Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 26

Wanangu, yatilieni maanani maneno Yangu, sikiliza kwa utulivu sauti Yangu na Nitafichua kwako. Uwe na utulivu ndani yangu, kwa maana Mimi ni Mungu wako, Mkombozi wenu wa pekee. Mnatakiwa kutuliza mioyo yenu nyakati zote, mkae ndani yangu; Mimi ni mwamba wako, msaidizi wenu. Msiwe na nia nyingine, lakini mnitegemee kwa mioyo yenu yote na Mimi nitaonekana kwenu kwa hakika—Mimi ni Mungu wenu! Ah, wale wenye mashaka! Hakika hawawezi kusimama imara na hawatapata chochote. Lazima mjue sasa ni wakati gani, ni wakati muhimu kiasi gani. Ni jambo muhimu kivipi! Msishughulike huku na kule katika mambo yasiyo na manufaa; sogeeni karibu na Mimi haraka, fanyeni ushirika na Mimi, na nitafichua siri zote kwenu.

Lazima usikilize maneno yote ambayo Roho Mtakatifu anafundisha; usimpuuze. Mara nyingi umesikia maneno Yangu na kisha ukayasahau. Ee wasio na fikra! Umepoteza baraka nyingi sana! Lazima usikilize kwa makini sasa na utilie maanani maneno Yangu, ufanye ushirika zaidi na Mimi na kusogea karibu na Mimi zaidi. Nitakufundisha juu ya chochote ambacho haukielewi, nami Nitawaongoza kwenye njia inayoendelea. Usizingatie sana kushirikiana na watu wengine maana kuna watu wengi sasa wanaohubiri maandishi na mafundisho, na wachache ambao wana uhalisi Wangu kwa kweli. Ushirika wao humfanya mtu achanganyikiwe na asiyehisi, bila kujua jinsi ya kuendelea. Hata ukiwasikiliza, unaishia tu kuelewa kidogo zaidi kuhusu maandishi na mafundisho. Lazima muangalie hatua zenu, mlinde mioyo yenu na kuishi mbele Yangu daima, muwasiliane na Mimi, mnikaribie na nitakuwezesha kuona ambayo huyaelewi. Lazima uangalie kile unachosema, uangalie kwa karibu moyo wako nyakati zote na kutembea katika njia Ninayotembelea.

Haitakuwa muda mrefu sasa, bado kuna muda kidogo uliobaki. Fanya haraka kuacha vitu vyote isipokuwa Mimi na uje unifuate! Sitakutendea vibaya. Mara nyingi mmeelewa visivyo matendo Yangu, lakini je, unajua ni kwa kiasi gani Ninakupenda? Ah, huelewi moyo Wangu kabisa. Bila kujali jinsi ulivyokuwa na mashaka na Mimi au ni kiasi gani nilikudai hapo zamani, Sitakumbuka. Lakini bado Niliwachagua ili mweze kwenda mbele na kutenda kulingana na mapenzi Yangu.

Sasa ni wakati ambao hauvumilii kukawia. Ikiwa kutoka sasa na kuendelea mnayo nia nyingine basi hukumu yangu itawafikia. Ukiniacha kwa muda kidogo tu basi utakuwa kama mke wa Lutu. Kasi ya kazi ya Roho Mtakatifu sasa inakusanya kasi na wale ambao hawawezi kwenda kasi sawasawa na mwanga mpya wako katika hatari kubwa. Wale ambao hawaangalii wataachwa; mnapaswa kujilinda wenyewe. Unapaswa kujua kwamba vitu vyote vilivyo katika mazingira yanayo wazunguka vipo hapo kwa ruhusa Yangu, Mimi napanga yote. Oneni wazi na muridhishe moyo Wangu katika mazingira Niliyokupa. Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu. Leo watu wana dhana nyingi sana na hili linanifanya Niweze kuonyesha mapenzi Yangu kupitia kwa wale ambao wanadharauliwa na wengine; wale ambao wanajisifu na kujidai, wenye kiburi na majivuno, wenye kutaka makuu na kujionyesha bora wataaibishwa. Ilimradi mnaonyesha kuzingatia kweli juu ya mzigo Wangu basi nitawaandaa kila kitu kwa ajili yenu. Nifuateni Mimi tu!

Iliyotangulia:Sura ya 25

Inayofuata:Sura ya 27

Maudhui Yanayohusiana

 • Unajua Nini Kuhusu Imani?

  Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binad…

 • Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

  Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila m…

 • Sura ya 3

  Kwa kuwa mnaitwa watu Wangu, mambo hayapo kama yalivyokuwa; mnapaswa kusikiliza na kutii matamshi ya Roho Wangu, fuateni kwa karibu kazi Yangu, na ms…

 • Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

  Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamb…