4. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji
Maneno Husika ya Mungu:
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. …
Ikiwa hujui tabia ya Mungu, bila shaka utaanguka wakati wa majaribu, kwa kuwa hufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu kuwa wakamilifu, na ni kwa njia gani Huwafanya wakamilifu, na majaribu ya Mungu yakikushukia na yasilingane na mawazo yako, utashindwa kusimama imara. Upendo wa kweli wa Mungu ni tabia Yake kamili, na tabia kamili ya Mungu inapoonyeshwa kwa watu, hili linauletea mwili wako nini? Tabia ya haki ya Mungu inapoonyeshwa kwa watu, bila shaka miili yao iapata uchungu mkubwa zaidi. Iwapo hutapata haya maumivu, basi huwezi kufanywa mkamilifu na Mungu, wala huwezi kumpa Mungu mapenzi ya kweli. Mungu akikufanya mkamilifu kwa hakika atakuonyesha tabia Yake kamili. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu hajawahi kumwonyesha mwanadamu tabia Yake kamili—ila katika siku za mwisho Anaifichua kwa hili kundi la watu ambao Aliwateua awali na kuwachagua, na kwa kuwafanya watu wakamilifu, Anaiweka wazi tabia Yake, na kupitia kwayo Analifanya kamili kundi la watu. Huo ndio upendo wa kweli wa Mungu kwa watu. Kuyapitia mapenzi ya kweli ya Mungu kunawapasa watu wastahimili uchungu mkali, na kulipa gharama kubwa. Ni baada tu ya hili ndipo watapatikana na Mungu na waweze kutoa tena mapenzi ya kweli kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo Moyo wa Mungu utaridhishwa. Ikiwa watu wanataka wafanywe wakamilifu na Mungu, na kama wanataka kufanya na mapenzi Yake, na kumpa Mungu mapenzi yao ya dhati kikamilifu, ni sharti wapitie mateso mengi na maumivu makali kutokana na hali hizo, kupata uchungu mkali kuliko mauti, hatimaye watashurutishwa kuirejesha mioyo yao ya kweli kwa Mungu. Ikiwa mtu anampenda Mungu kwa dhati au la, itafichuliwa wakati wa shida na usafishaji. Mungu hutakasa mapenzi ya watu, na hili vilevile hupatikana tu ndani ya shida na usafishaji.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli
Anapokabiliwa na hali ya mwanadamu na mtazamo wake kwa Mungu, Mungu amefanya kazi mpya, Akimruhusu mwanadamu kuwa na ufahamu Wake na utiifu Kwake, na upendo pia na ushahidi. Hivyo, mwanadamu lazima apitie usafishaji wa Mungu kwake, na pia hukumu, ushughulikiaji na upogoaji Wake kwake, ambazo pasi nazo mwanadamu hangewahi kumjua Mungu, na hangewahi kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli na kuwa na ushuhuda Kwake. Usafishaji wa Mungu kwa mwanadamu sio tu kwa ajili ya athari inayoegemea upande mmoja, bali kwa ajili ya athari inayogusia pande nyingi. Ni kwa jinsi hii tu ndiyo Mungu hufanya kazi ya usafishaji kwa wale ambao wako tayari kutafuta ukweli, ili upendo na uamuzi wao ufanywe timilifu na Mungu. Kwa wale walio tayari kuutafuta ukweli na wanaomtamani Mungu, hakuna kilicho cha maana zaidi, au cha usaidizi zaidi, kuliko usafishaji kama huu. Tabia ya Mungu haijulikani wala kueleweka kwa urahisi sana na mwanadamu, kwani Mungu, hatimaye, ni Mungu. Mwishowe, haiwezekani kwa Mungu kuwa na tabia sawa na mwanadamu, na hivyo si rahisi kwa mwanadamu kujua tabia Yake. Ukweli haumilikiwi kwa asili na mwanadamu, na hauleweki kwa urahisi na wale ambao wamepotoshwa na Shetani; mwanadamu hana ukweli na hana azimio la kutia ukweli katika vitendo, na asipoteseka, na asisafishwe au kuhukumiwa, basi uamuzi wake hautawahi kufanywa timilifu. Kwa watu wote, usafishaji ni wa kutesa sana na ni mgumu sana kukubali—ilhali ni katika usafishaji ndipo Mungu huweka wazi tabia Yake ya haki kwa mwanadamu, na Huweka hadharani mahitaji Yake kwa mwanadamu, na Hutoa nuru zaidi, na upogoaji na ushughulikiaji halisi zaidi; kwa kulinganisha mambo ya hakika na ukweli, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi kujihusu na ukweli, na Humpa mwanadamu ufahamu mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu, hivyo kumruhusu mwanadamu kuwa na upendo wa kweli zaidi na safi zaidi wa Mungu. Haya ndiyo malengo ya Mungu katika kutekeleza usafishaji. Kazi yote Afanyayo Mungu kwa mwanadamu ina malengo yake na maana yake; Mungu hafanyi kazi isiyo na maana, wala Hafanyi kazi isiyo na manufaa kwa mwanadamu. Usafishaji haumaanishi kuondoa watu kutoka mbele ya Mungu, wala haumaanishi kuwaangamiza katika kuzimu. Unamaanisha kubadilisha tabia ya mwanadamu wakati wa usafishaji, kubadilisha motisha zake, mitazamo yake ya kale, kubadilisha upendo wake kwa Mungu, na kubadilisha maisha yake yote. Usafishaji ni jaribio la kweli la mwanadamu, na aina ya mafunzo halisi na ni wakati wa usafishaji tu ndipo upendo wake unaweza kutimiza wajibu wake wa asili.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli
Kadiri usafishaji wa Mungu ulivyo mkubwa, ndivyo mioyo ya watu inaweza kumpenda Mungu zaidi. Mateso ndani ya mioyo yao ni ya manufaa kwa maisha yao, wanaweza zaidi kuwa na amani mbele ya Mungu, uhusiano wao na Mungu ni wa karibu zaidi, na wanaweza kuona vizuri zaidi upendo wa juu kabisa wa Mungu na wokovu Wake wa juu kabisa. Petro alipitia usafishaji mamia ya mara, na Ayubu alipitia majaribio kadhaa. Ikiwa mngependa kufanywa kamili na Mungu, nyinyi pia sharti mpitie usafishaji mamia ya mara; ni ikiwa tu mtapitia mchakato huu, na mtegemee hatua hii, ndiyo mnaweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, na kufanywa kamili na Mungu. Usafishaji ndio njia bora zaidi ambayo Mungu hutumia kuwafanya watu kamili; usafishaji na majaribio makali pekee ndiyo yanaweza kusababisha kuonekana upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo ya watu. Bila taabu, watu hukosa upendo wa kweli kwa Mungu; ikiwa hawajaribiwi ndani, na hawapitii usafishaji kwa kweli, basi mioyo yao daima itakuwa ikielea kwa nje. Baada ya kusafishwa hadi kiwango fulani, utayaona mapungufu na matatizo yako mwenyewe, utaona kiasi ambacho unakosa na kwamba huwezi kuzishinda zile shida nyingi unazokabiliwa nazo, na utaona jinsi kutotii kwako kulivyo kukubwa. Ni katika majaribu pekee ndipo watu wataweza kujua kwa kweli hali zao halisi, na majaribu huwafanya watu waweze kufanywa kamili vyema.
Katika maisha yake, Petro alipitia usafishaji mamia ya mara na alipitia majaribu mengi ya uchungu. Usafishaji huu ukawa msingi wa upendo wake mkubwa kabisa kwa Mungu na ukawa uzoefu muhimu zaidi katika maisha yake yote. Kwamba aliweza kuwa na upendo mkubwa kabisa wa Mungu ilikuwa, kwa namna moja, kwa sababu ya uamuzi wake kumpenda Mungu; la muhimu zaidi, hata hivyo, ilikuwa kwa sababu ya usafishaji na mateso aliyopitia. Mateso haya yakawa mwongozo wake katika njia ya kumpenda Mungu, na yakawa jambo lililokumbukwa zaidi kwake. Ikiwa watu hawapitii uchungu wa usafishaji wanapompenda Mungu, basi upendo wao umejaa uchafu na mapendeleo yao wenyewe; upendo kama huu umejaa mawazo ya Shetani, na hauwezi hata kabisa kuridhisha mapenzi ya Mungu. Kuwa na azimio la kumpenda Mungu sio sawa na kumpenda Mungu kwa kweli. Hata ingawa yote wanayofikiria mioyoni mwao ni kwa ajili ya kumpenda Mungu, na kumridhisha Mungu, kana kwamba fikira zao hazina mawazo yoyote ya kibinadamu, kana kwamba zote ni kwa ajili ya Mungu, fikira zao zinapoletwa mbele ya Mungu, fikira kama hizi hazisifiwi wala kubarikiwa na Mungu. Hata wakati watu wameelewa kikamilifu ukweli wote—wakati wamekuja kuujua wote—hili haliwezi kusemwa kuwa ishara ya kumpenda Mungu, haiwezi kusemwa kwamba watu hawa hakika wanampenda Mungu. Licha ya kuelewa ukweli mwingi bila kupitia usafishaji, watu hawana uwezo wa kutia ukweli huu katika vitendo; ni wakati wa usafishaji tu ndipo watu wanaweza kuelewa maana halisi ya ukweli huu, hapo tu ndipo watu wanaweza kufahamu kwa kweli maana yao ya ndani. Wakati huo, wanapojaribu tena, wanaweza kutia ukweli katika vitendo kwa njia ya kufaa, na kulingana na mapenzi ya Mungu; wakati huo, mawazo yao ya kibinadamu yanapunguzwa, upotovu wao wa kibinadamu unapunguzwa, na hisia zao za kibinadamu zinapunguzwa; ni wakati huo tu ndipo utendaji wao ni onyesho la ukweli la upendo wa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli
Wakati Mungu anafanya kazi ili kumsafisha mwanadamu, mwanadamu huteseka. Kadiri usafishaji wa mtu ulivyo mkubwa, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa mkubwa zaidi na ndivyo nguvu za Mungu zitakavyofichuliwa zaidi kwake. Kinyume chake, kadiri mtu apokeavyo usafishaji mdogo zaidi, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa kwa kiwango kidogo zaidi, na ndivyo nguvu za Mungu zitakavyofichuliwa kwake kwa kiwango kidogo zaidi. Kadiri usafishaji na uchungu wa mtu kama huyo ulivyo mkubwa na kadiri anavyopitia mateso mengi zaidi, ndivyo upendo wake kwa Mungu utakavyokuwa, ndivyo imani yake kwa Mungu itakavyokuwa ya kweli zaidi, na ndivyo maarifa yake ya Mungu yatakavyokuwa ya kina zaidi. Katika matukio unayopitia, utawaona watu wanaoteseka sana wanapokuwa wakisafishwa, wanaoshughulikiwa na kufundishwa nidhamu sana, na utaona kwamba ni watu hao ndio walio na upendo mkubwa kwa Mungu na maarifa ya kina na elekevu ya Mungu. Wale ambao hawajapitia kushughulikiwa wanayo maarifa ya juu juu tu, na wao wanaweza tu kusema: “Mungu ni mzuri sana, Yeye huwapa watu neema ili waweze kumfurahia Yeye.” Kama watu wamepitia kushughulikiwa na kufundishwa nidhamu, basi hao wanaweza kuzungumza kuhusu maarifa ya kweli ya Mungu. Hivyo kazi ya Mungu katika mwanadamu ilivyo ya ajabu zaidi, ndivyo ilivyo ya thamani zaidi na ni muhimu zaidi. Kadiri inavyokosa kupenyeza kwako zaidi na kadiri isivyolingana na mawazo yako, ndivyo kazi ya Mungu inavyoweza kukushinda, kukupata, na kukufanya mkamilifu. Umuhimu wa kazi ya Mungu ni mkubwa ulioje! Kama Mungu hangemsafisha mwanadamu kwa njia hii, kama Hangefanya kazi kulingana na njia hii, basi kazi Yake haingekuwa na ufanisi na ingekuwa isiyo na maana. Ilisemwa hapo awali kwamba Mungu angelichagua na kulipata kundi hili na kuwakamilisha katika siku za mwisho; hili lina umuhimu mkubwa sana. Kadiri kazi Anayofanya ndani yenu ilivyo kuu, ndivyo upendo wenu kwa Mungu ulivyo mkubwa na safi. Kadiri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi, ndivyo mwanadamu anavyoweza kuelewa kitu kuhusu hekima Yake na ndivyo maarifa ya mwanadamu Kwake yalivyo ya kina zaidi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji
Katika hali hasi, wewe ni dhaifu na hasi, na huhisi kuwa huna Mungu moyoni mwako, lakini Mungu hukuangaza, akikusaidia kupata njia ya kutenda. Kutoka nje ya hili ni kupata ukamilisho katika hali chanya. Mungu anaweza kumkamilisha mwanadamu katika vipengele hasi na chanya. Inategemea kama unaweza kupata uzoefu, na kama wewe hufuatilia kukamilishwa na Mungu. Kama kwa hakika unatafuta kukamilishwa na Mungu, basi kilicho hasi hakiwezi kukufanya upoteze, lakini kinaweza kukuletea mambo ambayo ni halisi zaidi, na kinaweza kukufanya uweze zaidi kujua kile kilichopunguka ndani yako, uweze zaidi kufahamu sana hali zako halisi, na kuona kwamba mtu hana kitu, wala si kitu; kama hupitii majaribio, hujui, na daima utahisi kuwa wewe ni wa hadhi ya juu kuliko wengine na bora kuliko kila mtu mwingine. Kwa njia hii yote utaona kwamba yote yaliyotangulia yalifanywa na Mungu na kulindwa na Mungu. Kuingia katika majaribio hukuacha bila upendo au imani, huna sala, na huwezi kuimba nyimbo—na, bila kulitambua, katikati ya hili unakuja kujijua. Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua “siri” katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa
Katika imani yao kwa Mungu, kile ambacho watu hutafuta ni kupata baraka kwa ajili ya siku zijazo; hili ndilo lengo lao katika imani yao. Watu wote wana kusudi na tumaini hili, lakini upotovu ulio katika asili yao lazima uondolewe kupitia majaribu. Katika hali ambazo bado hujatakaswa, hizi ndizo hali ambamo lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili uweze kujua upotovu wako mwenyewe. Hatimaye, unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu. Kwa hiyo, ikiwa watu hawana miaka kadhaa ya usafishaji, wasipovumilia kiwango fulani cha mateso, hataweza kujiondolea vifungo vya upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yake. Katika hali zozote zile ambazo bado ungali mtumwa wa Shetani, na katika hali zozote zile ambazo bado ungali na tamaa zako mwenyewe na matakwa yako mwenyewe, hizi ndizo hali ambamo unapaswa kuteseka. Ni kupitia mateso tu ndiyo mafunzo yanaweza kupatikana, kuweza kupata ukweli, na kuelewa mapenzi ya Mungu. Kwa kweli, ukweli mwingi unafahamika kwa kupitia majaribu makali. Hakuna anayeweza kufahamu mapenzi ya Mungu, kutambua uweza na busara ya Mungu, wala kuiona tabia ya haki ya Mungu anapokuwa katika mazingira ya utulivu na rahisi au wakati hali ni nzuri. Hilo halingewezekana!
Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi Mtu Anapaswa Kumridhisha Mungu Katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo