Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 74

Wamebarikiwa wale ambao wamelisoma neno Langu na kuamini kwamba litatimizwa—Sitakutendea vibaya, lakini Nitafanya yale unayoamini yatimizwe kwako. Hii ni baraka Yangu ikija juu yako. Neno Langu linapiga siri zilizofichwa ndani ya kila mtu. Kila mtu ana majeraha ya mauti, na Mimi ni tabibu mzuri ambaye anayaponya—njoo tu katika uwepo Wangu. Kwa nini Nilisema kuwa katika siku zijazo hakutakuwa tena na huzuni na hakutakuwa na machozi? Ni kwa sababu ya hili. Ndani Yangu, kila kitu kinatimizwa, lakini ndani ya wanadamu, vitu vyote ni vipotovu na bure, na vyote ni vidanganyifu kwa wanadamu. Katika uwepo Wangu utapokea vitu vyote, na utaona na pia kufurahia baraka zote ambazo hungewahi kufikiria. Wale wasiokuja mbele Yangu bila shaka ni waasi, na hakika ndio wanaonipinga Mimi. Hakika Sitawaacha kwa urahisi; Nitamwadibu vikali mtu wa aina hii. Kumbuka hili! Wale wanaokuja mbele Yangu zaidi watapata zaidi, lakini haitakuwa zaidi ya neema. Baadaye, watapata baraka nyingi zaidi.

Tangu uumbaji wa ulimwengu Nimeanza kuamulia kabla na kuchagua kundi hili la watu, yaani, ninyi leo. Tabia yenu, ubora wa tabia, sura, kimo, familia ambayo ulizaliwa kwayo, kazi yako na ndoa yako, ujumla wako, hata rangi ya nywele yako na ngozi yako, na wakati wa kuzaliwa kwako vyote vilipangwa na mikono Yangu. Hata mambo unayofanya na watu unaokutana nao kila siku hupangwa na mikono Yangu, sembuse ukweli kwamba kukuleta katika uwepo Wangu leo kwa kweli ni mpango Wangu. Usijitupe katika vurugu; unapaswa kuendelea kwa utulivu. Kile Ninachokuruhusu kufurahia leo ni mgawo ambao wewe unastahili, na Nilikipangia kabla katika uumbaji wa dunia. Wanadamu wote ni waliozidi sana—wao huwa vichwa ngumu sana au wasio na aibu kabisa. Hawawezi kufanya mambo kulingana na mpango Wangu na mpangilio. Usifanye hilo tena. Ndani Yangu vyote vinakombolewa; usijifunge mwenyewe, kwani kutakuwa na upotezaji unaohusiana na maisha yako. Kumbuka hili!

Amini kwamba kila kitu kiko mikononi Mwangu. Kile kilichoonekana kuwa siri kwenu katika siku za nyuma kinafichuliwa wazi leo; hakijafichika tena (kwa maana Nimesema kuwa katika siku za baadaye hakuna kitu kitakachobaki kikiwa kimefichika). Watu huwa bila subira mara nyingi; wao wana hamu sana ya kukamilisha kitu fulani na hawafikirii yaliyo ndani ya moyo Wangu. Nawafundisha ili muweze kushiriki mzigo Wangu na kusimamia nyumba Yangu. Nataka mkue kwa haraka ili muweze kuwaongoza ndugu zenu ambao ni wadogo kuliko ninyi, ili sisi Baba na wana tuweze kuunganishwa tena karibuni na kamwe hatutatengwa. Hii itaridhisha hamu ya moyo Wangu. Fumbo tayari limefichuliwa kwa watu wote, na hakuna chochote kinachobaki kikiwa kimefichika: Mimi—Mungu mkamilifu Mwenyewe, aliye na ubinadamu wa kawaida na uungu kamili—Nimefichuliwa mbele ya macho yenu leo. Nafsi Yangu nzima (mavazi, sura ya mwili, na umbo la mwili) ni dhihirisho kamili la Mungu Mwenyewe, na ni nafsi ya Mungu ambayo wanadamu wamewazia tangu kuumbwa kwa ulimwengu lakini hakuna mtu ambaye ameiona. Sababu ambayo vitendo Vyangu ni vizuri kama maneno Yangu ni kwamba ubinadamu Wangu wa kawaida na uungu kamili hukamilishana, na pia huwawezesha watu wote kuona kwamba nguvu kuu sana kama hiyo iko katika mtu wa kawaida. Wale kati yenu ambao mnaniamini kweli hufanya hivyo kwa sababu Nilikupa moyo wa kweli ili kukuwezesha kunipenda. Ninapokushughulikia, Ninakumulikia na kukupa nuru na kukuruhusu kunijua kupitia kwa hilo. Kwa hiyo, bila kujali jinsi Ninavyokushughulikia, hutatoroka. Badala yake, utakuwa na uhakika na Mimi zaidi na zaidi. Wakati wewe ni dhaifu, pia ni mpangilio Wangu, ambao unakuwezesha kuona kwamba punde unaponiacha Mimi utakufa na kunyauka. Kutokana na hilo unaweza kujifunza kwamba Mimi ndimi uhai wako. Unavyokuwa na nguvu baada ya kuwa dhaifu, litakuruhusu kuona kwamba kuwa dhaifu au mwenye nguvu hakukutegemei, lakini kunanitegemea Mimi kabisa.

Mafumbo yanafunuliwa kabisa. Katika shughuli zenu za baadaye, Nitawapa maagizo Yangu moja baada ya lingine. Sitakuwa asiye dhahiri; Nitakuwa wazi kabisa na hata kuzungumza nanyi moja kwa moja ili msihitaji kutafakari kuyahusu wenyewe, msije mkakatiza usimamizi Wangu. Ndiyo maana Mimi mara kwa mara Nasisitiza kwamba baadaye hakutakuwa na kingine tena ambacho kimefichika.

Iliyotangulia:Sura ya 73

Inayofuata:Sura ya 75

Maudhui Yanayohusiana