Sura ya 65

Maneno Yangu daima yanaendeleza barabara, yaani yanaonyesha udhaifu wenu wa jaala, vinginevyo bado mngekuwa mnakokota visigino vyenu, bila wazo la muda gani ulioko sasa. Fahamu hili! Mimi Hutumia njia ya upendo ili kuwaokoa. Bila kujali jinsi nyinyi mlivyo, bila shaka Nitakamilisha mambo ambayo Nimekubali bila kufanya kosa lolote. Je, Ninaweza, Mwenyezi Mungu Mwenye haki, kufanya kosa? Je, hiyo siyo dhana ya mtu? Niambieni, kila kitu Mimi Hufanya na kusema si kwa ajili yenu? Baadhi ya watu kwa unyenyekevu watasema: “Ee Mungu! Unafanya kila kitu kwa ajili yetu, lakini hatujui jinsi ya kushirikiana na Wewe.” Upumbavu ulioje! Kusema kwamba hamjui jinsi ya kushirikiana na Mimi! Yote hayo ni uongo za aibu! Kwa kuwa mnasema mambo kama haya, kwa nini, katika hali halisi, mara kwa mara mnaonyesha fikira kwa mwili? Maneno yenu ni matamu, lakini hamtendi kwa njia ya furaha na ya kupendeza. Lazima muelewa hili: Kile ambacho Ninahitaji leo kutoka kwenu sio kuomba mengi, wala hakiko nje ya ufahamu wenu, lakini kinaweza kutimizwa na mtu. Siwakadiri kupita kiasi; je, Mimi sijui ukubwa wa uwezo wa mtu? Ninauelewa kwa uwazi kamili.

Maneno Yangu huwapa nuru daima, lakini mioyo yenu yamefanywa kuwa ngumu mno na hamuwezi kuelewa mapenzi Yangu ndani ya roho zenu! Niambieni, ni mara ngapi Nimewakumbusha msisisitize juu ya chakula, mavazi na kuonekana kwenu, lakini badala yake kusisitiza maisha ya ndani? Lakini nyinyi hamsikilizi. Nimechoka kuisema. Je, mmekuwa ambao hamjali kiasi hiki? Je, mmekuwa wapumbavu kabisa? Je, ingewezekana kuwa maneno Yangu yamenenwa bure? Je, Nimesema lolote ambalo si sahihi? Wanangu! Muwe na busara kwa nia Zangu zenye ari! Wakati maisha yenu yamekomaa, hakutakuwa na haja ya kuwa na wasiwasi, na kila kitu kitatolewa. Hakuna thamani katika kusisitiza mambo hayo kwa sasa. Ufalme Wangu umefanikishwa kabisa na umekuja chini katika dunia kwa umma; hata zaidi hii inamaanisha kuwa hukumu Yangu imetokea kabisa. Je, mmeipitia? Mimi Ninachukia kabisa kuwahukumu nyinyi, lakini hamuonyeshi moyo Wangu fikira hata kidogo. Napenda kwa hicho ambacho mnapata mara kwa mara kuwa utunzaji na ulinzi wa upendo Wangu, na wala sio hukumu ya kikatili. Je, ingewezekana kuwa mko tayari kuhukumiwa? Kama si hivyo, mbona basi mara kwa mara hampati kuwa karibu nami, kushiriki na kuwasiliana na Mimi? Nyinyi hunichukulia Mimi kwa ubaridi sana, na wakati Shetani anakupa mawazo unahisi kufurahishwa, ukifikiri kwamba yanapatana na mapenzi yenu wenyewe, lakini hakuna kitu mnachofanya ni kwa ajili Yangu. Je, mnataka siku zote mnichukulie kwa ukatili?

Siyo kwamba Mimi sitaki kukupatia wewe, lakini kwa kuwa hamko tayari kulipa gharama, basi mko mikono mitupu, bila kushika chochote kabisa. Je, hamuoni kwamba kazi ya Roho Mtakatifu sasa inaendelezwa kwa haraka sana? Je, hamwoni kwamba moyo Wangu unakosa subira sana? Ninawaomba mshirikiane na Mimi lakini mnabaki kutotaka. Maafa yote yatatokea moja baada ya nyingine; mataifa yote na maeneo yote yatapitia maafa—tauni, njaa, mafuriko, ukame na matetemeko ya ardhi yatakuwa kila mahali. Maafa haya hayatokei tu sehemu moja au mbili, wala hayataisha kwa siku moja au mbili, lakini badala yake yataeneza juu ya eneo kubwa zaidi na zaidi, na maafa yatakuwa makali zaidi na zaidi. Wakati huu kila namna ya wadudu tauni watatokea kwa mfululizo, na tukio la watu kuwala watu litatokea kila mahali. Hii ni hukumu Yangu juu ya mataifa yote na watu. Wanangu! Lazima msipate maumivu wala shida za maafa. Napenda hivi karibuni nyinyi mkomae na mchukue mzigo ulioko kwenye mabega Yangu haraka iwezekanavyo; kwa nini nyinyi hamelewi mapenzi Yangu? Kazi iliyo mbele itahitaji juhudi nyingi zaidi na zaidi. Je, mu wenye moyo mgumu hadi kuniacha Mimi na mikono Yangu iliyojaa, kufanya kazi kwa bidii sana Pekee Yangu? Nitanena wazi zaidi; Wale ambao maisha yao hukomaa wataingia katika hifadhi na hawatateseka maumivu au taabu; wale ambao maisha yao hayakomai lazima wateseke maumivu na madhara. Maneno Yangu ni dhahiri ya kutosha, sivyo?

Jina Langu lazima litandazwe katika pande zote na kila mahali, kwamba kila mtu alijue jina Langu takatifu na kunijua Mimi. Watu wa kutoka kila pembe za dunia Marekani, Japani, Kanada, Singapore, Umoja wa Kisovyeti, Macau, Hong Kong na nchi nyingine watasongamana mara moja katika Uchina kwa pamoja, wakitafuta njia ya kweli. Jina Langu tayari limeshawashuhudia wao; kila kilichobaki ni nyinyi mkomae mapema iwezekanavyo ili mpate kuchunga na kuwaongoza. Hii ndiyo maana Nasema kwamba kuna hata kazi zaidi inayopasa kufanywa. Jina Langu litaenea nje katika mwamko wa maafa, na msipochunga mtapoteza sehemu inayopaswa kuwa yenu; je, hamuogopi? Jina Langu huenea kwa dini zote, na kila pembe za dunia, mataifa yote na madhehebu yote. Hii ni kazi Yangu inayofanywa kwa utaratibu, katika viungo vinavyohusiana kwa karibu, yote hutendeka kwa mipango Yangu ya busara. Ningependa tu muwe na uwezo wa kuendelea mbele kwa kila hatua, kwa karibu mkifuata nyayo Zangu.

Iliyotangulia: Sura ya 64

Inayofuata: Sura ya 66

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp