Wimbo wa Ufalme

Umati unanishangilia, umati unanisifu; watu wote wanalitaja jina la Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanayainua macho yao kuviangalia vitendo Vyangu. Ufalme unashuka katika dunia ya wanadamu, nafsi Yangu ni ya fahari na yenye neema. Nani asingesherehekea kwa ajili ya hili? Ni nani asingecheza kwa ajili furaha? Ee Sayuni! Inua bendera yako ya ushindi unisherehekee! Imba wimbo wako wa ushindi ili ulieneze jina Langu takatifu! Viumbe wote hadi miisho ya dunia! Harakisheni kujitakasa ili muweze kufanywa kuwa sadaka Kwangu! Nyota juu mbinguni! Rudini kwenye maeneo yenu kwa haraka ili muonyeshe nguvu Yangu kuu katika anga! Nazisikiliza sauti za watu duniani, wanaomimina upendo na uchaji wao mwingi kwa ajili Yangu kwa nyimbo! Katika siku hii, huku viumbe wote wakirudishiwa uhai, Nashuka katika dunia ya wanadamu. Katika wakati huu, mambo yalivyo, maua yanachanua kwa wingi, ndege wote wanaimba kwa sauti moja, vitu vyote vinajawa na furaha! Kwa sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaanguka, ukiangamizwa katika mngurumo wa wimbo wa ufalme, usiinuke tena kamwe!

Nani duniani anathubutu kuinuka na kupinga? Ninaposhuka duniani Naleta moto, Naleta ghadhabu, Naleta maafa ya aina yote. Falme za dunia sasa ni ufalme Wangu! Juu angani, mawingu yanagaagaa na kujongea kama mawimbi; chini ya anga, maziwa na mito inatapakaa na kutoa muziki wa kusonga kwa furaha. Wanyama wanaopumzika wanaibuka kutoka kwenye matundu yao, na watu wote ambao wamelala wanaamshwa na Mimi. Siku ambayo watu wengi wameingojea hatimaye imefika! Wananiimbia nyimbo nzuri sana!

Katika wakati huu mzuri, katika wakati huu wa kusisimua,

sifa zinasikika kila mahali, juu mbinguni na chini duniani. Nani asingesisimka kwa ajili ya hili?

Ni moyo wa nani usingechamka? Ni nani asingelia kwa sababu ya tukio hili?

Anga si anga ya zamani, sasa ni anga ya ufalme.

Dunia si dunia ya awali, sasa ni nchi takatifu.

Baada ya mvua kubwa kupita, ulimwengu mchafu wa kale unafanywa upya kabisa.

Milima inabadilika … maji yanabadilika …

watu pia wanabadilika … vitu vyote vinabadilika….

Aa, milima iliyo mitulivu! Inukeni na mnichezee!

Aa, maji yaliyotuama! Endeleni kutiririka kwa wingi!

Ninyi wanadamu mnaoota ndoto! Jiinueni na mfuate!

Nimekuja … Mimi ni mfalme….

Wanadamu wote watauona uso Wangu kwa macho yao wenyewe, wataisikia sauti Yangu kwa masikio yao wenyewe,

watafurahia wenyewe maisha katika ufalme….

Matamu sana… mazuri sana….

Yasiyosahaulika … yasiyoweza kusahaulika….

Katika mwako wa hasira Yangu, joka kubwa jekundu linapambana;

katika hukumu Yangu adhimu, pepo wanaonyesha sura zao za kweli;

kwa maneno Yangu makali, watu wote wanaona aibu sana, na hawana popote pa kujificha.

Wanakumbuka zamani, jinsi walivyonidhihaki na kunikejeli.

Hakukuwahi kuwa na wakati ambapo hawakujiringa, hakukuwa kamwe na wakati ambapo hawakuniasi.

Leo, nani halii? Nani hahisi majuto?

Ulimwengu dunia wote umejawa machozi …

umejaa sauti za kushangilia … umejaa sauti za vicheko….

Furaha isiyoweza kufananishwa … furaha isiyo na kifani….

Mvua nyepesi inatarakanya … theluji nzito inaanguka….

Ndani ya watu, huzuni na furaha zinachanganyika … baadhi wakicheka …

baadhi wakilia … na baadhi wakishangilia….

Kana kwamba watu wote wamesahau … ikiwa haya ni majira ya kuchipua yaliyojaa mvua na mawingu,

majira ya joto yenye maua yanayochanua, majira ya kupukutika kwa majani yenye mavuno mengi,

au majira ya baridi yaliyo baridi kama barafu na jalidi, hakuna anayejua….

Angani mawingu yanaenda pepe, duniani bahari zinavurugwa.

Wana wanapunga mikono yao … watu wanasogeza miguu yao wakicheza….

Malaika wanafanya kazi … malaika wanachunga….

Watu wote duniani wanashughulika, na vitu vyote duniani vinazidishwa.

Iliyotangulia: Sura ya 10

Inayofuata: Sura ya 11

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp