Sura ya 68

Neno Langu linatekelezwa katika kila nchi, mahali, taifa na kikundi, na neno Langu linakamilishwa katika kila pembe wakati wowote. Maafa yanayotokea kila mahali si vita kati ya watu, wala si mapigano na silaha. Hakutakuwa na vita tena baadaye. Wote wako katika mfumbato Wangu. Wote watakabili hukumu Yangu na watadhoofika kati ya maafa. Acha wale wanaonipinga na wale wasioanza kushirikiana na Mimi wateseke uchungu wa maafa mbalimbali. Acha walie na kusaga meno yao hadi milele, na kubaki katika giza daima. Hawataendelea kuishi. Natenda kwa unyoofu na wepesi, na Sifikiri jinsi umekuwa mwaminifu Kwangu zamani. Alimradi unipinge, mkono Wangu wa hukumu utakuachia huru ghadhabu kwa haraka bila kuchelewa hata kidogo, si hata sekunde, na bila chembe ya huruma. Nimekuwa Nikisema wakati huu wote kwamba Mimi ni Mungu anayetimiza neno Lake. Kila neno Ninalolisema litakamilishwa, na mtaona yote. Hii kweli ndiyo maana ya kuingia katika uhalisi katika kila kitu.

Maafa makuu hakika hayatawafikia wana Wangu, wapendwa Wangu. Nitawatunza wana Wangu kila wakati na kila sekunde. Hakika hamtavumilia uchungu na mateso hayo; badala yake, ni kwa ajili ya ukamilishwaji wa wana Wangu na utimizaji wa neno Langu ndani yao, ili kwamba muweze kutambua kudura Yangu, mkue zaidi katika maisha, mbebe mizigo kwa ajili Yangu karibuni, na kujitolea kabisa kwa ukamilisho wa mpango Wangu wa usimamizi. Mnapaswa kuwa na furaha na kuridhika na kushangilia kwa sababu ya hili. Nitawapa kila kitu, Nikiwaruhusu kuchukua usukani. Nitaiweka mikononi mwenu. Mwana akirithi mali nzima ya babake, je, ninyi wana Wangu wazaliwa wa kwanza mtaridhi zaidi kiasi gani? Kweli mmebarikiwa. Badala ya kuteseka kutokana na maafa makuu, mtafurahia baraka za milele. Utukufu ulioje! Utukufu ulioje!

Ongeza kasi yako, na ufuate nyayo Zangu kila mahali na nyakati zote; usibaki nyuma. Acheni mioyo yenu iufuate moyo Wangu, na akili zenu ziifuate akili Yangu. Shirikianeni na Mimi kwa moyo mmoja, akili moja. Kuleni nami, ishi nami, na kufurahia nami. Baraka za ajabu zinawasubiri kufurahia na kuchukua. Kuna utele mwingi usiolinganishika ndani Yangu. Hakuna hata kidogo kimetayarishwa kwa ajili ya mtu mwingine—Nafanya hili kwa ajili ya wana Wangu kabisa.

Sasa, Nilicho nacho akilini ndicho kitakachotimizwa. Punde ambapo Nimemaliza kuwasemea, masuala hayo tayari yamekamilishwa. Kazi kweli inaendelea haraka hivyo na inabadilika wakati wowote. Uangalifu wako ukipotea hata kwa muda, tukio la “kani nje” litatokea, na utatupwa mbali sana, na utaondoka kutoka kwa mkondo huu. Iwapo hamtafuti kwa ari mtaacha juhudi Zangu za uangalifu kuwa bure. Baadaye, watu kutoka mataifa mbalimbali watakusanyika wakati wowote. Katika kiwango chenu cha sasa, mtaweza kuwaongoza? Nitawafunza kikamilifu kuwa askari wazuri katika kipindi hiki kidogo cha muda ili kukamilisha agizo Langu. Ningependa mlitukuze jina Langu katika kila hali na kuwa na ushuhuda wa ajabu kwa ajili Yangu. Acha wale waliowadharau wakue juu yao leo na kuwaongoza na pia kuwatawala. Je, mnaelewa nia Zangu? Mmetambua juhudi Zangu za uangalifu? Nafanya haya yote kwa ajili yenu. Inategemea iwapo mnaweza kufurahia baraka Zangu au la.

Mimi, Mungu anayechunguza akili na moyo wa mwanadamu, Nasafiri kwa miisho ya dunia. Nani anayethubutu kutofanya huduma kwa ajili Yangu? Migogoro inaongezeka miongoni mwa mataifa yote na wanapambana kwa ukali, lakini hatimaye hawataepa kutoka kwa mfumbato Wangu. Hakika Sitawaruhusu waponyoke kwa urahisi. Nitawaleta kwa hukumu mmoja mmoja kwa msingi wa matendo yao, hadhi za kidunia, na raha za dunia. Sitamsamehe yeyote. Hasira Yangu imeanza kufichuliwa na yote itawajia. Yote yatatimizwa ndani yao mmoja mmoja na hiki kitakuwa kile walichojiletea wao wenyewe kabisa. Wale waliokosa kunijua au walionidharau zamani sasa watakabili hukumu Yangu. Na kuhusu wale waliowatesa wana Wangu zamani, hasa Nitawaadibu kwa mujibu wa kile walichokisema na kukifanya. Sitawaacha hata watoto. Wote ni wa namna ya Shetani. Hata wasiposema na kufanya chochote, kama wanawachukia wana Wangu mioyoni mwao, Sitamwacha hata mmoja wao. Nitawafanya wote waone kwamba wale wanaotawala na kushikilia mamlaka leo ni sisi, kundi hili la watu, hakika sio wao. Kwa sababu hii, nyote mnapaswa kutoa nguvu yenu ya juu sana na kwa kweli mjitumie kwa ajili Yangu, ili kulitukuza na kulishuhudia jina Langu katika kila mahali, pembe, dini na dhehebu, na mlieneze katika ulimwengu mzima na miisho ya dunia!

Iliyotangulia: Sura ya 67

Inayofuata: Sura ya 69

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp