Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 16

Baada ya ushuhudiaji wa Mwana wa Adamu, Mwenyezi Mungu alijifichua kwetu hadharani kama Jua la haki. Haya ndiyo mabadiliko mlimani! Sasa inakuwa halisi zaidi na zaidi, na zaidi kuwa jambo la uhalisi. Tumeona utaratibu wa kazi ya Roho Mtakatifu, Mungu Mwenyewe ameibuka kutoka kwa mwili wa damu. Yeye hayuko chini ya udhibiti wa mwanadamu, wala anga, wala jiografia; Yeye huvuka mipaka ya nchi na bahari, Yeye hufika miisho halisi ya ulimwengu, na mataifa yote na watu wa jumuia zote wanasikiliza sauti Yake kwa utulivu. Tunapofungua macho yetu ya kiroho tunaona kuwa neno la Mungu limetokea kwa mwili Wake mtukufu; ni Mun gu Mwenyewe anayetokea kutoka kwa mwili. Yeye ni Mungu Mwenyewe halisi na kamili. Yeye husema nasi hadharani, Yeye yuko nasi uso kwa uso, Yeye hutushauri, Yeye hutuhurumia, Yeye hutusubiri, Yeye hutufariji, Yeye hutufundisha nidhamu na hutuhukumu. Yeye hutuongoza kwa mkono na utunzaji Wake kwetu huwasha kama ulimi wa moto ndani Yake, kwa moyo wa hamu Yeye hutuharakisha kuamka na kuingia ndani Yake. Maisha Yake yanayozidi uwezo wa binadamu yameguzishwa ndani yetu sote, na wote wanaoingia ndani Yake watavuka mipaka na kuushinda ulimwengu na wale wote waovu, na kutawala pamoja naye! Mwenyezi Mungu ni mwili wa kiroho wa Mungu. Yeye akiliamua, ndivyo litakavyokuwa; Yeye akiliongea, litakuwa, na Yeye akiliamrisha, basi ndivyo; Yeye ndiye Mungu mmoja wa kweli! Shetani yuko chini ya miguu Yake, katika shimo la kuzimu. Kila kitu katika ulimwengu kimo mikononi Mwake; wakati umefika, na wote watarudi katika hali ya kutokuwepo na kuzaliwa upya.

Iliyotangulia:Sura ya 15

Inayofuata:Sura ya 17

Maudhui Yanayohusiana

 • Kazi na Kuingia (4)

  Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira…

 • Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

  Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II) Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wak…

 • Mazungumzo Mafupi Kuhusu “Ufalme wa Milenia Umefika”

  Mnayaonaje maono ya Ufalme wa Milenia? Baadhi ya watu hutafakari sana kuuhusu na kusema kuwa Ufalme wa Milenia utadumu duniani kwa miaka elfu moja, h…

 • Maono ya Kazi ya Mungu (1)

  Yohana alimfanyia Yesu kazi kwa miaka saba, na tayari alikuwa ameandaa njia Yesu alipofika. Kabla ya haya, injili ya ufalme wa mbinguni iliyohubiriwa…