Sura ya 10

Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. Huu utakuwa ni wajibu wako, vinginevyo utakabiliana na ghadhabu Yangu na mkono wangu uta…, na utavumilia mateso ya akili yasio na mwisho. Ni lazima uyavumilie yote; kwa ajili Yangu, lazima uwe tayari kuviachilia vitu vyote unavyomiliki na kufanya kila kitu unachoweza kunifuata Mimi, na uwe tayari kutumia kila kitu chako. Sasa ndio wakati ambao Nitakujaribu: Je, utanipa uaminifu wako? Je, unaweza kunifuata Mimi hadi mwisho wa barabara kwa uaminifu? Usiwe na hofu; kwa msaada Wangu, ni nani angeweza daima kuzuia barabara? Kumbuka hiki! Kumbuka! Kila kitu ambacho hutokea ni kwa kusudi Langu njema na yote yako chini ya uangalifu Wangu. Je, kila neno na tendo lako linaweza kufuata neno Langu? Wakati majaribio ya moto yatakuja juu yako, utapiga magoti na kuomba msaada? Au wewe utajikunyata, bila uwezo wa kusonga mbele?

Lazima uwe na ushujaa Wangu ndani yako na lazima uwe na kanuni wakati unakabiliana na ndugu wasioamini. Lakini kwa ajili Yangu, si lazima pia usikubali kushindwa na nguvu zozote za giza. Tegemea hekima Yangu ili kutembea kwa njia kamili; usiruhusu njama za Shetani kuchukua umiliki. Weka juhudi zako zote katika kuuweka moyo wako mbele Zangu, nami Nitakufariji na kukuletea amani na furaha. Usijitahidi kuwa namna fulani mbele ya watu wengine; Je, si kunifanya Mimi niridhike kuna thamani na uzito zaidi? Kwa kuniridhisha, si utajazwa na amani na furaha ya milele hata zaidi? Mateso yako ya sasa yanaonyesha jinsi baraka zako za baadaye zitakavyokuwa; ni zizisoelezeka. Wewe hujui ukubwa wa baraka ambazo utapata; huwezi hata kuziota. Leo zakuwa halisi, halisi kweli! Hii haiko mbali sana, unaweza kuiona? Kila chemba ya mwisho ya hii iko ndani Yangu na ni jinsi gani kuna ung’avu mbele! Futa machozi yako, na usihisi uchungu au huzuni tena. Vitu vyote vimepangwa na mikono Yangu, na lengo Langu ni kuwafanya ninyi muwe washindi na kuwaleta katika utukufu pamoja na Mimi. Kwa yote yanayokutendekea, unapaswa kushukuru sawasawa na uwe uliyejawa na sifa; hilo litanifanya Niridhike sana.

Maisha ya kuzidi uwezo wa binadamu ya Kristo tayari imeonekana; hakuna kitu chochote unachopaswa kuhofia. Mashetani wako chini ya miguu yetu, na wakati wao hautakuwepo kwa muda muda mrefu zaidi. Amka! Tupilia mbali ulimwengu wa uasherati; jinusuru mwenyewe kutoka dimbwi la kifo! Kuwa mwaminifu Kwangu bila kujali chochote, na usonge mbele kwa ujasiri; Mimi ni mwamba wako wa nguvu, kwa hivyo Nitegemee Mimi!

Iliyotangulia: Sura ya 9

Inayofuata: Sura ya 11

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp