26. Kufungua Mlango wa Moyo Wangu na Kukaribisha Kurudi Kwa Bwana

Na Yongyuan, Marekani

Mnamo Novemba mwaka wa 1982, familia yetu yote ilihamia Marekani. Sote tulimwamini Bwana tangu kizazi cha babu yangu, kwa hivyo tulipata kanisa la Wachina huko Chinatown mjini New York mara baada ya kufika Marekani ili tuweze kuhudhuria misa. Hatukuwahi kukosa kuhudhuria misa hata moja, na mama na dada yangu walikuwa hodari sana katika kusoma maandiko kila walipokuwa na wakati ili kutafuta baraka na ulinzi wa Mungu. Padri alisema mara nyingi: “Bwana atakapokuja, Atawahukumu watu hadharani na kuwagawanya katika makundi: Wale wanaotubu na kukiri na kutenda imani yao kwa kweli wataweza kwenda mbinguni; wale wanaotenda dhambi ndogo lakini si kuu watapata mateso mahali pa mateso ya muda lakini wataweza kuokolewa na kupaa mbinguni; wale ambao hawamwamini Mungu au hufanya dhambi ambazo ni kubwa sana watapitia adhabu ya kuzimu.” Maneno haya yaliacha picha kuu moyoni mwangu, kama tu kwamba yalikuwa yamepigwa chapa humo. Yalinichochea nimwamini Mungu kwa shauku, na bila kujali nilikuwa na shughuli nyingi kiasi gani, sikushindwa kuhudhuria misa.

Baada ya muda mfupi sana, mwaka wa 2014 ulifika. Siku moja, mkazi wa parokia aliniambia ghafla, “Dada yako sasa anamwamini Mwenyezi Mungu….” Na akasema mambo mengi mbali na kumkashifu na kumlaani Mwenyezi Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Niliposikia habari hizi za ghafula, nilihisi wasiwasi sana, na nikawa na wahaka sana kuwa dada yangu alikuwa amepotoka. Habari za dada yangu za kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho zilienea haraka katika kanisa lote. Padre alinisihi nikae mbali naye, na kulikuwa na washiriki wengine kadhaa wa kanisa ambao pia walisema mambo kadhaa wakimkashifu na kumlaani Mwenyezi Mungu pasipo kujaribu kuficha. Baada ya kasisi na wakaazi wengine wa parokia “kunisaidia” mara kadhaa, nilianza kuamini maneno yao na nikabainisha kuwa dada yangu alikuwa amepotoka. Nilimwambia padre na wakazi wa parokia kwamba sitamsikiza dada yangu tena, na kwamba iwapo ningepata fursa, ningejaribu kumrudisha katika kundi ili aweze kutubu kwa Bwana. Niliwaita ndugu zangu baada ya kufika nyumbani, na waliniunga mkono. Sote tulijaribu kumshawishi dada yangu kwa pamoja, lakini sio tu kwamba alikuwa thabiti katika imani yake katika Mwenyezi Mungu, lakini pia alishuhudia kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana aliyerejea. Alijaribu kutushawishi tukubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho ili tusikose nafasi yetu ya kupata wokovu wa Mungu. Lakini moyo wangu tayari ulikuwa umejawa na mawazo hasi ambayo yalitiwa ndani yangu polepole na padre na wakazi wa parokia. Bila kujali dada yangu alivyoshiriki nami au jinsi alivyoshuhudia, sikusikiza tu.

Baadaye, mimi na mama yangu tulibishana mara kadhaa na dada yangu kwa sababu ya imani yake katika Mwenyezi Mungu, lakini bila kujali alichosema, niliendelea kumwamini padre na uvumi ambao nilikuwa nimesoma kwenye mtandao, pasipo kamwe kuthubutu kutafuta au kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu. Hakukuwahi kuwa na suluhisho katika mabishano yetu, lakini niligundua kuwa mama yangu alikuwa akianza kukubaliana na ushirika na ushuhuda wa dada yangu polepole. Kwa kweli aliunda “muungano wa umoja” na dada yangu na mwishowe akakubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Nilipoona haya, nilianza kuwa na wasiwasi. Ikiwa mambo kweli yalikuwa kama padre na wakazi wa parokia walivyodai, itakuwa vipi kitu kikiitokea familia yangu? Huku nikikata tamaa, nilikwenda kumtafuta Dada Qianhe ambaye alikuwa na uhusiano mzuri na mimi na dada yangu, na nikamfanya ajaribu kuwashawishi mama na dada yangu. Lakini sio tu kwamba alishindwa kuwashawishi, lakini yeye mwenyewe pia alikuja kumwamini Mwenyezi Mungu. Jambo hili lilinikanganya sana: Dada huyu alikuwa mwadilifu na alikuwa mtafutaji mwenye shauku, kwa hivyo yawezekanaje kuwa hakuweza kuwashawishi, lakini kwa kweli alikuja kumwamini Mwenyezi Mungu yeye mwenyewe? Je, neno la Mwenyezi Mungu kweli lina nguvu nyingi sana? Inawezekana kwamba neno la Mwenyezi Mungu linaweza kwa kweli kutoa riziki kwa maisha ya mwanadamu? Hata hivyo, mara nilipofikiria maneno ya padre na wakazi wa parokia yaliyomshambulia Mwenyezi Mungu na vilevile yale ambayo nilikuwa nimeyaona mtandaoni yakipinga na kulilaani Kanisa la Mwenyezi Mungu, kwa mara nyingine nilihisi hofu moyoni mwangu na sikuweza kuwasiliana nao tena. Baada ya hapo, nilienda kumuona mama yangu mara chache. Nilienda tu kutembea mara chache na kisha kuondoka haraka, na nilikataa kusikiliza ushirika wa mama na dada yangu. “Vita hivi vya maneno” dhidi ya mama na dada yangu viliendelea hivi kwa mwaka mmoja na nusu.

Siku moja mnamo Machi mwaka wa 2016, nilisikia kwamba washiriki wengine mashuhuri wa kanisa pia walikuwa wamekwenda kumshawishi dada yangu, kwa hivyo nilitaka kwenda kuona ikiwa alikuwa amebadilisha msimamo au la. Nilipomwona, nilimuuliza kuhusu alichokuwa akifiria. Aliniambia, “Nimefikia nyayo za Mwanakondoo na nikathibitisha kwamba njia ya Mwenyezi Mungu ndiyo njia ya kweli. Mwenyezi Mungu ni Bwana aliyerejea na bila shaka sitamwacha.” Jinsi dada yangu alivyonikazia macho jibu lake kubwa sana na thabiti vilifanya moyo wangu usitesite kwa kiwango fulani na kuamsha udadisi wangu. Nilifikiri: Kati ya waumini katika familia yetu, dada yangu alikuwa mtafutaji mwenye shauku zaidi, na ndani ya kanisa Dada Qianhe pia alikuwa mtu ambaye alikuwa mtafutaji na alikuwa na utambuzi. Mama yangu, pia, alikuwa na imani thabiti kwa Bwana. Sasa, wote walikuwa waumini wa Mwenyezi Mungu, na imani yao ilikuwa imekua zaidi baada ya kumfuata. Waliongea kwa ufahamu mwingi zaidi na zaidi na hakuna mtu aliyeweza kuwatikisa au kuwakanusha. Ni nguvu gani ambayo ingeweza kuwaruhusu wadumishe imani kubwa kama hiyo wanapokabiliwa na upinzani wa watu wengi sana? Kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho inaweza kweli kuwa njia ya kweli? Mwenyezi Mungu anaweza kuwa ujio wa pili wa Bwana? Ilikuwa karibu miaka miwili tangu dada yangu, Dada Qianhe, na mama yangu wakubali kazi ya Mwenyezi Mungu, lakini nilipoona kwamba kila kitu kiliwaendea vizuri, niliweza kuona kuwa mbinu za kuogofya na za kutisha za padre na nilichokuwa nimesoma mtandaoni havikutimia kwao…. Nilipogundua hayo, moyo wangu ulipunguza ukali kidogo na pia nilitaka kuchunguza neno na kazi ya Mwenyezi Mungu. Nilishiriki mawazo yangu na dada yangu. Alikubali kwa furaha sana na akanialika nyumbani kwa mama yangu ili dada kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu aweze kushiriki nami na kushuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho.

Nilienda nyumbani kwa mama yangu kwa gari wikendi hiyo. Dada yangu, Dada Qianhe, na Zhang Xiao, dada kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu, wote walikuwa pale. Dada Qianhe alifurahi sana aliposikia kwamba nilitaka kutafuta na kuchunguza. Alishiriki nami: “Sababu kuu ya Mungu kuja katika siku za mwisho ni kuonyesha neno na kufanya kazi ya kuwahukumu na kuwatasa watu ili kutuokoa kutoka utumwani mwa dhambi. Kwa sasa, wale walio katika Enzi ya Neema wanaishi katika mzunguko wa kutenda na kisha kukiri dhambi. Hata ingawa tunavumilia kuhudhuria misa na kusoma maandiko, na vilevile kukiri kwa padre, bado tunaendelea kusema uwongo na kudanganya, na kuishi ndani ya tabia zetu potovu kama vile kiburi, tamaa, na ubinafsi. Licha ya sisi wenyewe, sisi hufanya dhambi na kumpinga Mungu, na hakuna mtu anayeweza kujitenga na utumwa wa asili hii ya dhambi, wala hakuna mtu yeyote anayeweza kufikia usafi na utakatifu kwa kutegemea kukiri na kutubu. Ndiyo maana bado tunahitaji kukubali kazi ambayo Mungu amekuja kufanya katika siku za mwisho ya kuwahukumu na kuwatakasa watu. Ni kwa kufanya hivyo tu ndiyo tunaweza kujitenga kabisa na utumwa wa dhambi, kutakaswa na kubadilishwa, na kupata wokovu kutoka kwa Mungu.” Niliposikia haya, niliuliza kwa kuchanganyikiwa: “Padre mara nyingi husema: ‘Watu wakitenda dhambi ndogo, basi Bwana atakaporudi kuhukumu watu hadharani, watakapokamilisha mateso yao mahali pa mateso ya muda wataweza kupaa mbinguni. Wale wanaotenda dhambi kubwa wataenda kuzimuni moja kwa moja kuadhibiwa.’ Unawezaje kusema kwamba kazi ya hukumu ambayo Mungu atafanya wakati wa kurudi Kwake ni ya kuwatakasa na kuwaokoa watu?” Dada Qianhe alisema: “Mimi pia nilikuwa nikiamini maneno hayo ya padre. Nilikuwa na mawazo kama yako juu ya jinsi Bwana atakavyorudi kufanya kazi ya hukumu, lakini ninapofikiria hilo sasa, je, kile anachosema padre kinakubaliana na Bibilia kweli? Kimetegemezwa kwa neno la Mungu? Je, Bwana Yesu alisema kwamba kuna mahali pa mateso ya muda? Alisema chochote juu ya watu ambao hufanya dhambi ndogo kuwa na uwezo wa kupaa mbinguni baada ya kumaliza mateso yao mahali pa mateso ya muda, na kwamba ni wale tu ambao hufanya dhambi kuu ndio watakwenda kuzimuni? Bila shaka hapana! Kwa hivyo maneno haya yametoka wapi? Bila shaka yametoka katika mawazo na fikira za watu, na ni kisio na dhana za mwanadamu tu. Hayakubaliani kabisa na maneno ya Mungu, na hayakubaliani na ukweli wa kazi ya Mungu. Kuna faida gani kwetu kutetea jambo hili?” Niliposikiza ushirika wake, niliamkia kwa kichwa kimyakimya. Aliendelea: “Kwa sasa, sisi sote tumejawa na dhambi, na hakuna mtu aliye safi. Kulingana na yale ambayo padre alisema, Bwana atakaporudi kuwahukumu watu wote hadharani, wale wanaotenda dhambi ndogo watakwenda mahali pa mateso ya muda ilhali wale wanaotenda dhambi kubwa wataenda kuzimuni. Kwa hivyo, si sote tutahukumiwa na kupata adhabu ya kwenda kuzimuni? Basi si kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu itakuwa bure? Kutakuwa na maana yoyote katika kuja kwa Bwana?” Yale ambayo dada huyo alishiriki yaliugusa moyo wangu. Ni kweli—hata ikiwa tunamwamini Mungu, ikiwa yote tunayofanya ni kutenda dhambi mara kwa mara na kisha kuziungama, hakuna atakayetakaswa. Kwa kweli, hakuna mtu atakayefaa kumwona Mungu, na ikiwa Mungu amekuja kuhukumu, kushutumu, na kuwaadhibu watu hadharani, basi kila mtu atalazimika kwenda kuzimuni. Hakuna mtu anayeweza kupata wokovu…. Ni wakati huo tu ndipo nilipogundua jinsi ambavyo maneno yasemayo “Bwana atakapokuja tena kuhukumu watu wote hadharani, wale wanaotenda dhambi kubwa watakwenda moja kwa moja kuzimuni wakati ambapo wale ambao hutenda dhambi ndogo wataingia mahali pa mateso ya muda, na baada ya kumaliza mateso yao watapaa mbinguni, yasivyo ya kweli.” Hayapatani kabisa na mapenzi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu. Dada Qianhe kisha akasema: “Kwa mintarafu ya kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, acha sote tuangalie jinsi ilivyoelezwa katika neno la Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu asema: ‘Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa. Kabla ya hitimisho ya mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000—kabla ya Yeye kuweka wazi mwisho wa kila aina ya binadamu—kazi ya Mungu ulimwenguni utakuwa kwa ajili ya wokovu, yote haya ni ili kuwafanya wale wanaompenda Yeye kukamilika kabisa, na kuwarejesha katika utawala Wake. Bila kujali jinsi ambavyo Mungu huwaokoa watu, yote hufanywa kwa kuwafanya wajitenge na asili yao ya zamani ya kishetani; yaani, Yeye huwaokoa kwa kuwafanya watafute uzima. Wasipotafuta uzima basi hawatakuwa na njia yoyote ya kukubali wokovu wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu). ‘Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).”

Baada ya kusoma neno la Mungu, Dada Zhang Xiao alitoa ushirika, akisema, “Neno la Mwenyezi Mungu linafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, hali halisi ya hukumu, na matokeo ya kazi ya hukumu kati ya wanadamu yawe wazi kabisa. Kazi ya Mungu ya hukumu si ya kuwaua au kuwaadhibu watu kama ilivyo katika fikira na mawazo yetu. Badala yake, kazi hii hutumia neno kufichua mawazo, kauli, na vitendo vya watu, ili kuondoa asili zetu za kishetani zilizofanywa madhubuti kabisa na tabia potovu zinazompinga Mungu. Inaturuhusu tutambue ukweli wa jinsi ambavyo tumepotoshwa na Shetani huku pia ikituruhusu tujue tabia ya Mungu yenye haki na takatifu. Tunapopata ufahamu wa mambo haya, tunaanza kujichukia, na hii inasababisha toba ya kweli na moyo wa kweli wa kumcha Mungu. Kupitia hukumu ya neno la Mungu tunaweza kuelewa vizuri zaidi na kupata njia ya kufikia ukweli, na kuishi kwa kutegemea ukweli kwa urahisi. Kwa njia hii, vitu vyovyote vya shetani ambavyo tunavyo ndani vitaondolewa polepole, na tutaweza kupatana na Mungu. Kuanzia wakati huo hatutamwasi au kumpinga Mungu tena, lakini tutaweza kumtii kwa dhati—huku pekee ndiko kupata wokovu. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hatuna tena mfano wa mwanadamu na tunapoteza dhamiri na mantiki ambayo mtu mzuri anapaswa kuwa nayo. Badala yake, tumejawa na kiburi, kujiamini, ubinafsi, na vipengele vingine vya tabia ya kishetani. Mitazamo na fikira zetu juu ya mambo pia hazipatani tena na Mungu. Kwa mfano: Tunapokabiliwa na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, sote tuna mambo tofauti ambayo tunayakubali na sote tunashikilia fikira zetu wenyewe bila kujali kama kuna msingi katika neno la Mungu. Hatutafuti mapenzi ya Mungu, lakini tunaamini kwa upofu kuwa njia yetu ya kufikiria ni sahihi. Kazi ya Mungu inapokosa kukubaliana na fikira na mawazo yetu, sisi hufanya uamuzi wetu wenyewe kumhusu Mungu, na tunamkataa, tunamshambulia, na kumhukumu. Haya ni matokeo ya tabia yetu yenye kiburi. Tukiwa na asili kama hiyo ya kishetani sisi sote tuna uelekeo mkubwa wa kumpinga Mungu, kwa hivyo tunahitaji sana Mungu aje kutekeleza hatua ya kazi ya hukumu, na Atakase na kubadilisha tabia yetu ya kishetani. Bila hiyo, hakuna mtu atakayeweza kuwa huru kutokana na upotovu na kupata wokovu.”

Baada ya kusikiliza neno la Mwenyezi Mungu na ushirika wa dada huyu, moyo wangu ghafla ukawa mwangavu na wazi, na nilihisi kuwa mambo haya yalisemwa vizuri sana. Ingawa kulikuwa na mambo kadhaa ambayo sikuyaelewa kabisa, bado yalinipa utambuzi wa hekima iliyopo ndani ya kazi ya Mungu na pia kiasi cha upendo ambacho Mungu anacho kwa mwanadamu. Hapo zamani, ilipofikia Mungu kuja kuwahukumu wanadamu, nilidhani kwamba watu wangekwenda kuzimuni au kupitia mateso ya mahali pa mateso ya muda. Kwa kweli, kazi ya Mungu ya hukumu si kama tulivyofikiria hata kidogo, lakini badala yake, ni Mungu kuja mwilini kuonyesha ukweli na kutekeleza kazi ya hukumu. Hivi ndivyo Anavyowatakasa na kuwaokoa watu. Kazi ya Mungu ya hukumu ina maana sana. Ni kile ambacho sisi wanadamu wapotovu tunakihitaji hasa!

Nilipokuwa nikisikiliza haya yote kwa shauku kubwa, mume wangu alipiga simu ghafla akisema kuwa alitaka kutumia gari. Alipoona kwamba wakati huu niliweza kuyasikia haya yote, nilipokuwa karibu kuondoka alinipa kitabu kiitwacho Kitabu Chafunguliwa na Mwanakondoo na akasema kwamba maneno yaliyokuwamo ndani yake yalikuwa sauti ya Mungu Mwenyewe. Pia alinishauri sana nisome neno la Mwenyezi Mungu. Baada ya kurudi nyumbani, nilikuwa nikisoma kitabu hicho kila nilipokuwa na wakati. Kupitia kusoma neno la Mwenyezi Mungu, nilielewa ukweli mwingi na nikapata maarifa mengi. Wakati huo huo, pia nilipitia uchunguzi makini wa Mungu wa ndani kabisa ya mioyo ya wanadamu. Kila neno la Mwenyezi Mungu lilipenya ndani ya moyo wangu, likifunua asili yangu potovu ya ndani. Wakati mwingine nilipoona jinsi neno la Mungu linavyofichua upotovu wetu, nilihisi jinsi Anavyouchukia sana. Ilionekana kuwa Mungu anaonyesha hasira Yake kwetu, na moyo wangu uliokuwa wenye ganzi na usio na huruma ulisismuliwa mara moja. Nilikua na heshima kwa Mungu moyoni mwangu, na sikuwa tena kama vile nilivyokuwa hapo awali, wakati ambapo nilikuwa nimefanya dhambi bila woga. Kupitia uzoefu mwingi na nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu, niliona kwamba kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu inaweza kweli kuwaokoa watu kutoka dhambini na kuwaruhusu wajitenge na dhambi. Kazi na maneno ya Mungu ni ya vitendo kama nini! Nilihisi majuto makuu nilipokumbuka jinsi ambavyo nilikuwa nimeipinga kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa miaka miwili iliyopita. Nilijichukia kwa kuwa mpumbavu na mjinga sana, kutotafuta kuelewa au kuchunguza jambo kubwa kama ujio wa pili wa Bwana. Lakini la, nilisikiza uvumi huo pasipo kufikiria, nikamfungia Mungu nje, nikamshutumu Mungu, na nikampinga Mungu. Karibu nikose wokovu wa Bwana katika siku za mwisho. Kwa kweli nilikuwa kipofu sana! Niliona waziwazi kuwa kashfa, hukumu, na kufuru dhidi ya Mwenyezi Mungu na kuharibiwa jina kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu vilikuwa vyote uwongo kutoka kwa Shetani. Huo ni ujanja unaotumiwa na Shetani hasa kuwachanganya na kuwanasa watu mtegoni, na kuwazuia kukubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Sitaamini tena uwongo wa Shetani. Bila kujali nitakachokabili au kusikia katika siku zijazo, nitatambua kilicho sahihi na kilicho kibaya kulingana na neno la Mungu na ukweli. Sitasikiza tena uwongo na udanganyifu wa Shetani—ni kwa kufanya hivyo tu ndiyo mtu anaweza kupatana na mapenzi ya Mungu. Kwa kuzingatia haya, nilimshukuru Mwenyezi Mungu kwa dhati kwa ajili ya rehema na wokovu ambao Amenipa. Mungu hakuacha kuniokoa kwa sababu ya uasi na upinzani wangu, lakini Aliendelea kupanga watu waeneze injili kwangu na kunirudisha ndani ya nyumba ya Mungu. Upendo wa Mungu ni mkubwa jinsi gani! Kila wakati ninaposikia maneno ya video ya muziki iitwayo “Wimbo wa Upendo wa Dhati,” ambayo husema: “Kuna Mmoja ambaye ni Mungu mwenye mwili. Yote Anayosema, yote Anayofanya, ni ukweli. Napenda sana haki Yake, hekima Yake. Kumwona, kumtii, hakika ni baraka,” moyo wangu huguswa na kutiwa msukumo sana. Ninahisi jinsi nilivyo mwenye bahati kukaribisha kurudi kwa Bwana na kukutana na neno la Mungu moja kwa moja. Hii ni baraka kubwa kama nini!

Baadaye nilianza kushiriki katika maisha ya kanisa la Kanisa la Mwenyezi Mungu. Ndugu huimba nyimbo, hucheza, na kumsifu Mungu pamoja. Wao husoma neno la Mungu, na ikiwa kuna upotovu wowote wa kufichuliwa wao hutoa hisia zao na kufanya ushirika juu ya jambo hilo. Kila mtu hujadili maarifa na uzoefu wake kuhusu neno la Mwenyezi Mungu na kutafuta njia ya utendaji na kuingia. Maisha ya aina hii kanisani yanakomboa sana na ninapata msaada mkubwa kutoka kwayo. Nimegundua kweli kwamba ni kanisa tu kama hilo ambamo Roho Mtakatifu anafanya kazi ndilo linaloweza kuwa nyumba ya Mungu. Hapa ndipo ninapostahili kuwapo. Sasa nimeamua kabisa kuwa Mwenyezi Munguni ndiye ujio wa pili wa Bwana, na nimeazimia kumfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho kabisa!

Iliyotangulia: 25. Baada ya Kuelewa Ukweli wa Kutambua Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo, Sijihadhari Tena Bila Kufikiria

Inayofuata: 27. Kukutana na Bwana Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

12. Fumbo la Utatu Linafichuliwa

Na Jingmo, MalaysiaNilikuwa na bahati katika mwaka wa 1997 kukubali injili ya Bwana Yesu na nilipobatizwa, mchungaji aliomba na kunibatiza...

43. Kupotea na Kurejea Tena

Na Xieli, MarekaniNilikuja Marekani kufanya kazi kwa bidii kama vile ningeweza kutafuta maisha yenye furaha na hali ya juu ya maisha....

44. Nimerudi Nyumbani

Na Chu Keen Pong, MalasiaNilimwamini Bwana kwa zaidi ya muongo mmoja na kuhudumu kanisani kwa miaka miwili, na kisha nikaliacha kanisa...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp