C. Maonyo ya Mungu kwa Mwanadamu

644. Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wenye mzaha mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba wale ambao hawamkubali Kristo wa siku za mwisho watachukiwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, na hakuna ambaye anaweza kumpita Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unamwamini Mungu, na hivyo ni lazima ukubali neno Lake na kulitii neno Lake. Usifikiri tu kuhusu kupata baraka huku ukikosa kuweza kupokea ukweli na ruzuku ya uzima. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili Aweze kuwatolea uzima wale wote ambao wanamwamini kwa dhati. Kazi hii ipo kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuiingia enzi mpya, na kazi hii ndiyo njia ambayo lazima ifuatwe na wale wote ambao wataingia katika enzi mpya. Kama humtambui Kristo, na zaidi ya hayo umhukumu, umkufuru au kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Hii ni kwa sababu Kristo huyu Mwenyewe ni onyesho la Roho Mtakatifu, onyesho la Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani, na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unamkufuru Roho Mtakatifu. Adhabu inayostahili kwa wale wanaomkufuru Roho Mtakatifu ni dhahiri kwa wote. Pia nakuambia hili: Ukimpinga Kristo wa siku za mwisho, ukimkataa Kristo wa siku za mwisho, basi hakuna mtu mwingine anayeweza kubeba matokeo ya hili kwa niaba yako. Zaidi ya hayo, kuanzia wakati huo na kuendelea hutawahi kuwa na nafasi ya kupata kibali cha Mungu kamwe; hata ukitaka kujikomboa, hutaweza kuutazama uso wa Mungu tena. Hii ni kwa sababu unayempinga si mwanadamu, unayemkataa si mtu asiye na maana, bali ni Kristo. Je, unajua matokeo ya hili ni yapi? Hufanyi kosa dogo, bali unatenda dhambi mbaya sana. Na kwa hivyo namshauri kila mtu asitoe kucha na meno au kutoa maoni kiholela mbele ya ukweli, kwa maana ukweli pekee ndio unaoweza kukuletea uzima, na hakuna chochote isipokuwa ukweli kinachoweza kukuwezesha kuzaliwa upya na kuutazama uso wa Mungu tena.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

645. Sote tunaamini kwamba hakuna nchi au nguvu inayoweza kuzuia kile ambacho Mungu anataka kutimiza, na kwamba wale wanaojaribu kuzuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, na wale wanaovuruga na kujaribu kuharibu mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Mtu yeyote anayepinga kazi ya Mungu atapelekwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka kwa dunia hii na Mungu, na litakoma kuwepo. Ninawahimiza watu wa mataifa yote na wa nchi zote, na hata wa tasnia zote wasikilize sauti ya Mungu, waitazame kazi ya Mungu, na wazingatie hatima ya wanadamu, na hivyo kumfanya Mungu kuwa kitu kitakatifu zaidi, chenye kuheshimiwa zaidi, cha juu, na kitu pekee cha kuabudiwa miongoni mwa wanadamu, na kuwawezesha binadamu wote waishi katikati ya baraka za Mungu, kama tu vile uzazi wa Ibrahimu walivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu vile Adamu na Hawa, ambao Mungu aliwaumba hapo mwanzo, walivyoishi katika Bustani ya Edeni.

Kazi ya Mungu inasonga mbele kama wimbi kubwa. Hakuna anayeweza kumzuia, na hakuna anayeweza kusimamisha mwendo Wake. Ni wale tu wanaosikiliza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na shauku na Yeye, ndio wanaoweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Yake. Wale wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makubwa na adhabu wanayostahili kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Ana Mamlaka Juu ya Hatima ya Wanadamu Wote

646. Mungu anawatafuta wale wanaotamani Aonekane. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, wale ambao hawajasahau agizo Lake na wanatoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Zake, na hawampingi. Kama hujazuiliwa na nguvu zozote katika ibada yako Kwake, basi Mungu atakutazama kwa upendeleo na Ataweka baraka Zake juu yako. Kama wewe ni wa cheo cha juu, mwenye sifa ya kuheshimika, mwenye maarifa mengi, mwenye mali nyingi, na kuungwa mkono na watu wengi, lakini mambo haya hayakuzuii kuja mbele za Mungu kuukubali wito Wake na agizo Lake, kufanya kile Mungu anachokuambia ufanye, basi yote unayoyafanya yatakuwa yenye umuhimu zaidi duniani na yenye haki zaidi kwa binadamu. Ukiukataa wito wa Mungu kwa sababu ya hadhi yako na malengo yako mwenyewe, yote utakayoyafanya yatalaaniwa na hata kudharauliwa na Mungu. Pengine wewe ni rais, ama mwanasayansi, ama mchungaji, ama mzee, lakini bila kujali ukuu wa ofisi yako, ukitegemea maarifa yako na uwezo katika shughuli zako, basi daima utakuwa wa kushindwa na kamwe utanyimwa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Hakubali kwamba kazi yako ni yenye haki, wala kukubali kwamba unafanya kazi kwa manufaa ya wanadamu. Atasema kwamba kila kitu unachofanya, ni kutumia maarifa na nguvu za wanadamu ili kumwondolea mwanadamu ulinzi wa Mungu, ambapo ni kukataa baraka za Mungu. Atasema kuwa unamwongoza mwanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa maisha yasiyo na mipaka ambapo mwanadamu amempoteza Mungu na baraka Zake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Ana Mamlaka Juu ya Hatima ya Wanadamu Wote

647. Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa kwanza kabisa kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli ulioonyeshwa na Yesu anaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

648. Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kikundi ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, vizazi vya malaika mkuu, kikundi ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Huenda watu wengi wasijali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifuµanayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu utakuwa wakati wa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako. Hata hivyo, lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia utakaokuwa wakati ambapo utashuka chini kuzimu kuadhibiwa, wakati ambapo mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi utakuwa umetangazwa, na wakati ambapo Mungu atawathawabisha wema na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo wametakaswa, watakuwa wameletwa mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatio la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anatenda ishara, lakini hawamkubali Yesu Anayeonyesha hukumu kali na Anatoa uzima na njia ya kweli. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Anawashughulikia tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wenye kiburi sana. Watu wabaya kabisa kama hawa wanawezaje kutunukiwa na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na hampaswi kukufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini muwe watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wana kiu na hamu ya kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndiyo mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua mambo kiholela bila kuzingatia suala zima; hata zaidi, msiwe wenye kuchukulia mambo kwa wepesi na msiwe hobelahobela katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, angalau, wale wanaomwamini Mungu wanafaa kuwa na mioyo ya unyenyekevu na imwogopayo Mungu. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wameusikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu ni watu wenye kiburi. Hakuna anayemwamini Yesu anayestahili kuwalaani au kuwashutumu wengine. Nyote mnafaa kuwa watu walio wenye mantiki na wanaoukubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno haya elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, na kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ukweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sicho chochote ila nuru kiasi ya Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na hampaswi kuwa watu wanaomkufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo, baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, si njia, na si maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi sana na kwa kawaida sana, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati ya kutosha kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe mwenye pupa wala wa haraka, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

649. Wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu. Wengi wana hisia mbaya kuhusu kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu angefanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Hata hivyo, lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi sana matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu tu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni utoneshaji wa hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu, ambalo kwalo Nasema ni wazi nani atapata hasara mwishowe. Nawasihi nyote msijichukulie kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Ni vipi ambavyo ninyi ni bora zaidi kuliko wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye hivyo pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu tu ya “mchango” ambao umetoa, na utajawa na majuto mengi kwa kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje tu kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani kipitishe hukumu juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambazwa kote ulimwenguni hadi miisho ya dunia. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu aje kukupeleka mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni kipande sugu cha mti mkavu[a]. Yesu hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Kinyume chake, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Tanbihi:

a. Kipande cha mti mkavu: nahau ya Kichina inayomaanisha “hali isiyo na matumaini.”


650. Mungu aliumba ulimwengu huu, Alimuumba mwanadamu huyu na, zaidi ya hayo, Alikuwa muasisi wa utamaduni wa kale wa Kigiriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu pekee Anayewafariji wanadamu hawa, na ni Mungu pekee Anayewajali wanadamu hawa usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatenganishwi na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu hauwezi kuepuka mipango inayofanywa na mikono ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi kwa hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote kunafanyika chini ya mipango ya Mungu. Mungu pekee ndiye Anayejua hatima ya nchi ama taifa lolote, na ni Mungu pekee ndiye Anayedhibiti mwenendo wa wanadamu hawa. Ikiwa wanadamu wanataka kuwa na hatima nzuri, ikiwa nchi inataka kuwa na hatima nzuri, basi mwanadamu lazima amsujudie Mungu katika ibada, na aje mbele za Mungu akitubu na kuungama, kama sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Ana Mamlaka Juu ya Hatima ya Wanadamu Wote

651. Kwa ajili ya majaliwa yenu, mnapaswa kutafuta kuidhinishwa na Mungu. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu mnatambua kwamba nyinyi mmehesabiwa miongoni mwa wale walio katika nyumba ya Mungu, basi mnapaswa kumletea Mungu utulivu wa akili katika mambo yote na kumtosheleza katika kila jambo. Kwa maneno mengine, ni lazima muwe na kanuni katika matendo yenu na mlingane na ukweli katika mambo kama hayo. Kama jambo hili linazidi uwezo wako, basi utachukiwa na kukataliwa na Mungu na vilevile kukataliwa kwa dharau na kila mwanadamu. Pale tu utakapokuwa katika hali mbaya kama hii, basi hauwezi kuhesabiwa miongoni mwa wale walio kwenye nyumba ya Mungu. Hii ndiyo maana ya kutoidhinishwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

652. Mahitaji Yangu yanaweza kuwa rahisi, lakini kile Ninachowaambia si rahisi hivyo kama kujumlisha moja na moja upate mbili. Kama kile mnachofanya ni kuzungumza tu kuhusu mambo haya bila kufikiria, au kuongea kwa kuropoka maneno matupu, yanayovutia, basi mipango yenu na matakwa yenu yatakuwa ukurasa mtupu milele. Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale walio miongoni mwenu ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Kinyume cha hayo, Nitawatendea wale ambao hawajatimiza mahitaji Yangu kwa adhabu, si thawabu, sembuse huruma yoyote. Mnaweza kuwa mnafikiri kwamba, kwa kuwa mmekuwa wafuasi kwa miaka mingi sana, mmeweka bidii bila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote mnaweza kupata bakuli la wali katika nyumba ya Mungu kwa kuwa watendaji huduma. Naweza kusema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu siku zote mmekuwa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani na usichukuliwe kwa manufaa ya wengine. Hivyo Ninawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi ambavyo kazi yako yenye bidii inavyostahili kusifiwa, jinsi ambavyo sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi ambavyo umeboresha mtazamo wako; mradi tu hujatimiza matakwa Yangu, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia mahitaji Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu, na hali ikiwa mbaya zaidi Nitageuza miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwa bure, kwa sababu Siwezi kuwaleta watu hao wanaonuka uovu na walio na sura ya Shetani katika ufalme Wangu au kuwapeleka katika enzi ijayo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

653. Sasa ndio wakati ambapo Roho Wangu anafanya kazi kuu, na ndio wakati ambapo Ninaanza kazi Yangu kati ya Mataifa. Zaidi ya hayo, ndiyo wakati ambapo Ninaainisha viumbe wote walioumbwa, Nikimweka kila mmoja katika aina yake, ili kazi Yangu iweze kuendelea kwa kasi zaidi na iweze kufikia matokeo zaidi. Na hivyo, kile Ninachowaomba bado ni kwamba utoe nafsi yako yote kwa kazi Yangu yote, na, zaidi ya hayo, kwamba utambue wazi na uone kwa usahihi kazi yote ambayo Nimefanya ndani yako, na kutumia nguvu zako zote ili kazi Yangu iweze kupata matokeo makuu zaidi. Hili ndilo unalopaswa kuelewa. Acha kushindana ninyi kwa ninyi, kutafuta njia ya kutokea, au kutafuta raha kwa ajili ya mwili wako, ili kuepuka kuchelewesha kazi Yangu, na kuzuia mustakabali wako wa ajabu. Badala ya kukulinda, kufanya hivyo kunaweza tu kuleta maangamizi juu yako. Je, si huu utakuwa ujinga kwa upande wako? Kile ambacho unajifurahisha nacho leo ndicho kile kile ambacho kinaharibu mustakabali wako, huku yale maumivu unayostahimili leo ndicho kile kitu ambacho kinakulinda hasa. Lazima ufahamu waziwazi kuhusu jambo hilo, ili uepuke kuwa windo la vishawishi ambavyo utaona ugumu kujinasua kutoka kwavyo, na kuepuka kuingia kwa kijinga kwenye ukungu mzito na kutoweza kupata jua daima. Ukungu huu mzito utakapotoweka, utajipata katikati ya hukumu ya siku kuu. Kufikia wakati huo, siku Yangu itakuwa imemkaribia binadamu. Utatorokaje hukumu Yangu? Utawezaje kuvumilia joto kali la jua? Ninapompa binadamu wingi Wangu, haufurahii kwa dhati, lakini badala yake anautupa nje kwenye sehemu zisizotambulika. Wakati siku Yangu itawadia, binadamu hataweza tena kugundua wingi Wangu au kupata ukweli mkali Niliompa zamani sana. Ataomboleza na kulia, kwa sababu amepoteza uangavu wa mwanga na kuanguka gizani. Kile mnachoona leo ni upanga tu mkali wa kinywa Changu. Bado hamjakiona kiboko kilicho katika mkono Wangu au moto Ninaotumia kumchoma binadamu, na ndiyo maana bado mna kiburi na msio na kiasi mbele Yangu. Ndiyo maana bado mnapigana na Mimi katika nyumba Yangu, huku mkipinga kwa ulimi wa mwanadamu kile ambacho Nimenena na kinywa Changu. Binadamu haniogopi Mimi. Akiwa bado katika uhasama na Mimi hadi leo, bado haniogopi kamwe. Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno. Kazi Yangu ni kuteketeza na kusafisha maneno na matendo yote ya binadamu yaliyotamkwa na kufanywa mbele ya Roho Wangu. Kwa njia hiyo, baada ya Mimi kuondoka ulimwenguni, binadamu wataweza bado kuendeleza utiifu Kwangu, na bado watanihudumia kama vile watumishi Wangu watakatifu wanavyofanya katika kazi Yangu, wakiruhusu kazi Yangu hapa ulimwenguni iendelee mpaka siku itakapokamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

654. Duniani, kila aina ya pepo wanazungukazunguka bila mwisho wakitafuta mahali pa kupumzika, na bila kukoma wanatafuta maiti za wanadamu zinazoweza kuliwa. Watu Wangu! Lazima mbaki ndani ya utunzaji na ulinzi Wangu. Kamwe msiwahi kuishi katika hali ya upotovu! Msiwahi tenda mambo kiholela! Badala yake, salimisha uaminifu wako katika nyumba Yangu, na ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kushinda hila za Shetani. Katika hali yoyote usiishi kama ilivyokuwa katika siku za awali, kufanya jambo moja mbele Yangu na jingine nyuma Yangu—ukifanya hivyo umeshapita kiwango cha kukombolewa. Hakika Nimetamka zaidi ya kiasi cha kutosha maneno ya aina hii, sivyo? Ni kwa sababu asili ya mwanadamu ya zamani hairekebiki ndiyo maana Nimemkumbusha tena na tena. Usichoke! Haya yote Niyasemayo ni kwa mujibu wa kuhakikisha hatima yako! Kile Shetani anahitaji kwa hakika ni uchafu na pahali pabaya; na kadri unavyokosa kuokoleka kabisa, na kadri unavyokuwa mpotovu, ukikataa kujiwasilisha kwa hali ya kujizuia, ndivyo roho wachafu watakavyotumia nafasi yoyote ya kupenyeza. Mara unapowasili katika hii nafasi, uaminifu wako utakuwa kelele tupu, bila uhalisi wowote, na azimio lako litaliwa na pepo wachafu, kugeuzwa kuwa uasi au hila za Shetani, na kutumiwa kuzuia kazi Yangu. Kuanzia hapo, unaweza kupigwa na Mimi wakati wowote. Hakuna anayeelewa uzito wa hali hii; watu wote hupuuza tu yale wanayosikia na hawachukui tahadhari kwa vyovyote. Sikumbuki kile kilichofanywa katika siku za nyuma. Je, bado unasubiri Niwe mpole kwako Nisahau kwa mara nyingine tena?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10

655. Watu wengi wanaona ni afadhali wahukumiwe kwenda kuzimu kuliko kunena na kutenda kwa uaminifu. Si ajabu kwamba Nina utendaji mwingine kwa wale ambao si waaminifu. Bila shaka, Ninaelewa ugumu mkubwa mnaokumbana nao kwa kuwa binadamu waaminifu. Ninyi nyote ni werevu sana na wastadi katika kuwapima watu kwa kipimo chenu kidogo; hii inafanya kazi Yangu iwe rahisi zaidi. Na kwa sababu nyinyi mnaficha siri katika mioyo yenu, basi, Nitawapeleka, mmoja baada ya mwingine, katika janga ili “mfundishwe” kwa moto, ili kwamba baada ya hapo mjitoe kikamilifu katika kuamini maneno Yangu. Hatimaye, Nitaondoa vinywani mwenu maneno “Mungu ni Mungu mwaminifu,” kisha ndipo mtakapojipiga vifua na kuomboleza, “Moyo wa mwanadamu ni mdanganyifu!” Je, hali za akili zenu zitakuwa vipi kwa wakati huu? Ninafikiri hamtakuwa na majivuno kama mlivyo sasa. Na hata hamtakuwa “wa kina sana kiasi cha kushindwa kueleweka” kama mlivyo sasa. Baadhi ya watu hutenda kwa ustaarabu na wanaonekana hasa “wana tabia nzuri” mbele za Mungu, lakini bado wanakuwa waasi na wasiojizuia mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa wale walio waaminifu? Kama wewe ni mnafiki, mtu ambaye ni stadi katika “mahusiano baina ya watu,” basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mtu ambaye unajaribu kumchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na uthibitisho usio na maana, basi Nasema kwamba wewe ni mtu ambaye unachukia kabisa kuuweka ukweli katika vitendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kuzitoa, na kama hauko tayari kabisa kuziweka wazi siri zako—yaani, magumu yako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia yenye mwanga, basi Ninasema kwamba wewe ni mtu ambaye hutapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hutaweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. … Jinsi ambavyo hatima ya mtu itakuwa mwishoni inategemea kama wana moyo wenye uaminifu na wa kweli, na ikiwa wana nafsi safi. Kama wewe ni mtu ambaye si mwaminifu kabisa, ni mtu mwenye moyo muovu, mwenye nafsi isiyo safi, basi una uhakika wa kuishia mahali ambapo mwanadamu anaadhibiwa, kama ilivyoandikwa katika rekodi ya majaliwa yako. Kama unadai kwamba wewe ni mwaminifu sana, na bado kamwe hutendi kulingana na ukweli au kuongea neno la kweli, hivyo je, bado unatarajia Mungu akupe thawabu? Je, bado unatumaini kwamba Mungu atakuchukulia kama mboni ya jicho Lake? Je, mawazo kama hayo si ya kipumbavu? Unamdanganya Mungu katika mambo yote, hivyo nyumba ya Mungu inawezaje kumpa nafasi mtu kama wewe, ambaye mikono yake si safi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

656. Sasa, iwapo ufuatiliaji wenu umekuwa wa kufaa au la linatathminiwa na kile mlicho nacho sasa. Hiki ndicho kinachotumiwa kuamua matokeo yenu; yaani, matokeo yenu yanafichuliwa katika kujitolea mlikofanya na mambo ambayo mmefanya. Matokeo yenu yatadhihirishwa na ufuatiliaji wenu, imani yenu na mambo ambayo mmefanya. Kati yenu nyote, kuna wengi ambao tayari hawawezi kuokolewa, kwani leo ndiyo siku ya kufichua matokeo ya watu, na Sitakanganyikiwa katika kazi Yangu; Sitawaongoza wale wasioweza kuokolewa kabisa katika enzi ifuatayo. Kutakuwa na wakati ambapo kazi Yangu itakuwa imekamilika. Sitafanya kazii juu ya maiti hizo ambazo haziwezi kuokolewa hata kidogo; sasa ndizo siku za mwisho za wokovu wa mwanadamu, na Sitafanya kazi isiyo ya maana. Usishutumu Mbingu na dunia—mwisho wa dunia unakuja. Hauepukiki. Mambo yamefika hapa, na hakuna kitu ambacho wewe kama mwanadamu unaweza kufanya kuyasimamisha; huwezi kubadili vitu jinsi utakavyo. Jana, hukulipa gharama ya kufuatilia ukweli na hukuwa mwaminifu; leo, wakati umewadia, huwezi kuokolewa; na kesho, utaondolewa, na hakutakuwa na uhuru wa matendo kwa ajili ya wokovu wako. Hata ingawa moyo wangu ni mpole na Ninafanya kila Niwezalo kukuokoa, usipojitahidi wewe mwenyewe ama kujifikiria hata kidogo, hili linanihusu vipi? Wale wanaofikiria tu miili yao na wanaofurahia faraja, wale wanaoonekana kuamini lakini wasioamini kwa kweli; wale wanaojihusisha katika uganga na uchawi; wale ambao ni wazinzi, walio duni kabisa; wale wanaoiba sadaka za Yehova na mali Yake; wale wanaopenda hongo; wale walio na njozi za kupaa mbinguni; wale ambao ni wenye majivuno na fidhuli, wanaojitahidi tu kwa sababu ya umaarufu na utajiri wa kibinafsi; wale wanaoeneza maneno yasiyofaa; wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe; wale wanaotoa tu hukumu dhidi ya Mungu Mwenyewe na kumkashifu; wale wanaounda vikundi na kutafuta kujitegemea; wale wanaojitukuza juu ya Mungu, wale wanaume na wanawake wadogo, wa makamo na wakubwa ambao ni wapuuzi na wametegwa katika uasherati; wale wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu na utajiri wa kibinafsi na wanafuatilia hadhi ya kibinafsi miongoni mwa wengine; wale watu wasiotubu walionaswa katika dhambi—je, si wote hawawezi kuokolewa? Uasherati, kutenda dhambi, uganga, uchawi, matusi na maneno yasiyofaayote yamejaa kwenu; na ukweli na maneno ya uzima yanakanyagwa miongoni mwenu, na lugha takatifu inachafuliwa miongoni mwenu. Ninyi Mataifa, mliojaa uchafu na uasi! Matokeo yenu ya mwisho yatakuwa yapi? Je, wale wanaopenda mwili, wanaotenda uchawi wa mwili, na waliotegwa katika dhambi ya uasherati wanawezaje kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi! Je, hujui kwamba watu kama ninyi ni mabuu wasioweza kuokolewa? Ni nini kinachowapa haki ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo katika wale wasiopenda ukweli na wanapenda tu mwili—watu kama hawa wanawezaje kuokolewa? Wale wasiopenda njia ya uzima, wasiomtukuza Mungu ama kumshuhudia, wanaopanga njama kwa ajili ya hadhi yao wenyewe, wanaojisifu sana—je, si bado wao wako vivyo hivyo, hadi leo? Kuna thamani gani katika kuwaokoa? Iwapo unaweza kuokolewa hakutegemei ukubwa wako ama ni miaka mingapi umekuwa ukifanya kazi, sembuse sifa ambazo umeongeza. Badala yake, kunategemea iwapo ufuatiliaji wako umezaa matunda. Unapaswa kujua kwamba wale waliookolewa ni “miti” inayozaa matunda, siyo miti iliyo na majani yaliyositawi sana na maua mengi lakini ambayo hayazai matunda. Hata kama umeshinda miaka mingi ukizurura mitaani, hilo lina maana gani? Ushuhuda wako uko wapi? Uchaji wako wa Mungu ni kidogo sana kuliko upendo wako kwako mwenyewe na hamu zako zenye tamaa—je, si mtu kama huyu ni mpotovu? Anawezaje kuwa kielelezo na mfano wa wokovu? Asili yako ni isiyorekebishika, wewe ni mwasi sana, huwezi kuokolewa! Je, si watu kama hawa ni wale watakaoondolewa? Je, si wakati ambapo kazi Yangu inakamilika ni wakati wa kufika kwa siku yako ya mwisho? Nimefanya kazi nyingi sana na kuzungumza maneno mengi sana miongoni mwenu—kweli mmeyasikiliza kiasi kipi? Mmewahi kutii kiasi kipi? Kazi Yangu ikamilikapo, huo utakuwa wakati ambapo unakoma kunipinga, wakati ambapo unakoma kusimama dhidi Yangu. Nifanyapo kazi, mnanipinga bila kukoma; kamwe hamyatii maneno Yangu. Nafanya kazi Yangu na wewe unafanya “kazi” yako mwenyewe, ukitengeneza ufalme wako mdogo. Ninyi ni kundi la mbweha na mbwa tu, mnaofanya kila kitu kunipinga! Mnajaribu kila wakati kuwakumbatia wale wanaowapa upendo wao wa dhati—uchaji wenu uko wapi? Kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu! Hamna utii wala uchaji, na kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hawa wanaweza kuokolewa? Wanadamu ambao ni waasherati na wakware daima hutaka kuwavutia makahaba wenye ubembe kwao kwa ajili ya raha zao wenyewe. Sitawaokoa mashetani wa kisherati kama hawa hata kidogo. Nawachukia ninyi mashetani wachafu, na ukware na ubembe wenu utawatumbukiza kuzimu. Mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi mashetani wachafu na pepo waovu ni wa kutia kinyaa! Mnachukiza! Watu ovyo kama ninyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi wanaweza kuokolewa bado? Leo, ukweli huu, njia hii, na uzima huu hauwavutii; badala yake mnavutiwa na utendaji dhambi, fedha, hadhi, umaarufu na faida; mnavutiwa na raha za mwili; sura nzuri za wanaume na uzuri wa wanawake. Ni nini kinachowastahiki kuingia katika ufalme Wangu? Sura yenu hata ni ya juu zaidi kuliko ya Mungu, hadhi yenu hata ni ya juu kuliko ya Mungu sembuse fahari yenu kubwa miongoni mwa wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hujageuka kuwa malaika mkuu? Wakati matokeo ya watu yanafichuliwa, ambao pia ndio wakati kazi ya wokovu itakaribia kuisha, wengi kati yenu mtakuwa maiti msioweza kuokolewa na lazima muondolewe. Wakati wa kazi ya wokovu, Mimi ni mwenye huruma na mzuri kwa watu wote. Kazi inapokamilika, matokeo ya watu wa aina tofauti yatafichuliwa, na wakati huo, Sitakuwa mwenye huruma na mzuri tena, kwa kuwa matokeo ya watu yatakuwa yamefichuliwa, na kila mmoja atakuwa ameainishwa kulingana na aina yake, na hakutakuwa na haja ya kufanya kazi zaidi ya wokovu, kwa sababu enzi ya wokovu itakuwa imepita, na kwa sababu imepita, haitarudi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

657. Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, mnaelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata kwa miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii na uasi wenu mwingi dhidi Yangu kwa hii miaka mingi, kwa sababu hakuna mtakatifu hata mmoja kati yenu, nyinyi pia ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba daima Narudia kuzungumza mbele yenu. Sitaki kuishi pamoja na ninyi kwa njia hii—lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, hapa Nitarudia Niliyoyasema kwa mara nyingine tena. Natumaini kuwa mtaweza kuonyesha uelewa zaidi, na Natumai hata zaidi kwamba mtaweza kuamini kila neno Ninalosema, na bado zaidi, kwamba mtaweza kufahamu kwa kina maana ya maneno Yangu. Msiwe na shaka juu ya yale Ninayosema, au hata kuyachukulia maneno Yangu mnavyotaka na kuyatupilia mbali kwa hiari, jambo ambalo Naliona kuwa halistahimiliki. Msiyahukumu maneno Yangu, sembuse hatamsiyachukulie kwa uzito, au kusema kwamba daima Nawajaribu, au mbaya zaidi, mseme kwamba kile ambacho Nimewaambia kinakosa usahihi. Ninaona kuwa mambo haya hayavumiliki. Kwa sababu mnanichukulia Mimi na kuyachukulia Ninayoyasema kwa mashaka na kamwe hamyazingatii, Ninamwambia kila mmoja wenu kwa uzito kabisa: Msiunganishe kile Ninachosema na falsafa, msikiweke pamoja na uongo wa matapeli, na hata zaidi, msiyajibu maneno Yangu kwa dharau. Labda katika siku zijazo hakuna mtu yeyote atakayekuwa na uwezo wa kuwaambia yale Ninayowaambia nyinyi, au kuzungumza na nyinyi kwa huruma sana, sembuse kuwaeleza mambo haya kwa uvumilivu hivi. Siku zijazo zitatumika katika kukumbuka nyakati zile nzuri, au kwa kulia kwa sauti kubwa, au kuugulia kwa maumivu, au mtakuwa mkiishi katika usiku wa giza bila hata chembe ya ukweli au kupewa maisha, au kusubiri tu bila matumaini, au kukaa katika majuto machungu kiasi kwamba hamwezi kufikiri…. Kwa kweli hakuna hata mmoja wenu anayeweza kuepuka uwezekano huu. Kwa sababu hakuna hata mmoja wenu anayechukua nafasi ya kumwabudu Mungu kwa kweli; mnajitumbukiza katika dunia yenye uasherati na maovu, mnachanganya ndani ya imani yenu, ndani ya roho zenu, nafsi, na miili, mambo mengi yasiyohusiana na maisha na ukweli na kwa kweli yanapingana nayo. Hivyo kile Ninachotumaini kwenu ni kuwa mtaweza kuletwa kwenye njia yenye mwanga. Tumaini Langu la pekee ni kwamba mtaweza kuwa na uwezo wa kujijali wenyewe, kujitunza wenyewe, na kwamba hamtaweka mkazo sana kwenye hatima zenu huku mkizitazama tabia zenu na dhambi zenu kwa kutokujali.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

658. Kadri dhambi zako zinavyozidi kuwa nyingi, ndivyo utakavyokuwa na fursa chache za kupata hatima iliyo nzuri. Kinyume chake, kadri dhambi zako zinavyozidi kuwa chache, ndivyo uwezekano wako wa kusifiwa na Mungu unavyoongezeka. Kama dhambi zako zitaongezeka hadi kiwango ambacho haiwezekani tena Mimi kukusamehe, basi utakuwa umepoteza kabisa nafasi yako ya kusamehewa. Hivyo hatima yako haitakuwa ya juu bali chini. Kama huniamini basi kuwa jasiri na ufanye maovu, na kisha uone kile kitakachokupata. Kama wewe ni mtu ambaye utendaji wako wa ukweli ni wenye bidii sana basi kwa hakika una fursa ya kusamehewa dhambi zako, na kiwango cha kutotii kwako kutapungua zaidi na zaidi. Kama wewe ni mtu ambaye hauko tayari kutenda ukweli basi kwa hakika dhambi zako mbele ya Mungu zitaongezeka, kiwango cha kutotii kwako kitaongezeka zaidi na zaidi, mpaka wakati wa mwisho ambapo utakuwa umeangamia kabisa, na huo ndio wakati ambao ndoto yako ya kupendeza ya kupokea baraka itaharibiwa. Usizichukulie dhambi zako kama ni makossa tu ya mtu asiye mkomavu au mpumbavu, usitumie kisingizio kwamba hukutenda ukweli kwa sababu ubora duni wa tabia yako ulikufanya usiweze kuutenda, na hata zaidi, usizichukulie tu dhambi ulizofanya kama ni matendo ya mtu ambaye hakujua vizuri zaidi. Kama unajua vizuri kujisamehe na unajua vizuri kujitendea kwa ukarimu, basi Ninasema wewe ni mwoga ambaye kamwe hautapata ukweli, na dhambi zako kamwe hazitakoma kukuandama, lakini zitakuzuia kuwahi kutosheleza mahitaji ya ukweli na kukufanya milele uwe mwandamani mwaminifu wa Shetani. Ushauri Wangu kwako bado ni huu: Usiwe makini sana kwa hatima yako tu na kutotilia maanani dhambi zako zilizofichika; zichukulie dhambi zako kwa makini, na usikose kutilia maanani dhambi zako zote kwa sababu ya kujali kuhusu hatima yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu

659. Ingawa sehemu ya kiini cha Mungu ni upendo, na Anaitoa rehema yake kwa kila mtu, watu hupuuza na kusahau ukweli kwamba kiini Chake halisi ni heshima vilevile. Kwamba Ana upendo haimaanishi kwamba watu wanaweza kumkosea Yeye wapendavyo na Hana hisia zozote, au miitikio yoyote. Kwamba Ana rehema haimaanishi kwamba Hana kanuni zozote katika jinsi Anavyowatendea watu. Mungu yu hai; kwa kweli Yupo. Yeye si kikaragosi kilichofikiriwa au kitu kingine tu. Kwa kuwa Yeye yuko, tunapaswa kusikiliza kwa makini sauti ya moyo Wake wakati wote, kuzingatia makini mtazamo Wake, na kuzielewa hisia Zake. Hatupaswi kutumia mawazo ya watu kumfafanua Mungu, na hatupaswi kulazimisha mawazo na matamanio ya watu kwa Mungu, na kumfanya Mungu atumie mtindo na kufikiri kwa mwanadamu katika jinsi Anavyowatendea wanadamu. Ukifanya hivyo, basi unamghadhabisha Mungu, unaijaribu hasira ya Mungu, na unapinga heshima ya Mungu! Hivyo basi, baada ya kuelewa ukali na uzito wa suala hili, Ninasihi kila mmoja wenu aliye hapa kuwa makini na wenye busara katika vitendo vyenu. Kuwa makini na wenye busara katika kuongea kwenu. Na kuhusu jinsi mnavyomtendea Mungu, kadiri mnavyokuwa waangalifu na wenye busara zaidi, ndivyo ilivyo bora! Wakati huelewi mtazamo wa Mungu ni nini, usizungumze kwa uzembe, usiwe mzembe katika vitendo vyako, na usipachike majina ovyo ovyo. Na hata zaidi, usikimbilie kufanya hitimisho kiholela. Badala yake, unafaa kusubiri na kutafuta; hili pia ndilo dhihirisho la kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Ikiwa wewe unaweza kufikia kiwango hiki zaidi ya yote, na kuwa na mtazamo huu zaidi ya yote, basi Mungu hatakulaumu kwa upumbavu wako, ujinga wako, na ukosefu wa kuelewa sababu za mambo. Badala yake, kwa sababu ya hofu yako ya kumkosea Mungu, heshima yako kwa mapenzi ya Mungu, na mtazamo wako wa kutaka kumtii, Mungu atakukumbuka, atakuongoza na kukupa mwanga, au kuvumilia uchanga na ujinga wako. Kinyume chake, endapo mtazamo wako Kwake utakuwa usio na heshima—kumhukumu Mungu kiholela, kukisia kiholela, na kufafanua mawazo ya Mungu—Mungu atakupa hukumu, nidhamu, au hata adhabu; au Atakupa kauli. Pengine kauli hii inahusisha matokeo yako. Hivyo basi, Ningali bado nataka kutilia mkazo jambo hili kwa mara nyingine tena: Unapaswa uwe makini na mwenye busara katika kila kitu kinachotoka kwa Mungu. Usiongee kwa uzembe, na usiwe mzembe katika matendo yako. Kabla ya kusema chochote, unafaa kufikiria: Je, kufanya hivi kutamghadhabisha Mungu? Je, kufanya hivi ni kumcha Mungu? Hata katika masuala mepesi, bado unafaa kujaribu kuelewa hakika maswali haya, yafikirie kwa kweli. Ikiwa unaweza kwa kweli kutenda kulingana na kanuni hizi katika nyanja zote, katika mambo yote, kila wakati, na kukubali mtazamo kama huu hasa wakati huelewi kitu, basi Mungu atakuongoza daima na kukupatia njia ya kufuata. Bila kujali ni nini ambacho watu wanaonyesha, Mungu anaona yote waziwazi, dhahiri, na Atakupa utathmini sahihi na unaofaa kwa maonyesho haya. Baada ya kupitia jaribio la mwisho, Mungu atachukua tabia yako yote na kuijumlisha ili kuamua matokeo yako. Matokeo haya yatamshawishi kila mmoja bila shaka lolote. Kile ambacho Ningependa kuwaambia ni kwamba kila kitendo chenu, kila hatua yenu, na kila fikira yenu vyote vitaamua majaliwa yenu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

660. Kuhusu jinsi watu wanavyotafuta na jinsi watu wanavyomkaribia Mungu, mitazamo ya watu ni ya muhimu sana. Usimpuuze Mungu kama vile Yeye ni rundo la hewa tupu linalozunguka nyuma ya kichwa chako. Daima mfikirie Mungu wa imani yako kama Mungu aliye hai, Mungu halisi. Yeye hayupo kule juu kwenye mbingu ya tatu bila chochote cha kufanya. Badala yake, Yeye hutazama kila mara ndani ya moyo wa kila mtu, Akiangalia kile unachotaka kufanya, katika kila neno dogo na kila tendo dogo, Akiangalia jinsi unavyotenda na mtazamo wako kwa Mungu ni upi. Iwe uko radhi kujitolea kwa Mungu au la, tabia yako yote na fikira zako na mawazo yako ya ndani zaidi yako mbele za Mungu, na yanaangaliwa na Yeye. Ni kulingana na tabia yako, kulingana na vitendo vyako, na kulingana na mwelekeo wako kwa Mungu, ambapo maoni Yake kwako, na mwenendo Wake kwako, vinaendelea kubadilika. Mimi Ningependa kutoa ushauri fulani kwa baadhi ya watu. Msijiweke kwenye mikono ya Mungu kama watoto wachanga, kana kwamba Yeye Anapaswa kukupenda sana, kana kwamba Hawezi kamwe kukuacha, na kana kwamba mwelekeo Wake kwako ni imara na usingeweza kubadilika, na Ninawashauri muache kuota ndoto! Mungu ni mwenye haki katika kumtendea kila mtu, na Yeye ni mwaminifu katika mtazamo Wake kwa kazi ya kuwashinda na kuwaokoa watu. Huu ndio usimamizi Wake. Anamtendea kila mmoja kwa umakinifu, na wala si kama kiumbe cha kufugwa cha kucheza nacho. Upendo wa Mungu kwa binadamu si ule wa kudekeza au kupotosha; rehema na uvumilivu Wake kwa wanadamu si wa kuendekeza au kutojali. Kinyume cha mambo, upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kutunza, kuhurumia, na kuheshimu maisha; rehema na uvumilivu Wake vyote vinaonyesha matarajio Yake kwa binadamu; rehema na uvumilivu Wake ndivyo ambavyo binadamu anahitaji ili kuishi. Mungu yuko hai, na kwa hakika Mungu yupo; Mtazamo Wake kwa wanadamu ni wa kanuni, sio sheria ya kiitikadi hata kidogo, na unaweza kubadilika. Mapenzi Yake kwa ubinadamu yanabadilika polepole na kurekebishwa kulingana na wakati, na hali, na mtazamo wa kila mtu. Kwa hiyo, unapaswa kujua ndani ya moyo wako kwa uwazi kabisa kwamba kiini cha Mungu hakibadiliki, na kwamba tabia Yake itajidhihirisha kwa nyakati tofauti na katika mazingira tofauti. Huenda usifikirie kwamba hili si suala zito, na unatumia mawazo yako binafsi kufikiria jinsi Mungu anapaswa kufanya mambo. Lakini kuna nyakati ambapo kinyume kabisa cha mtazamo wako ni kweli, na kwamba kwa kutumia mawazo yako binafsi katika kumjaribu na kumpima Mungu, tayari umemghadhabisha. Hii ni kwa sababu Mungu hafanyi kazi kama unavyofikiria wewe, Naye Mungu hatalishughulikia suala hili kama vile unavyosema Atalishughulikia. Kwa hivyo, Ninakukumbusha uwe makini na mwenye hekima katika mtazamo wako kwa kila kitu, na ujifunze namna ya kufuata kanuni ya kutembea kwenye njia ya Mungu katika mambo yote—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima uimarishe uelewa thabiti katika masuala ya mapenzi ya Mungu na mtazamo wa Mungu; lazima utafute watu walio na nuru ili wakujulishe mambo haya, na ni lazima utafute kwa bidii. Usimwone Mungu wa imani yako kama kikaragosi—ukimhukumu upendavyo, ukifanya hitimisho kiholela kuhusu Yeye, na kumtendea kwa mtazamo usio na heshima. Katika mchakato wa wokovu wa Mungu, Anapoamua matokeo yako, bila kujali kama Yeye atakupa rehema, au uvumilivu, au hukumu na kuadibu, kwa vyovyote vile, mtazamo Wake kwako unabadilika. Inategemea mtazamo wako kwa Mungu, na uelewa wako kuhusu Mungu. Usiruhusu kipengele kimoja cha kupita cha maarifa yako au uelewa wako katika Mungu kumfafanua Yeye milele. Usiamini katika Mungu aliyekufa; amini katika Aliye hai.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

661. Mnatamani sana kwa Mungu kufurahishwa nanyi, lakini bado mko mbali sana na Mungu. Tatizo ni nini hapa? Mnakubali tu maneno Yake, lakini sio ushughulikiaji na upogoaji Wake; hata zaidi hamwezi kukubali mpangilio Wake wote, kuwa na imani kamilifu Kwake. Tatizo, basi, ni gani hapa? Kimsingi, imani yenu ni ganda tupu la yai lisiloweza kutoa kifaranga. Kwani imani yenu haijawaletea ukweli ama kuwapa maisha, na badala imewaletea hisia danganyifu ya tumaini na msaada. Madhumuni ya imani yenu kwa Mungu ni kwa ajili ya tumaini hili na msaada huu badala ya ukweli na maisha. Kwa hivyo, Nasema kwamba mkondo wa imani yenu kwa Mungu si mwingine bali ni kujaribu kujipendekeza kwa Mungu kupitia utumwa na kutokuwa na aibu, na hauwezi kuchukuliwa kuwa imani ya kweli hata kidogo. Kifaranga anaweza kujitokezaje kwa imani kama hii? Kwa maneno mengine, ni tunda lipi ambalo imani kama hii inaweza kuzalisha? Kusudi la imani yenu kwa Mungu ni kumtumia Mungu ili kutimiza malengo yenu. Huu sio ukweli zaidi unaoonyesha kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnaamini kuwepo kwa Mungu aliye mbinguni lakini mnakataa yule Mungu aliye duniani. Hata hivyo, Siidhinishi maoni yenu. Nawapongeza tu wale wanadamu wanaosimama imara na kumtumikia Mungu wa duniani, kamwe sio wale wasiomkiri Kristo aliye duniani. Bila kujali jinsi wanadamu kama hawa walivyo waaminifu kwa Mungu aliye mbinguni, mwishowe, hawatauepuka mkono Wangu unaoadhibu waovu. Wanadamu kama hawa ni waovu; ni wale waovu wanaompinga Mungu na hawajawahi kumtii Kristo kwa furaha. Bila shaka, idadi yao inajumuisha wale wote wasiomjua na, zaidi, wasiomkiri Kristo. Unaamini kwamba unaweza kutenda utakavyo kwa Kristo alimradi wewe ni mwaminifu kwa Mungu aliye mbinguni? Makosa! Kutomjua Kristo kwako ni kutomjua Mungu aliye mbinguni. Haijalishi jinsi ulivyo mwaminifu kwa Mungu aliye mbinguni, ni mazungumzo matupu na ya kujifanya tu, kwani Mungu duniani sio tu chombo muhimu kwa mwanadamu kupokea ukweli na maarifa ya kina zaidi, lakini hata chombo muhimu zaidi kwa lawama ya mwanadamu na baadaye kwa kuukamata ukweli ili kuwaadhibu waovu. Umeelewa matokeo yenye faida na yanayodhuru hapa? Umepata kuyapitia? Ningependa siku moja hivi karibuni ninyi muelewe ukweli huu: Kumjua Mungu, mnapaswa kumjua sio tu Mungu wa mbinguni lakini, hata muhimu zaidi, Mungu aliye duniani. Msiyachanganye yaliyo kipaumbele ama kuruhusu yaliyo ya pili kuchukua nafasi ya yaliyo ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kujenga uhusiano mzuri na Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kupeleka moyo wako karibu na Yeye. Kama umekuwa wa imani kwa miaka nyingi na kushirikiana na Mimi kwa muda mrefu, lakini bado unabaki mbali na Mimi, basi Nasema kwamba ni lazima iwe kuwa mara nyingi unaikosea tabia ya Mungu, na mwisho wako utakuwa mgumu sana kufikiria. Kama miaka mingi ya ushirikiano na Mimi haijakubadilisha kuwa mwanadamu aliye na ubinadamu na ukweli, ila badala yake imeingiza njia zako ovu ndani ya asili yako, na huna maono maradufu ya uwongo kuhusu fahari kuliko awali pekee lakini kutonielewa kwako kumeongezeka pia, kiasi kwamba unakuja kunichukulia kuwa rafiki yako mdogo wa kando, basi Nasema kwamba mateso yako si ya juujuu tena, lakini yamepenya ndani kwa mifupa yako. Yote yaliyosalia ni wewe kusubiri matayarisho ya mazishi yako kufanywa. Huhitaji kunisihi basi Niwe Mungu wako, kwani umetenda dhambi inayostahili kifo, dhambi isiyosameheka. Hata kama Ningeweza kuwa na huruma nawe, Mungu aliye mbinguni Atasisitiza kuchukua maisha yako, kwani kosa lako dhidi ya tabia ya Mungu si shida ya kawaida, lakini lile lililo kubwa sana kiasili. Wakati utakapofika, usinilaumu kwa sababu ya kutokujulisha kabla. Yote yanarudi kwa hili: Wakati unashirikiana na Kristo—Mungu aliye duniani—kama mwanadamu wa kawaida, yaani, unapoamini kwamba Mungu huyu si chochote ila ni mwanadamu, ni hapo basi ndipo utaangamia. Hili ndilo onyo Langu la pekee kwenu nyinyi nyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

662. Kila mwanadamu, katika kuishi maisha yake ya imani katika Mungu, amefanya mambo ambayo yanampinga na kumdanganya Mungu. Baadhi ya matendo mabaya hayahitaji kurekodiwa kama kosa, lakini mengine hayasameheki; kwani mengi ni yale yanayokiuka amri za utawala, ambapo ni kusema, yanaikosea tabia ya Mungu. Wengi ambao wanajali kuhusu hatima zao wenyewewanaweza kuuliza matendo haya ni yapi. Lazima mjue kwamba nyinyi mna kiburi na mna majivuno kiasili, na hamko tayari kuutii ukweli. Kwa sababu hii, Nitawaambia kidogo kidogo baada ya ninyi kuwa mmejitafakari wenyewe. Ninawasihi muwe na ufahamu bora zaidi wa yaliyomo katika amri za utawala, na mfanye bidii kuijua tabia ya Mungu. Vinginevyo, mtapata ugumu sana wa kufunga vinywa vyenu, ndimi zenu zitaropoka kwa uhuru kwa maneno ya kujigamba, na bila kujua mtaikosea tabia ya Mungu na kujipata kwenye giza, mkipoteza uwepo wa Roho Mtakatifu na mwangaza. Kwa sababu ninyi hamna kanuni katika matendo yenu, kwa sababu mnafanya na kusema yale msiyopaswa, basi mtapata adhabu inayowafaa. Lazima ujue kwamba ingawa wewe ni mpotovu katika maneno yako na matendo yako, Mungu ana kanuni katika hayo yote. Sababu ya wewe kupokea adhabu ni kwa sababu umemkosea Mungu na wala si binadamu. Kama, katika maisha yako, unatenda makosa mengi dhidi ya tabia ya Mungu, basi utalazimika kuwa mtoto wa kuzimu. Kwa binadamu inaweza kuonekana kwamba umetenda matendo machache tu yasiyolingana na ukweli na si chochote zaidi. Je, una habari, hata hivyo, kwamba machoni pa Mungu, tayari wewe ni mmoja ambaye kwako hakuna tena sadaka ya dhambi? Kwani umevunja amri za utawala za Mungu zaidi ya mara moja na hujaonyesha ishara yoyote ya kutubu, kwa hivyo huna chaguo lolote ila kutumbukia kuzimu mahali ambapo Mungu anamwadhibu mwanadamu. Idadi ndogo ya watu, wakati wanamfuata Mungu, walifanya baadhi ya matendo ambayo yalikiuka kanuni, lakini baada ya kupogolewa na kupewa mwongozo, waligundua upotovu wao wenyewe hatua kwa hatua, kisha wakaingia kwenye njia sahihi ya ukweli, na wamebaki na msingi mzuri leo. Watu kama hao ndio watakaobaki mwishoni. Hata hivyo, ni wale walio waaminifu ndio Ninaowatafuta; ikiwa wewe ni mtu mwaminifu na ni mtu ambaye unatenda kulingana na kanuni, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu. Kama katika matendo yako huikosei tabia ya Mungu, na unatafuta mapenzi ya Mungu na una moyo wa kumcha Mungu, basi imani yako iko kwenye kiwango kinachotakiwa. Yeyote asiyemcha Mungu na asiye na moyo unaotetemeka kwa hofu kuna uwezekano wa kukiuka kwa urahisi amri za utawala za Mungu. Wengi wanamtumikia Mungu kwa nguvu ya shauku zao, lakini hawana ufahamu wa amri za utawala za Mungu, sembuse hata ufahamu wowote wa maana ya maneno Yake. Na kwa hivyo, kwa nia zao nzuri, mara nyingi wanaishia kufanya mambo ambayo yanatatiza usimamizi wa Mungu. Katika hali mbaya zaidi, wanafukuzwa kutoka kwenye nyumba ya Mungu, wakinyimwa nafasi yoyote zaidi ya kumfuata, na watatupwa kuzimu, hatimaye hawatakuwa na uhusiano mwingine wowote na nyumba ya Mungu. Watu hawa wanafanya kazi katika nyumba ya Mungu kwa nguvu ya nia zao nzuri zisizojua wanaishia kuikasirisha tabia ya Mungu. Watu huleta njia zao za kuwahudumia wakuu na mabwana katika nyumba ya Mungu na kujaribu kuzifanya zitumike, wakidhania kwa kiburi kwamba njia kama hizo zinaweza kutumika hapa kiurahisi. Hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu hana ile tabia ya mwanakondoo bali ile ya simba. Kwa hiyo, wale wanaojihusisha na Mungu kwa mara ya kwanza wanashindwa kuwasiliana na Yeye, kwani moyo wa Mungu ni tofauti na ule wa binadamu. Ni baada tu ya kuelewa ukweli mwingi ndipo utakapoweza kuendelea kumjua Mungu. Maarifa haya si tu maneno wala mafundisho, lakini yanaweza kutumika kama hazina ya kuingia katika matumaini ya kumkaribia Mungu, na uthibitisho kwamba Anafurahishwa na wewe. Kama unakosa uhalisia wa maarifa, na haujajiandaa na ukweli, basi huduma yako ya dhati itakuletea tu kuchukiwa na kudharauliwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

663. Kila sentensi Niliyoizungumza ina tabia ya Mungu ndani yake. Mtafanya vizuri endapo mtatafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka kwa maneno hayo. Dutu ya Mungu ni ngumu sana kuielewa, lakini Ninaamini kwamba angalau nyinyi nyote mna mawazo fulani kuhusu tabia ya Mungu. Ninatumai, basi, kwamba mtanionyesha Mimi na kufanya mengi zaidi ya yale ambayo hayakosei tabia ya Mungu. Kisha Nitatulizwa moyo. Kwa mfano, mweke Mungu moyoni mwako kila wakati. Unapochukua hatua, fanya hivyo kulingana na maneno Yake. Tafuta nia Zake katika kila kitu, na usifanye kile ambacho kitavunjia heshima na kumdhalilisha Mungu. Hata zaidi usimweke Mungu nyuma ya akili yako ili ujaze utupu wa siku zijazo katika moyo wako. Ukifanya hivyo, basi utakuwa umeikosea tabia ya Mungu. Tena, ikitokea kwamba hutawahi kutamka matamshi ya kukufuru au kulalamika dhidi ya Mungu maisha yako yote, na tena ikitokea kwamba unaweza kufanya kikamilifu kila kitu ambacho Amekuaminia wewe na pia kutii maneno Yake yote katika maisha yako yote, basi utakuwa umeweza kuepuka kuasi dhidi ya amri za utawala. Kwa mfano, kama umewahi kusema “Kwa nini sifikirii kwamba Yeye ni Mungu?” “Nafikiri kwamba maneno haya ni nuru kiasi tu ya Roho Mtakatifu,” “Katika maoni yangu, si kila kitu ambacho Mungu anakifanya lazima ni sahihi,” “Ubinadamu wa Mungu hauna ukuu zaidi kuliko wangu,” “Maneno ya Mungu hayaaminiki kabisa,” au matamshi mengine kama hayo ya kuhukumu, basi Nakusihi wewe ukiri na kutubu dhambi zako mara nyingi zaidi. Vinginevyo, hutawahi kuwa na fursa ya msamaha, kwani humkosei mwanadamu, ila Mungu Mwenyewe. Unaweza kuamini kwamba wewe unamhukumu mtu tu, lakini Roho wa Mungu haichukulii hivyo. Wewe kutoheshimu mwili Wake ni sawa na kumvunjia Yeye heshima. Kama hali ni hivi, basi si ni kweli kwamba umeikosea tabia ya Mungu? Lazima ukumbuke kwamba kila kitu kinachofanywa na Roho wa Mungu kinafanywa ili kulinda kazi Yake katika mwili na ili kazi hii ifanywe vizuri. Ukiyapuuza haya, basi Nasema kwamba wewe ni mtu ambaye kamwe hataweza kufaulu katika kumwamini Mungu. Kwani umechochea hasira ya Mungu, kwa hivyo Atatumia adhabu inayofaa ili kukufunza adabu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

664. Baada ya kuelewa tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho, je, umefanya hitimisho lolote kuhusu jinsi unavyopaswa kumtendea? Katika kulijibu swali hili, kwa hitimisho Ningependa kukupa onyo tatu: Kwanza, usimjaribu Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi unachoelewa kuhusu Mungu, haijalishi ni kiwango kipi unachojua kuhusu tabia Yake, kwa vyovyote vile usimjaribu Yeye. Pili, usishindane na Mungu kuhusiana na hadhi. Haijalishi ni aina gani ya hadhi ambayo Mungu anakupa au ni kazi ya aina gani Anayokuaminia kuifanya, haijalishi ni wajibu wa aina gani ambao Atakuinua ili uufanye, na haijalishi ni kiasi kipi ambacho umegharimika au kujitolea kwa ajili ya Mungu, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu kwa hadhi. Tatu, usishindane na Mungu. Haijalishi kama unaelewa au kama unaweza kutii kile ambacho Mungu anakufanyia, kile Anachopanga kwa ajili yako, na mambo Anayokuletea wewe, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu. Kama unaweza kutekeleza onyo hizi tatu, basi utakuwa salama kwa kiasi fulani, na hutamghadhabisha Mungu kwa urahisi.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

665. Labda umeteseka sana katika wakati wako, lakini sasa bado huelewi chochote; hujui kila kitu kuhusu uzima. Ingawa umeadhibiwa na kuhukumiwa, hujabadilika kamwe na ndani yako kabisa hujapata uzima. Wakati wa kutathmini kazi yako utakapofika, utapitia majaribio makali kama moto na hata majonzi makuu zaidi. Moto huu utageuza nafsi yako yote kuwa majivu. Kama mtu ambaye hana uzima, mtu asiye na hata chembe ya dhahabu safi ndani, mtu ambaye bado amekwama na tabia ya zamani ya ufisadi, na mtu ambaye hata hawezi kufanya kazi nzuri ya kuwa foili, unawezaje kutoondolewa? Je, mtu asiye na thamani yoyote, na asiye na uzima, anaweza kuwa na umuhimu wowote katika kazi ya ushindi? Wakati huo ufikapo, siku zenu zitakuwa ngumu zaidi kuliko za Nuhu na Sodoma! Maombi yenu hayatawasaidia wakati huo. Mara tu kazi ya wokovu ikiisha, utaanzaje tena kutubu? Mara tu kazi ya wokovu itakuwa imefanywa, hakutakuwa tena na kazi ya wokovu. Kitakachokuwepo ni mwanzo wa kazi ya kuadhibu uovu. Wewe hupinga, huasi, na hufanya mambo unayojua ni maovu. Je, wewe sio shabaha ya adhabu kali? Ninakuelezea hili wazi leo. Ukichagua kutosikiliza, maafa yatakapokupata baadaye, je, hautakuwa umechelewa ikiwa utaanza kujuta na kuanza kuamini? Nakupa nafasi ya kutubu leo, lakini wewe hauko radhi kufanya hivyo. Unataka kungoja kwa muda gani? Mpaka siku ya kuadibu? Sikumbuki dhambi zako za zamani leo; Nakusamehe tena na tena, kugeuka kutoka upande wako mbaya kutazama tu upande wako mzuri, kwa sababu maneno na kazi Yangu yote ya sasa yanatakiwa kukuokoa wewe na sina nia mbaya kwako. Lakini unakataa kuingia; huwezi kutambua mema kutoka kwa mabaya na hujui namna ya kufurahia wema. Je, mtu wa aina hii hanuii tu kungoja ile adhabu na malipo yenye haki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)

666. Kufanya kazi Kwangu miongoni mwenu sio kabisa sawa na Yehova kufanya kazi katika Israeli, na hasa si sawa na Yesu kufanya kazi Yudea. Ni kwa uvumilivu mkuu ndio Nanena na kufanya kazi, na ni kwa hasira na vilevile hukumu ndio Nawashinda wapotovu hawa. Si chochote kama Yehova kuwaongoza watu Wake katika Israeli. Kazi Yake katika Israeli ilikuwa kutoa chakula na maji ya uzima, na Alijawa huruma na upendo kwa watu Wake katika utoaji Wake wa vitu kwao. Kazi ya leo hufanywa katika taifa ambalo halijachaguliwa, ambalo limelaaniwa. Hakuna chakula tele, wala hakuna ustawishaji wa maji ya uzima ya kukata kiu sembuse utoaji wa bidhaa za mwili za kutosha; kunao tu utoaji wa hukumu, laana, na kuadibu vya kutosha. Hawa mabuu katika lundo la samadi hawastahili kwa uthabiti kupata vilima vya ng’ombe na kondoo, utajiri mwingi, na watoto wazuri zaidi kotekote katika nchi ambavyo Nilitoa kwa Israeli. Israeli ya siku hizi hutoa juu ya madhabahu ng’ombe na kondoo na vitu vya dhahabu na fedha ambavyo Mimi huwastawisha navyo, kushinda sehemu moja ya kumi inayotakiwa na Yehova chini ya sheria, na kwa hiyo Nimewapa hata zaidi, zaidi ya mara mia moja ya kile ambacho Israeli ilikuwa ipate chini ya sheria. Kile ambacho Nastawisha Israeli nacho kinashinda kile ambacho Abrahamu na Isaka walipata. Nitaifanya familia ya Israeli kuzaa na kuongezeka, na Nitawafanya watu Wangu wa Israeli kuenea kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa ulimwengu mzima. Wale ambao Mimi hubariki na kutunza bado ni wateule wa Israeli, yaani, watu ambao hutoa kila kitu Kwangu, ambao wamepata kila kitu kutoka Kwangu. Ni kwa sababu wao huniweka Mimi mawazoni ndiyo wao hutoa sadaka ya ndama na wanakondoo waliozaliwa karibuni juu ya madhabahu Yangu takatifu na hutoa mbele Yangu kila kitu walicho nacho, hata kwa kiwango cha kutoa wana wao wa kwanza waliozaliwa karibuni kwa matarajio ya kurudi Kwangu. Na ninyi je? Ninyi huamsha hasira Yangu, ninyi huwa na matakwa mengi kutoka Kwangu, ninyi huiba sadaka za wale wanaotoa vitu Kwangu na hamjui kwamba mnanikosea Mimi, hivyo mnachopata ni kutoa machozi na adhabu katika giza. Ninyi mmechochea hasira Yangu mara nyingi na Nimenyesha moto Wangu wa kuchoma, kiasi kwamba kumekuwa na wengi waliopatwa na mwisho wa majonzi, ambao makazi yao ya furaha yalikuwa makaburi ya kuhuzunisha. Yote Niliyo nayo kwa mabuu hawa ni hasira isiyoisha, na sina kusudi la baraka. Ni kwa ajili ya kazi Yangu tu ndiyo Nimefanya kinzano na kuwatia ninyi moyo, na kwamba Nimevumilia fedheha kuu kufanya kazi miongoni mwenu. Isingekuwa mapenzi ya Baba Yangu, Ningewezaje kuishi katika nyumba moja na mabuu wanaobingirika kutoka upande mmoja hadi mwingine ndani ya rundo la samadi? Nahisi chuki mno kwa vitendo na maneno yenu yote, na vyovyote vile, kwa sababu Nina “shauku” kiasi katika uchafu na uasi wenu, huu umekuwa mkusanyiko mkubwa wa maneno Yangu. La sivyo Mimi bila shaka singebaki miongoni mwenu kwa muda mrefu hivi. Kwa hiyo, mnapaswa kujua kwamba mtazamo Wangu kuelekea kwenu ni wa upole na huruma tu, mmoja ambao kwao hakuna upendo, ila stahamala tu kwenu, kwa sababu Mimi hufanya hili kwa ajili ya kazi Yangu tu. Na mmeyaona matendo Yangu tu kwa sababu Nimechagua uchafu na uasi kama “mali ghafi.” La sivyo Mimi bila shaka singeyafichua matendo Yangu kwa mabuu hawa; Nafanya tu kazi ndani yenu na usitaji; si chochote kama wepesi na hiari ya kazi Yangu katika Israeli. Nazungumza miongoni mwenu kwa kusita, Nikiibeba hasira Yangu. Isingekuwa kazi Yangu kuu zaidi, Ningewezaje kuvumilia mtazamo wenye kuendelea wa mabuu hawa? Isingekuwa kwa ajili ya jina Langu Ningekuwa Nimepanda vilele vya juu zaidi kitambo na kuwateketeza kabisa hawa mabuu na lundo la samadi! Isingekuwa kwa ajili ya utukufu Wangu, Ningewezaje kuwakubalia pepo hawa waovu kunipinga Mimi waziwazi na vichwa vyao vikitikiswa mbele ya macho Yangu? Isingekuwa kusababisha kazi Yangu kutekelezwa kwa urahisi bila kizuizi hata kidogo, Ningewezaje kuwakubalia hawa watu wanaofanana mabuu kunitusi Mimi kwa utukutu? Kama watu mia moja kijijini mwa Israeli wangeinuka kunipinga Mimi hivi, hata kama wangetoa sadaka Kwangu bado Ningewafutilia mbali chini ya nyufa zilizo ardhini ili watu katika miji mingine hawangeasi tena. Mimi ni moto uteketezao na Sivumilii kosa. Kwa sababu wanadamu wote waliumbwa na Mimi, chochote Nisemacho na kufanya, watu lazima watii na hawawezi kukiasi. Watu hawana haki ya kuingilia kazi Yangu, na wao hasa siyo wenye sifa zinazostahili kuchambua kilicho cha kweli au chenye makosa katika kazi Yangu na maneno Yangu. Mimi ni Bwana wa uumbaji, na viumbe wanapaswa kutimiza kila kitu Ninachohitaji kwa moyo wa kunicha Mimi; hawapaswi kutoa sababu ili kunishawishi Mimi na wao hasa hawapaswi kunipinga. Ninatumia mamlaka Yangu kuwatawala watu Wangu, na wale wote ambao ni sehemu ya uumbaji Wangu wanapaswa kuyatii mamlaka Yangu. Ingawa leo ninyi ni, jasiri na wenye kiburi mbele Yangu, ninyi hukaidi maneno ambayo Nawafunzia, na hamwogopi, Mimi hukumbana tu na uasi wenu na uvumilivu. Singekasirika na kuathiri kazi Yangu kwa sababu mabuu wadogo sana walipindua uchafu katika rundo la samadi. Mimi huvumilia kuendelea kuwepo kwa kila kitu ambacho Mimi huchukia kabisa na mambo ambayo Mimi huchukia kabisa kwa ajili ya mapenzi ya Baba Yangu, mpaka matamshi Yangu yawe kamili, mpaka dakika Yangu ya mwisho kabisa. Usijali! Siwezi kuzama katika kiwango sawa na buu asiyefaa kutajwa, na Sitafananisha kiwango cha ujuzi na wewe. Nakuchukia kabisa, ilhali Naweza kuvumilia. Wewe hunikaidi Mimi, ilhali huwezi kuepuka siku ya Mimi kukuadibu ambayo Baba Yangu ameniahidi Mimi. Je, buu aliyeumbwa anaweza kufananishwa na Bwana wa uumbaji wote? Katika majira ya kupukutika kwa majani, majani yaangukayo hurudi kwa mizizi yake, wewe hurudi kwa nyumba ya “baba” yako, na Mimi hurudi ubavuni pa Baba Yangu. Mimi huandamana na upendo mwema wa Baba Yangu, na wewe hufuatwa na kuvyogwa kwa baba Yako. Nina utukufu wa Baba Yangu, na wewe una aibu ya baba yako. Mimi hutumia kuadibu ambako Nimeshikilia kwa muda mrefu kuandamana na wewe, na wewe hukutana na kuadibu Kwangu na mwili wako uliooza ambao tayari umekuwa mpotovu kwa makumi ya maelfu ya miaka. Nimehitimisha kazi Yangu ya maneno ndani yako, ikiandamana na uvumilivu, na umeanza kutimiza wajibu wa kupitia msiba kutoka kwa maneno Yangu. Mimi hufurahia sana na kufanya kazi katika Israeli; wewe hulia na kusaga meno yako na huishi na kufa matopeni. Nimepata tena umbo Langu la asili na Sibaki tena ndani ya uchafu na wewe, huku umepata tena ubaya wako wa asili na bado unafukua kila mahali katika lundo la samadi. Wakati ambapo kazi na maneno Yangu yatakamilika, itakuwa siku ya furaha Kwangu. Wakati ambapo upinzani na uasi wako utakwisha, itakuwa siku ya kulia kwako machozi. Sitakuonea huruma, na hutaniona Mimi tena. Sitakuwa tena na mazungumzo na wewe, na hutakutana na Mimi tena. Nitachukia uasi wako, na utakosa kupendeza Kwangu. Nitakupiga wewe, na utanikosa Mimi. Nitaondoka kwako kwa furaha, na utafahamu deni lako Kwangu. Sitakuona wewe tena, lakini wewe kila mara utanitarajia Mimi. Nitakuchukia kwa sababu unanipinga Mimi sasa, na utanikosa Mimi; kwa sababu Nakuadibu sasa. Siko radhi kuishi ubavuni pako, lakini utalitamani sana kwa uchungu na kulia machozi katika milele, kwa sababu utajuta kila kitu ambacho umenifanyia Mimi. Utahisi majuto kwa ajili ya uasi na upinzani wako, hata utalala kifudifudi chini kwa majuto na kuanguka chini mbele Yangu na kuapa kutonitii tena. Katika moyo wako, hata hivyo, utanipenda Mimi tu, ilhali hutaweza kamwe kusikia sauti Yangu, Nitakufanya ujionee haya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

667. Sasa Ninatazama mwili wako usiozuiwa ambao umenibembeleza Mimi, na Nina onyo dogo tu kwako—ingawa Situmii kuadibu “kukusubiri” wewe. Unapaswa kujua ni jukumu gani unalobeba katika kazi Yangu, na ndipo Nitaridhika. Zaidi ya haya, ukinipinga Mimi au kutumia pesa Zangu, au kula sadaka za Mimi, Yehova, au ninyi mabuu mnaumana, au kuna ugomvi au kuingiliana kati ya ninyi viumbe mfano wa mbwa—Sihusiki na yoyote kati ya hayo. Mnahitaji tu kujua ninyi ni vitu vya aina gani, na Nitaridhika. Mbali na vitu hivi, ni sawa kama mko radhi kuvutiana panga au mikuki au kupigana kwa maneno yenu. Sina tamaa ya kuingilia mambo hayo, na Mimi sihusiki hata kidogo katika mambo ya binadamu. Sio kwamba Sijali kuhusu ugomvi kati yenu, lakini ni kwa sababu Mimi si mmoja wenu, hivyo, Sishiriki katika mambo yaliyo kati yenu. Mimi Mwenyewe si mmoja si kiumbe na si wa dunia hii, kwa hiyo, Nachukia kabisa maisha ya kuharakisha miongoni mwa watu na hayo mahusiano yasiyofaa, yasiyofaa kati ya watu. Mimi hasa Nachukia kabisa hayo makundi ya makelele ya watu. Hata hivyo, Najua kwa kina uchafu ndani ya mioyo ya kila kiumbe, na kabla ya Mimi kuwaumba ninyi, Nilijua tayari udhalimu uliokuwepo ndani ya kina cha mioyo ya binadamu, na Niliujua udanganyifu na uhalifu wote katika mioyo ya binadamu. Kwa hiyo, hata ingawa hakuna kabisa dalili zozote wakati ambapo watu hufanya mambo ya udhalimu, bado Najua kwamba udhalimu uliowekwa ndani ya mioyo yenu hushinda utajiri wa vitu vyote Nilivyoumba. Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote, mkitafuta mahali pa amani na mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani? Ninyi, minyoo wadogo wenye uvundo mnaiba sadaka kutoka kwa madhabahu ya Mimi, Yehova; kwa kufanya hivyo, mnaweza kuokoa majina yenu yaliyoharibika, yenye kasoro kuwa wateule wa Israeli? Ninyi ni mafukara wasio na haya! Hizo sadaka juu ya madhabahu zilizotolewa Kwangu na watu, kuonyesha hisia karimu kutoka kwa wale ambao hunicha Mimi. Ni za udhibiti Wangu na za matumizi Yangu, kwa hiyo inawezekanaje wewe kuniibia Mimi hua wadogo waliotolewa na watu? Je, huogopi kuwa Yuda? Je, huogopi nchi yako kuwa “konde la damu”? Wewe kitu kisicho na haya! Unadhani kwamba hua waliotolewa na watu wote ni wa kustawisha tumbo la wewe buu? Kile ambacho Nimekupa ni kile ambacho Nimefurahia na kuwa radhi kukupa wewe; kile ambacho Sijakupa kiko chini ya Mamlaka Yangu, na huwezi tu kuiba sadaka Yangu. Yule Anayefanya kazi ni Mimi, Yehova—Bwana wa uumbaji, na sababu ya watu kutoa sadaka ni Mimi. Unadhani kwamba ni fidia ya kukimbia kila mahali ambako wewe hufanya? Wewe kwa kweli ni usiye na haya! Ni nani ambaye unamkimbilia kila mahali? Je, si kwa ajili yako mwenyewe? Kwa nini wewe huiba sadaka Zangu? Kwa nini wewe huiba pesa kutoka kwa mfuko Wangu wa pesa? Je, wewe si mwana wa Yuda Iskariote? Sadaka Zangu, za Yehova, ni za kufurahiwa na makuhani. Je, wewe ni kuhani? Wewe huthubutu kula kwa kujisikia sadaka Zangu na hata unazitandaza juu ya meza; huna thamani yoyote! Wewe fukara asiye na thamani! Moto Wangu, wa Yehova, utakuteketeza wewe!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

668. Nimefanya kazi na kuzungumza kwa njia hii miongoni mwenu, Nimetumia nguvu na juhudi nyingi sana, ilhali ni lini mmewahi kusikiliza kile Ninachowaambia kwa uwazi? Ni wapi mmeniinamia Mimi, Mwenyezi? Kwa nini mnanitendea namna hii? Kwa nini kila kitu mnachokisema na kufanya huchochea hasira Yangu? Kwa nini mioyo yenu ni migumu sana? Je, Nimewahi kuwapiga? Kwa nini hamfanyi kitu chochote kingine ila kunifanya mwenye huzuni na wasiwasi? Mnasubiri siku ya ghadhabu Yangu, Yehova, kuja juu yenu? Je, mnanisubiri Mimi kutuma hasira kwenu iliyochochewa na makosa yenu? Si kila kitu Ninachokifanya ni kwa ajili yenu? Ilhali kila wakati mmenitendea Mimi, Yehova, kwa njia hii: kuiba sadaka Zangu, kupeleka sadaka ya madhabahu Yangu nyumbani kwa jamii ya mbwa mwitu kuwalisha wana wa mbwa mwitu na vitukuu vyake; watu wanapigana wenyewe kwa wenyewe, wakikabiliana na mtazamo wa hasira kwa panga na mikuki, kurusha maneno ya Mimi, Mwenyezi, kwenye choo kuwa machafu kama kinyesi. Uadilifu wenu uko wapi? Ubinadamu wenu umekuwa unyama! Mioyo yenu kwa muda mrefu imegeuka kuwa jiwe. Je, hamjui kwamba siku Yangu ya ghadhabu itakapofika itakuwa ndio wakati Nitakapokuhukumu mabaya mliyotenda dhidi Yangu leo, Mwenyezi? Je, mnafikiri kwamba kwa kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa kutupa maneno Yangu katika matope na kutoyasikiliza—unafikiri kwamba kwa kutenda namna hii nyuma Yangu mnaweza kutoroka macho Yangu ya ghadhabu? Je, hamjui kwamba mlikuwa tayari mmeonekana kwa macho Yangu, Yehova, mlipoiba sadaka Yangu na kutamani mali Yangu? Je, hamjui kwamba wakati mliiba sadaka Yangu, ilikuwa mbele ya madhabahu ambapo dhabihu hutolewa? Mnawezaje kujiamini wenyewe mlivyo wajanja kutosha kunidanganya Mimi kwa njia hii? Ghadhabu Yangu kali ingewezaje kuondoka kutoka katika dhambi zenu za kuchukiza? Ghadhabu Yangu yenye hasira ingepitaje juu ya matendo yenu maovu? Maovu mnayotenda leo hayawafungulii njia yenu kutokea, bali huhifadhi kuadibu kwa ajili ya kesho yenu; yanachochea kuadibu Kwangu, Mwenyezi, kwenu. Matendo yenu maovu na maneno yenu mabaya yangewezaje kuepuka kuadibu Kwangu? Maombi yenu yangeyafikiaje masikio Yangu? Ningefunguaje njia kwa ajili ya udhalimu wenu? Ningewezaje kuyatupilia mbali matendo yenu maovu ya kunikaidi? Ingewezekanaje Nisizikate ndimi zenu ambazo ni za sumu kama ya nyoka? Hamniombi msaada kwa ajili ya haki yenu, lakini badala yake mnahifadhi ghadhabu Yangu kama matokeo ya udhalimu wenu. Ningewezaje kuwasamehe? Katika macho Yangu, Mwenyezi, maneno na matendo yenu ni machafu. Macho Yangu, Mwenyezi, huona udhalimu wenu kama kuadibu kusikolegea. Kuadibu Kwangu kwa haki na hukumu vingeondokaje kwenu? Kwa sababu mmenitendea hivi, na kunifanya mwenye huzuni na ghadhabu, Ningewaachaje nyinyi muepe kutoka mikono Yangu na muondoke katika siku ambayo Mimi, Yehova, Nawaadibu na kuwalaani nyinyi? Je, hamjui kwamba maneno na matamshi yenu yote maovu tayari yamefika masikioni Mwangu? Je, hamjui kwamba udhalimu wenu tayari umechafua vazi Langu takatifu la haki? Je, hamjui kwamba kutotii kwenu tayari kumechochea hasira Yangu kali? Je, hamjui kwamba kwa muda mrefu mmeniacha Nikitokota, na kwa muda mrefu mmeujaribu uvumilivu Wangu? Je, hamjui kwamba tayari mmeshauharibu mwili Wangu kuwa matambara? Nimevumilia mpaka sasa, kiasi kwamba Natoa hasira Zangu, kutokuwa mvumilivu kwenu tena. Je, hamjui kwamba matendo yenu maovu tayari yamefika machoni Mwangu, na kwamba kilio changu tayari kimefika masikioni mwa Baba Yangu? Angewaruhusu vipi mnitendee Mimi jinsi hii? Kuna kazi yoyote Ninayofanya ndani yenu isiyo kwa ajili yenu? Ilhali nani kati yenu amekuwa na upendo zaidi kwa kazi Yangu, Yehova? Ningeweza kutokuwa mwaminifu kwa mapenzi ya Baba Yangu kwa sababu Mimi ni mnyonge, na kwa sababu ya uchungu Nilioupitia? Je, hamwelewi Moyo Wangu? Nasema na ninyi kama Yehova alivyofanya; je, Sijajinyima mengi kwa ajili yenu? Hata ingawa Niko tayari kuvumilia mateso haya yote kwa ajili ya kazi ya Baba Yangu, ni jinsi gani nyinyi mnaweza kuachwa huru kutokana na kuadibu ambako Nawaleteeni kama matokeo ya mateso Yangu? Je, hamjanifurahia kwa wingi sana? Leo, Nimekabidhiwa kwenu na Baba Yangu; hamfahamu kwamba mnafurahia zaidi ya maneno Yangu mengi? Je, hamjui kwamba maisha Yangu yalibadilishwa na maisha yenu na mambo yote mnayofurahia? Je, hamjui kwamba Baba Yangu alitumia maisha Yangu kupigana na Shetani, na kwamba Yeye pia ametoa maisha Yangu kwenu, na kusababisha nyinyi kupokea mara mia zaidi, na kuwaruhusu kuepuka majaribu mengi? Je, hamjui kwamba ni kwa njia ya Kazi Yangu kwamba mmepewa msamaha kutokana na vishawishi vingi, na kuadibu kwingi kukali? Je, hamjui kwamba ni kwa sababu Yangu tu ndio Baba Yangu anawaruhusu kufurahia mpaka sasa? Jinsi gani mmebaki wagumu na wasiyoyumba leo, kiasi kwamba ni kana kwamba ugume umemea rohoni mwenu? Maovu mnayoyatenda leo yangeepukaje siku ya ghadhabu itakayofuata kuondoka Kwangu duniani? Ningewezaje kuwaruhusu wale ambao ni wagumu na wasiokubali kuepuka hasira ya Yehova?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

669. Tafakarini kuhusu siku za nyuma: Ni lini macho Yangu yamekuwa na hasira, na sauti Yangu kuwa kali, kwenu? Ni wakati upi Nimegombana nanyi? Ni wakati upi Nimewakaripia bila sababu? Ni wakati upi Nimewakemea usoni mwenu? Je, si ni kwa ajili ya kazi Yangu ndio kwamba Mimi namwomba Baba Yangu kuwaweka mbali na majaribu? Kwa nini mnanitendea Mimi hivi? Je, Nimewahi kutumia mamlaka Yangu kuipiga miili yenu? Kwa nini mnanilipa Mimi kwa njia hii? Baada ya ninyi kuwa moto na baridi Kwangu, nyinyi si moto wala baridi, na kisha mnajaribu kunirairai Mimi na kuficha mambo kutoka Kwangu, na vinywa vyenu vimejaa mate ya wasio haki. Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kumdanganya Roho Wangu? Je, mnafikiri kwamba ndimi zenu zinaweza kuepuka ghadhabu Yangu? Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kupitisha hukumu kwa matendo Yangu, Yehova, jinsi zinavyopenda? Je, Mimi ni Mungu ambaye mwanadamu hupishia hukumu? Ningewezaje kuruhusu buu dogo linikufuru hivyo? Ningewezaje kudai wana wa uasi kuwa miongoni mwa baraka Zangu za milele? Maneno na matendo yenu kwa muda mrefu yamewafichua na kuwahukumu. Nilipozitandaza mbingu na kuumba vitu vyote, Sikuruhusu kiumbe chochote kushiriki jinsi kitakavyo, sembuse Sikuruhusu kitu chochote kuvuruga kazi Yangu na usimamizi Wangu jinsi kilivyotaka. Sikuvumilia mtu au kitu chochote; Ningewezaje kuwaacha walio wakatili na wa kinyama Kwangu? Ningewezaje kuwasamehe wale ambao wanaasi dhidi ya maneno Yangu? Ningewezaje kuwaacha wanaoniasi? Je, majaliwa ya mwanadamu hayako katika mikono Yangu, Mwenyezi? Ningeuchukua vipi udhalimu wako na uasi kama vitu vitakatifu? Jinsi gani dhambi zako zingenajisi utakatifu Wangu? Mimi sijanajisika na uchafu wa wasio haki, wala kufurahia sadaka ya wasio haki. Kama ungekuwa mwaminifu Kwangu, Yehova, je, ungeweza kujichukulia sadaka kutoka katika madhabahu Yangu? Je, ungeweza kutumia ulimi wako wa sumu kukufuru jina Langu takatifu? Ungeweza kuliasi neno Langu kwa njia hii? Je, ungeweza kuuchukua utukufu Wangu na jina langu takatifu kama chombo ambacho kwalo unamtumikia Shetani, yule mwovu? Maisha Yangu yametolewa kwa ajili ya furaha ya watakatifu. Ningewezaje kukuruhusu ucheze na maisha Yangu jinsi utakavyo, na kuyatumia kama chombo kwa ajili ya migogoro kati yenu? Mngewezaje kuwa wakatili sana, na watovu sana katika njia ya wenye wema, katika jinsi mlivyo Kwangu? Je, hamjui kwamba tayari Nimeandika matendo yenu maovu katika neno hili la maisha? Jinsi gani mngeweza kuepuka siku ya ghadhabu Ninapoadibu Misri? Ningewezaje kuwaruhusu kunipinga na kuniasi kwa njia hii, mara kwa mara? Nawaambia wazi, siku itakapokuja, basi kuadibu kwenu kutakuwa kusikovumilika zaidi kuliko ile ya Misri! Mnawezaje kuitoroka siku ya ghadhabu Yangu? Nawaambia kwa kweli: Uvumilivu Wangu ulitayarishwa kwa ajili ya matendo yenu maovu, na upo kwa ajili ya kuadibu kwenu siku hiyo. Je, ninyi si wale mtakaopata hukumu ya ghadhabu Yangu punde Nifikapo mwisho wa uvumilivu Wangu? Si mambo yote yapo mikononi Mwangu, Mwenyezi? Ningewezaje kuwaruhusu mniasi hivyo, chini ya mbingu? Maisha yenu yatakuwa magumu sana kwa kuwa mmekutana na Masiha, ambaye ilisemekana Angekuja, lakini ambaye kamwe Hakuja. Je, si nyinyi ni maadui Wake? Yesu amekuwa rafiki wenu, lakini bado mu maadui wa Masiha. Je, hamjui kwamba ingawa nyinyi ni marafiki wa Yesu, matendo yenu maovu yamejaza vyombo vya wale ambao ni wa kuchukiza? Ingawa nyinyi mu karibu sana na Yehova, je, hamjui kwamba maneno yenu mabaya yamefikia masikio ya Yehova na kuchochea ghadhabu Yake? Ingekuwaje awe karibu nawe, na jinsi gani Yeye asingevichoma hivyo vyombo vyako, ambavyo vimejaa matendo mabaya? Ingekuwaje Asiwe adui wako?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

670. Ninyi nyote huketi kwenye viti vya umbuji, mkiwakaripia wale wa vizazi vidogo ambao ni wa namna yenu na mkiwafanya waketi pamoja nanyi. Ila hamjui kwamba “wazawa” wenu waliishiwa na pumzi kitambo sana na kuipoteza kazi Yangu. Utukufu Wangu unang’aa kutoka katika nchi ya Mashariki hadi katika nchi ya Magharibi, lakini utakapoenea hadi miisho ya dunia na kuanza kuinuka na kuangaza, Nitauchukua utukufu Wangu kutoka Mashariki na kuuleta Magharibi ili kwamba watu waovu, ambao wamenitelekeza huko Mashariki watanyimwa mwangaza kuanzia wakati huo na kuendelea. Hilo litakapofanyika, mtaishi katika bonde la kivuli. Hata ingawa watu siku hizi ni bora mara mia moja kuliko hapo awali, bado hawawezi kutimiza matakwa Yangu, na bado wao sio ushuhuda kwa utukufu Wangu. Kwamba mnaweza kuwa bora mara mia moja kuliko hapo awali ni matokeo ya kazi Yangu kabisa; ni matunda yatokanayo na kazi Yangu duniani. Hata hivyo, bado Ninahisi kuchukizwa na maneno na matendo yenu, na vile vile na tabia yenu, na Ninahisi chuki kubwa sana kuhusu jinsi mnavyotenda mbele Yangu, kwa kuwa hamna ufahamu wowote kunihusu. Basi, mnawezaje kuja kuishi kwa kudhihirisha utukufu Wangu, na mnawezaje kuwa waaminifu kabisa kwa kazi Yangu ya baadaye? Imani yenu ni ya kupendeza sana; mnasema kwamba mko tayari kutumia maisha yenu yote kwa ajili ya kazi Yangu, na kwamba mko tayari kutoa maisha yenu kwa ajili ya kazi hiyo, lakini tabia zenu hazijabadilika sana. Mnazungumza tu kwa kiburi, licha ya ukweli kwamba tabia yenu halisi ni mbovu sana. Ni kana kwamba ndimi na midomo ya watu iko mbinguni lakini miguu yao iko chini duniani, na kwa sababu hiyo, maneno na matendo yao na sifa zao bado ni mbovu na zisizoheshimika. Sifa zenu zimeharibiwa, tabia yenu imepotoka, njia yenu ya kuzungumza ni duni, na maisha yenu ni yenye kustahili dharau; hata ubinadamu wenu wote umezama katika hali duni ya chini kabisa. Ninyi ni wenye mawazo finyu kuhusu wengine, na ninyi hubishana kuhusu kila jambo dogo. Ninyi hugombana kuhusu heshima na hadhi zenu wenyewe, hadi kufikia kiwango ambapo mko tayari kushuka kuzimu na kuingia kwenye ziwa la moto. Maneno na matendo yenu ya sasa yanatosha Mimi kubaini kwamba ninyi ni wenye dhambi. Mitazamo yenu kwa kazi Yangu inatosha Mimi kubaini kuwa ninyi ni wadhalimu, na tabia zenu zote zinatosha kuonyesha kwamba ninyi ni watu wachafu mliojaa machukizo. Maonyesho yenu na kile mnachofichua vinatosha kusema kwamba ninyi ni watu ambao mmekunywa damu ya roho wachafu hadi mkatosheka. Kuingia katika ufalme kunapotajwa, hamfichui hisia zenu. Je, mnaamini ya kwamba jinsi mlivyo sasa inatosha kwa ninyi kupita katika lango la kuingia katika ufalme Wangu wa mbinguni? Je, mnaamini ya kwamba mnaweza kuingia katika nchi takatifu ya kazi na maneno Yangu, bila maneno na matendo yenu wenyewe kujaribiwa na Mimi kwanza? Ni nani anayeweza kunihadaa? Tabia na mazungumzo yenu yenye kustahili dharau na yaliyo duni yanaweza kuepukaje macho Yangu? Maisha yenu yamebainiwa na Mimi kuwa maisha ya kunywa damu na kula nyama ya roho hao wachafu kwa sababu ninyi huwaiga mbele Yangu kila siku. Mbele Yangu, tabia yenu imekuwa mbaya hasa, kwa hiyo Ninawezaje kukosa kuwaona kuwa wenye kuchukiza? Maneno yenu yana uchafu wa roho wachafu: Mnabembeleza, kuficha na kujipendekeza kama tu wale wanaoshiriki katika uchawi na kama wale walio wadanganyifu na wanaokunywa damu ya wadhalimu. Maonyesho yote ya mwanadamu ni dhalimu mno, kwa hivyo watu wote wanaweza kuwekwaje katika nchi takatifu ambako wenye haki wako? Je, unafikiri kwamba hiyo tabia yako yenye kustahili dharau inaweza kukubainisha kama mtakatifu ikilinganishwa na wale wadhalimu? Ulimi wako ulio kama wa nyoka hatimaye utauangamiza huu mwili wako ambao huleta uharibifu na kutekeleza machukizo, na hiyo mikono yako iliyojaa damu ya roho wachafu pia hatimaye itaipeleka roho yako jehanamu. Basi, kwa nini huipokei kwa furaha nyingi fursa hii ili uitakase mikono yako iliyojaa uchafu? Na kwa nini huchukui fursa hii kwa manufaa yako uukate huo ulimi wako unaozungumza maneno ya kudhulumu? Je, inawezekana kwamba uko tayari kuteseka katika moto wa jehanamu kwa ajili ya mikono, ulimi na midomo yako? Mimi huuchunga moyo wa kila mtu kwa macho yote mawili, kwa sababu muda mrefu kabla Niwaumbe wanadamu, Nilikuwa nimeifumbata mioyo yao mikononi Mwangu. Nilikuwa nimeibaini mioyo ya watu kitambo, kwa hiyo mawazo yao yangeyaepukaje macho Yangu? Muda utakosaje kuwa umewaishia wa kuepuka kuchomwa na Roho Wangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

671. Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika imeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kuhusu kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu? Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi? Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu. Bila ubinafsi Nimewapa kila kitu, ili kwamba hata kama mnateseka, mmepata kutoka Kwangu kila kitu Nilichokileta kutoka mbinguni. Lakini hamna kujitolea kamwe, na hata kama mna mchango mdogo, mnalipa deni baada ya hapo. Je, si mchango wako utakuwa bure? Kile ambacho umenipa si chochote isipokuwa chembe moja ya mchanga, lakini kile ulichoomba kutoka Kwangu ni tani moja ya dhahabu. Je, si wewe unakuwa muhali? Ninafanya kazi miongoni mwenu. Hakuna kabisa dalili ya asilimia kumi ambayo Ninapaswa kupata, sembuse dhabihu za ziada. Zaidi ya hayo, asilimia kumi inayochangwa na wale ambao ni wacha Mungu inachukuliwa na wale waovu. Je, si nyinyi wote mmetawanyika kutoka Kwangu? Je, si nyinyi nyote mna uhasama na Mimi? Je, si nyinyi nyote mnaharibu madhabahu Yangu? Je, mtu wa aina hii anawezaje kuonekana kama hazina machoni Pangu? Je, si yeye ni nguruwe, mbwa ambao Ninawachukia? Ningewezaje kurejelea uovu wenu kama hazina? Kazi Yangu kwa kweli ni ya nani? Inawezekana kuwa tu ni ya kuwapiga nyinyi nyote ili kufichua mamlaka Yangu? Je, si maisha yenu yameshikiliwa na neno moja kutoka Kwangu? Ni kwa nini Ninatumia maneno tu kuwaagiza na Sijayageuza maneno kuwa ukweli ili kuwapiga haraka iwezekanavyo? Je, maneno Yangu na kazi Yangu ni ya kuwapiga wanadamu tu? Je, Mimi ni Mungu ambaye huwaua wasio na hatia bila ubaguzi? Hivi sasa, ni wangapi wenu ambao wako hapo mbele Yangu ambao wanatafuta njia sahihi ya maisha ya mwanadamu na nafsi zao nzima? Ni miili yenu tu iliyo mbele Yangu, lakini mioyo yenu iko huru, na iko mbali, mbali na Mimi. Kwa sababu hamjui kwa kweli kazi Yangu ni nini, kuna baadhi yenu ambao mnataka kuondoka Kwangu, mnaojitenga na Mimi, na mnataka kuishi katika mahali hapo pa raha ambapo hakuna kuadibu, hakuna hukumu. Je, hili ndilo watu wanatamani katika mioyo yao? Mimi hakika sikulazimishi. Njia yoyote utakayoichukua ni uchaguzi wako mwenyewe, na njia ya leo huenda sambamba na hukumu na laana, lakini nyote mnapaswa kujua kwamba kile Nilichowapa, iwe ni hukumu au kuadibu, zote ni zawadi bora kabisa Ninazoweza kuwapa, na vyote ni vitu ambavyo mnahitaji kwa dharura.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

672. Nafsi zote zilizopotoshwa na Shetani zimeshikwa mateka katika miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa, waliookolewa kutoka katika kambi ya Shetani, na kuletwa ndani ya ufalme wa leo. Watu hawa hawaishi tena chini ya ushawishi wa Shetani. Hata hivyo, asili ya mwanadamu bado imekita mizizi katika mwili wa mwanadamu, yaani, ingawa nafsi zenu zimeokolewa, asili yenu bado ni sawa na ilivyokuwa hapo awali, na uwezekano kwamba mtanisaliti unabaki kuwa asilimia mia moja. Hii ndiyo sababu kazi Yangu inadumu kwa muda mrefu sana, kwa kuwa asili yenu haiwezi kudhibitiwa kwa urahisi. Sasa, ninyi nyote mnapitia magumu kadri ya uwezo wenu mnapotimiza wajibu wenu, ilhali kila mmoja wenu anaweza kunisaliti na kurudi katika miliki ya Shetani, kambini mwake, na kurudia maisha yenu ya zamani—huu ni ukweli usiopingika. Wakati huo, haitawezekana kwenu kudhihirisha chembe ya ubinadamu au mfano wa binadamu, kama mnavyofanya sasa. Katika hali mbaya zaidi, mtaangamizwa, na zaidi ya hayo, mtahukumiwa milele, mtaadhibiwa vikali, msizaliwe upya kamwe. Hili ndilo tatizo lililowekwa mbele yenu. Ninawakumbusha kwa njia hii, kwanza, ni ili kazi Yangu isiwe imekuwa ya bure, na pili, ni ili ninyi nyote muweze kuishi katika siku zenye nuru. Kwa kweli, kama kazi Yangu ni ya bure si tatizo kubwa sana. Jambo la muhimu sana ni kwamba mnaweza kuwa na maisha yenye furaha na mustakabali mzuri sana. Kazi Yangu ni kazi ya kuziokoa nafsi za watu. Nafsi yako ikianguka mikononi mwa Shetani, mwili wako hautaishi kwa amani. Ikiwa Ninaulinda mwili wako, hakika nafsi yako pia itakuwa chini ya uangalizi Wangu. Nikikuchukia sana, mwili na nafsi yako vitaanguka mikononi mwa Shetani mara moja. Je, unaweza kukisia hali yako kwa wakati huo? Ikiwa, siku moja mtayapuuza maneno Yangu, basi Nitawakabidhi nyote kwa Shetani, ambaye atawatesa sana hadi hasira Yangu itakapoisha kabisa, au Mimi binafsi Nitawaadhibu ninyi wanadamu msioweza kuokoleka, kwa kuwa mioyo yenu inayonisaliti haitakuwa imewahi kubadilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

673. Natarajia tu kuwa katika hatua ya mwisho ya kazi Yangu, mtaweza kutoa utendaji wenu bora zaidi, na kwamba mtajitolea kwa moyo wote, na wala sio shingo upande tena. Bila shaka, Natarajia pia kuwa nyote mtaweza kuwa na hatima nzuri. Hata hivyo, bado Nina mahitaji Yangu ambayo ni kwa nyinyi kufanya uamuzi bora zaidi katika kutoa Kwangu uaminifu wenu wa pekee na wa mwisho. Ikiwa mtu hana huo uaminifu wa pekee, basi kwa hakika mtu huyo atakwenda kuwa hazina ya Shetani, na Sitaendelea tena kumtumia, bali Nitamrudisha nyumbani akatunzwe na wazazi wake. Kazi yangu imekuwa ya msaada sana kwa ajili yenu; kile Ninachotarajia kupata kutoka kwenu ni moyo wenye uaminifu na wenye motisha, lakini mpaka sasa mikono Yangu bado ni mitupu. Fikiria kuhusu hili: Ikiwa siku moja bado Nitakuwa nimekasirika sana, kupita maelezo, je, mtazamo Wangu kwako utakuwaje kwa wakati huo? Je, bado Nitakuwa mwema kwako kwa wakati huo kama Nilivyo sasa? Je, moyo Wangu bado utakuwa mtulivu kwa wakati huo kama ulivyo sasa? Je, mnaelewa hisia za mtu ambaye amelima kwa kujitahidi lakini hakuvuna hata nafaka moja? Je, mnaelewa ukubwa wa jeraha la mtu ambaye amepigwa kipigo kikubwa? Je, mnaweza kuonja uchungu wa mtu aliyejawa na matumaini ambaye anapaswa kuachana na mtu kwa uhusiano mbaya? Je, mmeona hasira ya mtu ambaye amekasirishwa? Je, mnaweza kujua hisia ya kulipiza kisasi kwa haraka ya mtu ambaye amekuwa akichukuliwa kwa uadui na udanganyifu? Kama mnaelewa fikira za watu hawa, Nadhani haiwezi kuwa vigumu kwenu kufikiria mtazamo ambao Mungu Atakuwa nao wakati ule wa adhabu Yake. Hatimaye, Natarajia nyote mtaweka juhudi kubwa kwa ajili ya hatima zenu wenyewe; hata hivyo, ni bora msitumie njia za udanganyifu katika juhudi zenu, ama sivyo Nitasikitishwa nanyi katika moyo Wangu. Je, kusikitishwa kwa aina hii kutasababisha nini? Je, hamjidanganyi wenyewe? Wale ambao wanafikiria juu ya hatima zao lakini bado wanaziharibu ni watu wenye uwezekano mdogo wa kuokolewa. Hata kama watu kama hao watakerwa na kukasirika, ni nani atakayemhurumia mtu kama huyo? Kwa ujumla, bado Ninatamani muwe na hatima inayofaa na nzuri. Hata zaidi, Ninatumai kwamba hakuna yeyote kati yenu atakayeanguka katika maafa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

674. Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi, tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Katikati ya dhiki, matendo yenu hayatafikiriwa kuwa yanafaa kabisa, kwa kuwa imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa ama waoga au wagumu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa dhiki, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Iliyotangulia: B. Kushawishi kwa Mungu wa Mwanadamu

Inayofuata: XIV. Maneno Juu ya Viwango vya Mungu vya Kuyafafanua Matokeo ya Mwanadamu na juu ya Mwisho wa Mtu wa Kila Aina

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp