeza, nitawasaidia kuyarekebisha; Ninawaunga mkono. Msiwe na wasiwasi. Kuna nini cha kuogopa tukiwa na Mungu? Mtu anapotafuta njia ya kweli, mnaweza kutoa ushuhuda au kushiriki kuhusu ukweli wa maono. Mimi nina jukumu la kushiriki tu kuhusu ukweli wa kuingia katika uzima. Kazi ya ushuhuda ni mzigo wenu mzito wa kubeba, msinitegemee mimi.” Kila wakati inapofikia wakati muhimu wa kutoa ushuhuda kwa kuhubiri injili, wanajificha. Wanajua fika kwamba hawana ukweli, hivyo kwa nini hawajitahidi kujizatiti na ukweli? Wakijua fika kwamba hawana ukweli, kwa nini kila wakati wanataka sana kuwa viongozi? Hawana kipaji chochote, na bado wana ujasiri wa kuchukua nafasi yoyote rasmi—wangechukua hata nafasi ya mfalme kama wangeruhusiwa—hawana aibu kamwe! Haijalishi kiwango cha uongozi walichonacho, hawawezi kufanya kazi halisi, lakini wanataka kufurahia manufaa ya hadhi bila kuhisi maumivu yoyote ya dhamiri. Je, si hawa ni watu wasio na haya kabisa? Ingeeleweka ikiwa mngetakiwa kuzungumza kwa lugha ya kigeni na hamuwezi; lakini kushirikiana juu ya ukweli wa maono na nia za Mungu katika lugha yenu asili kunafaa kuwezekana, sivyo? Watu ambao wameamini kwa miaka mitatu hadi mitano pekee wanaweza kusamehewa kwa kutoweza kufanya ushirika juu ya mambo ya ukweli. Lakini baadhi wamemwamini Mungu kwa karibu miaka 20 na bado kwa sababu fulani bado hawawezi kufanya ushirika ukweli kuhusu maono—je, watu kama hao si ni watu wasio na maana? Je, wao si ni watu wasiofaa? Linanishangaza Mimi kusikia kwamba mtu amemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hajui namna ya kushiriki ukweli kuhusu maono. Mnahisi vipi baada ya kusikia mambo haya? Si ni jambo linalowezekana? Wamekuwa wakifanya kazi zao vipi miaka hii yote? Wakiambiwa watoe mwongozo wa kutengeneza muziki, hawajui jinsi ya kuufanya, na wanasema kwamba taaluma hii maalum ni ngumu mno, si kitu ambacho mtu wa kawaida anaweza kuelewa. Wakiambiwa watoe mwongozo katika kazi ya utengenezaji wa sanaa, au katika kazi ya utengenezaji wa filamu, wanadai kwamba kazi hizi zinahitaji kiwango cha juu sana cha ujuzi wa kiufundi ambazo wao hawawezi kushughulikia. Wanapoambiwa waandike makala za ushuhuda wa uzoefu, wanasema kwamba kiwango chao cha elimu ni cha chini mno na hawajui jinsi ya kuziandikia, na kwamba hawajawahi kufunzwa. Ikiwa hawawezi kufanya kazi za aina hii, hilo linasameheka, lakini kazi ya injili ni sehemu ya wajibu wao kiasili. Hawana uwezo wa kuifahamu zaidi kazi hii—je, haipaswi kuwa rahisi kwao? Kipengele muhimu zaidi cha kufanya ushirika kwa ajili ya ukweli kuhusu maono ni kushiriki waziwazi ukweli wa hatua tatu za kazi. Mwanzoni, watu hukosa uzoefu mwingi wa kufanya hivyo na huenda wasifanya ushirika vizuri, lakini kwa kufunzwa kwa muda, wanaweza kuwa bora zaidi katika ushirika kadri wanavyofanya zaidi, kiasi kwamba wataweza kuzungumza kwa mpangilio, kwa lugha sahihi na wazi, na msemo wa maneno ulio mzuri. Je, hili sio sehemu maalum ya kazi ambayo viongozi wanapaswa kujua? Huku si kama kumlazimisha samaki aishi kwenye nchi kavu, sivyo? (Hapana, sivyo.) Lakini viongozi hao wa uongo hawana uwezo wa kufanya hata sehemu hii ndogo ya kazi. Lakini, bado wanatumikia kama viongozi? Wanafanya nini bado katika nafasi hiyo? Baadhi ya watu husema, “Mimi ni mtu ambaye mawazo yangu yamechanganyikiwa na yasiyo wazi, bila mantiki, na sina uwezo mzuri wa kuzungumzia ukweli kuhusu maono.” Kwa hivyo, je, unaweza kutambua na kutatua kasoro na upotofu mbalimbali unaotokea katika kazi ya injili? Ikiwa hamwezi kuutambua, basi kwa hakika hamtaweza kuutatua pia. Wakati viongozi wa uongo wanasimamia kazi ya injili, kutochukua jukumu lolote katika kukagua au kusimamia; wanawaacha walio chini yao wafanye watakavyo, ili mtu yeyote afanye mambo kwa namna anayotaka, na kumhubiria yeyote anayetaka—hakuna kanuni au viwango vinavyotumika kabisa. Baadhi ya watu hutenda kwa ghafla, kuwa bila busara na hasa bila kanuni wanapofanya mambo, na kufanya matendo mabaya bila kufikiri. Viongozi wa uongo hushindwa kabisa kugundua au kutambua masuala haya.
Inasemekana kwamba huko Amerika Kusini na Afrika, baadhi ya watu masikini wameletwa kundini kupitia kazi ya injili. Watu hawa hawana mapato ya kudumu, na hata kupata chakula cha kutosha na kuendelea kuishi ni shida. Kwa hivyo, ni nini kinachopaswa kufanywa? Kulikuwa na viongozi ambao walisema, “Ni nia ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu, na ili kuokolewa, ni lazima kwanza mtu awe na chakula cha kutosha, sivyo? Je, nyumba ya Mungu haipaswi kutoa afueni basi? Ikiwa wanamwamini Mungu, tunaweza kusambaza vitabu vichache vya maneno ya Mungu kwao. Hawana kompyuta wala simu, kwa hiyo tunapaswa kufanya nini wakiomba kufanya kazi? Fanya uchunguzi fulani, angalia kama wako tayari kufanya kazi kwa dhati.” Kupitia uchunguzi, iligundulika kwamba watu hawa kwa sasa hawakuwa na pesa, lakini kama wangekuwa na pesa wangekula mpaka washibe, wangekuwa tayari kwenda nje na kuhubiri injili na kufanya wajibu wao. Baada ya kuelewa hali hizi, viongozi walianza kusambaza fedha za msaada, wakiwapa kila mwezi. Chakula na makaazi, na hata ada za mtandao, na ununuzi wa simu, kompyuta, na vifaa vingine kwa watu hawa vyote vililipwa kwa fedha za nyumba ya Mungu. Kusambaza fedha kwa watu hawa hakukuleanga uenezaji wa kazi ya injili, lakini badala yake, ili kutoa msaada kwa ajili ya maisha yao. Je, hili lilikuwa kulingana na kanuni? (Hapana, halikulingana na kanuni.) Je, nyumba ya Mungu ina sheria ambayo, wakati wa kuhubiri injili na kukutana na watu maskini wasio na njia ya kujipatia riziki, mradi tu wanaweza kukubali hatua hii ya kazi, wanapaswa kupewa msaada? Je, kuna kanuni kama hiyo? (Hapana.) Basi ni kwa kanuni gani ndiyo viongozi hawa waliwagawia fedha za msaada? Je, ni kwa sababu walidhani kwamba nyumba ya Mungu ilikuwa na pesa lakini hakuna mahali pa kuzitumia, au kwa sababu waliwaona watu hawa kuwa watu wa kusikitisha sana, au walikuwa na matumaini kwamba watu hawa watasaidia kueneza injili? Nia hasa ni ipi? Walikuwa wanajaribu kufanikisha nini? Ilipokuja suala la kusambaza simu, kompyuta, na gharama za maisha, walionyesha shauku kubwa; walifurahia kushiriki katika kazi hiyo ambayo iliwasaidia wengine, kwa kuwa iliwawezesha kuwapeleka neema na watu hawa na kushinda mioyo yao, na walijitoa hasa katika katika kazi za aina hii, wakienda zaidi na zaidi na kukosa hata chembe ya aibu. Huku ni kutumia pesa za Mungu ili kupata sifa kutoka kwa watu na kununua upendo wao. Kwa kweli, watu hawa masikini hawakumwamini Mungu; walikuwa wakijaribu kujaza tumbo zao na kutafuta njia ya kupata riziki. Watu hao hawakuwa wanatafuta kupata ukweli au wokovu. Je, Mungu angewaokoa watu hawa? Wengine, hata kama walikuwa tayari kufanya kazi, hawakuwa waaminifu, lakini badala yake, walitiwa motisha na tamaa ya simu na kompyuta, kwa urahisi katika maisha. Lakini viongozi wa uongo hawakujali kuhusu hili; Kwa muda mrefu kama mtu alikuwa tayari kufanya kazi, walimtunza, sio tu kwa kutoa fedha kwa ajili ya makazi na chakula, lakini pia kwa kununua kompyuta, simu, na vifaa mbalimbali. Lakini ilitukia kwamba watu hawa walifanya kazi zao bila kufikia matokeo yoyote. Je, viongozi hawa wa uongo hawakuwa wakitupa tu fedha? Je, hawakutumia fedha za nyumba ya Mungu ili kuonyesha ukarimu wao? (Ndiyo.) Je, hii ni kazi ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya? (Hapana.) Je, si hawa walikuwa viongozi wa uongo? Viongozi wa uongo wanapenda kujifanya kwamba wana fadhila, upole, na wema. Ikiwa unataka kuonyesha wema, hilo ni jambo zuri, tumia pesa zako mwenyewe tu! Ikiwa hawana nguo, vua zako mwenyewe uwape; usitumie sadaka za Mungu! Sadaka za Mungu zimenuiwa kwa kazi ya kueneza injili, si kwa ajili ya kusambaza faida za ustawi, na hakika si kwa ajili ya kuwasaidia masikini. Nyumba ya Mungu sio taasisi ya ustawi. Viongozi wa uongo hawawezi kufanya kazi halisi, sembuse kuweza kukimu ukweli au uzima. Wao huzingatia tu kutumia matoleo ya Mungu kusambaza manufaa ya ustawi ili kujipatia sifa kutoka kwa watu na kudumisha sifa na hadhi yao wenyewe. Wao ni wabadhirifu wasio na haya, sivyo? Viongozi hao wa uongo wakigunduliwa, je, kuna yeyote anayeweza kuwafichua na kuwazuia kwa wakati? Hakuna mtu aliyesimama kuwazuia. Isingekuwa kwa Aliye juu kliugundua na kulikomesha, desturi ya kutumia pesa za Mungu kutoa manufaa kwa watu isingeisha. Watu hao masikini hunyoosha mikono yao zaidi, wakitaka zaidi kila wakati. Hawatosheki; haijalishi unawapa kiasi gani, hakiwatoshi kamwe. Wale wanaomwamini Mungu kwa dhati wanaweza kuacha familia zao na kazi zao nyuma kufanya wajibu wao ili waokolewe, na hata wakikabiliwa na magumu maishani, wao wanaweza kupata njia za kuyatatua peke yao bila kudai mambo kutoka kwa nyumba ya Mungu kila mara. Wanaamua wanachoweza peke yao, na kwa kile ambacho hawawezi kutatua, wao humwomba Mungu na kutegemea imani yao wapate uzoefu. Wale wanaoomba kutoka kwa Mungu kila wakati, wakitarajia nyumba ya Mungu iwape riziki na kuwategemeza, hawana akili kabisa! Hawataki kufanya wajibu wowote lakini wanataka kufurahia maisha, wanachojua ni kunyoosha mikono yao kudai vitu kutoka kwa nyumba ya Mungu, na hata hivyo, huwa haviwatoshi kamwe. Je, wao si waombaji? Na viongozi wa uongo—wapumbavu hawa—waliendelea tu kutoa faida, na hawakuacha, wakiwafurahisha watu kila mara ili wapate sifa zao, na hata wakifikiri kwamba vitendo kama hivyo vilimtukuza Mungu. Haya ndiyo mambo ambayo viongozi wa uongo hufurahia zaidi kuyafanya. Kwa hivyo, je, kuna mtu yeyote anayeweza kutambua masuala haya, ambaye anaweza kuona kiini cha matatizo haya? Viongozi wengi huyafumbia macho, wakiwaza, “Kwa namna yoyote, mimi sisimamii kazi ya injili, kwa nini nijali kuhusu mambo haya? Si pesa zangu zinazotumika. Mradi tu pesa zilizo mfukoni mwangu haziguswi, ni sawa. Mnaweza kumpa yeyote unayemtaka, hilo linanihusu nini? Si kama pesa hizo zinaishia kwenye kibeti changu hata hivyo.” Kuna watu wengi wasiowajibika, lakini ni watu wangapi wanaoweza kuitetea kazi ya nyumba ya Mungu?
Hivi sasa, kazi ya injili ughaibuni inaendelea kote ulimwenguni. Baadhi ya nchi zina watu wengi wanaoweza kukubali ukweli, huku zingine zikiwa na idadi ya watu wenye ubora wa tabia wa kiwango chachini, hivyo kusababisha upungufu wa watu wanaoweza kukubali ukweli. Baadhi ya nchi hazina uhuru wa imani, zikionyesha upinzani mkali kwa njia ya kweli na kazi ya Mungu, na sio watu wengi wanaoweza kukubali ukweli. Zaidi ya hayo, baadhi ya nchi zina idadi ya watu walio nyuma sana na wenye ubora duni wa tabia hivi kwamba hawawezi kuelewa ukweli bila kujali jinsi unavyoshirikishwa, na inaonekana kwamba watu huko wamepungukiwa na ukweli. Injili haipaswi kuhubiriwa katika sehemu kama hizo. Hata hivyo, wanaohubiri injili hawaoni kiini cha tatizo; hawawahubirii wale ambao wanaweza kukubali ukweli, badala yake wanasisitiza kutafuta visa vigumu huku wakipuuza vile rahisi zaidi. Hawahubiri katika sehemu ambazo kazi ya injili tayari inaenezwa na ni rahisi kuhubiri. Badala yake, wanasisitiza kuhubiri injili katika sehemu hizo maskini na zilizo nyuma, wakihubiri kwa vikundi vya watu wenye ubora duni zaidi, ambao hawawezi kuelewa ukweli, na kwa vikundi vya kikabila wenye dhana nzito za kidini na upinzani mkali wa Mungu. Je, huu sio upotovu? Kwa mfano, chukua Uyahudi, na baadhi ya dini za kikabila na kirangi zilizokita mizizi, ambazo huchukulia Ukristo kama adui na hata kuutesa. Katika kisa ya nchi kama hizi na makabila, injili haipaswi kuhubiriwa. Kwa nini isiwe hivyo? Kwa sababu kuhubiri hakuna maana. Hata kama utatumia rasilimali zote za watu, fedha na mali, miaka mitatu, mitano, au hata kumi inaweza kuisha bila kuona matokeo yoyote muhimu. Kwa kuzingatia hali hii, ni nini kinachopaswa kufanywa? Mwanzoni, pasi na ufahamu kamili, mtu angeweza kujaribu; lakini baada ya kuona hali kwa uwazi—kwamba kuhibiri injili kwao kwa gharama kubwa kunaweza kukosa kuzalisha matokeo mazuri mwishowe—lazima mtu achague njia nyingine, njia itakayozaa matokeo. Je, hili si jambo ambalo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuona wazi? (Ndiyo). Lakini Viongozi wa uongo hawaelewi hili. Suala la wapi pa kuanza kueneza injili ng’ambo linapoibuka, baadhi husema, “Anza na Israeli. Kwa kuwa Israeli ilikuwa msingi wa hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, lazima ihubiriwe huko. Haijalishi ni vigumu kiasi gani, lazima tuendelee kuwahubiria.” Hata hivyo, baada ya kuhubiri kwa muda mrefu, bila matokeo mazuri, yanayosababisha kukata tamaa. Viongozi wanapaswa kufanya nini wakati huu? Ikiwa ni kiongozi mwenye ubora wa juu na mwenye kubeba mzigo, angesema, “Mahubiri yetu ya injili hayana kanuni; hatujui jinsi ya kufuata mkondo, ila tunaona mambo kulingana na mawazo yetu—huko ni kukosa kujua kwa upande wetu! Upumbavu, ukaidi, na upuzi wa watu hawa haukuwa tulivyotarijia. Tulidhani kwamba kwa sababu wamekuwa wakimwamini Mungu kwa maelfu ya miaka, wanapaswa kuwa wa kwanza kusikiliza injili ya Mungu, lakini tulidhani vibaya; ni wapumbavu sana! Ukweli ni kwamba, Mungu alipokuwa akifanya kazi ya ukombozi, Alikuwa ameshakataa tamaa na wao. Kwetu sisi kurudi na kuwahubiria kutakuwa kujihusisha na juhudi isiyo ya maana; itakuwa kufanya kazi ya kuchoka bila matokeo na kufanya upumbavu. Hatujaelewa vizuri nia za Mungu. Mungu halifanyii kazi jambo hili, hivyo sisi binadamu tunawezaje kulifanya? Tumejaribu mno, lakini haijalishi njia tunayotumia kuhubiri, hawakubali njia ya kweli. Tunapaswa kuachana nalo, tuwaweke kando, na kutowajali kwa sasa. Iwapo kunao ambao wako tayari kutafuta, basi tutawakaribisha na kutoa ushahidi wa kazi za Mungu kwao. Iwapo hakuna wanaotafuta, basi hakuna haja ya sisi kuchukuwa hatua ya kuwatafuta.” Je, hii si kanuni ya kuhubiri injili? (Ndiyo.) Hivyo, kiongozi wa uongo anaweza zingatia kanuni? (Hapana.) Viongozi wa uongo wako na ubora duni na hawana uwezo wa kuona wazi kiini cha suala hilo; watasema, “Mungu amesema kwamba Waisraeli ndio watu Wake wateule. Hatuwezi kamwe kuwaacha wakati wowote. Wanapaswa kupewa kipaumbele; tunahitaji kuwahubiria kwanza kabla ya kuwahubiria watu walio katika nchi zingine. Kama kazi ya Mungu ingeeenzwa Israeli, huo ungekuwa utukufu mkubwa namna gani! Mungu alileta utukufu kutoka Israeli hadi Mashariki, na tunapaswa kurudisha utukufu huo Israeli kutoka Mashariki, na kuwaruhusu waone kwamba Mungu amerudi!” Je, hili si kauli mbiu tu? Je, linaambatana na ukweli? Haya ndiyo maneno ambayo yangesemwa na wasiolewa mambo ya kiroho. Na kuhusu viongozi wa uongo ambao hawafanyi kazi halisi, je? Hawatilii maanani mambo haya. Wanaohubiri injili wamekuwa wakitatizwa na suala hili kwa muda mrefu, wakiwa wamechanganyikiwa kati ya kukata tamaa au kuendelea kuhubiri, bila kujua jinsi ya kutenda. Viongozi wa uongo hawajui kabisa kwamba hili ni tatizo. Wakiwaona watu hawa wakihangaika kwa kutokuwa na njia ya kufuata, wanasema, “Kuna nini cha kuhangaikia? Tuna ukweli na ushuhuda ambao tumeuona; wahubirie tu!” Mtu anasema, “Huelewi, watu hawa ni vigumu sana kuwahubiria.” Masuala muhimu yanapotokea katika kazi hii yanayohitaji viongozi kuyatatua, viongozi hao bado wanapaza sauti wakisema kauli mbiu na maneno matupu. Je, hii ndiyo tabia inayotarajiwa kwa viongozi? Wanapoulizwa kama wapokeaji watarajiwa wa injili wanapaswa kuhubiriwa, wanasema, “Kila mtu anapaswa kuhubiriwa, hasa Waisraeli, wanapaswa kuhubiriwa.” Je, mnaskia tatizo lolote katika maneno haya? Wanajua huu ni upotovu, kasoro katika kazi ya injili inayohitaji kushugulikiwa nao? Watu hawa nyangarika hawana habari na bado wapo pale wakitetea maneno makubwa na kupiga kelele za kauli mbiu, kwa hakika, wao ni taka zisizo na thamani! Na bado wanadhani kwamba wao ni werevu na wenye ubora wa tabia na ni wenye akili. Hawajui hata kwamba dosari kubwa na upotovu kama huo umeonekana katika kazi hiyo; je, wanaweza hata kuanza kuitatua? Uwezekano hapo ni mdogo zaidi. Wanaohubiri injili wote wana wasiwasi mkubwa; kazi ya injili imeathiriwa, imezuiliwa, na haiwezi kuendelea vizuri, na la kushangaza viongozi wa uongo hawana ufahamu wowote kuhusu mkengeuko unaotokea katika kazi. Watu wengi, wanapokutana na matatizo au mkengeuko katika kazi, mara nyingi hawajali, hawagundui, na bado wanaamua kuendelea na mbinu isiyofaa kwa ukaidi bila kujali. Ikiwa viongozi na wafanyakazi pia hawataelewa hali na kuitambua kwa haraka, basi tatizo litakapokuwa kubwa na kuathiri kuendelea kwa kazi, na watu wengi pia waweze kugundua tatizo, viongozi na wafanyakazi hao hubaki wamechanganyikiwa. Hili linasababishwa na uzembe wa wajibu kutoka kwa viongozi na wafanyakazi. Basi, wanawezaje kuepuka matokeo mabaya kama hayo? Viongozi na wafanyakazi lazima wakague kazi mara kwa mara, na waelewe kwa haraka hali halisi na maendeleo ya kazi yenyewe. Ikitukia kwamba ufanisi wa kazi si wa hali ya juu, lazima waone ni sehemu gani yenye dosari na matatizo, na watafakari: “Sasa hivi, watu hawa wanaonekana kuwa na shughuli nyingi, lakini kwa nini hakuna ufanisi wowote dhahiri? Kama kazi ya timu ya injili; watu wengi sana huhubiri injili na kushuhudia kila siku, pamoja na baadhi ya watu wanaoshirikiana katika kazi hii, basi kwa nini watu wengi hawapatikani kila mwezi? Ni sehemu gani iliyo na tatizo? Ni nani anayesababisha tatizo? Mkengeuoko ulisababishwaje? Ulianza lini? Ninahitaji kwenda katika kila kundi ili nijue kila mtu anafanya nini kwa sasa, jinsi wapokeaji watarajiwa wa injili wa sasa walivyo, na kama mwelekeo wa kuhubiri injili ni sahihi; Ninahitaji kujua haya yote.” Kupitia kushauriana, kushirikiana, na kujadili, mkengeuko na dosari katika kazi huonekana wazi taratibu. Tatizo linapogunduliwa, haliwezi kuachwa hivyo; lazima litatuliwe. Basi, ni viongozi wa aina gani wanaoweza kugundua baadhi ya matatizo, mkengeuko, na dosari zinazoonekana katika kazi? Viongozi aina hii wanahitaji kubeba mzigo, kuwa waangalifu mno, na kushiriki katika kila undani wa kazi maalum; kufuatilia, kuelewa, na kufahamu kwa kina kila sehemu; kubaini anachofanya kila mtu, idadi ya watu wanaofaa katika kufanya kazi ipi, wasimamizi wao ni akina nani, ubora wa tabia ya watu hawa ni upi, na kama wanafanya kazi yao vizuri au la, na ufanisi wao ukoje, jinsi kazi inavyoendelea, na kadhalika—mambo haya yote lazima yabainishwe. Zaidi ya hayo, sehemu muhimu zaidi ya kazi ya injili ni kama wahubiri wa injili wana kweli au la, kama wanaweza kufanya ushirika juu ya kweli za maono waziwazi ili kutatua dhana na matatizo ya watu, kama wanaweza kukimu mahitaji ya wapokeaji watarajiwa wa injili ili kuwashawishi kabisa, na kama wanaweza kutumia njia ya mazungumzo katika ushirika wao juu ya ukweli, ili wapokeaji watarajiwa wa injili waweze kusikia sauti ya Mungu zaidi. Kwa mfano, ikiwa mpokeaji mtarajiwa wa injili anataka kujifunza kuhusu ukweli kuhusu umuhimu wa ufunuo wa mwili wa Mungu, lakini mhubiri fulani wa injili kila mara huzungumzia umuhimu wa kazi ya Mungu na kuhusu dhana za kidini ni zipi, je, hili si tatizo? Ikiwa mtu anataka tu kujifunza kuhusu jinsi anavyoweza kukombolewa na maudhui ya mpango wa usimamizi wa Mungu yanayohusu kuwakomboa wanadamu, je, si huu ni wakati wa kushiriki kuhusu ukweli wa maono wa hatua tatu za kazi ya Mungu? (Ndiyo.) Lakini mhubiri huyu wa injili anaendelea kuzungumzia kuadibu na hukumu ya Mungu, na kufichua Kwake kwamba tabia potovu za watu zinajumuisha kiburi, udanganyifu, na uovu, na mada zingine kama hizo. Kabla ya yule aliye upande huo mwingine kukubali kazi ya Mungu, mhubiri wa injili anaanza kuzungumza na yeye kuhusu kuadibu na hukumu, akifichua tabia zao potovu. Matokeo yake, mtu huyo anachukizwa, hapati anachotaka, na matatizo yake yanayohitaji kutatuliwa yanaendelea kubaki bila suluhisho; anapoteza hamu na hayuko tayari kuendelea kuchunguza. Je, hili si tatizo kwa mhubiri wa injili? Mhubiri wa injili haelewi ukweli, au hana uelewa wa mambo ya kiroho, na hivyo hajui kabisa kile ambacho mtu huyo mwingine anahitaji, kwa kushindwa kutoa hoja anapozungumza, akizungumza maneno yasioeleweka kwa muda, na kutotatua kabisa masuala ya mpokeaji mtarajiwa wa injili—je, wanawezaje kupata watu kwa kuhubiri injili kwa njia hii?
Viongozi wa uongo hupuuza masuala yoyote wanayokumbana nayo katika kazi yao. Haijalishi ni matatizo gani yanayotokea katika kazi ya injili, na haijalishi jinsi watu waovu wanavyovuruga na kuathiri kazi hii, hawazingatii uangalizi wowote humo, kana kwamba haina uhusiano nao. Viongozi wa uongo wamechanganyikiwa katika kazi yao; hata ikiwa mtu fulani ana matokeo fulani au anafuata kanuni za ukweli katika wajibu wake, hawapeani usimamizi au uchunguzi, wakiwaruhusu watu kufanya vyovyote kwa uhuru bila kujali matokeo. Hili husababisha kupotoka na dosari zinazoonekana katika kazi ya injili kutotatuliwa kamwe, na idadi isiyohesabika ya watu wanaotafuta njia ya kweli huishia kupotea, wasiweze kuletwa mbele za Mungu haraka iwezekanavyo. Baadhi ya watu, baada ya kukubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, husema, “Kwa kweli, mtu alinihubiria injili miaka mitatu iliyopita. Haikuwa kwamba sikutaka kuikubali au kwamba niliamini propaganda hasi; aliyenihubiria hakuwa na uwajibikaji. Hakuweza kujibu maswali niliyouliza, na hakuwa wazi katika ushirika nilipotafuta ukweli, akinena tu maneno yasiyo na maana. Kwa hivyo, sikuwa na budi ila kuondoka kwa masikitiko.” Miaka mitatu baadaye, baada ya kufanya uchunguzi mtandaoni na kisha kutafuta na kufanya ushirika na ndugu na dada, watu hawa hutatua dhana na mikanganyiko yote mioyoni mwao mmoja baada ya mwingine wakithibitisha kikamilifu kwamba ni Mungu anayeonekana na kufanya kazi, na kukubali. Hili ni wao kukubali kazi ya Mungu kupitia utafutaji na uchunguzi wao wenyewe. Kama aliyehubiri injili angeweza kushiriki ukweli waziwazi na kutatua dhana na maswali yao miaka mitatu iliyopita, wangeikubali miaka mitatu mapema zaidi. Ukuaji katika uzima ulicheleweshwa kwa kiasi gani katika miaka hii mitatu! Hili lazima litambulike kama uzembe wa kuwajibika kwa upande wa wale wanaohubiri injili na linahusiana kwa kina na wao kutoelewa ukweli. Baadhi ya wafanyakazi wa injili hawaweki umakini katika kujizatiti na ukweli, wakiwa tu na uwezo tu wa kusema mafundisho fulani bila kuweza kutatua mawazo ya watu au masuala halisi. Kwa sababu hiyo, watu wengi hawakubali injili kwa wakati unaofaa wanapoisikia, na hivyo kuchelewesha ukuaji wa maisha yao kwa miaka kadhaa. Lazima isemwe kwamba viongozi wanaosimamia kazi ya injili wana wajibu kwa hili kutokana na mwongozo wao hafifu na usimamizi usiotosha. Ikiwa viongozi na wafanyakazi kweli wanabeba mzigo na wanaweza kuvumilia mateso kidogo zaidi, kujifunza ushirika wa ukweli zaidi, na kuonyesha uaminifu zaidi, kushirikiana wazi katika nyanja zote za ukweli, ili wafanyakazi hao wa injili waweze kushiriki ukweli ili kutatua mawazo na mashaka ya watu, basi matokeo ya kuhubiri injili yatakuwa bora zaidi na zaidi. Hii ingewezesha watu wengi zaidi wanaochunguza njia ya kweli ya kukubali kazi ya Mungu mapema na kurudi mbele ya Mungu kupokea wokovu Wake mapema. Kazi ya kanisa inacheleweshwa kwa sababu tu viongozi wa uongo wamezembea katika uwajibikaji wa majukumu yao, hawafanyi kazi yao halisi wala kufuatilia na kusimamia kazi, na hawawezi kufanya ushirika juu ya ukweli ili kutatua matatizo. Bila shaka, pia ni kwa sababu viongozi hawa wa uongo hujishughulisha na faida za hadhi, hawatafuti ukweli hata kidogo, na hawataki kufuatilia, kusimamia, au kuelekeza kazi ya kueneza injili—na matokeo yake ni kwamba kazi inaendelea polepole, kukengeuka, upuuzi, na makosa ya uzembe yanayosababishwa na binadamu hushindwa kusuluhishwa au kutatuliwa haraka, hili huathiri vibaya ufanisi wa kueneza injili. Ni pale tu matatizo haya yanapogunduliwa na Aliye juu na viongozi na wafanyakazi kuambiwa lazima wayarekebishe ndipo matatizo haya yanarekebishwa. Kama vipofu, viongozi hawa wa uongo hawawezi kugundua matatizo yoyote, na hakuna kanuni zozote kamwe katika jinsi wanavyofanya mambo, na hata hivyo hawawezi kutambua makosa yao wenyewe, na wanakubali tu makosa yao wanapokatiliwa na Aliye juu. Kwa hivyo ni nani anayeweza kumudu kuchukua jukumu la hasara zilizosababishwa na viongozi hawa wa uongo? Hata kwa kuwaondoa kutoka kwenye nafasi zao, hasara walizosababisha zinawezaje kufidiwa? Kwa hivyo pale inapogunduliwa kwamba kuna viongozi wa uongo ambao hawawezi kufanya kazi yoyote halisi, wanapaswa kuachishwa kazi mara moja. Katika baadhi ya makanisa, kazi ya injili huendelea polepole sana, na haya ni matokeo ya viongozi wa uongo kutofanya kazi halisi tu, pamoja na visa vingi vya kupuuza na kufanya makosa kwa upande wao.
Katika vipengele vyote vya kazi ambavyo viongozi wa uongo hufanya, kwa kweli kuna masuala, mkengeuko, na dosari nyingi ambazo wanahitaji kutatua, kusuluhisha, na kurekebisha. Hata hivyo, kwa sababu viongozi hawa wa uongo hawana hisia ya mzigo, wakijiingiza tu katika faida za hadhi yao bila kufanya kazi yoyote halisi, wanaishia kuharibu kazi. Katika baadhi ya makanisa, watu hawajaungana katika mawazo yao, huku kila mtu akishuku, akijihadhari, na kudhoofishana, huku wakiogopa kuondolewa na nyumba ya Mungu. Wakikabiliwa na hali hizi, viongozi wa uongo hawafanyi juhudi za kuzitatua, wakishindwa kufanya kazi yoyote halisi, maalum. Kazi ya kanisa inasimama, lakini viongozi wa uongo hawakasirishwi na hili hata kidogo, bado wanaamini kwamba wamefanya kazi nyingi wenyewe na hawajachelewesha kazi ya kanisa. Viongozi hao wa uongo kimsingi hawawezi kufanya kazi ya kutoa uzima, wala hawawezi kutatua matatizo halisi kulingana na ukweli. Wanafanya tu kazi ndogo ya mambo ya jumla ambayo imepeanwa kwa namna maalum na kuainishwa na Aliye juu, kana kwamba kazi yao inafanywa kwa ajili ya Aliye juu pekee. Linapokuja suala la kazi ya msingi ya kanisa ambayo Aliye juu amekuwa akitoa sharti kila mara—kama vile kazi ya kutoa uzima na kazi ya kuwakuza watu—au kazi fulani maalum zinazoongozwa na Aliye juu, hawajui jinsi ya kuifanya na hawawezi kuifanya. Wanagawa kazi hizi kwa wengine na kisha wanafikiri kazi yao imekamilika. Wanafanya sawasawa na vile walivyoagizwa na Aliye juu, na wao huchukua hatua kidogo tu wanapochochewa; vinginevyo, wao si watendaji na wenye kufanya mambo kwa juujuu—hawa ni viongozi wa uongo. Kiongozi wa uongo ni nini? Kwa ufupi, ni mtu ambaye hafanyi kazi halisi, ambaye hafanyi kazi yake kama kiongozi, akionyesha kutowajibika kabisa katika kazi muhimu na ya msingi na kutochukua hatua yoyote—huyu ndiye kiongozi wa uongo. Viongozi wa uongo hujishughulisha tu na mambo ya jumla ya juu juu, wakikosea hili kwa kufanya kazi halisi, na kwa kweli, linapokuja suala la kazi yao kama kiongozi na kazi muhimu waliyopewa na nyumba ya Mungu, hawafanyi yoyote vizuri. Zaidi ya hayo, masuala mara nyingi hutokea ndani ya vipengele mbalimbali vya kazi ya kanisa vinavyohitaji azimio la kiongozi, lakini hawawezi kuyatatua, mara nyingi wanachukua mtazamo wa kuepuka, na ndugu hawawezi kuyapata wanapotaka kutatua suala. Wakifanikiwa kumpata kiongozi, kiongozi huwakwepa kwa kisingizio cha kuwa na shughuli nyingi na kazi na kuwaomba ndugu wasome maneno ya Mungu peke yao na kutafuta ukweli ili kutatua matatizo yao kwa kujitegemea, wakichukua mbinu ya kutofanya kazi kwa mikono yao wenyewe. Hii hatimaye husababisha mrundikano wa masuala mengi yasiyotatuliwa, kusimamisha maendeleo katika vipengele vyote vya kazi na kusimamisha kazi ya kanisa. Haya ni matokeo ya viongozi wa uongo kutofanya kazi halisi. Viongozi wa uongo kamwe si wenye ari au bidii kuhusu majukumu yao ya msingi, wala hawatafuti ukweli ili kutatua masuala mbalimbali. Hii ina maana kwamba viongozi wa uongo hawana uwezo wa kufanya kazi halisi na kutatua masuala yoyote. Kile ambacho viongozi wa uongo hufanya vizuri zaidi ni kuhubiri maneno na mafundisho, kuropokwa kauli mbiu, na kuwahimiza wengine, wakizingatia tu kujishughulisha na kazi za jumla. Kuhusu kazi ya msingi ya kanisa waliyokabidhiwa na nyumba ya Mungu, kama vile kukimu uzima na kushiriki ukweli ili kutatua masuala, hawajui jinsi ya kuyafanya, hawajifunzi jinsi ya kufanya hivyo, na hawawezi kutatua matatizo yoyote halisi—hawa ndio viongozi wa uongo.
Baadhi ya viongozi wa uongo, wanapoambiwa waelekeze kazi ya maandishi kama vile kuandika miswada, kuandika makala ya ushuhuda wa matukio, na kazi nyingine maalum, wanafikiri kwamba kwa vile ni maelekezo tu, hawahitajiki kufanya kazi thabiti, kwa hivyo badala yake wanazunguka huku na kule. “Zhang,” wanasema, “nakala yako inaendeleaje?” “Nakaribia kumaliza.” “Li, unapata ugumu wowote kuandika mswada huo?” “Ndiyo, je, unaweza kunisaidia kuutatua?” “Nyinyi nyote mjadiliane kati yenu. Mfanye maombi zaidi.” Hawa viongozi wa uongo hawakosi tu kuwaelekeza ndugu na dada, bali pia hawazingatii kutekeleza kazi zao vyema, wao daima huzurura na kuishi maisha ya mapumziko na starehe. Juu juu, inaonekana wanakagua kazi, lakini kwa kweli hawatatui matatizo yoyote—wao ni warasimu tu! Hao maofisa hodari katika baadhi ya nchi katika ulimwengu usioamini vilevile ni binadamu wapotovu, lakini hata ni wema zaidi ya hawa viongozi wa uongo, ambao hawana hisia za uwajibikaji ambazo maofisa hawa wanazo. Kwa mfano, baada ya mlipuko wa janga, nchi kote ulimwenguni zilianza kutekeleza hatua za kinga. Mwishowe, nchi nyingi kati ya hizi zilikubali kwamba jitihada za kinga za Taiwan zilikuwa zinazofaa, ikiashiria kwamba maofisa wa serikali wa Taiwan walitekeleza kazi zao za kupambana na janga kwa viwango vya juu sana na kwa utondoti mkubwa sana. Kwa nchi ya kilimwengu, kwa maofisa na wanasiasa miongoni mwa binadamu wapotovu, kutekeleza kazi kwa viwango vya juu sana na kwa utondoti hakika ni wa kusifiwa. Maofisa wengi wa Ulaya walikuwa tayari kuitembelea na kujifunza kutoka kwa Taiwan; kutokana na taswira hii maofisa wa serikali wa Taiwan walikuwa bora zaidi kuliko wa mataifa mengine. Kwa sababu tu, maofisa wao wengi waliweza kufanya kazi thabiti na kujitahidi kutimiza majukumu yao, inathibitisha kwamba hawa maofisa walitosheleza mahitaji. Baadhi ya viongozi na wafanyakazi kanisani daima huwa wazembe wanapofanya wajibu wao, na haijalishi wanavyopogolewa, hakuna ufanisi. Naona kwamba tabia ya hawa viongozi na wafanyakazi hata hailingani na ile ya maofisa wanaotoka katika ulimwengu usioamini ambao wanaweza kufanya kazi halisi. Wengi wao hudai kumwamini Mungu na kufuatilia ukweli, lakini kwa kweli, hawako tayari kulipa gharama. Kuna ukweli mwingi unaotolewa kwao, lakini huu ndio mtazamo wao kuhusu kufanya wajibu wao. Matokeo ni kwamba wote wanakuja kuwa viongozi wa uongo, ambao wanapungukiwa wakilinganishwa na maofisa bora wa serikali! Matakwa Yangu kwa watu kwa kweli si ya juu; Sihitaji kwamba waelewe ukweli mwingi au wawe na ubora wa tabia wa juu. Kiwango cha chini kinachostahili ni kutenda kwa dhamira na kutimiza majukumu yako. Iwapo hakuna lingine, basi angalau, unastahili kutimiza riziki yako na agizo ambalo Mungu amekupa; hilo linatosha. Lakini kazi ya Mungu imefanywa kufikia sasa, na, je, watu wengi wanaweza kutenda kwa dhamira? Ninaona kwamba baadhi ya maofisa katika nchi za kidemokrasia wanazungumza na kutenda kwa uaminifu. Hawatii chumvi au kuzungumza nadharia ndefu, hotuba zao hasa ni kali na za kweli, na wanaweza kushughulikia masuala mengi halisi. Kazi yao hakika ni nzuri kabisa, inatoa taswira kamili ya uadilifu na ubinadamu wao. Ukitazama wengi wa viongozi na wafanyakazi katika kanisa sasa hivi, katika kazi zao, wanafanya kwa namna isiyo ya dhati na ni wazembe, hawajatimiza matokeo mema zaidi, na kukamilisha kabisa majukumu yao. Baada ya wao kuwa viongozi, wanageuka kuwa maofisa wa dini, wanakuwa wafidhuli na kutoa amri, na kuwa warasimu. Wanazingatia tu kujiingiza katika faida za vyeo vyao na wanapenda kuona kila mtu akiwafuata kila mahali na kuzunguka mahali walipo. Kwa nadra wao hujishughulisha kwa kina na mashinani ya kanisa kutatua matatizo halisi. Mioyoni mwao, wanaenda mbali zaidi na zaidi kutoka kwa Mungu. Viongozi na wafanyakazi wa uongo wa aina hii hawabadilishiki kabisa! Nimefanya ushirika kuhusu ukweli kwa uangalifu sana, lakini hawa viongozi na wafanyakazi hawakubali, wanashikilia kwa ukaidi mawazo yasiyo sahihi na hawatikisiki. Mtazamo wao kuhusu wajibu wao daima ni wa uzembe na hawana nia kamwe ya kutubu. Ninaona kwamba watu hawa hawana dhamiri, hawana mantiki, hawana ubinadamu hata kidogo. Basi Ninatafakari: Je, bado ni muhimu kushiriki tena na tena kuhusu huu ukweli na watu wa aina hii? Je, Ninahitaji kufanya ushirika kuwa mahususi? Je, Ninahitaji kuvumilia mateso haya? Je, haya maneno yanapita kiasi? Baada ya kuwaza kiasi, Ninaamua bado lazima Niongee, kwa kuwa ingawa haya maneno hayana athari kwa wale bila dhamiri hata kidogo au mantiki, ni ya maana kwa wale ambao, ingawa ni wenye ubora wa chini wa tabia wanaweza kukubali ukweli na kufanya majukumu yao kwa kweli. Viongozi wa uongo hawafanyi kazi halisi na hawatimizi wajibu wao, lakini wale wanaofuata ukweli watajifunza mafunzo, wanakuja kuwa na msukumo na kutafuta njia ya kutia katika vitendo kutokana na haya maneno na masuala. Uingiaji katika uzima si rahisi sana; bila mtu wa kusaidia na kukukimu, bila kufafanua na kuainisha kila kipengele cha ukweli, watu ni dhaifu sana, mara kwa mara wakijipata katika hali ya kukosa msaada na kufadhaika, hali ya uhasi na kutoonyesha hisia. Kwa hivyo, mara nyingi, Ninapoona viongozi hawa wa uongo Ninapoteza hamu ya kushiriki nao. Hata hivyo Ninapowaza kuhusu mateso waliyovumilia na gharama waliyolipa kwa wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na wale wanaofanya wajibu wao kwa uaminifu, Ninabadili mawazo Yangu. Si kwa sababu nyingine yoyote kando na hii: Hata watu 30 hadi 50—au wakiwa wachache 8 au 10—wanaweza kujitoa na kuwa waaminifu kwa kufanya majukumu yao, na wako tayari kusikiliza na kunyenyekea, basi kuzungumza haya maneno ni kwa thamani. Singekuwa na motisha yoyote ndani Yangu kuongea na kushiriki na wale ambao hawana dhamiri na mantiki; kuzungumza na hawa watu kunachosha na ni bure. Wengi wenu hamfuatilii ukweli na hamlipi gharama katika wajibu wenu—hamhisi mzigo au uaminifu, mnafanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati, na mnafanya mambo kwa kusitasita kwa matumaini ya kupata baraka. Kusikiliza maneno haya hakika ni fadhila ambazo hamstahiki. Mnawatumia wale wanaofanya wajibu wao kwa kweli, ambao hulipa gharama kwa kweli, walio na uaminifu na wanaobeba mzigo, na ambao wako tayari kutend ukweli. Maneno haya yanawalenga watu hao, na mnapata fadhila isiostahiki kwa kuyasikiliza. Iwapo itatazamiwa kwa hii taswira—yaani, kwamba wengi wenu mna mtazamo wa kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati bila bidii yoyote katika wajibu wenu—basi ninyi hamstahili kusikia haya maneno. Je, mbona hamstahili? Kwa sababu hata mkiyasikia, yote ni kazi bure, haijalishi yanasemwa kiasi gani au jinsi yalivyo ya utondoti, ninyi mnayasikiliza tu kwa namna isiyo ya dhati, bila kuyatenda maneno haya haijalishi mnaelewa kiasi gani baada ya kuyasikiliza. Je, ni nani anayestahili kuzungumziwa haya maneno? Je, ni nani anayestahili kuyasikiliza? Wale tu walio tayari kulipa gharama, ambao wanaweza kujitumia kwa dhati, na ambao ni waaminifu katika wajibu wao na agizo lao ndio wanaostahili kuyasikiliza. Je, kwa nini Ninasema wanastahili kusikiliza? Kwa sababu mara tu wanapoelewa ukweli kidogo baada ya kusikiliza, wanaweza kuutia katika vitendo, na wanatenda yale wanayoelewa. Sio wenye kuponyoka na hawazembei; wanazingatia ukweli na matakwa ya Mungu kwa mtazamo wa ukweli na kutamani sana, wakiweza kupenda na kukubali ukweli. Hivyo, baada ya kusikiliza, haya maneno yana athari kwao na yanatimiza matokeo.
Februari 13, 2021