Maneno ya Mungu Yanaoongoza Njia

05/11/2020

Na Xiaocheng, Shaanxi

Maneno ya Mungu yanasema: “Kusudi la Mungu katika kuwafunua watu sio kuwaondoa, bali ni kuwafanya wakue(“Ni kwa Kuyatenda Maneno ya Mungu Tu Ndipo Kunaweza Kuwa na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Hapo zamani, kwa sababu sikuielewa nia ya Mungu ya kuwafichua watu, wakati wowote nilipofanya makosa yoyote katika kutimiza wajibu Wangu au kukumbana na matatizo yoyote, au kutofaulu au kupata shida, Ningekaa katika hali ya uhasi na kutoelewana: Nikizembea polepole katika kazi Yangu, bila kutafuta mapenzi ya Mungu, na kukosa kujisaili ili nijijue. Hii ilinifanya nipoteze fursa nyingi za kuupata ukweli. Kwa sababu ya mazingira ambayo Mungu alikuwa Amepanga, pamoja na nuru na mwongozo wa maneno Yake, baadaye niligundua mikengeuko katika uzoefu Wangu mwenyewe na kugundua kuwa Mungu hawafichui watu ili Atuangamize, lakini ili Ayasababishe maisha yetu yakue. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, Sikuwa na uhasi tena au kutomwelewa Mungu, nami nilipata njia ya kutenda na kupata kuufikia ukweli.

Katika kanisa, wajibu ninaotimiza ni kupanga nyaraka. Kwa muda, kwa ajili ya kuongozwa na Mungu, nilikuwa nimepata matokeo fulani katika kutimiza wajibu Wangu. Baada ya kurekebisha na kuweka pamoja matini ya injili ili ndugu zangu wayakague, hawakuwa wamegundua shida zozote, lakini ilipofika kwa matini ya injili waliyokuwa wameweka pamoja wao wenyewe, sikuweza tu kupata hitilafu kadhaa, lakini pia nilikuwa nimeweza kuhariri na kutatua hitilafu hizi kwa niaba yao. Ndugu zangu hawakuwa katika hali nzuri, lakini nilikuwa nimeweza kuleta uzoefu Wangu mwenyewe ili kushuhudia na kuwasiliana nao kwa kuzingatia maneno ya Mungu, kwa hivyo ikawawezesha kutoka katika hali yao mbaya. Pindi tu haya yaliponitendekea, nilihisi kufurahi. Nilihisi kana kwamba nimefanya kazi nzuri ya kutimiza wajibu wangu, na kwa kweli nilikuwa nimeendelea kwa kiasi fulani. Kwa mshangao mkubwa, hata hivyo, shida zimekuwa zikitokea mara kwa mara na matini ya injili ambayo nilikuwa nimekusanya hizi siku kadhaa zilizopita. Siku moja dada mmoja aliniambia, “Sentensi unazoandika kwenye matini ya injili wakati wote zilikuwa zimeboreshwa zaidi. Je, ni vipi kuna makosa mengi katika matini haya?” Kama mtu ambaye alikuwa mweledi katika kuhariri sentensi, nilikuwa na wakati mgumu kiasi kukubali jambo hili, nilijiwazia, “Nimetia bidii sana katika kuhariri matini haya ya injili, kwa hivyo kunawezaje bado kuwa na makosa yoyote katika sentensi zake?” Nilipoona marekebisho ambayo dada huyu alikuwa amefanya kwenye waraka, Sikufurahia kabisa. Hata hivyo, sikuwa nimetafuta mapenzi ya Mungu; sikuwa nimeyapitia tena matini haya ya injili. Siku iliyofuata, nilipokuwa nikikagua matini mengine ya injili, dada huyo huyo alisema bila kutarajiwa kwamba maoni Yangu katika marekebisho Yangu hayakueleweka na kwamba nilikuwa nimeshindwa kuweka mjadala wake wa jumla. Hata alisema kuwa mtu anayesimamia alikuwa ameona matini haya, na akatoa maoni yake. Niliposikia hivi, moyo Wangu ulipiga kwa mshindo masikioni mwangu. Nikajiwazia, “Je, hii ingewezaje kufanyika? Je, ningewezaje kukosa kuweka wazo dhahiri katika sentensi zangu, au kushindwa kuwasilisha maana ya maudhui hayo kwa jumla? Sasa, dada huyu hafikirii tu kuwa kazi yangu haijatayarishwa, lakini msimamizi pia anahisi vivyo hivyo. Je, hiyo haionyeshi kuwa kwa kweli kuna dosari kubwa katika mawazo kwenye waraka mzima? Sasa kwa kuwa sikuweza kutambua mambo kama haya ya waziwazi, je, nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu? Je, kuna shida na ubora wangu wa tabia kama mtu? Sistahili kutekeleza wajibu huu?…” Kadri nilivyozidi kuwaza kuhusu jambo hili, ndivyo nilivyozidi kuhisi kuwa dhaifu; nilikuwa nimekosa kumwelewa Mungu kabisa, na nilihisi kwamba Mungu hakuwa Anafanya kazi ndani yangu tena na kwamba alikuwa Amenipuuza. Wakati wa chakula cha mchana, niliwatazama dada zangu wakizungumza na kucheka kwa pamoja, lakini singeweza kuchangamka.

Wakati huo, nilikumbuka mojawapo ya matamshi ya Mungu: “Wakati watu hawaelewi au kutenda ukweli, mara nyingi wanaishi katika tabia potovu ya Shetani. Wanaishi kati ya mitego mingi ya kishetani, wakipiga bogo zao kwa sababu ya maisha yao ya usoni, heshima, hadhi, na masilahi yao mengine. Lakini ukitumia mtazamo huu kwa wajibu wako, katika kutafuta na kufuatilia ukweli, basi utapata ukweli(“Jinsi ya Kusuluhisha Shida ya Kuwa Mvivu na Mzembe Wakati wa Kutekeleza Wajibu Wako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalinizindua. Nilitulia, na kuanza kutafakari. Shida baada ya shida zilikuwa zimeibuka katika nyaraka ambazo nilikuwa nikihariri katika siku chache zilizopita, lakini hata baada ya kupata ufunuo kama huo, sikuwa nimetafuta mapenzi ya Mungu kamwe. Pia sikuwa nimejaribu kufahamu ni kitu gani kilikuwa kimesababisha kuibuka kwa shida hizi katika kutimiza wajibu wangu, ikiwa zilikuwa zimeibuka kwa sababu haya yalikuwa masuala kutokana na tabia na nia yangu au kwa sababu sikuwa nimepata ustadi katika kazi yangu na sikuwa na nimeelewa kanuni kadhaa vizuri kabisa, au kujaribu kutambua jinsi ya kuzuia makosa kama hayo kutokea baadaye ili niweze kupata matokeo bora katika kutimiza wajibu wangu. Sikuwa nimezingatia maswali haya ya kiutendaji kamwe; badala yake, nilikuwa nafikiria sana kwa kustaajabia jinsi watu wengine walivyoniona, na ikiwa Mungu alikuwa Anataka kunifichua na kuniondosha. Nilikuwa nimetumia wakati wangu wote kutafakari njia hizi potovu, bila kufikiria kuhusu njia sahihi kamwe, na kwa hivyo, kadri nilivyotafakari, ndivyo nilivyozidi kuwa na uhasi na mwenye mfadhaiko, nilikuwa nimepoteza hamu ya kutekeleza wajibu wangu. Ni wakati huo tu ndipo nilipooona mikengeuko katika uzoefu wangu. Baada ya kufichuliwa na Mungu, sikuwa nimelenga kuutafuta ukweli na kusuluhisha matatizo yangu, lakini badala yake nilikuwa nimefikiria kuhusu sifa na cheo changu, pamoja na hatma na maisha yangu ya usoni. Nilikuwa nimepumbazwa na Shetani, jambo ambalo lilinifanya kumwamini Mungu kwa miaka mingi bila kuwahi kupata kuingia kwa maisha. Singeweza kuendelea kuwa mwenye huzuni hivyo. Nilihitaji kutafuta mapenzi ya Mungu katika mazingira ya aina hii, nijitathmini ili nijijue, na kuingia kwenye uhalisi wa maneno ya Mungu.

Nilikuja mbele za Mungu ili nijitathmini: Kwa nini siku zote sikuweza kukubali ukweli uliofichuliwa? Kwa nini, kila wakati shida ilipotokea katika kutimiza wajibu wangu, nilikuwa nikiteseka hivyo? Ni nini hasa ilikuwa sababu ya kuteseka huku? Kwa njia ya maombi na kutafuta, niliyakumbuka maneno ya Mungu: “Ndani ya tabia potovu ya binadamu kuna suala la kubwa ambalo ninyi hamlifahamu; ni shida kubwa sana, na ambayo ni ya kawaida kwa ubinadamu wa kila mtu. Hii ndiyo sehemu dhaifu zaidi ya binadamu, na pia ni kipengele cha kiini cha asili ya binadamu ambacho ni kigumu sana kufunua na kubadili. Watu wenyewe ni viumbe. Je, viumbe wanaweza kufikia kudura? Vinaweza kufikia ukamilifu na kukosa dosari? Je, vinaweza kufikia ustadi katika kila kitu, viweze kuelewa kila kitu, na kutimiza kila kitu? Haviwezi, sivyo? Hata hivyo, ndani ya binadamu, kuna udhaifu. Mara wanapojifunza ufundi au taaluma, watu huhisi kuwa wana uwezo, kwamba wao ni watu wenye hadhi na wa thamani, na kwamba wao ni wataalamu wa aina fulani. Haijalishi jinsi wanavyoweza kuwa na uwezo, wanapojitokeza na talanta inayoonekana, wanapenda kujiandaa, wakijifanya kama watu muhimu, na kuonekana wakamilifu na wasio na dosari, bila kasoro hata moja; wanataka kuwa wakuu, wenye nguvu, wenye uwezo kamili, wenye kudura mbele ya wengine. … Kuhusu udhaifu, upungufu, ujinga, upumbavu, au ukosefu wa ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, watayafunika, kusitiri, wasiruhusu watu wengine wayaone, na kisha waendelee kujificha. Watu kama hao daima huwa ndotoni, sivyo? Si wanaota ndoto? Hawajijui wao wenyewe ni nani, wala hawajui jinsi ya kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Hajawahi kutenda kama binadamu halisi hata mara moja. Katika kutenda, watu wakichagua njia ya aina hii—kila mara wakiwa wanaota badala ya kuwa na mantiki, kila wakati wakitaka kuruka—basi hawana budi kukumbana na shida. Kusema ukweli, ukifanya hivi, basi haijalishi jinsi unavyomwamini Mungu, hutaelewa ukweli, wala hutaweza kupata ukweli, kwa sababu aina hii ya njia maishani unayoichagua si sahihi, na hatua yako ya kuanzia si sahihi. Lazima ujifunze jinsi ya kutembea ardhini, na kutembea kwa njia imara, hatua moja baada ya nyingine. Ikiwa unaweza kutembea, basi tembea; usijaribu kujifunza jinsi ya kukimbia. Ikiwa unaweza kutembea hatua moja baada ya nyingine, basi usijaribu kupiga hatua mbili kwa wakati mmoja. Lazima uwe mtu mwenye miguu yako ardhini kwa uthabiti. Usijaribu kuwa wa kimiujiza, mkubwa, au mkuu”

Wanadamu, wakitawaliwa na tabia yao ya kishetani, wanahodhi tamaa na hamu kiasi ndani yao, ambayo imejificha ndani ya ubinadamu wao. Yaani, wanadamu hawataki kamwe kubaki ardhini; wanashinda wakitaka kupaa hewani. Je, hewani ni mahali pa mtu kuishi? Huko ni mahali pa Shetani, sio mahali pa wanadamu. Wakati wa kuumba wanadamu, Mungu aliwaweka ardhini ili maisha yako ya kila siku yaweze kuwa ya kawaida na mitindo ya maisha yako iwe yenye nidhamu, na ili uweze kujifunza ujuzi wa kawaida kuhusu jinsi ya kuwa binadamu, na kujifunza jinsi ya kuishi maisha yako na jinsi ya kumwabudu Mungu. Mungu hakukupa mabawa; Hakukuruhusu ukae juu angani. Wale walio na mabawa ni ndege, na wale wanaozurura kote hewani ni Shetani na roho wabaya na pepo wachafu. Wao sio wanadamu! Watu wakiendelea kuwa na malengo kama haya, kila wakati wakitaka kujigeuza kuwa wa kimiujiza na wakuu, tofauti na wengine, na wa kipekee, basi hilo ni tatizo! Kwanza kabisa, chanzo cha mawazo yako si sawa. ‘Wa kimiujiza na mkuu’—hii ni fikira ya aina gani? ‘Kuwa bora kuliko wengine,’ ‘pinga ulinganisho wote,’ ‘asiye na dosari na safi ...’” (“Masharti Matano Ambayo Watu Wanayo Kabla ya Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). “Katika hali za kawaida, hakuna mtu ambaye ni stadi katika kila kitu, hakuna mtu aliye “stadi wa kila kazi.” Haijalishi ubongo wako umekomaa vipi, utambuzi wako ni wa kina vipi, daima kutakuwa na vitu usivyoelewa au usivyojua, kazi au ujuzi ambao hujui; katika kila safu ya biashara au kila kazi, daima kutakuwa na mapungufu katika ufahamu wako mwenyewe ambao hujui, kutakuwa daima na vitu ambavyo huwezi kufanya, au ambavyo vinakuzidi(“Ni kwa Kuyatenda Maneno ya Mungu Tu Ndipo Kunaweza Kuwa na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Ni baada tu ya kutafakari maneno ya Mungu na kuyalinganisha na hali yangu ndipo nilipogundua kuwa sikuwa niwewahi kukubali kufichuliwa na Yeye. Sababu ya kufanya hivi ni kwamba nilikuwa nimetawaliwa na asili yangu yenye kiburi ya kishetani; siku zote nilitaka kuwa mtu aliye mkamilifu, asiye na dosari, mwenye kiburi, na shujaa. Haijalishi nilikoenda au nilikokuwa nikitimiza wajibu wangu, kila wakati nilikuwa nataka kuwa mtu aliye bora zaidi. Ilikuwa imeonekana kana kwamba ilibidi niwe mtu wa aina hiyo ili nifanikiwe, na kwamba vinginevyo, ningekuwa mtu asiyefaa na asiyefanikiwa. Kwa hivyo, kila wakati shida ilipoibuka nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, sikuwa nimeishughulikia kwa utulivu, nikakubali kufichuliwa kwa aina hii na Mungu, na kuukubali upungufu wangu mwenyewe. Badala yake, nilikuwa nimehisi kushangaa na kwamba sikupaswa kufanya makosa yoyote, nikistaajabu ni jinsi gani ingeweza kutokea—kiasi kwamba hata ningeishi katika hali ya uhasi na kutokuelewa, nikishindwa kujitendea vizuri. Hakika sikujijua vizuri kabisa, na nilikuwa najichukua kuwa bora zaidi! Maneno ya Mungu yaliifanya iwe wazi kwamba kila wakati nilikuwa nikitafuta kuwa mtu mkamilifu, asiye na dosari, mwenye kiburi; hii ilikuwa imetokana kabisa na tamaa na matamanio ya Shetani. Ilikuwa ni Shetani akinitania na kunipotosha, ilhali kwa kweli nilikuwa chombo cha uumbaji, nisiweze kufikia ukamilifu daima. Mungu hajawahi kututaka tuwe wenye kiburi au wakamilifu; Angetaka tuwe wanyenyekevu, tuweze kupiga hatua thabiti, na tuenende kwa uaminifu kamili. Nikitumia aina yoyote ya kiwango na kimo nilivyokuwa navyo kama msingi, napaswa kutekeleza kazi yangu, nijifunze kuitii kazi ya Mungu, na nifanye niwezavyo kutimiza wajibu wangu; basi ndipo tu ningepata sababu inayofaa kuwa chombo cha uumbaji. Hakuna mtu aliye mkamilifu; watu wote wa kawaida wana dosari zao na njia ambazo hawako vizuri kama kawaida. Kwamba upungufu au shida zilitokea katika kutimiza wajibu wangu ilikuwa kawaida kabisa, na hakika kwa kufichuliwa, nilikuwa nimegundua mapungufu yangu. Ni kwa kuendelea kuboresha na kurekebisha upungufu huo tu ndipo ningeweza kusonga mbele zaidi na zaidi na kufanya kazi bora zaidi ya kutimiza wajibu wangu. Nisingeweza kushughulikia shida na mapungufu yangu vizuri, na nisiutafute ukweli ili kuyatatua, basi ningewezaje kupiga hatua? Ni wakati huo tu ndipo nilipogundua jinsi nilivyokuwa nimetawaliwa na tamaa na matarajio. Nilikuwa na kiburi sana hivi kwamba sikuwa najifahamu kamwe; hamu yangu ya kuwa mtu mkamilifu ilikuwa kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu na, kwa hivyo, singeweza kabisa kupata baraka na mwongozo Wake.

Nilisoma tena maneno ya Mungu: “Kusudi la Mungu katika kuwafunua watu sio kuwaondoa, bali ni kuwafanya wakue. Aidha, wakati mwingine unafikiria kwamba unafunuliwa, lakini kwa kweli haufunuliwi. Mara nyingi, kwa sababu hadhi ya watu ni duni na hawaelewi ukweli, na kuongezea wana tabia za kiburi, wanapenda kujionyesha, wana tabia ya uasi, hawana uangalifu, hawako makini, na hawajali, wanafanya kazi yao vibaya, na hawatekelezi wajibu wao ipasavyo. Kwa upande mwingine, wakati mwingine hukumbuki kanuni ambazo zimewekwa kwako, ukiziacha ziingiee katika sikio moja na kutokea lile lingine. Unafanya unavyopenda, kutenda kabla ya kushirikiana zaidi na wengine na kutenda kwa hiari yako mwenyewe. Unachofanya ni cha athari kidogo na kinaenda kinyume na kanuni. Katika hili, unapaswa kuwa na nidhamu—lakini inawezaje kusemwa kwamba umeondolewa? Lazima uchukulie hii kwa usahihi. Njia sahihi ya kuichukulia ni ipi? Katika masuala ambayo huelewi ukweli, lazima utafute. Siyo kutafuta uelewa wa mafundisho tu’. Lazima uelewe mapenzi ya Mungu, na uelewe kanuni ya jinsi familia ya Mungu inavyofanya kazi fulani. Je, kanuni hiyo ni ipi? Kanuni si mafundisho. Ina vigezo kadhaa, na lazima utafute maoni ni yapi kuhusu mpangilio wa kazi katika mambo kama haya, kile ambacho kiongozi Ameamuru juu ya kufanya kazi kama hiyo, kile ambacho maneno ya Mungu yanasema juu ya kutekeleza wajibu wa aina hii, na jinsi ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Je, vigezo vya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu ni vipi? Kutenda kulingana na kanuni za ukweli. Mwelekeo mpana ni kuweka masilahi ya familia ya Mungu na kazi ya familia ya Mungu kwanza. Hasa, katika vipengele vyote, hakupaswi kuwa na shida kubwa, na kwamba hakuna aibu inayopaswa kuletwa kwa Mungu. Watu wakishika kanuni hizi, je, wasiwasi wao utapungua polepole? Na je, kuelewa kwao vibaya pia kutapungua? Mara tu unapoweka kando kuelewa kwako vibaya na usiwe na maoni yasiyo na busara juu ya Mungu, mambo hasi yatakoma polepole kushikilia nafasi kubwa ndani yako, na utayakabili mambo kama haya kwa usahihi. Kwa hivyo ni muhimu kutafuta ukweli na kutafuta kuelewa mapenzi ya Mungu(“Ni kwa Kuyatenda Maneno ya Mungu Tu Ndipo Kunaweza Kuwa na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalinifanya nielewe kuwa Yeye kunifichua haikuwa ili Aniangamize, lakini iniwezeshe kugundua mapungufu katika kutimiza wajibu wangu na kujifunza ni sehemu zipi za tabia yangu potovu zilikuwa bado zikinizuia kutimiza wajibu wangu, ili kwamba ningeweza kusuluhisha shida hizi kwa wakati unaofaa, kuweza kuimarisha matokeo ya kazi yangu siku zote, na kubadilisha tabia yangu ya maisha haraka iwezekanavyo. Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, nilijituliza na kutafuta sababu ya shida zilizokuwa zimetokea katika uhariri wangu wa hivi karibuni wa matini yote mawili ya injili. Nilipofikiria kwa uangalifu sana, niligundua kuwa kila wakati nilipokuwa nimeona maendeleo fulani katika upangaji wangu wa nyaraka, nilikuwa nimeishi katika kujithamini na kujiridhisha. Sikuwa najitahidi kupiga hatua tena, na baada ya kushughulikia matini baadaye, nilikuwa nimefanya hivyo kwa uzembe kabisa, nikufanya hivyo tu kwa namna isiyo ya dhati. Kuhusiana na maelezo ya ukweli ulioko kwenye matini, sikuwa nimetafuta kanuni zao hata ingawa sikuweza kuzielewa; nilikuwa na wazo la juujuu tu kuhusu kile yaliyomaanisha, nami niliendelea katika hali yangu ya kuchanganyikiwa. Kwa hivyo, ilikuwa ajabu kwamba shida zilikuwa zimeibuka katika kutimiza wajibu wangu? Nilipofikiria kuhusu jambo hilo, niligundua kuwa ikiwa ningeutafuta ukweli ili kukomesha upotovu wangu mwenyewe na kutia bidii zaidi katika kumaliza kazi yangu kwa uangalifu, basi shida hizi zingeweza kuepukwa kwa kweli. Kwa kufichua ukweli huo, Mungu alinisababisha nitambue tabia yangu mwenyewe iliyo potovu na mtazamo niliokuwa nao katika kutimiza wajibu wangu, ili niweze kuutafuta ukweli wa kutatua shida hizi. Je, huu hasa haukuwa upendo Mungu aliokuwa nao kwangu? Utambuzi huu ulifanya moyo wangu ukachangamka: Niligundua kuwa ninapaswa kuacha kutomwelewa Mungu na kwamba lazima niharakishe na kubadilisha hali yangu ili nijitolee katika kutimiza wajibu wangu. Baada ya hapo, niliungana na msimamizi ili kuchunguza zaidi hoja katika matini hayo ya injili na, kwa kuzingatia kanuni, kuamua mwelekeo ambao unapaswa kufuatwa katika kuyahariri. Siku iliyofuata, nilipokuwa nikiyapitia tena, kwa mshangao, mambo kadhaa muhimu yalikuwa yameongezwa, na wakati nilipokuwa namalizia kuyahariri, nilihisi kujiamini zaidi na mtulivu.

Uzoefu huu ulinifanya nigundue kuwa ikiwa mikengeuko au shida zipo katika kutimiza wajibu wangu, sipaswi kuogopa, wala sipaswi kuogopa ikiwa Mungu ananifichua. Kinachoogofya ni kwamba, baada ya kufichuliwa, sitafuti ukweli ili nitatue shida zangu, na kisha nikae katika hali ya uhasi huku nikijiwekea mipaka, na hivyo nipoteze fursa nyingi za kuupata ukweli na kuchelewesha kuendelea kwangu maishani. Kuanzia sasa na kuendelea, haijalishi ni shida zipi au mapungufu gani ninayoweza kukumbana nayo, ninatamani kila wakati kuutafuta ukweli mbele za Mungu, kujishughulisha na kujitathmini ili niweze kujijua, kutumia maneno ya Mungu kurekebisha tabia yangu potovu, kutafuta njia ya kuingia katika ukweli. Ni kwa kufanya mazoezi kwa njia hii tu ndipo nitakapoweza kuendelea zaidi na zaidi katika maisha na kutimiza wajibu wangu kwa ustadi.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mbona Ujihusishe na Hila Unapomtumikia Mungu

Ee Mungu! Asante kwa kufunua asili yangu ya kiburi na majivuno. Kuanzia siku hii na kuendelea, hakika nitachukulia hili kama onyo na kuweka juhudi zaidi katika kujua asili yangu. Nitafanya kazi hasa kulingana na mipangilio ya kazi. Kwa kweli nitakuwa mtu mwenye mantiki, anayezingatia kanuni, na aliye na moyo wa uchaji Kwako.

Kuibuka Kutoka Kwenye Ukungu

Zhenxi Jijini Zhenzhou, Mkoani Hena Miaka kumi iliyopita, nikiendeshwa na asili yangu ya kiburi, sikuweza kamwe kutii kikamilifu...

Wokovu wa Mungu

Na Yichen, Uchina Mwenyezi Mungu anasema: “Kila hatua ya kazi ya Mungu—kama ni maneno makali, au hukumu, au kuadibu—humfanya mwanadamu kuwa...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp