Sura ya 31

Ninawapenda wale wote wanaonitaka Mimi kwa dhati. Mkilenga kunipenda, hakika Nitawabariki kwa kiasi kikubwa. Je, mnaelewa nia Zangu? Katika nyumba Yangu, hakuna tofauti kati ya hali ya juu na chini. Kila mtu ni mwanangu, Mimi ni Baba yenu, Mungu wenu. Mimi ni mkuu na wa pekee. Ninadhibiti kila kitu ulimwenguni!

Unapaswa “kunitumikia kwa unyenyekevu na katika mafumbo” katika nyumba Yangu. Maneno haya yanapaswa kuwa kama wito wako. Usiwe jani kwenye mti, bali uwe mzizi wa mti na ukite mizizi kwa kina katika uzima. Ingia katika uzoefu halisi wa maisha, uishi kwa kufuata maneno Yangu, unitafute zaidi katika kila suala, na unikaribie zaidi na uwasiliane na Mimi. Usizingatie mambo yoyote ya nje, na usidhibitiwe na mtu, tukio, au kitu chochote, bali uwasiliane tu na watu wa kiroho juu ya kile Nilicho. Elewa nia Zangu, acha uhai Wangu upite miongoni mwenu, na uishi kwa kudhihirisha maneno Yangu na mtii mahitaji Yangu.

Tumia nguvu zako zote katika mambo ambayo Nimekuteua; tumia uwezo wako wote kuuridhisha moyo Wangu. Mimi ni nguvu yako na Mimi ni furaha yako … Mimi ni kila kitu chako. Nifuatilie tu Mimi. Najua tamaa za kweli za moyo wako na kwamba unajitumia mwenyewe kwa dhati kwa ajili Yangu, lakini unapaswa kujua jinsi ya kujitoa mwenyewe Kwangu nyumbani Mwangu na jinsi ya kunifuata hadi mwisho.

Kanisa ni moyo Wangu na Ninawashwa na hamu kwa ajili ya ujenzi wa kanisa Langu. Unapaswa kujitumia mwenyewe kwa ajili Yangu kwa kujitoa mwenyewe bila kusita hata kidogo, na kuonyesha huruma kwa nia Zangu ili moyo Wangu uridhike.

Iliyotangulia: Sura ya 30

Inayofuata: Sura ya 32

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp