Sura ya 10

Enzi ya Ufalme ni, hata hivyo, tofauti na nyakati za kale. Haihusu jinsi ambavyo binadamu hutenda; badala yake, Nimeshuka duniani ili Nitekeleze kazi Yangu binafsi, jambo ambalo wanadamu hawawezi kuelewa wala kufanikisha. Kwa miaka mingi sana, tangu kuumbwa kwa ulimwengu, kazi imekuwa tu kuhusu kujenga kanisa, lakini hakuna mtu anayesikia kamwe kuhusu kujenga ufalme. Japokuwa Nazungumza kuhusu haya kwa kinywa Changu mwenyewe, yupo yeyote anayejua asili yake? Wakati mmoja Nilishuka kwenye ulimwengu wa binadamu Nikapitia na Nikaangalia kwa makini mateso yao lakini nilifanya hivyo bila ya kutimiza lengo la kupata mwili Kwangu. Punde ujenzi wa ufalme ulipoanza, Mimi nikiwa mwili nilianza rasmi kutekeleza huduma Yangu; yaani, Mfalme wa ufalme rasmi Alichukua ukuu wa mamlaka Yake makuu. Kutokana na hili ni dhahiri kwamba mshuko wa ufalme katika ulimwengu wa binadamu—mbali na kuwa tu suala la maonyesho ya moja kwa moja—ni wa ukweli halisi; hiki ni kipengele mojawapo cha maana ya “uhalisi wa kutenda.” Wanadamu hawajawahi kuona hata mojawapo ya matendo Yangu, wala hawajawahi kusikia hata mojawapo ya matamshi Yangu. Hata kama angekuwa ameona, yeye angegundua nini? Na kama angenisikia Nikiongea, yeye angeelewa nini? Kotekote katika ulimwengu, binadamu wote hukaa chini ya upendo Wangu, huruma Yangu, lakini pia binadamu wote hukaa chini ya hukumu Yangu, na vivyo hivyo chini ya majaribio Yangu. Nimekuwa mwenye huruma na upendo kwa wanadamu, hata wakati watu wote walikuwa wamepotoshwa kwa kiwango fulani; Nimegawa kuadibu kwa wanadamu, hata wakati watu wote walinyenyekea mbele ya kiti Changu cha enzi. Lakini, yupo binadamu yeyote ambaye hayuko katikati ya mateso na usafishaji Niliotuma? Ni watu wangapi wanapapasa kwenye giza kutafuta mwangaza, ni wangapi wanajitahidi kwa uchungu kupitia kwa majaribio yao? Ayubu alikuwa na imani, na hata hivyo, kwa hayo yote, hakuwa anajitafutia njia yake mwenyewe? Ingawa ninyi watu Wangu mnaweza kusimama imara katika majaribio, kunaye yeyote ambaye, bila kuongea kwa sauti, anaamini katika moyo wake? Je, si anaona ni afadhali kuongea kuhusu imani yake ilhali anaishuku moyoni mwake? Hakuna binadamu ambao wamesimama imara katika majaribio, ambao wanatoa utiifu wa kweli katika majaribio. Kama Singefunika uso Wangu ili kuepuka kuangalia dunia hii, jamii nzima ya binadamu ingeporomoka chini ya macho Yangu ya kuchoma, kwa maana Siulizi chochote kutoka kwa binadamu.

Wakati saluti kwa ufalme inapolia—ambao pia ni wakati sauti saba za radi zinanguruma—sauti hii inatetemesha mbingu na dunia, inatetemesha mbingu na kusababisha mishipa ya moyo wa kila binadamu kutetemeka. Wimbo wa taifa kwa ufalme unainuka kwa shangwe katika taifa la joka kuu jekundu, kuthibitisha kwamba Nimeliangamiza taifa la joka kuu jekundu na kisha kuanzisha ufalme Wangu. Hata la muhimu zaidi, ufalme Wangu unaanzishwa duniani. Wakati huu, Naanza kutuma malaika Wangu kwa kila mtu wa mataifa ya dunia ili waweze kuwachunga wanangu, watu Wangu; hili pia ni kukidhi mahitaji ya hatua ya pili ya kazi Yangu. Lakini Mimi binafsi Naenda mahali ambapo joka kuu jekundu limelala likiwa limejizongomeza, Nipigane nalo. Na wakati binadamu wote wanapata kunijua Mimi kutoka ndani ya mwili, na kuweza kuyaona matendo Yangu kutoka ndani ya mwili, wakati huo makazi ya joka kuu jekundu yatageuzwa kuwa jivu na kutoweka yasipatikane tena. Kama watu wa ufalme Wangu, kwa kuwa unalichukia joka kuu jekundu katika mifupa yako, ni lazima uuridhishe moyo Wangu na matendo yako na kwa njia hii uweze kuleta aibu juu ya joka. Je, unahisi kwamba joka kuu jekundu ni lenye chuki? Je, unahisi kweli kwamba yeye ndiye adui wa Mfalme wa ufalme? Je, una imani kwa kweli kwamba unaweza kuwa na ushuhuda wa ajabu Kwangu? Je, una imani kwa kweli ya kumshinda joka kuu jekundu? Haya ndiyo Ninayotaka kutoka kwako. Yote Ninayohitaji kutoka kwako ni kwamba uweze kufika mpaka hatua hii; je, utaweza kufanya hili? Je, una imani kwamba unaweza kufikia hili? Binadamu ana uwezo wa kufanya nini? Si ni afadhali Nifanye hivyo Mwenyewe? Mbona Ninasema kwamba Mimi binafsi Nateremka mahali ambapo vita hujiunga? Ninachotaka ni imani yako, sio matendo yako. Wanadamu hawana uwezo wa kupokea maneno Yangu kwa halisi, lakini wanachungulia tu kutoka kando. Na wewe umefikia malengo haya kwa njia hii? Umekuja kunijua kwa njia hii? Kwa kusema ukweli, kati ya wanadamu walio duniani, hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuniangalia Mimi moja kwa moja usoni, hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kupokea maana safi na nadhifu ya maneno Yangu. Na kwa hiyo Nimeweka mwendo wa kufaa usiokuwa wa kawaida wa kupanga mambo juu ya dunia, ili kufikia lengo Langu na kuanzisha mfano halisi Wangu mwenyewe katika mioyo ya watu, na kwa njia hii kutamatisha kipindi ambapo fikira huwa na mamlaka juu ya wanadamu.

Leo hii, Sishuki tu juu ya taifa la joka kuu jekundu, Mimi pia Nageuza uso Wangu kuelekea ulimwengu mzima, mpaka kila kitu cha mbingu kinatetemeka. Kunayo sehemu hata moja isiyopitia hukumu Yangu? Kunayo sehemu isiyo chini ya mateso Ninayovurumisha kuelekea chini? Kila Ninapoenda Nimesambaza “mbegu za maafa” ya kila aina. Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo. Nataka kufanya hata watu zaidi wapate kunijua Mimi, waweze kuniona Mimi, na kwa njia hii wapate kumcha Mungu ambaye wao hawajamwona kwa miaka mingi sana lakini ambaye, leo hii, ni halisi. Ni kwa sababu gani Niliumba dunia? Kwa sababu gani, wakati mwanadamu alipogeuka na kuwa mpotovu, Sikumwangamiza kabisa? Kwa sababu gani jamii ya wanadamu inaishi chini ya mateso? Ni kwa sababu gani Mimi Mwenyewe Niliuvaa mwili? Wakati Mimi Natekeleza kazi Yangu, binadamu haujui tu ladha ya uchungu pekee bali pia ya utamu. Kati ya watu wa dunia, ni nani asiyeishi ndani ya neema Yangu? Je, kama Sikuwapa wanadamu baraka yakinifu, nani angeweza kufurahia utoshelevu katika ulimwengu? Hakika, kuwaruhusu kuchukua nafasi kama watu Wangu si baraka pekee Niliyowapa, sivyo? Na kama msingekuwa watu Wangu na badala yake muwe watendaji-huduma, hamngekuwa mnaishi ndani ya baraka Zangu? Hapana mmoja kati yenu anayeweza kuelewa asili ya maneno Yangu. Binadamu—mbali na kuthamini vyeo ambavyo Nimeweka juu yao, wengi wao, kwa sababu ya jina “watendaji-huduma,” wanaweka chuki katika nyoyo zao, na wengi sana, kwa sababu ya jina “watu Wangu,” huzalisha upendo Kwangu katika nyoyo zao. Hakuna anayepaswa kujaribu kunidanganya; macho Yangu huona kila kitu! Ni nani kati yenu hupokea kwa hiari, ni nani kati yenu hunipa utiifu kamilifu? Kama saluti kwa ufalme haingelia, je ungeweza kutii mpaka mwisho? Kile ambacho mwanadamu ana uwezo wa kufanya, kufikiria, anaweza kwenda umbali gani—haya yote Nimeyaamua kabla tangu kitambo.

Idadi kubwa ya watu hukubali moto Wangu katika mwanga wa uso Wangu. Idadi kubwa ya watu, wakitiwa moyo na kutumainisha Kwangu, hujiamsha wenyewe kusonga mbele katika ukimbizaji. Wakati majeshi ya Shetani hushambulia watu Wangu, Mimi Niko pale kuwakinga dhidi yao; wakati mipango ya Shetani inaleta madhara katika maisha ya watu Wangu, Nampiga akimbie kwa kujiuzulu, na asiweze kurudi tena. Duniani, kila aina ya pepo wanazungukazunguka bila mwisho wakitafuta mahali pa kupumzika, na bila kukoma wanatafuta maiti za wanadamu zinazoweza kuliwa. Watu Wangu! Lazima mbaki ndani ya utunzaji Wangu na ulinzi. Kamwe msiwahi kuishi katika hali ya upotovu! Msiwahi tenda mambo kiholela! Badala yake, salimisha uaminifu wako katika nyumba Yangu, na ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kupinga hila ya Shetani. Katika hali yoyote usiishi kama ilivyokuwa katika siku za awali, kufanya jambo moja mbele Yangu na jingine nyuma Yangu—ukifanya hivyo umeshapita kiwango cha kukombolewa. Hakika Nimetamka zaidi ya kiasi cha kutosha maneno ya aina hii, sivyo? Ni kwa sababu asili ya mwanadamu ya zamani hairekebiki ndiyo maana Nimemkumbusha tena na tena. Usichoke! Haya yote Niyasemayo ni kwa mujibu wa kuhakikisha hatima yako! Kile Shetani anahitaji kwa hakika ni uchafu na pahali pabaya; na kadri unavyokosa kuokoleka kabisa, na kadri unavyokuwa mpotovu, ukikataa kujiwasilisha kwa hali ya kujizuia, ndivyo roho wachafu watakavyotumia nafasi yoyote ya kupenyeza. Mara unapowasili katika hii nafasi, uaminifu wako utakuwa kelele tupu, bila uhalisi wowote, na azimio lako litaliwa na pepo wachafu, kugeuzwa kuwa uasi au hila za Shetani, na kutumiwa kuzuia kazi Yangu. Kuanzia hapo, unaweza kupigwa na Mimi wakati wowote. Hakuna anayeelewa uzito wa hali hii; watu wote hupuuza tu yale wanayosikia na hawachukui tahadhari kwa vyovyote. Sikumbuki kile kilichofanywa katika siku za nyuma. Je, bado unasubiri Niwe mpole kwako Nisahau kwa mara nyingine tena? Ingawa binadamu umenipinga Mimi, Sitashikilia lolote dhidi yake, kwa maana kimo cha mwanadamu ni kidogo mno, na kwa hiyo Sihitaji makubwa kwake. Yote Ninayotaka ni kwamba yeye asijitumie mwenyewe kwa ubadhirifu, na ajiwasilishe kwa kujizuia. Hakika si zaidi ya uwezo wako kufikia sharti hili moja? Wengi wa watu wanasubiri Nifichue mafumbo zaidi ili walishe macho yao. Ilhali, iwapo utakuja kuelewa siri zote za mbinguni, je, ni nini utakalofanya na hayo maarifa? Je, yataweza kuongeza upendo wako Kwangu? Je, yatachochea upendo wako Kwangu? Mimi Simdharau mwanadamu, wala kukata kauli kwa wepesi juu yake. Kama hizi hazingekuwa hali halisi za mwanadamu, Mimi kamwe Singewahi kamwe kuwavisha watu taji na vitambulisho hivi kwa kawaida. Fikiria kuhusu siku za nyuma: Kumekuwepo na nyakati zozote ambazo Nimewahi kuwakashifu nyinyi? Nyakati zozote ambazo Niliwadharau nyinyi? Nyakati zozote ambazo Nimekutazama bila kuzingatia hali zako halisi? Nyakati zozote ambazo Nilichosema kilishindwa kujaza moyo wako na kinywa chako na kusadiki? Nyakati zozote ambazo Nimenena bila ya kuwa na sauti ya undani ndani yenu? Ni nani kati yenu ambaye amesoma maneno Yangu bila hofu na kutetemeka, akiwa na hofu sana kwamba Nitampiga na kumwingiza kuzimu? Ni nani asiyeweza kuvumilia majaribio ndani ya maneno Yangu? Ndani ya maneno Yangu kuna mamlaka, lakini haya si ya kupitisha hukumu ya kawaida juu ya mtu; Badala yake, kwa kujali hali halisi za mwanadamu, daima Namwonyesha mwanadamu maana iliyopo katika maneno Yangu. Kwa kweli, yupo aliye na uwezo wa kutambua nguvu za kudura katika maneno Yangu? Yupo ambaye anaweza kupokea ndani ya nafsi yake dhahabu safi zaidi ambayo maneno Yangu yanaundwa nayo? Nimezungumza maneno mangapi, lakini kuna yeyote ambaye amewahi kuyathamini?

Machi 3, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 9

Inayofuata: Wimbo wa Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp