6. Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” (Waebrania 9:28).

“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1).

Maneno Husika ya Mungu:

Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. Ni mpaka siku za mwisho tu ambapo Mungu Ametakasa binadamu kikamilifu kwa kufanya kazi ya hukumu na kuadibu mwanadamu kwa kuwa muasi, ndipo Mungu atakamilisha kazi Yake ya wokovu na kupumzika. Kwa hivyo, katika hatua tatu za kazi, ni mara mbili tu ndipo Mungu amekuwa mwili ili kufanya kazi Yake kati ya mwanadamu Mwenyewe. Hiyo ni kwa sababu moja tu kati ya hatua tatu za kazi ni kuwaongoza wanadamu katika maisha yao, ilhali zingine mbili ni kazi ya wokovu. Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Ni kwa namna hii tu ndipo Ataweza kuwapa wanadamu njia ya vitendo wanayohitaji kama viumbe. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki ni mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa njia zote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili. Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Mungu katika kupata mwili Kwake mara ya kwanza Hakukamilisha kazi ya kupata mwili; Alikamilisha tu hatua ya kwanza ya kazi iliyokuwa lazima kwa Mungu kuifanya katika mwili. Kwa hivyo, ili kuimaliza kazi ya kupata mwili, Mungu Amerudi katika mwili kwa mara nyingine tena, Akiishi kulingana na ukawaida na uhalisia wote wa mwili, yaani, kuifanya kazi ya Mungu ijitokeze katika mwili wa kawaida kabisa, na kwa njia hiyo Anahitimisha kazi Aliyoiacha bila kukamilisha katika mwili. Mwili wa pili uliopatikana kimsingi ni sawa na ule wa kwanza, lakini ni halisi zaidi, wa kawaida kabisa kuliko ule wa kwanza. Kwa sababu hiyo, mateso unayoyapitia mwili wa pili uliopatikana ni makubwa kuliko yale ya ule wa kwanza, ila mateso haya ni kwa sababu ya huduma Yake katika mwili, ambayo ni tofauti na mateso ya mwanadamu mwovu. Vilevile yanachipuka kutokana na ukawaida na uhalisi wa mwili Wake. Kwa kuwa Anatekeleza huduma Yake katika mwili wa kawaida na halisi kabisa, mwili ni sharti upitie mateso mazito. Kadiri mwili ulivyo wa kawaida na halisi, ndivyo unateseka zaidi katika utekelezaji wa huduma Yake. Kazi ya Mungu inaonyeshwa katika mwili wa kawaida sana, mwili ambao si wa rohoni kamwe. Kwa kuwa mwili Wake ni wa kawaida, na ni lazima ubebe kazi ya kumwokoa mwanadamu, Anateseka hata zaidi kuliko ambavyo mwili wa rohoni unaweza kuteseka—mateso haya yote yanatokana na uhalisi na ukawaida wa mwili Wake. Kutokana na mateso yaliyopitiwa na hii miili miwili iliyopatikana wakati wa kutekeleza huduma Zao, mtu anaweza kuona kiini cha mwili uliopatikana. Kadiri mwili ulivyo wa kawaida, ndivyo Anapata mateso mazito Afanyapo kazi, kadri mwili unaofanya kazi unavyokuwa wa kweli, ndivyo maoni ya watu yanaendelea kuwa makali, na hatari zinazomkabili zinaendelea kuongezeka. Lakini, kadiri mwili ulivyo halisi, kadiri mwili unavyokuwa na hali kamili ya binadamu wa kawaida, ndivyo Anaweza zaidi kuifanya kazi ya Mungu katika mwili. Ulikuwa mwili wa Yesu ulioangikwa msalabani, mwili Wake Alioutoa kama kafara kwa dhambi; ni kupitia kwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida ndipo Aliweza kumshinda Shetani na kumkomboa kabisa mwanadamu kutoka msalabani. Ni kupitia mwili kamili ndipo Mungu katika mwili mara ya pili Anatekeleza kazi ya ushindi na kumshinda Shetani. Ni mwili tu wa kawaida na halisi kabisa unaoweza kutekeleza kazi ya ushindi kwa ukamilifu wake na kutoa ushuhuda wa nguvu. Hii ni sawa na kusema kwamba ushindi juu ya mwanadamu inafanywa kuwa bora kupitia uhalisia na ukawaida wa mwili wa Mungu, si kupitia miujiza mikuu na ufunuo. Huduma ya huyu Mungu mwenye mwili ni ya kunena na kwa njia hiyo inamshinda mwanadamu na kumfanya mkamilifu; kwa maneno mengine, kazi ya Roho Aliyejitokeza katika mwili, wajibu wa mwili, ni kunena na kupitia kwa hili kumshinda, kumfichua, kumfanya kuwa kamilifu, na kumwondoa mwanadamu kabisa. Kwa hivyo, ni katika kazi ya kushinda ambapo kazi ya Mungu katika mwili itatimiziwa kwa ukamilifu. Kazi ya ukombozi ya kwanza ilikuwa mwanzo tu wa kazi ya kupata mwili kwa Yesu; mwili unaofanya kazi ya kushinda utaikamilisha kazi nzima ya kupata mwili kwa Yesu. … Katika hatua hii ya kazi, Mungu Hafanyi ishara na miujiza, ili kwamba kazi iweze kutimiza matokeo yake kupitia kwa maneno. Sababu ya jambo hili, aidha, ni kwa maana kazi ya Mungu mwenye mwili mara hii si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, ila kumshinda mwanadamu kupitia kunena, ikiwa na maana kwamba uwezo asili uliomo kwenye huu mwili uliopatikana wa Mungu ni kunena maneno na kumshinda mwanadamu, si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo. Kazi Yake katika ubinadamu wa kawaida si kutenda miujiza, si kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo, ila ni kunena, na kwa hivyo Yesu kupata mwili kwa mara ya pili kunaonekana kwa watu kuwa kawaida zaidi ya mara ya kwanza. Watu wanaona kuwa Mungu kupata mwili si uongo; lakini huyu Mungu mwenye mwili ni tofauti na Yesu Aliyekuwa mwili, na japo wote ni Mungu wenye mwili, Hawako sawa kabisa. Yesu Alikuwa na ubinadamu wa desturi, ubinadamu wa kawaida, lakini Aliambatana na ishara nyingi na miujiza. Katika huyu Mungu mwenye mwili, macho ya mwanadamu hayataona ishara au miujiza, wala kuponya wagonjwa au kufukuza mapepo, wala kutembea juu ya bahari, wala kufunga kwa siku arobaini… Hafanyi kazi sawa na Aliyoifanya Yesu, si kwa kuwa mwili Wake kimsingi ni tofauti na ule wa Yesu, ila ni kwa sababu si huduma Yake kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo. Haharibu kazi Yake mwenyewe, Havurugi kazi Yake mwenyewe. Kwa kuwa anamshinda mwanadamu kwa maneno Yake halisi, haina haja ya kumhini kwa miujiza, na kwa hivyo hii hatua ni kukamilisha kazi ya kupata mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kwa nini Ninasema kuwa maana ya kupata mwili haikukamilishwa katika kazi ya Yesu? Ni kwa sababu Neno halikuwa Mwili kikamilifu. Kilichofanywa na Yesu kilikuwa tu sehemu moja ya kazi ya Mungu katika mwili; Alifanya tu kazi ya ukombozi na Hakufanya kazi ya kumpata mwanadamu kikamilifu. Kwa sababu hii, Mungu Amekuwa mwili mara nyingine tena katika siku za mwisho. Hatua hii ya kazi, pia inafanywa katika mwili wa kawaida, ikifanywa na mwanadamu wa kawaida kabisa, ambaye ubinadamu wake haupiti mipaka ya ubinadamu. Kwa maneno mengine, Mungu Amekuwa mwanadamu kamili, na ni mtu ambaye utambulisho wake ni ule wa Mungu, mwanadamu kamili, mwili kamili, Ambaye Anatekeleza kazi. Katika jicho la mwanadamu, Yeye ni mwili tu ambao haujapita mipaka ya ubinadamu hata kidogo, mwanadamu wa kawaida kabisa Anayeweza kuzungumza lugha ya mbinguni, Ambaye Haonyeshi ishara za kimiujiza, Hafanyi miujiza, sembuse kuweka wazi ukweli wa ndani kuhusu dini katika kumbi kuu za mikutano. Kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili inaonekana kwa wanadamu kuwa tofauti kabisa na ile ya kwanza, kiasi kwamba kazi hizi mbili zinaonekana kutokuwa na uhusiano wowote, na hakuna chochote katika kazi ya kwanza kinachoweza kuonekana wakati huu. Japo kazi ya kupata mwili kwa mara ya pili ni tofauti na ile ya kwanza, hili halithibitishi kuwa chanzo Chao si kimoja na sawa. Iwapo chanzo Chao ni kimoja inategemea aina ya kazi iliyofanywa na miili na si katika maumbo Yao ya nje. Katika hatua tatu za kazi Yake, Mungu Amekuwa mwili mara mbili, na mara zote kazi ya Mungu kuwa mwili inaanzisha enzi mpya, inaanzisha kazi mpya; kuwa mwili kwa mara ya kwanza na pili kunakamilishana. Macho ya wanadamu hayawezi kugundua kuwa hii miili miwili kwa kweli imetokana na chanzo kimoja. Ni wazi kwamba hili liko nje ya uwezo wa macho ya wanadamu au akili za wanadamu. Ila katika kiini Chao, ni miili sawa, kwani kazi Yao inatokana na Roho mmoja. Iwapo hii miili miwili inatokana na chanzo kimoja haiwezi kuamuliwa kutokana na enzi na sehemu Ilipozaliwa, au vigezo vingine kama hivyo, ila kwa kazi ya uungu iliyoonyeshwa Nayo. Kupata mwili wa pili hakufanyi kazi yoyote iliyofanywa na Yesu, kwani kazi ya Mungu haifuati makubaliano, lakini kila wakati inafungua njia mpya. Kupata mwili wa pili hakulengi kuongeza au kuimarisha maono ya kupata mwili wa kwanza katika akili za watu, ila kuutimiza na kuukamilisha, kuongeza kina cha wanadamu kumwelewa Mungu, kuvunja sheria zote ambazo zipo katika mioyo ya watu, na kufuta picha za uongo kuhusu Mungu mioyoni mwao. Ni wazi kuwa hakuna hatua yoyote ya kazi ya Mungu mwenyewe inaweza kumpa mwanadamu ufahamu kamili wa Mungu; kila mojawapo inatoa kwa sehemu tu, si ufahamu mzima. Japo Mungu Ameonyesha tabia Yake kikamilifu, kwa sababu ya upungufu wa ufahamu wa wanadamu, ufahamu wake kuhusu Mungu si kamili. Haiwezekani, kutumia lugha ya wanadamu, kueleza tabia nzima ya Mungu; basi hatua moja tu ya kazi Yake itamwelezaje Mungu kikamilifu? Anafanya kazi katika mwili kwa kujisetiri katika ubinadamu Wake wa kawaida, na mtu anaweza kumjua tu kupitia kwa maonyesho ya uungu Wake, si kupitia kwa umbo Lake la kimwili. Mungu Anakuja katika mwili kumruhusu mwanadamu Amjue kupitia kazi Zake mbalimbali, na hakuna hatua mbili za kazi Yake zinafanana. Ni kwa njia hii tu mwanadamu anaweza kuwa na ufahamu kamili wa kazi ya Mungu katika mwili, si kwa kujifunga katika kipengele kimoja tu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Hatua ya kazi ambayo Yesu alitekeleza ilitimiza tu kiini cha “Neno alikuwako kwa Mungu”: Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka katika mwili huo. Yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa kupata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi hasa inatimiza maana ya ndani ya “Neno lakuwa mwili,” ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya “naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,” na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno “Hapo mwanzo kulikuwako na Neno.” Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na katika enzi ya mwisho, Yeye anafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumruhusu mwanadamu kuziona njia Zake zote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. Lazima uelewe mambo haya yote kabisa. Si suala la kuujua mwili, bali la jinsi unavyouelewa mwili na Neno. Huu ndio ushuhuda unaopaswa kuwa nao, kile ambacho kila mtu lazima akijue. Kwa sababu hii ni kazi ya kupata mwili kwa pili—na mara ya mwisho ambapo Mungu anapata mwili—inakamilisha kwa ukamilifu umuhimu wa kupata mwili, inatekeleza kabisa na kutoa kazi yote ya Mungu katika mwili, na kuitamatisha enzi ya Mungu kuwa katika mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (4)

Iliyotangulia: 5. Kwa nini husemwa kuwa wanadamu wapotovu wanahitaji zaidi wokovu wa Mungu aliyepata mwili?

Inayofuata: 7. Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp