Sura ya 59

Tafuta mapenzi Yangu zaidi katika mazingira unayoyakabili na kwa hakika utapata kibali Changu. Alimradi uwe tayari kwenda katika utafutaji na kuhifadhi moyo ambao unanicha, Mimi Nitakupea yote unayokosa. Kanisa sasa linaingia utendaji rasmi na mambo yote yanaingia kwenye alama sahihi. Mambo hayako yalivyokuwa wakati ilikuwa limbuko la mambo yajayo; lazima msiwe wa kuchanganyikiwa au mkose utambuzi. Ni kwa nini Mimi nahitaji kwamba muingie ndani ya uhalisi katika kila kitu? Je, kweli umelipitia jambo hili? Je, mnaweza kweli kunikidhi Mimi katika kile Ninachohitaji kwenu, kama vile Ninavyowakidhi nyinyi? Usiwe mdanganyifu! Sio zaidi ya stahamala Yangu kwenu tena na tena na bado hamna uwezo wa kujua ni kipi kizuri kwenu tena na tena, na kukosa kuonyesha shukrani!

Haki Yangu, uadhama Wangu, hukumu Yangu, na upendo Wangu—mambo yote haya Ninayomiliki, mambo Niliyo—je, umeyaonja hayo kwa kweli? Kweli nyinyi ni wapumbavu sana na hamtambui mapenzi Yangu. Nimewaambia tena na tena kwamba ninyi wenyewe lazima muonje karamu Ninazoziandaa, lakini mnazitupa tena na tena na hamuwezi kutofautisha mazingira mazuri na yale mbaya. Ni gani kati ya mazingira haya yamebuniwa na nyinyi wenyewe? Na ni gani ambayo yamepangwa kwa mikono Yangu? Msijitetee! Ninaona kila kitu kwa dhahiri kabisa na ni tu kwamba usitafute. Nini zaidi Ninaweza sema?

Daima Nitawaridhisha ambao wanatambua mapenzi Yangu na Mimi sitawaruhusu wateseke au wapate madhara. Jambo la muhimu sasa ni kwamba mna uwezo wa kuchukua hatua kwa mujibu wa mapenzi Yangu, na wale ambao wanatenda hili kwa hakika watapokea baraka Zangu na kuwa chini ya ulinzi Wangu. Ni nani kati yenu kwa kweli anaweza kabisa kutumia rasilmali kwa ajili Yangu na kutoa yote yao kwa ajili Yangu? Nyinyi nyote mu shingo upande, mawazo yenu yanaenda pande zote, yakifikiria juu ya nyumbani, dunia ya nje, chakula na mavazi. Licha ya ukweli kwamba uko mbele Yangu ukifanya mambo kwa ajili Yangu, katika moyo wako bado unafikiria mke, watoto na wazazi wako walio nyumbani. Je, haya yote ni mali yako? Mbona usiwakabidhi mikononi Mwangu? Je, hunisadiki vya kutosha? Au ni kwamba unahofia Nitafanya mipango isiyofaa juu yako? Mbona daima wewe huwa na wasiwasi kuhusu familia yako ya mwili? Wewe huwatamani sana wapendwa wako! Je, Ninamiliki nafasi fulani moyoni mwako? Na bado unazungumzia kuhusu kuniruhusu Mimi kutawala ndani yako na kumiliki nafsi yako nzima—haya yote ni uongo mdanganyifu! Ni wangapi kati yenu ambao ni wa kanisa kwa mioyo yenu yote? Na ni nani kati yenu hawafikiri juu yao, lakini ni wa ufalme wa leo? Fikiria kwa makini sana kuhusu hili.

Mmenisukuma hadi kiasi hiki, hivyo Ninaweza kutumia tu mikono Yangu kuwachochea mbele; Sitawashawishi tena mbele. Hii ni kwa sababu mimi ni Mungu Mwenye hekima, na Mimi huwatendea watu tofauti kwa njia tofauti, kutegemea jinsi ninyi ni waaminifu Kwangu. Mimi ni Mungu Mwenyezi—ni nani anathubutu kuzuia hatua Zangu za mbele? Yeyote anayethubutu kuniasi, mkono wa amri Zangu za utawala kuanzia sasa kuendelea utakuwa milele juu yao, ili kwamba wapate kujua uweza Wangu. Kile Ninachotaka si idadi kubwa ya watu, lakini ufanisi. Mimi Nitamuacha na kumwadhibu yeyote ambaye ni muasi, mdanganyifu, yeyote anayejishughulisha katika tabia potovu na ya ulaghai. Usifikirie tena kuwa Mimi ni Mwenye rehema, au kwamba Mimi ni mwenye upendo na mkarimu; huku ni wewe kujifurahisha tu. Najua kuwa Nitakavyokuendekeza zaidi ndivyo zaidi unaendelea kuwa hasi na kutoonyesha hisia zaidi, na hutakuwa tayari kujitoa mwenyewe. Wakati watu ni wagumu kwa kiasi hiki Ninaweza tu kuwachochea wao na kuwalazimisha wao mbele wakati wote. Fahamu hili! Kuanzia sasa Mimi ni Mungu Ambaye Anahukumu; Mimi tena si mwenye rehema, mkarimu na mwenye upendo tena wa ubunifu wa mtu!

Iliyotangulia: Sura ya 58

Inayofuata: Sura ya 60

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp