Sura ya 66

Kazi Yangu imeendelea hadi hatua ya sasa na yote imefuata mipango ya busara ya mkono Wangu, na pia kuwa fanikio Langu kuu. Nani kati ya wanadamu anaweza kufanya kitu kama hiki? Na je, si wanaona ni afadhali waingilie kati usimamizi Wangu? Lakini lazima ujue kuwa hakuna namna yeyote anaweza kufanya kazi Yangu badala Yangu, sembuse kuizuia, kwani hakuna yeyote anayeweza kusema au kufanya vitu Nifanyavyo na kusema. Ingawa hii ndio hali, watu bado hawanijui Mimi—Mwenyezi Mungu mwenye busara! Huthubutu kunikataa kwa wazi, ilhali unajiweka dhidi Yangu katika mioyo yenu na kwa akili zenu. Wapumbavu! Je hujui Mimi ni Mungu ambaye Anatazama moyo wa ndani kabisa wa mwanadamu? Je hujui kwamba Naangalia kila neno na tendo lako? Nasema kwako, Sitawahi tena kutamka maneno ya upole kutoka kwa midomo Yangu. Badala yake yote yatakuwa maneno ya hukumu kali, na Nitaona kama unaweza kuyastahimili au la. Kutoka sasa kuendelea, wale ambao mioyo yao haiko karibu na Mimi, ikimaanisha wale ambao hawana upendo wa dhati Kwangu, ndio wale ambao wananikataa Mimi kwa wazi.

Leo, kazi ya Roho Mtakatifu imefika katika hatua ambapo mbinu ya awali haihitaji kutumika tena, lakini badala yake mbinu mpya sasa inaingiwa. Wale ambao hawashirikiani na Mimi vyema na kikamilifu wataanguka Kuzimu, lindi kuu ya kifo (watu hawa watapitia maangamizi milele). Mbinu mpya ni kama ifuatavyo: Kama moyo wako na akili haviko sawa basi hukumu Yangu itakuangukia mara moja, na hii inajumuisha kushikilia dunia, mali, familia, mume, mke, watoto, wazazi, kula na kunywa na nguo na vitu vyote vilivyo nje ya ulimwengu wa kiroho. Kupata nuru kwa watakatifu kutaonekana zaidi, yaani, hisia za maisha zitakuwa dhahiri zaidi na zitakuwa zikisonga kila mara. Yeyote anayesababisha pingamizi hata kidogo atapata kuanguka kuliko na maafa na ataanguka nyuma zaidi katika njia ya mbio za maisha. Wale ambao ni vuguvugu, ambao hawatafuti kwa kujitolea Nawaacha kabisa na kuwapuuza wote bila kumwacha yeyote, na watadhoofika kwa majanga kwa miaka elfu. Wale wanaotafuta kwa shauku, yaani, wale ambao wanadakiza kila wakati, Nitatupa ujinga wao na kuwafanya kuwa waaminifu Kwangu, na zaidi watakuwa na busara na akili, na hivyo watatafuta kwa imani kuu hata zaidi. Naweka baraka Zangu maradufu juu ya wana Wangu wazaliwa wa kwanza na upendo Wangu unakuja juu yenu kila wakati. Nawaangalia na kuwalinda kila wakati na Sitakubali muanguke katika mtego wa Shetani. Nimeanza kuzindua kazi Yangu kati ya watu wote; yaani, Nimeongeza mradi mwingine wa kazi. Hao ni wao ambao watatoa huduma kwa Kristo kwa miaka elfu, na idadi kubwa mno ya watu itasongamana katika ufalme Wangu.

Wana Wangu, lazima mzidishe mazoezi yenu. Kuna kiwango kikubwa cha kazi kinachowangoja, kazi ambayo lazima ufanye na kumaliza. Nataka tu uharakishe na ukomae, ili kumaliza kazi ambayo Nimekukabidhi. Hili ni jukumu lako takatifu, na ni wajibu ambao lazima ufanywe na wale kati yenu ambao ni wana Wangu wazaliwa wa kwanza. Nitawalinda hadi mwisho wa njia na kuwalinda ili muweze kufurahia furaha kamili na Mimi milele! Kila mmoja wenu lazima awe na ufahamu katika ukweli kuwa Nimepanga dhabihu nyingi na kupanga mazingira mengi, yote ili kuwakamilisha ninyi. Mnajua kuwa zote hizi ni baraka Zangu, sivyo? Ninyi nyote ni wana Wangu wapendwa. Mradi tu mnanipenda Mimi kwa dhati basi Sitamwacha hata mmoja wenu, ingawa hili linategemea kama mnaweza kushirikiana kwa upatanifu na Mimi au la.

Iliyotangulia: Sura ya 65

Inayofuata: Sura ya 67

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp