Sura ya 15

Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiye anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, aliyevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi. Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume, upanga mkali wenye makali kuwili uko katika kinywa Chake na uso Wake ni kama jua liking’aa kwa nguvu zake!

Mwana wa Adamu Ameshuhudiwa, na Mungu Mwenyewe amefichuliwa waziwazi. Utukufu wa Mungu umekuja, uking’aa vikali kama jua lichomalo! Uso Wake mtukufu unawaka kwa mwanga ung’aao; ni macho ya nani yatathubutu kumtendea kwa upinzani? Upinzani husababisha kifo! Hakuna hata chembe ya rehema kwa kitu chochote unachofikiri katika moyo wako, neno lolote usemalo au chochote ufanyacho. Nyinyi nyote mtakuja kuelewa na kuja kuona ni nini ambacho mmekipata—hakuna chochote ila hukumu Yangu! Naweza kukistahimili wakati nyinyi hamuweki juhudi zenu katika kula na kunywa maneno yangu, lakini hudakiza kiholela na kuharibu ujenzi Wangu? Mimi sitamhurumia mtu wa aina hii! Mengine makubwa zaidi na utaangamizwa katika moto! Mwenyezi Mungu hudhihirika katika mwili wa kiroho, bila hata chembe ya mwili au damu ikiunganisha mwili mzima. Yeye huvuka mipaka ya ulimwengu dunia, kama Ameketi kwenye kiti kitukufu cha enzi katika mbingu ya tatu, Akisimamia mambo yote! Ulimwengu na vitu vyote vimo mikononi Mwangu. Kama Nikisema, itakuwa. Kama Nikiliamua, ndivyo litakavyokuwa. Shetani yu chini ya miguu Yangu, yu katika kuzimu! Sauti Yangu itakapotoka, mbingu na nchi zitapita na kuwa bure! Mambo yote yatafanywa upya na huu ni ukweli wa kweli sana usiobadilika. Nimeushinda ulimwengu, kuwashinda waovu wote. Naketi hapa nikizungumza nanyi; wale wote ambao wana masikio wanapaswa kusikiliza na wale wote wanaoishi wanapaswa kukubali.

Siku zitafika mwisho; mambo yote katika dunia yatakuwa bure, na mambo yote yatazaliwa upya. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Hapawezi kuwa na utata! Mbingu na nchi zitapita lakini maneno Yangu hayatapita! Acha Niwasihi kwa mara nyingine tena: Msikimbie bure! Amkeni! Tubuni na wokovu umekaribia! Tayari Nimeonekana miongoni mwenu na sauti Yangu imetokea. Sauti yangu imetokea mbele yenu, uso kwa uso na nyinyi kila siku, safi na mpya kila siku. Unaniona Mimi na Ninakuona wewe, Ninasema na wewe mara kwa mara, uso kwa uso na wewe. Na, bado unanikataa Mimi, hunijui Mimi; Kondoo Wangu wasikia sauti Yangu na bado mnasita! Mnasita! Mioyo yenu imepumbaa, macho yenu yamepofushwa na Shetani na hamuwezi kuuona uso Wangu mtukufu—ni kusikitisha kulikoje! Kusikitisha kulikoje!

Roho saba mbele ya kiti Changu cha enzi watumwa kwa kila pembe ya dunia na Mimi Nitamtuma Mjumbe Wangu kuzungumza kwa makanisa. Mimi ni mwenye haki na mwaminifu, Mimi ni Mungu achunguzaye sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mtu. Roho anaongea na makanisa na ni maneno Yangu yanayotiririka kutoka ndani ya Mwanangu; wale wote ambao wana masikio wanapaswa kusikiliza! Wale wote ambao wanaishi wanapaswa kukubali! Yaleni tu na kuyanywa, na msitilie shaka. Wale wote ambao huyatii na kuyasikiza maneno Yangu watapokea baraka kuu! Wale wote wautafutao uso Wangu kwa kweli watapata mwanga mpya kwa hakika, nuru mpya na ufahamu mpya; wote watakuwa wasafi na wapya. Maneno Yangu yataonekana kwako wakati wowote na yatafungua macho ya roho yako ili uweze kuona siri zote za ulimwengu wa kiroho na kwamba ufalme uko miongoni mwa binadamu. Ingia katika hifadhi na neema yote na baraka zitakuwa juu yako, njaa na baa hazitaweza kukugusa, mbwa mwitu, nyoka, chui wakubwa na chui hawataweza kukudhuru. Utaenda na Mimi, utembee na Mimi, na uingie katika utukufu pamoja na Mimi!

Mwenyezi Mungu! Mwili Wake mtukufu waonekana wazi wazi, mwili mtakatifu wa kiroho watokea na Yeye ndiye Mungu Mwenyewe kamili! Dunia na mwili vyote vimegeuzwa na mabadiliko Yake juu ya mlima ambaye ni nafsi ya Mungu. Amevaa taji la dhahabu kichwani, mavazi Yake ni meupe kabisa, kifuani ana ukanda wa dhahabu na vitu vyote katika dunia ni mahali pa kuweka miguu yake. Macho Yake ni kama mwale wa moto, na upanga mkali wenye makali kuwili uko ndani ya kinywa Chake na Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume. Njia ya kwenda kwa ufalme ni ng’avu bila kikomo na utukufu Wake watokea na kuangaza; milima huwa na furaha na maji hucheka, jua, mwezi na nyota zote zazunguka kwa mpango wao wa taratibu, ukimkaribisha Mungu wa kweli na wa kipekee, ambaye kurudi kwake kwa ushindi kunaashiria ukamilisho wa miaka elfu sita ya mpango Wake wa usimamizi. Zote zaruka na kucheza kwa furaha! Shangilia! Mwenyezi Mungu amekaa juu ya kiti Chake kitukufu cha enzi! Imbeni! Bendera ya ushindi ya Mwenyezi inainuliwa juu ya mlima mwadhimu, mtukufu wa Sayuni! Mataifa yote yanashangilia, watu wote wa mataifa wanaimba, Mlima Sayuni unacheka kwa furaha, utukufu wa Mungu umetokea! Hata katika ndoto Sijawahi kufikiri kwamba Ningeuona uso wa Mungu lakini leo Nimeuona. Uso kwa uso na Yeye kila siku, nauweka wazi moyo wangu Kwake. Yeye kwa ukarimu hutoa vyote vinavyoliwa na kunywewa. Maisha, maneno, matendo, mawazo, nia—mwanga Wake mtukufu huwatia nuru wote. Yeye huongoza kila hatua ya njia, na kama moyo wowote ni muasi basi hukumu Yake itatokea mara moja.

Kula pamoja na Mungu, kukaa pamoja, kuishi pamoja, kuwa pamoja na Yeye, kutembea pamoja, kufurahia pamoja, kupata utukufu na baraka pamoja, kushiriki ufalme na Mungu, na kuwa pamoja katika ufalme—oo, ni furaha iliyoje! Oo, ni utamu ulioje! Uso kwa uso kila siku, kuzungumza kila siku, kuzungumza mara kwa mara, kupata nuru upya na ufahamu mpya kila siku. Macho yetu ya kiroho yanafunguliwa na tunaona kila kitu, siri zote za kiroho zinafichuliwa kwetu. Maisha matakatifu si ya kujali. Kimbia kwa haraka na usisite, songa mbele mfululizo, kuna maisha ya ajabu zaidi mbele. Usiridhike tu na ladha tamu lakini siku zote tafuta kuingia ndani ya Mungu. Yeye anajumuisha yote na mkarimu, na Ana kila aina ya vitu ambavyo tumekosa. Shirikiana kwa vitendo, ingia ndani Yake na hakuna kitu kitakachokuwa kama awali tena. Maisha yetu yatakuwa ya uvukaji mipaka na hakuna mtu, jambo, au kitu kitakachoweza kutuvuruga.

Uvukaji mipaka! Uvukaji mipaka! Uvukaji mipaka wa kweli! Maisha ya Mungu ya uvukaji mipaka yako karibu na vitu vyote kwa kweli vinakuwa na pumziko! Tunavuka mipaka ya dunia na mambo ya kidunia, hatuhisi upendo kwa waume au watoto. Tunavuka mipaka ya udhibiti wa ugonjwa na mazingira. Shetani hatothubutu kutuvuruga. Kuvuka kabisa mipaka ya maafa yote—hii ni kumruhusu Mungu kuuchukua ufalme! Tunamkanyaga Shetani chini ya miguu, kuwa shahidi kwa ajili ya kanisa na kuifunua kikamilifu sura mbovu ya Shetani. Ujenzi wa kanisa u katika Kristo, mwili mtukufu umetokea—huku ni kuishi katika hali ya kuchukuliwa kuenda mbinguni!

Iliyotangulia: Sura ya 14

Inayofuata: Sura ya 16

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp