Kuishi kwa Kudhihirisha Mfano wa Binadamu Mwishowe

24/01/2021

Na Zhou Hong, Uchina

Nilipokuwa kiongozi wa kanisa mnamo 2018, niligundua kwamba kulikuwa na dada aliyeitwa Yang ambaye alikuwa na ubora mzuri wa tabia na alifuatilia ukweli. Niliwaza, “Nikiweza kumfundisha vizuri, maisha yangu yatakuwa rahisi, kazi yetu itakuwa bora zaidi na kiongozi wangu pia atanisifu.” Kwa hivyo nilianza kumfundisha kwa bidii. Nilifanya ushirika naye kila alipopata tatizo lolote na nikamteua awe kiongozi wa timu. Alifanya maendeleo ya haraka na alikuwa msikivu katika wajibu wake. Punde, kazi ya timu yetu iliboreka. Niliwaza, “Kama ningekuwa na watu wengi zaidi ambao ni kama Dada Yang, basi kazi yetu yote ya kanisa ingeboreka sana. Ningeweza kupumzika kidogo na tungepata matokeo mazuri zaidi na kila mtu angesema kwamba ninafanya kazi nzuri.” Siku moja, tulimhitaji mtu kwa haraka atunge hati iliyohusu kuwaondoa na kuwafukuza wapinga Kristo na waovu. Sote tulikubaliana kwamba Dada Yang alipaswa kufanya kazi hii. Ajabu ni kwamba, alielewa kanuni hizo upesi na akatunga hati ambazo zilikuwa sahihi na bila upendeleo. Kiongozi wangu aliuliza mara nyingi iwapo tulikuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa hodari katika kutunga hati na nilijua kwamba Dada Yang alistahili kufanya kazi hiyo. Lakini nilipofikiria juu yake kuhamishwa na jinsi ambavyo hilo lingeathari kazi yetu, sikutaka kumwacha aende na sikumpendekeza kwa kiongozi.

Siku moja katika mkutano, kiongozi alisema kwamba walihitaji mtu atakayetunga hati juu ya kuwaondoa na kuwafukuza wapinga Kristo na waovu na akatuuliza iwapo tungeweza kumpa mtu yeyote. Niliwaza, “Dada Yang atafaa kazi hii, lakini nikimwacha aende, nitalazimika kumfundisha mtu mwingine. Nitahitaji kutia juhudi nyingi sana. Je, kiongozi wangu atanionaje iwapo kazi yetu itaanza kuwa duni? Dada Tang pia ni hodari katika kutunga hati, lakini yeye si mwenye bidii sana katika wajibu wake na yeye huhitaji msaada mwingi mara kwa mara. Nitampendekeza badala yake. Kwa njia hii, nitatoa mtu wa kufanya kazi hiyo na Dada Yang ataweza kusalia. Kazi yetu haitaathirika.” Kwa hivyo nilipendekeza Dada Tang na nikazungumza juu ya uwezo wake na kumfanya Dada Yang asionekane mzuri kwa makusudi. Siku chache baadaye, Dada Tang alichaguliwa kwa ajili ya kazi hiyo. Baadaye, niligundua kwamba Dada Tang hakuweza kuifanya peke yake. Niliwaza, “Dada Yang ataweza kuishughulikia, hamna tatizo. Lakini sitaki aende. Yeye ni hodari sana katika wajibu wake, nini kitatendekea kazi yetu akiondoka?” Kwa hivyo nilichagua tena kutompendekeza Dada Yang. Siku chache baada ya hayo, kiongozi wangu aliulizia Dada Yang hasa na akatuambia tutafute mtu atakayebadilishwa naye haraka iwezekanavyo. Kwa kweli nilipinga wazo hili. Niliwaza, “Dada Yang akiondoka, ni nani atakayetunga hati za kanisa letu? Hata kama tunaweza kupata mtu anayefaa, hatakuwa na ujuzi na hatajua kanuni. Atahitaji mafunzo. Mbali na kazi yetu kuathirika, pia itakuwa kazi ngumu na itahitaji juhudi nyingi kwa upande wangu.” Nilijua kwamba nilikuwa nimekosea kwa kufikiria hayo, lakini niliendelea kujipa visingizio: “Mimi mwenyewe nilimfundisha Dada Yang. Akiondoka, hatutakuwa na mtu katika timu yetu atakayeweza kufanya kazi yake. Itafanyikaje? La, lazima nijadili jambo hili na wafayakazi wenzangu na nimwandikie barua kiongozi nikimsihi amruhusu Dada Yang akae miezi michache zaidi hadi tutakapomfundisha mtu mwingine.” Niliposhiriki haya na wabia wangu wawili, walinikemea wakisema, “Sisi huwafundisha watu kufanya kazi ya nyumba ya Mungu. Mara Dada Yang atakapoondoka, tutaweza kumfundisha mtu mwingine. Je, wewe si mbinafsi kwa kujaribu kumzuia Dada Yang ili asiondoke?” Lakini sikutafakari juu yangu mwenyewe na badala yake nikawaza “Wewe ni mkarimu sana. Unafikiri kwamba ni rahisi kuwafundisha watu?” Nilizidi kufadhaika na kupinga na niliwachukia wabia wangu kwa kutoweza kuzingatia maoni yangu. Muda mfupi baadaye, nilianza kuhisi kana kwamba nilikuwa nikiungua, kana kwamba nilikuwa nikiwaka moto na nilihisi dhaifu kila mahali. Niliwaza, “Hali ya hewa ni nzuri, na sina mafua. Hii si kawaida.” Niligundua kwamba ni Mungu aliyekuwa Akiniadibu na kunifundisha nidhamu. Nilikumbuka maneno ya Mungu: “Sasa, Nafanyapo kazi miongoni mwenu, mnakuwa wenye tabia ya aina hii—ijapo siku ile ambapo hakutakuwa na mtu wa kuwalinda, hamtakuwa kama wezi waliojitangaza kuwa wafalme?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)). Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili Nilishangaa nilipogundua kwamba maneno ya Mungu yalikuwa yakifunua kabisa hali yangu mwenyewe. Nilikuwa nikimtendea Dada Yang kana kwamba alikuwa mali yangu. Nilidhani kwamba kwa kuwa nilikuwa nimemfundisha, alipaswa kuwa wangu na alipaswa kukaa katika kanisa langu na kuniletea sifa nzuri. Sikumruhusu mtu yeyote amchukue Kwa kweli, kina ndugu wote hufanya wajibu wao katika nyumba ya Mungu na maagizo yao yote hutoka kwa Mungu. Wao hufanya wajibu wao wakati wowote na mahali popote ambapo nyumba ya Mungu inahitaji wafanye na kama Mungu apangavyo. Lakini bado nilikuwa mdanganyifu na niliwahadaa wengine kwa sababu ya sifa na hadhi yangu mwenyewe, nikifanya kile nilichoweza ili kusalia na Dada Yang. Je, sikuwa mmoja wa “wanyang’anyi ambao wamejitangaza kuwa wafalme”? Nilikuwa nimejaribu kumdhibiti Dada Yang na kumpokonya kutoka kwa Mungu. Hivi ndivyo wapinga Kristo walivyofanya na ilikuwa njia ya maangamizi. Nilijuta sana nilipotambua haya. Nilikuwa mwenye kiburi na mbinafsi sana.

Kisha nikasoma maneno haya ya Mungu: “Ni kiwango kipi ambacho kulingana nacho matendo ya mtu yanaonwa kuwa mema au mabaya? Inategemea na iwapo katika fikira, maonyesho, na matendo yako, una ushuhuda wa kutia ukweli katika vitendo na wa kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli au la. Ikiwa huna uhalisi huu au huishi kwa kudhihirisha hili, basi bila shaka wewe ni mtenda maovu.” “Iwapo mtu anamwamini Mungu lakini hasikizi maneno Yake, hakubali ukweli au kutii utaratibu na mipango Yake; iwapo yeye huonyesha tu tabia fulani nzuri bali hawezi kuukana mwili na haachi kiburi au masilahi yake; iwapo bado anaishi kulingana na tabia zake za kishetani hata ingawa anaonekana kutimiza wajibu wake, na hajaacha falsafa na namna za kuishi za Shetani hata kidogo, na habadiliki—basi anawezaje kumwamini Mungu? Hiyo ni imani katika dini. Watu kama hao huacha vitu na kujitolea kijuujuu, lakini njia wanayoitembea na chanzo na msukumo wa kila kitu wanachofanya havitegemei maneno ya Mungu au ukweli; badala yake, wanaendelea kutenda kulingana na mawazo yao, tamaa zao na dhana zao za dhahania, na falsafa na tabia za Shetani zinaendelea kuwa msingi wa uwepo wao na matendo yao. Kuhusiana na mambo ambayo hawauelewi ukweli wake, hawautafuti; kuhusiana na mambo ambayo wanauelewa ukweli wake, hawautekelezi, hawamtukuzi Mungu kama mkuu au kuthamini ukweli. Ingawa kwa jina wao ni wafuasi wa Mungu, ni kwa neno tu; kiini cha matendo yao ni onyesho tu la tabia zao potovu. Hakuna ishara kwamba nia na dhamira yao ni kutenda ukweli na kutenda kulingana na maneno ya Mungu. Watu ambao huzingatia masilahi yao kuliko vyote, ambao hutimiza tamaa na nia zao kwanza—je, hawa ni watu wanaomfuata Mungu? (La.) Na, je, watu wasiomfuata Mungu wanaweza kusababisha mabadiliko katika tabia zao? (La.) Na iwapo hawawezi kubadilisha tabia zao, je, wao si wa kusikitisha?(Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilifikiri juu ya maneno ya Mungu na kutafakari tabia yangu. Nilionekana kana kwamba nilijitolea kwa Mungu, lakini nia yangu katika wajibu wangu ilikuwa kutosheleza maslahi yangu mwenyewe. Kiongozi wangu alipoulizia mtu ambaye angeweza kutunga hati, nilijua kwamba Dada Yang ndiye aliyekuwa bora zaidi kwa kazi hiyo. Lakini nilisema uwongo na kudanganya ili kulinda maslahi yangu mwenyewe na badala yake, nikampendekeza Dada Tang. Hata nilipomwona Dada Tang akitatizwa na kazi hiyo na nilipojua kwamba atachelewesha kazi hiyo, bado sikumpendekeza Dada Yang. Sikuwaza juu ya nyumba ya Mungu au kuzingatia mapenzi ya Mungu. Niliwatumia tu kina ndugu kama vyombo vya kulinda sifa na hadhi yangu mwenyewe. Nilikuwa mwovu, mbinafsi na mbaya sana. Nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini mawazo na maoni yangu yote yalitegemea tabia zangu za kishetani na mbinu za Shetani za kuendelea kuishi. Sikufuata maneno ya Mungu au kutenda ukweli. Sikuwa muumini, kama tu maneno ya Mungu yanavyoeleza. Sikupaswa kuwa mbinafsi tena. Ilibidi nimtoe mtu aliyekuwa na kipaji na kisha kuwafundisha watu zaidi kwa ajili ya kanisa letu. Tulimpangia mtu fulani afanye kazi ya Dada Yang katika timu yetu na akahamishwa. Baadaye, Niligundua kwamba Dada Yang alikuwa ametunga upesi hati iliyohusu kuwaondoa na kufukuza watu. Nilihisi vibaya niliposikia haya. Laiti ningempendekeza mapema na kuacha masilahi yangu, kazi hii isingecheleweshwa kwa muda mrefu sana. Hii ilikuwa imetokea kwa sababu ya ubinafsi wangu. Nilikuwa nimetenda dhambi na kutenda maovu. Nilichukulia jambo hili kama onyo la kuyapa maslahi yangu kipaumbele zaidi ya nyumba ya Mungu tena.

Nilidhani kwamba tukio hili lilikuwa limenibadilisha kidogo, lakini tatizo lili hili la zamani lilikuwa likingojea tu hali nzuri ili litokee tena. Muda mfupi baadaye, kiongozi wangu aliniuliza juu ya Dada Liu. Alimtaka aende kusaidia kuwanyunyizia waumini wapya katika kanisa lililokuwa karibu. Nilisita kidogo, lakini nikadhani kwamba sikupaswa kuwa mbinafsi, kwamba sikuwa na budi kutetea kazi ya Kanisa na ningeweza kumfundisha mtu mwingine wakati wowote. Nilikubali kumruhusu Dada Liu aende. Lakini baadaye akasema kwamba Dada Li ambaye alikuwa na wajibu wa kutunga hati alikuwa apandishwe cheo na akanitaka niandike tathmini. Jambo hili lilikuwa gumu sana kwangu. Iwapo Dada Li angeondoka, ni nani angewsimamia utunzi wa hati? Sikutaka kumwacha Dada Li aende kwa hivyo niliahirisha kuandika tathmini yake. Nilitaka kumchelewesha asiende kwa siku chache ili kiongozi wangu amtafute mtu mwingine kwa wakati huo na amruhusu Dada Li akae. Mbia wangu aligundua kwamba sikuwa nikiandika tathmini na akanishinikiza niandike. Nilimdanganya tu na nikasema kwamba nitaiandika mara moja lakini bado sikuiandika. Karibu siku 10 baadaye, mbia wangu alisema, “Kiongozi wetu amemhamisha Dada Li bila tathmini.” Ilinichukua muda kukubali habari hii. Jambo hili lilikuwa likitokea haraka sana! Washiriki wangu wote wazuri wa timu walikuwa wamechukuliwa. Kazi yoyote haingeweza kufanyika kanisani sasa. Mawazo haya yalijaa akilini mwangu. Nilihisi kama kwamba uzito fulani ulikuwa umetua moyoni mwangu. Sikuwa na hamu ya kula katika siku chache zilizofuata. Nilifikiria tu jinsi ambavyo sikuwa na budi kuwatafuta watu na jinsi nilivyokuwa chini ya shinikizo kuu. Mambo hayo yote yangehitaji jududi nyingi sana. Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo, ndivyo nilivyozidi kuwa na wasiwasi, na nilichoka.

Siku moja nilikuwa nikishuka kwenye ngazi kisha nikateleza. Nilihisi mguu wangu ukikatika, kama mfupa unaovunjika. Niliwaza, “Sasa nimefika kikomo. Siwezi kufanya wajibu wangu mguu wangu ukiwa umevunjika.” Nilijua kwamba ni Mungu aliyekuwa Akinifundisha nidhamu. Nilikumbuka jinsi nilivyowaona watu wakihamishwa mmoja mmoja na jinsi nilivyobishana na Mungu moyoni mwangu na kupinga hayo yote. Mtazamo wangu kwa wajibu wangu hakika ulimchukiza Mungu, kwa hivyo Mungu alikuwa Ameondoa wajibu wangu. Niliogopa sana nilipofikiria haya. Mguu wangu uliumia vibaya sana pia. Niliendelea kumwomba Mungu, nikiwa tayari kutubu kwa kweli. Ajabu ni kwamba, baada ya chakula cha mchana siku hiyo mguu wangu uliacha kuuma ghafla, kana kwamba sikuwa nimeujeruhi hata kidogo. Nilijua moyoni mwangu kwamba hili lilikuwa onyo kutoka kwa Mungu ili nijitafakari na kujijua. Nilijiuliza, “Kwa nini mimi daima huyapa masilahi yangu kipaumbele?”

Baadaye, nilitazama video ya usomaji wa maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Mpaka watu wawe wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli, ni asili ya Shetani inayotwaa madaraka na kuwatawala kwa ndani. Ni nini, hasa, kilicho ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini wewe hulinda nafasi yako mwenyewe? Kwa nini una hisia kali sana namna hiyo? Kwa nini unafurahia hivyo vitu visivyo vya haki? Kwa nini unapenda maovu hayo? Msingi wa kupenda kwako vitu hivi ni upi? Mambo haya hutoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali? Kufikia sasa, nyote mmekuja kuelewa kwamba sababu kuu ya mambo haya yote ni kwamba sumu ya Shetani iko ndani yenu. Kuhusu sumu ya Shetani ni nini, inaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini walitenda jinsi walivyotenda, watajibu, ‘Kwa sababu kila mwamba ngoma huvutia upande wake.’ Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida. Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu. Wanaweza kutenda mambo kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, lakini wanajifanyia tu. Kila mtu hudhani kwamba kwa kuwa ni kila mwamba ngoma huvutia upande wake, watu wanafaa kuishi kwa sababu yake mwenyewe tu, na kufanya kila awezalo kupata wadhifa mzuri kwa ajili ya chakula na mavayi mazuri. ‘Kila mwamba ngoma huvutia upande wake’—haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya binadamu. Maneno haya ya Shetani ni sumu ya Shetani hasa, na watu wanapopoiweka moyoni, inakuwa asili yao. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia maneno haya; yanamwakilisha yeye kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya watu pamoja na msingi wa kuwepo kwao; na wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na sumu hii kwa maelfu ya miaka(“Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).

Maneno ya Mungu yanasema kwamba baada ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, kila aina ya sumu za kishetani zilitiwa mioyoni mwetu na zikawa asili yetu. Kama vile “Kila mwamba ngoma huvuta upande wake.” Kila mtu anaishi kulingana na sumu hii ya kishetani, kila kitu tunachofanya ni kwa faida yetu na sisi hufikiri kwamba hii ni sawa na inafaa, kwa hivyo tunazidi kuwa wabinafsi na wadanganyifu. Nilitafakari juu yangu mwenyewe. Kiongozi alipohamisha watu kutoka katika kanisa langu, nilipinga na kujaribu kuzuia hayo, hata kufika hatua ya kuwa mdanganyifu. Niliwachukulia watu kama kwamba walikuwa wangu na nilikataa nyumba ya Mungu iwachukue. Nilikuwa mbinafsi, mwenye kustahili dharau na asiye na mantiki kabisa. Nilikuwa nikizuia kazi ya nyumba ya Mungu! Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi, Mafarisayo walijaribu kulinda hadhi na riziki zao wenyewe kwa kuwazuia watu ili wasimfuate. Waliwachukulia waumini kama wao na walishindana na Bwana juu yao. Mwishowe walimkosea Mungu na Aliwaadhibu. Je, nilikuwa nikitenda tofauti na Mafarisayo kwa jinsi gani? Kina ndugu ni kondoo wa Mungu na nyumba ya Mungu ina haki ya kuwapangia kadiri itakavyo. Sikuwa na haki ya kuingilia kati. Kama kiongozi wa kanisa, ninapaswa kufanya wajibu wangu kama nyumba ya Mungu inavyohitaji na kulingana na kanuni, kushiriki juu ya ukweli ili kutatua matatizo na kuwafundisha watu. Huu ulikuwa wajibu wangu na jukumu langu. Lakini sikuwa nimefikiria mapenzi ya Mungu au kuwapangia watu kulingana na kanuni. Sikuwa tayari kutia juhudi katika kuwafundisha watu wengi zaidi. Sikuwa nimewatoa wale niliojua kwamba walikuwa na vipaji bali nilikuwa nimejaribu kuwadhibiti, nikiwashurutisha wafanye kazi na wahudumu kwa ajili ya hadhi yangu mwenyewe. Je, sikuwa nikifanya mambo yangu mwenyewe kinyume cha nyumba ya Mungu? Nilikuwa nikimkaidi Mungu na kutembea katika njia ya wapinga Kristo. Niliogopa nilipofikiria hayo na nikamshukuru Mungu kwa kunifundisha nidhamu Alipofanya hivyo na kunizuia kufanya maovu zaidi.

Baadaye, nilitazama video nyingine ya usomaji wa maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Hisia za wanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo hazipo kwa ajili ya mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo mwanadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa hapohapo. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na ni mwenye heshima kila wakati, ilhali mwanadamu siku zote ni wa chini, siku zote asiye na thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa wanadamu; mwanadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na kujitahidi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia kwa dhati kuendelea kuishi kwa wanadamu, ilhali mwanadamu kamwe hachangii kitu kwa ajili ya mwangaza au haki. Hata kama mwanadamu anajitahidi sana kwa muda, ni dhaifu sana kiasi cha kutoweza kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake mwenyewe na wala si kwa ajili ya wengine. Mwanadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mwenye ubinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo vya haki, vyema, na vya uzuri, huku naye mwanadamu ni yule anayerithi na kudhihirisha vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na uzuri, ilhali mwanadamu anaweza kabisa, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu). Maneno ya Mungu yalinionyesha kuwa Mungu hana ubinafsi. Kila Anachofanya hufanywa ili kutuokoa na yote hutunufaisha. Nyumba ya Mungu huwapandisha watu vyeo na kuwafundisha ili wale ambao hutafuta ukweli na ambao wana ubora mzuri wa tabia waweze kupata kutenda zaidi na mwishowe watekeleze maagizo ya Mungu. Jambo hili huwanufaisha kina ndugu na kazi ya nyumba ya Mungu. Kuhusiana nami, nilikuwa nimepokea unyunyizaji, riziki ya maneno ya Mungu na mafunzo ya bure kutoka kwa nyumba ya Mungu, lakini sikufikiria kutenda wajibu wangu ili kulipa upendo wa Mungu. Niliwazia tu jinsi ya kuwadhibiti watu. Kwa ajili ya sifa na hadhi yangu mwenyewe, sikusita kuzuia nyumba ya Mungu kuwafundisha watu, jambo ambalo lilichelewesha kazi yake. Nilikuwa mbinafsi, mwovu sana na sikustahili kuishi mbele za Mungu. Nilijua kwamba sikustahili kuendelea kuishi kwa njia hiyo. Sikuwa na budi kuipa nyumba ya Mungu watu wenye vipaji ili kina ndugu wengi zaidi waweze kufanya wajibu waliotakiwa kufanya mahali panapofaa. Mara niliporekebisha mawazo yangu, nilimpata mtu upesi wa kufanya ya kazi ya Dada Li na nikamshukuru Mungu. Ingawa yule mtu mgeni hakujua kanuni na ilibidi nijitahidi zaidi, nilihisi mwenye amani na raha. Nilikuwa tayari kujitolea kufanya chochote nilichoweza, na kuomba pamoja na ndugu zangu ili tufanye kazi yetu ya kanisa vizuri.

Wiki mbili baadaye, kiongozi wangu alisema, “Tunahitaji Dada Zhao aende kuhariri miswada ya makala katika kanisa lingine.” Niliposikia haya, niliwaza, “Lazima nizingatie kazi ya jumla ya nyumba ya Mungu. Sistahili kuwa mbinafsi tena. Lakini hata hivyo, ndio kwanza tumeanza kumfundisha dada mwingine kufanya kazi hii na hajui kanuni. Kazi yetu bila shaka itaathirika. Itakuwa vyema zaidi iwapo Dada Zhao atakaa hapo alipo.” Niligundua kwamba nilikuwa nikifikiria maslahi yangu mwenyewe tena. Nilikumbuka jinsi nilivyotembea kwenye njia ya wapinga Kristo, nikivuruga kazi ya kanisa mara kwa mara na kuikosea tabia ya Mungu. Niliogopa sana. Wakati huo huo, nilikumbuka maneno ya Mungu: “Usifanye mambo kwa ajili yako daima na usiyafikirie masilahi, hadhi na sifa yako mwenyewe kila wakati. Pia usiyafikirie masilahi ya mwanadamu. Lazima kwanza uyafikirie masilahi ya nyumba ya Mungu, na uyape kipaumbele. Unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu na uanze kwa kutafakari kama umekuwa mwenye najisi katika utimizaji wa wajibu wako au la, kama umefanya kila uwezalo kuwa mwaminifu, kama umefanya kila uwezalo kutimiza majukumu yako, na kufanya kadiri uwezavyo au la, na vile vile kama umefikiria wajibu wako na kazi ya nyumba ya Mungu kwa moyo wote au la. Lazima uyazingatie mambo haya. Yafikirie mara kwa mara, na itakuwa rahisi kwako kutekeleza wajibu wako. Iwapo wewe ni mwenye ubora duni wa tabia, uzoefu wako ni wa juu juu, au wewe hujabobeba katika kazi yako ya kitaalamu, basi kunaweza kuwa na makosa au upungufu katika kazi yako, na matokeo huenda yasiwe mazuri sana—lakini utakuwa umetiajuhudi zako zote. Wakati hufikirii tamaa zako za binafsi ama kufikiria maslahi yako mwenyewe katika mambo unayoyafanya, na badala yake unafikiria kila wakati kuhusu kazi ya nyumba ya Mungu, ukifikiria maslahi yake, na kutimiza wajibu wako vizuri, basi utakuwa ukikusanya matendo mema mbele za Mungu. Watu wanaotenda matendo haya mema ndio wale walio na uhalisi wa ukweli; hivyo, wamekuwa na ushuhuda(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinipa njia ya kutenda. Sikuwa na budi kuzingatia mapenzi ya Mungu na kazi ya kanisa. Sikupaswa kuwa mbinafsi na kujaribu kujiwekea watu wenye vipaji. Kwa hivyo nilimwomba Mungu: “Ee Mungu, nimekuwa mbinafsi na mbaya sana, kila mara nikiizuia nyumba ya Mungu kuwapandisha cheo watu na hivyo kuathiri kazi ya kanisa. Sitaki kukupinga tena. Tafadhali niongoze ili niukane mwili wangu na nitende kweli ...” Baada ya kuomba, nilienda kuzungumza na Dada Zhao juu ya uhamisho wake. Ingawa alihamishwa, sikufadhaika kama hapo awali. Badala yake, nilihisi kwamba wema na baraka ya Mungu ndiyo iliyoniwezesha kuipa nyumba ya Mungu talanta kama hiyo. Nilikuwa pia nimeweza kufanya wajibu wangu mwenyewe na moyo wangu ulijawa na amani na furaha. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu!

Iliyotangulia: Tiba ya Wivu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Nilifurahia Karamu Kubwa

Xinwei Mkoa wa Zhejiang Juni 25 na 26, mwaka wa 2013 zilikuwa siku zisizosahaulika. Eneo letu lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp