XIV. Maneno Juu ya Viwango vya Mungu vya Kuyafafanua Matokeo ya Mwanadamu na juu ya Mwisho wa Mtu wa Kila Aina
675. Kabla ya binadamu kuingia rahani, iwapo kila aina ya mtu ataadhibiwa ama kutuzwa kutaamuliwa kulingana na iwapo wanatafuta ukweli, iwapo wanamjua Mungu, iwapo wanaweza kumtii Mungu anayeonekana. Waliomhudumia Mungu anayeonekana lakini bado hawamjui wala kumtii hawana ukweli. Watu hawa ni watenda maovu, na watenda maovu bila shaka wataadhibiwa; zaidi ya hapo, wataadhibiwa kulingana na mienendo yao mibovu. Mungu ni wa mwanadamu kumwamini, na pia Anastahili utii wa mwanadamu. Wale wanaomwamini tu Mungu asiye yakini na asiyeonekana ni wale wasiomwamini Mungu; zaidi ya hapo, hawawezi kumtii Mungu. Kama hawa watu bado hawawezi kumwamini Mungu anayeonekana wakati kazi Yake ya ushindi inakamilika, na pia wanaendelea kutomtii na kumpinga Mungu anayeonekana katika mwili, hawa wanaoamini isiyo yakini bila shaka, wataangamizwa. Ni kama ilivyo na wale miongoni mwenu—yeyote anayemtambua Mungu Aliyepata mwili kwa maneno lakini bado hatendi ukweli wa utii kwa Mungu Aliyepata mwili hatimaye ataondolewa na kuangamizwa, na yeyote anayemtambua Mungu anayeonekana na pia kula na kunywa ukweli ulioonyeshwa na Mungu anayeonekana lakini bado anamtafuta Mungu asiye yakini na asiyeonekana pia yeye ataangamizwa baadaye. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kubaki hadi wakati wa pumziko baada ya kazi ya Mungu kukamilika; hakuwezi kuwa yeyote kama watu hawa atakayebakia hadi wakati wa pumziko. Watu wenye pepo ni wale wasiotenda ukweli; asili yao ni ile inayompinga na kutomtii Mungu, na hawana nia hata kidogo za kumtii Mungu. Watu wote kama hao wataangamizwa. Iwapo una ukweli na iwapo unampinga Mungu hayo yanaamuliwa kulingana na asili yako, si kulingana na sura yako ama hotuba na mwenendo wako wa mara kwa mara. Asili ya kila mtu inaamua iwapo ataangamizwa; hii inaamuliwa kulingana na asili iliyofichuliwa na mienendo yao na kutafuta kwao ukweli. Miongoni mwa watu wanaofanya kazi sawa na pia kufanya kiasi sawa cha kazi, wale ambao asili yao ni nzuri na wanaomiliki ukweli ni watu wanaoweza kubaki, lakini wale ambao asili yao ya ubinadamu ni mbovu na wasiomtii Mungu anayeonekana ni wale watakaoangamizwa. Kazi ama maneno yoyote ya Mungu yanayoelekezwa kwa hatima ya binadamu yanahusiana na binadamu ipasavyo kulingana na asili ya kila mtu; hakuna kosa lolote litakalotokea, na hakutakuwa na kosa hata moja litakalofanywa. Ni pale tu ambapo watu wanafanya kazi ndipo hisia za binadamu ama maana itaingilia. Kazi anayofanya Mungu ndiyo inayofaa zaidi; hakika Hataleta madai ya uongo dhidi ya kiumbe yeyote.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
676. Watenda maovu wote na yeyote na wote ambao hawajaokolewa wataangamizwa wakati watakatifu miongoni mwa binadamu wataingia rahani, bila kujali kama wao ni roho za wafu ama wale wanaoishi bado katika mwili. Bila kujali enzi ya hizi roho zitendazo maovu na watu watenda maovu, ama roho za watu wenye haki na watu wanaofanya haki wako, mtenda maovu yeyote ataangamizwa, na yeyote mwenye haki ataishi. Iwapo mtu ama roho inapokea wokovu haiamuliwi kabisa kulingana na kazi ya enzi ya mwisho, lakini inaamuliwa kulingana na iwapo wamempinga ama kutomtii Mungu. Kama watu wa enzi ya awali walifanya maovu na hawangeweza kuokolewa, bila shaka wangekuwa walengwa wa adhabu. Kama watu wa enzi hii wanafanya maovu na hawawezi kuokolewa, hakika wao pia ni walengwa wa adhabu. Watu wanatengwa kwa msingi wa mema na mabaya, sio kwa msingi wa enzi. Baada ya kutengwa kwa msingi wa mema na mabaya, watu hawaadhibiwi ama kutuzwa mara moja; badala yake, Mungu atafanya tu kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wema baada ya Yeye kumaliza kutekeleza kazi Yake ya ushindi katika siku za mwisho. Kwa kweli, Amekuwa akitumia mema na mabaya kutenga binadamu tangu Afanye kazi Yake miongoni mwa binadamu. Atawatuza tu wenye haki na kuwaadhibu waovu baada ya kukamilika kwa kazi Yake, badala ya kuwatenga waovu na wenye haki baada ya kukamilika kwa kazi Yake mwishowe na kisha kufanya kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wazuri mara moja. Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
677. Kiwango ambacho mwanadamu anamhukumu mwanadamu kinatokana na tabia zake; aliye na mwenendo mzuri ni mtu mwenye haki, na aliye na mwenendo wa kuchukiza ni mwovu. Kiwango ambacho Mungu anamhukumu mwanadamu kinatokana na iwapo asili ya mtu inamtii Yeye; anayemtii Mungu ni mtu mwenye haki, na asiyemtii Mungu ni adui na mtu mwovu, bila kujali iwapo tabia ya mtu huyu ni nzuri ama mbaya, na bila kujali iwapo hotuba ya mtu huyu ni sahihi ama si sahihi. Watu wengine wanatamani kutumia matendo mazuri kupata hatima nzuri ya baadaye, na watu wengine wanataka kutumia hotuba nzuri kununua hatima nzuri. Watu wanaamini kimakosa kwamba Mungu anaamua matokeo ya mwanadamu kulingana na tabia ama hotuba yake, na kwa hivyo watu wengi watataka kutumia haya kupata fadhila ya muda mfupi kupitia udanganyifu. Watu ambao baadaye watasalimika kupitia pumziko wote watakuwa wamevumilia siku ya dhiki na pia kumshuhudia Mungu; wote watakuwa watu ambao wamefanya jukumu lao na wana nia ya kumtii Mungu. Wanaotaka tu kutumia fursa kufanya huduma ili kuepuka kutenda ukweli hawataweza kubaki. Mungu ana viwango sahihi vya mipangilio ya matokeo ya kila mtu; Hafanyi tu maamuzi haya kulingana na maneno na mwenendo wa mtu, wala Hayafanyi kulingana na tabia zao wakati wa kipindi kimoja cha muda. Hakika Hatakuwa na huruma na mwenendo wowote mbaya wa mtu kwa sababu ya huduma ya mtu ya zamani kwa Mungu, wala Hatamnusuru mtu kutokana na kifo kwa sababu ya gharama kwa Mungu ya mara moja. Hakuna anayeweza kuepuka adhabu ya uovu wake, na hakuna anayeweza kuficha tabia zake mbovu na hivyo kuepuka adhabu ya maangamizi. Kama mtu anaweza kweli kufanya jukumu lake, basi inamaanisha kwamba ni mwaminifu milele kwa Mungu na hatafuti tuzo, bila kujali iwapo anapokea baraka ama bahati mbaya. Kama watu wana uaminifu kwa Mungu waonapo baraka lakini wanapoteza uaminifu wao wasipoweza kuona baraka na mwishowe bado wasiweze kumshuhudia Mungu na bado wasiweze kufanya jukumu lao kama wapasavyo, hawa watu waliomhudumia Mungu wakati mmoja kwa uaminifu bado wataangamizwa. Kwa ufupi, watu waovu hawawezi kuishi milele, wala hawawezi kuingia rahani; watu wenye haki tu ndio mabwana wa pumziko.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
678. Iwapo mtu anapokea baraka ama kupata bahati mbaya inaamuliwa kulingana na kiini cha mtu, na haiamuliwi kulingana na asili ya kawaida ambayo mtu anashiriki na wengine. Ufalme hauna kabisa usemi kama huu ama kanuni kama hii. Kama mtu anaweza kusalimika hatimaye, ni kwa sababu amefikia mahitaji ya Mungu, na kama mtu hawezi hatimaye kubaki katika kipindi cha pumziko, ni kwa sababu mtu huyu hamtii Mungu na hajakidhi mahitaji ya Mungu. Kila mtu ana hatima inayofaa. Hatima hizi zinaamuliwa kulingana na asili ya kila mtu na hazihusiani kabisa. Mwenendo ovu wa mtoto hauwezi kuhamishwa kwa wazazi wake, na haki ya mtoto haiwezi kushirikishwa wazazi wake. Mwenendo ovu wa mzazi huwezi kuhamishwa kwa watoto wake, na haki ya mzazi haiwezi kushirikishwa watoto wake. Kila mtu anabeba dhambi zake husika, na kila mtu anafurahia bahati yake husika. Hakuna anayeweza kuchukua ya mwingine. Hii ni haki. Kwa mtazamo wa mwanadamu, iwapo wazazi wanapata bahati nzuri, watoto wao pia wanaweza, na watoto wakifanya maovu, wazazi wao lazima walipie dhambi zao. Huu ni mtazamo wa mwanadamu na njia ya mwanadamu ya kufanya vitu. Si mtazamo wa Mungu. Matokeo ya kila mtu yanaamuliwa kulingana na asili inayotoka kwa mwenendo wao, na daima yanaamuliwa inavyofaa. Hakuna awezaye kubeba dhambi za mwingine; hata zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kupokea adhabu badala ya mwingine. Hii ni thabiti. Malezi ya upendo ya mzazi kwa watoto wake hayamaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya watoto wake, wala upendo wenye utiifu wa mtoto kwa wazazi wake haumaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya wazazi wake. Hiyo ndiyo maana ya kweli ya maneno haya, “Basi kutakuwa na watu wawili shambani; mmoja wao atachukuliwa, na mwingine kuachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga katika kisiagi; mmoja atachukuliwa, na mwingine kuachwa.” Hakuna anayeweza kuwaingiza watoto wake watenda maovu rahani kwa msingi wa upendo wao wa kina kwa watoto wao, wala hakuna anayeweza kumwingiza mke wake (ama mume) rahani kwa sababu ya mwenendo wao wa haki. Hii ni kanuni ya utawala; hakuwezi kuwa na ubaguzi kwa mtu yeyote. Wanaotenda haki ni wanaotenda haki, na watenda maovu ni watenda maovu. Watenda haki watasalimika, na watenda maovu wataangamizwa. Watakatifu ni watakatifu; wao si wachafu. Wachafu ni wachafu, na hawana sehemu yoyote takatifu. Watu wote waovu wataangamizwa, na watu wote wa haki watasalimika, hata kama watoto wa watenda maovu wanafanya matendo ya haki, na hata kama wazazi wa mtu wa haki wanafanya matendo maovu. Hakuna uhusiano kati ya mume anayeamini na mke asiyeamini, na hakuna uhusiano kati ya watoto wanaoamini na wazazi wasioamini. Ni aina mbili zisizolingana. Kabla ya kuingia rahani, mtu ana jamaa wa kimwili, lakini baada ya mtu kuingia rahani, mtu hana jamaa wa kimwili tena wa kuzungumzia. Wanaofanya wajibu wao na wasiofanya ni adui, wanaompenda Mungu na wanaomchukia Mungu ni wapinzani. Wanaoingia rahani na wale ambao wameangamizwa ni aina mbili ya viumbe wasiolingana. Viumbe wanaotimiza wajibu wao watasalimika, na viumbe wasiotimiza wajibu wao wataangamizwa; zaidi ya hayo, hii itadumu milele.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
679. Watenda maovu na wenye haki, hata hivyo, ni viumbe. Viumbe wafanyao maovu wataangamizwa hatimaye, na viumbe wafanyao matendo ya haki watasalimika. Huu ni mpangilio unaofaa sana wa viumbe wa aina hizi mbili. Watenda maovu hawawezi, kwa sababu ya kutotii kwao, kukataa kwamba ni viumbe wa Mungu lakini wameporwa na Shetani na hivyo hawawezi kuokolewa. Viumbe wa mwenendo wa haki hawawezi kutegemea ukweli kwamba watasalimika kukataa kwamba wameumbwa na Mungu na bado wamepokea wokovu baada ya kupotoshwa na Shetani. Watenda maovu ni viumbe wasiomtii Mungu; ni viumbe ambao hawawezi kuokolewa na tayari wameporwa na Shetani. Watu wanaotenda maovu ni watu pia; ni watu waliopotoshwa mno na watu wasioweza kuokolewa. Jinsi walivyo viumbe pia, watu wa mwenendo wa haki pia wamepotoshwa, lakini ni watu walio tayari kuacha tabia yao potovu na wanaweza kumtii Mungu. Watu wa mwenendo wa haki hawajajaa haki; badala yake, wamepokea wokovu na kuacha tabia yao potovu kumtii Mungu; watashikilia msimamo huo mwishowe, lakini hii si kusema kwamba hawajapotoshwa na Shetani. Baada ya kazi ya Mungu kuisha, miongoni mwa viumbe Wake wote, kutakuwa na wale watakaoangamizwa na wale watakaosalimika. Huu ni mwelekeo usioepukika wa kazi Yake ya usimamizi. Hakuna anayeweza kuyakataa haya. Watenda maovu hawawezi kusalimika; wanaomtii na kumfuata Mungu hadi mwishowe hakika watasalimika. Kwa sababu kazi hii ni ya usimamizi wa binadamu, kutakuwa na wale watakaobaki na wale watakaoondolewa. Haya ni matokeo tofauti ya watu wa aina tofauti, na hii ndiyo mipango inayofaa zaidi ya viumbe Wake.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
680. Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati ya hawa wafuasi wote, kuna wale wanaohudumu kama makuhani, wale wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Nawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina zao, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu. Moja baada ya mwingine, Nayaita makundi ya wale Ningependa kuwaokoa kurejea katika nyumba Yangu, kisha Nawaruhusu watu hawa wote wakubali kazi Yangu katika siku za mwisho. Wakati uo huo, Nawaainisha wanadamu kulingana na aina, kisha Namtunuku au kumwadhibu kila mmoja kulingana na matendo yake. Hizi ndizo hatua zinazojumuisha kazi Yangu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa
681. Sasa unajua kweli ni kwa nini unaniamini Mimi? Kweli unajua kusudi na umuhimu wa kazi Yangu? Kweli unajua wajibu wako? Kweli unaujua ushuhuda Wangu? Kama unaniamini Mimi tu, ilhali si utukufu Wangu wala ushuhuda Wangu vinaweza kuonekana ndani yako, basi Nimekutupa nje kitambo kirefu. Kwa wale wanaoona wanajua kila kitu, wao ni miiba zaidi katika macho Yangu, na katika nyumba Yangu, wao ni vizuizi tu Kwangu. Wao ndio magugu yanayopaswa kupepetwa kabisa na kuondolewa kwenye kazi Yangu, bila ya jitihada hata kidogo na bila ya uzito wowote; Nimevichukia kitambo kirefu. Na kwa wale bila ya ushuhuda, hasira Yangu siku zote iko juu yao, na kiboko Changu hakijawahi kutoka kwao. Kitambo kirefu Nimewakabidhi kwenye mikono ya yule mwovu, na hawana tena baraka Zangu zozote. Na siku hiyo ikifika, adhabu yao itakuwa mbaya zaidi kuliko ile ya wanawake wajinga. Sasa hivi Ninafanya kazi ile ambayo ndiyo wajibu Wangu kufanya; Nitakusanya pamoja ngano yote, pamoja na magugu. Hii ndiyo kazi Yangu sasa. Magugu haya yataweza kupepetwa na kuondolewa wakati wa kupepeta Kwangu, kisha nafaka za ngano zitakusanywa kwenye ghala, na magugu ambayo yatakuwa yamepepetwa yatawekwa motoni na kuchomwa hadi kugeuka jivu. Kazi Yangu sasa ni kuwaweka tu binadamu wote kwa pamoja, yaani, kuweza kuwashinda wote kabisa. Kisha Nitaanza upepetaji wa kufichua mwisho wa binadamu wote.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?
682. Wanaotafuta na wasiotafuta sasa ni aina mbili tofauti ya watu, na wao ni aina mbili ya watu na hatima mbili tofauti. Wanaotafuta maarifa ya ukweli na kutenda ukweli ni watu ambao Mungu ataokoa. Wale wasiojua njia ya ukweli ni mapepo na adui; ni vizazi vya malaika mkuu na wataangamizwa. Hata wacha Mungu wanaomwamini Mungu asiye yakini—je, si mapepo pia? Watu wanaomiliki dhamiri nzuri lakini hawakubali njia ya ukweli ni mapepo; asili yao ni ile inayompinga Mungu. Wale wasiokubali njia ya ukweli ni wale wanaompinga Mungu, na hata kama watu hawa wanavumilia taabu nyingi, bado wataangamizwa. Wasio tayari kuiwacha dunia, wasioweza kuvumilia kutengana na wazazi wao, wasioweza kuvumilia kujiondolea raha zao za mwili, wote hawamtii Mungu na wote wataangamizwa. Yeyote asiyemwamini Mungu aliyepata mwili ni pepo; zaidi ya hayo, wataangamizwa. Wanaoamini lakini hawatendi ukweli, wasiomwamini Mungu aliyepata mwili, na wale ambao hawaamini kabisa kuwepo kwa Mungu wataangamizwa. Yeyote anayeweza kubaki ni mtu ambaye amepitia uchungu wa usafishaji na kusimama imara; huyu ni mtu ambaye kweli amepitia majaribio. Yeyote asiyemtambua Mungu ni adui; yaani, yeyote aliye ndani ama nje ya mkondo huu ambaye hamtambui Mungu aliyepata mwili ni adui wa Kristo! Shetani ni nani, mapepo ni nani, na nani ni maadui wa Mungu kama si wapinzani wasiomwamini Mungu? Wao si watu wasiomtii Mungu? Wao si watu wanaodai kwa maneno kuamini lakini hawana ukweli? Wao si wale watu wanaofuata tu kupata kwa baraka lakini hawawezi kumshuhudia Mungu? Bado unachanganyika na wale mapepo leo na kuwa na dhamiri na mapenzi kwao, lakini kwa hali hii huenezi nia nzuri kuelekea kwa Shetani? Je, huchukuliwi kuwa unashiriki na mapepo? Kama watu siku hizi bado hawawezi kutofautisha kati ya mema na maovu, na wanaendelea kuwa wenye kupenda na kuhurumia bila kufikiri na bila nia yoyote ya kutafuta mapenzi ya Mungu au kuweza kwa njia yoyote kushikilia nia za Mungu kama zao wenyewe, basi miisho wao utakuwa dhalili zaidi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
683. Namna ambavyo Mungu anawatendea watu wanaomkufuru au hata wanaompinga, au hata wale wanaomkashifu—watu wanaomshambulia kimakusudi, kumkashifu, na kumlaani—hajifanyi kwamba kila kitu kiko sawa. Anao mwelekeo wazi kwa hawa. Anawadharau watu hawa, na moyoni Mwake anawashutumu. Anatangaza waziwazi hata matokeo kwa ajili yao, ili watu waweze kujua kwamba Anao mwelekeo wazi kwao wanaomkufuru Yeye, na ili wajue namna atakavyoamua matokeo yao. Hata hivyo, baada ya Mungu kusema mambo haya, watu bado wangeona kwa nadra ukweli wa namna ambavyo Mungu angeshughulikia watu hao, na wasingeelewa kanuni zinazotawala matokeo ya Mungu, hukumu Yake kwao. Hiyo ni kusema, wanadamu hawawezi kuuona mwelekeo na mbinu fulani za Mungu katika kuwashughulikia. Hali hii inahusu kanuni za Mungu za kufanya mambo. Mungu hutumia ujio wa hoja katika kushughulikia tabia yenye uovu ya baadhi ya watu. Yaani, Hatangazi dhambi yao na haamui matokeo yao, lakini Anatumia moja kwa moja ujio wa hoja ili kuwaruhusu kuadhibiwa, wao kupata adhabu wanayostahili. Wakati hoja hizi zinapofanyika, ni miili ya watu inayoteseka kwa adhabu; hili ni jambo ambalo linaweza kuonekana kwa macho ya binadamu. Wakati wa kushughulikia tabia ya uovu kwa baadhi ya watu, Mungu huwalaani tu kwa matamshi, lakini wakati uo huo, ghadhabu ya Mungu huwapata, na adhabu wanayopokea inaweza kuwa jambo ambalo watu hawalioni, lakini aina hii ya matokeo inaweza kuwa hata mbaya zaidi kuliko matokeo ambayo watu wanaweza kuona ya kuadhibiwa au kuuawa. Hii ni kwa sababu katika hali zile ambazo Mungu ameamua kutomwokoa mtu wa aina hii, kutoonyesha tena rehema au uvumilivu kwao, kutowapa fursa zaidi, mwelekeo Anaouchukua kwao ni kuwaweka pembeni. Ni nini maana ya “kuweka pembeni”? Maana ya kauli hii kibinafsi ni kuweka kitu kwa upande mmoja, kutokizingatia tena. Lakini hapa, wakati Mungu “anapomweka mtu pembeni,” kuna fafanuzi mbili tofauti kuhusu kile Alicho: Ufafanuzi wa kwanza ni kwamba Amempa Shetani kuyashughulikia maisha ya mtu huyo, na kila kitu cha mtu huyo. Mungu hatamwajibikia tena na Hataweza kumsimamia tena. Kama mtu huyo amerukwa na akili, au ni mpumbavu, na kama katika maisha au kifo, au kama angeshushwa jahanamu ili kupata adhabu yake, hayo yote yasingemhusu Mungu. Hiyo ingemaanisha kwamba kiumbe hicho hakitakuwa na uhusiano wowote na Muumba. Ufafanuzi wa pili ni kwamba Mungu ameamua kwamba Yeye Mwenyewe anataka kufanya kitu na mtu huyu, kwa mikono Yake mwenyewe. Inawezekana kwamba Ataweza kutumia huduma ya mtu wa aina hii, au kwamba atatumia mtu wa aina hii kama foili[a]. Inawezekana kwamba Atakuwa na njia maalum ya kushughulikia mtu wa aina hii, njia maalum ya kumshughulikia—kama tu Paulo. Hii ndio kanuni na mwelekeo katika moyo wa Mungu kuhusu namna Alivyoamua kumshughulikia mtu wa aina hii. Hivyo basi wakati watu wanapompinga Mungu, na kumkashifu na kumkufuru Yeye, kama wataendelea kusema ubaya kuhusu tabia Yake, au kama watafikia ile hali ya kimsingi ya Mungu, athari zake hazifikiriki. Athari zile mbaya zaidi ni kwamba Mungu anayakabidhi maisha yao na kila kitu chao kwa Shetani, mara moja na kabisa. Hawatasamehewa daima dawamu. Hii inamaanisha kwamba mtu huyu amekuwa chakula katika kinywa cha Shetani, mwanasesere katika mikono yake, na kuanzia hapo, Mungu hahusiki naye.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
684. Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, bali si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya lingine, njia ambayo kwayo wameitumia kunifuata, sifa zao asilia, na hatimaye jinsi ambavyo wamejistahi. Kwa njia hii, haijalishi ni mtu wa aina gani, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu, na wote watakuwa pamoja na wa aina yake kama Nilivyopanga. Ninaamua hatima ya kila mtu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anataka huruma, bali kulingana na ikiwa anao ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili. Sharti mtambue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa pia. Huu ni ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako
685. Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.