299 Nitainuka Tena kwa Nguvu

I

Kwa kujua tabia ya Mungu ya haki,

upendo wangu kwa Mungu unakita mizizi.

Iwe nimebarikiwa au kupitia taabu

yote yanaamuliwa kabla na Mungu.

Hukumu, adhabu na majaribio

huja kuutakasa upendo wangu.

Kushindwa kwa mwanadamu ni kwa kawaida

na hakuna sababu ya hofu.

Ingawa maneno Yake ni makali kama upanga,

moyo wa Mungu ni karimu daima.

Nawezaje kukataa dawa chungu

inayofaidi maisha yangu?

Kupitia hukumu ya Mungu na kuadibu,

nimehisi upendo wa Mungu wa kweli.

Kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu ni halisi sana,

moyo wangu unampa Mungu sifa.

Moyo wangu unampa Mungu sifa.

II

Watu wenye kiburi na wadanganyifu

wataishia kujikwaa na kuanguka.

Ingawa namtumikia Mungu, bado nampinga.

Napaswa kuvumilia kuadibu Kwake.

Ingawa hukumu yaweza kuniletea uchungu mkubwa,

ni kile maisha yangu kinahitaji.

Nina hakika kwamba Mungu ni haki

na hivyo moyo wangu unatoa sifa.

Kwamba naweza kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu

ni heshima Anayotoa.

Ningalilalamika au kugombana naye,

singalistahili upendo Wake.

Wanadamu potovu hawana ukweli,

wamejaa tabia za Shetani.

Nina uhai leo kwa sababu tu ya

wokovu wa Mungu wa wakati mzuri, wokovu wa Mungu wa wakati mzuri.

III

Roho ya Petro ni msingi

wa jinsi wanadamu wanapaswa kutenda.

Mwanadamu kuweza kumpenda Mungu kuna maana sana,

Nitajitahidi kumpenda kikamilifu.

Kutamani baraka, kubadilishana na Mungu,

mwishowe, mwanadamu atajikwaa.

Kwa kuelewa ukweli na kutakaswa,

nina amani moyoni mwangu.

Mwamini Mungu, mpende Mungu, mtii Mungu,

huu ni wajibu wa kweli wa mwanadamu.

Kupitia kuadibu na hukumu

kunaimarisha upendo wangu kwa Mungu.

Haijalishi jinsi Mungu anavyonishughulikia ,

bado naisifu haki Yake.

Ndoto yangu ni kuweza kumjua Mungu.

Siombi kingine tena.

Siombi kingine tena.

IV

Baada ya kupitia hukumu

na kuonja upendo wa Mungu, nitainuka tena.

Sina heshima ya kumwona Mungu,

lakini nitapambana tena kwa ajili yangu.

Nimeyaelewa mapenzi ya Mungu,

upendo Wake unanitia moyo niendelee.

Bila kujali ukubwa wa majaribu na taabu,

nitatoa ushuhuda wenye nguvu.

Baraka au majonzi hayajalishi kabisa.

Utukufu wa Mungu ni kila kitu.

Kama Petro, nitampa Mungu upendo mkuu.

Na nitakapokufa, nitapumzika kwa amani.

Nitatii kazi ya Mungu bila uchaguzi.

Kumridhisha Mungu ni muhimu.

Kumpenda Mungu na kutekeleza mapenzi Yake

ni heshima kuu zaidi ya mwanadamu, heshima kuu zaidi ya mwanadamu.

Iliyotangulia: 298 Nataka Kuwa Mwandani wa Mungu

Inayofuata: 300 Kuwa Jasiri Katika Njia ya Kumpenda Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki