Sura ya 64

Unapaswa kutoelewa maneno Yangu kwa njia ya upuuzi; unapaswa kuelewa maneno Yangu kwa kuangalia vipengele vyote na unapaswa kujaribu kuyaelewa zaidi na kuyafikiri sana kwa kurudia, sio tu kwa siku moja ama usiku mmoja. Hujui mahali ambapo mapenzi Yangu yapo ama ni katika kipengele kipi Nalipa gharama Yangu ya bidii za kazi; unawezaje kuyazingatia mapenzi Yangu? Ninyi watu mko hivi; hamna uwezo wa kuchunguza kwa utondoti, mkisisitiza tu sehemu ya juu na mkiwa tu na uwezo wa uigaji. Hii inawezaje kuitwa mambo ya roho? Ni shauku ya mwanadamu tu, ni kile ambacho Sikisifu na zaidi ni kile ambacho Nakichukia sana. Nakwambia, vitu vyote ambavyo Navichukia sana lazima viondolewe, lazima vidhoofike katika maafa, na lazima vipitie uchomaji Wangu na hukumu Yangu. Vinginevyo watu hawatajua “hofu” inamaanisha nini na watakuwa wamepotoshwa sana, daima wakiniona na macho ya mwanadamu—ni wapumbavu sana! Kuja karibu na Mimi na kufanya ushirika na Mimi ni njia bora zaidi ya kuondoa mawazo ya Shetani. Nataka ninyi nyote mtende kulingana na amri hii kuepuka kuhukumiwa na kupatwa na hasara katika maisha yenu.

Mwanadamu ni mgumu sana kushughulikia, daima akiwa chini ya udhibiti wa watu wa nje, matukio, na mambo na chini ya udhibiti wa dhana zake mwenyewe, hivi kwamba hawawezi kuwa na ushuhuda mzuri kwa ajili Yangu na hawana uwezo wa kushirikiana vyema na Mimi. Mimi daima huwasaidia na kuwakimu, ilhali hamwezi tu kufanya kila mnaloweza kushirikiana na Mimi. Hivi vitu vyote vinaonyesha kwa kutosha ukosefu wenu wa ufahamu Kwangu. Wakati utakapofika ambapo huna tena shaka zozote kabisa kunihusu, basi hakuna mtu anayeweza kukuzuia kutembelea njia ya kweli, na hakuna dhana za mwanadamu zinaweza kukuzuia. Mbona Nasema hili? Kweli unaelewa maana ya maneno Yangu? Ni wakati tu ambapo Nabainisha maneno kama haya ndipo mna ufahamu mdogo. Watu ni wajinga hivi na ni dhaifu sana kichwani. Ni wakati tu ambapo sindano inagonga mfupa ndipo wanaanza kuhisi uchungu kidogo. Yaani, wakati tu ambapo maneno Yangu yanaonyesha chanzo cha ugonjwa wako ndipo unashawishika kabisa. Hata kama hali iko hivi, wakati mwingine bado hamtaki kuweka maneno Yangu katika vitendo, na hamtaki kujijua. Sasa, mbona bado hamjatambua jinsi mwanadamu ni mgumu kushughulikia? Je, ni kwamba maneno Yangu hayazungumzwi dhahiri ama wazi kikamilifu? Ninachotaka ni ninyi kushirikiana na Mimi kwa bidii na kwa dhati; bila kujali iwapo unazungumza maneno yanayosikika kuwa ya kufurahisha au la, mradi uko radhi kushirikiana na Mimi na unaweza kuniabudu na moyo wako wa kweli, basi utakuja chini ya ulinzi Wangu. Hata kama mtu wa aina hii ni mpumbavu sana Nitampa nuru ili aweze kutoa upumbavu wake. Hii ni kwa sababu matendo Yangu lazima yakubaliane na kile Ninachosema; Mimi ni Mwenyezi Mungu ambaye kamwe hatoi ahadi ambayo Hawezi kutimiza.

Mapenzi Yangu yatafichuliwa mara moja kwa makanisa yote na wazaliwa wa kwanza wa kiume wote, hakuna kitakachofichwa tena asilani, kwani siku ambayo yote yanafichuliwa imewadia. Hiyo ni kusema kwamba neno “fichwa” kuanzia sasa halitatumiwa, sembuse chochote ambacho kimefichwa kuwepo. Watu, matukio na mambo yote ambayo yamefichwa lazima yafunuliwe moja moja. Mimi ni Mungu wa busara Anayeshika mamlaka tele. Matukio yote, mambo yote na kila mtu, yote yako katika mikono Yangu. Nachukua hatua Zangu mwenyewe kuyafunua na Nitayafunua yote moja baada ya nyingine, kwa njia ya mtindo mzuri. Kwa yeyote anayethubutu kunirairai au kujaribu kuficha chochote kutoka Kwangu, Nitahakikisha hatainuka tena. Nitachukua hatua kwa njia hii ili nyote muweze kuona hilo. Tazama kwa udhahiri! Gharama ya bidii za kazi ambayo Nimelipa si bure lakini itazaa matunda. Yeyote asiyetilia maanani ama kutii atapambana na hukumu Yangu mara moja. Ni nani ambaye bado anathubutu kuenda dhidi Yangu? Ni lazima nyote mnitii. Nasema kwako, kila kitu Ninachosema na kufanya, kila tendo, kila wazo, fikira na mpango Ninayo leo ni sahihi, na hayamwachii mwanadamu nafasi ya kufikiria. Mbona Ninawaambia tena na tena kwamba mnahitaji tu kufuata na hakuna haja ya kulifikiria tena? Ni kwa sababu hii; bado mnahitaji Nilibainishe?

Dhana zenu zinawazuia, lakini hamfikiri kwamba ni kwa sababu ninyi wenyewe hamjajitahidi, badala yake mkinitazama kwa ajili ya sababu, mkisema kwamba Sijakupa nuru—haya ni mazungumzo ya aina gani? Hamwajibiki wenyewe, daima mkinilalamikia. Ninakuonya! Ukiendelea hivi, kutolipa gharama yoyote, basi utatupwa! Sijidai siku nzima ili kuwatisha. Huu kwa kweli ni ukweli, na Mimi hufanya kile Ninachosema. Punde tu maneno yanapotoka kinywani Mwangu, mara moja yanaanza kutimizwa. Kabla, maneno Niliyoyazungumza yalitimizwa polepole. Lakini sasa mambo ni tofauti, na mambo hayatafanyika polepole tena. Kwa kusema waziwazi, Sishawishi na kubembeleza tena, lakini badala yake Nawahimiza na kuwalazimisha, Kulisema hata wazi zaidi, wale wanaoweza kuenda kwa mwendo sawa hufanya hivyo; wale wasioweza kuenda kwa mwendo sawa na hawawezi kuendelea kutembea wataondolewa. Zamani, Niliwazungumzia kwa subira kwa kila njia, lakini hasa hamkusikiza. Kwa kuwa sasa kazi imeendelea hadi hatua hii, mtafanya nini? Bado mnajifurahisha? Mtu wa aina hii hawezi kufanywa kuwa mkamilifu, lakini hakika atakuwa chombo cha kuondolewa na Mimi!

Iliyotangulia: Sura ya 63

Inayofuata: Sura ya 65

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp