C. Maneno Juu ya Kufichua Mawazo, Uzushi na Uongo wa Kidini wa Wanadamu Wapotovu

135. Katika imani yako kwa Mungu, utamjuaje Mungu? Unapaswa kumjua Mungu kupitia maneno na kazi ya leo ya Mungu, bila upotovu au uwongo, na hata kabla jambo lolote lile ni sharti uijue kazi ya Mungu. Huu ndio msingi wa kumjua Mungu. Huo uwongo wa aina mbalimbali unaokosa ukubalifu wa maneno ya Mungu ni dhana za kidini, ni ukubalifu ambao ni potovu na wenye makosa. Ujuzi mkubwa zaidi wa watu mashuhuri wa kidini ni kuyachukua maneno ya Mungu yaliyokuwa yakikubalika zamani na kuyalinganisha na maneno ya Mungu ya leo. Unapomhudumia Mungu wa leo, ikiwa unashikilia vitu vilivyoangaziwa nuru na Roho Mtakatifu hapo zamani, basi huduma yako itasababisha hitilafu na vitendo vyako vitakuwa vimepitwa na wakati na havitakuwa tofauti na ibada ya kidini. Ikiwa unaamini kuwa wanaomhudumia Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wavumilivu…, na ukiweka ufahamu wa aina hii katika vitendo leo hii, basi vitendo kama hivi ni dhana ya kidini, na vitendo kama hivyo ni maigizo ya kinafiki. “Dhana za kidini” inarejelea vitu vilivyopitwa na wakati (kutia ndani ukubalifu wa maneno yaliyonenwa na Mungu zamani na kufichuliwa na Roho Mtakatifu), na vikiwekwa katika vitendo leo, basi vitahitilafiana na kazi ya Mungu na havitamfaidi mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kuyatakasa dhana za kidini yaliyomo ndani yake, basi yatakuwa kizuizi kizito katika kumuhudumia Mungu. Walio na dhana za kidini hawana njia ya kuendelea sawia na hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, watakuwa nyuma hatua moja, halafu mbili—kwani hizi dhana za kidini humfanya mwanadamu kuwa mtu wa kujitukuza na mwenye kiburi. Mungu hahisi kumbukumbu kwa ajili ya Alichokinena na kukifanya hapo zamani; kama kimepitwa na wakati, basi Anakiondoa. Hakika unaweza kuziacha dhana zako? Ukiyakatalia maneno aliyoyanena Mungu hapo zamani, je hili linadhihirisha kuwa unaijua kazi ya Mungu? Kama huwezi kukubali mwangaza wa Roho Mtakatifu leo na badala yake unashikilia mwangaza wa zamani, hili laweza kuthibitisha kuwa unafuata nyayo za Mungu? Je, bado huwezi kuziacha dhana za kidini? Ikiwa ndivyo ilivyo, basi utakuwa mpinga Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

136. Kwa sababu kazi ya Mungu mara zote huwa na masuala mapya, kuna kazi ambayo inakuwa iliyopitwa na wakati na nzee kazi mpya inapoibuka. Hizi aina tofauti tofauti za kazi, nzee na mpya, hazikinzani, bali zinatoshelezana, kila hatua ikifuata iliyotangulia. Kwa kuwa kuna kazi mpya, mambo ya zamani, kwa hakika, ni sharti yaondolewe. Kwa mfano, baadhi ya vitendo vilivyokita mizizi na misemo ya mwanadamu iliyozoeleka, kuongeza juu miaka mingi ya mazoea na mafundisho ya mwanadamu, ilimuumbia mwanadamu kila aina ya dhana. Maelezo ya mwanadamu kuhusu dhana kama hizi ni kwamba bado Mungu hajafichua uso Wake halisi na tabia Yake asili kwa mwanadamu, pamoja na kuenea kwa nadharia za kale kwa miaka mingi yamekuwa ya kupendelea uundaji wa mwanadamu wa fikira kama hizo. Inaweza kusewa kwamba, katika kipindi cha imani ya mwanadamu kwa Mungu, ushawishi wa fikira mbalimbali umesababisha kutengenezwa na kubadilika kwa ufahamu wote wa fikira kumhusu Mungu ndani ya watu, jambo ambalo limewafanya watu wengi wa kidini wanaomtumikia Mungu wageuke kuwa adui Zake. Hivyo, kadiri fikira za watu za kidini zinavyokuwa thabiti, ndivyo wanavyozidi kumpinga Mungu, na ndivyo wanavyozidi kuwa maadui wa Mungu. Kazi ya Mungu daima huwa mpya, si kongwe na huwa haitengenezi mafundisho ya kidini na badala yake inabadilika kila mara na kuwa mpya kwa kiwango fulani. Kazi hii ni onyesho la tabia ya asili ya Mungu Mwenyewe. Vilevile ni kanuni ya asili ya kazi ya Mungu na mojawapo ya njia ambazo Mungu hutimiza usimamizi Wake. Iwapo Mungu asingefanya kazi kwa njia hii, mwanadamu asingebadilika au kuweza kumfahamu Mungu, na Shetani asingeshindwa. Hivyo basi, kila mara katika kazi Yake, kunatokea mabadiliko ambayo yanaonekana hayatabiriki, ila ambayo, kwa hakika, yana kipindi chake. Njia mwanadamu anavyomwamini Mungu hata hivyo ni tofauti. Anashikilia mifumo ya zamani ya kidini na kadiri yalivyo ya zamani, ndivyo yanavyokuwa ya kupendeza kwake. Akili ya kipumbavu ya mwanadamu, akili isiyobadilika kama mawe inawezaje kukubali kazi nyingi isiyoeleweka mpya na maneno ya Mungu? Mwanadamu anamchukia Mungu ambaye ni mpya kila siku na si wa zamani; anampenda tu Mungu wa zamani, ambaye ni mzee kwa umri, aliyejaa mvi na Asiyekwama papo hapo. Hivyo, kwa sababu Mungu na mwanadamu kila mmoja analo alipendalo, mwanadamu amekuwa adui wa Mungu. Kwa kiwango kikubwa, huu utata upo hata leo, wakati ambao Mungu amekuwa akifanya kazi mpya kwa takribani miaka 6000. Hawawezi kusaidika. Labda ni kwa sababu ya usumbufu wa mwanadamu, au kutokiukwa kwa kazi ya Mungu—ila hawa wahubiri bado wanashikilia vitabu vizee na karatasi ilhali Mungu anaendelea na kazi Yake ambayo haijakamilika ya usimamizi kana kwamba hana msaidizi. Japo huu utata unaleta uadui kati ya mwanadamu na Mungu, kiasi kwamba hawapatanishiki, Mungu haujali ukinzani huu. Hata hivyo mwanadamu bado anashikilia imani na dhana zake, na kamwe haiachilii. Ila kitu kimoja kiko wazi: Japo mwanadamu haachi misimamo yake, Mungu mara zote anapiga hatua na kubadilisha misimamo Yake kulingana na muktadha na hatimaye ni mwanadamu atakayeshindwa bila mapambano. Mungu ndiye adui mkubwa zaidi wa maadui wake walioshindwa na vilevile ni bingwa wa wale miongoni mwa wanadamu ambao wameshindwa na wale ambao bado hawajashindwa. Ni nani anaweza kushindana na Mungu na ashinde? Dhana za mwanadamu zinaonekana kutoka kwa Mungu kwani wengi wao walizaliwa kipindi cha kazi ya Mungu. Na bado Mungu hamsamehei mwanadamu kwa sababu ya hili na hata zaidi Hammiminii sifa mwanadamu kwa “kumzalishia Mungu” mazao baada ya mazao ambayo yamo nje ya kazi ya Mungu. Badala yake, Yeye hughadhabishwa sana na fikira na imani za zamani za uungu, za mwanadamu na hata hachukui hatua kufikira tarehe ambayo hizi fikira zilitokea mara ya kwanza. Hakubali kamwe kwamba hizi dhana zinaletwa na kazi Yake kwani dhana za mwanadamu husambazwa na mwanadamu; chanzo chao ni fikira na akili za mwanadamu, na si Mungu, ila ni Shetani. Madhumuni ya Mungu mara zote ni kuona kazi Yake ikiwa mpya na hai, si kongwe na iliyokufa, na kile Anachotaka mwanadamu ashikilie kwa nguvu kinabadilika kulingana na enzi na kipindi, na si cha kudumu milele na kisichobadilika. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye husababisha mwanadamu kuishi na kuwa mpya, tofauti na ibilisi anayemsababishia mwanadamu kufa na kuwa mzee. Je, bado hamlielewi hili? Una dhana kuhusu Mungu na umeshindwa kuziacha kwa kuwa hutafakari. Si kwa sababu kuna maana kidogo sana ndani ya kazi ya Mungu, wala kwa sababu kazi ya Mungu inatofautiana na matakwa ya binadamu, wala kwamba Mungu mara zote ni “mzembe katika wajibu Wake.” Huwezi kuacha dhana zako kwa kuwa umepungukiwa na utiifu, na huna sifa hata kidogo za kiumbe wa Mungu, na si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu. Yote haya umejisababishia na hayana uhusiano na Mungu; mateso na misukosuko yote husababishwa na mwanadamu. Dhamira za Mungu mara zote huwa nzuri: hakusudii kukufanya uzitoe dhana, ila angependa ubadilike na uwe mpya kadiri enzi zinavyopita. Ila bado huwezi kutofautisha chokaa na jibini na kila mara ama unachunguza au unachanganua. Si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu, ila ni kuwa humheshimu Mungu na uasi wako umezidi. Kiumbe mdogo anathubutu kuchukua sehemu ndogo ya kile alichopewa mwanzo na Mungu, na kisha kubadilika na kukitumia kumvamia Mungu—je, huu si uasi wa mwanadamu? Ni haki kusema kuwa binadamu hawana sifa kabisa za kutoa maoni yao mbele za Mungu, na sembuse hawana sifa za kuonyesha hadharani maneno yao yasiyo na thamani, yanukayo, yaliyooza wapendavyo—bila kutaja chochote kuhusu hizo fikira zilizooza. Haina maana?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

137. Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, dhamira ya Mungu milele itaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

138. Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa “kumfuata Mwanakondoo popote Aendapo.” Hawa tu ndio watu wanaotafuta njia ya kweli, na wao tu ndio wanaoifahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaofuata tu kanuni na mafundisho ya dini kiutumwa ni wale ambao wameondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa na uhakika juu ya hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? Wakristo ulimwenguni kote ambao hawajazingatia kazi mpya ya sasa wote wameshikilia imani kwamba wao ni wenye bahati na kwamba Mungu atawatimizia kila mojawapo ya malengo yao. Lakini hawawezi kueleza mbona Mungu atawapeleka katika mbingu ya tatu na wala hawafahamu jinsi Yesu atakavyokuja juu ya wingu jeupe na kuwachukua, wala kusema kwa uhakika kamili kama kweli Yesu atawasili akiwa juu ya wingu jeupe siku ambayo wanaiwaza. Wote wana wasiwasi, na kukanganywa; wao wenyewe hata hawafahamu kama Mungu atachukua kila mmoja wao, watu wachache sana, wanaotoka katika madhehebu yote. Kazi ambayo Mungu anafanya kwa sasa, enzi ya sasa, mapenzi ya Mungu—ni vitu ambavyo watu hawavifahamu, na hawana cha kufanya bali kusubiri na kuhesabu siku katika vidole vyao. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho, huku wale “watu werevu,” ambao hawawezi kumfuata hadi mwisho ilhali wanaamini wamepata yote, ndio wasiokuwa na uwezo wa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Wote huamini wao ndio werevu zaidi duniani, na wanasitisha maendeleo ya kazi ya Mungu bila sababu yoyote kabisa, na huonekana kuamini pasi na shaka kwamba Mungu atawachukua mbinguni, wao “wenye uaminifu wa juu zaidi kwa Mungu, humfuata Mungu, na hutii neno la Mungu”. Hata ingawa wana “uaminifu wa hali ya juu” kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao? Wengi hata wanaamini kuwa wale wanaokana sheria ya zamani na kukubali kazi mpya hawana dhamiri. Watu hawa, ambao huongea tu kuhusu “dhamiri,” na hawajui kazi ya Roho Mtakatifu, hatimaye watapata kuwa matarajio yao yamekatizwa na dhamiri yao yenyewe. Kazi ya Mungu haizingatii mafundisho, na ingawa ni kazi Yake Mwenyewe, bado Mungu haishikilii. Kile kinachopaswa kukataliwa kinakataliwa, kile kinachopaswa kuondolewa kinaondolewa. Lakini mwanadamu anajiweka kwenye uadui wa Mungu kwa kushikilia sehemu moja ndogo ya kazi ya usimamizi wa Mungu. Si huu ndio upuuzi wa mwanadamu? Si huu ndio ujinga wa mwanadamu? Kadri watu wanakuwa waoga na wenye tahadhari sana kwa sababu wanachelea kutopata baraka za Mungu, ndivyo wanavyopungukiwa zaidi na uwezo wa kupata baraka zaidi, na wa kupata ile baraka ya mwisho. Watu wale wanaoshikilia kiutumwa sheria huwa wanadhihirisha uaminifu wa hali ya juu kwa sheria, na kadri wanavyodhihirisha uaminifu jinsi hiyo kwa sheria, ndivyo wanavyokuwa waasi wanaompinga Mungu. Kwa kuwa sasa ni Enzi ya Ufalme na wala si Enzi ya Sheria, na kazi ya leo na kazi ya zamani haziwezi kulinganishwa, wala kazi ya zamani haiwezi kulinganishwa na kazi ya sasa. Kazi ya Mungu imebadilika, na vitendo vya mwanadamu pia vimebadilika; si kushikilia sheria au kuubeba msalaba. Basi, uaminifu wa watu kwa sheria na msalaba hautapata kibali cha Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

139. Watu, ambao wamepotoshwa, wote huishi katika mtego wa Shetani, wao kuishi katika mwili, kuishi katika tamaa za ubinafsi, na hakuna hata mmoja kati yao anayelingana na Mimi. Kuna wale ambao wanasema kwamba wao wanalingana na Mimi, lakini ambao wote huabudu sanamu zisizo yakini. Ingawa wanakubali jina Langu kama takatifu, wao hutembea kwenye njia ambazo huenda kinyume na Yangu, na maneno yao yamejaa kiburi na kujiamini, kwa sababu, katika mizizi, wote wananipinga na hawalingani Nami. Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu “vinavyofaa” hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo? Mafarisayo Wayahudi walitumia sheria ya Musa kumhukumu Yesu. Hawakutafuta uwiano na Yesu wa wakati huo, bali waliifuata sheria kwa makini, kwa kiasi kwamba wao hatimaye walimpiga misumari Yesu asiye na hatia juu ya msalaba, baada ya kumshitaki Yeye kwa kukosa kufuata sheria za Agano la Kale na kutokuwa Masihi. Kiini chao kilikuwa ni nini? Haikuwa kwamba hawakutafuta njia ya uwiano na ukweli? Walitamani na kutilia maanani mawazo yao na kila neno la Maandiko, bila kuyajali mapenzi Yangu na hatua na mbinu za kazi Yangu. Hawakuwa watu waliotafuta ukweli, ila walikuwa watu walioshikilia maneno kwa ugumu; hawakuwa watu walioamini katika Mungu, bali walikuwa watu walioamini katika Biblia. Kimsingi, walikuwa walinzi wa Biblia. Ili kulinda maslahi ya Biblia, na kuzingatia hadhi ya Biblia, na kulinda sifa za Biblia, wao walitenda kiasi kwamba walimsulubisha Yesu mwenye huruma msalabani. Haya walifanya tu kwa ajili ya kuitetea Biblia, na kwa ajili ya kudumisha hali ya kila neno la Biblia katika mioyo ya watu. Hivyo waliona ni heri kuyaacha maisha yao ya baadaye na sadaka ya dhambi kwa sababu ya kumhukumu Yesu, ambaye hakuwa Anazingatia kanuni za Maandiko, mpaka kifo. Je hawakuwa watumishi kwa kila mojawapo ya maneno ya Maandiko?

Na je watu leo? Kristo amekuja kutoa ukweli, lakini wanaona ni afadhali wao kumfukuza Yeye kutoka kati ya wanadamu ili wapate kuingia mbinguni na kupokea neema. Wanaona ni afadhali kabisa kukataa kuja kwa ukweli, ili kulinda maslahi ya Biblia, na ni afadhali kumtundika Kristo ambaye Alirudi kwa mwili kwa misumari msalabani tena ili kuhakikisha kuwepo kwa Biblia milele. Jinsi gani mwanadamu anaweza kupokea wokovu Wangu, wakati moyo wake una nia mbaya namna hiyo, na asili yake inanipinga Mimi? Mimi huishi miongoni mwa wanadamu, ilhali bado wanadamu hawajui kuhusu kuwepo Kwangu. Ninapoangaza mwanga Wangu juu ya wanadamu, bado yeye hana ufahamu kuhusu kuwepo Kwangu. Wakati Ninatoa ghadhabu Yangu juu ya wanadamu, wao hukanusha kuwepo Kwangu kwa nguvu kubwa zaidi. Binadamu hutafuta uwiano na maneno, na Biblia, ilhali bado hakuna mwanadamu hata mmoja huja Kwangu kutafuta njia ya uwiano na ukweli. Binadamu huniheshimu sana Nikiwa mbinguni, na kujishughulisha hasa na kuwepo Kwangu mbinguni, ilhali hakuna anayenijali Nikiwa katika mwili, kwa maana Mimi Ninayeishi miongoni mwa wanadamu sina umuhimu kwao hata kidogo. Wale ambao hutafuta tu uwiano na maneno ya Biblia, na ambao hutafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, mbele Yangu ni fidhuli. Hiyo ni kwa sababu wanachokiabudu ni maneno yaliyokufa, na Mungu Aliye na uwezo wa kuwapa hazina isiyoambilika. Wanachoabudu ni Mungu anayedhibitiwa na mtu, na ambaye hayuko. Ni nini, basi, ambacho watu wa namna hiyo wanaweza kupokea kutoka Kwangu? Mwanadamu ni kiumbe duni sana kiasi kwamba maneno hayawezi kueleza hali yake. Wale wanaonipinga, wanaofanya madai yasiyo na kipimo dhidi Yangu, wasio na upendo kwa ukweli, wanaoniasi—wangewezaje kulingana na Mimi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo

140. Mkitumia fikira zenu wenyewe kumpima na kumwekea Mungu mipaka, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiyobadilika, na mkimwekea Mungu mipaka kabisa katika vigezo vya Biblia na kumweka katika mawanda ya kazi yenye mipaka, basi hii inathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu Wayahudi katika Agano la Kale walimchukulia Mungu kuwa sanamu yenye umbo lisilobadilika waliloshikilia mioyoni mwao, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yeye aliyeitwa Masihi pekee ndiye Angeweza kuwa Mungu, na kwa sababu binadamu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—hivyo Yesu asiye na hatia Alihukumiwa kifo. Mungu hakuwa na kosa lolote, mwanadamu alikataa kumsamehe, naye alisisitiza kumhukumu afe na basi Yesu akasulubishwa. Kila wakati mwanadamu huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kwa msingi wa kitabu kimoja tu, Biblia, kana kwamba mwanadamu ana ufahamu wa kina kuhusu usimamizi wa Mungu, kana kwamba mwanadamu anavyo vitu vyote atendavyo Mungu katika kiganja cha mkono wake. Wanadamu ni wapumbavu kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha kutia chumvi sana wanapoelezea jambo. Bila kujali jinsi kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu kilivyo, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba wewe ni mtu ambaye humpinga Mungu zaidi, na kwamba umemshutumu Mungu, kwa sababu huna uwezo kabisa wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kamilifu na Mungu. Kwa nini Mungu hatosheki kamwe na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu, kwa sababu ana fikira nyingi sana, na kwa sababu maarifa yake kuhusu Mungu hayaafikiani na uhalisi hata kidogo, lakini badala yake hurudia tu mada ile ile bila mabadiliko na hutumia mwelekeo ule ule katika kila hali. Na hiyo, kwa kuwa Amekuja duniani leo, Mungu anasulubishwa kwa mara nyingine na mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Waovu Hakika Wataadhibiwa

141. Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani aweze kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamemtamani sana na kumwonea shauku kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, kwa Yesu Mwokozi kuwarudia watu ambao Amekuwa mbali nao kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumai kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atazisamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Anatamani Yesu Mwokozi awe jinsi Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi ambaye anapendeka, mwema na wa heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kuume wa Aliye Juu. Mwanadamu anawaza kuwa vilevile, Yesu atashuka tena juu ya wingu jeupe (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kwamba Atachukua mfano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atawapa chakula, na kusababisha maji ya uzima kumwagika kwa ajili yao, naye Ataishi miongoni mwa wanadamu, akiwa Amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na halisi. Na kadhalika. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya hivi; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alidhania. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, naye hakutokea kwa wanadamu wote akiwa Amepanda juu ya wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, naye anasalia kuwa mjinga kumhusu. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa Ameshuka tayari juu ya “wingu jeupe” (wingu ambalo ni Roho Wake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote Aliyo), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu jambo hili: Ingawa Mwokozi Yesu mtakatifu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Angewezaje kufanya kazi katika “mahekalu” yaliyomilikiwa na uchafu na pepo wachafu? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Angewezaje kuwaonekania wale wanaokula mwili wa wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi amejawa na upendo na huruma, naye ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, uadhama, ghadhabu, na hukumu, na Aliye na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hiyo ingawa mwanadamu anazamia kwa hamu na kuonea shauku kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa kwa maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

142. Iwapo, kama mwanadamu anavyofikiria, Yesu Atakuja, akiwa anaitwa Yesu wakati wa siku za mwisho, na bado juu ya wingu jeupe, akishuka miongoni mwa wanadamu kwa mfano wa Yesu: huko hakutakuwa kurudia kazi yake? Je, si Roho Mtakatifu Atakuwa Ameshikamana na ya kale? Yote yale ambayo mwanadamu anaamini ni mawazo, na yote ambayo mwanadamu anakubali ni kulingana na maana halisi, na ni kwa mujibu wa mawazo yale; yanakinzana na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na hayafuatani na nia ya Mungu. Mungu pia hawezi kufanya hivyo; Mungu si mpumbavu na mjinga kiasi hicho, na kazi Yake si rahisi kama unavyofikiria. Kwa kutegemeza mambo yote yanayofikiriwa na mwanadamu, Yesu Atarejea juu ya wingu na Atateremka kati yenu. Mtamwona Yeye ambaye, akiwa amepaa juu ya wingu, atawaambia kwamba yeye ni Yesu. Nanyi pia mtatazama alama za misumari katika mikono yake, na mtamjua Yeye ni Yesu. Naye ndiye Atakayewaokoa tena, na Atakuwa Mungu wenu Mwenye nguvu. Yeye ndiye Atakayewaokoa, na kuwakabidhi ninyi jina jipya, na kumpa kila mtu jiwe jeupe, ambapo baadaye mtakubaliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni na kulakiwa kwenye paradiso. Je, imani kama hizo si fikira za mwanadamu? Je, Mungu hufanya kazi kulingana na fikira za mwanadamu, au, je, Yeye hufanya kazi kinyume cha fikira za mwanadamu? Je, si fikira zote za mwanadamu zatoka kwa Shetani? Je, mwanadamu hajapotoshwa na Shetani? Kama Mungu Alifanya kazi yake kulingana na fikira ya mwanadamu, je, si Mungu Angekuwa Shetani? Je, si Angekuwa wa aina sawa na viumbe Wake wenyewe? Kwa kuwa viumbe Wake wamepotoshwa na Shetani hadi mwanadamu amekuwa mfano halisi ya Shetani, kama Mungu Angefanya kazi kwa mujibu wa vitu vya Shetani, si angekuwa katika ligi ya Shetani. Mwanadamu anawezaje kupima kina cha kazi ya Mungu? Na kwa hivyo, Mungu hafanyi kazi kwa mujibu wa fikira ya mwanadamu, na hangefanya kazi kwa njia unazofikiria. Kuna wale ambao husema kwamba Mungu mwenyewe Alisema kuwa Atawasili kwa wingu. Ni ukweli kuwa Mungu mwenyewe Alisema hivyo, lakini, je, hujui kuwa siri za Mungu haziwezi kueleweka na mwanadamu? Je, unajua kuwa maneno ya Mungu hayawezi kuelezwa na mwanadamu? Na wewe una hakika, bila tashwishi yoyote, kuwa ulipewa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu Aliyekuonyesha moja kwa moja kwa namna hii? Je, haya ni maelekezo ya Roho Mtakatifu, au ni fikira zako? Ulisema, “Haya yalisemwa na Mungu mwenyewe.” Lakini hatuwezi kutumia fikira zetu na akili zetu kupima maneno ya Mungu. Na kuhusu maneno ya Isaya, je, unaweza kueleza maneno yake kwa kujiamini kikamilifu? Je, wewe unathubutu kueleza maneno yake? Kwa sababu huthubutu kueleza maneno ya Isaya, mbona unathubutu kueleza maneno ya Yesu? Nani ameinuliwa kuliko mwingine, Yesu au Isaya? Kwa vile jibu ni Yesu, kwa nini unaeleza maneno yaliyosemwa na Yesu? Je, Mungu Angeweza kukwambia kuhusu kazi yake mapema? Hakuna kiumbe kinachoweza kufahamu, wala hata wajumbe walio mbinguni, wala hata Mwana wa Adamu, kwa hivyo wewe ungejuaje?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

143. Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

144. Uaminifu wenu uko kwa maneno pekee, maarifa yenu ni ya kiakili tu na ya dhana, kazi yenu ni kwa sababu ya kupata baraka za mbinguni, na kwa hivyo imani yenu inafaa kuwa vipi? Hata leo, bado mnapuuza kila neno la ukweli. Hamjui Mungu ni nini, hamjui Kristo ni nini, hamjui jinsi ya kumcha Yehova, hamjui jinsi ya kuingia katika kazi ya Roho Mtakatifu, na hamjui jinsi ya kutofautisha kati ya kazi ya Mungu Mwenyewe na uongo wa mwanadamu. Unajua tu kukashifu neno lolote la ukweli linaloelezwa na Mungu lisilolingana na mawazo yako. Unyenyekevu wako uko wapi? Utiifu wako uko wapi? Uaminifu wako uko wapi? Tamaa yako ya kupata ukweli iko wapi? Uchaji Mungu wako uko wapi? Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Atawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua mambo bila kuzingatia suala zima; kilicho zaidi, msiwe wenye kuchukulia mambo bila uzito na wenye msiofikiria katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kucha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anastahili kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

145. Hujaamini katika Mungu kwa muda mrefu, ilhali una mawazo mengi kuhusu Mungu, kiasi kwamba unathubutu kutofikiri hata kwa sekunde moja kuwa Mungu wa Waisraeli Anaweza kuwatunukia na uwepo wake. Wala hamthubutu kufikiri jinsi mnavyoweza kumwona Mungu Akijitokeza binafsi, ikitiliwa maanani jinsi mlivyo wachafu. Aidha hamjawahi kufikiri jinsi Mungu anavyoweza kushuka miongoni mwa Mataifa. Anapaswa kushuka juu ya Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa Waisraeli. Je, si watu wa Mataifa (yaani watu wa nje ya Israeli) ndio walengwa wa chuki Yake? Anawezaje kufanya kazi miongoni mwao? Haya yote ni mawazo yaliyokita mizizi ndani yenu ambayo mmeyakuza kwa miaka mingi. Kusudi la kuwashinda leo ni kuyaharibu haya mawazo yenu. Kwa njia hiyo mmeweza kumwona Mungu akijionyesha Mwenyewe miongoni mwenu—si katika Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni, bali miongoni mwa watu ambao Hajawahi kuwaongoza hapo awali. Baada ya Mungu kufanyia hatua mbili za kazi Yake Israeli, Waisraeli na watu wa Mataifa walishikilia wazo hili: Japo ni kweli Mungu aliumba viumbe wote, yuko radhi kuwa Mungu wa Waisraeli tu, si Mungu wa Mataifa. Waisraeli wanaamini yafuatayo: Mungu anaweza tu kuwa Mungu wetu, sio Mungu wenu Mataifa, na kwa sababu humchi Yehova, Yehova—Mungu wetu—Anawachukia. Zaidi, Wayahudi hao huamini hili: Bwana Yesu alichukua sura yetu Wayahudi na ni Mungu aliye na alama ya Wayahudi. Mungu anafanyia kazi miongoni mwetu. Sura ya Mungu na sura zetu zinafanana; sura zetu na sura ya Mungu zinakaribiana. Bwana Yesu ni Mfalme wetu Wayahudi; watu wa Mataifa hawajawezeshwa kupokea wokovu mkubwa kiasi hicho. Bwana Yesu ni sadaka ya dhambi kwetu Wayahudi. Ni kwa misingi ya hatua hizi mbili za kazi ndipo Waisraeli na Wayahudi walijijengea haya mawazo mengi. Wanamdai Mungu kuwa wao tu, bila kukubali kwamba Mungu vilevile ni Mungu wa Mataifa. Kwa njia hii, Mungu alikuwa pengo katika mioyo ya watu wa Mataifa. Hii ni kwa sababu kila mtu aliamini kuwa Mungu hataki kuwa Mungu wa watu wa Mataifa na kuwa Anawapenda tu Waisraeli—Wateule wake—na Anawapenda Wayahudi hasa wafuasi waliomfuata. Je, wajua kuwa kazi aliyoifanya Yehova na Yesu ilikuwa ni kwa ajili ya uzima wa wanadamu wote? Je, sasa unatambua kuwa Mungu ni wa wale wote waliozaliwa nje ya Israeli? Je, Mungu Hayumo miongoni mwenu leo? Hii haiwezi kuwa ndoto, ama vipi? Je, hamkubali uhalisi huu? Mnathubutu kutoamini au kulifikiria. Licha ya jinsi mnavyolitazama, je, Mungu hayumo miongoni mwenu? Je, bado mnaogopa kuyaamini maneno haya? Kuanzia leo, je, wote walioshindwa, na wale wote wanaotaka kuwa wafuasi wa Mungu, si wateule wa Mungu? Je, nyote mlio wafuasi leo, si wateule nje ya Israeli? Je, nafasi yenu si sawa na ya Waisraeli? Je, hili silo mnalopaswa kutambua? Je, hili si lengo la kazi ya kukushinda? Kwa kuwa mwaweza kumwona Mungu, basi Atakuwa Mungu wenu milele, tangu mwanzo hadi siku za baadaye. Hatawaacha, mradi tu nyinyi nyote mko radhi Kumfuata na kuwa viumbe Wake waaminifu na watiifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)

146. Ni katika kuweka dhana zako za kale kando tu ndipo utakapoweza kupata maarifa mapya, ilhali maarifa ya zamani si lazima yawe dhana za zamani. “Dhana” inamaanisha vitu vinavyodhaniwa na mwanadamu ambavyo viko mbali na uhalisi. Kama maarifa ya zamani yalikuwa yamepitwa na wakati katika enzi ya kale, na yalimzuia mwanadamu kuingia katika kazi mpya, basi maarifa kama yale pia ni dhana. Ikiwa mwanadamu ataweza kuchukua mwelekeo mzuri kwa maarifa kama yale, na anaweza pata kumjua Mungu kutoka kwa vipengele tofauti, kuunganisha ya zamani na mapya, basi maarifa ya kale yatamsaidia mwanadamu, na yatakuwa msingi wa mwanadamu kuingia katika enzi mpya. Funzo la kumjua Mungu linahitaji kwamba uwe stadi wa kanuni nyingi: jinsi ya kuingia kwenye njia ya kumjua Mungu, ukweli gani unapaswa kuelewa ili kumjua Mungu, na jinsi ya kuondoa dhana zako na asili yako ya kale ili kwamba uweze kutii mipango yote ya kazi mpya ya Mungu. Ukitumia kanuni hizi kama msingi wa kuingia kwenye somo la kumjua Mungu, basi maarifa yako yatakuwa na kina zaidi na zaidi. Kama una maarifa wazi ya hatua tatu za kazi—ambayo ni kusema kwamba, ya mpango mzima wa usimamizi wa Mungu—na ikiwa utaweza kupatanisha hatua mbili za awali na hatua ya sasa, na unaweza kuona kwamba ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja, basi utakuwa na msingi imara zaidi. … Ikiwa mwanadamu anaweza kuona katika hatua tatu za kazi kuwa zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe wakati tofauti, katika maeneo tofauti, na kwa watu tofauti; ikiwa mwanadamu anaweza kuona kuwa ingawa kazi ni tofauti, yote imefanywa na Mungu mmoja, na kwa kuwa ni kazi ambayo imefanywa na Mungu mmoja, basi lazima iwe sawa, na bila dosari, na kwamba ingawa hailingani na dhana za mwanadamu, hakuna kupinga kuwa ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja—ikiwa mwanadamu anaweza kusema kwa hakika kuwa ni kazi ya Mungu mmoja, basi dhana zake zitakuwa duni, na ambazo hazifai kutajwa. Kwa sababu maono ya mwanadamu hayako wazi, na mwanadamu anamjua tu Yehova kama Mungu, na Yesu kama Bwana, na ana mitazamo miwili kumhusu Mungu mwenye mwili wa leo, watu wengi wamejitoa kwa ajili ya kazi ya Yehova na Yesu, na wamezingirwa na dhana kuhusu kazi ya leo, watu wengi daima huwa na shaka na hawachukulii kazi ya leo kwa makini. Mwanadamu hana uelewa kuhusu hatua mbili za mwisho, ambazo hazikuonekana. Hio ni kwa sababu mwanadamu haelewi uhalisi wa hatua mbili za mwisho za kazi, na wala hakuzishuhudia binafsi. Ni kwa sababu haziwezi kuonekana ndiyo mwanadamu anawaza jinsi anavyopenda; bila kujali atakayodhania, hakuna ukweli wa kudhibitisha, na yeyote wa kurekebisha. Mwanadamu anaruhusu silika yake ya asili itawale, huku akikosa kujali na kuachilia mawazo yake yaende popote, kwa kuwa hakuna ukweli wa kudhibitisha, na kwa hivyo dhana za mwanadamu zinakuwa “ukweli,” bila kujali kama zina dhibitisho. Kwa hivyo mwanadamu anaamini Mungu wake aliyemuwazia akilini mwake, na hamtafuti Mungu wa uhalisi. Ikiwa mtu mmoja ana aina moja ya imani, basi kati ya watu mia moja kuna aina mia moja za imani. Mwanadamu ana imani kama hizi kwa maana hajaona uhalisi wa kazi ya Mungu, kwa sababu amesikia tu kwa masikio yake na hajaona kwa macho yake. Mwanadamu amesikia hekaya na hadithi—lakini amesikia kwa nadra kuhusu maarifa ya ukweli ya kazi ya Mungu. Hivyo ni katika dhana zao ndivyo watu ambao wamekuwa waumini kwa mwaka mmoja tu wanaamini Mungu, na hilo ni kweli pia kwa wale ambao wamemwamini Mungu katika maisha yao yote. Wale ambao hawawezi kuona ukweli daima hawawezi kuepuka imani ambayo wana dhana kwazo kumhusu Mungu. Mwanadamu anaamini kuwa amejiweka huru kutokana na vifungo vya dhana zake za kale, na ameingia eneo jipya. Je, mwanadamu hajui kuwa maarifa ya wale wasioweza kuona uso wa kweli wa Mungu kuwa ni dhana na tetesi? Mwanadamu anafikiria kuwa dhana zake ni sawa, na wala hayana kasoro, na hufikiri kuwa hizi dhana zimetoka kwa Mungu. Leo, mwanadamu anaposhuhudia kazi ya Mungu, anaachilia dhana zilizokuwa zimeongezeka kwa miaka mingi. Mawazo na dhana za awali zilikuwa vizuizi vya kazi ya hatua hii, na inakuwa vigumu kwa mwanadamu kuachana na dhana kama hizo na kupinga mawazo kama yale. Dhana kuhusu kazi hii ya hatua kwa hatua ya wengi wa wale wanaomfuata Mungu hadi leo zimekuwa za kuhuzunisha na watu hawa pole pole wamefanya uadui wa kikaidi na Mungu mwenye mwili hatua kwa hatua, na chanzo cha chuki ni mawazo na dhana za mwanadamu. Ni hasa kwa sababu ukweli haumruhusu mwanadamu kuwa na uhuru wa hiari ya mawazo yake, na, zaidi ya hayo, hauwezi kupingwa na mwanadamu kwa urahisi, na mawazo na dhana za mwanadamu hazistahimili uwepo wa ukweli, na hata zaidi ya hayo, kwa sababu mwanadamu hawezi kufikiria kuhusu usahihi na unyofu wa ukweli, na kwa nia moja tu huachilia mawazo yake, na hutumia dhana yake, kwamba dhana na mawazo ya mwanadamu zimekuwa adui wa kazi ya leo, kazi ambayo haiambatani na dhana za mwanadamu. Hili linaweza kusemwa kuwa kasoro ya dhana za mwanadamu, na wala si dosari ya kazi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

147. Watu husema Mungu ni Mungu wa haki, na kwamba mradi tu mwanadamu atamfuata mpaka mwisho, basi Hatakuwa na upendeleo kwa mwanadamu, kwani Yeye ni mwenye haki. Je, mwanadamu akimfuata mpaka mwisho kabisa, Mungu anaweza kumtupa mwanadamu nje? Sina upendeleo kwa mwanadamu yeyote, na Huwahukumu wanadamu wote kwa tabia Yangu ya haki, ilhali kuna mahitaji yanayofaa Ninayohitaji kutoka kwa mwanadamu, na Ninahitaji yakamilishwe na wanadamu wote, bila kujali ni nani. Sijali kiwango cha kufuzu kwako au kuheshimiwa kwako; najali tu kama utatembea kwa njia Yangu, na kama unapenda na una kiu ya ukweli. Kama huna ukweli, na unaleta aibu katika jina Langu, na matendo yako ni kinyume cha njia Yangu, kufuata tu bila kujali, basi wakati huo nitakupiga na kukuadhibu kwa uovu wako, na utakuwa na nini la kusema? Utaweza kusema Mungu si mwenye haki? Leo kama umezingatia maneno ambayo nimenena, basi wewe ni mtu ambaye Namkubali. Unasema umeumia ukifuata Mungu, kwamba umemfuata kwa marefu na mapana, na umeshiriki na yeye katika wakati mzuri na mbaya, lakini hujaishi kulingana na maneno yaliyosemwa na Mungu; unataka tu kukimbia huku na kule kwa ajili ya Mungu na kujitumia kwa ajili ya Mungu kila siku, na hujafikiria kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Unasema pia, “Kwa vyovyote, naamini Mungu ni mwenye haki. Nimeteseka kwa ajili Yake, nikashughulika kwa ajili Yake, kujitoa kikamilifu Kwake, na nimefanya bidii ingawa sijapata kutambuliwa; Yeye hakika atanikumbuka.” Ni ukweli kwamba Mungu ni mwenye haki, na haki hii haijatiwa doa na uchafu wowote: Haina mapenzi ya binadamu, na haijatiwa doa na mwili, ama kitendo chochote cha binadamu. Wale wote ambao ni waasi na wako kwa upinzani, na hawazingatii njia Zake wataadhibiwa; hakuna atakayesamehewa, na hakuna atakayeepuka! Watu wengine husema, “Leo nakimbia juu yako; mwisho ukifika, utanipa baraka kidogo?” Sasa Nakuuliza, “Umezingatia maneno Yangu?” Haki unayoongelea inategemea matendo. Unafikiria kwamba Mimi ni mwenye haki, na asiye na mapendeleo kwa binadamu wote, na kwamba wale wanifuatao hadi mwisho wataokolewa na kupata baraka Yangu. Kuna maana ya ndani kwa maneno Yangu kwamba “wale wote wanifuatao hadi mwisho wataokolewa”: Wale wanifuatao mpaka mwisho ndio Nitakaowapata, ni wale, baada ya kushindwa Nami, watautafuta ukweli na kufanywa wakamilifu. Ni hali gani umepata? Umepata kunifuata hadi mwisho, lakini nini kingine? Je, umezingatia maneno Yangu? Umekamilisha moja kati ya tano ya mahitaji Yangu, ilhali huna mpango wa kumaliza manne yaliyobaki. Umepata ile njia rahisi, na ukafuata ukifikiria umebahatika. Kwa mtu kama wewe, haki Yangu ni adabu na hukumu, ni adhabu ya haki, na ni adhabu ya haki kwa watenda maovu wote; wale wote wasiotembea kwa njia Yangu wataadhibiwa, hata kama watafuata mpaka mwisho. Hii ndio haki ya Mungu. Wakati tabia hii ya haki inapodhihirishwa katika adhabu ya mwanadamu, mwanadamu atakosa la kusema, na kujuta kwamba, alipokuwa akimfuata Mungu hakutembea katika njia Yake. “Wakati huo niliteseka kidogo tu nikimfuata Mungu, lakini sikutembea katika njia ya Mungu. Kuna udhuru gani? Hakuna namna ila kuadibiwa!” Ila kwa akili yake anafikiria, “Nimefuata hadi mwisho, hata Ukiniadibu haitakuwa adabu kali, na baada ya kuadibu kwa kuchosha, bado Utanihitaji. Najua Wewe ni mwenye haki, na Hutanifanyia hivyo milele. Mimi si kama wale watakaofagiliwa nje; wale watakaofagiliwa watapokea adabu kuu, na adabu Yangu itakuwa kidogo.” Adabu ya Mungu ya tabia ya haki si unavyosema. Sio kwamba wale ambao wanatubu dhambi zao kila wakati wataadibiwa kwa huruma. Haki ni utakatifu, na ni tabia ambayo haivumilii makosa ya mwanadamu, na yale yote ambayo ni machafu na hayajabadilika ndiyo shabaha ya chukizo kwa Mungu. Haki ya Mungu si sheria, lakini amri ya utawala: Ni amri ya utawala katika ufalme, na hii amri ya utawala ni adhabu ya haki kwa yeyote asiye na ukweli na hajabadilika, na hakuna kiwango cha wokovu. Mwanadamu akiwekwa kulingana na aina, wazuri watazawadiwa na wabaya kuadhibiwa. Ndio wakati hatima ya mwanadamu itawekwa wazi, na ndio ni wakati ambao kazi ya wokovu itafika mwisho, baada ya hapo, kazi ya kuokoa binadamu haitafanyika tena, na adabu italetwa kwa wale waliotenda maovu. Watu wengine husema, “Mungu hukumbuka kila mmoja ambaye huwa kando Yake kila wakati. Hatasahau hata mmoja wetu. Tumehakikishiwa kufanywa wakamilifu na Mungu. Hatawakumbuka wowote walio chini, wale kati yao watakaofanywa wakamilifu wana uhakika kuwa watakuwa duni kutuliko sisi, tunaokutana na Mungu kila wakati; kati yetu hakuna ambaye amesahaulika na Mungu, wote tumeshakubaliwa na Mungu, na tunalo hakikisho la kufanywa wakamilifu na Mungu.” Nyote mna mawazo ya aina hii. Je, hii ni haki? Je, umeweka ukweli katika vitendo au la? Kwa hakika unaeneza uvumi kama huu—huna aibu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

148. Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

149. Baada ya ukweli wa Yesu aliyepata mwili kutokea, mwanadamu aliamini hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ni sehemu hizo tatu pekee ambazo zimefanywa moja ambazo ni Mungu kamili. Bila Baba Mtakatifu, Mungu asingekuwa mkamilifu. Vivyo hivyo, wala Mungu asingekuwa mkamilifu bila Mwana au Roho Mtakatifu. Katika mawazo yao, wanaamini kuwa Baba au Mwana pekee hawezi kuwa Mungu. Ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu tu kwa pamoja wanaoweza kuwa Mungu Mwenyewe. Sasa, waumini wote wa kidini, na hata kila mfuasi miongoni mwenu, anashikilia hii imani. Ilhali, ikiwa hii imani ni sahihi, hakuna anayeweza kuelezea, kwani daima mmechanganyikiwa kuhusu masuala ya Mungu Mwenyewe. Japo hizi ni fikra tu, hamjui kama ni sawa au mbaya, kwani mmeathiriwa vibaya na mawazo ya kidini. Mmeyakubali kwa kina haya mawazo ya kidini yaliyozoeleka, na hii sumu imezama kwa kina ndani yenu. Hivyo basi, hata kwa hili mmeanguka katika huu ushawishi wenye madhara, kwani Utatu haupo. Yaani, Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haupo. Hizi zote ni fikra za kawaida za mwanadamu, na imani za uongo za mwanadamu. Kwa karne nyingi, mwanadamu ameamini katika huu Utatu, ambao umebuniwa na mawazo katika akili za mwanadamu, ukatengenezwa na mwanadamu, na ambao haujawahi kuonekana na mwanadamu. Kwa miaka mingi, kumekuwa na watu maarufu wa kiroho ambao wameeleza “maana ya kweli” ya Utatu, ila maelezo hayo ya Utatu kama nafsi tatu dhahiri yamekuwa si yakini na hayapo wazi na watu wote wamepumbazwa na “ujenzi” wa Mungu. Hakuna mtu maarufu yeyote aliyewahi kutoa maelezo kamili; maelezo mengi yanafaa katika masuala ya mjadala na katika maandishi, ila hakuna hata mtu mmoja ambaye ana ufahamu kamili na wa wazi kuhusu maana ya Utatu. Hii ni kwa sababu huu Utatu huu mkuu ambao mwanadamu anashikilia moyoni kwa hakika haupo. …

Ikiwa hatua tatu za kazi zitakadiriwa kulingana na dhana hii ya Utatu, basi ni lazima kuwe na Mungu watatu kwani kazi iliyofanywa na kila mmoja si sawa. Ikiwa yeyote miongoni mwenu anasema kwamba hakika Utatu upo, basi eleza huyu Mungu mmoja katika nafsi tatu ni nini hasa. Baba Mtakatifu ni nini? Mwana ni nini? Roho Mtakatifu ni nini? Je, Yehova ni Baba Mtakatifu? Je, Yesu ni Mwana? Basi, Roho Mtakatifu je? Je, Baba si Roho? Je, kiini cha Mwana vilevile si Roho? Je, kazi ya Yesu haikuwa ya Roho Mtakatifu? Je, kazi ya Yehova haikufanywa wakati ule na Roho sawa tu na kazi ya Yesu? Mungu Anaweza kuwa na Roho wangapi? Kulingana na maelezo yako hizi nafsi tatu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja; kama ni hivyo, kuna Roho watatu lakini kuwa na Roho watatu kunamaanisha kuwa kuna Mungu Watatu. Hii inamaanisha kuwa hakuna Mungu Mmoja wa kweli; Mungu wa aina hii anawezaje kuwa kiini asili cha Mungu? Kama unakubali kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi Anawezaje kuwa na Mwana na awe Baba? Je, hizi si fikra zako mwenyewe? Kuna Mungu Mmoja tu, nafsi moja katika Mungu huyu, na Roho mmoja tu wa Mungu sawa tu na ilivyoandikwa katika Biblia kwamba “Kuna tu Roho Mtakatifu mmoja na Mungu mmoja tu.” Haijalishi kama Baba na Mwana unaowazungumzia wapo, kuna Mungu mmoja tu, na kiini cha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu mnaowaamini ni kiini cha Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati huo huo awe ndani na juu ya ulimwengu. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote! Mungu ni Roho mmoja tu, na nafsi moja; na huyo ni Roho wa Mungu. Ikiwa ni kama usemavyo, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, basi Hawa si watatu? Roho Mtakatifu ni kitu kimoja, Mwana ni kingine, na Baba vilevile ni kingine. Nafsi Zao ni tofauti na viini Vyao ni tofauti, iweje basi ziwe kila moja Yao ni sehemu ya Mungu mmoja? Roho Mtakatifu ni Roho; hili ni rahisi kueleweka kwa wanadamu. Ikiwa ni hivyo basi, Baba ni Roho zaidi. Hajawahi kushuka kuja duniani na Hajawahi kupata mwili; Yeye ni Yehova Mungu katika mioyo ya mwanadamu, na kwa hakika Yeye vilevile ni Roho. Basi kuna uhusiano gani kati Yake na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Baba na Mwana? Au ni uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na Roho wa Mungu? Je, kiini cha kila Roho ni sawa? Au Roho Mtakatifu ni chombo cha Baba? Hili linaweza kuelezwaje? Aidha kuna uhusiano gani kati ya Mwana na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Roho wawili au ni uhusiano kati ya mwanadamu na Roho? Haya yote ni masuala ambayo hayawezi kuelezewa! Ikiwa Wote ni Roho mmoja, basi hapawezi kuwepo na mjadala kuhusu nafsi tatu, kwani zote zinamilikiwa na Roho mmoja. Kama Zingekuwa nafsi tofauti, basi Roho Zao Zingetofautiana katika nguvu zao na kamwe hawangekuwa Roho mmoja. Hii dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni upuuzi mtupu! Hili linamweka Mungu katika vitengo na kumgawanya kuwa nafsi tatu, kila moja ikiwa na hadhi na Roho; basi Atawezaje kuwa Roho mmoja na Mungu mmoja? Hebu niambie, je, mbingu na dunia na vyote vilivyomo viliumbwa na Baba, Mwana, au na Roho Mtakatifu? Wengine husema Waliviumba kwa pamoja. Basi ni nani alimkomboa mwanadamu? Alikuwa Roho Mtakatifu, Mwana, au Baba? Wengine husema ni Mwana aliyewakomboa wanadamu. Basi Mwana ni nani katika kiini? Siye kupata mwili kwa Roho wa Mungu? Mungu aliyepata mwili anamwita Mungu aliye Mbinguni Baba katika mtazamo wa mwanadamu aliyeumbwa. Je, hufahamu kuwa Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba kupitia Roho Mtakatifu. Ndani yake mna Roho Mtakatifu; lolote usemalo, Yeye bado ni mmoja na Mungu wa Mbinguni, kwani Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu. Hili wazo la Mwana si kweli Kabisa. Ni Roho mmoja anayefanya Kazi yote; Mungu Mwenyewe pekee, yaani, Roho wa Mungu anafanya kazi Yake. Roho wa Mungu ni nani? Je, si Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani ya Yesu? Ingekuwa kazi haikufanywa na Roho Mtakatifu (yaani Roho wa Mungu), je, kazi Yake ingemwakilisha Mungu Mwenyewe? Yesu alipomwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba alipokuwa akiomba, hili lilifanywa katika mitazamo ya mwanadamu aliyeumbwa, kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa amevaa mwili wa kawaida na Alikuwa na umbile la nje la mwanadamu aliyeumbwa. Hata ikiwa ndani yake mlikuwa na Roho wa Mungu, umbo Lake la nje bado lilikuwa lile la mtu wa kawaida; kwa maana nyingine, Alikuwa “Mwana wa Adamu” jambo ambalo watu wote, akiwemo Yesu Mwenyewe, walilizungumzia. Na kwa sababu Anaitwa Mwana wa Adamu, Yeye ni mtu (Mwanamke au mwanamume, kwa vyovyote vile mwenye umbo la nje la mwanadamu) aliyezaliwa katika familia ya kawaida ya watu wa kawaida. Kwa hivyo, Yesu kumwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba kulikuwa sawa na mlivyomwita mara ya kwanza Baba; Alifanya hivyo kutokana na mtazamo wa Mwanadamu aliyeumbwa. Je, mnakumbuka Sala ya Bwana ambayo Yesu aliwafundisha kukariri? “Baba Yetu Uliye mbinguni….” Aliwaambia wanadamu wote wamwite Mungu wa Mbinguni kwa jina la Baba. Na kwa kuwa Naye pia alimwita Baba, alifanya hivyo kutoka kwa mtazamo wa mtu aliye katika daraja moja nanyi nyote. Kwa kuwa mlimuita Mungu wa mbinguni Baba, hili linaonyesha kuwa Yesu alijichukulia kuwa katika daraja sawa nanyi, kama mwanadamu duniani aliyeteuliwa na Mungu (yaani, Mwana wa Mungu). Kama mnamwita Mungu “Baba,” je, hii si kwa sababu nyinyi ni wanadamu walioumbwa? Haijalishi Yesu alikuwa na mamlaka makubwa kiasi gani duniani, kabla ya kusulubiwa, Alikuwa tu Mwana wa Adamu, akiongozwa na Roho Mtakatifu (yaani, Mungu), Akiwa miongoni mwa viumbe wa duniani, kwani bado Alikuwa hajaikamilisha kazi Yake. Kwa hivyo, kumwita kwake Mungu wa mbinguni Baba kulikuwa tu unyenyekevu na utiifu Wake. Yeye kumwita Mungu (yaani, Roho aliye mbinguni) kwa namna ile, hata hivyo, hakudhibitishi kuwa Yeye ni Mwana wa Roho wa Mungu aliye mbinguni. Badala yake, ni kuwa mtazamo wake ni tofauti, si kwamba ni nafsi tofauti. Uwepo wa nafsi tofauti ni uongo. Kabla ya kusulubiwa kwake, Yesu alikuwa Mwana wa Adamu aliyefungwa katika udhaifu wa kimwili, na Hakuwa na mamlaka kamilifu ya Roho. Hiyo ndiyo maana Angeweza tu kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe. Ni kama tu Alivyoomba mara tatu huko Gethsemane: “Si kama Nitakavyo, bali kama Utakavyo.” Kabla Atundikwe msalabani, Hakuwa zaidi ya Mfalme wa Wayahudi; alikuwa Kristo, Mwana wa Adamu, na wala si mwenye utukufu. Hiyo ndiyo maana, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, Alimwita Mungu Baba. Sasa, huwezi kusema kuwa wote wamwitao Mungu Baba ni Wana. Ingekuwa kweli, basi wote si mngekuwa Mwana punde Yesu alipowafundisha Sala ya Bwana? Ikiwa bado hamjaridhika, basi niambieni hili, ni nani mmwitaye Baba? Ikiwa mnamrejelea Yesu, je, Baba ya Yesu ni nani kwenu? Baada ya Yesu kurudi mbinguni, hii dhana ya Baba na Mwana ilikoma. Hii dhana ilifaa tu kipindi ambacho Yesu alikuwa mwili; katika mazingira mengine yoyote, uhusiano ni ule wa kati ya Bwana wa uumbaji na kiumbe mnapomwita Mungu Baba. Hakuna wakati ambapo wazo hili la Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu linaweza kuwa na mashiko; ni uongo ambao ni nadra kuonekana na halipo!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

150. Katika Agano la Kale la Biblia, hapakutajwa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ni Mungu mmoja tu wa kweli, Yehova, akiifanya kazi yake nchini Israeli. Anaitwa majina tofauti kadri enzi zinavyobadilika, ila hili haliwezi kuthibitisha kuwa kila jina linarejelea mtu tofauti. Ingekuwa hivi, basi je, si kungekuwa na nafsi nyingi sana katika Mungu? Kilichoandikwa katika Agano la Kale ni kazi ya Yehova, hatua ya kazi ya Mungu Mwenyewe tangu mwanzo wa Enzi ya Sheria. Ilikuwa ni kazi ya Mungu, ambapo Alinena, ilikuwa, na Alipoamuru, ilitendeka. Hakuna hata wakati mmoja ambapo Yehova alisema kuwa alikuwa Baba aliyekuja kufanya kazi, wala Hakutabiri kuja kwa Mwana kuwakomboa wanadamu. Wakati wa Yesu ulipowadia, ilisemekana tu kwamba Mungu alikuwa Ameupata mwili kuwakomboa wanadamu, si kwamba ni Mwana aliyekuwa amekuja. Kwa sababu enzi hazifanani na kazi ambayo Mungu Mwenyewe hufanya vilevile inatofautiana, Anapaswa kufanya kazi Yake katika milki tofauti, kwa njia hii utambulisho Alionao vilevile unatofautiana. Mwanadamu anaamini kwamba Yehova ndiye Baba ya Yesu, ila hili halijakiriwa na Yesu ambaye alisema: “Hatukubainishwa kamwe kama Baba na Mwana; Mimi na Baba aliye Mbinguni ni kitu kimoja. Baba yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake; wanadamu wanapomwona Mwana, wanamwona Baba.” Baada ya yote kusemwa, iwe Baba au Mwana, Wao ni Roho mmoja, Hawajagawanywa kuwa nafsi tofautitofauti. Mara tu wanadamu wanapojaribu kueleza, mambo hutatizwa na wazo la nafsi tofauti, na vilevile na uhusiano kati ya Baba, Mwana na Roho. Mwanadamu akizungumzia nafsi tofauti, je, hili halimfanyi Mungu kuwa kitu? Mwanadamu hata zaidi huziorodhesha nafsi hizi kama nafsi ya kwanza, ya pili, na ya tatu; haya yote ni mawazo ya mwanadamu yasiyofaa kurejelewa, hayana uhalisi kabisa! Ukimwuliza: “Kuna Mungu wangapi?” atasema kuwa Mungu ni Utatu Mtakatifu wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu: Yule mmoja wa kweli. Ukiuliza tena: “Baba ni nani?” atasema: “Baba ni Roho wa Mungu aliye mbinguni; anatawala kila kitu, na kiongozi wa mbinguni.” “Je, Yehova ni Roho?” Atasema: “Ndiyo!” Ukimuuliza tena, “Mwana ni nani?” atasema kuwa Yesu ndiye Mwana, bila shaka. “Basi kisa cha Yesu ni kipi? Alitoka wapi?” Atasema: “Yesu alizaliwa na Maria kupitia kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu.” “Je, kiini Chake si Roho vilevile? Je, kazi Yake si kiwakilishi cha Roho Mtakatifu? Yehova ni Roho, vivyo hivyo na kiini cha Yesu. Sasa katika siku za mwisho, bila shaka ni Roho Anayeendelea kufanya Kazi; Wangewezaje kuwa nafsi tofauti? Je, si Roho wa Mungu anafanya kazi ya Roho kutoka katika mitazamo tofauti?” Kwa hivyo, hakuna tofauti bayana kati ya nafsi. Yesu alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu, na bila shaka, Kazi Yake hasa ilikuwa ile ya Roho Mtakatifu. Katika hatua ya kwanza ya kazi iliyofanywa na Yehova, Hakuwa mwili au kuonekana kwa mwanadamu. Kwa hivyo mwanadamu hakuona uso Wake. Haijalishi Alikuwa mashuhuri au mrefu kiasi gani, bado Alikuwa Roho, Mungu Mwenyewe aliyemuumba mwanadamu mwanzoni. Yaani, alikuwa Roho wa Mungu. Aliponena na wanadamu kutoka mawinguni, alikuwa Roho tu. Hakuna hata mmoja aliyeuona Uso wake; ni katika Enzi ya Neema tu ambapo Roho wa Mungu alikuwa mwili na Alipata mwili kule Uyahudi ndipo mwanadamu aliona sura ya kupata mwili kama Myahudi. Hisia ya Yehova haingeweza kuhisika. Hata hivyo, Alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho Mtakatifu, yaani, Alipatikana kwa utungaji mimba wa Roho wa Yehova Mwenyewe, na Yesu bado alizaliwa kama mfano halisi wa Roho wa Mungu. Alichokiona mwanadamu mwanzoni kilikuwa ni Roho Mtakatifu Akimshukia Yesu kama njiwa; Hakuwa Roho mwenye upekee kwa Yesu tu, badala yake alikuwa Roho Mtakatifu. Basi roho wa Yesu anaweza kutenganishwa na Roho Mtakatifu? Ikiwa Yesu ni Yesu, Mwana, na Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, basi wangewezaje kuwa kitu kimoja? Ingekuwa hivyo kazi isingefanywa. Roho ndani ya Yesu, Roho aliye mbinguni, na Roho wa Yehova wote ni mmoja. Anaweza kuitwa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho aliyezidishwa mara saba, na Roho mwenye vyote. Roho wa Mungu anaweza kufanya kazi nyingi. Ana uwezo wa kuumba na kuiangamiza dunia kwa kuleta mafuriko duniani; Anaweza kuwakomboa wanadamu, aidha, kuwashinda na kuwaangamiza wanadamu wote. Kazi hii yote inafanywa na Mungu Mwenyewe na haiwezi kufanywa na yeyote katika nafsi za Mungu kwa niaba Yake. Roho Wake anaweza kuitwa Yehova na Yesu, na vilevile mwenye Uweza. Yeye ni Bwana na Kristo. Anaweza pia kuwa Mwana wa Adamu. Yuko mbinguni na vilevile duniani; Yuko juu ya dunia na pia miongoni mwa umati. Yeye tu ndiye Bwana wa Mbingu na dunia! Tangu wakati wa uumbaji hadi sasa, kazi hii imekuwa ikifanywa na Roho wa Mungu Mwenyewe. Iwe ni kazi mbinguni au katika mwili, yote hufanywa na Roho Wake Mwenyewe. Viumbe wote, wawe mbinguni au duniani, wamo katika kiganja cha mkono Wake wenye nguvu; yote hii ni kazi ya Mungu na haiwezi kufanywa na yeyote kwa niaba Yake. Mbinguni Yeye ni Roho na vilevile Mungu Mwenyewe; miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwili ila anaendelea kuwa Mungu Mwenyewe. Japo Anaweza kuitwa mamia ya maelfu ya majina, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, na kazi yote ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Wake. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubiwa Kwake ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho Wake, na vilevile tangazo kwa mataifa yote na nchi zote wakati wa siku za mwisho. Wakati wote Mungu anaweza kuitwa mwenye uweza na Mungu mmoja wa kweli, Mungu Mwenyewe mwenye vyote. Nafsi bayana hazipo, aidha dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haipo. Kuna Mungu mmoja mbinguni na duniani!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

151. Hata hivyo, wengine wanaweza kusema: “Baba ni Baba; Mwana ni Mwana; Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, na mwishowe, Watafanywa kitu kimoja.” Je, Utawafanyaje kitu kimoja? Baba na Roho Mtakatifu Wawezaje kufanywa kitu kimoja? Ikiwa Walikuwa wawili kiasili, haijalishi Wamewekwa pamoja kwa namna gani, je, Hawataendelea kuwa sehemu mbili? Unaposema kuwa kuwafanya kuwa kitu kimoja, huko si kuunganisha sehemu mbili kutengeneza kitu kamili? Je, Hawakuwa sehemu mbili kabla ya kufanywa kitu kizima? Kila Roho ana kiini kinachotofautiana, na Roho wawili Hawawezi kufanywa kuwa kitu kimoja. Roho si chombo cha kutengenezwa, si kama chombo chochote katika ulimwengu. Kulingana na mitazamo ya wanadamu, Baba ni Roho mmoja, Mwana ni mwingine, na Roho Mtakatifu tena ni mwingine, halafu Roho Hawa huchanganyika sawa na glasi tatu za maji kuunda kitu kimoja kizima. Je, hizo si sehemu tatu zimefanywa kuwa kitu kimoja? Haya bila shaka ni maelezo ya kimakosa! Je, huku si kumgawa Mungu? Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wanawezaje kufanywa kuwa kitu kimoja? Je, Wao si sehemu tatu zenye asili tofauti? Aidha kuna wale wasemao, “je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa?” Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa naye—haya bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, “Mimi ni ndani ya Baba naye Baba yu ndani yangu,” hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe. Kutokana na kubadilika kwa enzi, mahitaji ya kazi, na hatua mbalimbali za mpango Wake wa usimamizi, vilevile jina wamwitalo wanadamu hubadilika. Alipokuja kufanya hatua ya kwanza ya kazi, Angeweza kuitwa tu Yehova, mchungaji wa Waisraeli. Katika hatua ya pili, Mungu mwenye mwili Angeweza kuitwa tu Bwana, na Kristo. Lakini wakati huo, Roho aliye mbinguni alikariri tu kwamba Alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, bila kutaja kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu. Hili halikufanyika kabisa. Mungu angewezaje kuwa na Mwana wa pekee? Basi, Mungu asingekuwa mwanadamu? Kwa kuwa Alikuwa Mwili, Aliitwa Mwana mpendwa wa Mungu na kutokana na hili, kukazuka uhusiano wa Baba na Mwana. Ni kwa sababu tu ya utengano kati ya mbingu na dunia. Yesu aliomba kutokana na msimamo wa mwili. Kwa sababu Alikuwa Amepata mwili wa ubinadamu wa kawaida, ni kutokana na msimamo wa mwili ndipo Alisema: “Umbo Langu la nje ni la kiumbe. Kwa sababu Nilijivisha mwili kuja duniani, sasa Niko mbali, mbali sana na mbinguni.” Kwa sababu hii, Angeomba tu kwa Baba kutokana na msimamo wa mwili. Huu ulikuwa wajibu Wake, ambao ni sharti Roho wa Mungu aliyepata mwili anapaswa kupewa. Haiwezekani kusema kwamba Hawezi kuwa Mungu kwa sababu tu Anamwomba Baba kutokana na msimamo wa mwili. Ijapokuwa Anaitwa Mwana mpendwa wa Mungu, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, ni vile tu Yeye ni mwili wa Roho, na kiini chake bado ni Roho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Iliyotangulia: B. Maneno Juu ya Kukifichua Asili ya Shetani ya Wanadamu Wapotovu na Kiini na Asili Yao

Inayofuata: D. Maneno Kuonyesha Ukweli ni Nini

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp