Mungu Yuko Kando Yangu

04/07/2023

Na Guozi, Marekani

Nilizaliwa katika familia ya Kikristo, na nilipokuwa na umri wa mwaka mmoja, mama yangu alikubali kazi mpya ya Bwana Yesu aliyerudi—Mungu Mwenyezi—ingawa bibi yangu alikuwa dhidi ya jambo hilo sana. Nakumbuka nilipokuwa mdogo, bibi yangu mara nyingi angeniambia, “Ikiwa hujisikii vizuri au huwezi kufanya kazi ya nyumbani, omba tu kwa Bwana Yesu. Atakupa akili na busara, na Atakulinda.” Mama yangu, hata hivyo, mara nyingi angeniambia, “Mungu aliuumba ulimwengu huu na Akawaumba wanadamu. Yeye daima yuko nasi. Kumbuka kumwomba Mwenyezi Mungu unapokumbana na shida yoyote na Yeye atakulinda na kukuhifadhi.” Sauti hizi mbili tofauti zilisikika masikioni mwangu mara kwa mara. Niliwahi kumuuliza mama yangu nilipokuwa bila uhakika, “Bibi anataka nimwombe Bwana Yesu na wewe unataka nimwombe Mwenyezi Mungu. Napaswa kumsikiliza nani?” Alisema, “Kwa kweli, Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja. Ni kwamba tu nyakati ni tofauti, majina anayotumia Mungu ni tofauti, na kazi Anayoifanya pia inatofautiana. Bwana Yesu alifanya kazi ya Enzi ya Neema, na Mwenyezi Mungu anafanya kazi ya Enzi ya Ufalme. Anabadilisha jinsi Anavyofanya kazi katika kila enzi, na pia Anabadilisha jina Lake. Lakini haijalishi jina Lake na kazi Yake vinavyoweza kubadilika, kiini Chake hakibadiliki. Kwa mfano, leo umevalia nguo nyekundu kwenda shuleni na kesho utavalia ya rangi ya bluu kwenda kwenye mkahawa—hata ingawa umevalia mavazi tofauti, na unafanya vitu tofauti katika maeneo tofauti, wewe bado ni yule yule. Lakini enzi mpya ya Mungu inapofika, lazima twende kwa mwendo sawa na kazi Yake mpya. Hiyo ndiyo maana tunapaswa kumwomba Mwenyezi Mungu sasa.” Hata ingawa nilisikiliza maelezo ya mama yangu, bado nilihisi wasiwasi na bado nilikuwa na mtazamo wa shaka juu ya kazi mpya ya Mwenyezi Mungu.

Mnamo Agosti 2014, nilikuja Marekani kusoma nje ya nchi. Mama yangu pia alikuja baada ya miezi michache na aliwasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu nchini Marekani. Kuanzia wakati huo, nilianza kidogo kidogo kujua uwepo wa Mwenyezi Mungu. Wakati nilipokuwa nimefika tu Marekani kwa ajili ya masomo yangu, niliona vigumu sana kuzoea maisha hapa, hasa kuishi katika nyumba ya mtu mwingine nikiwa peke yangu. Mimi ni mwoga sana, kwa hivyo niliogopa kulala peke yangu. Mama yangu aliniambia, “Lazima tuamini kwamba mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Shetani na pepo pia wako chini ya mamlaka Yake, kwa hivyo wakati unaogopa usiku mwombe Mungu tu. Mradi tu una Mungu moyoni mwako, Shetani hawezi kukukaribia.” Kila nilipomsikiliza mama yangu akinipa ushirika, nilihisi mwenye amani na utulivu zaidi.

Mnamo Desemba 2015 nilianza kuhudhuria mikutano katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, lakini kwa sababu sikuwa na ufahamu mwingi juu ya masuala ya imani, mara nyingi nilijilazimisha kuhudhuria. Ilikuwa tu baadaye baada ya kupitia matukio mawili ndipo nilitambua kwa vitendo uwepo wa kweli wa Mungu, baada ya hapo niliweza kuthibitisha kutoka moyoni mwangu kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli, na kwamba Yeye yuko kando yangu kila wakati…

Ilikuwa Ijumaa alasiri na nilikuwa na somo moja tu la sanaa kabla ya kumaliza na shule siku hiyo na ningeweza kwenda nyumbani. Mwanafunzi mwenzangu aliniambia ghafla, “Acha tukose kuhudhuria darasa letu la mwisho na katikati ya jiji tupate chakula na tutazame bidhaa dirishani. Nilisikia kuna mkahawa mpya wa vyakula vya baharini ambao ni mzuri kabisa.” Kusikia hii, nilishawishiwa—sikuwa nimekula chakula cha mchana na nilikuwa na njaa kweli. Tumbo langu lilikuwa likiuma, kana kwamba lilikuwa likinihimiza niende haraka kwenye mkahawa wa chakula cha baharini. Lakini nilikuwa bado nasita. “Sijawahi kukosa kuhudhuria darasa,” niliwaza. “Na, je, nikishikwa?” Lakini nikawaza: “Xiaoli kutoka katika darasa letu hukosa kuhudhuria hata masomo muhimu na amefanya hivuo mara nyingi bila kupatikana, kwa hivyo sitashikwa pia.” Kwa hivyo nilikubali kwenda na mwanafunzi mwenzangu na kumuuliza mwalimu wangu wa sanaa aruhusu kutokuwepo kwangu, nikisema kwamba ilinibidi niende kwa daktari alasiri hiyo na nilihitaji kuondoka mapema. Kisha mimi na mwanafunzi mwenzangu tulipanda teksi kuelekea kati kati ya jiji kutazama bidhaa dirishani na kula, na sikufika nyumbani hadi saa mbili au saa tatu jioni hiyo. Baada ya kurudi, nilipokea barua pepe kutoka kwa mwalimu anayesimamia wanafunzi wa kimataifa akiniuliza nipeleke hati kutoka kwa ziara yangu kwa daktari nikirudi shuleni. Kuona hivyo, nilishikwa na wasiwasi, na kwa haraka nikajadiliana na wanafunzi wenzangu. Mmoja alisema, “Sio lazima umpe mwalimu hati zozote. Hilo ni jambo la faragha.” Nilihisi kuwa alichosema ni sawa, lakini kwa kuwa nilikuwa nimekosea katika suala hili, nilihisi aibu kujipingania kwa hasira. Kwa hivyo niliuliza mwenye nyumba yangu anisaidie kufikiria njia ya kujiondoa katika jambo hilo. Aliniambia niende kwa mtu anayesimamia na nikubali kosa langu. Baada ya kusikiliza kile alichosema, moyo wangu ulikuwa umefungwa kwa mafundo—sikujua nikubali kosa au niendelee na udanganyifu wangu. Niligaagaa kitandani usiku ule, nikishindwa kulala. Nilitaka kukubali kosa langu, lakini niliogopa kile ambacho mwalimu wangu na wanafunzi wenzangu darasani wangefikiria juu yangu, kwamba taswira nzuri ambayo nilidumisha kwa kawaida ingeharibiwa kufumba na kufumbua. Katikati ya uchungu wangu, nilikuja mbele za Mungu kuomba na kutafuta, kisha nikasoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Lakini watu wadanganyifu hutegemea falsafa yao wenyewe, mambo, na dutu kuishi. Wao si kama wale walio waaminifu; lazima wawe na tahadhari katika kila kitu wanachofanya isiwe wengine wawe na kitu dhidi yao, lazima watumie njia zao, utawala wao wenyewe wa udanganyifu na uhalifu ili kulinda na kuficha nyuso zao za kweli katika kila kitu wanachofanya. Karibuni au baadaye wataonyesha tabia zao za kweli, na wakifanya hivi watajaribu kugeuza mambo. Wanapojaribu kusema kitu ili kugeuza mambo, kuna nyakati ambazo si rahisi sana, na wasipoweza, wanaanza kuwa na wasiwasi. Wanaogopa kuwa wengine wataweza kuona ndani yao; hiyo inapofanyika, wanahisi wamejiaibisha wenyewe, na wanapoaibika lazima wafikirie njia za kusema kitu cha kuokoa hali. … Katika akili zao, daima lazima wafikiri kuhusu jinsi ya kukuzuia kutowaelewa, jinsi ya kukufanya usikize kile wanachosema na kutazama wanachofanya kwa njia inayofikia malengo na motisha zao. Na hivyo wanaipitia tena na tena katika akili yao: Wanapokosa uwezo wa kulala usiku wanafikiri kuihusu; wakati wa mchana, kama hawana uwezo wa kula wanafikiri kuihusu; wakati wa majadiliano na wengine wanaifikiri sana. Daima wanavalia sura ya kujifanya, ili usifikiri wako hivyo, ili usifikiri wano ni wazuri, au kuwa hivyo sivyo walivyomaanisha(“Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Moja baada ya lingine, kila moja ya maneno ya Mungu liliyafunua mawazo yangu ya ndani, kana kwamba nuru ilikuwa imeangaza ghafla upande wa giza wa moyo wangu, ikiufunua kwa mwanga, na kuniacha nikiona aibu sana na bila mahali pa kujificha. “Ni kweli!” Niliwaza. “Nilikosa kuhudhuria darasa na kusema uwongo, na baadaye sio tu kwamba sikuchukua hatua ya kukubali kosa langu, lakini nilipiga bongo zangu kufikiria njia ya kuficha ukweli wangu, kuufunika ukweli. Sikuhisi hatia au majuto kidogo. Hata nilihisi kwamba mwalimu anayesimamia wanafunzi wa kimataifa anapaswa kufanya shughuli zake. Ah! Tabia ya aina hii ni ya uasi dhidi ya Mungu na inamchukiza Mungu! Hakuna hata moja ya mawazo yangu au vitendo vyangu vinavyopatana na mahitaji ya Mungu—hivi sivyo jinsi mwumini katika Mungu anavyotenda! Hapana, lazima nisisuluhishe shida zangu kama wale wasioamini wanavyofanya. Lazima nitubu kwa Mungu na nitende kulingana na mahitaji Yake. Lazima nizungumze kwa uaminifu na niwe mtu mwaminifu.”

Kwa hivyo, siku iliyofuata ya shule nilienda kwa mwalimu na nikakubali kosa langu la kukosa kuhudhuria darasa. Nilishtuka wakati mwalimu anayesimamia hakunikosoa hata kidogo, lakini badala yake alisema mimi ni mwaminifu sana na kwamba ni vizuri kuweza kukubali kosa! Lakini bado ilibidi kuwe na adhabu kwa kukosa kuhudhuria darasa, kwa hivyo mwalimu alinifanya niwe kizuizini kwa kipindi cha darasa moja baada ya darasa kuishatolewa, ili niweze kufikiria juu ya kile nilichokuwa nimefanya. Ingawa nilipokea adhabu ndogo sana kwa kukosa kuhudhuria darasa na kusema uwongo, nilihisi kuwa huyu ni Mungu aliyekuwa akinilinda. Baadaye, nilifanya ushirika na dada yangu wa kanisa juu ya tukio hili kwenye mkutano. Baada ya kusikiliza maelezo yangu, alinisomea kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kama unaamini katika utawala wa Mungu, basi lazima uamini kuwa mambo ambayo hutokea kila siku, yawe mema au mabaya, si matukio ya kubahatisha. Sio kwamba mtu fulani ni mkali kwako au anakulenga kwa makusudi; yote kwa kweli husafidiwa na kupangwa na Mungu. Kwa nini Mungu hupanga mambo haya? Sio ili kuzifichua kasoro zako au kukukashifu; kukukashifu si lengo la mwisho. Lengo la mwisho ni kukukamilisha na kukuokoa. Mungu anafanyaje hilo? Kwanza, Anakufanya ufahamu tabia yako potovu, kufahamu asili na hali yako, kasoro zako, na kile unachokosa. Ni kwa kuelewa mambo haya yaliyomo katika moyo wako tu ndiyo utaweza kufuatilia ukweli na kuacha tabia yako potovu hatua kwa hatua. Huku ni Mungu kukupa fursa(“Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kupitia ushirika juu ya maneno ya Mungu, nilikuja kuelewa kwa nini hakuna kilichotokea hata wanafunzi wenzangu walipokuwa wamekosa kuhudhuria darasa mara nyingi, lakini mimi niligunduliwa na mwalimu mara ya kwanza tu: Kwa kweli ilikuwa ni ukuu wa Mungu. Mungu aliweka mazingira katika njia ya vitendo ili kunifunua, kunirudi, na kunifundisha nidhamu; ilifanywa ili niweze kuelewa asili yangu mwenyewe ya kishetani na kujua tabia yangu potovu ya kusema uwongo na kudanganya, na hivyo kufuatilia ukweli, kuwa mtu mwaminifu, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Huku kulikuwa Mungu kunipenda na kuniokoa! Hapo zamani, kila mtu alinisifu kwa kuwa mtoto mzuri, na kila wakati nilifikiria hivyo pia. Lakini kupitia kufichuliwa kwa ukweli na kuhukumiwa na kufunuliwa na maneno ya Mungu, mwishowe niligundua uovu na udanganyifu wa asili yangu mwenyewe. Niliweza kusema uwongo na kudanganya bila haya, na nilikuwa mtu mwenye kimo kidogo sana; wakati wote na kila mahali, nilikuwa na uwezo wa kuandamana na wasioamini na kuishi ndani ya tabia zangu potovu, na hivyo kulitia aibu jina la Mungu. Mwalimu aliniweka kizuizini—ingawa niliteseka kidogo katika mwili, ilinifanya nikumbuke somo hili, na singesema tena uwongo au kudanganya kamwe katika siku zijazo. Kama singengunduliwa nilipokosa kuhudhuria darasa wakati huo, ningependa kufanya hivyo tena wakati baadaye ningekabiliwa na majaribu na majaribio. Kisha, ningesema uwongo na kusema uwongo, ningezidi kuteleza na kudanganya, na mwishowe ningekuwa nimechukuliwa kabisa na Shetani. Kufikia wakati huo Mungu asingeweza kunitambua tena kwa sababu Yeye anawapenda na kuwaokoa watu waaminifu na Anawachukia na kuwaondoa watu wadanganyifu. Wakati huo hatimaye niliona dhahiri madhara mabaya ambayo uongo huleta, na pia niliona jinsi ilivyo muhimu, na jambo la maana kuwa mtu mwaminifu!

Tulikuwa na mtihani wa hisabati muda mfupi baadaye. Wakati nilikuwa nikipekuapekua jioni ya siku iliyotangulia, niligundua kuwa bado kulikuwa na mada nyingi ambazo sikuwa nimeelewa. Kuzingatia kuwa mtihani ulikuwa siku iliyofuata, nilikuwa na wasiwasi sana. Kwa sababu alama za muhula huo zilikuwa muhimu zaidi kwa sababu ya kuingia katika chuo kikuu, wangeangalia alama zangu kutoka mwaka huo, na ikiwa ningeznguka hisabati, bidii yangu yote ya zamani ingekuwa bure. Kadiri nilivyofikiria zaidi kuhusu hilo, ndivyo nilivyohisi mfadhaiko zaidi. Siku iliyofuata, dakika chache tu kabla ya mtihani, ghafla niligundua kuwa nilikuwa nimesahau kuja na kijitabu nilichokuwa nimeandika fomula zote. Nilichanganyikiwa kabisa. Nilikuwa nimeandika kwa siri maswali mengi ya mfano kwenye daftari hilo, lakini kwa kuwa lilikuwa limepotea, nilikuwa na uhakika wa kuanguka mtihani. Nikiwa na matumaini madogo zaidi, nilitazama kila mahali, nikitumaini kuwa nilikuwa nimeliangusha kwa bahati mbaya sakafuni mahali fulani. Nilipokuwa tu nikiangalia juu na chini, niliona majibu kwenye karatasi ya mitihani ya mwanafunzi aliyeketi karibu nami. Nilifurahi kwa ajili ya bahati hii nzuri, nikihisi kama kwamba nilikuwa nimeona matumaini ghafla. Nilimwangalia mwalimu kwa haraka na kuona kwamba alikuwa amezama kazini mbele ya kompyuta. Kisha nilipitia kwa haraka maswali yote ya mtihani wa hisabati na kisha nikamgusa mwanafunzi aliyekuwa kando yangu, na kumwaishiria tulinganishe majibu yetu. Ingawa nilisema kuwa nilitaka kulinganisha majibu, kwa kweli nilitaka kunakili majibu yake kwenye karatasi yangu ya mitihani. Nikiwa na wasiwasi wakati wote, nilifaulu kwa hila katika mtihani wote wa hisabati kwa njia hii.

Nilidhani mwishowe nilikuwa nimeshughulikia somo ambalo sikuwa bora zaidi katika na nilikuwa napanga kwenda kuwa na wakati mzuri mara likizo ilipoanza. Kwa mshangao wangu, hata hivyo, siku chache baadaye shule hiyo ilifanya mkutano wa wazazi na walezi, na mwenye nyumba alichukua nafasi yangu kuchukua matokeo yangu ya mtihani. Alisema kuwa nilipata alama nzuri katika kila kitu, lakini alama yangu ya hisabati haikuwekwa pamoja na zinginge kwa sababu shule ilishuku kuwa kunaweza kuwa na suala la uadilifu wa elimu. Niliposikia hili, moyo wangu ulishtuka mara moja—nilikuwa na wasiwasi na mwenye kuvurugika, na sikujua la kufanya. Nilijiuliza tena na tena: “Suala la uadilifu wa elimu? Je, wangeweza kugundua kuwa nilinakili majibu ya mwanafunzi mwenzangu? Ikiwa ndivyo hivyo, nifanye nini? Wizi wa maandishi ni shida kubwa sana na unaweza kuathiri nafasi yangu ya kuingia katika chuo kikuu. Lakini hivi sasa, shule inashuku tu, kwa hivyo bado nina tumaini. Itakuwa sawa mradi tu naweza kutoa maelezo ya wazi, lakini ni napaswa kulielezaje? Kwa kweli nilifanya wizi wa maandishi. Labda niende tu na nikubali?” Nilifikiria hili tena na tena akilini mwangu. Wanafunzi wenzangu walipendekeza kwamba kamwe nisikubali hili katika hali yoyote ile, kwamba nitoe tu kisingizio chochote na nijinasue kwa uwongo. Lakini nikawaza: “Hilo silo jambo ambalo muumini katika Mungu anapaswa kufanya. Je, nitafanya nini?” Ilitukia tu kwamba kulikuwa na mkutano wa kanisa jioni hiyo, kwa hivyo niliwaambia dada zangu katika ushirika juu ya hali niliyokuwa ndani. Dada yangu mmoja aliniambia nisome kifungu cha maneno ya Mungu: “Tangu hapo mpaka sasa, watu wamesikiliza mahubiri mengi ya ukweli, na wamepitia kazi nyingi ya Mungu. Ilhali kwenye uingiliaji kati na uzuiaji wa mambo mengi tofauti na hali, watu wengi hawawezi kufikia hali ya kutia ukweli katika matendo, na hawawezi kufikia hali ya kumtosheleza Mungu. Watu wanazidi kuwa goigoi, wanazidi kuikosa imani…. Tamanio tu la Mungu ni kuukabidhi ukweli huu kwa binadamu, na kutia moyoni mwa binadamu njia Yake, na kupangilia hali mbalimbali ili kujaribu binadamu katika njia tofauti. Shabaha yake ni kuweza kuchukua maneno haya, ukweli huu, na kazi Yake, na kusababisha matokeo ambapo binadamu anaweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Watu wengi ambao Nimewaona wanalichukua tu neno la Mungu na kuliona kuwa falsafa, kuliona kuwa barua, kuliona kuwa kanuni za kufuatwa. Wanapoendelea na shughuli zao na kuongea au kukabiliwa na majaribio, hawachukulii njia ya Mungu kama njia ambayo wanafaa kuifuata. Hali hii hasa ni kweli wakati watu wanapokabiliwa na majaribio makuu; Sijamwona yeyote ambaye alikuwa anatia katika matendo kwa mwelekeo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha). Nilihisi aibu moyoni mwangu baada ya kusoma maneno haya. Hata ingawa nilielewa kidogo juu ya ukweli kuhusu kuwa mtu mwaminifu na sio muda mrefu uliopita Mungu alikuwa ameniadibu na kunifundisha nidhamu kuhusu jambo hilo, mara tu nilipokabili jaribio lingine bado sikuweza kutenda ukweli. Nilijua wazi kabisa kuwa wizi wa maandishi haukuwa sawa, lakini kwa sababu ya alama zangu mwenyewe, nilisahau kabisa kuhusu ukweli wa Mungu kututaka tuwe watu waaminifu. Sio tu kwamba sikuweza kushuhudia, lakini nilikuwa nimemwaibisha Mungu. Sikuweza kulala usiku huo, nikilifikiria tena na tena akilini mwangu. Mwishowe niliamua kuwa mtu mwaminifu na kutoliabisha tena jina la Mungu kwa sababu ya kuendeleza masilahi yangu binafsi. Mara tu nilipofikia uamuzi huo, niliruka kutoka kitandani, nikawasha kompyuta, na kuandika maneno ya kujikosoa, nikikiri kosa langu. Asubuhi iliyofuata, nilifika shuleni mapema sana na kumkabidhi mwalimu wangu maandiko hayo ya kujikosoa, nikamwomba msamaha kwa sababu ya tabia yangu, na nikamhakikishia kwamba katika siku zijazo sitawahi kushiriki tena katika udanganyifu. Nilijitayarisha kupata alama ya sifuri katika hisabati na nilikuwa tayari kukubali adhabu yoyote ambayo shule ingenipa. Sikuwahi kufikiria kuwa kweli mwalimu angeamua kuniruhusu niufanye mtihani tena. Katika wakati huo, sikuweza kujizuia ila kutoa shukrani zangu na sifa kwa Mungu kutoka kina cha moyo wangu: Shukrani ziwe kwa Mungu kwa kunionea huruma! Hii ilinionyesha kuwa Mungu huchunguza ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu, na wakati niliweka kando masilahi yangu mwenyewe na kutenda ukweli wa kuwa mtu mwaminifu, Mungu alinifungulia njia na kumfanya mwalimu aniruhusu niufanye mitihani tena. Kwa kweli nilihisi kuwa Mungu alikuwa kando yangu, Akiangalia kila hatua niliyochukua, na kuwapanga watu, hafla, vitu na mazingira yote karibu na mimi ili niweze kujionea mwenyewe uwepo Wake wa kweli. Upendo wa Mungu kwangu ni halisi sana!

Kilichokuja kama mshangao mkubwa zaidi ni kwamba, siku chache baadaye, kulikuwa na kusanyiko la shule nzima ili kuwapa wanafunzi waliopata alama ya A vyeti vya ustahili muhula huo. Mwalimu alipotangaza jina langu, nilidhani kuwa lilikuwa kosa. Ni wakati tu wanafunzi wenzangu waliniambia jambo fulani ndipo niligundua kuwa kweli nilikuwa napokea cheti cha ustahili. Wanafunzi wenzangu walishangaa sana, wakistaajabu kuwa ningewezaje kupata cheti cha ustahili baada ya kufanya wizi wa maandishi katika mtihani wangu wa hisabati. Nilitamka kimya kimya ndani ya moyo wangu: “Haya yote ni matendo ya Mungu! Ninajua cheti hiki sio cha alama zangu, lakini ni Mungu anayenipa tuzo kwa kufanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu.” Hili lilinithibitishia hata zaidi kwamba kweli Mungu yuko karibu nami wakati wote na ananitazama kila wakati. Kila kitu ambacho Mungu hunipangia kila wakati huwa na matokeo bora zaidi.

Sasa ninafurahia mikutano na kusoma maneno ya Mungu zaidi na zaidi. Hata ingawa bado ninafichua tabia zangu potovu maishani, haijalishi ninachokutana nacho, ninaweza kushirikiana na dada zangu kila wakati na kutafuta ukweli kutoka katika maneno ya Mungu kutatua shida zangu. Kupitia kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana kwa njia za vitendo, nimeelewa ukweli zaidi na zaidi, na nimeuweka katika vitendo kwa nguvu kubwa zaidi na zaidi. Ninahisi kuwa Mungu yuko kando yangu, na kwamba Anaweza kunifunua wakati wowote kupitia watu, matukio na vitu mbalimbali, na pia Yeye hutumia maneno Yake kuniongoza na kunielekeza niingie katika ukweli. Sasa nahisi kuwa uhusiano wangu na Mungu unazidi kuwa wa karibu zaidi, na nina hakika kabisa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu wa kweli, na kwamba wakati wote na kila mahali, Yeye ndiye Mungu anayenilinda kando yangu, na Anayenijali na kunilinda!

Iliyotangulia: Kurejea Kutoka Ukingoni
Inayofuata: Bahati na Bahati Mbaya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Toba ya Afisa

Na Zhenxin, Uchina Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu uumbaji wa dunia hadi sasa, yote ambayo Mungu amefanya katika kazi Yake ni upendo, bila...

Bahati na Bahati Mbaya

Na Dujuan, Japani Nilizaliwa katika familia fukara katika kijiji cha mashambani. Tangu niwe mtoto, niliishi maisha magumu na...

Kurejea Kutoka Ukingoni

Na Zhao Guangming, China Mwanzoni mwa miaka ya 1980, nilikuwa katika miaka yangu 30 nami nilikuwa nikifanyia kazi kampuni ya ujenzi....

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp