Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 29

Je, unajua kwamba wakati unawadia? Hivyo kwa muda mfupi wa hivi karibuni utanitegemea Mimi na kuyatupilia mbali mambo yote kutoka kwako ambayo hayalingani na tabia Yangu: upumbavu, upole wa kuonyesha hisia, mawazo yasiyo wazi, moyo wa upole, nia hafifu, upuuzi, hisia zilizotiwa madoido mengi, kuchanganyikiwa na ukosefu wa utambuzi. Haya lazima yatupiliwe mbali upesi iwezekanavyo. Mimi ndimi mwenyezi Mungu! Mradi tu uko radhi kushirikiana na Mimi, Nitayatibu yote yanayokuuguza. Mimi ni Mungu anayeangalia ndani kabisa ya mioyo ya watu, Naujua magonjwa yako yote na kule ambako dosari zako ziko. Haya ndiyo mambo ambayo yanakuzuia wewe kuwa na maendeleo maishani, na ni lazima yatupiliwe mbali hivi karibuni. La sivyo, mapenzi Yangu hayawezi kutekelezwa juu yako. Kile ambacho mwanga Wangu unamulika juu yake, lazima unitegemee Mimi kukitupilia mbali, Nitegemee kila mara, kuwa karibu na Mimi, na matendo yako lazima yafichue sura Yangu. Utakuwa na ushirika na Mimi zaidi wakati huna uhakika kuhusu kile cha kufanya, na Nitakuongoza kuelekea kwa matendo sahihi ili kwamba uweze kusonga mbele. Kama huna uhakika, usifanye vitendo vya kiholela; ngoja tu wakati Wangu. Dumisha silika thabiti, usiruhusu hisia zako kali ziwe moto au baridi; lazima uwe na moyo ambao daima inanicha. Kile unachofanya mbele Yangu au nyuma Yangu lazima daima kiwe kulingana na mapenzi Yangu. Usiwe mwenye huruma kwa yeyote kwa niaba Yangu, awe ni mumeo au mmoja wa jamii yako; halikubaliki, haijalishi wao ni wazuri kiasi gani. Lazima uchukue hatua kwa msingi wa ukweli. Ukinipenda Mimi, Nitakuridhia baraka kubwa. Sitamstahimili yeyote anayepinga. Wapende wale Ninaowapenda, na uwachukie Ninaowachukia. Usitilie maanani mtu yeyote, kitu chochote au chombo chochote. Angalia na moyo wako na uone kwa udhahiri watu wanaotumiwa na Mimi, kuwa katika mawasiliano zaidi na wanadamu wa kiroho. Usiwe mpumbavu; lazima utofautishe. Ngano itakuwa ngano daima na vigugu mwitu havitawahi kua viwe ngano, na ni lazima utambue aina tofauti za watu. Lazima uwe hasa mwangalifu katika usemi wako na uweke miguu yako katika njia ambayo inaupendeza moyo Wangu. Maneno haya lazima yatafakariwe kwa uangalifu. Lazima utupilie mbali uasi wako na ujifanye anayefaa kwa matumizi Yangu upesi iwezekanavyo, ili kwamba moyo Wangu uridhishwe.

Iliyotangulia:Sura ya 28

Inayofuata:Sura ya 30

Maudhui Yanayohusiana

 • Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu

  Unampenda Mungu kiasi gani hasa leo? Na unajua kiasi gani hasa kuhusu yote ambayo Mungu amefanya ndani yako? Haya ni mambo unayopaswa kujifunza. Mun…

 • Sura ya 31

  Sijawahi kuwa na nafasi ndani ya mioyo ya watu. Ninapowatafuta watu kweli, wao hufunga na kubana macho yao na kupuuza matendo Yangu, kana kwamba yote…

 • Kazi na Kuingia (3)

  Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, manen…

 • Maono ya Kazi ya Mungu (1)

  Yohana alimfanyia Yesu kazi kwa miaka saba, na tayari alikuwa ameandaa njia Yesu alipofika. Kabla ya haya, injili ya ufalme wa mbinguni iliyohubiriw…