Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

266 Ee Mungu, Moyo Wangu Tayari ni Wako

1

Ee Mungu, Maneno Yako yote ni ukweli. Ufunuo wa maneno Yako unaniwezesha kujiona vizuri zaidi.

Ingawa nilikuwa nikitangaza kwa sauti upendo wangu Kwako, nilijitolea Kwako, na kuacha vitu kwa ajili Yako, leo najua kwamba yote yalikuwa ili kupata baraka na taji.

Nahisi majuto sana moyoni mwangu, na ni jambo la kudharauliwa sana kufanya mikataba na Wewe.

Kuadibu na usafishaji Wako ni ili kunitakasa na kuondoa uchafu katika upendo wangu.

Ee Mungu! Moyo wangu unakupenda daima. Sasa najua tabia Yako ya haki.

Maneno Yako mema yameandikwa moyoni mwangu. Nataka kukupenda milele.

2

Ee Mungu, Maneno Yako yote ni ukweli. Maneno Yako ni msingi wa maisha yangu.

Kupitia mateso, shida, majaribu na usafishaji, Maneno Yako daima yako pamoja nami.

Naachwa na kumbukumbu nzuri za miaka ya shida na maumivu, uzuri Wako unabaki moyoni mwangu daima.

Maneno Yako yameikamilisha imani yangu, sitawahi tena kufa moyo au kukata tamaa.

Ee Mungu! Moyo wangu unakupenda daima. Haki yako kweli ni ya kupendeza.

Maneno Yako mema yameandikwa katika moyo wangu. Nataka kukupenda milele.

3

Ee Mungu, Maneno Yako yote ni ukweli. Ni Wewe unayenitakasa na kuniokoa kwa maneno Yako.

Maneno Yako ni ya thamani sana, yamekuwa maisha yangu na kuujaza moyo wangu.

Maneno Yako yote yametimizwa na kufanikishwa, utakatifu Wako na haki vinaonekana duniani.

Ee Mungu! Moyo wangu ni Wako, nina upendo mwingi sana wa kukuambia kuhusu.

Ee Mungu! Moyo Wangu unakupenda daima. Wewe tu ndiye mzuri zaidi, wa kupendeza zaidi.

Maneno Yako mema yameandikwa moyoni mwangu. Nataka kukupenda milele.

Iliyotangulia:Nimeona Moyo wa Mungu Ndio Unaopendeza na Karimu Zaidi

Inayofuata:Mwishowe Naweza Kumpenda Mungu

Maudhui Yanayohusiana