29 Ufalme wa Mungu Umetimizwa

1

Kristo wa siku za mwisho Ananena maneno,

siri za ufalme zinasemwa.

Sote tunasikia sauti ya Mungu

na tunainuliwa mbele ya kiti Chake.

Tunafurahia kunyunyiziwa.

Tunahudhuria karamu ya harusi ya Kristo,

tunafurahia malezi kutoka kwa maneno ya Mungu.

Kwa furaha watu wote wa Mungu wanang’aa.

Haya ni maji ya uzima, mana iliyojaa manufaa.

Tunafurahia maneno ya Mungu ya uzima.

Mungu sasa Ameonekana kufanya kazi,

Akitimiza ndoto ya milenia mwanadamu.

Eh, ufalme wa Kristo,

nchi ya asali na maziwa.

Eh, ufalme wa Kristo,

nchi yenye furaha ya haki na raha.

Eh, ufalme wa Kristo,

nchi ya asali na maziwa.

Eh, ufalme wa Kristo,

nchi yenye furaha ya haki na raha.

2

Mwenyezi Mungu ananena ukweli,

tunaelekezwa katika ufalme wa Mungu.

Kanisa Lake ni ufalme wa Kristo,

Mungu yuko mamlakani duniani.

Wale wanaopenda ukweli wanasikia sauti ya Mungu,

wanauona uso Wake, wanamgeukia.

Na kila mmoja

wa watu wa Mungu ana furaha.

Watakatifu wa zamani wanazaliwa upya katika siku za mwisho.

Ni baraka wao kukutana na Mungu.

Wakifurahia maisha ya ufalme,

Watu wa Mungu wanaimba kwa bidii.

Eh, ufalme wa Kristo,

Hema la Mungu liko hapa.

Eh, ufalme wa Kristo,

Ahadi Zake zinakuwa kweli.

Eh, ufalme wa Kristo,

Hema la Mungu liko hapa.

Eh, ufalme wa Kristo,

Ahadi Zake zinakuwa kweli.

Nguvu za giza zaondolewa,

kwa kuwa maneno ya Mungu ndiyo mwanga wa kweli.

Mungu anamhukumu mwanadamu kwa maneno Yake,

mataifa na watu wanatii.

Watu wote wa Mungu wanatakaswa.

Tunalitukuza jina takatifu la Mungu.

Tunakusanyika kwa furaha,

ulimwengu unasherehekea.

3

Watu wa Mungu wanamfukuza Shetani.

Tunapata ukweli na kuwekwa huru.

Kuwa pamoja na Mungu

kunatufanya tuwe na raha na furaha.

Maafa makubwa yanauharibu

ufalme wa Shetani,

na umetokea duniani

ufalme wa haki na mtakatifu.

Eh, msifu Mwenyezi Mungu,

Ameupata ufalme Wake, Amekuja.

Eh, msifu Mwenyezi Mungu,

mapenzi ya Mungu yametendeka.

Eh, msifu Mwenyezi Mungu,

Ameupata ufalme Wake, Amekuja.

Eh, msifu Mwenyezi Mungu,

mapenzi ya Mungu yametendeka.

Iliyotangulia: 28 Tunakusanyika kwa Furaha Kumsifu Mungu

Inayofuata: 30 Shukrani na Sifa kwa Mwenyezi Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp