Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni ya Kudharauliwa

34

Ding Ning Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong

Katika siku chache zilizopita, kanisa limepanga mabadiliko katika kazi yangu. Nilipopokea wajibu huu mpya, niliwaza, “Ninahitaji kuchukua fursa hii ya mwisho kuita mkutano na ndugu zangu wa kiume na wa kike, niongee nao wazi juu ya mambo, na niwaache na picha nzuri.” Kwa hiyo, nilikutana na mashemasi kadhaa, na kufikia mwisho wa wakati wetu pamoja, nikasema, “Nimeulizwa kuondoka hapa na kuenda kwa kazi tofauti. Natumaini mtamkubali kiongozi ambaye anakuja kuchukua nafasi yangu na kufanya kazi pamoja naye kwa moyo mmoja na wazo moja.” Mara tu waliposikia nikisema maneno haya, baadhi ya dada waliokuwepo walipauka, na tabasamu zikawatoka nyusoni. Baadhi yao walishika mikono yangu, baadhi yao walinikumbatia, na hali wakilia walisema, “Huwezi kutuacha! Huwezi kututupa kando na kupuuza mahitaji yetu! …” Dada wa familia mwenyeji hasa hakuwa radhi kuniruhusu niende. Aliniambia, “Ni vizuri sana kwamba uko hapa pamoja nasi. Wewe ni mtu ambaye anaweza kuvumilia shida, na wewe ni mzuri katika kushirikiana juu ya ukweli. Bila kujali ni wakati upi tulikuhitaji, daima ulikuwa hapo kutusaidia kwa uvumilivu. Kama ukienda, tutafanya nini? …” Kwa kuona kusita kwao kutengana nami, moyo wangu ulijaa furaha na ridhaa. Niliwafariji kwa maneno haya: “Mtegemeeni Mungu. Nitakapoweza, nitarudi na kuwatembelea.”

Lakini baada ya hapo, kila wakati nilipotazama nyuma tukio hilo la kuachana na ndugu zangu wa kiume na kike, nilikuwa na wasiwasi moyoni mwangu. Nilijiuliza, “Je, maonyesho hayo ya huzuni ni yanavyotarajiwa kuwa? Kwa nini walitenda kana kwamba kuondoka kwangu kulikuwa kitu cha kutisha? Kwa nini kanisa lilitaka nibadili kazi kwa vyovyote vile?” Sikuweza kuelewa hilo kabisa, na hivyo mara nyingi nilikuja mbele ya Mungu kutafuta majibu. Siku moja nilikuwa nikisoma mahubiri na nikaona kifungu hiki: “Wale ambao wangemtumikia Mungu ni lazima katika mambo yote wamtukuze Mungu na wawe na ushuhuda kwa Mungu. Ni kwa njia hiyo tu wanavyoweza kufikia matunda ya kuwaongoza wengine kumjua Mungu na ni kwa kumtukuza Mungu na kuwa na ushuhuda kwa Yeye pekee ndio wanaweza kuwaleta wengine mbele ya Mungu. Hii ni moja ya kanuni za huduma kwa Mungu. Matunda ya msingi ya kazi ya Mungu ambayo lazima yafikiwe ni kuwafanya watu waje mbele ya Mungu kwa njia ya kujua kazi ya Mungu. Ikiwa wale wanaohudumu kama viongozi hawamtukuzi Mungu na kuwa na ushuhuda Kwake, lakini badala yake wanajitokeza kwa maonyesho daima…, basi kwa kweli wanajiweka katika upinzani na Mungu. Wanakaa pahali pa Mungu na kuwafanya watu kuwatendea kama Mungu. Kazi yao inakuwa kazi inayoshindania watu na Mungu. Hivi sivyo hasa jinsi Shetani anavyompinga Mungu? Sasa, kuna viongozi wengi ambao kila mmoja ana msafara wa wafuasi chuni yake, na wanakuza na kufundisha watu jinsi wao wenyewe wanavyopenda. Mwishowe, Mungu hajapata yeyote anayejua moyo Wake. Watu wanafanyia nani kazi zao zote? Ni watu wangapi wamewafundisha ambao ni wa akili sawia na Mungu? Wameongoza watu wangapi kumjua Mungu kwa kweli na kumpenda? Kwa hiyo, ikiwa huduma ya watu haimtukuzi Mungu na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, basi kwa kweli wanajionyesha wenyewe. Ingawa wanadai kumtumikia Mungu, kwa kweli wanafanya kazi kwa ajili ya hadhi yao wenyewe na kweli wanafanya kazi kwa ajili ya raha ya miili yao. Hawafanyi kazi hata kidogo kumtukuza Mungu au kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Yeyote akikiuka kanuni hii ya utumishi kwa Mungu, basi inathibitisha kwamba yeye anamkataa Mungu” (“Kanuni Ambazo Zinapaswa Kueleweka za Kumtumikia Mungu” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu). Nilivyozidi kusoma, ndivyo moyo wangu ulivyozidi kutatizika. Nilivyozidi kusoma, ndivyo nilivyozidi kushtuka. Hisia yangu ya kujisuta ilizidishwa mara nyingi. Kutoka kwa mtazamo waliokuwa wamenionyesha ndugu zangu wa kiume na wa kike, niliweza kuona kazi yangu kweli haikuwa kuwaongoza ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele ya Mungu, lakini badala yake kuwaongoza mbele yangu. Sasa sikuweza kujizuia kupima tena matukio mengi wakati wa muda niliotumia na ndugu zangu wa kiume na wa kike. Mara kwa mara nilikuwa nimemwambia dada wa familia mwenyeji, “Angalia jinsi mlivyo na bahati nyote. Familia yako nzima ni waumini. Ninapokuwa nyumbani, mume wangu hunitesa mchana kutwa. Kama hanigongi, ananilaani. Nimetekeleza wajibu wangu kwa kadri linalowezekana, na angalia kiasi cha uchungu nilichovumilia kwa sababu ya imani yangu kwa Mungu.” Wakati ndugu zangu wa kiume na wa kike walipokabiliwa na shida, sikuwasiliana nao mapenzi ya Mungu; sikufanya kazi kama shahidi kwa kazi ya Mungu na upendo wa Mungu. Badala yake, mimi daima niliuweka mwili kwanza na nilijaribu kuwafanya watu kufikiri kuwa mimi ni mkarimu na mwenye huruma. Wakati wowote nilipomwona ndugu wa kiume au wa kike akifanya kitu kilichokuwa kinyume na kanuni, niliogopa kumkosea, hivyo singesaidia au kutoa mwongozo, daima nikijaribu kulinda uhusiano kati ya watu. Katika kila kitu nilichokifanya, kile nilichokijali zaidi kilikuwa ni cheo changu na picha yangu katika mioyo ya watu. … Kusudi langu kuu lilikuwa daima kupata huruma na upendezwaji kwa wengine; hii ikawa ridhaa yangu kubwa sana. Hili kwa hakika linafichua kwamba nilikuwa ninajiinua mwenyewe, nikijitumikia mwenyewe kama shahidi. Yote niliyoyatenda kwa kweli yalikuwa ni upinzani kwa Mungu. Nilifikiria juu ya maneno ya Mungu, ambayo yanasema, “Nafanya kazi miongoni mwenu sasa lakini bado mko hivi. Kama siku moja hakutakuwa na mtu wa kuwalinda na kuwaangalia, si nyote mtakuwa wafalme wa kilima?[a] Kwa wakati huo, nani atavisafisha vitu tena na kuondoa uchafu mnaposababisha janga kubwa?” (“Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu tena yalinileta kwa ufahamu wa jinsi huduma yangu kwa Mungu kwa kweli ilikuwa ni kujishuhudia mwenyewe na kujiinua na yalinisaidia kuona matokeo mabaya ya tabia hii. Maneno ya Mungu yalinisaidia kuona kwamba asili yangu, kama ile ya malaika mkuu, ingeweza kuniongoza kuwa gaidi dhalimu, na kwamba ningeweza kusababisha maangamizi makubwa. Nilifikiria kuhusu jinsi huduma yangu kwa Mungu haikutimizwa kulingana na kanuni sahihi za huduma; haikuwa ikimwinua Mungu na kumshuhudia Mungu, si kufanya wajibu wangu. Badala yake, siku zangu zilitumiwa kujionyeshwa mwenyewe, kujishuhudia mwenyewe, kuwavuta ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele yangu. Je, si aina hii ya huduma ni ya kudharauliwa? Je, si hii ni “huduma” ya mpinga Kristo tu? Kama haikuwa uvumilivu wa Mungu na rehema, ningekuwa tayari nimelaaniwa na Mungu na kuangushwa.

Wakati huo, nilitetemeka kwa uoga na aibu; hisia ya deni kubwa nililowiwa ikifurika moyoni mwangu, na nikasujudia chini, nikalia kwa uchungu na kumsihi Mungu: “Ewe Mungu! Kama haingekuwa ufunuo Wako na kupata nuru, sijui ni kwa kina gani ningeanguka. Kwa hakika ninakuwia Wewe zaidi ya ninavyoweza kulipa. Asante kwa wokovu Unaonipa! Asante kwa kunisaidia kuona nafsi mbaya na yenye kustahili dharau katika vina vya roho yangu. Asante kwa kunionyesha kwamba huduma yangu Kwako ilikuwa kwa kweli ni upinzani Kwako. Kama ningehukumiwa na matendo yangu, sistahili chochote isipokuwa laana Yako, lakini Umefungua macho yangu, Umeniongoza, na kunipa fursa ya kutubu na kuanza upya. Ewe, Mungu, niko radhi kuchukua uzoefu huu kama somo kuubeba kwa maisha yangu yote. Naomba kuadibu Kwako na hukumu yako ziende nami daima, na ninaomba zinisaidie mapema kutupa nafsi ya zamani ya Shetani na zinisaidie kweli kuwa mtumishi wa Mungu wa kustahi sana ili nipate kulipa deni kubwa ninalowiwa.”

Tanbihi:

a. Msemo wa Kichina, maana halisi ambayo ni “magaidi wanaoimiliki milima na kujitangaza kama wafalme.”

Maudhui Yanayohusiana

 • Chochote Mungu Asemacho Ndiyo Hukumu Hasa ya Mwanadamu

  Nilikuwa nikidhani kwamba Mungu alimhukumu na kumuadibu mwanadamu wakati tu Alipoufichua upotovu wa asili wa mwanadamu au alipoeleza maneno mkali ambayo yaliuhukumu mwisho wa mwanadamu. Ilikuwa ni baadaye kabisa tu ambapo tukio moja liliponiongoza kutambua kwamba hata maneno mapole ya Mungu pia yalikuwa ni hukumu na kuadibu Kwake. Niligundua kuwa kila neno Alilolisema Mungu ni hukumu Yake kwa mwanadamu.

 • Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu

  Wakati fulani kitambo, hata kama daima nilipata msukumo kiasi na fadhila wakati dada mmoja aliyeshiriki nami alishiriki nuru aliyokuwa amepata wakati alipokula na kunywa neno la Mungu, pia kila wakati nilikuwa na hisia ya muda mrefu kuwa alikuwa anajionyesha. Ningejiuliza, “Nikimjibu sasa hivi, sitakuwa nikimtia moyo? Kwa namna hiyo, sitaonekana basi kuwa duni kuliko yeye?” Matokeo yake yakawa, nilikataa kutaja maoni yangu mwenyewe katika ushirika au kutoa maoni kuhusu mawazo yoyote aliyoshirikisha.

 • Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo

  Kupitia uzoefu huu, nimepata kuelewa kwamba kuweka ukweli katika vitendo lazima kuwekwe kwa msingi wa neno la Mungu na lazima kuanzishwe kwa kanuni za kweli. Mtu akiacha neno la Mungu, basi kila kitu kinakuwa kitendo cha nje, yaani, kuweka ukweli wa mawazo yao wenyewe katika matendo. Hata ikiwa ningefanya mambo vizuri na kwa usahihi, bado haingechukuliwa kama kuweka ukweli katika vitendo, na hata zaidi haingeleta mabadiliko kwa tabia ya maisha yangu.

 • Kutupa mbali Jozi La Shetani Kunakomboa

  Kabla ya kumwamini Mungu, bila kujali chochote nilichokuwa nikifanya, sikuwahi kutaka kubaki nyuma. Nilikuwa tayari kukubali shida yoyote ili mradi ingemaanisha ningeinuka juu ya kila mtu mwingine zaidi. Baada ya kumkubali Mungu, mtazamo wangu uliendelea kuwa sawa, kwa sababu niliamini kikamilifu msemo, "Hakuna maumivu, hakuna faida," na kuona mtazamo wangu kama ushahidi wa msukumo wangu. Wakati Mungu alinifichulia ukweli, hatimaye niligundua kuwa nilikuwa nikiishi chini ya jozi la Shetani, nikiishi chini ya miliki yake.