Dhambi Zitamwongoza Mwanadamu Jahanamu

Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, mnaelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anavyopaswa kuwa, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata kwa miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii na uasi wenu mwingi dhidi Yangu kwa hii miaka mingi, kwa sababu hakuna mtakatifu hata mmoja kati yenu, nyinyi pia ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba daima Narudia kuzungumza mbele yenu. Sitaki kuishi pamoja na ninyi kwa njia hii—lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, hapa Nitarudia Niliyoyasema kwa mara nyingine tena. Natumaini kuwa mtaweza kuonyesha uelewa zaidi, na Natumai hata zaidi kwamba mtaweza kuamini kila neno Ninalosema, na bado zaidi, kwamba mtaweza kufahamu kwa kina maana ya maneno Yangu. Msiwe na shaka juu ya yale Ninayosema, au hata kuyachukulia maneno Yangu mnavyotaka na kuyatupilia mbali kwa hiari, jambo ambalo Naliona kuwa halistahimiliki. Msiyahukumu maneno Yangu, sembuse hatamsiyachukulie kwa uzito, au kusema kwamba daima Nawajaribu, au mbaya zaidi, mseme kwamba kile ambacho Nimewaambia kinakosa usahihi. Ninaona kuwa mambo haya hayavumiliki. Kwa sababu mnanichukulia Mimi na kuyachukulia Ninayoyasema kwa mashaka na kamwe hamyazingatii, Ninamwambia kila mmoja wenu kwa uzito kabisa: Msiunganishe kile Ninachosema na falsafa, msikiweke pamoja na uongo wa matapeli, na hata zaidi, msiyajibu maneno Yangu kwa dharau. Labda katika siku zijazo hakuna mtu yeyote atakayekuwa na uwezo wa kuwaambia yale Ninayowaambia nyinyi, au kuzungumza na nyinyi kwa huruma sana, sembuse kuwaeleza mambo haya kwa uvumilivu hivi. Siku zijazo zitatumika katika kukumbuka nyakati zile nzuri, au kwa kulia kwa sauti kubwa, au kuugulia kwa maumivu, au mtakuwa mkiishi katika usiku wa giza bila hata chembe ya ukweli au kupewa maisha, au kusubiri tu bila matumaini, au kukaa katika majuto machungu kiasi kwamba hamwezi kufikiri…. Kwa kweli hakuna hata mmoja wenu anayeweza kuepuka uwezekano huu. Kwa sababu hakuna hata mmoja wenu anayechukua nafasi ya kumwabudu Mungu kwa kweli; mnajitumbukiza katika dunia yenye uasherati na maovu, mnachanganya ndani ya imani yenu, ndani ya roho zenu, nafsi, na miili, mambo mengi yasiyohusiana na maisha na ukweli na kwa kweli yanapingana nayo. Hivyo kile Ninachotumaini kwenu ni kuwa mtaweza kuletwa kwenye njia yenye mwanga. Tumaini Langu la pekee ni kwamba mtaweza kuwa na uwezo wa kujijali wenyewe, kujitunza wenyewe, na kwamba hamtaweka mkazo sana kwenye hatima zenu huku mkizitazama tabia zenu na dhambi zenu kwa kutokujali.

Watu ambao wamemwamini Mungu kwa muda mrefu sasa wametumainia hatima iliyo nzuri, watu wote ambao wanamwamini Mungu wanatumai kwamba bahati nzuri itawajia kwa ghafla, na wote wanatumai kwamba bila kujua, watajikuta wameketi kwa amani sehemu moja au nyingine kule mbinguni. Lakini Ninasema kwamba watu hawa, pamoja na mawazo yao mazuri hawajawahi kujua kama wana sifa ya kupokea bahati nzuri kama hiyo inayoanguka kutoka mbinguni, au kukaa juu ya kiti huko mbinguni. Kwa sasa ninyi mna maarifa mazuri kujihusu, lakini bado mnatarajia kwamba mnaweza kuepuka maafa ya siku za mwisho na mkono wa Mwenyezi anapowaadhibu wale waovu. Inaonekana kana kwamba kuwa na ndoto tamu na kutaka vitu kama tu wanavyopenda ni sifa ya kawaida ya watu wote ambao Shetani amewapotosha, na sio fikra ya mtu fulani binafsi. Hata hivyo, bado Nataka kukomesha tamaa zenu badhirifu na hamu zenu za kupata baraka. Kwa kuwa dhambi zenu ni nyingi na ukweli wa kutotii kwenu ni mwingi na unaongezeka kila wakati, haya yanawezaje kupatana na mipango yenu mizuri ya baadaye? Kama unataka kuendelea unavyopenda kuwa mwenye makosa, bila chochote kinachokuzuia, lakini bado unataka ndoto zitimie, basi Nakusihi uendelee katika usingizi wako na usiamke kamwe, kwa sababu unaota ndoto isiyoweza kutimia, na haitatumika kukufanya upate upendeleo mbele za Mungu mwenye haki. Kama unataka tu ndoto zitimie, basi usiote kamwe, lakini kabiliana na ukweli milele, kabiliana na mambo ya hakika. Hiyo ndiyo njia ya pekee ya kukuokoa. Je, kwa maneno thabiti, hatua za mbinu hii ni zipi?

Kwanza, fanya uchunguzi wa dhambi zako zote, na uchunguze tabia na mawazo yako yote ambayo hayafuati ukweli.

Hiki ni kitu ambacho mnaweza kukifanya kwa urahisi, na Ninaamini kwamba watu wote wenye akili wanaweza kufanya hivi. Hata hivyo, wale watu ambao hawajui kamwe kile kinachomaanishwa kuwa ni dhambi na ukweli ni tofauti, ni kwa sababu kwa kiwango cha chini, wao si watu wenye akili. Ninazungumza na watu ambao wameidhinishwa na Mungu, ambao ni waaminifu, hawajakiuka kwa uzito amri zozote za kiutawala, na wanaweza kutambua dhambi zao wenyewe kwa urahisi. Ingawa hiki ni kipengele kimoja ambacho Ninahitaji kutoka kwenu ambacho ni rahisi kwenu, sicho kipengele cha pekee Ninachohitaji kutoka kwenu. Haijalishi ni nini, Ninatumai kwamba hamtalicheka hitaji hili kwa siri, au hata zaidi, kwamba hamtaliangalia kwa dharau au kulichukulia kimzaha. Lichukulieni kwa umakini, na msilipuuze.

Pili, kwa kila moja ya dhambi na kutotii kwako unapaswa kutafuta ukweli unaolingana, na kisha uutumie ukweli huu kutatua masuala hayo. Baada ya hayo, badilisha matendo yako ya dhambi na mawazo yako na vitendo vya kutotii kwa kutenda ukweli.

Tatu, unapaswa kuwa mtu mwaminifu, si mtu ambaye siku zote anakuwa mjanja, na usiwe mtu mdanganyifu daima. (Hapa Ninakusihi tena uwe mtu mwaminifu.)

Kama unaweza kutimiza vipengele hivi vyote vitatu basi una bahati, wewe ni mtu ambaye ndoto zako zinatimia na ambaye umepata bahati nzuri. Labda mtayachukulia mahitaji haya matatu yasiyovutia kwa umakini, au labda mtayachukulia kwa uzembe. Kwa vyovyote vile, nia Yangu ni kutimiza ndoto zenu, kuweka mawazo yenu katika matendo, si kuwafanyia mzaha au kuwadanganya.

Mahitaji Yangu yanaweza kuwa rahisi, lakini kile Ninachowaambia si rahisi hivyo kama kujumlisha moja na moja upate mbili. Kama kile mnachofanya ni kuzungumza tu kuhusu mambo haya bila kufikiria, au kuongea kwa kuropoka maneno matupu, yanayovutia, basi mipango yenu na matakwa yenu yatakuwa ukurasa mtupu milele. Mimi Sitakuwa na hisia ya huruma kwa wale walio miongoni mwenu ambao wanateseka kwa miaka mingi na kufanya kazi kwa bidii bila matokeo yoyote. Kinyume cha hayo, Nitawatendea wale ambao hawajatimiza mahitaji Yangu kwa adhabu, si thawabu, sembuse huruma yoyote. Mnaweza kuwa mnafikiri kwamba, kwa kuwa mmekuwa wafuasi kwa miaka mingi sana, mmeweka bidii bila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote mnaweza kupata bakuli la wali katika nyumba ya Mungu kwa kuwa watendaji huduma. Naweza kusema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu siku zote mmekuwa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani na usichukuliwe kwa manufaa ya wengine. Hivyo Ninawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi ambavyo kazi yako yenye bidii inavyostahili kusifiwa, jinsi ambavyo sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi ambavyo umeboresha mtazamo wako; mradi tu hujatimiza matakwa Yangu, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia mahitaji Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu, na hali ikiwa mbaya zaidi Nitageuza miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwa bure, kwa sababu Siwezi kuwaleta watu hao wanaonuka uovu na walio na sura ya Shetani katika ufalme Wangu au kuwapeleka katika enzi ijayo.

Nina matamanio mengi. Natamani muweze kutenda kwa njia inayofaa na yenye mwenendo mzuri, muwe waaminifu kutimiza wajibu wenu, muwe na ukweli na ubinadamu, muwe watu ambao wanaweza kuacha vitu vyote na kuyatoa maisha yao kwa ajili ya Mungu, na mengineyo. Matumaini haya yote yanatokana na upungufu wenu na upotovu na kutotii kwenu. Kama kila mojawapo ya mazungumzo ambayo Nimekuwa nayo pamoja nanyi hayajatosha kuvuta umakini wenu, basi huenda Sitasema mengine. Hata hivyo, nyinyi mnaelewa matokeo ya hayo. Sipumziki kamwe, kwa hiyo Nisiponena, Nitafanya kitu ili watu wakitazame. Ninaweza kuufanya ulimi wa mtu uoze, au mtu afe na viungo vyake vitolewe, au kumpa mtu kasoro za neva na kumfanya atende kama mwendawazimu. Au, hata tena, Ninaweza kuwafanya baadhi ya watu wavumilie maumivu makali Ninayowasababishia. Kwa njia hii Ningejihisi mwenye furaha, mwenye furaha sana na kuridhika sana. Imesemwa daima kwamba “Mema hulipizwa kwa mema, na maovu kwa maovu,” mbona isiwe hivyo sasa? Kama unataka kunipinga Mimi na unataka kutoa hukumu fulani kunihusu, basi Nitauozesha mdomo wako, na hilo litanipendeza Mimi sana. Hii ni kwa sababu mwishowe hujafanya lolote linalohusiana na ukweli, sembuse na maisha, ilhali kila kitu Ninachofanya ni ukweli, kila kitu kinahusiana na kanuni za kazi Yangu na amri za utawala Nilizoweka rasmi. Kwa hiyo, Namsihi sana kila mmoja wenu ajikusanyie matendo mema kiasi, acheni kufanya maovu mengi sana, na mtii matakwa Yangu katika wakati wenu wa bure. Kisha Nitajihisi furaha. Kama mngetoa (au kuchangia) katika ukweli mara elfu mojaya juhudi mnazoweka katika mwili, basi Nasema hungekuwa na dhambi za mara kwa mara na midomo mibovu. Je, hili si dhahiri?

Kadri dhambi zako zinavyozidi kuwa nyingi, ndivyo utakavyokuwa na fursa chache za kupata hatima iliyo nzuri. Kinyume chake, kadri dhambi zako zinavyozidi kuwa chache, ndivyo uwezekano wako wa kusifiwa na Mungu unavyoongezeka. Kama dhambi zako zitaongezeka hadi kiwango ambacho haiwezekani tena Mimi kukusamehe, basi utakuwa umepoteza kabisa nafasi yako ya kusamehewa. Hivyo hatima yako haitakuwa ya juu bali chini. Kama huniamini basi kuwa jasiri na ufanye maovu, na kisha uone kile kitakachokupata. Kama wewe ni mtu ambaye utendaji wako wa ukweli ni wenye bidii sana basi kwa hakika una fursa ya kusamehewa dhambi zako, na kiwango cha kutotii kwako kutapungua zaidi na zaidi. Kama wewe ni mtu ambaye hauko tayari kutenda ukweli basi kwa hakika dhambi zako mbele ya Mungu zitaongezeka, kiwango cha kutotii kwako kitaongezeka zaidi na zaidi, mpaka wakati wa mwisho ambapo utakuwa umeangamia kabisa, na huo ndio wakati ambao ndoto yako ya kupendeza ya kupokea baraka itaharibiwa. Usizichukulie dhambi zako kama ni makossa tu ya mtu asiye mkomavu au mpumbavu, usitumie kisingizio kwamba hukutenda ukweli kwa sababu ubora duni wa tabia yako ulikufanya usiweze kuutenda, na hata zaidi, usizichukulie tu dhambi ulizofanya kama ni matendo ya mtu ambaye hakujua vizuri zaidi. Kama unajua vizuri kujisamehe na unajua vizuri kujitendea kwa ukarimu, basi Ninasema wewe ni mwoga ambaye kamwe hautapata ukweli, na dhambi zako kamwe hazitakoma kukuandama, lakini zitakuzuia kuwahi kutosheleza mahitaji ya ukweli na kukufanya milele uwe mwandamani mwaminifu wa Shetani. Ushauri Wangu kwako bado ni huu: Usiwe makini sana kwa hatima yako tu na kutotilia maanani dhambi zako zilizofichika; zichukulie dhambi zako kwa makini, na usikose kutilia maanani dhambi zako zote kwa sababu ya kujali kuhusu hatima yako.

Iliyotangulia: Maonyo Matatu

Inayofuata: Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp