25. Baada ya Kuelewa Ukweli wa Kutambua Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo, Sijihadhari Tena Bila Kufikiria

Na Xiangwang, Malesia

Kutoka nikiwa wa umri mdogo nimemfuata mama yangu, shemasi wa kanisa na mwalimu wa shule ya Jumapili, katika kumwamini Bwana. Mara nyingi nilihudhuria mikutano na kusoma Biblia pamoja naye, na nilipokuwa nikikomaa, nilijiunga na kikundi cha vijana kutoka kwa kikundi cha watoto.

Mchungaji aliyewajibikia kutoa mahubiri kwa kikundi cha vijana alikuwa daktari wa teolojia. Alituambia mara nyingi kwamba kuwa mchungaji hakukuwa rahisi na kwamba bila msukumo wa Roho Mtakatifu, ilikuwa vigumu sana kuvumilia katika kazi ya uchungaji. Kwa hiyo tulimpenda sana, tukimwamini kuwa yule ambaye Mungu alipendezwa naye na ambaye alipokea msukumo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Alipotuhubiria, mara nyingi angetumia mistari miwili kutoka Biblia: “Na basi mtu yeyote akiwaambia, Tazameni, Kristo yuko hapa; ama, tazameni, yuko pale; msimwamini: Kwani Makristo wasio kweli na manabii wasio kweli watatokea, na wataonyesha ishara na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata walioteuliwa(Marko 13:21-22). Angetuambia kwamba kungekuwa na Makristo wengi wa uongo wakitokea katika siku za mwisho na angetusihi tuwe waangalifu daima na tusiende na kusikiliza mahubiri wengine kwa kawaida tu. Hasa kwa wale kati yetu ambao bado hawakuwa na msingi thabiti katika Biblia na ambao vimo vyetu vilikuwa vidogo sana, alisema ingekuwa bora kwetu kutosikiliza, kusoma ama kuchunguza mahubiri yoyote yaliyohubiriwa na yeyote kutoka dhehebu lingine, ili kuepuka kudanganywa.

Kando na haya, mchungaji pia alitaja mara nyingi makanisa fulani ambayo tulilazimika kuepukana nayo kabisa, likiwemo Umeme wa Mashariki, na alitusimulia baadhi ya habari hasi ambayo ilikuwa ikienea kuhusu Umeme wa Mashariki. Wakati washirika wa kikundi changu walisikia hili, wote walisema kwamba wangeliepuka kanisa hilo. Mchungaji mara nyingi angetuhubiria kwamba, alimradi tusome Biblia mara nyingi, tuendelee kuhudhuria mikutano yetu kwa kawaida na kufanya ibada zetu za kiroho kwa kawaida, tukiri na kutubu dhambi zetu kwa Bwana kila siku na tukeshe kwa subira kila wakati, basi Bwana atakapokuja tungenyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Niliamini alichosema kabisa, sikuthubutu kuenda kwa kawaida kusikiliza mahubiri yaliyohubiriwa katika makanisa mengine, na kutenda kulingana kabisa na maagizo ya mchungaji. Kwa hiyo, nilihisi kwamba tayari nilikuwa nimehifadhi nafasi kati ya wale wanaosubiri kurudi kwa Bwana.

Siku moja mnamo Agosti mwaka wa 2017, Ndugu Hu kutoka kanisa letu alikuja kunitembelea shuleni kwa ghafla na kuniambia kwa sauti ya ari, “Nina jambo muhimu sana kukuambia. Inaonekana kana kwamba mamako na dadako sasa wanaamini katika Umeme wa Mashariki.” Nilishangaa niliposikia habari hii, na nikajiwazia: “Je, si mchungaji hutusihi kila siku tusijihusishe na Umeme wa Mashariki? Mamangu ameanzaje kuliamini?” Kisha Ndugu Hu aliniambia baadhi ya habari hasi kuhusu Umeme wa Mashariki, na nilivyozidi kusikiliza, ndivyo nilivyohofia na kuwa na wasiwasi zaidi. Sikuwa na budi kuwaza: “Naweza kufanya nini? Naweza kufanya nini?” Wakatii huo tu, Ndugu Hu alisema, “Harakisha uende nyumbani na umuulize mamako kama kweli ameanza kuliamini Umeme wa Mashariki. Lakini unapomuuliza, jifanye kwamba hujui chochote. Kwanza sikia atakachosema, kisha unipe rekodi ya mazungumzo yenu.” Kwa sababu nilihofia kwamba mamangu alikuwa amepotoka, nilikubali.

Hakika kabisa, punde tu niliporudi nyumbani mamangu aliniambia kwamba Bwana Yesu alikuwa amerudi tayari kama Mwenyezi Mungu na kwamba, katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu alikuwa akionyesha maneno mengi na alikuwa akitenda kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu ili kumtakasa na kumbadili mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu kabisa kutoka katika utumwa wa dhambi. Aliendelea kusema kwamba hii ilikuwa hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu na kwamba, ikiwa tungeikosa, hatungekuwa na nafasi nyingine ya kuokolewa. Alisema kwamba alitumai ningeharakisha kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kuhudhuria mkutano katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Aliposema hili, nilifikiria mara moja juu ya habari hasi kuhusu Umeme wa Mashariki ambayo Ndugu Hu alikuwa ameniambia kuhusu na nilihisi chuki kubwa sana kwa kile alichokuwa akisema. Lakini ili kurekodi mazungumzo yetu kwa siri, nilizuia hisia zangu na kuendelea kumsikiliza.

Siku iliyofuata, mamangu aliniomba niende mtandaoni kwa ajili ya mkutano na watu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu, lakini nilimkatiza mara moja na kusema, “Mama, sitahudhuria mikutano yao, na pia wewe hupaswi kuihudhuria tena. Unaonekana kuegemea kwao zaidi na zaidi.” Mamangu alijibu kwa upole, “Tangu nianze kuhudhuria mikutano na ushirika na ndugu zangu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu, nimepata umaizi mpya na ufahamu wa maneno ya Mungu katika Biblia, na nahisi hakika moyoni mwangu kwamba ushirika wao umejawa mwanga na kwamba unaibuka kutoka katika nuru ya Roho Mtakatifu. Aidha, maneno ya Mwenyezi Mungu yametatua mkanganyiko wangu mwingi, na sasa nina uhakika kabisa kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu kweli lina kazi ya Roho Mtakatifu na kwamba maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli….” Wakati huo, akili yangu ilijawa fikira kuhusu Umeme wa Mashariki na singeweza kabisa kukubali chochote alichosema mamangu. Baadaye, nilienda mtandaoni kumwonyesha mamangu baadhi ya habari hasi kuhusu Umeme wa Mashariki ambayo Ndugu Hu alikuwa ameniambia kuhusu, na nikasema, “Unaona mama? Yamesemwa waziwazi kabisa hapa mtandaoni, na mchungaji wetu hutuambia mara nyingi tusichunguze Umeme wa Mashariki pia. Tafadhali niambie hutahusiana na wao kuanzia sasa kuendelea.”

Mamangu hakuangalia hiyo habari hasi, lakini aliendelea tu kunizungumzia kwa subira, akisema, “Binti yangu mpendwa, serikali ya Kikomunisti ya China ni shirika linalomkana Mungu linalodharau kuonekana na kazi ya Mungu na humdharau yeyote aliye na imani ya dini. Huku Uchina, Ukristo na Ukatoliki unashutumiwa na serikali ya CCP kama dhehebu ovu, na Biblia inashutumiwa kama kitabu cha dhehebu ovu, huku nakala nyingi zikichomwa ama kuharibiwa, na sasa hata kimepigwa marufuku kuuzwa Uchina. Wakristo na Wakatoliki wengi wamekamatwa, kuteswa na kufungwa gerezani na serikali ya CCP, na wengine hata wamelemazwa ama kuuawa. Vikundi vya kimataifa vya haki za kibinadamu na mataifa ya magharibi yameshutumu kwa ukali serikali ya Kikomunisti ya China mara nyingi. Kweli unaweza kuamini maneno ya mfumo wa utawala wa kishetani unaompinga Mungu kama huu? Je, una sifa zinazostahili kukadiria na kushutumu kuonekana na kazi ya Mungu? Na kwa nini wachungaji na wazee hawaturuhusu kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Je, matendo yao yanakubaliana na mafundisho ya Bwana? Bwana Yesu alituambia, ‘Wamebarikiwa wao walio maskini kiroho: kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao(Mathayo 5:3). Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Bwana kwamba Bwana anatutaka tuwe wafuasi wanaokubali mawazo mapya wanaochunguza kwa ari tunapomsikia mtu akishuhudia kurudi kwa Bwana, kwani ni hapo tu ndipo tunaweza kukaribisha kurudi kwa Bwana. Binti yangu mpendwa, kama waumini wa Bwana, kwa nini tunasikiza maoni ya watu wengine lakini hatusikilizi maneno ya Bwana? Tukiamini kile ambacho mchungaji anasema na habari hasi inayotolewa na mfumo huo wa utawala wa kishetani, na tuwe wasioonyesha hisia na kujihadhari tunapomsikia mtu akishuhudia kurudi kwa Bwana, je, hilo linakubaliana na mapenzi ya Bwana? Kwa kufanya hivyo, je, si tunaenda dhidi ya maneno ya Bwana? Waumini wa Kiyahudi wakati wa Yesu hawakutafuta ama kuchunguza maneno na kazi ya Bwana, lakini badala yake waliamini uvumi uliobuniwa kumhusu Bwana na Mafarisayo, na kwa hiyo walimpinga na kumshutumu Bwana Yesu na hatimaye wakamsulubisha msalabani na wakaadhibiwa na Mungu kwa sababu hiyo. Lazima tujifunze funzo la kushindwa kwa Wayahudi na kuepuka kupoteza nafasi yetu ya kumkaribisha Bwana. Imetabiriwa mara nyingi katika Ufunuo: ‘Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa(Ufunuo 2,3). Kutoka katika mstari huu tunaweza kuona kwamba, Bwana atakaporudi, pia Ataonyesha maneno Yake, na ikiwa tunataka kukaribisha kurudi Kwake, basi lazima tujifunze kusikiliza sauti ya Mungu. Ni kwa kusoma na kuchunguza maneno ya Mwenyezi Mungu tu ndiyo utajua ikiwa ni sauti ya Mungu au la.” Baada ya kusema maoni yake, mamangu alikichukua kitabu chenye jina Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho na kunikabidhi.

Nilikiangalia kitabu kilichokuwa mikononi mwake lakini sikukichukua. Kwa sababu bado singekubali alichokuwa akisema, nilisema tu, “Sitaki kukisoma,” kisha nikageuka na kwenda katika chumba changu cha kulala.

Nikiwa nimeketi mezani pangu, nilipata tena utulivu wangu na kutafakari kuhusu kile ambacho mamangu alikuwa ametoka kusema. Nilijiwazia: “Kile alichosema mama kweli hakikuwa makosa. Umeme wa Mashariki linashuhudia kwamba Bwana amerudi, lakini nimekuwa tu nikiamini bila kufikiria kile mchungaji anasema na kuamini habari hasi iliyotolewa kuhusu Umeme wa Mashariki na serikali ya Kikomunisti ya China bila kusoma maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu. Nadhani kwamba hilo lilikuwa uamuzi wa kiholela kiasi kutoka kwangu. Ikiwa Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi na nikatae kumkubali, basi nitapoteza nafasi yangu ya kumkaribisha Bwana. Lakini mchungaji hutuhubiria kila siku kwamba Makristo wa uongo wataonekana katika siku za mwisho, na ikiwa nitapotoka, je, si imani yangu katika Bwana itakuwa bure?” Moyo wangu uliyumbayumba, na sikujua kabisa nimwamini nani, kwa hiyo nilimwita Bwana: “Ee Bwana! Nimetamani sana kurudi Kwako daima lakini sasa ninaogopa kudanganywa na Makristo wa uongo wanaoonekana katika siku za mwisho. Ee Bwana! Watu kutoka Umeme wa Mashariki sasa wanashuhudia kwamba Umerudi, kwa hiyo ikiwa kweli Umerudi kama Mwenyezi Mungu, basi nakuomba Unipe nuru na uniongoze, na uniruhusu niitambue sauti Yako.”

Siku iliyofuata, mamangu alinitia moyo tena nihudhurie mkutano wake mmoja. Baada ya kusita kiasi, niliamua kwenda mtandaoni na kusikiliza kile walichokuwa nacho cha kusema. Wakati tu mkutano ulikuwa umeanza, nilihisi mwenye wasiwasi sana na kweli sikusikiliza kile ambacho ndugu hao walikuwa wakishiriki kuhusu. Baadaye, Ndugu Zhang alitoa ushirika kuhusu vipengele vya ukweli kama vile mpango wa Mungu wa usimamizi wa kuwaokoa wanadamu, siri ya hatua tatu za kazi ya Mungu na vilevile kazi ya hukumu ambayo Mungu hutenda katika siku za mwisho; moyo wangu ulivutiwa na kadiri nilivyozidi kusikiliza, ndivyo yote hayo yalihisi kuwa mapya zaidi. Ingawa nilikuwa nimehudhuria madarasa ya mafunzo ya Biblia awali, wahubiri walikuwa wamezungumza tu kuhusu asili ya miujiza ya kazi ya Mungu kwa kutaja miujiza Aliyotenda, ama vinginevyo kuzungumza kuhusu jinsi watakatifu wa zamani walikuwa wamemtii Mungu ili kutimiza maagizo ya Mungu, na kadhalika. Hawakuwahi taja hata mara moja chochote kuhusu mpango wa Mungu wa usimamizi wa kuwaokoa wanadamu. Ushirika wa Ndugu Zhang uliniruhusu kupata ufahamu kiasi kuhusu kazi ya Mungu ya kuwasimamia wanadamu; haya yote yalikuwa mambo ambayo sikuwa nimewahi kuelewa awali licha ya kusoma Biblia kwa miaka mingi sana. Kufikia wakati ambao mkutano uliisha, nilikuwa nimebadili mawazo yangu. Niliamua kwamba kwanza ningechunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na kwamba ningefuta rekodi niliyochukua ya mazungumzo yangu na mamangu.

Wakati wa mkutano wetu katika siku ya tatu, tulijadili tofauti kati ya wanawali wenye busara na wanawali wapumbavu. Ndugu Zhang alisema, “Wanawali wenye busara ni wenye busara kwa sababu wanatamani sana kuonekana kwa Mungu na wanajua jinsi ya kuisikiliza sauti ya Mungu. Wao ni werevu, wana ubora wa tabia, na ni watu wanaopenda na kutafuta ukweli. Kwa hiyo, wanaposikia habari kwamba Bwana amekuja, wanatafuta na kuchunguza kwa ari—watu kama hawa hawawezi kudanganywa na Makristo wa uongo. Wanawali wapumbavu hawapendi ukweli, hawazingatii kusikiliza sauti ya Mungu, wala hawajui jinsi ya kufanya hivyo; wamechanganyikiwa na hawana utambuzi, na kuhusu kuja kwa Bwana, wanaweza tu kushikilia fikira na mawazo yao wenyewe tu kupinga na kushutumu kazi ya Mungu. Kwa mfano, ndugu wengine hawaweki umuhimu wowote juu ya kusikiliza maneno ya Bwana katika kumwamini kwao, lakini badala yake wanaamini kile ambacho wachungaji na wazee husema. Chochote wasemacho wachungaji na wazee, hiki ndicho wanachoamini, na ingawa wanamwamini Bwana kwa jina, kwa kweli wanafuata na kuwatii wachungaji na wazee. Kisha kuna ndugu wengine wanaolenga tu kujihadhari dhidi ya Makristo wa uongo bila kufikiria, na hawatafuti ama kuchunguza hata wanapomsikia mtu akieneza habari kuhusu kurudi kwa Bwana—je, si huku ni kama kuacha kula kwa sababu ya hofu ya kukabwa? Je, watu kama hawa wana uwezo wa kukaribisha kurudi kwa Bwana?”

Maneno ya Ndugu Zhang yalinipa mlipuko wa ghafla wa utambuzi, na nikawaza, “Hiyo ni kweli! Kwa muda mrefu sasa, nimeamini kile ambacho mchungaji wangu huhubiri, na sijachunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Ikiwa Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi, basi kwa nini sijafunuliwa kama mwanamwali mpumbavu? Bwana Yesu alisema, ‘Ombeni, na mtapatiwa; tafuteni, na mtapata; pigeni hodi, na mtafunguliwa(Mathayo 7:7). Daima nimengojea kwa hamu kukaribisha kurudi kwa Bwana na sasa Kanisa la Mwenyezi Mungu linashuhudia kwamba Bwana amerudi. Napaswa kuwa mwanamwali mwenye busara na nitafute na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa ari, kwani ni hilo tu linalokubaliana na mapenzi ya Mungu.” Na kwa hiyo, niliamua kuendelea kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.

Katika mkutano siku iliyofuata, niliuliza, “Ndugu, ulishiriki jana kwamba cha muhimu katika kuwa mwanamwali mwenye busara ni kulenga kuisikiliza sauti ya Mungu. Nahisi kwamba sasa nina njia ya kufuata ili kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, lakini mchungaji wangu husema mara nyingi katika mahubiri yake kwamba Makristo wa uongo wataonekana katika siku za mwisho ili kuwadanganya watu, kwa hivyo tunapaswaje kutambua kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo? Sielewi kipengele hiki cha ukweli, kwa hivyo nimekuwa nikiwaza ikiwa unaweza kushiriki ushirika wako nami?”

Ndugu Zhang alisema, “Swali ambalo umeuliza ni muhimu kwani linahusiana moja kwa moja na iwapo tunaweza kukaribisha kurudi kwa Bwana au la. Alimradi tunaweza kuelewa ukweli kuhusu kutambua kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo, basi bila kujali jinsi Makristo wa uongo wanaweza kujaribu kujifanya kuwa Mungu, tutabaki wasiodanganywa nao. Kuhusu jinsi ya kutambua kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo, Bwana asema, ‘Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi(Mathayo 24:23-24). Maneno ya Bwana yanatuambia waziwazi kwamba Makristo wa uongo katika siku za mwisho mara nyingi watatumia ishara na miujiza kuwadanganya watu. Kwa sababu Makristo wa uongo hawana ukweli na kiini chao ni kile cha roho wabaya na pepo, wanaweza tu kuiga kazi ya zamani ya Mungu na kutenda ishara na miujiza kiasi rahisi, ama vinginevyo waeleze Biblia vibaya ili kuwachanganya watu kwa nadharia za kunga. Kristo pekee ndiye ukweli, njia na uzima, na ni Yeye pekee anayeweza kuonyesha ukweli, atuonyeshe njia na kutupa uzima. Wote wajiitao Kristo lakini ambao hawawezi kuonyesha ukweli, hakika ni Makristo wa uongo na walaghai, na hii ndiyo kanuni ambayo kwayo tunaweza kuwa na upambanuzi wa msingi wa Makristo wa uongo.”

Baada ya kusikiliza ushirika wa ndugu huyu, kwa uangalifu nilisoma kifungu hiki cha Maandiko tena na kisha yote yakawa dhahiri ghafla: “Ndiyo, kweli Biblia inasema kwamba Makristo wa uongo watatenda ishara na miujiza kubwa ili kuwadanganya watu. Je, basi wale wachungaji ambao wametopea sana katika Biblia wamekosaje kuona kanuni hii ambayo kwayo tunaweza kutambua Makristo wa uongo?”

Kisha Ndugu Zhang alituma kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu: “Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. … Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo).

Ndugu Zhang alitoa ushirika, akisema, “Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya mwenyezi Mungu kwamba Mungu ni mpya daima na kamwe si Mungu mzee, na Hajawahi kufanya kazi sawa mara mbili. Kila wakati Mungu huanzisha hatua mpya ya kazi, Anaonyesha maneno mapya na humpa mwanadamu njia mpya ya kutenda. Kwa mfano, Bwana Yesu alipokuja, Hakurudia kazi ya kutangaza sheria na amri, lakini badala yake Alitumia kazi hiyo kama msingi wa kutenda kazi ya kuwakomboa wanadamu wote, na Aliwapa watu wa wakati huo njia mpya za kutenda. Kwa mfano, Aliwafunza watu kukiri na kutubu, kuwapenda maadui wao, kujifunza kusamehe, kupendana, na kadhalika. Sasa Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho na Haonyeshi njia ya toba tena, lakini badala yake Anatumia kazi ya ukombozi kama msingi wa kutenda kazi ya kuhukumu na kumtakasa mwanadamu kupitia maneno. Katika hatua hii ya kazi, Mungu hatendi ishara na miujiza, lakini badala yake Anaonyesha maneno Yake kwa matendo ili kufichua tabia zetu potovu na kuhukumu udhalimu wetu. Wakati uo huo, Mungu hutupa ukweli wote tunaohitaji ili kupata wokovu wa kweli na Anatuwezesha kuelewa njia ya mabadiliko ya tabia, ambayo kwayo tunaweza kutupilia mbali tabia zetu potovu na kuongozwa na Mungu hadi katika ufalme Wake. Kwa upande mwingine, Makristo wengi wa uongo wana roho wabaya na wote ni wenye majivuno na wapuuzi kabisa. Hawawezi kuanzisha enzi mpya, wala hawawezi kuhitimisha enzi, sembuse kuonyesha ukweli ili kuwaonyesha watu njia ya mabadiliko ya tabia. Yote wanayoweza kufanya ni kuiga kazi ya zamani ya Bwana Yesu na kutenda ishara na miujiza kiasi rahisi ili kuwadanganya watu. Hata hivyo, kuhusu miujiza mikubwa ambayo Bwana Yesu alitenda, kama vile kuwafufua wafu na kuwalisha watu elfu tano kwa samaki wawili na mikate mitano, Makristo wa uongo hawawezi kabisa kuiga vitendo hivi, kwani ni Mungu tu aliye na mamlaka na uweza kama huo, na Makristo wa uongo hawawezi kamwe kufanikisha mambo kama hayo.”

Ni kupitia tu ushirika wa ndugu huyo ndiyo nilipata kuelewa kwamba kazi ya Mungu ni mpya daima na kamwe si nzee, na Makristo wa uongo wanaweza tu kuiga kazi ya zamani ya Mungu na kutenda ishara na miujiza kiasi rahisi. Hata hivyo, hawawezi kufanya kazi ya Mungu, na alimradi tuelewe kanuni za kazi ya Mungu, basi hatutadanganywa. Zamani, nilihofia daima kudanganywa na kwa hiyo sikuthubutu kusikia mahubiri yoyote ya Umeme wa Mashariki, sembuse kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Badala yake, niliishi maisha ya kujitenga kanisani, nikasikiliza mahubiri hapa na kumsifu Bwana, nikifikiria kwamba hiyo ilikuwa njia salama zaidi ya kufuata, na kwamba ningepatanishwa na Bwana baadaye. Hata hivyo, nikifikiria hili sasa, kuwa asiyeonyesha hisia na kujihadhari sana na kutotafuta kwa ari matamshi ya Bwana katika siku za mwisho kweli kulinifanya wa kuelekea kupoteza nafasi yangu ya kumkaribisha Bwana.

Ndugu Zhang aliendelea na ushirika wake, akisema, “Mungu ndiye ukweli, njia na uzima, na kando na kutambua kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo kwa kanuni za kazi ya Mungu, pia tunaweza kuwatambua kwa kiini cha Kristo.” Wakati huo, Ndugu Zhang alituma kifungu cha maneno ya Mungu: “Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale wanaojifanya kuwa Kristo wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele).

Ndugu Zhang aliendelea na ushirika wake, akisema, “Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Mungu kwamba Kristo ndiye kupata mwili kwa Roho wa Mungu—Ana kiini kitakatifu, Anatenda kazi ya Mungu, Anaonyesha tabia ya Mungu, Anaweza kuonyesha ukweli ili kumruzuku na kumwongoza mwanadamu wakati wowote na mahali popote, na Kristo pekee ndiye anayeweza kutenda kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kwa mfano, Bwana Yesu alikuwa Kristo, na kuonekana na kazi Yake yalihitimisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema. Pia Alizungumza maneno Yake ili kuwapa wanadamu njia ya toba, kuwawezesha kujua wazi mapenzi na mahitaji ya Mungu na kuwapa njia ya kufuata ugumu unapoibuka. Kupitia katika maneno ya Bwana Yesu, mwanadamu alielewa jinsi ya kumwomba Bwana, jinsi ya kuelewana, jinsi ya kusameheana, na kadhalika. Aidha, Bwana Yesu alionyesha tabia Yake ya wema na rehema, Aliwaponya wagonjwa, kufukuza pepo na kumpa mwanadamu neema isiyo na mwisho. Mwishowe, Alisulubiwa ili kuwakomboa wanadamu, hivyo kukamilisha kazi ya kuwakomboa wanadamu wote na kutuokoa kutoka kwa pingu na minyororo ya sheria, na vilevile kutuokoa kutoka katika hatari ya kushutumiwa na kuuawa kwa ajili ya kukiuka sheria. Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo Bwana Yesu alifanya, na hakuna mtu mwingine ambaye angeweza kuyafanya badala Yake. Kutoka kwa kazi na maneno ya Bwana Yesu, tunaweza kuona kwamba Yeye ndiye ukweli, njia na uzima. Vivyo hivyo, Mungu amepata mwili tena katika siku za mwisho na amehitimisha Enzi ya Neema na kuanzisha Enzi ya Ufalme. Ametamka mamilioni ya maneno, Anatenda kazi ya hukumu na utakaso, na Anaonyesha tabia ya haki ya Mungu ambayo ni ya uadhama, hasira na isiyokosewa. Maneno yaliyonenwa na Mwenyezi Mungu yanafichua siri za mpango mzima wa Mungu wa usimamizi na kikomo na hatima ya mwisho ya mwanadamu, na pia yanaeleza kwa uwazi kamili ukweli tunaohitaji ili kutakaswa na kupata wokovu wa kweli kulingana na mahitaji yetu. Kwa mfano, Anaeleza jinsi Shetani anavyompotosha mwanadamu, ukweli wa upotovu wa mwanadamu mikononi mwa Shetani, jinsi Mungu anavyohukumu na kutakasa tabia potovu za mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kumwamini Mungu na kumtii Mungu, jinsi Mungu anampenda mtu wa aina gani na Yeye anachukia na kumwondoa mtu wa aina gani, jinsi tunavyopaswa kufuatilia ili kukamilishwa na Mungu, na kadhalika. Kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, tunaona dhahiri asili na chanzo cha kupotoshwa kwetu na Shetani na tunapata kuelewa tabia ya Mungu yenye haki, takatifu na isiyokosewa. Hatuna budi basi kuanguka sakafuni mbele za Mungu kwa majuto ya kweli, tunakuwa wenye heshima na watiifu zaidi na zaidi kwa Mungu, na taratibu, tunatupilia mbali tabia zetu potovu za kishetani, kujiweka huru dhidi ya pingu za dhambi na kupata wokovu wa kweli wa Mungu. Matamshi na kazi ya Mwenyezi Mungu hutuletea ukweli, njia na uzima—Mwenyezi Mungu ni Mungu Mwenyewe na Yeye ni Kristo aliyepata mwili. Makristo wa uongo hawana kiini cha Mungu na hawawezi kuonyesha ukweli, sembuse kutenda kazi ya kuwaokoa wanadamu. Wanaweza tu kutoa matangazo ya hadaa ili kuwadanganya na kuwadhuru watu. Mtu anapowasikiliza, hawapati ruzuku yoyote tu, lakini zaidi ya hayo, moyo wake unakuwa mwovu zaidi na zaidi, unazama chini zaidi na zaidi, hana pahali pa kugeukia, na bila kuepukika anaishia kuteketezwa na Shetani. Kwa hiyo, tunaweza kuhakikisha kutoka kwa matamshi ya Mungu, kazi na tabia ambayo Mungu huonyesha iwapo Yeye ni Kristo mwenye mwili.”

Baada ya kusikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wa ndugu, nilielewa kabisa ukweli wa jinsi ya kutambua kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa uongo. Kristo pekee ndiye ukweli, njia na uzima, na Kristo pekee ndiye anayeweza kuonyesha ukweli na kutenda kazi ya Mungu Mwenyewe. Wote wajiitao Kristo lakini wasioweza kuonyesha ukweli na wasioweza kutenda kazi ya kumwokoa mwanadamu ni Makristo wa uongo. Hatimaye niligundua njia ya kuelekea mbele na sikujihadhari na kutoonyesha hisia tena kwa hofu ya kudanganywa na Makristo wa uongo. Shukrani ziwe kwa Mungu!

Baada ya hapo, Ndugu Zhang alinipa ushirika kuhusu ukweli mwingine, kama vile siri ya kupata mwili, tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, maelezo ya ndani ya Biblia, na zaidi. Nilivyozidi kusikiliza, ndivyo nilivyohisi kutosheka zaidi, na nilikuwa na hamu kila siku kuhudhuria mikutano na ndugu. Kila wakati ambapo mkutano uliisha, mimi na mamangu tungejadili mwangaza mpya tuliopata kupitia mkutano huo, na polepole, nilipata kuwa na ufahamu kiasi kuhusu kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Baada ya muda wa kutafuta na kuchunguza, nilikuwa na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu kweli alikuwa Bwana Yesu aliyerudi. Kisha nilianza kueneza injili na kuwaambia watu hata zaidi waliotamani kuonekana kwa Mungu habari kuhusu kurudi kwa Bwana.

Baadaye, mimi na mamangu tulienda katika kanisa letu la zamani kuhudhuria ibada ya Ijumaa. Baada ya mkutano kuisha, nilishangaa mchungaji alipoanza kucheza video ambayo ilitoa mashtaka ya uongo dhidi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilipoona uvumi uliobuniwa na kashfa zilizotolewa dhidi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, nilikasirika, na nikawaza: “Kanisa la Mwenyezi Mungu haliko jinsi wanavyosema hata kidogo. Hawajawasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu wala hawajachunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Wanawezaje kuhukumu kazi ya Mungu bila msingi na kiholela sana?”

Baada ya video kuisha, mchungaji, mashemasi wawili na washirika wawili wa baraza la kanisa waliniomba mimi na mamangu tubaki nyuma. Mchungaji alituuliza, “Ninyi wawili sasa ni waumini wa Mwenyezi Mungu?” Tulijibu, “Ndiyo.”

Punde tuliposema hili, shemasi mmoja aliamka kwa ghafla, na huku akimwelekezea mamangu kidole, akasema kwa ukali, “Kwa hiyo sasa unamwamini Mwenyezi Mungu? Kuanzia kesho, huruhusiwi tena kufundisha shule ya Jumapili. Kesho alasiri, nitakuja nyumbani kwako na kuchukua fedha ya kanisa.”

Mamangu alisema, “Unaweza kuzichukua wakati wowote utakapo.”

Mchungaji akauliza kwa hasira, “Dunia nzima ya dini inapinga na kulishutumu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa nini ushikilie kuwasiliana nao?”

Mamangu alijibu vikali, akisema, “Mchungaji, je, dunia ya dini ina ukweli? Je, Bwana Yesu aliwahi kusema kwamba ni kwa kufuata tu dunia ya dini ndiyo tunaweza kumkaribisha Bwana? Bwana Yesu alipoonekana na kutenda kazi Yake miaka hiyo yote iliyopita, viongozi wa Kiyahudi walikataa kutafuta ama kuchunguza kazi Yake wao wenyewe, na pia waliwakomesha waumini kuikubali, na hata wakabuni uvumi kumhusu Bwana Yesu, wakimpinga, kumhukumu na kumkufuru kwa hasira. Mwishowe, waliikosea tabia ya Mungu na kwa hiyo wakalaaniwa na kuadhibiwa na Mungu. Tukifuata unachosema, kwamba njia yoyote ambayo dunia ya dini inapinga na kushutumu siyo njia ya kweli, basi si hiyo itamaanisha kwamba unaikana hata kazi ya Bwana Yesu? Unakataa kutafuta ama kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa sababu dunia ya dini inalipinga na kulishutumu Kanisa la Mwenyezi Mungu—je, hili linakubaliana na ukweli? Kama mchungaji na mashemasi wa kanisa, kwa nini mnashutumu na kuihukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho kiholela bila hata kushughulika kuichunguza? Kupitia kusoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu, kwa kuona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ndiyo ukweli na kwamba ni sauti ya Mungu, tumekuwa na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi.” Nilishangaa walipopuuza kwa dharau kile ambacho mamangu alikuwa amesema na hawakukikubali hata kidogo.

Mamangu alifungua programu kwenye simu yake na kuwasomea maneno ya Mungu. Kisha mshirika mmoja wa baraza la kanisa alizungumza kwa majivuno sana na akasema maneno kiasi ya kukufuru kumhusu Mwenyezi Mungu. Mamangu alisema kwa hasira, “Wewe ni fidhuli kupindukia. Maneno haya ni ukweli—huwezi kuusikia? Huwezi kuielewa sauti ya Mungu unapoisikia? Kweli wewe ni kondoo wa Mungu?”

Wakiwa na tabasamu zisizo na furaha, walitutazama kwa maringo. Kisha mchungaji akasema kwa kiburi, “Tunayemsubiri ni Bwana Yesu aliye na majeraha ya msumari mikononi Mwake na Anayekuja na sura ya Myahudi. Kando na Bwana Yesu, hatutakubali chochote, hata kama kile ambacho Mwenyezi Mungu anaonyesha ni ukweli.” Tulipoona jinsi walivyokuwa wakaidi, mimi na mamangu tuliacha kujaribu kuwazungumzia. Niliona kwamba tabia yao ilikuwa sawa kabisa na ile ya Mafarisayo waliokuwa wamempinga Bwana Yesu; walimwamini Mungu lakini hawakutafuta ukweli, wala hawakulenga kuisikiliza sauti ya Mungu. Badala yake, walikuwa tu fidhuli na wenye majivuno, walishikilia fikira na mawazo yao kwa ukaidi na waliihukumu na kupinga kazi ya Mungu kiholela—kweli walikuwa wale walioonekana kumhudumia Mungu lakini ambao kwa kweli walimpinga.

Kisha mchungaji alitutishia, akisema, “Tutawapa mwezi mmoja kufikiria tena. Bado mkishikilia imani yenu katika Mwenyezi Mungu baada ya mwezi mmoja, nitawafukuza kutoka katika kanisa letu.”

Nilisema kwa hasira, “Hakuna haja ya kusubiri mwezi mmoja. Tufukuze tu sasa. Baada ya kutumia muda huu kutafuta na kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, tayari tuna uhakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Hatimaye tumeisikia sauti ya Mungu, kwa hivyo hata usipotufukuza, hatutarudi kuhudhuria mikutano katika kanisa hili kwa vyovyote vile.”

Mchungaji alipunguza sauti yake na kusema kwa ujanja, “Hilo haliwezekani. Tukiwafukuza sasa, ndugu watafikiria nini kutuhusu? Watasema kwamba tumewafukuza tu kwa sababu ya kuhudhuria mikutano kiasi mtandaoni, na basi tutaonekana katili kabisa. Baada ya mwezi mmoja, tutawaambia ndugu katika kanisa letu kwamba tumejaribu sana kuwashauri na kuwapa muda wa kutosha kufikiria tena, lakini mwishowe mlishikilia katika kumwamini Mwenyezi Mungu na kuamua kuliacha kanisa, na hapo tu ndipo tuliwafukuza.”

Nilipomsikia mchungaji akisema hili, nilihisi kuchukizwa, na sikutaka kuwaambia neno lingine. Kisha nikaanza kuondoka, nikimvuta mamangu pamoja nami. Tulipokuwa tu tukiondoka, mchungaji alitupa onyo: “Ni shauri yenu iwapo mnamwamini Mwenyezi Mungu au la, lakini sitawaruhusu kuwa na mawasiliano yoyote na ndugu katika kanisa letu tena.”

Tulipoondoka kanisani, tayari ilikuwa imepita saa saba asubuhi. Nilipokuwa nikifikiria kuhusu kile kilichokuwa kimetendeka muda mfupi uliotangulia, sikuweza kuamini kabisa kwamba mchungaji, mhubiri ambaye daima tulimheshimu kwa sababu ya maadili na wema wake angeweza kutenda kwa njia hii. Wakati huo tu, maneno ya Mungu yalinijia akilini: “Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye ‘mwili imara,’ wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu).

Nilifikiri daima kwamba wachungaji na wazee walikuwa watumishi wa Bwana na kwamba wanapaswa kuwa na ufahamu bora wa Biblia na kukubaliana zaidi na mapenzi ya Mungu. Nilifikiri daima kwamba, Bwana atakaporudi, kweli wangeweza kumkaribisha Bwana. Singewahi kufikiri kwamba mchungaji aliposikia habari ya kurudi kwa Bwana, hangekosa tu kuitafuta ama kuichunguza, lakini pia angegeuka kuwa mwenye kiburi na wa kujidai sana, akishikilia fikira na mawazo yake kwa ukaidi, na kwamba angemhukumu na kumshutumu Mungu na kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Hakuwa kabisa na moyo unaomcha Mungu, kiasi kwamba chini ya kisingizio cha “kulinda kondoo,” aliwazuia na kuwakomesha waumini dhidi ya kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho kwa ajili tu ya kudumisha hadhi na riziki yake mwenyewe. Kwa wale waumini ambao hawakukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, wachungaji na wazee waliishia kuwaogofya kwa vitisho vya kufukuzwa kutoka katika kanisa na hata kuwafanya wale ndugu wengine katika kanisa lao wawakatae ili wasiweze kuwahubiria ndugu zao injili. Walikuwa wabaya na waovu kweli! Ili kudumisha vyeo na riziki zao, Mafarisayo wakati wa Yesu walimpinga na kumshutumu Bwana kwa ukali na kumsulubisha msalabani. Wachungaji na wazee wa leo wana kiini sawa kabisa na Mafarisayo—wao ni wapinga Kristo ambao wamefunuliwa na kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na ni pepo wanaoteketeza nafsi za mwanadamu. Wakati huo, hatimaye nilielewa kabisa kwamba mtu anapomwamini Mungu bila kumjua Mungu na kazi Yake, basi bila kujali jinsi anavyoonekana kuteseka ama jinsi anavyoonekana kujitumia, daima atampinga Mungu na kuikosea tabia ya Mungu kwa kutegemea tabia zake fidhuli na zenye maringo za kishetani.

Wakati huo, sikuwa na budi ila kuonyesha shukrani na sifa kwa Mungu moyoni mwangu. Nikifikiria nyuma, nilikuwa nimedanganywa na sura nafiki ya wachungaji na wazee na daima nilikuwa nimewapenda mno, kuwafuata na kuwatii. Ilipofika suala la kumkaribisha Bwana, hata nilikuwa nimefuatana nao na kumpinga Mungu. Mungu kufichua asili yao ya kweli kuliniruhusu kuona, hatimaye, kiini cha pepo cha wachungaji na wazee kinachochukia ukweli na kumchukia Mungu, na kisha niliweza kupita matata mengi waliyokuwa wameniwekea na kukaribisha kurudi kwa Bwana. Kweli nampa Mungu shukrani kwa kuniokoa, na ninataka kufuatilia ukweli kwa ari kwenye njia ya imani katika Mungu ili niweze kulipiza upendo wa Mungu!

Iliyotangulia: 24. Ni Nani Aliye Kizuizi kwenye Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni?

Inayofuata: 26. Kufungua Mlango wa Moyo Wangu na Kukaribisha Kurudi Kwa Bwana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

13. Sauti Hii Yatoka Wapi?

Na Shiyin, ChinaNilizaliwa katika familia ya Kikristo, na jamaa wangu wengi ni wahubiri. Nilimwamini Bwana pamoja na wazazi wangu tangu...

3. Kufichua Fumbo la Hukumu

Na Enhui, MalasiaJina langu ni Enhui; nina umri wa miaka 46. Ninaishi Malaysia, nami nimekuwa mwumini katika Bwana kwa miaka 27. Mnamo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp