Sura ya 60

Si jambo rahisi kwa maisha kukua; yanahitaji mchakato, na aidha, kwamba muweze kulipa gharama na kwamba mshirikiane na Mimi kwa uwiano, na hivyo mtapata sifa Yangu. Mbingu na dunia na vitu vyote vinaanzishwa na kufanywa kamili kupitia maneno Nitamkayo, na chochote kinaweza kutimizwa nami. Matakwa Yangu ya pekee ni kwamba mkue haraka, mchukue mzigo kutoka kwa mabega Yangu na kuuweka kama wenu, mfanye kazi Zangu kwa niaba Yangu, na hilo litauridhisha moyo Wangu. Ni mwana yupi angekataa mizigo ya babake? Ni baba yupi hangefanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya mwana wake? Lakini ninyi hamwelewi mapenzi Yangu, hamfikirii mizigo Yangu, maneno Yangu hayana maana kwenu na hamfanyi jinsi maneno Yangu yanavyosema. Daima mnajitawala; ninyi ni wabinafsi kiasi gani! Mnajifikiria wenyewe tu!

Je, kwa kweli unaelewa mapenzi Yangu, au unajifanya kutoelewa? Kwa nini daima unajishughulisha na mienendo mitundu kama hiyo? Je, dhamiri yako inasema kuwa unanitendea haki kwa kufanya hivyo? Ukishapata chanzo cha ugonjwa, mbona huwasiliani na Mimi ili upate matibabu? Nitakuambia: Kuanzia siku hii kuendelea hamtakuwa na magonjwa ya mwili tena. Sehemu yenu yoyote ikihisi gonjwa msijishughulishe kutafuta chanzo cha nje. Badala yake, kujeni mbele Yangu na kutafuta kujua nia Yangu—mtakumbuka hili? Hii ni ahadi Yangu: Kuanzia siku hii kuendelea mbele mtaondoka kwa mwili wenu kabisa na kuingia dunia ya roho, yaani, mwili wenu hautasumbuliwa na ugonjwa tena. Mnafurahia hilo? Mnahisi furaha? Hii ni ahadi Yangu na aidha, kile ambacho mmetamani kwa muda mrefu. Leo kimetimika kwa ninyi mliobarikiwa; jambo la ajabu na lisiloeleweka vipi!

Kazi Yangu inaendelea usiku na mchana; muda kwa muda, haikomi kamwe. Hii ni kwa sababu tamaa Yangu ya dharura ni kukufanya uupendeze moyo Wangu, na kwamba moyo Wangu utafarijiwa na ninyi hivi karibuni. Wana Wangu! Wakati umefika wa ninyi kushiriki katika baraka Zangu za wema! Zamani, ninyi mliteseka kwa ajili ya jina Langu, lakini sasa siku zenu za majaribu zimekwisha. Yeyote akijaribu kuumiza unywele kutoka kwa vichwa vya Wanangu, Sitamsamehe kwa urahisi, wala wao hawataweza kuinuka tena. Hii ni amri Yangu ya utawala na yeyote atakayekiuka hii atajihatarisha. Wanangu! Furahieni mpaka mridhike! Imbeni na kuita kwa shangwe! Hamtadhulumiwa na kukandamizwa tena, na hamtapitia mateso tena. Hamtalazimika kuwa waoga juu ya imani yenu Kwangu; mnapaswa kutangaza hadharani imani yenu Liiteni jina Langu takatifu kwa sauti ya kutosha kufanya ulimwengu na miisho ya dunia kutingika. Acha wao waone, wale waliowaangalia kwa dharau, walioangamizwa na kuteswa na wao, leo kuwa na mamlaka juu yao na kuwatawala, waongoze, na, muhimu zaidi, wahukumu.

Mnapaswa kujihusisha na kuingia kwenu pekee, na Nitawapa baraka hata nzuri zaidi ili mweze kuzifurahia, na baraka hizi zitawaruhusu kuonja utamu wao usiolinganika vyema zaidi na kuhisi kwa nguvu siri zao zisizoisha na kwamba ni kubwa sana kuelewa!

Iliyotangulia: Sura ya 59

Inayofuata: Sura ya 61

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp