977 Unapaswa Kutafuta Kukubaliwa na Mungu

1 Kwa minajili ya majaliwa yenu, mnastahili kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Kwa sababu mnatambua kwamba nyinyi mmehesabiwa miongoni mwa wale walio katika nyumba ya Mungu, basi mnastahili kumletea Mungu utulivu wa akili katika mambo yote na kumtosheleza katika kila jambo. Kwa maneno mengine, lazima muwe wenye maadili katika matendo yenu na kutii ukweli katika mambo kama hayo. Kama hali hii inazidi uwezo wako, basi utachukiwa na kukataliwa na Mungu na vilevile kukataliwa kwa dharau na kila mwanadamu. Punde utakapokuwa katika hali mbaya kama hii, basi hauwezi kuhesabiwa miongoni mwa wale walio kwenye nyumba ya Mungu. Hii ndiyo maana ya kutoidhinishwa na Mungu.

2 Kila mwanadamu, katika kuishi maisha yake ya imani katika Mungu, amemkataa na kumdanganya Mungu wakati fulani. Baadhi ya matendo mabaya hayahitaji kurekodiwa kama kosa, lakini mengine hayasameheki; kwani mengi ni yale yanayokiuka amri za utawala, yaani, yanaikosea tabia ya Mungu. Ninawashawishi kuwa na ufahamu bora zaidi wa yaliyomo katika amri za utawala na kujua tabia ya Mungu. Vinginevyo, mtapata ugumu sana kuendelea kufunga vinywa vyenu na kufyata ndimi zenu dhidi ya kuropokwa bila kizuizi kwa mazungumzo ya mbwembwe, na bila kujua mtaikosea tabia ya Mungu na kujipata kwenye giza, mkipoteza uwepo wa Roho Mtakatifu na mwangaza.

3 Kwa sababu nyinyi hamna maadili katika matendo yenu, kufanya na kutenda kile ambacho hufai kufanya hivyo, basi utapokea adhabu inayokufaa. Lazima ujue kwamba ingawa wewe ni mpotovu katika maneno yako na matendo yako, Mungu ni mwenye maadili sana katika hali hizi zote. Sababu ya wewe kupokea adhabu ni kwa sababu umemkosea Mungu na wala si binadamu. Kama, katika maisha yako, wewe hutenda makosa mengi dhidi ya tabia ya Mungu, basi huna budi ila kuwa mtoto wa kuzimu. Kama wewe ni mtu mwaminifu na unayetenda kwa maadili, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu. Kama katika matendo yako huikosei tabia ya Mungu, na unatafuta mapenzi ya Mungu na unao moyo wa kumcha Mungu, basi imani yako ni ya kiwango kilichowekwa.

Umetoholewa kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 976 Yatii Mapenzi ya Mungu kwa Kufuata Amri Kumi

Inayofuata: 978 Onyo la Mungu kwa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp