Sura ya 69

Mapenzi Yangu yatokapo, yeyote anayethubutu kupinga na yeyote anayethubutu kuhukumu au kuwa na shaka, mara moja Nitamfukuza. Leo, yeyote ambaye hatendi kulingana na mapenzi Yangu, au yeyote anayeyafikiria mapenzi Yangu visivyo, ni lazima atupwe nje na kuondolewa kutoka kwa ufalme Wangu. Katika ufalme Wangu hakuna mtu mwingine—wote ni wana Wangu wa kiume, wale ambao Nawapenda na hunifikiria Mimi. Zaidi ya hayo, ndio ambao hutenda kulingana na neno Langu na ambao wana uwezo wa kutawala katika uongozi kwa niaba Yangu kuhukumu mataifa yote na watu wote. Aidha, wao ni kundi la wana wa kiume wazaliwa wa kwanza, ambao ni maasumu na wa kusisimua; sahili na wazi; waaminifu na wenye hekima. Mapenzi Yangu yameridhika ndani yenu, na kile ambacho Nataka kufanya kimetimia ndani yenu, bila makosa, wazi kabisa na kufichuliwa. Wale ambao wana nia mbaya na madhumuni—Nimeanza kuwaacha, na Nitafanya waanguke mmoja mmoja. Nitawaangamiza mmoja baada ya mwingine kufingia hatua ambapo wasiweze kuendelea kuishi—na haya yote yanarejelea roho zao, nafsi zao na miili yao.

Elewa kwamba kile ambacho mkono Wangu unafanya—kuwaruzuku maskini, kuwatunza na kuwalinda wale wanaonipenda Mimi, kuwaokoa wajinga na wenye raghba ambao hawaingilii kazi ya usimamizi Wangu, kuwaadhibu wale ambao hunipinga Mimi na wale ambao hawashirikiani Nami kikamilifu—mambo yote haya yatathibitishwa moja kwa moja kwa mujibu wa kile Nimesema tayari. Je, wewe ni mtu ambaye kwa kweli ananipenda Mimi? Je, wewe ni mtu ambaye kwa uaminifu hutumia rasilmali mwenyewe kwa ajili Yangu? Je, wewe ni mtu ambaye husikiliza neno Langu na kutenda ipasavyo? Je, wewe ni mtu ambaye hunipinga Mimi, au wewe ni mtu unayelingana na Mimi? Je, mawazo yako mwenye yako wazi juu ya mambo haya? Je, unaweza kujibu kwa mambo haya ambayo Nimeyasema moja kwa moja? Kama huwezi, wewe ni mtu ambaye hufuata kwa shauku, lakini hayaelewi mapenzi Yangu. Aina hii ya mtu kwa urahisi zaidi ataingilia usimamizi Wangu na kufikiria mapenzi Yangu visivyo. Iwapo mtu kama huyo kwa muda mfupi ana nia mbaya, yeye atafanyiwa uhamisho Wangu na maangamizo.

Ndani Yangu kuna mafumbo yasiyokuwa na mwisho, yasiyoweza kueleweka. Nitayafichua kwa watu moja kwa moja kulingana na mpango Wangu. Hiyo ni kwamba, Nitayafichua kwa wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume. Kwa wale ambao si waumini na ambao kunipinga Mimi, Nitawaruhusu kwenda na mkondo, lakini mwishowe lazima Niwafanye waelewe kwamba Mimi ni hukumu na uadhama. Watu wasioamini wa leo wanajua tu kinachotokea mbele ya macho yao, lakini hawajui mapenzi Yangu. Ni Wanangu wa kiume tu, ambao Nawapenda, wanaojua na kuelewa mapenzi Yangu. Kwa Wanangu wa kiume, Nimefichuliwa wazi wazi, lakini kwa Shetani Mimi ni hukumu na uadhama, sijafichwa hata kidogo. Leo ni wanangu wazaliwa wa kwanza wa kiume tu ambao wanastahili kujua mapenzi Yangu—hakuna mtu mwingine anayehitimu—na hili ndilo Nililopanga kabla ya uumbaji. Ni nani amebarikiwa na ni nani amepigwa mijeledi wote walikuwa wamepangwa vizuri nami mapema, Nilikuwa wazi kuhusu hili, na kwa sasa tayari limedhihirika kikamilifu: Wale waliobarikiwa wameanza kufurahia baraka zao, ilhali wale ambao wamechapwa viboko pia wameanza kuteseka kwa maafa. Wale ambao hawataki kuteseka na baa hata hivyo watateseka kwa sababu hili ndilo Nimeamua na hili ndilo mikono Yangu ya amri za kiutawala imepanga. Hasa ni aina gani ya mtu amebarikiwa na ni aina gani ya mtu amepigwa viboko? Tayari Nimefichua mambo haya; hili si siri kwenu, lakini limejitokeza waziwazi: Wale wanaonikubali Mimi lakini ambao nia zao ni mbaya; wale wanaonikubali Mimi lakini hawafuatilii; wale wanaonijua Mimi lakini si watiifu; wale wanaojiingiza katika uhalifu na udanganyifu kunihadaa Mimi; wale wanaosoma maneno Yangu lakini hutapika ukanaji; wale ambao hawajijui wenyewe, ambao hawajui wao ni nini, ambao wanajidhani kuwa wao wenyewe ni wakubwa, na ambao wanadhani kwamba wamefikia ukomavu (mfano wa Shetani), hawa ni vifaa vya baa. Wale ambao hunikubali Mimi na ambao nia yao ni kunielekea Mimi (na kama wakisababisha madakizo Mimi sitakumbuka makosa yao, lakini nia zao ni lazima ziwe za haki na ni lazima daima wawe na tahadhari, wawe makini na wasiwe wapotovu, na lazima daima waweke mioyoni mwao kunisikiliza Mimi na kunitii); wale ambao ni wasafi; wale ambao wako wazi; wale ambao ni waaminifu, wale ambao hawadhibitiwi na mtu yeyote, kitu, au jambo; watu walio kama watoto kwa kuonekana ingawa wao ni wakomavu katika maisha, hawa ndio wapendwa Wangu, vifaa vya baraka Yangu. Sasa, kila mmoja atachukua nafasi yake sahihi kwa mujibu wa hali yake. Na wewe utajua kama umebarikiwa au umepigwa viboko—hakuna haja Kwangu kusema dhahiri. Wale waliobarikiwa lazima washangilie na kuwa na furaha, huku wale ambao watafikwa na baa hawapaswi kuhuzunika. Yote mawili yamepangwa na mkono Wangu, lakini Mimi si wa kulaumiwa: Ni ukosefu wako mwenyewe wa ushirikiano hai na Mimi, na kushindwa kwako kuelewa kwamba Mimi ni Mungu anayetafuta ndani kabisa ya moyo wa binadamu; ni kile ambacho Nimeamua kabla, na ni kwa hila yako ndogo ambapo umejidhuru mwenyewe; ni kujiumiza mwenyewe! Kwamba lazima utumbukie Kuzimu si kutendewa vibaya! Huu ni mwisho wako; haya ni matokeo yako!

Wabarikiwa wazaliwa wa kwanza wa kiume! Amkeni upesi kushangilia! Amkeni upesi kutoa sifa! Kuanzia sasa, hakutakuwa na uchungu zaidi, hakuna mateso tena, na kila kitu ki katika mikono yetu. Mtu yeyote ambaye anapatana nami ndiye Ninayempenda, na hatawekwa kwa mateso ya mabaa. Chochote ambacho ni hamu ya moyo wako, Nitakitimiza (lakini haiwezi kuwa kiholela), hii ni kazi Yangu.

Iliyotangulia: Sura ya 68

Inayofuata: Sura ya 70

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp