Sura ya 30

Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri. Mwisho wa dunia unafunguka mbele ya macho yenu wenyewe, majanga makubwa yanakaribia upesi; Je, maisha yenu ni muhimu au kulala, kula, kunywa, na kuvaa kwenu ndivyo muhimu? Wakati umekuja wa ninyi kufikiria kwa makini mambo haya. Msiwe wenye shaka tena na msiogope kuwa na uhakika!

Ni wa kusikitisha jinsi gani! Jinsi gani walivyo duni! Jinsi gani walivyopofuka! Jinsi gani wanadamu walivyo wakatili! Kwa kweli mnalipuuza neno Langu—je, Ninazungumza nanyi bure? Bado ninyi ni wazembe sana, kwa nini? Kwa nini hivyo? Je, hamjawahi kufikiria kuhusu hilo kabla? Ninasema mambo haya kwa ajili ya nani? Niamini! Mimi ni Mwokozi wenu! Mimi ni Mwenyezi wako! Kesheni! Kesheni! Muda uliopotea hautakuja tena kamwe, kumbuka hili! Hakuna mahali popote duniani ambapo unaweza kununua dawa ambayo itapoza majuto! Kwa hiyo Nitawaambiaje hili? Je, neno Langu halistahili uzingatifu wenu wa makini na kutafakari kwa kurudia? Ninyi ni wazembe sana kwa maneno Yangu na ni msiowajibikia maisha yenu sana; Ninawezaje kustahimili haya? Ninawezaje?

Kwa nini, katika muda huu wote, maisha yanayofaa ya kanisa hayajaweza kuibuka miongoni mwenu? Ni kwa sababu mnakosa imani, hamko tayari kulipa gharama, hamtaki kujitoa wenyewe, na hamko radhi kujitumia wenyewe mbele Yangu. Amkeni, wanangu! Niamini, wanangu! Wapendwa Wangu, kwa nini hamuwezi kufikiria yaliyo ndani ya moyo Wangu?

Iliyotangulia: Sura ya 29

Inayofuata: Sura ya 31

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp