218 Wimbo Wa Kurudi kwa Mwana Mpotevu

1

Kwa nini bado uko namna hii baada ya kumwamini Mungu kwa miaka mingi sana?

Unaposimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, unaonekana kama kwamba wewe hujali hata kidogo;

uso wako ulioharibika unaonyesha mtazamo wako usiojali,

kama kwamba umepitia udhalimu mkubwa na huna moyo wa kumfuata Mungu tena.

Wewe, mwana mpotevu aliyeanguka, unakwenda wapi, mkaidi sana?

Inaonekana kuwa unatii mipango ya Mungu na hujichagulii mwenyewe.

Unakawia katika njia panda na umepoteza “imani” uliyokuwa nayo mwanzoni.

Unaikabili kifo kwa uthabiti na kusonga mbele hadi kwenye mustakabali usio dhahiri.

2

Katika fadhaa, unaonekana kuwa na “imani kubwa”—

Mungu hatakuacha, kwa hivyo unaendelea jinsi unavyopenda.

Tamaa za kupita kiasi zinachukua nafasi ya jitihada zako za dhahania.

Umelemewa na uhasi na bado hujauondoa mwenyewe.

Dhamiri na mantiki yako vimekwenda wapi? Hata sasa bado hujaamka.

Kwa kweli huna maana na huwezi kujimudu kabisa.

Unadhani kuwa tabia yako nzuri ni takatifu na ya heshima.

Hata Mungu katika mwili ni mnyenyekevu, mtu mwovu hana heshima.

3

Msiba ni kwamba wewe hujijui hata kidogo.

Ndani ya sura yako ya nje inayovutia kuna mwovu mbaya anayejificha.

Ni kwa sababu Mungu amekukosea au ni kwa sababu huna ukweli ndiyo kwamba unahisi aibu?

Unawezaje kuzungumza juu ya kutekeleza wajibu wako wakatitabia yako potovu haijabadilika hata kidogo?

Hukumu ya Mungu ina athari ipi kwako kwa vyovyote vile?

Siku moja, upepo utapeperusha makapi yote,

na hilo litakapotokea, majuto yako yatakuwa yamechelewa, na utaomboleza na kusaga meno yako.

Kwa hivyo sasa, jikaze na kufuatilia ukweli. Hiyo inakufanya mwenye hekima.

Iliyotangulia: 217 Ninajuta Sana

Inayofuata: 219 Eh Mungu! Sistahili Upendo Wako Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp