80. Kutumikia Wakati wa Upeo wa Ujana Gerezani

Na Chenxi, China

Kila mtu husema kuwa upeo wa ujana wetu ndio wakati bora sana na safi zaidi wa maisha. Labda kwa wengi, miaka hiyo imejaa kumbukumbu nzuri, lakini kile ambacho singetarajia kamwe ni kwamba nilitumia upeo wa ujana wangu ndani ya Kambi ya kazi ngumu. Unaweza kuniangalia kiajabuajabu kwa hili, lakini silijutii. Ingawa wakati huo katika jela ulijaa uchungu na machozi, ilikuwa ni zawadi ya thamani sana ya maisha yangu, na nilipata mengi sana kutoka kwayo.

Nilizaliwa katika familia yenye furaha, na tangu utoto nimemwabudu Yesu pamoja na mama yangu. Nilipokuwa na miaka kumi na mitano, familia yangu na mimi, tukiamini kwamba Mwenyezi Mungu ni Yesu aliyekuja tena, kwa furaha tuliikubali kazi Yake ya siku za mwisho.

Siku moja Aprili mwaka wa 2002, nilipokuwa nikiishi nyumbani kwa dada fulani, tulikamatwa. Mnamo saa saba usiku, tuliamshwa kwa ghafla na sauti kubwa fulani, migoto ya haraka mlangoni. Tulimsikia mtu nje akipiga yowe, “Fungueni mlango! Fungueni mlango!” Mara tu dada alipoufungua maafisa kadhaa wa polisi kwa ghafla walipita ndani na kusema, kwa ukali, “Tumetoka kwa Ofisi ya Usalama wa Umma.” Kusikia maneno haya matatu, “Ofisi ya Usalama wa Umma,” kulinifanya niwe na wasiwasi mara moja. Walikuwa hapa kutukamata kwa sababu ya imani yetu katika Mungu? Nilikuwa nimesikia kuhusu ndugu fulani wa kiume na wa kike wakikamatwa na kuteswa juu ya imani yao; iliwezekana kuwa hili lilikuwa linafanyika kwangu sasa? Wakati huo tu moyo wangu ulianza kudunda ovyo ovyo, tha-thamp! tha-thamp! na katika hofu yangu, sikujua nifanyeje. Kwa hivyo nikamwomba Mungu kwa haraka: “Mungu, nakusihi Wewe kuwa nami. Nipe imani na ujasiri. Bila kujali kinachotokea, nitakuwa radhi daima kuwa shahidi kwa ajili Yako. Pia nakuomba Wewe sana unipe hekima Yako na uniridhie maneno ninayopaswa kuyasema, ili nisikuhaini au kuwasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike.” Baada ya kuomba, moyo wangu hatua kwa hatua ukatulia. Nikaona hao polisi waovu wanne au watano wakikipekua chumba kama majambazi, wakichakura matandiko, kila almari sanduku, na hata kile kilichokuwa chini ya kitanda mpaka hatimaye wakaibuka na vitabu kadhaa vya maneno ya Mungu pamoja na sahani za nyimbo. Kiongozi wao aliniambia kwa sauti isiyoonyesha hisia, “Umiliki wako wa vitu hivi ni ushahidi kwamba unamwamini Mungu. Njoo nasi na unaweza kutoa taarifa.” Nikiwa nimeshtuka, nikasema, “Ikiwa kuna kitu cha kusema, naweza tu kukisema hapa; Sitaki kwenda nanyi.” Mara moja akatabasamu na kujibu, “Usiogope; hebu tuchukue safari kidogo tu kutoa taarifa. Nitakurudisha hapa hivi punde.” Nikiliamini neno lake, nilikwenda nao na kuingia gari la polisi. Wazo halikunijia kwamwe kwamba safari hiyo ndogo ingekuwa mwanzo wa maisha yangu ya gerezani. Mara tu tulipoingia kwenye uga wa kituo cha polisi, polisi hao waovu walianza kunipigia kelele nitoke nje ya gari. Maonyesho yao ya uso yalibadilika haraka sana, na kwa ghafla walionekana kuwa watu tofauti kabisa na walivyokuwa awali. Tulipofika kwa ofisi, maafisa kadhaa wenye miraba minne waliingia baada yetu na kusimama upande wangu wa kushoto na wa kulia. Nguvu yao kwangu sasa ikiwa imehifadhiwa, kiongozi wa kikundi hicho cha polisi waovu akaniambia kwa hasira, “Unaitwa nani? Unatoka wapi? Je, mko wangapi kwa jumla?” Nilikuwa nimefungua tu kinywa changu na nilikuwa katikati ya kujibu aliponirukia na kunipiga kofi mara mbili kwa uso—chwap, chwap! Nilishikwa na bumbuwazi hadi nikanyamaza. Nilijiuliza, Kwa nini alinipiga? Sikuwa nimemaliza hata kujibu. Kwa nini walikuwa wakali kiasi hicho na wasio na ustaarabu, tofauti kabisa na kile nilichofikiri polisi wa watu kuwa? Baadaye, aliendelea kuniuliza umri wangu, na wakati nilipomjibu kwa uaminifu kwamba nilikuwa na miaka kumi na saba, kofi, kofi, alinipiga kofi tena kwa uso na kunikaripia kwa kusema uongo. Baada ya hayo, bila kujali nilichokisema, bila mpango aliwasilisha pigo baada ya pigo kwa uso wangu kiasi kwamba ni kama uso wangu ulikuwa na moto wa maumivu. Nilikumbuka kusikia ndugu zangu wa kiume na wa kike wakisema kuwa kujaribu kutoa hoja na polisi hawa waovu hakungefaulu. Sasa, baada ya kupitia hili mwenyewe, tangu wakati huo kwendelea sikutamka neno bila kujali waliuliza nini. Walipoona kwamba singezungumza, waliningurumia, “Wewe mjinga! Mimi nitakupa kitu cha kufikiria! Vinginevyo huwezi kutupa taarifa ya kweli!” Hili liliposemwa, mmoja wao alinipiga ngumi kali mara mbili kwa kifua, na kunisababisha nianguke kwa kishindo sakafuni. Kisha akanipiga teke kwa nguvu, mara mbili, akanivuta juu tena kutoka sakafuni kunipigia yowe nipige magoti. Sikumtii, kwa hiyo akanipiga mateke mara chache kwa magoti. Wimbi la maumivu makali lililonipitia lilinilazimisha kupiga magoti kwa sakafu kwa mshindo mzito. Alininyakua kwa nywele na kuvuta kwelekea chini kwa nguvu, na kisha kwa ghafla akakivuta kichwa changu kwelekea nyuma, akanilazimisha kuangalia juu. Akanitusi hali akiupiga uso wangu ngumi mfululizo mara kadhaa tena, na hisi yangu tu ilikuwa kwamba dunia ilikuwa inazunguka. Hivi karibuni, nilianguka chini. Wakati huo huo, kiongozi wa askari hao waovu kwa ghafla akaona saa kwa mkono wangu. Alipokuwa akiiangalia kwa tamaa, alipaaza sauti, “Umevaa nini hapo?” Mara moja, mmoja wa polisi hao akanyakua mkono wangu na kuivua saa kwa nguvu, kisha akampa “bwana” wake. Kuona tabia kama hiyo kulinijaza na chuki kwao. Baada ya hapo, waliponiuliza maswali zaidi, niliwakazia tu macho kwa kimya, na hilo liliwakasirisha hata zaidi. Mmoja wa polisi hawa waovu alininyakua kwa kola kana kwamba alikuwa akimwinua kuku mdogo, na akaniinua kutoka kwa sakafu kuningurumia, “Aha, wewe ni mtu mkubwa, sivyo? Nitakwambia wakati wa kunyamaza!” Alipokuwa akisema hili, alinigonga kikatili mara kadhaa zaidi, na tena nilipigwa hadi kwa sakafu. Kufikia wakati huo mwili wangu wote ulikuwa unauma kwa namna isiyovumilika, na sikuwa na nguvu yoyote tena ya kushindana. Nililala tu sakafuni kama nimefunga macho yangu, bila kusogea. Moyoni mwangu, nikamwomba Mungu kwa kusisitiza: “Mungu, sijui ni maovu gani zaidi genge hili la polisi waovu litatenda dhidi yangu. Unajua mimi ni mdogo kwa kimo, na kwamba mimi ni dhaifu kimwili. Ninakusihi Wewe unilinde. Afadhali nife kuliko kuwa Yuda na kukusaliti Wewe.” Baada ya kukamilisha maombi yangu, Mungu alinipa nguvu na nishati. Afadhali nife karibuni kuliko kuwa Yuda kwa kumsaliti Mungu na kuwasaliti ndugu zangu. Ningemshuhudia Mungu kwa udhabiti. Wakati huo huo, nikasikia mtu mmoja karibu nami akisema, “Je, kwa nini hasogei tena? Je, amekufa?” Baada ya hapo, mtu fulani alisimama juu ya mkono wangu kwa makusudi na kuufinyilia chini kwa mguu wake huku akinguruma kikatili, “Simama! Tutakupeleka mahali pengine.” Kwa sababu Mungu alikuwa Amenipa imani na nguvu, kunitisha kwao hakukuniogofya kamwe. Moyoni mwangu, nilikuwa nimejitayarisha kupigana dhidi ya Shetani.

Baadaye, nilisindikizwa hadi kwa Ofisi ya Wilaya ya Usalama wa Umma. Tulipofika kwa chumba cha masaili, kiongozi wa wale polisi waovu na msafara wake walinizunguka na kuniuliza maswali mara kwa mara, wakitembea polepole nyuma na mbele yangu na kujaribu kunilazimisha kuwasaliti viongozi wangu wa kanisa na ndugu zangu wa kiume na wa kike. Walipoona kwamba bado singewapa majibu waliyotaka kusikia, wote watatu walibadilishana zamu kunipiga makofi kwa uso tena na tena. Sijui ni mara ngapi niligongwa; yote niliyoweza kusikia yalikuwa ni chwa, chwa, walipokuwa wakiupiga uso wangu, sauti iliyoonekana ikivuma kwa sauti fulani dhidi ya usiku huo wa utulivu. Mikono yao sasa ikiwa inauma, polisi wale waovu walianza kunipiga kwa vitabu. Walinipiga hadi mwisho sikuweza kuhisi maumivu tena; uso wangu ulihisi tu kuvimba na kufa ganzi. Hatimaye, wakiona kwamba hawangeweza kupata taarifa yoyote muhimu kutoka kinywani mwangu, hawa polisi waovu walitoa kitabu cha simu na, kama wamefurahishwa na wao wenyewe, wakasema, “Tuligundua hiki katika mfuko wako. Hata kama hutatuambia chochote, bado tuna hila nyingine ya siri!” Kwa ghafla, nilihisi kuwa na wasiwasi mno: Kama yeyote wa ndugu zangu wa kiume na wa kike angejibu simu hiyo, ingewasababishia kukamatwa. Ingeweza pia kuwahusisha na kanisa, na matokeo yangeweza kuwa mabaya sana. Wakati huo huo, nikakumbuka kifungu cha maneno ya Mungu: “Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu. Ni kitu gani kilichopo ambacho hakiko mikononi Mwangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 1). “Hiyo ni kweli,” Nilijiwazia. “Vitu na matukio yote hupangwa na kuratibiwa mikononi mwa Mungu. Hata simu ipigwe au la inaamuliwa kabisa na Mungu. Niko tayari kumtumainia na kumtegemea Mungu na kutii mipango Yake.” Kwa hiyo nilimwomba Mungu tena na tena, nikimsihi kuwalinda hawa ndugu wa kiume na wa kike. Matokeo yake yakiwa, walipopiga hizo namba za simu moja baada ya nyingine, baadhi yazo zililia bila mtu yeyote kujibu huku zingine zikikosa kuingia kamwe. Mwishowe, wakifoka matusi kwa kukata tamaa, wale polisi waovu walitupa hicho kitabu cha simu kwa meza na kuacha kujaribu. Sikuweza kujizuia kutoa shukrani zangu na sifa kwa Mungu.

Hata hivyo, hawakuwa wamekata tamaa, na waliendelea kunihoji kuhusu mambo ya kanisa. Sikujibu. Wakiwa wameingiwa na wasiwasi na kughadhabika, walifikia tendo lenye hizaya hata zaidi ya kujaribu kunifanya niteseke: Mmoja wa polisi waovu alinilazimisha kuchuchumaa, na nilipaswa kushikilia mikono yangu mbele sawasawa na mabega yangu na sikuruhusiwa kusogea kamwe. Kabla muda mfupi, miguu yangu ilianza kutetemeka na sikuweza tena kushikilia mikono yangu mbele tena, na mwili wangu pasipo kutaka ulianza kuinuka tena. Huyo polisi alichukua ufito wa chuma na akanikazia macho kama chui milia akiyaangalia mawindo yake. Mara tu niliposimama alinipiga kikatili miguuni, akisababisha maumivu mengi kiasi kwamba karibu nianguke kwa magoti yangu tena. Kwa kipindi cha zaidi ya nusu saa iliyofuata, miguu yangu au mikono yangu iliposogea tu hata kidogo, mara moja angenipiga na ule ufito wa chuma. Sijui ni mara ngapi alinipiga. Kutokana na kuchuchumaa kwa muda mrefu kama huo, miguu yangu yote ilivimba mno na ilijihisi uchungu usiovumilika kana kwamba ilikuwa imevunjika. Muda ulipoendelea kupita, miguu yangu ilikuwa ikitetemeka hata vikali zaidi na meno yangu yalikuwa yakitatarika bila kusita. Wakati huo huo nilihisi kama nguvu zangu zingekwisha. Hata hivyo, wale polisi waovu walinidhihaki na kunifanyia mzaha kutoka pembeni, daima wakinibeza na kunicheka kwa chuki, kama watu wakijaribu kwa kikatili kumfanya tumbili afanye vitimbi. Nilivyozidi kuangalia nyuso zao mbaya, zenye kudharauliwa, ndivyo nilivyozidi kuwachukia polisi hawa waovu. Kwa ghafla nikasimama na kuwaambia kwa sauti kubwa, “Sitachuchumaa tena. Endeleeni na kunihukumu kifo! Leo sina chochote cha kupoteza! Hata siogopi kufa, kwa hiyo ninawezaje kuwaogopa? Wanaume wakubwa jinsi mlivyo, lakini yote mnayoonekana kujua ni jinsi ya kumdhulumu msichana mdogo kama mimi!” Kwa mshangao wangu, baada ya kusema hayo, polisi walipiga kelele maneno machache ya laana kisha wakaacha kunihoji.

Hili kundi la polisi waovu lilikuwa limenitesa muda mwingi sana wa usiku; walipositisha, kulikuwa macheo. Walinifanya nitie sahihi ya jina langu na wakasema wangeniweka kizuizini. Baada ya hapo, polisi mmoja mzee, akijifanya mwenye fadhili, aliniambia, “Binti, angalia; wewe ni mchanga sana—katika upeo wa ujana wako—hivyo ni bora ikiwa utaharakisha na kuelezea dhahiri unayoyajua. Ninahakikisha kuwa nitawafanya wakuwachilie. Kama una shida yoyote, usisite kuniambia. Angalia; uso wako umevimba kama mkate wa boflo. Je, si umeteseka vya kutosha?” Baada ya kumsikia akizungumza kwa njia hii, nilijua alikuwa tu akijaribu tega ili nikiri. Nilikumbuka pia kitu ambacho ndugu zangu wa kiume na wa kike walikuwa wamesema wakati wa mikutano: Ili kupata kile walichotaka, polisi waovu wangetumia vitisho na hongo na huishia kwa namna zote za hila ili kukudanganya. Kufikiri juu ya hili, nikamjibu yule polisi mzee, “Usijifanye kama wewe ni mtu mzuri; ninyi nyote ni sehemu ya kundi hili moja. Unataka nikiri nini? Kile unachokifanya kinaitwa kughusubu ungamo. Hii ni adhabu isiyo halali!” Aliposikia hili, alivaa onyesho la asiye na hatia na akatoa hoja, “Lakini sikukugonga hata mara moja. Ni hao waliokugonga.” Nilishukuru kwa mwongozo na ulinzi wa Mungu, ambao uliniruhusu kushinda tena majaribu ya Shetani.

Baada ya kuondoka kutoka kwa Ofisi ya Wilaya ya Usalama wa Umma, moja kwa moja nilifungiwa katika kituo cha kizuizi na wao. Mara tu tulipoingia ndani ya lango la mbele, niliona kuwa mahali hapo palizungukwa na kuta ndefu sana zilizokuwa na nyaya za umeme za konsertina juu yazo, na katika kila mojawapo ya pembe nne kulikuwa na kile kilichoonekana kama mnara wa ulinzi. Ndani ya minara hiyo polisi wenye silaha walilinda. Yote hayo yalionekana kuwa mabaya na ya kuogofya. Baada ya kupitia lango la chuma baada ya lango la chuma, nilifika kwa seli. Nilipoona mifarishi iliyochakaa, iliyofunikwa na kitani juu ya kitanda baridi cha matofali, ambayo ilikuwa mieusi na michafu, na nikahisi harufu kali, ya kuchukiza ikitoka kwazo, sikuweza kujizuia kuhisi wimbi la maudhi likipita ndani yangu, likifuatwa kwa haraka kwa wimbi la huzuni. Nikawaza mwenyewe: Watu wanawezaje kuishi hapa? Hili ni sawa na banda la nguruwe. Wakati wa mlo, kila mfungwa alipewa tu andazi dogo la kupikwa kwa mvuke lililokuwa chachu na nusu mbichi. Ingawa nikuwa nimeteswa na polisi kwa nusu usiku na sikukula chochote, kuona chakula hiki kwa kweli kulinifanya nipoteze hamu ya chakula. Zaidi ya hayo, uso wangu ulikuwa umevimba sana kutokana na kupigwa na polisi, ulihisi kukazwa kana kwamba ulifungwa na utepe. Nilihisi maumivu hata kwa kufungua kinywa changu tu ili kuzungumza, sembuse kula. Katika hali hizi, nilikuwa katika hali ya kusononeka mno na nilihisi kukosewa sana. Fikira ya kuwa kwa kweli ningepaswa kukaa hapa na kuvumilia maisha ya kinyama hivyo ilinifanya kuwa na mhemko sana kiasi kwamba nilitokwa na machozi bila kukusudia. Dada tuliyekuwa tumekamatwa pamoja alishiriki nami maneno ya Mungu, nilielewa kwamba Mungu Alikuwa ameruhusu hali hii inifikie, na hii ilikuwa Yeye kunijaribu na kunipima kuona ikiwa ningeweza kumshuhudia. Alikuwa akitumia nafasi hii kukamilisha imani yangu. Kutambua jambo hili, nikaacha kuhisi kudhulumiwa, na ndani yangu nilipata utashi fulani wa kuniwezesha kuvumilia dhiki yangu.

Nusu mwezi ulipita, na kiongozi wa wale askari waovu akaja tena kunihoji. Kuniona nikiwa kimya na mtulivu, na kwamba sikuwa na woga kamwe, alipaaza sauti na kuita jina langu na kusema kwa sauti kubwa, “Niambie kwa ukweli: Ni wapi pengine umekwisha wahi kukamatiwa? Hii bila shaka sio mara yako ya kwanza ndani; vinginevyo, ungewezaje kutenda kwa utulivu na uzoefu sana, kana kwamba huogopi hata kidogo?” Nilipomsikia akisema haya, singeweza kujizuia kumshukuru na kumsifu Mungu moyoni mwangu. Mungu alikuwa amenilinda na kunipa ujasiri, hivyo kuniruhusu mimi kukabiliana na polisi hawa waovu bila woga kabisa. Wakati huo huo, hasira ilipanda kutoka ndani ya moyo wangu: Unatumia vibaya mamlaka yako kwa kuwatesa watu kwa sababu ya imani zao za kidini, kuwakamata, kuwadhulumu, na kuwaumiza bila sababu wale ambao humwamini Mungu. Matendo yako ni kinyume cha zote mbili haki na sheria za Mbinguni. Ninamwamini Mungu, na ninaitembea njia sahihi; sijavunja sheria yoyote. Kwa nini nikuogope? Sitashindwa na majeshi maovu ya kundi lako! Kisha nikajibu vikali, “Je, unadhani kuwa kila mahali pengine panachosha hivi kwamba kwa kweli ningependa kuja hapa? Mmenikosea na kunionea! Jitihada zenu zaidi za kupata ungamo kwa kutumia nguvu au kunisingizia zitakuwa bure!” Baada ya kusikia jambo hili, kiongozi wa askari hao waovu alikasirika sana kiasi kwamba alionekana karibu kutokwa na moshi masikioni mwake. Alininguruma, “Wewe ni mkaidi mno huwezi kutuambia kitu chochote. Huwezi kuzungumza, sivyo? Nitakupa hukumu ya miaka mitatu, na kisha tutaona kama unasema ukweli au la. Ninakutolea changamoto uendelee kuwa mkaidi!” Wakati huo nilijihisi kuudhika sana kiasi kwamba ningeweza kulipuka. Nikajibu kwa sauti kubwa, “Mimi bado ni mchanga; miaka mitatu ni nini kwangu? Nitatoka gerezani kufumba na kufumbua.” Katika ghadhabu yake, yule polisi muovu alisimama kwa ghafla na kunung'unika kwa vikaragosi wake, “Naacha; endeleeni kumhoji.” Kisha akabamiza mlango na kuondoka. Kuona kile kilichotokea, wale polisi wawili waovu hawakunihoji zaidi; walimaliza tu kuandika taarifa ili niiweke sahihi na kisha kutoka nje. Kushuhudia kushindwa kwa polisi waovu kulinipa furaha sana. Katika moyo wangu niliushukuru ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani. Wakati wa duru ya pili ya usaili, walibadilisha mbinu. Mara tu walipoingia mlangoni walijifanya kunihangaikia: “Umekuwa hapa kwa muda mrefu sana. Inakuwaje hakuna yeyote wa familia yako amekuja kukuona? Ni lazima wamekata tamaa juu yako. Je, si uwapigie simu mwenyewe, na uwaombe waje kukutembelea.” Kusikia jambo hili kulinifanya nihisi huzuni na kufadhaika moyoni. Nilijihisi pweke na asiyejiweza. Nilikuwa nina tamaa ya kwenda nyumbani na niliwakosa wazazi wangu, na hamu yangu ya uhuru ilikuwa ikiongezeka zaidi na zaidi. Bila kukusudia, macho yalifurika na machozi, lakini sikupenda kulia mbele ya kundi hili la polisi waovu. Kimoyomoyo, nikamwomba Mungu: Mungu, hivi sasa najihisi mnyonge sana na mwenye maumivu, na asiyejiweza kabisa. Tafadhali nisaidie, sitaki kumruhusu Shetani aone udhaifu wangu. Hata hivyo, hivi sasa siwezi kufahamu malengo Yako. Ninakuomba Unipatie nuru na kuniongoza. Baada ya kuomba, wazo fulani kwa ghafla lilinijia mawazoni mwangu: Huu ulikuwa ujanja wa Shetani; kujaribu kwao kunifanya niwasiliane na familia yangu kwaweza kuwa hila kuwafanya walete malipo ya kukomboa mateka ili kutimiza lengo lao la siri la kuchuma pesa kiasi, au huenda wanajua kwamba wanakaya wangu wote walimwamini Mungu na wangetaka kutumia fursa hii kuwakamata. Polisi hawa waovu kwa kweli walikuwa wamejaa mipango. Kama haingekuwa kwa kupata nuru kwa Mungu, ningepiga simu nyumbani. Si basi ningekuwa Yuda kwa njia isiyo dhahiri? Kwa hivyo, nikamtangazia Shetani kwa siri: Ibilisi muovu, siwezi kukuruhusu ufaulu katika udanganyifu wako. Jinsi yoyote mnavyotaka kunishughulikia haijalishi kwangu kamwe!” Polisi hawa waovu hawakuwa na mipango mingine ya siri ya kutumia. Baada ya hapo, hawakunihoji tena.

Mwezi mmoja ulipita. Siku moja, mjomba wangu kwa ghafla alikuja kunitembelea, akisema kwamba alikuwa katikati ya kujaribu kuniondoa huko siku chache baadaye. Nilipokuwa nje ya chumba cha kutembelewa, nilihisi furaha mno. Nilidhani hatimaye ningeweza kujumuika na umma tena, pamoja na ndugu zangu wa kiume, ndugu wa kike, na wapendwa wangu. Kwa hiyo nikaanza kuwa na fikira nzuri na kumtarajia mjomba wangu kuja kunichukua; kila siku, nilikaa chonjo nikingoja sauti ya walinzi wakiniita kwamba ulikuwa wakati wa kuondoka. Kwa hakika, wiki moja baadaye, mlinzi mmoja alinizuru. Moyo wangu ulihisi kama ungedunda hadi nje ya ngome ya ubavu nilipowasili kwa furaha katika chumba cha kutembelewa. Hata hivyo, nilipomwona mjomba wangu, aliinamisha kichwa chake chini. Ulikuwa ni muda mrefu kabla hajasema kwa sauti ya kuhuzunisha, “Wamekamilisha kesi yako tayari. Umehukumiwa miaka mitatu.” Niliposikia jambo hilo, nilitiwa bumbuazi. Mawazo yangu yalikuwa matupu kabisa. Niliyazuia machozi, na hakuna yaliyotoka. Ilikuwa ni kama sikuweza kusikia chochote alichokisema mjomba wangu baada ya hapo. Niliyumbayumba hadi nje ya chumba cha kutembelewa nikiwa katika hali ya mpagao, miguu yangu ilihisi ni kama iliyojaa timazi, kila hatua ikiwa nzito kuliko ile ya awali. Sikumbuki katu nilivyorudi kwa seli yangu. Nilipofika huko, niliganda, nikiwa nimepooza kabisa. Nilijiwazia, Kila siku ya mwezi uliopita au zaidi ya maisha haya ya kinyama imepita kwa kujiburuta na kuonekana kama mwaka mmoja; nitawezaje kusalia kwa miaka mitatu mirefu ya haya? Jinsi nilivyozidi kufikiria hili, ndivyo maumivu yangu makali yalivyozidi kukua, na ndivyo mustakabali wangu ulivyozidi kutokuwa dhahiri na kutoweza kueleweka. Nikiwa nimeshindwa kuyazuia machozi tena, niliangua kilio. Nilifikiria kuwa kama mtoto mdogo sitahukumiwa, au kwa zaidi nitazuiliwa kwa miezi michache tu. Nilifikiri kuwa naitajika kuvumilia uchungu na shida kidogo tu na kisha itakuwa yameisha; haijawahi tokea kwangu kwamba nilipaswa kukaa gerezani kwa miaka mitatu. Katika huzuni yangu, nilikuwa nimekuja tena mbele ya Mungu. Nikamfungulia Yeye hisia zangu, nikisema, “Mungu, najua kwamba vitu vyote na matukio yote yako mikononi Mwako, lakini hivi sasa moyo wangu unajihisi mtupu kabisa. Najihisi kama niko karibu kusambaratika; Nafikiri itakuwa vigumu sana kwangu kuvumilia miaka mitatu ya kuteseka gerezani. Mungu, nakuomba Unifichulie mapenzi Yako kwangu, na ninakusihi Wewe uongeze kwa imani yangu na nguvu ili niweze kabisa kukutii Wewe na kwa ushupavu niyakubali yaliyonifika.” Baada ya kuomba, nifikiria maneno ya Mungu: “katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu na nilikuwa tayari kutii. Bila kujali kitakachonijia au mateso kiasi gani nitakayopitia, sitamlaumu; ningetoa ushuhuda kwake. Miezi miwili baadaye, nilisafirishwa hadi kwa kambi ya kazi ngumu. Nilipopokea karatasi zangu za uamuzi na kuzitia sahihi, niligundua kwamba hukumu hiyo ya miaka mitatu ilikuwa imebadilishwa kuwa mwaka mmoja. Katika moyo wangu nilimshukuru na kumsifu Mungu tena na tena. Haya yote yalikuwa ni matokeo ya mpango wa Mungu, na ndani yake niliweza kuona upendo mkubwa na ulinzi Aliokuwa nao kwangu.

Katika kambi ya kazi ngumu, niliona upande mwingine hata mkatili zaidi na wa kihayawani mno wa hao polisi waovu. Alfajiri na mapema tungeamka na kwenda kufanya kazi, tulijazwa na kazi kwa uzito sana ya kufanya kila siku. Tulipaswa kufanya kazi kwa saa nyingi sana kila siku, na wakati mwingine tungefanya kazi usiku na mchana kwa siku kadhaa. Baadhi ya wafungwa waliugua na walihitaji kungoekwa kwa vifaa vya matibabu kwa njia ya mishipa, na ilibidi mwendo wa matone ya dawa kudondoka iongezwe kwa kasi ya juu zaidi ili mara tu wanapoikamilisha dawa wangeweza kurudi kazini kwa haraka. Hili lilisababisha idadi kubwa ya wafungwa hatimaye kupata magonjwa fulani yaliyokuwa vigumu sana kutibu. Baadhi ya watu, kwa sababu walifanya kazi polepole, walikuwa mara nyingi wakitolewa matusi na walinzi; lugha yao chafu ilikuwa isiyowazika kabisa. Baadhi ya watu walikiuka masharti wakati wakifanya kazi, hivyo waliadhibiwa. Kwa mfano, waliwekwa kwa kamba, ambayo ilimaanisha walipaswa kupiga magoti kwa ardhi na kufungwa mikono yao kwa nyuma ya migongo yao, mikono yao ikilazimishwa kuinuka kwa maumivu hadi kwa kiwango cha shingo. Wengine walifungiliwa kwa miti na minyororo ya chuma kama mbwa na walichapwa bila huruma kwa mjeledi. Baadhi ya watu, wakishindwa kuvumilia mateso haya ya kinyama, wangejaribu kujinyima chakula ili wafe njaa, lakini walinzi hao waovu waliwafunga pingu kwa vifundo vyao vya miguu na mikononi na kisha kuwashikilia miili yao kikiki, wakiilazimisha kwa nguvu mirija ya kulia na vinywaji ndani ya miili yao. Walihofia kuwa wafungwa hawa wangeweza kufa, si kwa kuwa walitunza maisha, lakini kwa sababu walikuwa na hofu ya kupoteza kazi bahasa waliotoa. Matendo maovu yaliyofanywa na askari hawa wa magereza kwa kweli yalikuwa mengi mno kuhesabu, kama yalivyokuwa matukio makatili ya kuogofya na ya umwagaji wa damu yaliyotokea. Haya yote yalinifanya nione dhahiri kwamba Serikali ya Chama cha Kikomunisti cha Kichina ilikuwa mfano halisi wa Shetani aliyekuwa katika ulimwengu wa kiroho; ilikuwa ndiyo katili zaidi ya pepo wote na magereza yaliyo chini ya utawala wake yalikuwa kuzimu duniani—sio kwa jina tu, lakini kwa hakika. Nakumbuka baadhi ya maneno kwa ukuta wa ofisi ambamo nilihojiwa yalivutia macho yangu: “Ni marufuku kuwapiga watu upendavyo au kuwapa adhabu kinyume cha sheria, na hata ni haramu zaidi kupata maungamo kwa njia ya mateso.” Hata hivyo, katika hali halisi, matendo yao yalikuwa katika upinzani wazi kwa hili. Walikuwa wamenipiga kikatili, msichana ambaye hakuwa hata mtu mzima bado, na wakanipa adhabu iliyokuwa kinyume cha sheria; aidha, walikuwa wamenihukumu kwa sababu tu ya imani yangu katika Mungu. Haya yote yalikuwa yamenisababisha kuona dhahiri kwamba serikali ya CCP ilitumia hila kuwahadaa watu huku ikiwadanganya kuwa kila kitu kilikuwa shwari. Ilikuwa tu kama Mungu alivyosema: “Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu bila hisia yoyote, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, wanaenda kinyume na dhamiri yote, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)).

Baada ya kupitia mateso ya polisi wovu, niliridhika kabisa kuhusu kifungu hiki cha maneno yaliyonenwa na Mungu, na sasa nilikuwa na maarifa na uzoefu kiasi wa kweli kukihusu: Serikali ya CCP kweli ni kikosi cha pepo inayomchukia na kumpinga Mungu, na ambayo inatetea uovu na vurugu, na kuishi chini ya ukandamizaji wa utawala wa kishetani ni sawa na kuishi katika jehanamu ya binadamu. Aidha, katika kambi ya kazi ngumu, niliona kwa macho yangu mwenyewe ubaya wa kila aina ya watu: nyuso za kukirihi za nyoka wanafiki wenye kuangalia masilahi yao ambao walijipendekeza kwa viongozi, nyuso mbaya za watu wakatili vikali wakizusha ghasia waliowadhulumu wadhaifu, na kadhalika. Kwa mimi, ambaye alikuwa bado hajaingiza mguu katika jamii, katika mwaka huu wa maisha katika jela, hatimaye niliona dhahiri uovu wa binadamu. Nilishuhudia usaliti katika mioyo ya watu, na kutambua jinsi ulimwengu wa mwanadamu unaweza kuwa. Nilijifunza pia kutofautisha kati ya chanya na hasi, meusi na meupe, mema na mabaya, uzuri na uovu, na kubwa na ya kudharauliwa; niliona wazi kwamba Shetani ni mbaya, muovu, mkatili, na kwamba ni Mungu tu aliye ishara ya utakatifu na haki. Ni Mungu pekee anayeashiria uzuri na wema; ni Mungu pekee aliye upendo na wokovu. Nikilindwa na kuhifadhiwa na Mungu, mwaka huo usiosahaulika ulipita haraka sana kwangu. Sasa, nikitazama nyuma kwa mwaka huo, ingawa nilipitia mateso ya mwili kiasi kwa kipindi cha mwaka huo wa maisha gerezani, Mungu alitumia maneno Yake kuniongoza na kunielekeza, hivyo kuyawezesha maisha yangu kukomaa. Haya mateso na jaribio ni baraka maalum ya Mungu kwangu. Shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu.

Iliyotangulia: 75. Hili Jaribu Langu

Inayofuata: 81. Mateso na Majaribio Ni Baraka za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

40. Tiba ya Wivu

Na Xunqiu, UchinaMwenyezi Mungu anasema, “Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za uasi, ni mchafu kiasi cha kusikitisha, na ni...

69. Kurudi kwenye Njia Sahihi

Chen Guang, MarekaniMwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp