Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 70

Kwamba siri Yangu imefichuliwa na kuonyeshwa bayana, pasi kufichwa tena, ni kwa njia ya neema Yangu na huruma kabisa. Kwamba neno Langu linaonekana miongoni mwa wanadamu, pasi kufichwa tena, hata zaidi ni kwa neema na huruma Zangu. Ninawapenda wote wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu na kujitolea Kwangu. Ninawachukia wale wote waliozaliwa na Mimi ilhali ambao hawanijui, hata hunipinga Mimi. Sitamtelekeza mtu yeyote ambaye kwa kweli yu upande Wangu, ila Nitafanya baraka zake ziwe maradufu. Nitawaadhibu mara mbili wale wasio na shukrani, na Sitawahurumia kwa urahisi. Katika ufalme Wangu hakuna udanganyifu au ulaghai, hakuna umalimwengu, yaani, hakuna harufu ya wafu, lakini yote ni uaminifu, haki, yote ni utakatifu, uwazi, bila kujificha, hakuna maficho; yote ni safi, yote ni furaha, yote ni ujenzi wa maadili. Mtu yeyote akibaki na harufu ya wafu, hakika hawezi kusalia katika ufalme Wangu, lakini atatawaliwa na fimbo Yangu ya chuma. Mafumbo yasiyokuwa na mwisho tangu zama za kale hadi sasa yamefichuliwa kikamilifu kwenu—wale wanaopatwa na Mimi katika siku za mwisho—je, hamhisi kubarikiwa? Siku ya udhihirisho wa wazi hata zaidi ni siku ambayo mtashiriki utawala Wangu.

Wale ambao kweli hutawala kama wafalme wanategemea majaaliwa na uteuzi Wangu, na lazima pasiwe na dhamira yoyote ya kibinadamu. Mtu akithubutu kushiriki katika hili, lazima apitie pigo la mkono Wangu, na yeye ni lengo la moto Wangu mkali; huu ni upande mwingine wa haki na uadhama Wangu. Nimesema, Ninatawala vitu vyote, Mimi ndiye Mungu mwenye hekima ambaye anashika mamlaka kamili, na Mimi si mpole kwa mtu yeyote, Asiye na huruma, bila hisia za kibinafsi. Mimi humtendea mtu yeyote (bila kujali jinsi anavyozungumza vizuri, Sitamsamehe) kwa haki, unyofu, na uadhama Wangu, wakati huo huo Nikimwezesha kila mtu kuona vizuri ajabu ya matendo Yangu, aone kile ambacho matendo Yangu yanamaanisha. Naadhibu kila aina ya matendo ya roho wabaya mmoja mmoja, Nikiwatupa mmoja baada ya mwingine, katika shimo la kuzimu. Niliimaliza kazi hii kabla ya wakati kuanza, Nikiwaacha bila nafasi, na kuwaacha bila mahali pa kufanyia kazi yao. Watu Wangu wote wateule, walioamuliwa na kuchaguliwa na Mimi, hawawezi kamwe kutawaliwa nao wakati wowote, lakini daima wao ni watakatifu. Wale ambao Sijawajaalia na kuwachagua Mimi huwakabidhi kwa Shetani na kuwaacha wasisalie tena. Amri Zangu za utawala katika vipengele vyote zinahusisha haki Yangu, uadhama Wangu. Sitamwachia huru hata mmoja kati ya wale ambao Shetani anawafanyia kazi, lakini Nitawatupa pamoja na miili yao kuzimuni, kwa maana Ninamchukia Shetani. Bila shaka Sitamhurumia kwa urahisi, lakini Nitamharibu kabisa na Sitamwachia fursa hata kidogo ya kufanya kazi yake. Wale ambao Shetani amewapotosha kwa kiasi fulani (wale ambao ni lengo la maafa) wako hivyo kwa sababu ya utaratibu wa hekima ya mkono Wangu wenyewe. Usifikiri ni kwa ajili ya ukatili wa Shetani, lakini jua kuwa Mimi ni Mwenyezi Mungu anayetawala vitu vyote katika ulimwengu! Kwangu Mimi hakuna matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa, sembuse kuwa na kitu chochote kisichoweza kufanikishwa au neno lolote ambalo haliwezi kusemwa. Sharti mtu asifanye kazi ya washauri Wangu. Jihadharini msiangushwe kwa mkono Wangu na kutupwa kuzimuni. Nakwambia!Wale ambao leo wanashirikiana na Mimi kwa shauku ni wale werevu zaidi, wakiepuka hasara, wakikimbia maumivu ya hukumu. Yote haya yako katika utaratibu Wangu, majaaliwa Yangu; usiseme maneno yasiyo na adabu, ukizungumza kwa fahari, ukifikiri wewe ni mkuu sana. Je, si yote ni kwa njia ya majaaliwa Yangu? Ninyi ambao mngekuwa washauri Wangu hamna aibu! Hamjui vimo vyenu wenyewe, vidogo na vya kusikitisha jinsi gani! Hata hivyo, mnachukulia hilo kwa urahisi, na hamjielewi. Kila mara mnayapa kisogo maneno Yangu, mkisababisha bidii Zangu za mchwa ziwe bure, mkifikiri kidogo tu kuwa ni neema na huruma Yangu. Badala yake mnaonyesha ujanja wenu tena na tena. Je, mnakumbuka hili? Ni kuadibu gani ambako watu wanaofikiri kuwa ni werevu wanapokea? Wasiojali na wasiokuwa waaminifu kwa maneno Yangu, pasipo kuyatia mioyoni mwenu, mnatumia uongo Kwangu ili kufanya hili na lile. Waovu! Je, ni lini mnaweza kuufikiria moyo Wangu kikamilifu? Hamuufikirii moyo Wangu, na hivyo kuwaita waovu si kuwanyanyasa. Kunawafaa vizuri kabisa!

Leo Nawaonyesha, kimoja baada ya kingine, vitu vilivyofichwa kwa wakati mmoja. Joka kubwa jekundu linatupwa katika shimo la kuzimu na kuharibiwa kabisa, kwa kuwa kulihifadhi hakuna manufaa kabisa, ambayo ina maana kuwa haliwezi kumhudumia Kristo. Baadaye hakutakuwa na hicho kitu chekundu tena; lazima liharibike hatua kwa hatua hadi liangamie. Ninafanya kile Ninachosema; ni kukamilika kwa kazi Yangu. Ondoa mawazo ya kibinadamu, kila kitu ambacho Nimesema, Nimefanya. Yeyote anayejaribu kuwa mwenye busara anajiletea uharibifu, akijitia aibu juu yake mwenyewe, na hataki kuishi. Kwa hiyo Nitakutosheleza na hakika Sitawahifadhi watu kama hao. Baada ya hapo, idadi ya watu itaongezeka kwa ubora, huku wote ambao hawashirikiani Nami kwa shauku wataondolewa hadi kuharibika. Wale ambao Nimewaidhinisha ni wale Nitakaowakamilisha. Sitamtupa hata mmoja. Hakuna utata katika kile Ninachosema. Wale ambao hawashirikiani Nami kwa shauku watapitia kuadibu kwingi zaidi, lakini hatimaye hakika Nitawaokoa, lakini wakati huo, kiwango cha maisha yao kitakuwa tofauti kabisa. Je, unataka kuwa mtu kama huyo? Inuka na ushirikiane na Mimi! Hakika Sitawatendea vibaya watu wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu. Wale wanaojitoa Kwangu kwa dhati, Nitawapa baraka Zangu zote. Jitoe kabisa Kwangu! Kile unachokula, kile unachovaa, na mustakabali wako yote yako mikononi Mwangu, Nitayapanga vizuri kabisa, kwa ajili ya furaha yako isiyokuwa na mwisho, isiyoisha, kwa maana Nimesema, "Kwa wale wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu, hakika Nitakubariki kwa wingi." Baraka zote huja kwa kila mtu anayetumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu.

Iliyotangulia:Sura ya 69

Inayofuata:Sura ya 71

Maudhui Yanayohusiana