27. Kukutana na Bwana Tena

Na Jianding, Amerika

Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki, na tangu nikiwa na umri mdogo mamangu alinifunza kusoma Biblia. Wakati huo, Chama cha Kikomunisti cha China kilikuwa kikijenga tena taifa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, na wakati CCP kilipokuwa kikikandamiza dini zote, nilikuwa na umri wa miaka 20 kabla hatimaye nipate fursa ya kuenda kanisani na kusikiza mahubiri. Kasisi alituambia mara kwa mara: “Sisi Wakatoliki lazima tukiri dhambi zetu kwa njia inayofaa na kutubu. Ni lazima tufanye mema, siyo mabaya, na tuende kwenye Misa daima. Katika siku za mwisho, Bwana atakuja na kumhukumu kila mtu na kuwapeleka watu mbinguni au kuzimu kulingana na jinsi ambavyo wametenda na kufanya duniani. Watenda dhambi wakubwa zaidi wataadhibiwa kuzimu milele, ilhali wale wanaotenda dhambi ndogo wanaweza bado kuenda mbinguni alimradi wakiri dhambi zao kwa Bwana na kutubu. Mtu yeyote ambaye hamwamini Bwana hataenda mbinguni kamwe, bila kujali jinsi alivyo mzuri.” Kila wakati niliposikia hili, daima nilijipongeza kwa kuwa na bahati nzuri ya kuwa mshirika wa mkusanyiko wa waumini wa Katoliki kutoka kuzaliwa. Daima ningejiambia kufuatilia kwa nguvu, kuhudhuria Misa zaidi, na kukiri dhambi na kutubu kwa Bwana zaidi, na kwa njia hiyo ningeenda mbinguni na si kuteseka kuzimu. Kwa hivyo hapo ndipo nilikuza azma ya kuenda kanisani na kushiriki katika Misa mara kwa mara. Wakati huo, kasisi alituambia pia kwamba mnamo mwaka wa 2000 Bwana angerudi, na habari hii ilitufanya kusisimka sana. Kwa hiyo sote tulianza kufuatilia kwa ari, tukisubiri kurudi kwa Bwana. Lakini mwaka wa 2000 ulifika na kuenda na hatukuona ishara yoyote ya kurudi kwa Bwana. Wengi katika mkusanyiko wetu walipoteza imani yao, na watu wachache zaidi na zaidi walihudhuria kanisani kwa ajili ya Misa. Pia nilihisi kuchanganyikiwa, lakini bado nilihisi kwamba imani yangu katika Bwana haingetikiswa, bila kujali kile wengine walifanya. Hiyo ilikuwa hasa kwa sababu kumekuwa na nyakati nyingi ambapo nimekuwa katika hatari na Bwana alikuwa amenilinda na kufanya hatari hiyo kupotea. Bila ya ulinzi wa Bwana ningekufa kitambo, kwa hiyo singekuwa bila shukrani kiasi cha kupoteza imani kwa Bwana.

Katika miaka iliyofuata nilisikia kutoka kwa watu walionizunguka kwamba Amerika ilikuwa “mbingu duniani,” na kwa hiyo shauku kubwa ya kuja hapa ilikua ndani yangu. Mnamo Desemba 2014 mimi na familia yangu nzima tulihamia Amerika, lakini uhalisi wa maisha hapa haukuwa kama taswira nzuri niliyokuwa nayo akilini mwangu. Mwanzoni, kila kitu Amerika kilionekana kigeni na hatukumjua mtu yeyote. Mazingira na hali ya nchi hiyo yalikuwa tofauti sana na kile nilichozoea Uchina, na punde mwili wangu ukaanza kulalamika. Nilihisi mnyonge na mlegevu mara nyingi, lakini madaktari hospitalini hawakuweza kupata chochote kibaya na mimi. Sikujua cha kufanya, kwa hiyo nilianza kuomba kwa uaminifu hata zaidi kwa Bwana, nikitumai kwamba Bwana angenilinda. Niliomba zaidi na kuanza kutafuta kanisa ambapo ningehudhuria Misa na hatimaye nilipata kanisa la Wakristo wa Kichina. Lakini baada ya kuenda katika kanisa hilo mara kadhaa niligundua kwamba halikuwa tofauti sana na kile kilichokuwa kikiendelea katika jamii ya kawaida: Washirika wa mkusanyiko walikuwa kirafiki kwa juu juu lakini uingiliano wao uliongozwa na mamlaka na pesa. Huku nikikabiliwa na aina hii ya hali kanisani, nilipoteza moyo sana. Nilijiwazia: “Ee Bwana, Utarudi lini? Utakaporudi, watu wema watatenganishwa na watu waovu na dunia itakuwa imetakaswa.” Ingawa bado niliendelea kwenda kwenye Misa sikuwahi kuhisi uwepo wa Mungu kanisani, na hili lilinifanya kuvunjika moyo na kuhuzunika na kuathiri imani yangu katika Bwana. Lakini siku moja mnamo Julai 2015, nilipokuwa nikifanya kazi nje ya jimbo, nilipigiwa simu na mke wangu. Aliniambia kwa msisimko: “Bwana amerudi. Anaonyesha maneno na kufanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho! Harakisha urudi ili tuweze kukubali kazi mpya ya Mungu pamoja.” Baada ya kusikia hili, singeweza kujizuia kushuku kiasi: Bwana amerudi? Hilo linawezekana vipi? Bwana atakaporudi kuhukumu dunia watu wema watatenganishwa na watu wabaya. Lakini sasa wema na wabaya bado wamechanganywa pamoja, kwa hiyo kwa nini mke wangu anasema kwamba Bwana amerudi? Je, mke wangu ameungana na madhehebu mengine? Tumekuwa Wakatoliki kwa muda mrefu zaidi wa maisha yetu, hatuwezi kupotoka sasa! Kwa hiyo kwa haraka nilimaliza kazi niliyokuwa nikifanya na kurudi nyumbani.

Nilipofika nyumbani nilimwuliza mke wangu: “Unajua vipi kwamba Bwana amerudi? Hujapotoka kutoka kwenye imani zetu za Katoliki, siyo? Unasema kwamba Bwana amerudi kufanya kazi ya hukumu, lakini sasa hivi watu wema na watu wabaya bado wamechanganywa pamoja kwa hiyo Bwana anawezaje kuwa amerudi tayari? Tunaweza kungojea kwa hamu kurudi kwa Bwana, lakini hatuwezi kutokuwa waaminifu Kwake!” Mke wangu alinisikiza na kisha akajibu kwa subira: “Usiwe mwenye wasiwasi sana. Nimegundua karibuni mwenyewe kuhusu kurudi kwa Bwana. Kwa sasa, Kanisa la Mwenyezi Mungu linashuhudia kurudi kwa Bwana na Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli kufanya kazi ya hukumu ambayo imeanza katika nyumba ya Mungu. Sijaelewa vizuri kuhusu maelezo ya kile kinachofanyika, lakini nimekuwa nikisoma mtandaoni maneno mengi ambayo Mwenyezi Mungu ameonyesha na niko na hakika kwamba yote ni sauti ya Mungu. Bwana alisema wakati mmoja: ‘Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Tunaweza kutambua iwapo Mwenyezi Mungu ni Bwana aliyerudi kwa kwenda katika Kanisa la Mwenyezi Mungu kuchunguza, siyo?” Kile mke wangu alichosema kilionekana kuwa cha maana, na kurudi kwa Bwana kufanya kazi ya hukumu ni jambo ambalo limetabiriwa katika Biblia, kwa hivyo haikuwa tatizo mimi kwenda naye katika kanisa kuangalia na kisha ningekata shauri.

Kufikia hili, mimi na mke wangu tulipanga kutembelea nyumba ya mmoja wa washirika wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, mwanamume aliyejulikana kama Ndugu Zhang. Ndugu Wang na Dada Li, na Wakatoliki wenza wengine pia walikuja. Kuona kwamba nilikuwa na watu wengine wengi kulituliza akili yangu sana. Baada ya mazungumzo kiasi ya adabu sote tuliketi chini na niliwauliza ndugu hili: “Kuhusu kurudi kwa Bwana ufahamu wangu ni huu: Wakati ambapo Bwana atarudi kufanya kazi ya hukumu, watu wema watatenganishwa na watu waovu. Kisha watu wema watakubaliwa mbinguni na Bwana na watakutana naye, ilhali waovu watapelekwa kuzimu na kuadhibiwa. Mnasema kwamba Bwana amerudi na Anafanya kazi ya hukumu, kwa hiyo mbona hatujaona yoyote kati ya mambo haya yakitokea?” Ndugu Wang akajibu: “Ndugu, maoni yangu yalikuwa sawa na yako yaani pia niliamini kurudi kwa Bwana kulimaanisha kwamba watu wema wangetenganishwa kutoka kwa watu waovu, kwamba watu wazuri wangeishi mbinguni milele na waovu wangeadhibiwa, na kama hatungeona hili likifanyika basi hilo lilithibitisha kwamba Bwana hakuwa amerudi. Lakini baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu nilitambua kwamba hilo ni fikira na mawazo yetu tu na si njia halisi ambayo Mungu anafanya kazi. Jinsi Mungu anavyofanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho ni jambo ambalo Mungu mwenyewe anapanga na kuandaa. Hekima ya Mungu iko juu zaidi kuliko mbingu, na machoni pa Mungu wanadamu ni wadogo kama doa la vumbi, kwa hiyo tunawezaje kuelewa kazi ya Mungu? Katika Biblia inasema: ‘Ni nani ambaye amemhimiza mbele roho wa Yehova? au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake, na kumfunza? Ameshauriwa na nani, na nani amemwagiza, na kumfunza njia ya haki, na kumfunza maarifa, na kumwonyesha njia ya ufahamu? Tazama mataifa ni mithili ya tone la maji ndooni, na wanahesabiwa kama chembe ndogo sana ya mizani: tazama visiwa ni mithili ya vumbi dogo’ (Isaya 40:13-15). Kila mmoja wetu anatumia ubongo wetu kufikiri, kwa hivyo tunaweza kuwazia kuhusu kazi ya Mungu kadiri tunavyotaka lakini Mungu hafanyi kazi Yake kamwe kulingana na mawazo yetu. Tukitumia mawazo kuweka vigezo kwa kazi ya Mungu basi hatutendi kwa kiburi mno? Kwa hiyo, Mungu anafanyaje kazi Yake ya hukumu? Anatenganisha vipi wema kutoka kwa waovu? Hebu tusome mafungu kadhaa ya maneno ya Mwenyezi Mungu kutusaidia kuelewa. Mwenyezi Mungu alisema: ‘Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli…. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). ‘Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). ‘Madhumuni Yangu katika kufanya kazi ya ushindi si tu kushinda kwa sababu ya ushindi, lakini kushinda ili kufichua haki na udhalimu, kupata ushahidi kwa ajili ya adhabu ya mwanadamu, kulaani waovu, na hata zaidi, kushinda kwa sababu ya kuwakamilisha wale walio radhi kutii. Mwishowe, wote watatengwa kulingana na aina, na mawazo ya wale wote waliokamilishwa yatajazwa na utii. Hii ndiyo kazi itakayokamilishwa mwishowe. Lakini waliojawa na uasi wataadhibiwa, kutumwa kuchomeka motoni na milele kulaaniwa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu). Tuna wazo kwamba kazi ya Mungu ya hukumu ni kutenganisha ngano na magugu moja kwa moja, mbuzi na kondoo, watumishi wema na watumishi waovu, kwa maneno mengine, kutenganisha watu wema na waovu na kuweka kila moja na aina yake yenyewe. Lakini tukifikiri kulihusu, kwa sasa kuna Wakristo zaidi ya bilioni 2 duniani kote—na wote wanasema wana imani ya kweli katika Mungu na wanampenda Mungu—kwa hiyo tunapaswa kutofautisha vipi wema na wabaya, wenye haki na waovu? Mungu akiamua kwamba wewe ni mwema na kwamba mimi ni mwovu, hakika sitakubaliana na hilo kwa sababu nitahisi kwamba mimi pia ni mtu mwema. Mungu akiamua kwamba mimi ni mwema na kwamba mtu mwingine ni mwovu, hakika hatakubaliana na hilo. Kwa hivyo tunawezaje kujua nani ni mwema na nani ni mwovu? Hatuwezi, kwa sababu sisi wanadamu hatuna kanuni au viwango vya kutathmini hili. Ikiwa Mungu angetutathmini hivi hakika hatungetii na tungekuwa na fikira kulihusu, kama vile kufikiri kwamba Mungu alikuwa mwenye upendeleo na hakuwa mwenye haki. Kwa hiyo kazi ya kuweka kila mmoja na aina yake ingeendelea vipi basi? Bwana anayerudi katika siku za mwisho ni Kristo wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu—anayetumia ukweli kufanya kazi ya hukumu. Kwa Wakristo wote, kufichua nani ni ngano, nani ni magugu, nani ni mbuzi, nani ni kondoo, nani ni watumishi wema, nani ni watumishi waovu, nani ni wanawali wenye busara, nani ni wanawali wapumbavu, kote kunafanywa kwa kutumia ukweli. Maneno ya Mungu humfichua kila mtu, na wanawali wenye busara ni wale wanaomwamini Mungu kweli na kupenda ukweli. Wanaposikia kwamba mtu anashuhudia kuja kwa Mungu wanaondoka na kulikubali na kuchunguza kwa vitendo maneno ya Mungu na kazi ya Mungu. Wanatambua sauti ya Mungu na kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na mwishowe wanapata utakaso na wokovu kupitia hukumu ya Mungu. Wakati wa misiba mikuu wana ulinzi wa Mungu na wanaweza kuendelea kuishi, na hatimaye wanapelekwa katika ufalme wa Mungu. Kinyume chake, kwa sababu wanawali wapumbavu hawapendi ukweli, kwa sababu wanasisitiza kushikilia fikira na mawazo yao au kuamini uvumi, kwa sababu hawatafuti au kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho—na wengine wao hata hufuata viongozi wa dini katika kumpinga na kumshutumu Mungu na kukataa wokovu wa Mungu wa siku za mwisho—watafichuliwa kama watenda maovu na kazi ya Mungu ya siku za mwisho na wataondolewa. Majaliwa yao yatakuwa kupitia adhabu wakati wa misiba mikuu. Kutoka katika hili, tunaweza kuona kwamba kazi ya Mungu ya kuweka kila mmoja na aina yake wakati wa siku za mwisho haifanywi kulingana na fikira na mawazo yetu. Badala yake, Mungu hutumia mbinu ya hukumu kufanya kazi ya kuwafichua watu, na tokeo la mwisho ni kwamba kila mtu anafichuliwa kikamilifu na kuwekwa na aina yake kulingana na iwapo anakubali ukweli au kupinga ukweli. Je, hii si hekima ya Mungu, kutopendelea kwa Mungu, haki ya Mungu hasa?”

Baada ya kusikiza maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wa Ndugu Wang, nilikumbuka kile kasisi katika kanisa letu alisema kuhusu “Wakati Bwana atakuja watu wema watatenganishwa na watu wabaya” na kutambua kwamba fikira hii ni isiyo yakini sana, isiyofaa sana, na hailingani na uhalisi wa kazi ya Mungu hata kidogo. Sote tunaishi katika dhambi, tunatenda dhambi na kutubu siku zote bila kuweza kuepuka mzunguko huu, kwa hiyo watu wema kweli ni nani? Wakati ambapo Bwana atarudi, kama hatujatakaswa dhambi zetu, tutaruhusiwa kuingia ufalme wa mbinguni? Kufikiria hili kulikuwa kama kuwasha mwanga moyoni mwangu, na nilimshukuru Bwana kwa ajili ya uongozi Wake. Ziara yangu haikuwa bure, kwa sababu sasa nilielewa kwamba Mungu hutenganisha mema na maovu kulingana na jinsi watu wanavyotendea ukweli. Kwa maneno mengine, watu ni wema au waovu kulingana na iwapo wanakubali na kutii hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu au la, na hii ni haki ya Mungu ikidhihirishwa kikamilifu. Mungu hutumia maneno na kazi kutenganisha ngano na magugu, kondoo na mbuzi, wanawali wenye busara na wanawali wapumbavu, waumini wa kweli na waumini wa uongo, wanaopenda ukweli na wanaochukia ukweli. Mungu ni mwenye hekima kweli! Hata hivyo, pia nilikumbuka kasisi akisema kwamba wakati ambapo Bwana anarudi kuwahukumu watu Anafanya hivyo mmoja baada ya mwingine, na dhambi za kila mtu pia zinaorodheshwa na kuhukumiwa moja baada ya nyingine, kabla ya Yeye kuamua kama mtu huyo ataenda mbinguni au kuzimu. Lakini sasa Mwenyezi Mungu anasema kwamba kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho inafanywa kupitia maneno Yake, kwa hiyo maneno haya yanatumiwa vipi kuwahukumu watu?

Kwa hiyo niliibua swali hili kwa kundi hilo na Ndugu Zhang akalijibu kwa kusoma mafungu mawili ya maneno ya Mwenyezi Mungu kwangu: “Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo Atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo hakungekuwa kazi ya hukumu. Je, upotovu wa wanadamu wote si ni sawa? Je, kiini cha wanadamu wote hakifanani? Kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu kilichopotoka, kiini cha mwanadamu kilichopotoshwa na Shetani, na dhambi zote za mwanadamu. Mungu hahukumu makosa madogo madogo ya mwanadamu na yasiyokuwa na umuhimu. … bali anawahukumu wasio na haki wote miongoni mwa wanadamu—upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, kwa mfano, au mwanadamu kutomcha Yeye, au kusababisha usumbufu katika kazi ya Mungu, na kadhalika. Kile kinachohukumiwa ni kiini cha mwanadamu cha kumpinga Mungu, na kazi hii ni kazi ya ushindi ya siku za mwisho(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili). “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Kisha Ndugu Zhang alishiriki hili na mimi: “Tuna fikira kwamba wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho Atamwita kila mtu kuja mbele ya kiti Chake cheupe cha enzi na kisha Atamhukumu. Itampasa kila mtu kupiga magoti sakafuni na kisha kukiri kila dhambi zake zilizotendwa katika maisha yake yote. Kisha Mungu ataamua iwapo kila mtu ataenda mbinguni au kuzimu kulingana na ubaya wa dhambi zake. Tunafikiri kwamba Mungu huwahukumu watu kulingana na dhambi kama vile kuwadhulumu watu kimwili au kwa maneno, kutowatii wazazi, kuiba na kupora, nk. Lakini kwa kweli kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho haijihusishi na mienendo hii ya nje au dosari za tabia ambazo tunazo lakini badala yake inalenga kuhukumu asili ya shetani ya wanadamu ya kumpinga Mungu na kila tabia potovu. Hizi ni pamoja na kiburi na kujipenda kwetu, kutokuwa waaminifu na ujanja wetu, ubinafsi na ubaya wetu, ulafi na uovu wetu, n.k. Pia tuna maoni mengi ambayo hayalingani na Mungu, fikira nyingi za dini zilizopitwa na wakati na mawazo ya kikabaila. Haya mambo yote ni chanzo cha upinzani wetu kwa Mungu. Ni shida ambazo ni za kawaida kwa wanadamu wote wapotovu, na hivyo ni vitu ambavyo kazi ya Mungu ya hukumu inalenga kutakasa na kubadili. Kwa hiyo, maneno ambayo Mungu huonyesha yanafichua asili na kiini cha wanadamu na kila mtu mpotovu duniani ni sehemu ya hili, bila yeyote kuachwa. Au kulielezea kivingine, maneno ya Mungu yanalengwa kwa wanadamu wote na kwa hiyo hakuna haja ya kuwahukumu watu binafsi. Kwa kuyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu tunaweza kuelewa ukweli mwingi na kuona dhahiri asili, kiini chetu, na hali halisi ya sisi kupotoshwa na Shetani. Kufanya hili kutaturuhusu pia kutambua tabia ya Mungu ya haki na kukuza mioyo inayomcha Mungu na kujidharau ili tuwe radhi kusaliti mwili wetu na kutenda ukweli. Kwa njia hii, tabia yetu potovu ya shetani itatakaswa polepole na maoni yetu na mtazamo kuhusu maisha yatabadilika pia. Tunapoanza kuishi kwa maneno ya Mungu, tunapokoma kupinga na kumkana Mungu na badala yake tumtii na kumcha Mungu kweli na kuepukana na maovu, basi tutapata wokovu wa Mungu na kuwa watu wanaolingana na nia za Mungu. Hii ndiyo hali halisi na, na kusudi la, Mungu kuonyesha ukweli ili kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho.”

Baada ya kusikiza ushirika wa Ndugu Zhang, nilihisi kwamba kazi ya Mungu ya hukumu ni ya utendaji sana na imewekwa katika msingi wa uhalisi! Niliweza kukubali alichosema, na nilikielewa ndani sana ya moyo wangu. Ndiyo, watu wana kiburi, wanatafuta umaarufu na mali na hadhi, na wanaishi katika tabia zao mbalimbali potovu. Mungu hutumia hukumu ya maneno Yake kutuondolea sisi uchafu na upotovu wote ulio ndani yetu. Asili yetu ya kumpinga Mungu inatatuliwa hivyo na tabia yetu potovu inabadilishwa, na tunakuwa watu wazuri kweli. Kuangalia kwa njia hii, ningeweza kuona kwamba wazo hili ambalo kasisi alizungumzia kuhusu watu kuhukumiwa binafsi na dhambi kuhukumiwa moja baada ya nyingine wakati Bwana atakaporudi kuwahukumu wanadamu ni fikira na mawazo ya binadamu tu na hakuna uhusiano na namna ambavyo Mungu anafanya kazi Yake kwa kweli. Maneno ya Mwenyezi Mungu kweli yana ukweli; kweli ni sauti ya Mungu! Kile nilichosikia siku hiyo kilinifanya kuamua kuchunguza kikamilifu kazi ya Mwenyezi Mungu.

Katika uchunguzi wangu, nilitazama idadi fulani ya filamu za injili zilizotungwa na Kanisa la Mwenyezi Mungu, ikiwemo Siku za Nuhu Zimekuja, Siri ya Utauwa, na Nimewahi Treni ya Mwisho, na vilevile video fulani za nyimbo za maneno ya Mungu kama Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu. Pia nilisoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu na kuwasikiza ndugu wakishiriki kuhusu kila kipengele cha ukweli. Hili lilinisaidia kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi! Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli na ni Bwana aliyerudi ambaye tumekuwa tukimsubiri! Nilikuwa na furaha sana kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.

Tangu kuamini katika Mwenyezi Mungu nimekuwa nikikutana na ndugu zangu mara nyingi au kusikiza mahubiri nao, na sasa kila siku nahisi furaha na kuhisi kwamba napata riziki ya roho. Nafurahia faraja inayokuja kutoka kwenye kazi ya Roho Mtakatifu, na ninaanza kuelewa ukweli zaidi na zaidi. Katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, ndugu wanajuana wote na ni waaminifu wenyewe kwa wenyewe, na hakuna mtu anayejaribu kumdanganya mtu mwingine au kujihadhari. Watu wote ni sahili, wawazi na waaminifu, na hata wakati wanapofichua tabia zao potovu kila mmoja anaweza kujijua kupitia maneno ya Mungu na kutafuta ukweli kutatua tabia zao potovu. Kwangu, wao ni ndugu wa kweli wa Kikristo. Kile kinachonivutia hasa ni video za nyimbo, video za muziki, video za densi na nyimbo, filamu za injili, n.k. zilizotungwa na Kanisa la Mwenyezi Mungu, ambazo zote zinaheshimu ukweli sana na kumshuhudia Mungu na kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Kusudi la tungo hizi zote ni kuwasaidia watu kumtii Mungu, kumwabudu Mungu, na kanisa kweli linahisi kama mahali ambapo Mungu anafanya kazi Yake! Kile ambacho nimeona, kusikia, na kupitia ni thibitisho kwa moyo wangu kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu ni kanisa la kweli ambapo Mungu mwenyewe anaelimisha na kuongoza kondoo Wake binafsi. Ukweli kwamba nimeweza kuingia katika nyumba ya Mungu na kuishi ana kwa ana na Mungu unamaanisha kwamba nimeinuliwa kipekee na Mungu. Kweli nina bahati sana! Asante, Mwenyezi Mungu!

Iliyotangulia: 26. Kufungua Mlango wa Moyo Wangu na Kukaribisha Kurudi Kwa Bwana

Inayofuata: 28. Kupenya Ukungu ili Kuona Mwanga

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

32. Ufanisi

Na Fangfang, ChinaSote katika familia yangu tunamwamini Bwana Yesu, na wakati nilikuwa muumini wa kawaida tu katika kanisa letu, babangu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp