Sura ya 11

Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Ambayo ni kusema, Nianzapo binafsi kazi Yangu duniani, na wakati enzi ya hukumu inakaribia tamati yake, Naanza kuelekeza maneno Yangu kwa ulimwengu mzima, na kutoa sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima. Kupitia maneno Yangu, Nitasafisha wanadamu na mambo yote miongoni mwa yote yaliyo mbinguni na duniani, ili nchi si chafu na fisadi tena, lakini ni ufalme takatifu. Nitatengeneza upya mambo yote, ili yatolewe kwa matumizi Yangu, na yasiwe na pumzi ya dunia tena, na yasichafuliwe na ladha ya ardhi tena. Duniani, mwanadamu ametafuta malengo na asili ya maneno Yangu, na amechunguza matendo Yangu, lakini bado hakuna aliyewahi kujua kwa kweli asili ya maneno Yangu, na hakuna aliyewahi kuona kwa kweli matendo Yangu ya ajabu. Ni leo tu, Nikujapo binafsi miongoni mwa wanadamu na kuongea maneno Yangu, ndipo mwanadamu anapata maarifa kidogo kunihusu, kutoa nafasi “Yangu” ndani ya mawazo yao, badala yake kutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya fahamu zake. Mwanadamu ana dhana na amejawa na udadisi; ni nani ambaye hangetaka kumwona Mungu? Ni nani ambaye hangetamani kukutana na Mungu? Lakini bado kitu pekee kilicho na nafasi ya uhakika ndani ya moyo wa mwanadamu ni Mungu ambaye mwanadamu anahisi kuwa dhahania na asiye dhahiri. Nani angetambua haya kama Singewaeleza wazi? Nani angeamini kwa kweli Mimi nipo? Kwa hakika bila shaka yoyote? Kuna tofauti kubwa kati ya “Mimi” aliye ndani ya mwanadamu na “Mimi” wa ukweli, na hakuna anayeweza kuwalinganisha. Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi Nijua, na hata angekuja kunijua, je, maarifa kama hayo bado hayangekuwa dhana? Kila siku Natembea miongoni mwa watu wengi, na kila siku Nafanya kazi ndani ya kila mtu. Wakati mwanadamu kweli ananiona, ataweza kunijua kwa maneno Yangu, na kuelewa njia Ninazotumia kuzungumza na pia nia Zangu.

Ufalme ufikapo rasmi duniani, ni nini, kati ya mambo yote, sio kimya? Nani, kati ya watu wote, hana hofu? Natembea kila mahali katika ulimwengu dunia wote, na kila kitu kinapangwa na Mimi binafsi. Wakati huu, nani asiyejua vitendo Vyangu ni vya ajabu? Mikono Yangu inashikilia mambo yote, lakini bado Niko juu ya mambo yote. Leo, si kupata mwili Kwangu na kuwepo Kwangu binafsi miongoni mwa wanadamu maana ya ukweli ya unyenyekevu na kujificha Kwangu? Kwa nje, watu wengi wananipongeza kama mzuri, wananisifu kama mzuri, lakini ni nani anayenijua kweli? Leo, mbona Nauliza kuwa mnijue? Lengo Langu sio kuaibisha joka kubwa jekundu? Sitaki kumlazimisha mwanadamu kunisifu, lakini kumfanya anijue kupitia hapo atakuja kunipenda, na hivyo kunisifu. Sifa kama hiyo inastahili jina lake, na si mazungumzo yasiyokuwepo; ni sifa tu kama hii inaweza kufikia kiti Changu cha enzi na kupaa angani. Kwa sababu mwanadamu amejaribiwa na kupotoshwa na Shetani, kwa sababu amechukuliwa na fikira na kuwaza, Nimekuwa mwili ili kuwashinda binafsi wanadamu wote, kufichua dhana zote za mwanadamu, na kupasua mawazo ya mwanadamu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu hajionyeshi mbele Yangu tena, na hanitumikii tena akitumia dhana zake mwenyewe, na hivyo, “Mimi” katika dhana za mwanadamu ameondoka kabisa. Ufalme ufikapo, Naanza kwanza hatua hii ya kazi, na Nafanya hivyo miongoni mwa watu Wangu. Sababu nyinyi ni watu Wangu waliozaliwa kwa nchi ya joka kubwa jekundu, kwa hakika hakuna tu hata kidogo, ama kipimo cha sumu ya joka kubwa jekundu ndani yenu. Hivyo, hatua hii ya kazi Yangu hasa inawaangazia, na hiki ni kipengele kimoja cha umuhimu wa kupata mwili Kwangu Uchina. Watu wengi hawawezi kuelewa hata chembe cha maneno Ninayoyasema, na wanapoweza, uelewa wao ni wenye ukungu na ovyo. Hii ni ile hatua ya kugeuka amabayo Ninaizungumzia. Iwapo watu wote wangeweza kusoma maneno Yangu na kuelewa maana yao, basi nani miongoni mwa wanadamu angeweza okolewa, na kutupwa kuzimu? Mwanadamu anijuapo na kunitii ndio wakati Nitakapopumzika, na itakuwa wakati hasa ambapo mwanadamu ataweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Leo, kimo chenu ni kidogo sana, karibu kiwe kiwango cha kusikitisha, na hakistahili hata kuinuliwa—sembuse ujuzi wenu kunihusu.

Ingawa Nasema malaika wameanza kutumwa mbele kuchunga wana na watu Wangu, hakuna anayeweza kuelewa maana ya maneno Yangu. Nikujapo binafsi miongoni mwa binadamu, malaika wanaanza wakati huo huo kazi ya uchungaji, na wakati huo wa uchungaji wa malaika, wana na watu wote hawapati tu majaribio na uchungaji, lakini wanaweza pia kuona, na macho yao, tukio la kila aina ya maono. Kwa sababu Nafanya kazi moja kwa moja kwa uungu, kila kitu kinaingia katika mwanzo mpya, na kwa sababu uungu huu unafanya kazi moja kwa moja, hauzuiliwi hata kidogo na ubinadamu, na unaonekana kwa binadamu kufanya kazi huru chini ya hali isiyo ya kawaida. Lakini bado, Kwangu, yote ni kawaida (mwanadamu anaamini si ya kawaida kwa sababu hajawahi kukutana na uungu moja kwa moja); hauna fikira zozote za kibinadamu, na haujachafuliwa na mawazo ya kibinadamu. Watu wataona haya wakati tu wote wataingia katika njia sawa; kwa sababu sasa ndio mwanzo, inapokuja suala la kuingia kwake, mwanadamu ana mapungufu mengi, na makosa kama haya na upofu huwezi ukaepukwa kwa urahisi. Leo, sababu Nimewaongoza hadi hapa, Nimefanya mipango ya kufaa, na Nina malengo Yangu Mwenyewe. Ningewaeleza kuyahusu leo, mngeweza kweli kuyajua? Nayajua vizuri mawazo ya akili ya mwanadamu na matakwa ya moyo wa mwanadamu: Nani hajawahi kutafuta njia ya kujitoa mwenyewe? Nani hajawahi fikiria matarajio yake mwenyewe? Lakini hata kama mwanadamu ana akili tajiri na wa mche nani aliweza kutabiri kwamba, kufuatia enzi, sasa kungekuwa kulivyo? Hili kweli ni tunda la juhudi zako binafsi? Haya ni malipo ya kazi yako ya bidii? Hii ndiyo picha nzuri iliyoonwa na akili yako? Nisingewaongoza wanadamu wote, nani angeweza kujitenga na mipango Yangu na kupata njia nyingine ya kutoka? Ni fikira akilini mwa mwanadamu na tamaa yake ambayo yamemleta hadi leo? Watu wengi wanaishi maisha yao yote bila kutimiziwa kwa matakwa yao. Kweli hili ni kwa sababu ya kosa katika fikira zao? Maisha ya watu wengi yamejawa na furaha na ridhaa isiyotarajiwa. Kweli ni kwa sababu wanatarajia kidogo sana? Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Je, kuishi kwa mwanadamu kifo chake kinatokana na uchaguzi wake mwenyewe? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu. Ingawa Sijitokezi binafsi kumruhusu mwanadamu kunitazama vizuri, watu wengi wanaogopa kuona uso Wangu, wanaogopa sana Nitawapiga chini, kwamba Nitawaangamiza. Mwanadamu kweli ananijua Mimi ama hanijui? Hakuna anayeweza kusema kwa hakika. Sivyo? Mnaniogopa na pia kuadibu Kwangu, lakini bado mnasimama na kunipinga wazi na kunihukumu hadharani. Sivyo? Kwamba mwanadamu hajawahi kunijua ni kwa sababu hajawahi kuuona uso Wangu ama kuisikia sauti Yangu. Hivyo, hata kama Niko ndani ya moyo wa mwanadamu, je, kuna wale ambao Sionekani mwenye ukungu na asiye dhahiri katika mioyo yao? Kuna wale Ninaoonekana vizuri ndani ya mioyo yao? Sitamani wale walio watu Wangu pia kutoniona vizuri, na hivyo Naanza kazi hii kubwa.

Nakuja polepole miongoni mwa wanadamu, na Naondoka taratibu. Kuna aliyewahi kuniona? Jua linaweza kuniona kwa sababu ya moto wake unaochoma? Mwezi unaweza kuniona kwa sababu ya uwazi wake unaong’aa? Kundinyota zinaweza kuniona kwa sababu ya mahali zipo angani? Nikujapo, mwanadamu hajui, na mambo yote yanabakia gizani, na Niondokapo, bado mwanadamu hafahamu. Nani anaweza kuwa na ushuhuda Kwangu? Inaweza kuwa sifa ya watu wa dunia? Inaweza kuwa mayungiyungi yanayochanua porini? Inaweza kuwa ndege wanaoruka angani? Inaweza kuwa simba wanaonguruma milimani? Hakuna anayeweza kunishuhudia kikamilifu. Hakuna anayeweza kufanya kazi Nitakayoifanya! Hata kama wangefanya kazi hii, ingekuwa na athari gani? Kila siku Naona vitendo vyote vya watu wengi, na kila siku Nachunguza mioyo na akili za watu wengi; hakuna aliyewahi kutoroka hukumu Yangu, na hakuna aliyewahi kuachana na uhalisi wa hukumu Yangu. Nasimama juu ya mawingu na kuangalia kwa umbali: Nimewaangamiza watu wengi, lakini pia watu wengi wanaishi katika huruma, na wema Wangu. Nyinyi pia hamuishi chini ya hali kama hizi?

Machi 5, 1992

Iliyotangulia: Wimbo wa Ufalme

Inayofuata: Sura ya 12

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp