229 Kujitafakari Hunipa Njia ya Kufuata

1 Kumfuata Mungu njia yote hadi leo, nimeelewa ukweli mwingi. Kushindwa kwangu kwingi na uchungu wote ambao nimepitia vimeniamsha kana kwamba ni kutoka ndotoni. Kwa kujiangalia kupitia maneno Yake, Ninapata upotovu wangu ni wenye kina. Tabia yangu ya kishetani mara nyingi hunisababisha niseme uwongo na kudanganya, na kila wakati mimi ni hobelahobela katika wajibu wangu—sina mfano mwingi wa mwanadamu. Ninatenda kulingana na mapenzi yangu, na ni mara chache natenda ukweli. Matendo yangu hayana misimamo, lakini nafikiri nina uhalisi wa ukweli. Mimi ni mnafiki tu, mimi simtii Mungu kabisa. Nafanya kazi kwa ajili ya sifa na hadhi pekee; kuingia kwa maisha yangu ni kwa juu juu. Naitazama roho ya Petro kwa makini na najua ninapungukiwa na roho yake. Mwenye aibu sana, ninakosa maneno.

2 Mateso na dhiki vinafunua kukosa kwangu ibada na upendo kwa Mungu. Ninajali tu juu ya mwili wangu, na simjali Mungu hata kidogo. Ninahofia mateso ya kukamatwa, na ninahofia kuwa kama Yuda. Nimekuwa nikiogopa kifo, na nimeishi maisha isiyoheshimika, nikikataa hata kutekeleza wajibu wangu. Naona kimo changu halisi kutoka ufunuo wa ukweli. Bila uhalisi wa ukweli, Nitakuwa na uhakika wa kumsaliti Mungu. Bila upendo moyoni mwangu kwa Mungu, ningewezaje kujitoa na kutii? Ninajutia miaka yangu ya imani si kwa ajili ya kufuatilia ukweli. Kupitia vipingamizi na kushindwa, naona kwamba maisha yangu yako ukingoni. Bila uhalisi wa ukweli, hakuwezi kuwa na shahidi mwenye nguvu.

3 Majaribio, utakaso, kushughulikiwa na kupogolewa, yananifunua mimi na kile ninachofanya. Ninaeleza juu ya mafundisho na kutumia visingizio kujitetea. Kwa uwongo na udanganyifu moyoni mwangu, ningewezaje kuwa mwaminifu kwa kweli? Sijawahi kuwa na uchaji kwa Mungu, wala kamwe sijawahi kumtii Mungu kweli. Kwa kuakisi, ninapata kwamba tabia yangu haijabadilika sana kwa kuwa na imani miaka hii yote. Ni upumbavu kweli kutotaka kutafuta ukweli, ila kutaka kuingia ufalme! Tabia ya Mungu, ya uaminifu, ya haki, bila ukweli nitafukuzwa na Mungu. Nimemwamini Mungu kwa miaka bila kufuatilia ukweli, hivyo mimi ni fukara sana. Bila kujiakisi, ningewezaje kujua kwamba ninatembea njia ya Paulo? Ninaamua kumuiga Petro na kufuatilia kumpenda Mungu na kutimiza mapenzi ya Mungu.

Iliyotangulia: 228 Yaliyopita Yananichoma Kama Upanga

Inayofuata: 230 Kutoenda Mbali na Maneno ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

901 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

64 Upendo wa Kweli

1Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao,nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini.Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki