249 Upendo wa Mungu

I

Katika bahari hii ya watu,

nani anajua kuwa Mungu amekuwa mwili katika siku za mwisho?

Anatembea kanisani, akinena na kufanya kazi Yake,

akieleza ukweli kwa kimya.

Mnyenyekevu na aliyejificha.

Anavumilia aibu kubwa.

Ee Mungu! Unakuwa mwili

na kupitia taabu za aina zote kwa sababu ya wokovu wa binadamu.

Kwa nini binadamu wanakukana Wewe kila wakati?

Ee Mungu, ukweli Wako ni njia ya uzima wa milele.

Maneno Yako ni ukweli, njia na uzima.

Hayo ni upendo na baraka kwa mwanadamu.

Baada ya kupitia hukumu na mateso mengi,

tunatakaswa na kuishi kama binadamu wa kweli.

Hukumu ya Mungu ni wokovu na ni baraka Yake.

Mungu anastahili upendo wa mwanadamu na sifa za milele.

Asante kwa upendo Wako, asante kwa upendo Wako,

asante kwa upendo Wako, ee Mungu.

II

Katika bahari hii ya watu,

sisi ni kama chembe moja ya mchanga pwani,

bila yeyote wa kutujali au kutusikiliza

tuliishi katika dhambi na kupambana kwa uchungu,

tukitafutatafuta gizani, bila kuwa na mwelekeo maishani.

Ni Mungu ndiye aliyetuona sisi,

ni Mungu ndiye aliyetuinua juu.

Tumepotoshwa kwa kina na Shetani,

tukapakwa madoa kama uchafu na taka.

Ilhali Mungu hajatutupa,

badala yake Anatuhukumu, kutuadibu, na kututakasa,

Akiamsha mioyo yetu ilioganda

kuwa na utambuzi wa upendo Wake,

wa upendo na uzuri Wake.

Baada ya kupitia hukumu na mateso mengi,

tunatakaswa na kuishi kama binadamu wa kweli.

Hukumu ya Mungu ni wokovu na ni baraka Yake.

Mungu anastahili upendo wa mwanadamu na sifa za milele.

Asante kwa upendo Wako, asante kwa upendo Wako,

asante kwa upendo Wako, ee Mungu.

III

Katika hukumu ya maneno ya Mungu,

Naona upotovu wa ndani wa mwanadamu.

Wote wanakataa kuja kwa Mungu wa kweli.

Wanampinga Mungu na kuchukia ukweli.

Neno la Mungu ni mwangaza wa kweli, unamulika dunia ya giza.

Tumeona mwanga wa maisha ya mwanadamu na tumaini la binadamu.

Baada ya kupitia hukumu na mateso mengi,

tunatakaswa na kuishi kama binadamu wa kweli.

Hukumu ya Mungu ni wokovu na ni baraka Yake.

Mungu anastahili upendo wa mwanadamu na sifa za milele.

Asante kwa upendo Wako, asante kwa upendo Wako,

asante kwa upendo Wako, ee Mungu.

Iliyotangulia: 248 Nimemwona Mungu

Inayofuata: 250 Kutiwa Moyo na Upendo wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

132 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki