Wajibu wa Mtu Unaweza Tu Kutekelezwa Vizuri Baada ya Kurekebisha Uzembe

05/11/2020

Na Jingxian, Japan

Kwa kawaida, wakati wa mkutano au wakati wa kufanya ibada yangu ya kiroho, ingawa mara nyingi ningesoma maneno ya Mungu ambayo yanahusiana na kufunua uzembe wa watu, sikutilia maanani sana kuingia kwangu mwenyewe; moyoni mwangu, sikuamini kuwa hili lilikuwa suala kubwa ndani yangu, na hivyo nilitafuta ukweli kwa nadra sana ili kurekebisha tatizo la kutekeleza wajibu wangu kwa uzembe. Hadi, wakati huo, uzembe wangu mwenyewe ulisababisha matatizo makubwa katika kazi yangu. Wakati uzembe huu ulileta madhara kwa kazi ya injili ya kanisa, ililkuwa ni kupitia tu kwa hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu ndipo nilipata ufahamu wa udhihirisho na asili ya uzembe wangu mwenyewe wakati nikitimiza wajibu wangu. Niliona kwamba likiachwa bila kutatuliwa, tatizo langu la uzembe lingeleta chuki na dharau la Mungu, na kwamba siku moja Angenifunua na kuniondoa. Baada ya hapo, nilianza kulenga kufuatilia ukweli ili nitatue tatizo la uzembe, ili niweze kutekeleza wajibu wangu kwa utoshelevu.

Siku moja, nilipokuwa nikiwasikiliza ndugu wa makanisa mengine wakizungumza kuhusu njia zingine nzuri za kutenda katika kueneza injili, niligundua kuwa nilikuwa nimesikia kitu kama hicho mwaka uliokuwa umepita. Wakati huo, nilikuwa pia nimehisi kwamba kutenda hivyo kulikuwa bora zaidi kuliko njia yetu ya sasa—lakini baadaye, nilipojaribu kuwapata watu kadhaa wenye uwajibikaji wa vikundi vya injili kutekeleza vitendo hivi, walisema kwamba kwa sababu nyingi, utendaji kama huo haungewezekana kwetu. Ingawa nilihisi kusikitishwa kuwasikia wakisema hivi, sikusisitiza kuhusu suala hilo; hivyo tu ndivyo mambo yalivyokuwa. Kusikia mazungumzo kama hiyo tena, nilihisi mwenye kuhakikishiwa tena; niliifikira njia hii ya kueneza injili kuwa nzuri sana, na nilikuwa na hamu ya kuwasiliana na watu husika kuhusu jinsi ya kutumia uwezo wa wengine. Na hivyo, wakati wa mkutano, niliwaambia watu husika kuhusu maoni na mapendekezo yangu mwenyewe. Baadaye, niliona kuwa baadhi yao hawakuonekana kuwa na shauku sana, huku wengine wakitoa sababu kwa nini njia hii ya kueneza injili haingewezekana hapa. Niliweza kuona kuwa walikuwa na njia nyingi za kufikiria na maoni yaliyopitwa na wakati ambayo hawakutaka kuyaacha, na kwamba ushirika wangu haukuwa na athari yoyote. Lakini kisha nilifikiria jinsi watu hawa husika walivyokuwa na uzoefu katika kueneza injili: Ingawa niliwajibikia kazi yao, sikuwa na uzoefu mwingi wa kueneza injili. Ikiwa nilikuwa nisiye na uwezo wa kushiriki kuhusu njia ya vitendo, ingekuwa vigumu sana kubadilisha njia yao ya kufikiria kwa maneno machache rahisi. Moyoni mwangu, niliwaza: “Haitakuwa rahisi kuwafanya wakubali njia hizi mpya za kutenda! Kama napasa kueleza msingi wa kuwezekana kwa njia hizi na kuzishiriki vizuri, lazima niwapate ndugu wengine wenye uzoefu zaidi wasaidie na kujaribu kupata suluhisho la jambo hili. Labda itanibidi nijadili kwa undani na watu wengi, na nizungumze mengi, ili niweze kuwa na matokeo yanayostahili. Ah! Hakuna ndugu kama hawa karibu na mimi, na simjui yeyote katika nchi zingine, pia. Kwangu, kutatua tatizo hili kutakuwa vigumu sana. Itachukua muda na bidii, na nitalazimika kulipa gharama kubwa. Ni shida sana. Pia nina kazi nyingine ya kufanya. Siwezi kutoa juhudi zangu zote katika kutatua tatizo hili moja! Nimesema kile ninachopaswa kusema; kiasi ambacho watu wengine wanakubali ni juu yao. Ni afadhali nisahau hili, na sipaswi kulifikira kwa uzito. Nimefanya ya kutosha kufikia hatua hii.” Na kwa njia hii, kwa sababu tatizo hili halikutatuliwa kwa wakati, hakukuwa na mabadiliko katika kazi ya injili.

Kwa siku kadhaa zilizofuata, nilihisi nisiye na uhuru kila nilipofikiria kuhusu hili. Nilipotambua kwamba hali yangu ilikuwa mbaya, nilikuja mbele ya Mungu kuomba na kutafuta. Baadaye, nilisoma maneno ya Mungu: “Wakati unafanya vitu na kutekeleza wajibu wako, je, mara nyingi unatafakari juu ya tabia na nia zako? Ikiwa unafanya hivyo kwa nadra sana, basi una uwezekano wa kufanya makosa sana, ambayo inamaanisha kuwa bado kuna shida na kimo chako. Ikiwa hufanyi hivyo kamwe, basi huna tofauti na wasioamini; hata hivyo, ikiwa kuna nyakati ambazo unatafakari, basi una sura kiasi ya muumini. Lazima utumie wakati zaidi kutafakari. Unapaswa kutafakari juu ya kila kitu: Tafakari juu ya hali yako mwenyewe ili uone ikiwa unaishi mbele za Mungu, ikiwa nia za vitendo vyako ni sawa, ikiwa motisha na chanzo cha vitendo vyako vinaweza kupita ukaguzi wa Mungu, na ikiwa umekubali uchunguzi wa Mungu. Wakati mwingine wazo litakujia, ‘Kuifanya kwa njia hii ni sawa; inatosha kufanya hivi, sivyo?’ Hata hivyo, wazo asili katika fikira hiyo linafichua mtazamo wa aina fulani ambao watu wanao wanaposhughulikia masuala, na vile vile jinsi wanavyoutazama wajibu wao. Mawazo haya ni aina ya hali. Je, hali kama hiyo sio mtazamo ambao mtu amekosa uwajibikaji na anafanya mambo tu bila shauku anapotazama wajibu wake? Mnaweza kuwa bado hamjatafakari hili, na mnaweza kuhisi kwamba ni maonyesho ya asili, kwamba ni dhihirisho la kawaida la ubinadamu tu, na kwamba halimaanishi chochote, lakini ikiwa mara nyingi uko katika hali kama hii, katika mazingira kama haya, basi nyuma yake ni tabia inayokutawala. Hili linastahili uchunguzi, na linastahili kuchukuliwa kwa uzito; usipofanya hivyo, basi hakuna mabadiliko yoyote yatatokea ndani yako(kutoka katika “Jinsi ya Kusuluhisha Shida ya Kuwa Mvivu na Mzembe Wakati wa Kutekeleza Wajibu Wako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). “usipouweka moyo wako katika wajibu wako na uwe holela, ukifanya vitu kwa njia rahisi Zaidi tu, basi hii ni akili ya aina gani? Ni ile ya kufanya mambo tu bila shauku, bila uaminifu kwa wajibu wako, bila hisia ya uwajibikaji, na bila hisia ya misheni. Kila unapofanya wajibu wako, unatumia tu nusu ya nguvu yako; unaufanya shingo upande, hufanyi kwa dhati, na unajaribu tu kuumaliza bila umakinifu wowote. Unaufanya kwa njia ya utulivu sana kana kwamba unachezacheza tu. Je, hili halitasababisha shida? Mwishowe, mtu atasema kwamba wakati unafanya wajibu wako, unapitia tu mchakato. Na Mungu atasema nini kuhusu hili? Atasema kuwa hauaminiki. Yaani, ikiwa umeaminiwa na kazi na, iwe ni kazi ya jukumu la msingi au ya jukumu la kawaida, usipoifanya kwa dhati na ukose kutimiza jukumu lako, na ikiwa huioni kama misheni ambayo Mungu amekupa au jambo ambalo Mungu amekuaminia, na huifanyi kama wajibu na jukumu lako mwenyewe, basi shida itakupata. ‘Huaminiki’—neno hili litafafanua jinsi unavyofanya wajibu wako, na Mungu atasema kwamba tabia yako haijafikia kiwango. Jambo likiaminiwa kwako na uchukue mtazamo huu katika jambo hilo na ulishughulikie kwa njia hii, basi utaaminiwa kufanya wajibu wowote katika siku zijazo? Je, unaweza kuaminiwa na kitu chochote muhimu? Pengine unaweza kuaminiwa, lakini inategemea ni jinsi unavyotenda. Katika moyo wa Mungu, hata hivyo, daima kutakuwa na kutokuamini wewe. Daima kutakuwa na ukosefu wa imani na kutoridhika katika akili ya Mungu, kwa hivyo hii si shida?(kutoka katika “Ni Kupitia Kutafakari Mara kwa Mara Juu ya Ukweli Tu Ndipo Unaweza Kuwa na Suluhisho” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilipokabiliwa na ufunuo wa maneno ya Mungu, nilihisi lawama na tuhuma kubwa moyoni mwangu. Niliona kuwa mtazamo wangu kwa wajibu wangu ulikuwa ule wa kufanya kazi kwa uzembe na kufanya kazi kidogo kuliko uwezo wangu. Nilifikiria nyuma wakati ambapo nilikuwa nimesikia kwanza kuhusu njia nzuri za kueneza injili. Nilikuwa nimekubaliana na kuziidhinisha njia hizi, na nilihisi kwamba tulipaswa kuzikubali na kuzitenda. Hata hivyo, kwa kweli nilipojaribu kushiriki na ndugu kuhusu kuanzisha njia hizi—na nikashindwa—nilikuwa najua kuwa nilipaswa kushiriki ukweli nao ili nibadili mawazo yao ya zamani na maoni. Lakini nilipofikiria kuhusu gharama ambayo ningelazimika kulipa ili nitatue tatizo hili, kuhusu muda na juhudi itatakayogharimu—huu ulikuwa “mradi mkubwa,” na si kitu ambacho kingeweza kusuluhishwa mara moja—nilidhani kwamba ilikuwa ni shida kubwa sana, niliogopa ugumu wa mwili, na hivyo nilikuwa mzembe, nilipitia tu utaratibu, kufanya tu kazi kutimiza wajibu, nikiamini kwamba “nilijaribu,” “niliweka juhudi,” “Hilo linatosha tu,” na “Hakuna mtu anayeweza kuweka bidii katika kila kitu.” Nilitumia haya kujiondoa katika lawama, kulimaliza tatizo hili na jicho moja wazi na jicho moja lililofungwa; wala sikujali kama nilikuwa nimepata mafanikio yanayotarajiwa, nikiamini kwamba ilitosha tu kumaliza. Hivyo ndivyo viwango ambavyo kwavyo nilitenda kwa wakati wote. Ushirika wangu na watu husika haukuwa wa kina kirefu. Sikuwa nimeteseka kweli na kulipa gharama ya kutatua matatizo yao; badala yake, niliamini kwamba tayari nilikuwa nimefanya ya kutosha. Kwa kweli, nilikuwa nimetumia njia za muda mfupi za juujuu tu kuwahadaa watu, ili baadaye, wakati ambapo mtu angeliibua tatizo hili, ningekuwa na jibu kwao; aidha, uwajibikaji wa utendaji duni katika kueneza injili haukuwa wangu mwenyewe—yalikuwa matokeo ya wao kutokubali njia nzuri za kutenda. Nilijaribu hata kumdanganya Mungu: “Ee Mungu, haya ndiyo yote ninayoweza kufanya.” Ni sasa tu ndiyo niligundua kuwa sikujaribu kweli kuelewa mapenzi ya Mungu, sikujitahidi kutenda na kumridhisha Mungu kulingana na yale Anayohitaji, kila wakati nilipokumbana na ugumu. Badala yake, mara nyingi nilikuwa mzembe, na nilijaribu kumdanganya Mungu. Nilikuwa mlaghai na mjanja sana! Nilikuwa najua wazi kuwa shida za ndugu katika kueneza injili hazikuwa zimetatuliwa, na kwamba sikuwa nimetekeleza jukumu langu. Lakini kwa sababu ya kuepuka ugumu wa mwili, sikujali hata nilipoona kuwa kazi ya injili ilikuwa ikizuiliwa. Huku hakukuwa kuifanyia utani kazi ya Mungu? Niliona kwamba sikuwa na hata chembe ya dhamiri au busara, kwamba singeweza kutegemewa hata kidogo! Kwa mara nyingine tena, nilisoma maneno ya Mungu: “… kabla ya Mimi kuwaumba ninyi, Nilijua tayari udhalimu uliokuwepo ndani ya kina cha mioyo ya binadamu, na Niliujua udanganyifu na uhalifu wote katika mioyo ya binadamu. Kwa hiyo, hata ingawa hakuna kabisa dalili zozote wakati ambapo watu hufanya mambo ya udhalimu, bado Najua kwamba udhalimu uliowekwa ndani ya mioyo yenu hushinda utajiri wa vitu vyote Nilivyoumba(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya). Wakati huo, ilikuwa wazi kwangu kwamba hukumu na kuadibu kwa Mungu vilikuwa vimenijia. Mungu alikuwa ameona ndani ya kina cha nafsi yangu, na ingawa hakuna mwanadamu aliyejua kuhusu mawazo yangu mabaya, kwa Mungu, yalikuwa wazi kabisa. Sikuwa nimewajibikia agizo ambalo Mungu alikuwa ameniaminia. Nilikuwa mdanganyifu, jambo ambalo lilikuwa limeizuia kazi ya injili. Katika kila njia, ilionekana kana kwamba nilikuwa nikitekeleza wajibu wangu—lakini kwa kweli, nilikuwa mzembe na kujaribu kumdanganya Mungu. Sikumwogopa Mungu. Mbele ya maneno ya Mungu, nilihisi aibu.

Later, I read the words of God: “Ikiwa, unapofanya vitu, unatia moyo zaidi ndani yake, na pia fadhila, uwajibikaji, na uzingatiaji kiasi, basi utaweza kufanya juhudi zaidi. Unapoweza kufanya hili, matokeo ya wajibu unaotekeleza yataboreka. Matokeo yako yatakuwa bora, na hili litawaridhisha watu wengine na Mungu pia(“Uingiaji Katika Maisha Lazima Uanzie Katika Kutimiza Wajibu Wako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Katika ushirika, inasemekana: “Inamaanisha nini kuwa mzembe? Kwa maneno rahisi, inamaanisha kufanya jambo ili watu wengine waone tu, kwa hivyo wanafikiria ‘Yeye amekifanya.’ Je, mbinu kama hii inaweza kufanikisha matokeo? (Hapana.) Hivyo ndivyo wale wasio na mzigo hufanya mambo; hivi ndivyo wao hutekeleza wajibu wao. Hawajitwiki mzigo wa kazi hii kwa kweli, lakini hawawezi kuepukana na kuifanya. Wasipoifanya watu wataona kwamba kuna shida na kiongozi huyu, na kwa hivyo lazima wafanye kazi kwa uzembe tu kwa sababu ya kuonekana. Mungu alisema, ‘Huku ni kufanya huduma. Hawatekelezi wajibu wao.’ Kwa hivyo, kuna tofauti gani kati ya kufanya huduma na kutekeleza wajibu wa mtu? Watu ambao hufanya wajibu wao kwa kweli wana hali ya uwajibikaji—ambao hutokana na kutaka kutatua tatizo kwa kweli, kutaka kufanya kazi hii vizuri kwa kweli, kutaka kumridhisha Mungu, na kutaka kulipiza upendo wa Mungu. Na hivyo, azimio lao ni nini wanapofanya mambo haya? Kwamba lazima yafanyike, na lazima yafanyike vizuri. Tatizo lazima lisuluhishwe. Hawawezi kupumzika hadi ikamilike, hawatakoma hadi litatuliwe. Ndio ulivyo mzigo ambao wao hufanya nao kazi yao, na kwa hivyo ni rahisi kwao kufanikisha matokeo yanayotarajiwa. Hii ndiyo maana ya kutekeleza wajibu wa mtu. Ni wakati tu ambapo kazi yako na utendaji wa wajibu wako ni mzuri ndipo utakuwa unatekeleza wajibu wako; ikiwa hakuna matokeo, basi wewe ni mzembe, unaboronga tu. Huku ndiko kunakojulikana kama kufanya huduma; utekelezaji wa wajibu usio na matokeo yanayotarajiwa ni kufanya huduma—kuhusu hili hakuna shaka, hakuna kitu kibaya kuhusu hili!” (“Jinsi ya Kuingia Katika Ukweli wa Kuwatambua Viongozi wa Uongo na Wapinga Kristo” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha XI). Kutoka katika maneno ya Mungu na ushirika huu, nilipata njia ya kutenda: Kutekeleza wajibu wa mtu kunahitaji bidii na uaminifu, kunahitaji kuchukulia kila kitu kwa uzito na kwa uwajibikaji; hili tu ndilo litakaloyaridhisha mapenzi ya Mungu. Kujaribu kuepuka kutatua matatizo ya kweli, kuwa mzembe na kufanya mambo ili kutimiza wajibutu ni kumdanganya Mungu na kucheza na Yeye, na hakika hakutakuwa na athari yoyote. Mungu hakutamani anione nikiwa mzembe, na kumpinga, huku nikitekeleza wajibu wangu. Alitumaini kwamba ningeweza kulikabili agizo Lake kwa uaminifu, nirekebishe mtazamo wangu katika kutekeleza wajibu wangu, kukabiliana na magumu yote kwa vitendo, na kutumia wakati mwingi kufikiria kuhusu jinsi ya kutatua matatizo, jinsi ya kufanikisha matokeo yanayotarajiwa; ni kutenda tu kwa njia hii ndiko kunakoupendeza moyo wa Mungu. Wakati huo, niligundua kuwa matatizo na vikundi vya injili hayangewekwa kando tena. Ingawa kushiriki kuhusu na kuigeuza mitizamo ya zamani ya vikundi vya injili haingekuwa rahisi, sikutaka kuizuia tena. Kufuatia, nilitafuta nafasi ya kujadili shida za kueneza injili kwa undani na watu husika Ndugu Zhang na Ndugu Zhao—jinsi ya kuchukua njia za kueneza injili katika sehemu zingine na kujumuisha manufaa yao kwa njia ya kubadilika kwa urahisi. Baada ya ushirika, Ndugu Zhang na Ndugu Zhao walisema kwamba walifurahi kukubali hili na kuchunguza jinsi ya kutenda hili. Baada ya hapo, ndugu walikuwa wepesi zaidi huku wakieneza injili, na ufanisi wao wa matokeo yanayotarajiwa uliboreka pia.

Baada ya kupitia jambo hili, nilikuwa na uwezo wa utambuzi kidogo ikija kwa hali yangu ya binafsi ya uzembe wakati nikitekeleza wajibu wangu. Nilianza kuutelekeza mwili wangu kwa makusudi na kulenga kutenda ukweli na kutekeleza wajibu wangu kwa uaminifu. Lakini bado sikuwa na ufahamu mwingi wa kiini, chanzo, na uzito wa matokeo ya uzembe wangu. Baadaye, Mungu aliweka mazingira ya kuniruhusu niendelee kujifunza, kutatua tatizo la uzembe.

Wakati fulani baadaye, niligundua maswala kadhaa katika vikundi vya injili. Kama mtu anayesimamia kazi hiyo, Ndugu Zhang alikuwa mwenye kiburi sana. Alikuwa mwenye kulazimisha wengine katika maneno na tabia yake, na mwenye kusita kukubali maoni ya ndugu wengine. Pia alikuwa na mvuto wa kudhibiti juu ya Ndugu Zhao, ambaye alifanya kazi naye. Kwa pamoja, wawili hao hawakuweza kujadili na kutafuta kutatua ugumu wa kweli katika kazi ya injili. Ndugu Zhao pia alikuwa mtu asiyependa kubadili mambo, na alitii mafundisho mengi katika kueneza kwake injili. Sababu hizi mbili zilizuia maendeleo katika kazi ya injili. Nilikuwa nimefanya ushirika maalum nao ili kuzungumzia maswala yao, lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote makubwa. Baadaye, niliacha kujaribu kuwafanya washirikiane kwa usawa; ilitosha kuyaacha mambo kama yalivyokuwa. Kuelekea shida ya kutotaka kwa Ndugu Zhang kukubali maoni ya wengine, kuna wakati ambao nilichagua kukubali, na nyakati ambazo nilichunga tu mambo. Lakini sikutafuta ukweli ili nitatue tatizo hili. Miezi kadhaa hapo awali, kufuata madhubuti kwa mafundisho kwa Ndugu Zhao kulikuwa kumeikatiza kazi; nilishiriki na yeye kuhusu hili, naye akalichukua, lakini baadaye nikagundua kuwa katika maeneo fulani, alikuwa bado anashikilia mafundisho na kuwa asiyepindika. Wakati mwingine nilikuwa nikimwonyesha mambo haya, lakini alikuwa mzuri kujiendeleza. Moyoni mwangu, nilifikiria: “Itachukua juhudi nyingi kubadili maoni yake. Nahitaji kutafuta kanuni kadhaa, nizungumze naye kwa kuzingatia kile kinachodhihirika kwa kweli ndani yake. Naweza kulazimika kupata ndugu wengine walio na uzoefu wa kueneza injili wawasiliane na yeye ili kuwe na matokeo.” Nikifikiria kuhusu shida ambayo kutatua tatizo hili kunaweza kuhusisha, niliamua kuacha mambo yafuate mkondo wake. Ingawa niligundua kuwa matatizo ya Ndugu Zhang na Ndugu Zhao yangeathiri kazi ya injili, nilihisi kwamba, kwa wakati huo, hakukuwa na mtu bora zaidi katika makundi ya injili ambaye angechukua agizo hili. Sio kwamba utekelezaji wa majukumu yao haukuwa na matokeo yanayotarajiwa—yalikuwa ya kuridhisha tu. Ilikuwa sawa almradi tu uongozi wa ngazi ya juu haungekuwa na chochote cha kuniambia kulihusu. Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo yangekusumbua kila wakati, na matatizo mengine ambayo hayawezi kusuluhishwa kamwe. Kwa hivyo ilipokuja kwa matatizo ya hawa ndugu wawili, sikutumia muda wowote zaidi kutafuta tu jinsi ya kulikabili hili, wala sikupima kama faida za utekelezaji wao wa wajibu wao ulizidi vikwazo.

Muda mfupi baadaye, kanisa lilifanya uchunguzi wa maoni ya umma. Matokeo yaliniacha nikiwa nimeshtuka sana. Ndugu wengi waliripoti kwamba Ndugu Zhang hakukubali maoni ya watu wengine, kwamba mara nyingi alitenda kiholela, kwamba kila mara uamuzi wake ndio uliokuwa wa mwisho, na mara nyingi aliwakaripia na kushughulika na watu wengine kwa madharau. Ndugu wengine waliogopa kukutana naye. Hawakuwa na chaguo isipokuwa kukubaliana na mipango yake shingo upande, wakihisi kuwa wamezuliwa na kuishi katika uzembe. Ukweli ulionyesha kwamba Ndugu Zhang alikuwa akitembea katika njia ya mpinga Kristo. Ilipokuja kwa Ndugu Zhao, ndugu waliripoti kwamba alikuwa mtu mwenye msimamo usiobadilika, na alifuata mafundisho bila kutikisika. Aliwaongoza ndugu katika kuingia katika kanuni kwa nadra sana. Wakati wa mchakato wa kueneza injili, aliwauliza wale ndugu wengine wafanye kazi nyingi ambayo haikuwa na umuhimu wowote. Yote haya yalionyesha kuwa hakuelewa roho na hakuelewa kanuni. Matendo yao yalisababisha kuzingirwa sana na uingiliaji kati wa kazi ya injili. Pia walileta vizuizi na maumivu mengi kwa ndugu. Kulingana na kanuni, Ndugu Zhang na Ndugu Zhao lazima waondolewe.

Kuwa kwangu mzembe na kutofanya kazi halisi kulikuwa kumeleta madhara kwa kazi ya injili. Pia kulikuwa kumesababisha shida nyingi kwa ndugu. Nilipofikiria hili, nilihisi shutuma kubwa sana moyoni mwangu. Nikihisi kwamba singeweza kuchukua jukumu hili, nilimwomba Mungu: “Ee Mungu! Mimi kuletea madhara kama haya kwa kazi ya kanisa leo ni matokeo ya mimi kutojali wajibu wangu, kuwa mzembe, kujiingiza katika baraka za hadhi yangu, na kutofanya kazi halisi. Mimi ni mdeni Wako, na ninawaonea huruma ndugu zangu. Ee Mungu! Ningekubali hukumu na kuadibu Kwako katika jambo hili, ili nijue mwenyewe kwa undani zaidi, na nitubu Kwako kweli.”

Baadaye, nilisoma katika ushirika kwamba, “Kama wewe ni mtu anayeboronga tu katika wajibu wake na anajifanya kuwa mdanganyifu, hili linaonyesha kuwa wewe ni mtu mdanganyifu na mwovu ambaye ni wa Shetani” (“Udhihirisho Tano wa Mabadiliko Katika Tabia” katika Mikusanyiko ya Mahubiri—Utoaji wa Maisha). “Kila mtu ana shida hiyo hiyo katika kutimiza wajibu wake, na huko ni kutenda kwa uzembe. Ni kana kwamba hakuna mtu anayestahili uangalifu wao—mtu akimfanyia mtu kitu na akichukulia kwa uzito sana, basi mtu huyo lazima awe mtu anayemheshimu sana, mtu anayeweza kumsaidia sana, au mtu anayemwia shukrani kubwa, la sivyo asingelichukulia kwa uzito. Neno ‘faida’ limeandikwa kwa maandiko makubwa katika asili ya wanadamu; watu huchukulia kitu kwa uzito ikiwa tu watapata faida kama malipo, na ikiwa sio jambo la faida kwao watalichukua kwa tabia ya uzembe. Hiyo ndiyo asili ya wanadamu, na pia tabia ya binadamu waliopotoka. Watu wote ni wa kujitakia wenyewe, kwa hivyo watu wote hutenda kwa uzembe na wanafurahi kuwepo tu. Inaweza kuwa bora zaidi kama binadamu wangeona kweli kuwa kutekeleza wajibu wao kama kitu ambacho ni cha Mungu na kinapaswa kuchukuliwa kwa uzito kwa ajili ya Mungu. Kama wanadamu kweli wana mioyo inayomwogopa Mungu, basi watu wasingeweza kutenda kwa uzembe wakati wa kutimiza wajibu wao” (“Ni kwa Kujua Kiini Chake Kipotovu Ndiyo Mtu Anaweza Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu “katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Utoaji wa Maisha). Nikijilinganisha na ushirika huu, na kutafakari juu ya vitendo vyangu mwenyewe, nilihisi aibu kubwa sana. Niliona kuwa asili yangu mwenyewe ilikuwa hasa ya ubinafsi na ujanja, kwamba kila kitu nilichofanya kilikuwa kwa ajili ya kulinda masilahi yangu mwenyewe. Wito wangu ulikuwa sheria ya kuishi wa “Kamwe usirauke mapema isipokuwa kama kuna manufaa husika” Vitu vya faida lazima vifanyike, vile visivyo vya faida, sio lazima. Utendaji wa wajibu wa mtu haukuwa kulipiza upendo wa Mungu, bali ni kufanya makubaliano na Mungu. Siku zote nilikuwa nikijaribu kupata baraka nyingi kwa kulipa gharama ya chini, na kwa hivyo ilikuwa rahisi kuwa mzembe na kujaribu kumdanganya Mungu. Nilifikiria nyuma kuhusu jinsi, katika kuyakabili matatizo ya Ndugu Zhang na Ndugu Zhao, nilikuwa najua wazi kuwa kile kilichoonyeshwa ndani yao kingezuia kazi ya injili—lakini kwa kuona kwamba, kwa kuonekana kote kwa nje, walikuwa wakitekeleza wajibu wao, na nikihisi kwamba hakukuwa na mtu mwingine bora wa kuchukua nafasi zao, sikufanya chochote zaidi ya kushiriki nao mara chache, bila ya kuwa radhi ya kulipa gharama yoyote zaidi ya kutatua hili. Nilipokuwa nikitekeleza wajibu wangu, niliridhika tu na kuwafanya wengine wafikirie kuwa nilifanya kazi nzuri, au wakati uongozi wa ngazi ya juu haungeweza kupata tatizo lolote; sikufikiria kabisa kuhusu kile ambacho Mungu alifikiria, au jinsi Alivyoliona hili. Nilijua vizuri kabisa kuwa sikuwa nimelitatua tatizo hili kabisa, wala sikujaribu kujua chanzo na kiini cha maswala yao ni nini, kwamba ilikuwa imechukua wakati huu wote kuwabadilisha—jambo ambalo lilikuwa kizuizi kikubwa sana kwa kazi ya injili. Mungu alikuwa ameniinua kwa kunipa wajibu muhimu kama huo, Akitumaini kuwa ningeyajali mapenzi Yake—lakini sikufikiria kulipiza mapenzi ya Mungu, na badala yake nikachukua nafasi ya kikaragosi wa Shetani, nikijaribu kumdanganya na kumhadaa Mungu na kuleta uharibifu katika kazi ya Mungu. Nilikosa ubinadamu hata mdogo. Nilikuwa wa kustahili dharau kweli na mwenye kuchukiza, kwa kweli sikuwa nastahili kuishi mbele ya Mungu! Tabia ya Mungu yenye haki haiwezi kukosewa na mwanadamu; ni jinsi gani matendo yangu hayangechukiwa na Mungu?

Baadaye, nilisoma maneno ya Mungu: “Kuhusu makusudi yao ni yapi na ni kiasi kipi cha juhudi wanaweka katika kutekeleza wajibu wao, Mungu huchunguza na anaweza kuona. Ni muhimu kwamba watu waweke mioyo na nguvu zao zote katika kile wanachofanya. Ushirikiano wao ni muhimu pia. Kujitahidi kutokuwa na majuto juu ya wajibu ambao mtu amekamilisha na juu ya vitendo vya zamani vya mtu, na kufika mahali ambapo mtu hana deni la Mungu—hii ndiyo maana ya kutoa moyo na nguvu zote za mtu. Ikiwa, leo, hutoi moyo na nguvu zako zote, basi baadaye, wakati kitu kitaenda vibaya, na kuna athari, si muda wa kujuta utakuwa umeisha? Utakuwa mwenye deni milele, na litakuwa doa kwako! Kuwa na doa ni makosa watu wanapotekeleza wajibu wao. Jitahidi kuutoa moyo na nguvu zako zote kwa kile kinachopaswa na kinachohitajika kufanywa wakati wa kutekeleza wajibu wako. Ikiwa huutekelezi tu kwa uzembe, na ikiwa huna majuto yoyote, basi wajibu unaotenda wakati huu utakumbukwa. Kinachokumbukwa ni matendo mema mbele za Mungu. Na ni vitu gani ambavyo havikumbukwi? (Makosa na matendo mabaya.) Ni makosa. Watu wanaweza kukosa kukubali kuwa ni vitendo viovu vikielezewa namna hiyo sasa, lakini siku ikija ambapo kuna athari mbaya katika jambo hili, wakati lina athari hasi, basi wakati huo utagundua kuwa hili si kosa la tabia tu, bali ni tendo ovu. Na utakapogundua hilo, utajiwazia mwenyewe, ‘Hili halingefanyika kama ningegundua hili mapema! Ikiwa ningelifikiria zaidi, ikiwa ningefanya bidii zaidi, basi hili halingetendeka.’ Hakuna kitu kitakachofuta doa hili la milele kutoka moyoni mwako. Likisababisha deni ya milele, basi utakuwa taabani(“Jinsi ya Kusuluhisha Shida ya Kuwa Mvivu na Mzembe Wakati wa Kutekeleza Wajibu Wako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kutafakari maneno ya Mungu, nilihisi kuguswa sana. Nilifikiria jinsi nilivyoelekezwa na asili yangu mwenyewe ya ujanja na ubinafsi, juu ya jinsi kila wakati nilijaribu kuzuia kulipa gharama kwa ujanja wakati wa kutekeleza wajibu wangu, juu ya jinsi ambavyo sikuwa nimewatambua mara moja na kuwabadilisha wale watu husika ambao hawakustahili kutumiwa, kiasi kwamba kazi ya injili ilizuiliwa, na ndugu waliishi katikati ya giza na vizuizi. Nilikuwa nimekosa mbele za Mungu. Kama hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa wakati hakungesitisha hatua zangu mbaya, ni nani ajuaye ni mabaya gani makuu ambayo ningekuwa nimefanya wakati ujao? Wakati huo, nilipofikiria zaidi juu ya hili, ndivyo nilivyoogopa zaidi. Kuwa mzembe katika utekelezaji wa wajibu wa mtu kulikuwa hatari sana—kunaweza kuvuruga kazi ya kanisa wakati wowote! Ni baada tu ya kuona matokeo mabaya ya kuwa mzembe ndipo niligundua kwamba kama singelenga kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kwa kutenda maneno ya Mungu, kama ningekuwa mlegevu katika utekelezaji wa jukumu langu, basi singeweza kamwe kufikia uaminifu kwa Mungu, sembuse ukombozi kutoka kwa tabia yangu potovu na wokovu wa Mungu. Wakati huo, nilikuwa na azimio na hamu fulani ya kufuatilia ukweli na kufikia uaminifu katika kutekeleza wajibu wangu.

Baada ya hapo, tulitumia kanuni kupata watu wanaofaa kuchukua nafasi za Ndugu Zhang na Ndugu Zhao. Lakini bado shida katika vikundi vya injili zilibaki, na kwa hivyo nilimwomba Mungu: “Ee Mungu! Bado kuna shida nyingi katika vikundi vya injili ambazo hazijatatuliwa. Baadhi ya njia nzuri za matendo hazijatekelezwa kikamilifu. Kwa sababu, hapo awali, nilikuwa goigoi katika kutafuta ukweli, shida zingine zimesalia hadi sasa. Wakati huu lazima nitafute vizuri ili nione jinsi ya kutatua shida hizi. Ee Mungu! Naomba uniongoze.” Baadaye, nilipata ndugu wengine wanaofanya vizuri zaidi katika vikundi vya injili ili tujadili kwa undani njia ya kuhubiri injili. Nilijifunza mengi. Kufuatia, nilijiandaa kufanya mkutano na kila mtu na kushiriki kuhusu shida za kutekeleza wajibu wetu. Jioni hiyo, nilitafakari juu ya vitu nilipokuwa nikisoma hati, nikijaribu kujua jinsi ya kufanya maandalizi vizuri. Nilijumuisha shida katika maeneo kadhaa na niliangalia maneno husika ya Mungu katika kutafuta jibu. Wakati nilikuwa nimefika katikati, nikagundua kuwa bado kulikuwa na maelezo mengi ya kushughulikiwa—na, nilipoona kuwa tayari muda ulikuwa umeisha, yale mawazo ya kujiuzulu na kuwa mzembe yalizuka tena wakati huu bila kuzuiwa: “Shida hizi zinatachukua muda na juhudi nyingi kupata marejeleo yake. Lo, muda umeisha sana—labda sipaswi kwenda kwa undani sana; kwa hali yoyote, tayari nina mwelekeo wa jumla, na ndugu wataweza kuielewa. Hii inatosha.” Lakini nilipofikiria kuacha nipumzike, nilihisi wasiwasi ndani ya moyo wangu. Wakati huo, nilifikiria kuhusu maneno ya Mungu: “Wakati wowote unapotaka kuwa mzembe na kufanya tu mambo bila shauku, kila unapotaka kuwa mvivu, na kila unapojiruhusu uondolewe katika shughuli na kutamani kwenda tu upate raha, unapaswa kulifikiria jambo hili kwa makini: Katika kutenda kwa namna hii, je, mimi nimekosa kuwa anayeaminika? Je, huku ni kutekeleza wajibu wangu kwa dhati? Je, nimekosa kuwa mwaminifu kwa kufanya hivi? Kwa kufanya hivi, je, nashindwa kuridhisha imani ambayo Mungu ameweka kwangu? Hivi ndivyo unavyopaswa kujitafakari. Unapaswa kuwaza, “Sijachukulia jambo hili kwa uzito. Hapo zamani, nilihisi kwamba kulikuwa na shida, lakini sikuichukulia kama nzito; niliipitia tu bila kuwa makini. Sasa shida hii bado haijasuluhishwa. Mimi ni mtu wa aina gani?” Utakuwa umeigundua shida na upate kujijua kidogo. Je, unapaswa kuacha wakati una maarifa kidogo? Je, umemaliza mara unapokiri dhambi zako? Lazima utubu na ubadilike!(“Ni Kupitia Kutafakari Mara kwa Mara Juu ya Ukweli Tu Ndipo Unaweza Kuwa na Suluhisho” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu kulinifanya nigundue kuwa nilikuwa tena mzembe; kwamba, kwa mara nyingine tena, nilikuwa nikifuata mwili na kujaribu kuchukua njia za mkato. Wakati huo huo, nilikuwa wazi moyoni mwangu kwamba kama singegundua maswala muhimu na kutekeleza ushirika uliolengwa, kwa kweli hili lingekuwa na athari kwenye ufanisi wa matokeo yanayotarajiwa. Ili kufikia matokeo bora zaidi, ilinibidi niutelekeze mwili. Kama matokeo, niliifikiria sana na kuorodhesha kila mojawapo ya shida ambazo zilikuwa zinahitaji sana utatuzi. Ingawa hili lilinichukua muda hadi usiku, nilihisi thabiti moyoni mwangu. Siku iliyofuata, tulikusanyika ili kushiriki kuhusu shida zilizokuwepo. Ndugu waliidhinisha kwa nguvu njia na hatua mpya. Kuona kwamba shida ambazo zilitusumbua kwa muda mrefu sasa zilikuwa zimetatuliwa, na kwamba kila mtu alikuwa amewekwa huru, nilihisi faraja kuu moyoni mwangu. Baada ya hapo, tulianza kutenda kulingana na njia na namna mpya. Kazi ya injili ilifanikisha matokeo yaliyotarajiwa pole pole na sikuwa na budi ila kumshukuru Mungu moyoni mwangu.

Baada ya kupitia haya, nilikuwa na hali halisi ya jinsi nilivyokuwa nimepotoshwa na Shetani. Nilikuwa nimepoteza dhamiri na busara yangu; ingawa, kwa nje, niliweza kuacha vitu na kujitumia—na hata niliweza kulipa gharama katika mambo kadhaa—kwa sababu sikuwa nimepata ukweli na uzima, tabia yangu potovu bado ilikuwa na mamlaka ndani yangu. Asili yangu ya hila na ujanja, asili ambayo ilikuwa haioni kila kitu chochote isipokuwa masilahi yangu mwenyewe, ilinielekeza kila wakati. Chochote nilichofanya, kilikuwa kwa ajili ya faida yangu mwenyewe. Wakati wa kutekeleza wajibu wangu, kila mara nilikuwa mjanja na kujaribu kumdanganya Mungu; sikuwa na utambuzi wowote kabisa wa kuwa kiumbe aliyeumbwa anapaswa kulipa upendo wa Mungu na kuyajali mapenzi Yake. Kwa sababu ya ufunuo wa Mungu, niliona jinsi nilivyokuwa mdogo na nisiye wa maana, kwamba sikuwa na sura ya binadamu hata kidogo. Hasa nilipofikiria madhara ambayo nilileta kwenye kazi ya nyumba ya Mungu kwa sababu ya uzembe wangu, nilihisi kuwa sikuwa mwaminifu kabisa, na mwenye kumwumiza sana Mungu. Nilihisi pia chukizo kubwa sana kwangu mwenyewe, na nilikuwa na hamu kubwa ya kuitupilia tabia yangu potovu na kuokolewa na Mungu. Naomba Mungu aniandalie mazingira zaidi ya kunihukumu na kuniadibu, ili niweze kuupendeza moyo Wake wakati natekeleza wajibu wangu haraka iwezekanavyo.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mbona Ujihusishe na Hila Unapomtumikia Mungu

Ee Mungu! Asante kwa kufunua asili yangu ya kiburi na majivuno. Kuanzia siku hii na kuendelea, hakika nitachukulia hili kama onyo na kuweka juhudi zaidi katika kujua asili yangu. Nitafanya kazi hasa kulingana na mipangilio ya kazi. Kwa kweli nitakuwa mtu mwenye mantiki, anayezingatia kanuni, na aliye na moyo wa uchaji Kwako.

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp