Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

14/01/2018

Wu Xia Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong

Baada ya kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli. Hata hivyo, ilikuwa ni kwa njia ya ufunuo kutoka kwa Mungu tu nilipoweza kuona kwamba kwa hakika sikujifahamu kulingana na neno la Mungu.

Siku moja, nilikwenda mahali fulani na kiongozi wa wilaya ili kutoa pesa kiasi. Wakati kiasi cha fedha kilipothibitishwa na risiti ikaandikwa, nilifikiria kwamba ukandamizaji wa kikatili wa serikali ya CCP wa imani za kidini sasa ulikuwa unazidi kuwa mkali zaidi na zaidi, na walikuwa wanajaribu kila wawezalo kuchukua rasilmali ya kanisa. Hivyo kuwa katika usalama, nilipendekeza kuwa rekodi zote za mapokezi ya pesa za awali ziharibiwe. Wakati huo, kiongozi wa wilaya ghafla aliropoka: “Ukiharibu risiti ya mwisho, basi hakutakuwa na ushahidi. Je, na kama tu ukijiwekea pesa?” Sikujua nihisi nini baada ya kusikia hili, lakini kwa hakika nilihisi kama ni matusi makubwa kwa uadilifu wangu; ilikuwa vigumu sana kwangu kulikubali. Nilifikiri: Unadhani mimi ni mtu wa aina gani? Nimemfuata Mungu kwa miaka hii yote na mimi ni mtu mzuri. Ningewezaje kufanya kitu kama hicho? Aidha, nimesimamia kazi hii kwa miaka mingi sana na sijawahi kufanya makosa na fedha, kwa hiyo ni kwa nini niibe fedha za kanisa? Ni kwa njia gani nilifanana na Yuda? … Jinsi nilivyozidi kulifikiria, ndivyo nilivyozidi kukasirika. Jinsi nilivyozidi kulifikiria, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba aliniangalia kwa dharau na kuniamuru huku na kule. Niliumwa sana kiasi kwamba lilikuwa karibu kunifanya nilie.

Katika maumivu yangu, kwa ghafla nilikumbuka maneno ya Mungu, “Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6). Kisha nikawaza: Kwa nini Mungu asababishe hali ambapo huyu dada angesema jambo kama hilo? Mungu ananifundisha nini? Wakati nikitafakari jambo hili, moyo wangu ulianza kuhisi amani. Mawazo yangu yalianza kuhoji mijibizo michungu niliyokuwa nayo punde juu ya maneno ya huyu dada: Je, alikuwa na makosa aliposema “Je, na kama ukijiwekea tu pesa?” Mungu alisema kwamba mtu ataisaliti haki na kujitenga mbali na Mungu wakati wowote na mahali popote. Hakuna mtu kwa hakika anayeaminika. Je, mimi ni tofauti? Aidha, tabia yangu imebadilika kiasi gani? Nimepata ukweli kiasi gani? Kama sijapata ukweli wala kubadilika sana katika tabia, kwa nini siipaswi kuwaruhusu wengine kuniona kwa njia hiyo na ni kwa msingi upi napaswa nijione kama mwenye tabia nzuri na safi? Na ni kwa nini napaswa kuwa na hakika sana kwamba kamwe singeweza kuiba sadaka? Mungu wakati mmoja alisema: “Asili ya binadamu imejawa na asili ya Shetani, wao ni wenye ubinafsi kabisa, wachoyo, wenye tamaa, na wabadhirifu(“Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Je, hili linawahusu wengine tu na sio mimi mwenyewe? Kila mtu ni mwenye uroho kwa asili, je, mimi ni tofauti? Je, kile dada alichokisema kinakubaliana na ukweli? Wakati ninapokula na kunywa neno la Mungu, ninaonekana kuweza kwa utambuzi kujichunguza mwenyewe katika mwanga wa ufunuo wa Mungu. Hata hivyo, wakati dada huyu, bila kuwa na hisia, aliposema ukweli kulingana na ufunuo wa Mungu juu ya hali ya mwanadamu, nilikuwa na hasira sana. Si hili linafichua kwamba sijifahamu mwenyewe kulingana na neno la Mungu? Si hili linaashiria kwamba sina ufahamu wa kweli wa asili ya Shetani ndani yangu? Ni wakati huo tu nilipotambua kuwa kujijua mwenyewe kwa kula na kunywa neno la Mungu kulikuwa si kitu zaidi ya utambuzi wa nadharia na ufahamu wa juujuu. Sikuwa na uangalifu maalum kuelewa asili yangu ya kweli kupitia ufunuo wa neno la Mungu. Kwa hiyo, hali hii ilibidi itokee kwangu: Wakati ninapowasiliana, ni kawaida kusema kama kwamba ninajifahamu mwenyewe; mimi hukubali kwa kichwa changu na kuridhiana na neno ambalo Mungu hutumia kumfichua mwanadamu, lakini wakati nimekabiliwa na ukweli, ningekufa kabla ya kukubali kuwa mtu huyo ambaye Mungu hunionyesha. Nikitafakari juu ya siku za nyuma: Mara ngapi nimetangaza kwamba mimi sina hisia za binadamu, lakini wakati watu wengine wanasema mimi hukosa hisia ya binadamu, mimi mara moja hukana na kujitetea kwa njia zote. Mara ngapi midomo yangu imesema kuwa mimi hutekeleza wajibu wangu kwa uzembe, lakini watu wengine wanapoonyesha kuwa mimi hutekeleza wajibu wangu kwa uzembe, daima mimi hufikiria kila njia inayowezekana kujitetea na kuthibitisha uhalali wangu ili kujitola katika lawama. Mara ngapi nimetambua mbele ya wengine kuwa mimi si kitu, lakini wengine wanaposema huwa sifanyi chochote kwa usahihi, mimi huvunjika moyo na kuwa hasi sana kiasi kwamba siwezi kuchangamka. Mara ngapi nimetangaza kuwa nina ubora duni wa tabia na sina uwezo wa kufanya kazi, lakini ninapowasikia wengine wakisema kuwa nina ubora duni wa tabia na kwamba singeweza kamwe kuwa kiongozi mzuri, nakubali kushindwa na kuzembea. ... Ni wazi kwamba mimi ni mnafiki. Ninapojisemea kuwa mimi ni mpotovu, basi ni sawa, lakini wengine wanaposema kitu fulani kunihusu, siwezi kukikubali, na huwa ninakipinga. Hii inaonyesha vya kutosha kwamba ufahamu wangu kunihusu uko mdomoni mwangu tu. Huwadanganya wengine na ni wa kinafiki. Kwa kuwa sijawahi kweli kuweza kuchangua na kuelewa asili yangu ya kweli ya binafsi kupitia ufunuo wa maneno ya Mungu, kwa hakika bado sijaingia katika ufahamu wa nafsi yangu na tabia yangu haijabadilika.

Wakati huo, nilitafakari juu ya mtazamo wangu mwenyewe wa kujipenda na nikaona kuwa wa aibu kweli. Ufunuo wa Mungu umenidhihirishia kwa hakika na kuniruhusu nione wazi kwamba kwa hakika sijifahamu mwenyewe. Kuanzia sasa kwendelea, niko radhi kutambua kiini changu kipotovu kupitia kwa neno ambalo Mungu humfichulia mwanadamu; niko radhi kukabiliana na ukweli kwa ujasiri na kwa hakika kujifahamu ili hivi punde niweze kubadilisha tabia yangu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp