Ni Sasa tu Ndipo Ninaelewa Kuingia Kwa Maisha Ni Nini

18/10/2019

Na Yulu, Ureno

Mwanzoni mnamo mwaka wa 2017, nilikuwa nikitimiza wajibu wa uongozi kanisani. Baada ya kujifundisha kwa kipindi fulani cha muda, baadhi ya ndugu walinipa pendekezo: Walisema kuwa nilikuwa na ufahamu mdogo sana kuhusu hali na matatizo yao, na sikuwa nimefanya kazi yoyote halisi. Ili kugeuza mkengeuko huu, nilijiandaa kufanya ufuatiliaji mkamilifu ili niweze kuelewa hali za ndugu wote wa kanisa. Kwa hivyo, nilikwenda na kurudi kutoka kanisani kila siku, nikijishughulisha na kufanya ushirika na ndugu na kutoa msaada na mauawana. Walipopata mabadiliko kidogo katika hali zao na azimio kwa matatizo yao, nilifikia uamuzi kuwa hakika nilikuwa na uwezo wa kufanya kazi halisi kwa kiasi fulani, na nikahisi kuridhika kabisa. Ajabu ni kwamba, siku moja kiongozi wa timu ya kunyunyizia aliniambia, “Wakati wa mkutano wa leo, baada ya kufahamu hali yetu, uongozi wa ngazi ya juu ulisema kwamba hivi karibuni tumekuwa tukijishughulisha tu na kazi na wala sio kuingia kwa maisha.…” Baada ya kusikia haya, nilihisi kushtuka sana, nami nikawaza, “Nilidhani ndugu walikuwa wamewasiliana kuhusu hali zao wakati wa mkutano na wakapata maarifa kiasi kujihusu, kwa hivyo inawezaje kusemwa kwamba hawana kuingia kwa maisha? Ikiwa hakuna hata mmoja wao aliyepata kuingia kwa maisha, na mimi ndiye ninayewajibikia kazi yao, basi si hii inamaanisha kwamba mimi pia sijapata kuingia kwa maisha?” Nilihisi mwenye mawazo yaliyogongana, na sikuweza kukubali viashiria vya wakubwa wangu.

Siku chache baadaye, Dada Li alinijia baada ya mkutano na kuniambia kwa sauti ya huzuni, “Baada ya kusikiliza ushirika wako leo, sikuhisi raha yoyote. Ulipokuwa ukiwasiliana ulisema kwamba viongozi wa ngazi ya juu walikuwa wamesema ndugu wa timu ya kunyunyizia hawakuwa wamepata kuingia kwa maisha—hivyo unajuaje kuhusu jambo hili? Je, umezingatia kuingia kwako kwa maisha hivi karibuni? Unapaswa kutumia muda kiasi kujitathmini.” Maneno ya dada huyo yalikuwa kama beseni la maji ya barafu yaliyomiminwa juu ya mwili wangu wote. Huku nikihisi kushindwa kabisa kuyakubali, nilijiwazia, “Mimi hufanya mikutano na ushirika pamoja na ndugu kila siku, na hata iweje, mimi huweza kutoa msaada na mauawana. Ninapowasilisha maneno ya Mungu, mimi huunganisha na kuzungumza juu ya uzoefu wangu binafsi, pia, kwa hivyo unawezaje kusema sijapata kuingia kwa maisha? Je, unaweza kweli kutambua ikiwa nimepata au la? Unataka mengi sana kutoka kwangu. Kwa maoni yangu, unaposhiriki, huna hata kina cha ufahamu ambacho ninacho; nikifuata matakwa yako, sijui nitashiriki vipi.” Maneno ya yule dada yalilimatia akilini mwangu, na kadiri nilivyozidi kuyafikiria, ndivyo nilivyozidi kuhisi hasira. Sikutaka hata kumwangalia Dada Li tena. Asubuhi iliyofuata, mwenzangu, Dada Wang, aliniambia, “Jana jioni, Dada Zhang pia aliniuliza ikiwa tulikuwa tumezingatia tu kufanya kazi hivi karibuni wala si kupata kuingia kwa maisha au la.” Niliposikia hivi, nilifadhaika sana. Nilijiwazia, “Dada Zhang anawezaje pia kusema hivyo? Mara nyingi mimi hufanya mikutano na yeye, na kila mara mimi huunganisha uzoefu wangu mwenyewe katika ushirika wangu, na amenisikia nikifanya hivyo—hivyo anawezaje kusema sijapata kuingia kwa maisha kokote? Sasa dada wawili wamesema jambo sawa; inawezekana kwamba kweli sijapata kuingia kwa maisha kokote? Ikiwa ni hivyo, ningewezaje kuwanyunyizia ndugu? Je, ni kwamba siwezi kutekeleza wajibu huu?” Kufikia wakati huo nilikuwa kama mpira ulioondolewa hewa; nilihisi kuvunjika moyo kabisa. Katikati ya mateso yangu, nilimwomba Mungu: “Mwenyezi Mungu! Ninahisi uchungu mwingi moyoni mwangu hivi sasa. Sijui jinsi ya kupitia hali hii, wala sijui ni somo gani ninalopaswa kujifunza. Mungu! Ninakusihi Uniongoze; Nifanye nielewe mapenzi Yako.…”

Baada ya sala, nilifikiria kuhusu kifungu katika ushirika, “Mapenzi ya Mungu ni rahisi sana. Ni kutumia kila aina ya mazingira, kila aina ya ndugu, na maswala ya kila aina ili kukujaribu, kukufanya ufadhaike, kukusababisha upitie usafishaji na kisha kukusababisha ujielewe. Mwishowe, utajijua kweli na kuona kuwa wewe si kitu hata kidogo, ukiukubali ukweli kwa furaha, kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, na kutii kazi ya Mungu ili kuingia kwenye njia sahihi katika imani yako. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Mapenzi ya Mungu bila shaka si kutumia mazingira ili kukufanya uanguke na usiweze kuamka, kisha kukusababisha ufe. Si hivyo. Ni kukufanya ujielewe kikamilifu na kisha ujisimamishe haraka na uufuatilie ukweli. Hii ni kwa sababu watu humtegemea Mungu tu na huufuatilia ukweli wanapokata tamaa. … Je, sababu ya kukupunguzia nguvu na kukupogoa ni kukufanya ulale au kukufanya uwe wa kufaa kwa matumizi? Je, kufunua ukosefu wako kuhusu ukweli na uhalisi hufanywa ili kukuhukumu na kukulaani, au kukufanya usimame na kujizatiti kwa ukweli na kuufuatilia ukweli? Ukifikiria jambo hili, si utaelewa mapenzi ya Mungu?” (“Maswali na Majibu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha VII). Baada ya kutafakari mahubiri haya, niligundua kwa ghafla kuwa watu, matukio, na mambo haya mabaya ambayo nilikuwa nimekabiliana nayo moja baada ya lingine hivi karibuni kwa kweli yalikuwa yametokana na upogoaji na ushughulikiaji wa Mungu kwangu; yalikuwa tabia Yake ya haki, iliyoonyeshwa juu yangu, na ndani ya mambo hayo kulikuwa na nia njema za Mungu. Mapenzi Yake hayakuwa ili kunifanya nijiondoe kwa uhasi, wala hayakuwa ili kunifanya niishi katika hali ya kubishana juu ya mema na mabaya; badala yake, yalikuwa ili kunileta mbele Yake katika hali ya kujitathmini ili nijijue, nilenge kuufuatilia ukweli, na kujitahidi kufikia mabadiliko katika tabia yangu. Hata hivyo, baada ya kupogolewa na kushughulikiwa, badala yake nilikuwa nimekataa kujitathmini au kuutafuta ukweli. Moyo wangu ulikuwa umejaa ubishi na uasi, na hata nilikuwa nimefikiria kwamba kusudi langu la kusukumwa katika mazingira kama haya lilikuwa kunifunua kwa kuwa asiyestahili kutimiza wajibu wa aina hii, na kwa hivyo nilikuwa nimeishi katika hali ya uhasi kwa kutoonyesha hisia. Kwa kweli nilikuwa mwenye kutosikia mantiki! Katika siku chache zilizopita, nilifikiria kuhusu jinsi, dada wachache walivyokuwa wameniambia kwamba sikuwa nimepata kuingia kwa maisha kokote, na nikagundua kuwa Mungu alikuwa Akiwatumia kunikumbusha kuwa lazima nitulie na kujitathmini kwa bidii ili nijue matatizo yangu yalikuwa yapi, kwa nini dada hao walikuwa wamesema sikuwa nimepata kuingia katika maisha, na kwanza kabisa maana ya kuingia kwa maisha ni nini haswa.

Baadaye, nilisoma yafuatayo kutoka kwa ushirika “Kuingia Katika Maisha na Njia ya Kuingia Katika Maisha Ni Nini”: “Kuingia katika maisha kunamaanisha kuingia katika ukweli na katika maneno ya Mungu. Kunarejelea kuelewa ukweli wa upotovu wa watu, na kiini cha upotovu wao, na kisha kuweza kuukubali ukweli, kuyakubali maneno ya Mungu, na kuyafanya yawe maisha yao. Kitu chochote cha pekee kinachohusika na aina hii ya uzoefu ndicho kuingia katika maisha.” “Kuingia katika maisha kunamaanisha kuingia katika ukweli. Kuingia katika ukweli kunategemea watu kufuata neno la Mungu na kufikia ufahamu wa ukweli.” “Tunapokuwa na maarifa ya kweli kumhusu Mungu, inathibitisha kwamba tunako kuingia kwa kweli katika maneno Yake. Tunapokuwa na ufahamu wa kweli wa kiini chetu wenyewe kipotovu na ukweli wa upotovu wetu wenyewe, hiyo pia inathibitisha kuwa tunako kuingia kwa kweli katika maneno ya Mungu. Wakati ambapo tu watiifu kwa kazi ya Mungu, uhalisi Wake, na kiini Chake kwa kweli, tunapoyakidhi mahitaji Yake yote kwa kweli, hiyo inathibitisha vile vile kuwa tunako kuingia kwa kweli katika maneno Yake. Almradi kuna kuingia kwa kweli ambako kunategemea maneno Yake, ambako ni kuingia kwa kweli katika ukweli, na matokeo ambayo yanapaswa kupatikana yamepatikana, hii inamaanisha tunao uhalisi wa kuingia katika maisha”. (Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II). Maneno haya yalinipa nuru ya ghafla ya umaizi: Kama ilivyotokea, kuingia katika maisha kulimaanisha watu kuyafuata maneno ya Mungu na kupata ufahamu wa ukweli, na kuingia katika uhalisi wa ukweli. Kwa maneno mengine, kulimaanisha kwamba wakati wakipitia kazi ya Mungu, wangeweza kuweka maneno Yake katika vitendo na kuuelewa ukweli polepole mpaka wakapata maarifa kuhusu tabia ya Mungu na kazi Yake, na vile vile maarifa halisi ya asili yao wenyewe potovu na kiini na ukweli wa upotovu wao. Kulimaanisha kuwa wangeweza kujidharau, kupuuza nia zao wenyewe zisizo sahihi na asili ya kishetani, na kuutekeleza ukweli, kumtii Mungu, na kumridhisha kwa kufuatana na mapenzi na mahitaji Yake. Ni kwa njia hii tu ndipo wangeweza kuhesabiwa kama waliopata kuingia kwa maisha. Huku nikijilinganisha na hali na masharti haya, sikuwa na budi kutafakari juu ya hali yangu ya hivi karibuni: Tangu ndugu zangu watoe pendekezo kwamba sikuwa nimeubeba mzigo wa wajibu wangu na sikuwa nimezingatia kutatua matatizo yao, ili kuwazuia wasiseme mambo kama haya juu yangu, nilikuwa nimejishughulisha na kufuatilia hali za ndugu zangu na hata nikatumia wakati uliotengwa kwa ajili ya ibada za kiroho ili kutafuta vifungu vya maneno ya Mungu ambavyo vingeweza kusuluhisha matatizo yao. Ni mara chache sana ambapo nilikuwa nimetulia na kuyatafakari maneno ya Mungu binafsi, hata hivyo, au kuutafuta ukweli na mapenzi ya Mungu katika matamshi hayo. Katika kutimiza wajibu wangu, sikuwa nimezingatia fikira na mawazo yangu mwenyewe hata kidogo, wala sikuwa nimejitathmini ili kugundua ni tabia zipi potovu ambazo nilikuwa nimefunua na ni ukweli upi ambao nilihitaji kuuingia ndani yake, sembuse ikiwa njia ambayo nilikuwa nikiitembea ilikuwa sahihi au mbaya. Kila mara niliposhiriki katika mikutano pamoja nao, nilikuwa tu nimeyachukua maneno ya Mungu na kuwapasha ndugu zangu ili waweze kwenda kuutenda ukweli, lakini mimi mwenyewe sikuwa nimechukua fursa hizi kujitathmini au kuingia katika maneno ya Mungu pamoja nao. Wakati mwingine, baada ya baadhi ya tabia yangu potovu kufunuliwa, nilikuwa tu nimeipatanisha na maneno ya Mungu au kutafuta vifungu kadhaa vya kutia moyo au kufariji ili nivisome. Hii ilikuwa imeridhisha usumbufu niliouhisi moyoni mwangu, lakini nilikuwa nimejitathmini au kujichunguza kwa nadra sana kulingana na matamshi ya Mungu ili kupata kujua kiini changu kipotovu. kwa hivyo, sikuwa nimejichukia, na kisha sikuwa nimelenga kuufuata ukweli. Nilipokuwa nikikabiliwa na mazingira kama haya, nilikuwa nimeonyesha tena upotovu huo huo. Kwa kuzingatia dalili hizi zote zilizokuwa dhahiri ndani yangu, ningewezaje kusema nilikuwa nimepata kuingia kwa maisha? Kwa ajili ya sifa na hadhi, nilikuwa nimefanya juu chini kujitolea kwa kazi, lakini sikuwa nimetilia maanani kuzitafakari nilipokuwa nikila na kunywa maneno ya Mungu kwa kawaida. Nilikuwa tu nimejiridhisha na maarifa ya mafundisho, lakini sikuwa nimeelewa mapenzi na matakwa Yake kwa kweli na vile vile ni matokeo gani Aliyonuia kufanikisha kwa maneno haya Aliyotamka. Sikuwa nimeuelewa ukweli kwa hakika, sembuse kuwa na ushuhuda wa kutenda maneno ya Mungu. Kwa kweli sikuwa na uzoefu halisi, na sikuwa nimepata kuingia kwa maisha kokote! Baada ya kufikiria zaidi juu ya jinsi nilivyopogolewa na kushughulikiwa hivi karibuni na viongozi wa ngazi ya juu pamoja na ndugu zangu, niliona kwamba nilikuwa nimefunuliwa kuwa mpinzani, mwasi, na mbishi. Kama kweli ningekuwa nimepata kuingia kwa maisha, basi baada ya kupogolewa na kushughulikiwa ningeweza kuutafuta ukweli na kujitathmini, lakini singejipata nikiishi kwa uhasi na ukinzani. Ni sasa tu ndipo niliposhawishika kabisa kuwa kweli sikuwa nimepata kuingia kwa maisha, na kwamba katika ushirika wangu na ndugu zangu, nilikuwa tu nimeongea mazungumzo mengi kuhusu maneno na mafundisho. Kama msemo usemavyo, “Vitendo vya majenerali huathiri vitendo vya askari wao.” Kwa kuwa mimi mwenyewe sikuwa nimepata kuingia kwa maisha, ningewezaje kuwaleta ndugu zangu katika uhalisi wa maneno ya Mungu? Je, si njia hii ambayo nilikuwa nikifanya kazi haikuwa na uwezekano wa kuwanasa na kuwaangamiza ndugu zangu? Utambuzi huu ulinifanya nihisi hofu kwa kiasi fulani. Kwa bahati nzuri, Mungu alikuwa Amewatumia dada hao kunipa ukumbusho wa wakati ufaao wa kujitathmini ili nijijue; vinginevyo, ningeendelea tu kuzingatia kazi za nje na sarafi fupi, lakini singeingia katika maisha mimi mwenyewe, na mwishowe kusingekuwa na mabadiliko hata kidogo kabisa katika tabia yangu ya maisha—na ningefunuliwa na kuondolewa tu na Mungu. Ninamshukuru Mungu kwa mwongozo Wake! Mpangilio wa Mungu kwa ajili ya watu, matukio, na vitu kama hivyo vilikuwa vya ajabu sana, na vitu hivyo ndivyo nilivyohitaji hasa. Ni kwa njia ya kupogolewa na kushughulikiwa kwa namna hiyo tu ndipo nilipokuja kuelewa kuingia halisi kwa maisha ni nini, na kupata maarifa kiasi kuhusu hali yangu mwenyewe ya kweli. Niliona kwamba katika kutofuata ukweli wala kuzingatia kupata kuingia kwa maisha, ningeendelea katika imani yangu, hadi mwishowe niishie kutofaulu.

Baada ya hayo, nililenga kwa makusudi kuingia kwangu mwenyewe. Kila siku wakati wa ibada zangu za kiroho, nilijizoeza kwa bidii kujaribu kutafakari maneno ya Mungu na kuzingatia kuutafuta ukweli ndani ya maneno hayo, na pia kuyatekeleza katika maisha halisi. Kati ya watu, matukio, na mambo niliyokabiliwa nayo, nililenga kufahamu fikira na mawazo yangu mwenyewe, nikitafakari juu ya nia zangu na uchafu wangu katika kutimiza wajibu wangu, nikichangua asili yangu na kiini changu, na kutafuta njia ya kutenda na kuingia katika maisha kutoka kwa maneno ya Mungu. Nilipokuwa nikitatua shida za ndugu zangu, sikufanya tena ushirika tu ili kutatua hali zao; nililenga kujitathmini na kujijua ili nijue ikiwa nina maswala yale yale au la, ili nipate kuingia pamoja na ndugu zangu. Baada ya kufanya hivi kwa muda, nilihisi uhusiano wangu na Mungu ulikuwa wa karibu zaidi, na nilipata uzoefu mdogo na ufahamu kuhusu maneno Yake. Pia nilipata matokeo kiasi katika kazi yangu kwa kanisa. Baadaye, niliona kutoka kwa ushirika wa ndugu zangu kwamba walipokabiliwa na shida, wote walikuwa wameanza kutafakari juu ya dhamira na uchafu wao wenyewe, na walikuwa wakichambua asili na viini vyao. Wao, pia, waliweza kuingia katika maneno kadhaa ya Mungu. Mshukuru Mungu!

Baada ya kupogolewa na kushughulikiwa kwa namna hii, nilikuwa nimepata maarifa kuhusu kuingia katika maisha kweli ni nini, na nilikuwa nimekuja kuona waziwazi zaidi kasoro zangu mwenyewe. Katika kutimiza wajibu wangu, nilianza kuzingatia kuingia kwangu mwenyewe na nikaonja ladha ya jinsi ilivyokuwa tamu kufuatilia ukweli na kuweka kwenye vitendo. Haya yote yalikuwa matokeo ya kazi ya Mungu kwangu. Mshukuru Mungu! Katika kila kitu nitakachopitia kuanzia sasa, natumai kuwa thabiti na mwenye uhalisi katika ufuatiliaji wangu wa ukweli, na kujitahidi kufikia mabadiliko katika tabia yangu siku moja hivi karibuni.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Roho Yangu Yakombolewa

Na Mibu, Uhispania “Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi...

Utajiri wa Maisha

Wang Jun Mkoa wa Shandong Kwa miaka mingi tangu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, mke wangu na mimi tumepitia hili...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp