3. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Hukumu na Kuadibu

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaoruhusiwa kubaki wote watatakaswa na kuingia katika hali ya juu zaidi ya ubinadamu ambapo watafurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni walengwa wa adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Leo Mungu anawahukumu, na kuwaadibu, na kuwashutumu, lakini jueni kwamba shutuma yako ni ili kukufanya kuweza kujijua. Shutuma, laana, hukumu, kuadibu—haya yote ni ili kwamba uweze kujijua, ili tabia yako iweze kubadilika, na, zaidi ya hayo, ili uweze kujua thamani yako, na kutambua kwamba vitendo vyote vya Mungu ni vyenye haki, na kulingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ndiye Mungu mwenye haki anayempenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu, na Anayemhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kama utajua tu kwamba wewe ni mwenye hadhi ya chini, kwamba umepotoka na hutii, lakini hujui kwamba Mungu angependa kuweka wazi wokovu Wake kupitia kwa hukumu na kuadibu ambako Anafanya ndani yako leo, basi huna njia yoyote ya kupitia haya, isitoshe huwezi kuendelea mbele. Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa. Kabla ya hitimisho ya mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000—kabla ya Yeye kuweka wazi mwisho wa kila aina ya binadamu—kazi ya Mungu ulimwenguni utakuwa kwa ajili ya wokovu, yote haya ni ili kuwafanya wale wanaompenda Yeye kukamilika kabisa, na kuwarejesha katika utawala Wake. Bila kujali jinsi ambavyo Mungu huwaokoa watu, yote hufanywa kwa kuwafanya wajitenge na asili yao ya zamani ya kishetani; yaani, Yeye huwaokoa kwa kuwafanya watafute uzima. Wasipotafuta uzima basi hawatakuwa na njia yoyote ya kukubali wokovu wa Mungu. Wokovu ni kazi ya Mungu Mwenyewe na kutafuta uzima ni kitu ambacho mwanadamu anapaswa kumiliki ili kupokea wokovu. Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa kwa baraka na neema Zake, ili kwamba waweze kumpa Mungu mioyo yao. Hivyo ni kusema, Yeye kumgusa mwanadamu ni kumwokoa. Aina hii ya wokovu inafanywa kwa kufanya makubaliano. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu atatiimbele ya jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Wokovu uliopewa leo unatokea wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, iwe hukumu ya haki au usafishaji na adhabu visivyo na huruma, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kila anaainishwa kulingana na aina yake, ama makundi ya wanadamu yanafichuliwa, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na hivyo, mbinu ya leo ya wokovu haifanani na ya kitambo. Leo, kuhukumu kwa haki kunakuokoa wewe, na ni zana nzuri pia ya kumuainisha kila mmoja wenu kulingana na aina, na kuadibu kusiko na huruma kunawaletea wokovu mkubwa—na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? Nyote mmeona Mungu mwenye mwili na kutambua kudura na hekima Yake; zaidi ya hayo, umepitia hali ya kupigwa na kufundishwa nidhamu mara kwa mara. Lakini je, hujapokea pia neema kubwa? Je, baraka zako si kubwa zaidi kuliko za mtu yeyote mwingine? Neema zako ni nyingi zaidi kuliko utukufu na utajiri uliofurahiwa na Sulemani! Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Mngeweza, enyi viumbe wenye dhambi wa mwili na damu, kuishi hadi leo? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, kuwaadhibu ninyi wanadamu wa kufa hakuwezi kufanywa kwa kutamka neon moja tu? Ningekuwa bado na haja ya kuwaangamiza baada ya kuwashutumu kwa makusudi? Je, bado hamwamini haya maneno Yangu? Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia tu kwa upendo na huruma? Au Ningetumia tu kusulubishwa kwa minajili ya kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki si nzuri zaidi ya kumfanya mwanadamu kuwa mtiifu kabisa? Je, haiwezi kabisa kumwokoa mwanadamu zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zote zilizorudiwa zinapenyeza mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri kwa njia ya moja kwa moja hatima yao na inalenga kujeruhi mioyo yao ili waweze kuachilia yale mambo hayo yote na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kadri aina hii ya kuadibu na kuhukumu inavyozidi, ndivyo moyo wa binadamu unavyoweza kujeruhiwa zaidi na ndivyo roho yake inavyoweza kuzinduliwa zaidi. Kuzindua roho za watu hawa waliopotoka pakubwa na kudanganywa kabisa ndiyo shabaha ya aina hii ya hukumu. Mwanadamu hana roho, yaani, roho yake ilikufa kitambo na hajui kwamba kuna Mbingu, hajui kwamba kuna Mungu, na bila shaka hajui kwamba yeye mwenyewe anang’ang’ana kwenye lindi kuu la kifo; anaweza kujuaje kwamba anaishi katika kuzimu hii yenye maovu hapa ulimwenguni? Angewezaje kujua kwamba maiti hii yake ambayo imeoza, kwa kupotoshwa na shetani, imeanguka Kuzimuni kwenye kifo? Angewezaje kujua kwamba kila kitu hapa ulimwenguni kimeharibiwa kitambo kiasi cha kutokarabatika na mwanadamu? Na angewezaje kujua kwamba Muumba amekuja ulimwenguni leo na anatafuta kundi la watu waliopotoka ambao Anaweza kuokoa? Hata baada ya mwanadamu kupitia kila usafishaji na hukumu inayowezekana, ufahamu wake wa chini unashtuka kwa shida na kwa kweli hauitikii chochote. Binadamu wamezoroteka kweli! Ingawa aina hii ya hukumu ni kama mvua katili ya mawe inyeshayo kutoka mbinguni, ni yenye manufaa makubwa zaidi kwa binadamu. Kama isingekuwa ya kuhukumu watu hivi, kusingekuwa na matokeo yoyote na haingewezekana kabisa kuwaokoa watu dhidi ya janga la umaskini. Kama isingekuwa kwa kazi hii, ingekuwa vigumu sana kwa watu kutoka Kuzimuni kwa sababu mioyo yao imekufa kitambo na roho zao kukanyagiwa kitambo na Shetani. Kuwaokoa nyinyi ambao mmeanguka kwenye kina kirefu cha uozo kunahitaji kuwaita kwa bidii sana, kuwahukumu kwa bidii sana, na kwa kufanya hivi tu ndipo mioyo hiyo yenu migumu itakapozinduka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Nyinyi nyote mnaishi mahala pa dhambi na ufisadi; nyinyi nyote ni watu wapotovu na wenye dhambi. Leo hii hamwezi tu kumwona Mungu, ila la muhimu zaidi, mmepokea kuadibu na hukumu, mmepokea wokovu wa kina, yaani, mmepokea upendo mkubwa zaidi wa Mungu. Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anawahukumu kwa sababu ya dhambi zenu, ili kwamba mweze kujichunguza wenyewe na kupokea wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kwa kusudi la kumkamilisha mwanadamu. Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angalikuchukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kukuongoza wewe Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. Kwa kuwa hamjui jinsi ya kuishi, na mnaishi katika mahala pa ufisadi na dhambi na ni mapepo wenye ufisadi na uchafu, Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya kushinda miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu. Iwapo huwezi kuona kuwa kila kitu unachofanyiwa ni mapenzi na wokovu, ukidhani kuwa ni mbinu tu, njia ya kumtesa mwanadamu na kitu kisichoaminika, basi ni bora urudi duniani mwako uendelee kupata mateso na ugumu wa maisha! Ikiwa uko tayari kuwa kwenye mkondo huu na kufurahia hukumu hii na wokovu huu wa ajabu, na kufurahia baraka hizi ambazo haziwezi kupatikana kokote katika ulimwengu wa wanadamu, na kufurahia upendo huu, basi kuwa mzuri: Salia kwenye mkondo huu ili kukubali kazi ya ushindi ili uweze kufanywa mkamilifu. Leo, unaweza kupitia mateso na usafishaji kidogo kwa sababu ya hukumu ya Mungu, mateso haya ni ya thamani na ya maana. Japo kuadibu na hukumu ni usafishaji na ufichuzi usio na huruma kwa mwanadamu, uliokusudiwa kuadhibu dhambi zake na kuadhibu mwili wake, kazi hii haijanuiwa kukashifu na kuuzima mwili wake. Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi. Ninyi wenyewe mmeipitia sana kazi hii na ni wazi, haijawaongoza kwenye njia mbaya! Yote ni ili kukufanya uishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na yote yanatimizwa na ubinadamu wako wa kawaida. Kila hatua ya kazi hufanywa kwa misingi ya mahitaji yako, kulingana na udhaifu wako, kulingana na kimo chako halisi, na hamjatwikwa mzigo msioweza kuubeba. Japo huwezi kuliona hili wazi kwa sasa, na unajihisi Ninakuwa mgumu kwako, japo unadhani kuwa Ninakuadibu na kukuhukumu na kukuadibu kila siku kwa kuwa Ninakuchukia, na ingawa unachokipokea ni kuadibu na hukumu, hali halisi ni kuwa yote ni mapenzi kwako, pia ni ulinzi mkubwa kwako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)

Mungu alipata mwili katika mahali palipokuwa nyuma kimaendeleo na pachafu zaidi, na ni kwa njia hii tu ndiyo Mungu anaweza kuonyesha wazi tabia Yake yote iliyo takatifu na yenye haki. Na tabia Yake yenye haki inaonyeshwa kupitia nini? Inaonyeshwa Anapozihukumu dhambi za mwanadamu, Anapomhukumu Shetani, Anapochukia dhambi sana, na Anapowadharau maadui wanaompinga na kuasi dhidi Yake. Maneno Ninayonena leo ni kwa ajili ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, kuhukumu udhalimu wa mwanadamu, kulaani uasi wa mwanadamu. Upotovu na udanganyifu wa mwanadamu, maneno na vitendo vya mwanadamu—yote ambayo hayapatani na mapenzi ya Mungu lazima yatapitia hukumu, na uasi wa mwanadamu kushutumiwa kama dhambi. Maneno Yake yanahusu kanuni za hukumu; Yeye hutumia hukumu ya udhalimu wa mwanadamu, laana ya uasi wa mwanadamu, na mfichuo wa asili mbaya za mwanadamu ili kudhihirisha tabia Yake mwenyewe yenye haki. Utakatifu ni kielelezo cha tabia Yake yenye haki, na kwa kweli utakatifu wa Mungu ni tabia Yake yenye haki. Tabia zenu potovu ni muktadha wa maneno ya leo—Ninazitumia kunena na kuhukumu, na kutekeleza kazi ya ushindi. Hii pekee ndiyo kazi halisi, na hii pekee inadhihirisha kabisa utakatifu wa Mungu. Ikiwa hakuna dalili ya tabia potovu ndani yako, basi Mungu hatakuhukumu, wala hatakuonyesha tabia Yake yenye haki. Kwa kuwa unayo tabia potovu, Mungu hatakusamehe, na ni kwa njia hii ndiyo utakatifu Wake unaonyeshwa. Mungu angaliona kuwa uchafu na uasi wa mwanadamu vilikuwa vikubwa sana lakini Asinene au kukuhukumu, wala kukuadibu kwa ajili ya udhalimu wako, basi hii ingethibitisha kwamba Yeye si Mungu, kwa maana Asingeichukia dhambi; Angelikuwa mchafu sawasawa na mwanadamu. Leo, ni kwa sababu ya uchafu wako ndiyo Ninakuhukumu, na ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako ndiyo Ninakuadibu. Mimi sijivunii nguvu Zangu kwenu au kuwadhulumu kwa makusudi; Ninafanya mambo haya kwa sababu ninyi, ambao mmezaliwa katika nchi hii ya uchafu, mmenajisiwa vikali kwa uchafu. Mmepoteza uadilifu na ubinadamu wenu kabisa na mmekuwa kama nguruwe waliozaliwa katika pembe chafu zaidi za ulimwengu, na kwa hiyo ni kwa sababu ya jambo hili ndiyo mnahukumiwa na ndiyo Ninawaachia huru hasira Yangu. Ni kwa sababu hasa ya hukumu hii ndiyo mmeweza kuona kuwa Mungu ndiye Mungu mwenye haki, na kwamba Mungu ndiye Mungu mtakatifu; ni kwa sababu hasa ya utakatifu Wake na haki Yake ndiyo Anawahukumu na kuachia huru hasira Yake juu yenu. Kwa sababu Anaweza kufichua tabia Yake yenye haki Aonapo uasi wa mwanadamu, na kwa sababu Anaweza kufichua utakatifu Wake anapoona uchafu wa mwanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na wa asili, na bado Anaishi katika nchi ya uchafu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa

Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu. Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Iliyotangulia: 2. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

Inayofuata: 4. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp