Mimi Kweli ni Uzao wa Joka Kubwa Jekundu

18/10/2019

Na Zhang Min, Hispania

Maneno ya Mungu yanasema: “Ilisemwa hapo awali kwamba watu hawa ni uzao wa joka kubwa jekundu. Kwa kweli, ili kuwa wazi, wao ni mfano halisi wa joka kubwa jekundu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 36). Ingawa nilikiri kwa maneno kuwa maneno ya Mungu ni ukweli na kwamba yanafichua hali yetu halisi, sikukubali moyoni mwangu kuwa nilikuwa uzao wala mfano halisi wa joka kubwa jekundu. Badala yake, nilihisi daima kwamba nilikuwa na uwezo wa kumfuata Mungu na kujitumia kwa ajili Yake, kwamba niliweza kuelewana vizuri na ndugu zangu wengi, na kwamba watu waliokuwa wakinizunguka waliniheshimu sana. Ingawa nilikuwa na tabia potovu, nilidhani, hiyo haikumaanisha kwamba nilikuwa mwovu kama joka kubwa jekundu. Ni baada tu ya kupitia uzoefu wa kufunuliwa ndipo nilipoona hatimaye ukweli wa jinsi nilivyokuwa nimepotoshwa na Shetani, na nikaona kwamba nilikuwa nimejawa na sumu za joka kubwa jekundu, na kwamba nilikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya vitu sawa kabisa na joka kubwa jekundu.

Wajibu wangu kanisani ulikuwa kukusanya makala. Siku moja, kiongozi wa kikundi changu aliniambia kuwa tangu wakati huo na kuendelea, mimi na dada yule niliyefanya naye kazi tungewajibikia kazi yote ya kukusanya makala kutoka kwa makanisa yote, na kwamba iwapo mtu yeyote angekuwa na tatizo, basi sote tungelijadili na kushiriki kwa pamoja. Niliposikia habari hii, nilishangaa kidogo na kuhisi kubanwa sana, na hata hivyo nilihisi kuridhika. Nilijiwazia: “Tutahusika katika kukusanya makala yote kutoka kwa makanisa yote. Inaonekana kana kwamba ninaweza kutekeleza wajibu wangu na mimi ni mtu anayeweza kufanya kazi ndani ya kanisa.” Ghafla hisia ya "jukumu" ilifoka ndani yangu na, bila kujua, nilikuwa nikitenda na kuongea katika nafasi ya mhakiki. Wakati mmoja, tulipokuwa tukibadilishana mawazo na ndugu kutoka kwa kikundi cha kazi cha makala cha kanisa lote, niligundua kuwa ndugu mmoja katika kikundi hicho alikuwa akijihusisha sana katikakazi yetu. Wakati wowote tatizo lilipotokea, kila mara angekuwa na ari ya kutoa maoni yake mwenyewe, na wakati mwingine ndugu mwingine alipouliza swali na tayari nilikuwa nimejibu katika kikundi chetu cha mtandanoi, bado angeendelea kusisitiza kutoa maoni yake baada yangu, na maoni yake juu ya suala hilo kwa hakika yangekuwa tofauti na yangu. Kila mara hili lilipofanyika, nilihisi kutofurahi kabisa, na nilijiwazia: “Anajishughulisha sana na kikundi hiki na watu wengi wanakubaliana na maoni yake. Inawezekana kwamba anataka kunishinda? Mmh! Anajua machache sana kunihusu. Hajui mimi hufanya wajibu gani, lakini anataka kushindana na mimi. Je, si amekosa kujitambua?” Nilipofikiria hili, nilianza kuhisi chuki dhidi ya ndugu huyu ikiinuka moyoni mwangu.

Baadaye, nilipanga ndugu katika kikundi cha kazi ya makala cha kanisa lote ili wabadilishane mawazo kuhusu matatizo katika makala. Ndugu wengi sana walikubaliana na mapendekezo yangu, lakini kwa mara nyingine tena ndugu huyu alikuwa na maoni tofauti kuhusu mambo na akaonyesha kasoro zangu. Nilijua kuwa ilikuwa kawaida kwa watu kuwa na maoni tofauti wakati wowote tatizo lilipotokea na kwamba tulipaswa kukubali pendekezo lolote lile lililonufaisha utekelezaji wa wajibu wetu, lakini nilipofikiri kuhusu jinsi ndugu huyu alivyokataa pendekezo langu mbele ya ndugu wengine wengi, nilijawa na upinzani na kutoridhika. Nilifikiri: “Ndugu wengine wanaweza kukubali pendekezo langu bila maoni yoyote yanayotofautiana. Lakini lazima ufanye kila kitu kikuhusu—je, unajaribu kufanya mambo yawe magumu kwangu kwa makusudi ili kuonyesha jinsi ulivyo mwaminifu kwa kazi na jinsi unavyoelewa mambo waziwazi? Una kiburi sana na ni vigumu sana kuelewana nawe!” Kadiri nilivyozidi kufikiri juu ya hilo, ndivyo nilivyozidi kuwa na chuki kwa ndugu huyu, hadi kufikia kiwango ambacho hata sikutaka kumwambia lolote. Siku kadhaa baadaye, ndugu huyu alitutumia makala tuyasome. Alisema makala hayo yaliandikwa vizuri sana na kwamba tulipaswa kuyagawa yawe kumbukumbu kwa kila mtu. Nilipomsikia akiongea kwa sauti ya kujiamini, nilianza kuhisi kutotulia, na nikawaza: “Tayari tumesoma makala haya. Kama makala haya tayari hayajachaguliwa basi lazima yawe na kosa. Lazima uwe kipofu kama popo ikiwa hata huwezi kung’amua hilo.” Kwa njia hii, nilikomesha kutoridhika nilikohisi ndani yangu na nikasoma makala haya tena bila ridhaa kabisa. Baadaye nilimpasha maoni yangu na maswala fulani ambayo nilihisi yalikuwamo ndani ya makala hayo, lakini alikataa kukubali maoni yangu na badala yake akanikumbusha niwe na mtazamo wa makini kwa kila makala, au kwamba niwasihi wakubwa wangu wasome makala haya tena. Upinzani ambao nilihisi ndani yangu ulikua wakati huo, na nikawaza: “Tangu nilipokutana na wewe, umekubali au kufuata mapendekezo yangu yoyote kwa nadra sana, lakini badala yake kila wakati wewe hutoa mapendekezo tofauti ili kila mtu ayarejelee na kuyakubali. Wewe huonyesha uwezo wako upatapo fursa yoyote na una kiburi sana. Huniheshimu hata kidogo. Kufanya shughuli na mtu kama wewe kunakera sana na kufadhaisha sana!” Hata nilifikiri: “Je, kanisa liliwezaje kumchagua akusanye makala? Mtu kama yeye aliye na tabia ya kiburi sana hafai kabisa kutekeleza wajibu huu. Pengine ninafaa kuripoti matatizo yake kwa kiongozi wangu na kumwacha kiongozi wangu aamue ikiwa anafaa kwa wajibu huu. Huenda ikawa bora kwa kiongozi wangu kumhamisha mahali pengine.” Nilipofikiria hili, niligundua kuwa hali yangu ilikuwa mbaya. Sikuelewa kiasi cha kutosha kuhusu ndugu huyu na nilijua kuwa sipaswi kufanya maamuzi juu yake kwa wepesi sana, lakini kwamba ninapaswa kuwa nikimtendea kwa haki. Hata hivyo, nilifikiri tu juu ya mambo haya, na sikujitafakari kuhusiana na suala hili zaidi, wala sikutafuta ukweli ili kutatua upotovu wangu mwenyewe, lakini badala yake niliendelea kuwaza sana juu ya ndugu huyu.

Siku moja, kiongozi wangu alipendekeza kwamba tubadilishane mawazo na viongozi na wafanyikazi wenza kutoka makanisa mengine yote ili kujadili jinsi ambavyo tungeelewa vyema kanuni za uandishi wa makala na kufanya kazi hii iliyokuwa ikishughulikiwa. Nilikubali lakini nilihisi woga mkubwa. Hii ingekuwa mara yangu ya kwanza kuhudhuria mkutano wa mtandaoni ili kubadilishana mawazo na viongozi wa kiwango cha kati na wafanyikazi wenza. Aidha, sikuwa hodari sana katika kujieleza, na nilikuwa na wasiwasi kuwa singeweza kushiriki waziwazi na kwamba ningesababisha kioja cha kujiaibisha, na kwa hivyo nilihisi kuudhiwa na matarajio hayo. Hata hivyo, siku moja kabla ya mkutano huo wa mtandaoni kuanza, nilipokea ghafla ujumbe kutoka kwa ndugu huyu akiuliza ikiwa angeweza kuhudhuria mkutano huo. Niliposoma ujumbe wake, nilikuwa karibu kupandwa na mori. Nilifikiri: “Umehudhuria mikusanyiko ili kubadilishana mawazo mara kadhaa hapo awali na hujawahi kukubali mapendekezo yetu yoyote, kwa hivyo kuna haja gani ya kuhudhuria mkutano huu? Tayari ninahisi kubanwa sana kwa ajili ya mkutano huu. Ukiniuliza swali gumu kesho, utafanya tukio zima liwe la kutovumilika zaidi kwangu.” Nilipofikiria kuhusu yeye kuhudhuria mkutano huo siku iliyofuata, nilijua kwamba kwa kweli sikumtaka kabisa awe hapo, na nilijaribu kufikiria kitu cha kusema cha kumfanya asitake kuhudhuria. Nilifikiria kitu cha kusema kwa muda lakini bado sikuweza kufikia sababu iliyofaa, kwa hivyo nikasema bila kuficha, “Maudhui ya mkusanyiko huu yatakuwa sawa na yale ya mkutano wetu uliopita. Huhitaji kuhudhuria.” Nilikuwa nimedhani kwamba kama ningemjibu kwa njia hii basi asingejibu lolote. Hata hivyo, ajabu ni kwamba, alituma ujumbe mwingine akisema, “Kesho nitakuwa na muda kiasi na ningependa kusikia kile ambacho kila mtu atakuwa akijadili.” Niliposoma ujumbe wake, nilihisi kufadhaika sana, lakini bado sikuwa na sababu ya kumnyima ruhusa ya kwenda. Yote niliyoweza kufanya ni kukubali kwa kusita, lakini bado nilisita kumjumuisha kwenye kundi. Nilijiwazia: “Wewe ni kero sana! Kwa nini siwezi kukuepuka kamwe? Je, tutaweza kufanikisha chochote katika mkutano huu ukihudhuria? Unajaribu kufanya mambo yawe magumu kwangu kwa makusudi?” Niliendelea kujaribu kufikiria sababu ya kumzuia kuhudhuria, na hata nilifikiria kumwondoa kwenye orodha ya marafiki, lakini nikafikiri: “Sawa, unaweza kuhudhuria. Ikiwa wewe ni msumbufu na mwenye kutoridhika na chochote kama jinsi ulivyokuwa kwenye mkutano uliopita basi kila mtu ataona jinsi ulivyo na kiburi na majivuno, na kisha hakuna mtu atakayekuheshimu sana....” Wakati huohuo, niligundua kuwa hisia zangu za chuki dhidi yake zilikuwa zimebadilika kuwa kinyongo na kwamba nilikuwa tu nikionyesha nia zangu mbaya. Ikiwa ningeruhusu hali hii iendelee kukua, niliogopa kufikiria jinsi ambavyo ningemtendea kaka huyu. Na kwa hivyo, nilimwomba na kumwita Mungu kwa haraka, nikimsihi Aulinde moyo wangu. Mara tu baada ya kutulia, nilianza kufikiria ni kwa nini nilikuwa nimejibu kwa ukali sana nilipokutana na kitu ambacho hakikubaliana na maoni yangu, kwa nini sikuweza kukubali sauti yoyote ambayo ilinipinga, na kwa nini nilikuwa nimeunda hisia kali sana za chuki dhidi ya kaka huyu.

Nilipokuwa nikitafuta, nilisoma kifungu katika ushirika: “Jinsi wale wanaohudumu kama viongozi wanavyowatendea ndugu wa kiume na wa kike ambao huwaona kuwa wenye kusumbua, ambao wanawapinga, na ambao wana maoni tofauti kabisa kuwaliko—hili ni suala la maana sana na linapaswa kushughulikiwa kwa tahadhari. Wasipoingia katika ukweli, kwa hakika watabagua na kuwakaripia watu kama hawa wanapokumbwa na aina hii ya suala. Aina hii ya hatua hasa ni dhihirisho la asili ya joka kubwa jekundu linalompinga na kumsaliti Mungu. Ikiwa wale wanaohudumu kama viongozi wanafuatilia ukweli, na kuwa na dhamiri na mantiki, watatafuta ukweli na kushughulikia suala hili kwa usahihi. … Kama watu, tunahitaji kuwa wa haki na wa kutopendelea. Kama viongozi, tunapaswa kushughulikia mambo kulingana na maneno ya Mungu ili kuwa mashahidi. Tukifanya mambo kulingana na mapenzi yetu wenyewe, tukiipa uhuru tabia yetu potovu, basi huo utakuwa ushinde wa kuogofya” (Ushirika Kutoka kwa wa Juu). Ushirika huu ulinigusa sana. Nilifikiria ni kwa nini nilikuwa mwenye upinzani na chuki sana kwa kaka huyu, kiasi kwamba hata nilikuwa nimeanza kumchukia—haikuwa tu kwa sababu hakukubaliana na ushirika wangu na alikuwa ametoa maoni mengine ambayo yalikuwa yamesababisha niaibike? Je, haikuwa tu kwa sababu nilikuwa nimemwona akijishughulisha sana katika kikundi chetu na kupata kibali cha kila mtu, na kwa hivyo nilihisi kwamba alikuwa amenipiku? Mwanzoni, sisi ndugu tulikuwa tumefanya kazi kwa pamoja ili kutekeleza wajibu wetu, na kwa sababu ya ubora na ufahamu wetu tofauti, ilikuwa kawaida kuwa na maoni tofauti juu ya maswala fulani. Yote ambayo ndugu huyu alikuwa akifanya ni kuonyesha maoni yake mwenyewe—hakuficha nia zozote mbaya. Na bado daima nilikuwa namtaka anisikilize na kunitii. Nilimtaka akubaliane nami na akubali chochote nilichosema, na asingesema kabisa chochote tofauti na mimi. Vitendo vyake vilipogusa kujiheshimu kwangu na cheo changu, upinzani mwingi ulitokea ndani yangu, kiasi kwamba hata nikamtenga na sikutaka ahudhurie mkutano huo. Na iwapo ningemruhusu ahudhurie, ilikuwa tu kwa sababu nilimtaka ajifanye yeye mwenyewe kuonekana mjinga. Nilichangua fikira na mawazo haya na nikaona kwamba yote niliyokuwa nikionyesha ilikuwa ni tabia ya kishetani yenye nia mbaya na kiburi. Matendo yangu kweli yalikuwa yamekuwa mabaya sana na ya kustahili kudharauliwa!

Kisha nikasoma katika ushirika: “Bila kujali wewe ni nani, almradi hukubaliani nao, unakuwa lengo la adhabu yao—hii ni tabia gani? Je, si ni sawa na ya joka kubwa jekundu? Joka kubwa jekundu hutafuta ukuu juu ya vyote na hujiona kama kitovu cha vitu vyote: ‘Usipokubaliana nami basi nitakuadhibu; ukithubutu kunipinga basi nitatumia vikosi vya jeshi kukunyamazisha.’ Hizi ndizo sera za joka kubwa jekundu, na tabia ya joka kubwa jekundu ni ile ya Shetani, malaika mkuu. Kuna watu wengine ambao, mara wanapokuwa viongozi au wafanyikazi, huanza kutekeleza sera za joka kubwa jekundu. Je, wao hufanyaje hivyo? ‘Mimi sasa ni kiongozi na wajibu wangu wa kwanza ni kumfanya kila mtu anitii moyoni na kwa maneno, na wakati huo tu ndipo ninaweza kuanza kazi yangu rasmi’” (“Ili Kuingia Katika Uhalisi wa Ukweli, Mtu Anapaswa Kulenga Kubadilisha Tabia Yake ya Maisha” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha XIII). “Ndugu akiwa na maoni au awe na dhana juu ya mtu ambaye kwa kweli ana ukweli na ambaye anaweza kukubali ukweli na kuutenda, au akigundua kwamba mtu huyo ana dosari na hufanya makosa, na amsute, amkosoe au kumpogoa na kumshughulikia, je, si mtu huyo ataishia kumchukia? Mtu huyo lazima kwanza achunguze suala hilo na afikirie: ‘Je, kile unachosema ni kweli au si kweli? Je, kinakubaliana na ukweli? Iwapo kinakubaliana na ukweli, basi nitakikubali. Ikiwa kile unachosema kina ukweli nusu au kimsingi kinakubaliana na ukweli, basi nitakikubali. Ikiwa unachosema hakipatani na ukweli, lakini naweza kuona kuwa wewe si mtu mwovu, kuwa wewe ni ndugu, basi nitakuwa mvumilivu, na nitakutendea kwa njia muwafaka’” (“Mikengeuko na Makosa Ambayo Lazima Yatatuliwe ili Kutenda Kujijua Mwenyewe” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha VIII). Kutoka kwa ushirika huo, niliona kwamba tangu joka kubwa jekundu lianze kutawala, halijawahi kudhukuru masilahi ya watu wa kawaida, wala halifikirii hata kidogo jinsi ya kusimamia nchi vizuri au jinsi ya kuwaruhusu watu wa China kuishi maisha ya furaha. Badala yake, kila kitu ambacho joka hilo hufanya hufanywa ili kulinda tu cheo na mamlaka yake. Ili kuwa na utawala wa kudumu juu ya watu na kuwadhibiti watu kabisa, hutekeleza sera ya itikadi moja na sauti moja, huwakataza watu kuwa na maoni yanayopingana na kulikata. Almradi wazo litolewe na kutetewa nalo lenyewe, basi kila mtu lazima alikubali liwe ni sahihi au si sahihi, na kila mtu lazima akubaliane nalo. Mtu yeyote asipokubaliana nalo au alipinge, basi litachukua maisha yake na kumwekea vikwazo, likifuatilia sheria ya kishetani ya “Acha wale wanaokubaliana nami waneemeke na wale wanaonipinga waangamie.” Yeyote atoaye vipingamizi huonekana kama saratani ambayo inahitaji kukatwa na lina hamu ya kuwaua wote wanaolipinga haraka iwezekanavyo na kuwaangamiza kabisa. Mauaji ya kinyama ya wanafunzi wa chuo kikuu huko Tiananmen Square mnamo Juni 4, 1989 ni mfano mmoja. Hao wanafunzi wa chuo kikuu walikuwa tu wakipinga ufisadi na kutetea demokrasia, lakini walionekana na Chama cha Kikomunisti cha China kama maadui. Chama cha Kikomunisti cha China kiliita tapo hilo la wanafunzi uasi wa kupinga mapinduzi na kikaamua kufanya ukandamizaji mkali wa wanafunzi. Nilipolinganisha tabia yangu mwenyewe na ile ya joka kubwa jekundu, niligundua kuwa asili ambayo nilikuwa nimeonyesha ilikuwa sawa kabisa na ya joka kubwa jekundu. Nilikuwa mtu mpotovu na tabia yangu haikuwa imebadilika hata kidogo. Wala sikuwa na uhalisi wa ukweli hata kidogo, na maoni niliyoibua si lazima kwamba yalikuwa sahihi kila wakati. Niliwataka wengine daima wanisikilize na kuniitii bila swali, la sivyo ningechoshwa nao na ningewaepa sana, kiasi kwamba hatungeweza kupatanishwa. Ningefikiria kila njia inayowezekana ya kuwaondoa—nilikuwa mwovu sana na asiye na ubinadamu! Nilifikiria jinsi kanisa lilivyopanga mimi na ndugu tutekeleze wajibu wetu pamoja ili tuweze kujifunza kutoka kwa uwezo wa kila mmoja, tufanye kazi pamoja kwa amani, na kutekeleza wajibu wetu pamoja ili kumridhisha Mungu. Na hata hivyo sikuwa nimefikiria mambo haya hata kidogo, lakini badala yake nilikuwa nimefikiria tu ikiwa ningeweza kushikilia cheo changu mwenyewe au la, ikiwa kujiheshimu kwangu na hadhi yangu vingeumizwa au la, na ikiwa mtu mwingine yeyote angenisikiliza au la. Kwa wale ambao walikuwa na maoni ambayo yalitofautiana na yangu, ningewatenga na kuwakandamiza—kwa kweli nilikuwa nimetenda kama jahili aliyetawala kilima chake mwenyewe kama bwana. Kwa kufanya hivyo, ningewezaje kumridhisha Mungu katika utendaji wa wajibu wangu? Nilikuwa tu nikifanya uovu na kumpinga Mungu! Nilipofikiri juu ya mambo haya, nilihisi aibu hata zaidi; nililiona kwamba nilikuwa mwenye kiburi na majivuno sana, kwamba nilikuwa na tabia sawa na ya joka kubwa jekundu na kwamba pia nilikuwa na uwezo sana wa kutenda vitu vyote ambavyo joka kubwa jekundu lilivitenda. Wakati huo tu ndipo nilipoona kuwa kwa kweli nilikuwa uzao wa joka kubwa jekundu na kwamba nilijawa na sumu za joka kubwa jekundu. Nisingefuatilia mabadiliko ya kitabia, basi ningefanya mambo ambayo yangekatiza na kuvuruga kazi ya Mungu bila kujua na, mwishowe, ningeadhibiwa na kulaaniwa na Mungu kwa sababu ya kukosea tabia Yake. Wakati huo, nilianza kuelewa mapenzi ya Mungu na makusudi Yake mazuri. Hali hii isingenifika, nisingekuwa kabisa na uwezo wa kutambua kuwa nilikuwa na kiini cha joka kubwa jekundu—ambacho kilikuwa cha kiburi na majivuno na ambacho kilitafuta ukuu juu ya yote—na asili ya Shetani ya kumpinga Mungu. Wakati huo huo, pia nilikuja kuelewa kuwa kupangwa kwa aina hii ya hali na Mungu kwa kweli kulikuwa kinga bora kwa mtu kama mimi ambaye alikuwa na kiburi na majivuno, na ambaye alijiona mkuu zaidi. Kama ndugu wote wangeniunga mkono na kuniidhinisha, na kama hakuna mtu ambaye angetoa kipingamizi chochote kingine, basi ningekuwa mwenye kiburi na majivuno hata zaidi, ningewafanya wengine wanifuate na kunitii kwa kila namna, ningesimama mahali pa Mungu bila hata kufahamu hilo, nikitawala ufalme wangu mwenyewe na mwishowe kukosea tabia ya Mungu hadi Mungu anichukie na kunikataa. Nilipoelewa mambo haya, nilitoa shukrani na sifa kwa Mungu kwa dhati. Niliacha pia hisia zangu za chuki na maoni yangu kuhusu ndugu huyu. Bila kujali jinsi ambavyo mkutano huu wa kubadilishana mawazo ungekuwa mwishowe, nilikuwa tayari kuachana na asili yangu ya kishetani na kutii mipango na utaratibu wa Mungu. Sikuwahi kufikiria kuwa matokeo ya mkusanyiko huo yangekuwa zaidi ya matarajio yangu yote. Siku hiyo, chini ya mwongozo wa Mungu, mkusanyiko uliendelea kwa utaratibu sana, na nilipobadilishana mawazo na ndugu huyo, tuliweza kuafikiana na sote wawili tukasaidiana kuimarisha udhaifu wa kila mmoja. Tulitegemea mwongozo wa Mungu na tukamaliza mkutano kwa utulivu.

Kupitia kufunuliwa na Mungu, nilikuja kugundua kwamba kwa kweli nilikuwa uzao wa joka kubwa jekundu na kwamba sumu za joka kubwa jekundu ziligeuka kuwa maisha yangu kitambo. Iwapo singeweza kuachana na tabia hizi potovu, basi mwishowe ningechukiwa tu na kukataliwa na Mungu, Mungu angeniondoa, na ningepoteza nafasi yangu ya kupata wokovu milele. Nilifikiri juu ya maneno ya Mungu ambayo yanasema: “Sababu nyinyi ni watu Wangu waliozaliwa kwa nchi ya joka kubwa jekundu, kwa hakika hakuna tu hata kidogo, ama kipimo cha sumu ya joka kubwa jekundu ndani yenu. Hivyo, hatua hii ya kazi Yangu hasa inawaangazia, na hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu wa kupata mwili Kwangu Uchina(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 11). “Ilisemwa hapo awali kwamba watu hawa ni uzao wa joka kubwa jekundu. Kwa kweli, ili kuwa wazi, wao ni mfano halisi wa joka kubwa jekundu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 36). Nilikuja pia kuelewa kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu ni ya kiutendaji na ya busara sana. Mungu huonyesha maneno Yake ili kufunua sumu za joka kubwa jekundu na asili ya kishetani ambayo imo ndani yetu, na kwa kufichua ukweli, Mungu aliniruhusu niwe na ufahamu na utambuzi kiasi kuhusu sumu za joka kubwa jekundu zilizokuwa ndani yangu, na hivyo kulikataa na kuliacha, kamwe nisidanganywe au kudhuriwa nalo tena. Nilijua bado kulikuwa na falsafa na semi nyingi zinazochukuliwa kuwa ukweli za kishetani, na sumu nyingi za joka kubwa jekundu ndani yangu. Lakini kuanzia siku hiyo kuendelea, nilitamani tu kufuatilia ukweli kwa dhati, kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, kujitahidi kuepukana na sumu zote za joka kubwa jekundu haraka iwezekanavyo, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu ili kuuletea moyo wa Mungu faraja!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp