Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Uzoefu Mbele ya Kiti cha Hukumu cha Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

82. Ukombozi wa Moyo

Na Zheng Xin, Marekani

Mnamo Oktoba 2016, mimi na mume wangu tulikubali wokovu wa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho tulipokuwa ng'ambo. Baada ya hapo, nilianza kuhudhuria mikutano mara kwa mara tukiwa na ndugu ili kusoma maneno ya Mungu, kushiriki uzoefu wetu na uelewa maneno Yake, na kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu. Nilihisi kwamba maisha kama hayo ya kanisani yalijaa furaha, na niliyafurahia sana.

Miezi michache ilipita kama kufumba na kufumbua macho na ndugu wote walikuwa wamekua maishani katika viwango tofauti tofauti. Hasa Dada Wang, ambaye alikuwa amemwamini Mungu kwa kipindi kifupi zaidi, lakini akawa na ukuaji wa kasi zaidi. Iwe ni katika maombi au kushiriki uzoefu na kuelewa kwake maneno ya Mungu, mambo haya aliyaweka kimatendo zaidi, na aliyaelewa vyema kuliko wengine wetu. Ushirika wake pia ulieleweka na aliufanya kwa utaratibu. ndugu wote walisema kuwa alikuwa na tabia bora na kwamba aliimarika haraka. Mwanzoni, nilipendezwa sana naye, na mara kwa mara ningewaambia ndugu zangu baada ya mkutano: “Zaidi ya ushirika wa Dada Wang kuwa wa wazi na unaofanywa kwa utaratibu, pia ana uelewa mzuri sana. Pia yeye huweza kutafuta mapenzi ya Mungu anapokumbana na jambo.” Lakini baada ya muda fulani, nilianza kuhisi hali ya kutoridhika. Niliwaza: “Mbona kila mtu anamsifu badala ya kunisifu mimi? Je, inawezekana kuwa sijakua kamwe? Kwani kuna jambo baya na ushirika wangu?” Polepole nilianza kutoridhishwa na Dada Wang, na nikaanza kumpinga kisiri. Niliwaza:"Unaweza kushiriki maneno ya Mungu, nami pia ninaweza kufanya hivyo. Siku itafika wakati ambapo nitamshinda.” Hata nilipanga hila: “Ninapaswa kuhifadhi uelewa na mwanga ninaopata kwa jumla kutokana na maneno ya Mungu na niushiriki tu nitakapokuwa kwenye mkutano na kila mtu. Kwa njia hiyo wote wataona kwamba hata mimi ninaweza pia kuelewa kazi Yake, na uelewa ninaoshiriki pia ni wa kiutendaji.” Kuanzia wakati huo kuendelea, ningesoma maneno ya Mungu kila mara nilipokuwa na nafasi na niliandika kwenye kijitabu kila kitu nilichopata, ambacho nilikuwa mimeelewa kutoka kwa maneno Yake. Ilipofika wakati wa mkutano, ningechunguzaa kwa makini nuru hii iliyokuwa ndani yangu ili kuona jinsi ambavyo ningeushiriki katika ushirika ambao ungekuwa wa wazi na uliopangwa, na ulio na utaratibu kama Dada Wang Sikujua ni kwa nini, lakini kadri nilivyotaka kujionyesha mbele ya ndugu, ndivyo nilivyoonekana mjinga. Mara ilipofika wakati wa ushirika wangu, sikuweza kuweka mawazo yangu wazi. Badala yake, maneno yangu yalitoka kwa kuvurugika. Singeweza kutaja kwa uwazi mambo niliyotaka kufafanua, na kila mkutano ulikuwa wa kunifedhehesha mno. Siku hizo chache nilikasirika na mawazo yangu yalinichanganya. Sikujihisi karibu na dada kama nilivyokuwa hapo awali. Polepole nikaanza kuhisi kwamba mikutano ilikuwa kama mfadhaiko kwangu, na singeweza kuweka moyo wangu huru.

Halafu siku moja, nikamwambia mume wangu yaliyokuwa yakinitendekea tulipokuwa tukipiga gumzo: “Siku za hivi karibuni nimeona kwamba katika mikutano, ushirika wa Dada Wang ni bora kuliko wangu. Nimejihisi mwenye wasiwasi mwingi …” Lakini kabla sijamaliza kuongea, mume wangu alifungua macho yake kwa upana na kuniambia kwa ukali sana: “Ushirika wa Dada Wang ni mzuri, na jambo hili liliturekebisha maadili. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwalo. Je, si hangaiko lako ni wivu tu?” Maneno yake yalikuwa kama kofi alilonipiga usoni. Nilitingisha kichwa changu haraka na kukana shutuma hiyo: “La, si hivyo. Mimi siko hivyo.” Halafu akasema: “ndugu zetu wote wamepata kitu kutokana na ushirika wa Dada Wang. Ikiwa unapatwa na wasiwasi unapousikia, je, si huo ni wivu kwamba ana uwezo mwingi kukuliko?” Maneno ya mume wangu yaliuchoma moyo wangu kwa mara nyingine. Nilifadhaika sana. Inawezekana kweli kuwa mimi ni mbaya jinsi hiyo? Nilijisi kukosewa sana na karibu nidondokwe na machozi. Nikamwambia: Usiseme zaidi. Hebu nitulie, na nitaliwaza mwenyewe. Baadaye, lililoshangaza ni kuwa mume wangu alimwambia Dada Liu, ambaye ni kiongozi katika kanisa, kuhusu yale yaliyokuwa yakinitendekea. Alitaka Dada Liu anisaidie. Nilimkemea kwa kuzungumza na Dada Liu bila kuniuliza kwanza. Nilihisi, ningejitokezaje kwa ndugu baada ya jambo hilo? Kama wangejua kuwa ninamwonea Dada Wang wivu si wangenidunisha? Kadri nilivyowaza kuhusu jambo hilo ndivyo nilivyoendelea kufadhaika, lakini kujitenga na uhalisia hakungesaidia chochote. Niliomba: “Ewe Mungu! Nifanye nini?”

Siku iliyofuata, nilikuwa nikichunguza yale niliyokuwa nimefichua katika kipindi hicho cha muda. ndugu kwa kawaida wangeshiriki yale waliyojifunza na kuelewa kutokana na kusoma maneno ya Mungu na watu wote wakati wowote, lakini nilibana nilichojifunza ili nikitoe wakati wa mikutano. Nilitaka kuzungumzia mambo ambayo watu wengine hawakuyajua ili ndugu waniheshimu. Nilipoona kwamba ndugu wengine walishiriki vyema kunishinda, niliingiwa na wasiwasi na kutaka kuwashinda. Nilikuwa nikidhani kuwa nilikuwa mtu mwenye uwezo wa kuingiliana kirahisi na watu wengine na sikulalamikia kila jambo dogo, kwamba nilikuwa mtu mzuri, mwenye moyo mwepesi. Lakini sikufikiria kwamba ninaweza kumwonea mtu wivu, na kwamba ningeweza hata kumpinga mtu mwingine na kushindana naye. Mbona nikawa kama mtu huyo? Kama saa sita adhuhuri, nilimpigia simu dada mmoja kumuuliza ikiwa aliwahi kuona wivu wakati wa mikutano aliposikia kuwa ushirika wa ndugu au dada wengine ulikuwa mzuri kuliko wake. Alisema hakuwahi kusikia hivyo. Pia alisema: “Kama ndugu zetu wanashiriki vizuri, hili ni jambo zuri na lenye kuadilisha kwetu. Mimi hupendezwa sana, na hunifanya nifurahi!” Nilihisi hata vibaya zaidi aliposema hivyo, na ni wakati huo tu nilipotambua kuwa nilikuwa na wivu mwingi ndani yangu. Nililia na kumwomba Mungu: “Ewe Mungu! Sitaki kuwa mtu mwenye wivu, lakini kila mara ninaposikia ushirika mzuri wa dada huyu, nashindwa kujizuia kumwonea wivu. Nimehisi kusumbuka na kufungwa na jambo hili siku nzima. Hakika sijui nifanyeje. Mungu! Naomba unisaidie kutupilia mbali pingu za wivu katika moyo wangu…” Baadaye, kiongozi wa kanisa Dada Liu alikuja kuniona. Alisoma vifungu kadhaa vya maneno ya Mungu ambavyo vilikuwa na ufaafu kwa hali yangu. “Wanadamu dhalimu, wakatili! Kufumba macho na kula njama, kusukumana, kung’ang’ania sifa na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Mungu Amezungumza maelfu na mamia ya maneno, ilhali hakuna hata mmoja ambaye amejifahamu. ... Ni wangapi wasiobagua na kuonea wengine wakiwa na nia ya kudumisha hali yao?” (kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili). “Watu wengine daima wana hofu kwamba wengine wataiba maarufu wao na kuwashinda, wakipata utambuzi ilhali wao wenyewe wanatelekezwa. Hili huwasababisha kuwashambulia na kuwatenga wengine. Je, huku si kuwaonea jicho wale walio na uwezo zaidi kuliko wao? Je, mwenendo kama huu si wa binafsi na wa kudharauliwa? Hii ni tabia ya aina gani? Ni ovu! Kujifikiria tu, kuridhisha tu tamaa zako mwenyewe, kutofikiria wajibu wa wengine, na kufikiria tu kuhusu maslahi yako mwenyewe” (Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Pia alishiriki kifungu kutoka Mahubiri na Ushirika Juu ya Kuingia Katika Maisha: “Kwa hivyo je, watu wanaowaonea wengine wivu ni wenye mawazo finyu? Kuna manufaa yoyote ya kuwa mtu aliye na mawazo finyu na mwenye wivu? Hakuna manufaa hata moja. Ni watu wanaoshughulishwa na mambo madogo, wenye mawazo finyu na waovu na watu huwaona kama mzaha. Hawafai kuishi. Ufinyu wa mawazo si mzuri, na hilo ni wazi. Watu wengine husema: ‘Wakati mwingine hatuwezi kuuondoa. Mara tu tunapokumbana na mtu bora kutushinda, tunamwonea wivu na kukasirika. Mara tu ninapomwona mtu huyo, hata hujihisi kama siwezi kuendelea kuishi. Ninaweza kufanya nini ninapokumbana na jambo hili?’ Kwani huwezi kumwomba Mungu na kujilaani? Na unapaswa kuomba vipi? Unasema: ‘Siwezi kumstahimili mtu mwingine akiwa bora kunishinda. Mimi ni mtu wa aina gani? Mtu kama mimi hapaswi kuishi. Ninaingiwa na wivu kila mara ninapomwona mtu mwngine akiwa bora kunishinda. Huu ni moyo wa aina gani? Huu si ubinadamu wa kawaida. Mungu aniadhibu na anipogoe.’ Baada ya hapo, sema omba lifuatalo: ‘Mungu nakusihi uniokoe kutokana na ufinyu wangu wa mawazo, unifanye niwe mkarimu zaidi katika roho, niishi kama binadamu ili Usiaibike kwa sababu yangu.’ Hivyo ndivyo unavyopaswa kuomba. Baada ya kuomba kama hivyo kwa muda, kabla hujajua huenda utakuwa mkarimu zaidi katika roho. Mara nyingine utakapokutana na mtu ambaye ana uwezo mwingi kukushinda, hutahisi wivu mwingi sana. Utaweza kukubali na kuingiliana nao kwa kawaida. Muda utakavyopita, hili litakuwa sawa. Mara tu utakapokuwa na ubinadamu wa kawaida, utaweza kuishi kwa furaha, bila kujali na kwa wepesi. Mtu mwenye mawazo finyu huishi kwa mfadhaiko, kwa uchungu na uchovu.” kutoka kwa Mahubiri na Ushirika Juu ya Kuingia Katika Maisha Nilichomwa moyo wangu niliposoma ushirika huu. Hiyo ilikuwa hali yangu mwenyewe! Ushirika wa Dada Wang ulikuwa wa kutia nuru, lakini sikupata maarifa yoyote kutokana nao. Kinyume chake ni kuwa ili kulinda majivuno yangu mwenyewe, niliendelea kuishi katika hali hiyo ya kushindana na Dada Wang. Nilimpinga na kutafakari namna za kushiriki ushirika bora kushinda wake. Hata kwa kweli nilitumai kusiwe na mtu yeyote atakayesema jambo lolote zuri kumhusu wala kushangilia ushirika wake. Wakati ambapo ushirika wangu haukuwa mzuri, wakati singeweza kujionyesha na nikaishia kujiaibisha, akili yangu ilinichanganya, na nikawa na uchungu na kufadhaika. Nilitumia siku nzima kwenye shauku zangu, hofu nikiogopa kwamba watu wengine wangenidunisha. Nilikuwa na mawazo finyu sana. Nilichowaza tu ni kuweza kuonekana bora zaidi, lakini singeweza kustahimili mtu mwingine kuwa bora kunishinda. Je, si huo ni wivu, kijicho kwa wale wanaofanikiwa? Hakuna ubinadamu wa kawaida katika jambo hilo! Nikirejesha mawazo nyuma, nilikuwa hivyo pia kabla ya kumwamini Mungu. Nilipokuwa nikitangamana na marafiki na jamaa zangu, majirani na wenzangu, kila mara niliwaza kuhusu watu wengine wakizungumza mema kunihusu. Wakati mwingine mwenzangu alipomsifu mtu mwingine mbele yangu, ningeingiwa na wasiwasi na ili kuwafanya watu wengine wanisifu, ningejaribu kufanya kazi yangu vizuri, na nilifurahia kuifanya licha ya ugumu wake au namna ilivyochokesha. Ni sasa tu ambapo nimetambua kwamba wakati wote hizo zilikuwa ishara za tabia mbovu za kishetani Nilipotambua hivyo, Dada Liu kwa mara nyingine akahusisha tabia hii na kifungu cha ushirika na akanielekeza kwa njia ya matendo. Yaani kuja kwa Mungu na kumwomba Yeye, kumweleza Mungu mambo yanayonitatiza na ubovu ninaoufichua ili Anisaidie niwe mtu mwenye roho karimu. Baada ya hapo, nilikuja mbele ya Mungu mara kwa mara na kumwomba kuhusu mambo yaliyonitatiza. Nilianza pia kusoma kwa ufahamu maneno zaidi ya Mungu akihukumu na kudhihirisha tabia za mwanadamu. Nilipopata uelewa, na nuru kutoka kwa maneno ya Mungu, ningeyashiriki na ndugu zangu wakati wowote. Wao pia walizungumza kuhusu yale waliyoyapata na kuyaelewa. Sikuwahi kufikiria, lakini mazoea kama haya yaliniruhusu kupata hata zaidi ya kusoma maneno ya Mungu mimi mwenyewe. Katika mikutano, nilishiriki katika ushirika kulingana na yale niliyoyaelewa, na nililenga kutuliza moyo wangu na kusikiliza ushirika wa wengine. Ni kupitia utendaji kama huu pekee ambapo nilipata kujua kuwa wakati ndugu zangu walipokuwa na uwezo wa kuzungumzia uzoefu na ushuhuda wao wa kutenda kama yalivyosema maneno ya Mungu, mimi pia nilipata kurekebika kitabia kwa njia kubwa. Baada ya muda wa mazoea kama haya, wivu wangu ulipungua kuliko ulivyokuwa, lakini katika kila mkutano, nilipoona kwamba ndugu wengine walisifu sana ushirika wa Dada Wang, bado singejizuia bali nilihisi wivu kidogo. Kila wakati nilihisi umbali fulani baina yangu na yeye, na singeweza kuingiliana naye kikawaida. Wakati nikiishi katika hali hiyo, sikudhubutu kuwaambia ndugu zangu kwa uwazi. Nilihofia kwamba kama ningewaambia, wangenidunisha. Kwa hivyo, katika mikutano kadhaa, sikuweza kunasua moyo wangu. Niliomwomba tu Mungu kuhusu matatizo yangu: “Ewe Mungu! Kwa mara nyingine leo niko katika hali isiyofaa. Naomba Uniongoze…”

Jioni moja, Dada Liu alinipigia simu. Aliniuliza kwa wasiwasi ikiwa nilikuwa na matatizo siku za hivi karibuni. Nilijibu pasi kuwa dhahiri: “Ubovu wangu ni mwingi sana. Je, inawezekana kwamba Mungu hamwokoi mtu kama mimi?” Nilihofia kwamba huenda angenidharau, kwa hivyo sikusema kitu kingine chochote baadaye. Dada Liu akanisomea kifungu cha maneno ya Mungu: “‘sitawaambia wengine kuhusu upande wangu mwovu ama mpotovu, siyo?’ Iwapo huzungumzi mambo haya, na hujichambui, basi hutawahi kujijua, na hutawahi kujua wewe ni kitu cha aina gani, na hakutakuwa na uwezekano wa wengine kukuamini. Huu ni ukweli. Iwapo unawataka wengine wakuamini, kwanza lazima uwe mwaminifu. Kuwa mwaminifu, lazima kwanza uuweke wazi moyo wako, ili kila mtu aweze kuuona, na vyote unavyofikiri, na wanaweza kuona uso wako wa kweli; hupaswi kujifanya ama kujionyesha usivyo” (Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Baada ya kusoma maneno hayo kutoka kwa Mungu, alishiriki katika ushiika: Kuongea kwa uwazi na kushiriki katika ushirika ni mojawapo ya njia za kuweka moyo huru. Tukificha matatizo yetu kwenye mioyo yetu, tutachezewa kwa urahisi na Shetani na maisha yetu yataathirika. Kuongea kwa uwazi na kuleta mambo hadharani ndio kuweka ukweli katika vitendo, na kuwa mtu mkweli. Halafu pia tunaweza kupata msaada kutoka kwa ndugu zetu. Hii huruhusu matatizo yetu kutatuliwa haraka zaidi. Tutapata ukuaji katika maisha yetu na mioyo yetu itakombolewa. Si hilo ni jambo zuri?” Baada ya kusikiliza ushirika wa Dada Liu, nilipata ujasiri na nikamwambia yale niliyokuwa nikipitia. Daima singedhani kuwa baada ya kunisikiliza, hakungekuwa na chembe ya yeye kunidunisha wala kunidharau, bali alishiriki nami uzoefu wake bila haraka. Aliniambia jinsi alivyokuwa mwenye wivu hapo awali, na jinsi alivyojinasua kutokana nao. Nilishangaa sana baada ya kusikia ushirika wake. Niliwaza: “Kwa hivyo hata wewe ulikuwa na ubovu kama huu!” Dada Liu alisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu kilichohusiana na hali yangu: “Watu ambao Mungu anaokoa wana tabia potovu; walipotoshwa na Shetani, na hawakosi dosari au si wanadamu wakamilifu, wala hawaishi katika ombwe. Kwa hiyo, watu wengine wanapofikiria, ‘Nilimpinga Mungu tena. Je, hilo halimaanishi kwamba mambo yangu yamekwisha? Siwezi kupata wokovu; nimekata tamaa kuhusu mimi mwenyewe, kwa hiyo Mungu kwa hakika amekata tamaa kunihusu pia,’ unafikiria nini kuhusu mtazamo huu? Je, huu si ufahamu uliokosea kuhusu Mungu? Huku kunaitwa kumwelewa Mungu visivyo. Kuwa hasi sana si sahihi; unajiacha wazi sana kwa Shetani kukudanganya. Shetani atakuwa amefaulu wakati huo. Hupaswi kukata tamaa!” (kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kisha akashiriki katika ushirika: “Sisi wote ni watu waliotiwa ubovu mwingi na Shetani. Kiburi, udanganyifu, ubinafsi, kuonea wengine wivu—tabia hizi zote mbovu zimejikita kwelikweli kwa watu wengi. Mungu sasa amekuja kufanya kazi ya kuhukumu na kuadhibu ili kututakasa na kutubadilisha. Lazima tujishughulikie vizuri, na tusiishi kwa uhasi na kutoelewana. Mradi tunatafuta ukweli kwa nia, tunakubali hukumu na adhabu ya maneno ya Mungu, tunawaza kwa makini na kuelewa tabia zetu mbovu kulingana na maneno ya Mungu, na kuunyima mwili na kuweka ukweli katika utendaji, siku itafika wakati ambapo tutabadilishwa tabia zetu, na tutaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu halisi.” Moyo wangu ulihisi huru sana baada ya kusikiliza ushirika wa Dada Liu, na nilielewa mapenzi ya Mungu pia. Licha ya kukabiliana vyema na ubovu wangu, na kulenga kujijua na kutafuta ukweli kutatua tabia zangu mbovu, pia ninapaswa kutenda kama mtu mkweli na kuelezea yanayonikumba kwa ndugu kuhusu ubovu niliokuwa nao wakati huo wote. Jambo hili lingemnyima Shetani nafasi ya kufanya kazi yake na vilevile ingekuwa kumwaibisha Shetani kupitia kutenda mambo ya ukweli. Dada Liu alikuja nyumbani kwangu tena siku iliyofuata na tukasoma pamoja kifungu kutoka kwenye maneno ya Mungu: “mara tu inapogusia cheo, sura au sifa, moyo wa kila mtu huruka kwa matazamio, na kila mmoja wenu daima hutaka kujitokeza, kuwa maarufu, na kutambuliwa. Kila mtu hayuko radhi kushindwa, bali daima ku hata ingawa kupinga kunaleta fedheha na hakukubaliwi katika nyumba ya Mungu. Hata hivyo, bila kupinga, bado huridhiki. Unapomwona mtu fulani akitokeza, unahisi wivu, chuki, na kuwa hiyo si haki. “Mbona nisitokeze? Mbona kila mara ni mtu huyo anayetokeza, na hauwi wakati wangu kamwe?” Kisha unahisi chuki fulani. Unajaribu kuizuia, lakini huwezi, kwa hiyo unaomba. Baada ya kumaliza kuomba, unahisi nafuu kwa muda mfupi, lakini baadaye unapokutana na jambo hili tena, huwezi kulishinda. Je, hii si hali ya kimo kichanga? Je, si mtu kuanguka katika hali hizi ni mtego? Hizi ndizo pingu za asili potovu ya Shetani ambazo huwafunga wanadamu. ... Lazima ujifunze kuacha na kuweka kando vitu hivi, kushindwa, kuwapendekeza wengine, na kuwaruhusu wengine kutokeza. Using’ang’ane vikali au kukimbilia kujinufaisha punde unapopata nafasi ya kutokeza au kupata utukufu. Lazima ujifunze kujiondoa, lakini hupaswi kuchelewesha utekelezaji wa wajibu wako. Kuwa mtu anayefanya kazi kwa ukimya bila kuonekana, na ambaye hajionyeshi kwa wenigne unapotekeleza wajibu wako. Kadiri unavyoacha na kuweka kando, ndivyo utakavyokuwa mwenye amani zaidi, na ndivyo nafasi itakavyofunguka zaidi ndani ya moyo wako na ndivyo hali yako itakuwa bora zaidi. Kadiri unavyong’ang’ana na kushindana zaidi, ndivyo hali yako itakuwa mbaya zaidi. Ikiwa huamini hili, jaribu na uone! Ikiwa unataka kugeuza hali hii, na usidhibitwe na vitu hivi, basi lazima uviweke kando kwanza na kuviacha. Vinginevyo, kadiri unavyong’ang’ana, ndivyo giza litakuzingira zaidi, na ndivyo utakavyohisi wivu na chuki, na hamu yako ya kupata itaongezeka na kuongezeka tu. Kadiri hamu yako ya kupata ilivyo kuu, ndivyo utakaavyopunguza kuweza kufanya hivyo, na unapopata kidogo chuki yako itaongezeka. Chuki yako inapoongezeka, utakuwa mbaya zaidi. Kadiri ulivyo mbaya ndani yako, ndivyo utakavyotekeleza wajibu wako vibaya zaidi; kadri unavyotekeleza wajibu wako vibaya, ndivyo utakuwa mwenye manufaa kigogo zaidi. Huu ni mzunguko mwovu uliofungamana” (Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, basi alilihusisha na uzoefu wake mwenyewe na akashiriki kuhusu chanzo cha wivu wa watu. Ni wakati huo tu nilipotambua kwamba haya yote yalitokea kwa sababu hamu yangu binafsi ya kuwa na jina na hadhi ilikuwa kubwa sana, na nilikuwa na kiburi kingi. Nikiwa nimejawa na tabia hizi mbovu, tamaa ya makuu na ushari wangu zilikuwa kubwa, na licha ya jnilichofanya, nilitaka kuwa tu juu ya wengine. Nilikuwa hivyo nilipokuwa sehemu ya jamii, na nilikuwa vivyo hivyo nikiwa kanisani. Hata katika mikutano, ushirika na maombi, bado nilikuwa nikifikiria kuwa bora kuliko watu wengine, na nilifurahi tu ikiwa watu wengine walinisifu. Mara tu mtu mwingine alipokuwa bora kunishinda, nilishindwa kukubali na nilimwonea wivu. Nilikuwa muasi na kufanya kazi kupinga jambo hilo. Wakati sikuweza kulishinda kabisa, niliishi tu katika uhasi na singeweza kujikubali vizuri. Hata nilishindwa kumwelewa Mungu na nikaamini kuwa singekuwa mlengwa wa wokovu wa Mungu. Niliona kwamba ubovu wa Shetani ulikuwa umenifanya mwenye kiburi, dhaifu, mbinafsi na mwenye kustahili dharau na maisha yangu yakawa yenye taabu kupindukia Nilipata njia ya kutenda kutokana na maneno ya Mungu. Lazima nijifunze kukubali kushindwa, kuweka mambo kando na kwenda kinyume na tamaa za mwili wangu kulingana na mahitaji ya Mungu, na kujifunza zaidi kutokana ustadi wa dada yangu, na kufidia udhaifu wa kila mmoja wetu. Haya tu ndiyo mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo njia ya pekee ya kuelewa na kupata ukweli zaidi. Baada ya hapo, Dada Liu alisoma kifungu kingine kutoka kwenye maneno ya Mungu: “Shughuli si za aina moja. Kuna mwili mmoja. Kila mmoja hufanya kazi yake, kila mmoja kwa nafasi yake na kufanya kadiri ya uwezo wake—kila cheche ya shauku mwako wa mwanga—kutafuta ukomavu katika maisha. Ni hivyo ndivyo nitakavyoridhika” (“Sura ya 23” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma maneno haya kutoka kwa Mungu, nilielewa kwamba uhodari na zawadi ambazo mungu hutupa ni tofauti kwa kila mtu. Lakini bila kujali ni uhadari au zawadi zipi, zinapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kushuhudia na kumtukuza Mungu. Ilikuwa imeamuriwa na Mungu kwamba Dada Wang ni wa tabia nzuri, na kwamba anaelewa ukweli haraka. Ninapaswa kushughulikia hili vyema, na pia ninapaswa kushughulikia vyema uwezo na udhaifu wangu mwenyewe kwa sababu alivyotupa kila mmoja wetu ni vitu bora zaidi. Haijalishi ni hulka gani ameamuru niwe nayo, lazima nitii sheria Yake, na mipango Yake, na nirekebishe nia zangu, na nitafute ukweli kwa moyo wangu wote. Nitashiriki lile nililo wazi nalo- bila kuzidisha wala kupunguza. Nitatenda yale ninayoyaelewa - bila kuzidisha wala kupunguza. Lazima nifanye kila linalowezekna mbele ya Mungu ili Afarijike na ridhike - hili tu ndilo linaloweza kuwa na maana Ndilo jambo ambalo mimi pia ninapaswa kutafuta. Ili kufikia hili, ninaazimia kufanya yafuatayo mbele ya Mungu: Kuanzia sasa kuendelea, niko tayari kufanya juhudi za kufuata ukweli, kujitenga na tabia za kishetani zenye kiburi na ubinafsi, na kuishi katika mfano wa binadamu wa kweli wa kumridhisha Mungu.

Mkutano mwingine wa kanisa ulifika haraka sana. Nilitaka kuzungumzia na kuwa mkweli kwa Dada Wang kuhusu ubovu ambao nilikuwa nimefichua kuhusu wivu wangu kwake katika kipindi hicho cha muda, lakini pindi tu nilipowaza kuhusu namna ambavyo angeniona baada ya kujua kwamba nilikuwa nimefichua ubovu mwingi sana, sikudhubutu kufanya hivyo. Ndani yangu nilimwonba Mungu kimya kimya: “Ewe Mungu! Naomba unipe imani na ujasiri. Niko tayari kuweka majivuno yangu kando na kushiriki katika ushirika na dada yangu kwa uwazi, ili kuvunja kilicho baina yetu.” Baada ya kuomba, nilihisi amani zaidi katika moyo wangu, halafu nikasema kila kitu kuhusu hali na uzoefu wangu katika kipindi hicho cha muda. Matokeo yalikuwa kwamba licha ya ndugu zangu kuacha kunidunisha, wote walinienzi ujasiri wangu katika kuwa mtu msema ukweli. Pia walisema kuwa kutokana na uzoefu wangu, walitambua kwamba ni kupitia kutenda kulingana na maneno ya Mungu ndipo waliweza kutupilia mbali tabia zao za kishetani na kupata kuachiliwa na kuwa huru, na kisha walijua namna ya kukabiliana na jambo kama hilo ikiwa wangekumbana nalo. Katika mikutano ya siku za baadaye, nilisikiliza ushirika wa dada yangu kwa moyo na nikagundua uwezo wake mwingi. Niliona kwamba alipokumbana na mambo, aliweza kulenga kuja mbele ya Mungu na kutafuta ukweli, na kutafuta njia ya kutenda kutoka kwenye maneno ya Mungu. Haya yote yalikuwa mambo ambayo nilihitaji kujifunza kutokana nayo. Ni wakati huo tu ambapo kwa hakika nilelewa kwamba kuwa na uwezo wa kusikiliza uzoefu na ushuhuda wa kuweka katika vitendo kama yalivyosema maneno ya Mungu ulioshirikiwa na ndugu katika kila mkutano ilikuwa nafasi nzuri zaidi ya ukuaji katika maisha. Mungu alipanga dada huyu awe karibu nami. Alishiriki kuhusu mambo ambayo hayakuwa wazi kwangu, na alifidia barabara kile nilichokosa. Hii ni baraka kutoka kwa Mungu! Nilipolifikiria kwa njia hiyo, nilihisi kuachiliwa kabisa katika moyo wangu. Kupitia kudhihirishwa kupitia ukweli, na hukumu na adhabu ya maneno ya Mungu, tabia yangu mbovu ya kuonea wengine wivu ilipata mabadiliko fulani, na nilianza kupata uelewa wa juu juu wa tabia Yake ya haki. Pia nilipata kujua kuwa maneno ya Mungu kwa kweli yanaweza kusafisha, kubadilisha na kumwokoa mwanadamu. Maneno ya Mungu yanaweza kuwa maisha ya mtu na yanaweza kutatua matatizo yetu yote na uchungu wa wanadamu. Niko tayari kuweka katika vitendo maneno ya Mungu yalivyosema, na kutii hukumu na adhabu Yake. Naomba hivi karibuni nitakaswe na Mungu, niishi kwa mfano wa binadamu wa kweli na nipate sifa Zake.

Iliyotangulia:Kupitia kwa Majonzi Makuu, Nimevuna Faida Kubwa

Inayofuata:Hatimaye Naishi kwa Kudhihirisha Kiasi Kama Mwanadamu

Maudhui Yanayohusiana

 • Sababu ya Kweli ya Kazi Isiyofaa

  Xinyi Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi Katika ziara zangu za karibuni kwa makanisa, mara nyingi niliwasikia viongozi na wafanyakazi wakisema kwamba watu …

 • Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu

  Ilikuwa ni katika ufunuo wa Mungu ambapo hatimaye nilitambua asili yangu ya kishetani ya kiburi na hali ya kutojali: sikuwa na chembe ya uchaji mbele ya Mungu. Niligundua wakati huo huo kwamba mawazo ya mwanadamu ni shimo la maji ya kunuka. Njia yangu “iliyofanywa kwa werevu”, bila kujali ni nzuri kiasi gani, ilikuwa matakwa ya Shetani, na ingeweza tu kumchukiza Mungu. Ingeweza tu kumkosea Yeye na kuvuruga kazi Yake.

 • Si Rahisi Kwako kwa Hakika Kujijua Mwenyewe

  Zhang Rui Mji wa Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang Niliona katika maneno ya Mungu kwamba Mungu anawapenda watu waaminifu na anawachukia watu wadanganyifu, n…

 • Jitiishe Mwenyewe ili Kufundisha Wengine Nidhamu

  Xiaoyan Jiji la Xinyang, Mkoa wa Henan Nilikuwa na ubia wa kazi wa karibu na dada mmoja mzee katika masuala ya jumla. Baada ya kufanya kazi naye kwa …