16. Neno La Mungu Ni Nguvu Yangu

Na Jingnian, Kanada

Nimefuata imani ya familia yangu katika Bwana tangu nilipokuwa mtoto, nikisoma Bibilia mara nyingi na kuhudhuria ibada. Nilishiriki injili ya Bwana Yesu na mama mkwe wangu baada ya kufunga ndoa, na tangu wakati huo hakukasirika tena mambo yalipofanyika au kutenda kulingana na mawazo yake ya ghafla kama alivyokuwa amefanya hapo zamani. Uhusiano katika familia yetu ulianza kuwa nzuri kwa jumla. Mume wangu alipoona mabadiliko ndani ya mama yake, alianza pia kumwamini Bwana mnamo mwaka wa 2015, na alienda kanisani pamoja nami kila wiki. Familia yangu ilikuwa na amani baada ya kukubali injili ya Bwana, na nilipoona hayo nilijua kuwa hii ilikuwa neema ya Bwana—nilimshukuru Bwana kwa dhati.

Nilipokuwa kazini siku moja mnamo Februari mwaka wa 2017, mteja wa kike aliniona na akasisimka sana. Alinivuta kando na kusema, “Unafanana sana na rafiki yangu. Naweza kukutambulisha kwake? Amekuja Canada hivi karibuni tu na hamjui mtu yeyote, ungependa kukutana naye ukiwa na wakati?” Nilishangaa sana kusikia hayo na nilifikiri: Je, kitu kama hicho kinaweza kutokea? Rafiki yake anafanana nami kweli? Lakini niligundua kuwa mapenzi mema ya Bwana yapo ndani ya vitu vyote, na kwamba kuwasaidia wengine kwa upendo pia ni moja ya mafundisho ya Bwana, kwa hivyo nikakubali ombi lake. Siku chache baadaye, nilikutana na rafiki yake Xiao Han, ambaye kwa kweli alifanana nami; watu waliotuona waliuliza ikiwa tulikuwa dada ambao ni pacha. Sijui ikiwa ni kwa sababu tulifanana sana au kwa sababu ya mipango ya Bwana, lakini nilipomwona, nilihisi kuwa karibu sana naye papo hapo. Tulikutana mara chache tu na tukawa kama dada ambao waliweza kuzungumza juu ya kitu chochote. Kilichonishangaza zaidi ni kwamba kupitia Xiao Han, nilisikia injili ya Bwana Yesu aliyerudi katika siku za mwisho.

Siku moja, Xiao Han alinipeleka nyumbani kwa shangazi yake, ambapo shangazi yake alishiriki nasi injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu. Alitutaka tusome maneno yaliyonenwa na Mungu katika siku za mwisho, na akashiriki nasi juu ya mapenzi ya Mungu katika uumbaji wa Adamu na Hawa, mawazo ya Mungu na kusudi Lake alipomwagiza Nuhu ajenge safina, jinsi moyo wa Mungu ulivyomuuma alipowaangamiza watu wa wakati wa Nuhu na mengine zaidi. Alisema kwamba siri hizi zote zinafichuliwa katika maneno ya Mungu ya siku za mwisho, vinginevyo hakuna mtu ambaye angeweza kuzielewa. Nilimwamini, kwa sababu ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kueleza mawazo yanayohusu kila kitu anachofanya. Mungu asingekuja binafsi kuzungumza na kufanya kazi, ni nani mwingine angeweza kufafanua kabisa mawazo na makusudi ya Mungu? Nilivutiwa sana na maneno ya Mungu, na niliamua kuchunguza kwa dhati kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Katika kipindi cha muda ambacho niliichunguza, niliibua maswali kadhaa ambayo sikuwahi kuelewa wakati ambapo nilisoma Biblia, na shangazi ya Xiao Han alinipa majibu kulingana na maneno ya Mwenyezi Mungu—majibu yale yalikuwa ya kweli, na yalikuwa dhahiri na yanayoeleweka kwangu. Nilipokuwa nikisoma maneno zaidi na zaidi ya Mungu, utata uliokuwa ndani ya moyo wangu ulitatuliwa polepole, na nikaja kuelewa kuwa katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anafanya kazi ya hukumu kupitia maneno Yake, jambo ambalo linatimiza unabii uliopo katika Bibilia kuwa “Lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Hatua hii ya kazi ya Mungu ni kuendelezwa na kuzidishwa kwa kazi ya Bwana Yesu, na ni hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu katika siku za mwisho ya kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu. Baada ya kuchunguza kwa muda, nilikuwa na hakika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerejea; nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa furaha na nikaanza kuhudhuria mikutano pamoja na ndugu.

Asubuhi moja baadaye kidogo ya miezi mitatu, nilikuwa nikikutana na dada wengine kama kawaida, wakati ghafla simu yangu ya rununu ilipoanza kulia. Niliangalia na nikaona taarifa kwamba mtu fulani alikuwa akijaribu kutafuta mahali nilipokuwa kwa kutumia iPhone yangu. Nilishangaa sana na sikujua kilichoendelea, lakini mara tu baada ya hapo, lakini mume wangu alinitumia ujumbe wa WeChat akiuliza, “Uko wapi?” Niliangalia ujumbe huo na nikasita kidogo; nilikumbuka kwamba, baada ya kurudi kutoka kwenye ibada ya kanisa zaidi ya mwezi mmoja uliopita, mume wangu aliniambia kwamba mchungaji alikuwa amesema mambo mengi mabaya kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, na aliwaonya waumini wawe macho na wasiwasiliane na watu kutoka Umeme wa Mashariki. Wakati huo, niliogopa kwamba mume wangu angepotoshwa na mchungaji na mzee wa kanisa, na kwamba uvumi wao ungemfanya alichukie Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilitaka kusubiri ili nishiriki injili naye baada ya kuelewa ukweli zaidi na kuweza kushuhudia waziwazi kazi ya Mungu ya siku za mwisho, kwa hivyo sikuthubutu kamwe kumwambia kuhusu mikutano yangu na kina dada wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa kuzingatia hilo, nilimjibu, “Niko njiani kuelekea kazini.” Lakini nilipofikiria tena, nilihisi kuwa kulikuwa na tatizo, “Hanitumii ujumbe wakati huu asilani. Kwa nini ananiuliza ghafla niko wapi leo? Kuna nini?”

Nilipofika nyumbani kutoka kazini jioni hiyo, nilimwona mume wangu akiketi kitandani akiwa ameukunja uso. Alikuwa amepata kitabu cha maneno ya Mungu ambacho nilikuwa nimekificha ndani ya nyumba, na alikuwa amekitandaza dawatini. Kuona hili kulinishangaza sana, lakini kabla ya kuwa na wakati wa kufikiri, mume wangu aliniuliza, “Ulianza kumwamini Mwenyezi Mungu lini? Kuna mambo mengi mabaya mtandaoni kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, hujui hilo? Ulinidanganya leo. Hukuwa njiani kuelekea kazini asubuhi ya leo. Ulikuwa wapi?” Nilijibu nikiwa nimeudhika kidogo, “Kwa hivyo simu yangu ilipoanza kulia leo ni kwa kuwa ulikuwa unajaribu kutafuta nilipokuwa!” Alisema, “Katika mapumziko yangu kazini asubuhi ya leo nilitaka kujua ulikuwa wapi, kwa hivyo nilitafuta mahali ulipokuwa na nikagundua hukuwa mahali uliposema ulikuwapo.” Alilainisha sauti yake na kuendelea, “Serikali ya China ilisema mtandaoni kwamba mipaka kati ya wanaume na wanawake haidumishwi waziwazi kati ya waumini wa Mwenyezi Mungu, na kulikuwa na vitu vingine fulani vibaya, pia. Tafadhali unaweza kutowasiliana nao tena? Itakuwa bora zaidi ukienda tu kwenye ibada za kanisa—naweza kwenda nawe kila wiki. Kwa nini una uhusiano wowote nao?” Baada ya kusema hayo alienda mtandaoni na akapata habari nyingi hasi juu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu ili nisome. Baada ya kusoma uvumi huo usio na msingi, nilisema kwa hasira, “Watu hawa hawajawahi kuwasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa nini wanapiga domo kulihusu? Haya yote hayana msingi kabisa, ni uvumi. Huu ni uwongo na uvumi na hauwezi kusadikika kabisa! Zaidi ya miezi michache iliyopita, nimekuwa karibu na ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kile nilichoona ni kwamba mavazi yao ni rahisi na ya kuvutia, na wanazungumza na kuishi kwa namna yenye heshima. Kuna mipaka dhahiri kati ya ndugu wa kiume na kike na kuna kanuni ya jinsi wanavyoingiliana. Wao si kama uvumi ambao serikali ya CCP na wachungaji na wazee wa kanisa hueneza. Moja ya amri za utawala ya Enzi ya Ufalme iliyotolewa na Mwenyezi Mungu inasema waziwazi, ‘Mwanadamu anayo tabia ya upotovu na, zaidi ya hayo, amejawa na hisia. Kwa hivyo, ni marufuku kabisa kwa watu wa jinsia mbili tofauti kufanya pamoja kazi wakati wa kumtumikia Mungu bila kuwepo na mtu mwingine. Yeyote yule atakayepatikana na kosa hili atatupiliwa mbali, bila ubaguzi—na hakuna atakayeepuka hili(“Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii” katika Neno Laonekana katika Mwili). Mungu ni mtakatifu na mwenye haki, na Anachukia tabia ya uasherati zaidi. Kwa hivyo, Mungu ametoa amri kali ya utawala kwa watu Wake wateule, na yeyote atakayezikiuka atafukuzwa kanisani. Ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu hufuata amri za Mungu za utawala kwa akali, na hakuna mtu anayethubutu kuzikiuka. Nimeona hilo na kulipitia mimi mwenyewe. Uvumi ulioenezwa na serikali ya CCP na wachungaji na wazee wa kanisa kwamba mipaka kati ya wanaume na wanawake wa Kanisa la Mwenyezi Mungu si dhahiri ni uwongo na kashfa tu!” Lakini bila kujali nilichosema, mume wangu hakusikiza, na alisisitiza kwamba nisiende tena kwenye mikutano pamoja na ndugu. Nilipoona jinsi alivyokosa kushawishika, nilianza kuhisi uhasi kiasi, kwa sababu mtu pekee ambaye tulisafiana nia katika eneo hili la kigeni ni mume wangu na sikutaka kugombana naye. Aidha, niliogopa kwamba angeambia familia yangu huko China na mchungaji, jambo ambalo lingenisababishia shida zaidi. Kwa hivyo, aliposisitiza nisiende kwenye mikutano, nilikubali, lakini nikasema kwamba nilitaka kuendelea kusoma maneno ya Mungu nyumbani; alikubali. Na kwa hivyo, dhoruba ikatulia kwa muda mfupi sana.

Kwa kuwa nilikuwa tu nikisoma maneno ya Mungu nyumbani peke yangu, kulikuwa na mambo mengi ambayo sikuelewa. Kwa hivyo, nilitumia simu yangu ya rununu kuwasiliana na dada fulani mume wangu alipokuwa kazini, jambo ambalo liliniruhusu niendelee kukusanyika na kina dada. Nilipowaambia dada zangu juu ya jinsi mume wangu alivyonizuia kuhudhuria mikutano, mmoja wao alinisomea kifungu cha maneno ya Mungu, “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. … Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Dada yangu alifanya ushirika, “Tunapokutana na kitu cha aina hii mara baada ya kumkubali Mwenyezi Mungu, kutoka nje inaonekana kwamba familia yetu inatuzuia na kutukataza kwenda kwenye mikutano, lakini tukiangalia jambo hilo kupitia maneno ya Mungu, ni vurugu la Shetani unaolisababisha: Hivi ni vita vya kiroho. Mungu anataka kutuokoa, lakini Shetani hataki kufa moyo kwa urahisi, kwa hivyo yeye humfuata Mungu nyuma ili kutuvuruga, na huwatumia watu waliotuzingira kutuzuia kuja mbele za Mungu. Lengo la Shetani ni kuharibu uhusiano wetu mzuri na Mungu, kutufanya tuhisi hasi na dhaifu ili tujitenge na Mungu na kumsaliti, na hatimaye kurudi kwenye miliki yake na kupoteza nafasi yetu ya kuokolewa na Mungu. Ndiyo maana lazima tujifunze utambuzi, tuangalie vitu kulingana na maneno ya Mungu, tubainishe hila za Shetani, tumwombe na kumtegemea Mungu zaidi, na tuwe na imani ya kweli katika Mungu. Kisha tutaweza kuona matendo ya Mungu kupitia imani yetu.” Baada ya kusikia neno la Mungu na ushirika wa yule dada, nilianza kugundua, “Mume wangu ananizuia kumwamini na kumfuata Mungu kwa sababu Shetani anamtumia kunivuruga na kunifanya nimsaliti Mungu—hii ni sawa na jaribio ambalo Ayubu alipitia. Shetani alijaribu kila mbinu aliojua kumjaribu Ayubu. Alimfanya apoteze utajiri wake mkubwa na kundi lake la ng’ombe na kondoo, Akamfunika kwa majipu ya kutisha, na akatumia marafiki wa Ayubu kumvuruga na kumshambulia. Alimtumia hata mkewe kumjaribu Ayubu ili amtelekeze Mungu. Shetani alijaribu kwa kiburi kuharibu imani ya Ayubu kwa Mungu na kumfanya amkane na kumkataa Mungu. Shetani ni mwovu na wa kustahili dharau kabisa!” Mawazo haya yalijaza moyo wangu chuki kwa Shetani, lakini wakati huo huo nikawaza, “Ingawa Shetani alimtesa Ayubu kwa hasira, kamwe hangethubutu kumdhuru Ayubu bila idhini ya Mungu, kwa hivyo si hiyo inamaanisha kuwa kile ninachopitia pia kiko mikononi mwa Mungu? Mradi nimtegemee Mungu na kumtumainia Mungu kwa kweli, hakika Ataniongoza kushinda majaribu ya Shetani.” Wazo hilo lilinipa imani zaidi katika Mungu, na niliamua kuendelea kuwasiliana na kina dada na kuendelea kuhudhuria mikutano na ushirika kupitia simu yangu ya rununu.

Usiku mmoja niliweka simu yangu mezani, bila kutarajia kwamba mume wangu angeichukua na kuikagua—aliona rekodi ya mazungumzo yangu na dada mmoja. Aliniambia kwa hasira, “Bado unawasiliana nao, na wewe huzungumza nao kwa saa mbili kwa wakati mmoja.” Kisha alinishambulia kwa propaganda zaidi zilizokuwa hasi ambazo zilikuwa mtandaoni, na kuanza kunifuatia kupitia njia mbalimbali. Sikuweza kuwasiliana na yule dada kwenye simu yangu tena. Na kwa hivyo hivi ndivyo nilivyopoteza maisha yangu ya kanisa tena na sikuweza kupata msaada wowote kutoka kwa dada huyo. Baada ya hapo, mume wangu alianza kunitumia uvumi aliopata mtandaoni siku nenda siku rudi, na pia aligombana nami na kunizuia kuwasiliana na kina ndugu. Nilipokabiliwa na dhuluma na kizuizi cha mume wangu, nilitaabika sana, na sikuwa na budi kuanza kuhisi dhaifu tena. Nilifikiri, “Kwa nini mume wangu anakataa kabisa nimwamini Mwenyezi Mungu? Nataka tu kumwamini Mungu, kwa nini ni vigumu sana? Nitaweza kutenda imani yangu lini bila kugombezwa sana? Je, haya yatakuwa maisha yangu kuanzia sasa na kuendelea?” Nilipofikiria hivyo sikuweza kabisa kuzuia machozi—nilihisi mpweke na asiyejiweza. Sikujua niende wapi kutoka pale. Siwezi hata kuhesabu ni mara ngapi nililia juu ya jambo hilo. Katika kutaabika kwangu, nilichoweza tu kufanya ni kumwomba Mungu, “Mungu! Sijui nifanye nini ninapokabiliwa na vizuizi vya mume wangu au jinsi ninavyopaswa kupitia haya, lakini ninaamini kuwa kwa hali yoyote ile, kuna mapenzi Yako mema. Nakuomba Uniongoze na Unipe imani ya kupitia haya.”

Kimuujiza, nilipomaliza tu sala yangu, nilipokea vifungu viwili vya neno la Mungu kutoka kwa yule dada, “Shetani yuko vitani na Mungu, akifuata nyuma Yake. Lengo lake ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka Kufanya, kuwamiliki na kudhibiti wale wote ambao Mungu anawataka, kuwafisha kabisa wale ambao Mungu anataka. Kama hawajafishwa, basi wanakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV). “Lazima uwe na ushujaa Wangu ndani yako na lazima uwe na kanuni wakati unakabiliana na ndugu wasioamini. Lakini kwa ajili Yangu, si lazima pia usikubali kushindwa na nguvu zozote za giza. Tegemea hekima Yangu ili kutembea kwa njia kamili; usiruhusu njama za Shetani kuchukua umiliki. Weka juhudi zako zote katika kuuweka moyo wako mbele Zangu, nami Nitakufariji na kukuletea amani na furaha(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 10). Kwa kutafakari maneno ya Mungu, nilipata utambuzi kiasi juu ya nia mbaya za Shetani. Mungu hufanya kazi ili kuwaokoa wanadamu huku Shetani akifikiria sana jinsi ya kuharibu kazi ya Mungu na hushindana na Mungu kwa ajili ya watu, kwa hivyo yeye hueneza uvumi wa kila aina mtandaoni ili kuwapotosha na kuwadanganya watu. Yeye pia hutumia familia zetu kutuzuia na kutusumbua ili tusiweze kuja mbele za Mungu kupokea wokovu. Mume wangu alikuwa amepofushwa na kudanganywa na uvumi ulioenezwa na Shetani kwa sababu hakujua ukweli, ndiyo sababu pekee alikuwa akizuia imani yangu kwa ukaidi. Shetani pia alikuwa ameelewa na kutumia udhaifu wangu kunizuia na kunidhuru. Shetani alijua kuwa udhaifu wangu mbaya ulikuwa hisia, kwa hivyo alikuwa akinishambulia kupitia hisia zangu kwa mume wangu, akinifanya niache kumfuata Mungu kwa sababu ya shauku yangu ya upendo na tamaa yangu ya mwili ya kulinda upatanifu wa familia, na hivyo niachane na njia ya kweli na kupoteza nafasi yangu ya wokovu wa Mungu. Shetani ni mwenye kustahili dharau kweli! Wakati huo huo, nilihisi Mungu akinifariji kwa maneno Yake, Akinitia moyo nisijisalimishe kwa nguvu za giza za Shetani. Mungu pia alikuwa akinipa njia ya utendaji. Mungu alisema, “Tegemea hekima Yangu ili kutembea kwa njia kamili.” Katika mazingira kama hayo, ningeshirikianaje na Mungu na kutumia hekima Yake kwenda mikutanoni? Nilikumbuka kuwa wakati uliopita mume wangu alikuwa ametumia simu yangu kunifuatia, kwa hivyo sikuweza tena kwenda katika mikutano nyumbani kwa dada, na sikuweza kutumia simu yangu kukutana naye pia, lakini ningeenda kukutana naye katika mojawapo ya maeneo yenye benchi katika jengo lenye maduka. Kama mume wangu angeniuliza tena, ningesema nilikuwa nikienda ununuzi dukani. Kwa hivyo, kwa mwongozo wa Mungu, niliweza kukutana naye tena. Mara alipokuja kuelewa shida zangu, alinipa ushirika juu ya maneno ya Mungu na alinifariji na kunitia moyo. Baada ya kuelewa ukweli, uhasi wangu uliondolewa haraka.

Siku moja, nilifika nyumbani kutoka kazini na nilitaka kusoma maneno ya Mungu; nilipekua kila dawati na kabati ambamo nilihifadhi kitabu changu kwa kawaida, lakini sikufaulu. Nilikuwa na wasiwasi sana na nikafikiri, “Haya! Mume wangu hakika alikitupa kitabu changu. Yeye ni mtu mwangalifu sana, kwa hivyo bila shaka hangekitupa kwenye pipa la taka ambapo naweza kukipata. Iwapo alikiondoa ofisini mwake, sitawahi kukipata.” Kufikiri hivyo kulinifanya niwe mnyonge, na sikujua la kufanya.

Nilikwenda pamoja na mume wangu kwenye mtihani wake wa leseni ya dereva siku chache baadaye na nikamuona dada mmoja huko. Nilimjulisha kwa siri kwamba kitabu changu cha maneno ya Mungu kilikuwa kimepotea. Aliniambia niombe zaidi, nimtegemee Mungu, na kutafuta tena kwa bidi sana. Mungu hudhibiti na kutawala vitu vyote, aliniambia, kwa hivyo ikiwa mume wangu alikuwa amekitupa kilikuwa mikononi mwa Mungu, na kwamba sifai kuyaruhusu mawazo yangu yawe bila mpango na kufanya uamuzi kwa haraka. Nilimtumia dada mwingine ujumbe kuhusu jambo hilo nilipofika nyumbani, ambaye aliniambia jambo lile lile. Baada ya kupokea ushirika ule ule kutoka kwa dada wawili tofauti, niliamini kwamba nia nzuri za Mungu hakika zilisababisha jambo hili. Je, Mungu alikuwa akiwatumia kina dada kunikumbusha? Kisha nikafikiria kifungu kutoka kwa maneno ya Mungu, “Mwenyezi Mungu Hutawala mambo yote na matukio yote! Mradi tunamtegemea mioyoni mwetu kila wakati na tuingie rohoni na kufanya ushirika na Yeye, basi Atatuonyesha mambo yote tunayotafuta na mapenzi Yake kwa hakika yatafichuliwa kwetu; mioyo yetu kisha yatakuwa katika furaha na amani, thabiti kwa uwazi kamili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 7). Nilielewa kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba Mungu yuko kila wakati ili watu wamtegemee na kupata msaada. Tunapokabiliwa na shida na kukosa suluhisho, mradi tumwite Mungu kwa kweli, Atatupa nuru na kutuongoza, na kutusaidia hadi mwisho wa shida zetu. Kwa msaada wa nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu, imani yangu katika Mungu imeimarishwa tena, na nilipata tena njia ya utendaji. Pia nilielewa kuwa kwa mintarafu ya suala la kupoteza kitabu changu cha maneno ya Mungu, singekipata kamwe iwapo ningetegemea tu juhudi zangu. Mungu ni mwenye nguvu zote, na mradi nimtegemee na kumtumainia Mungu, na kisha kushirikiana na Yeye katika njia ya kiutendaji kwenda kukitafuta, niliamini kuwa Mungu angeniongoza na kunisaidia. Kwa hivyo, nilikuja mbele za Mungu na kuomba kwa dhati, “Mungu! Siwezi kupata kitabu changu cha maneno Yako. Mwanzoni, nilitegemea fikira na mawazo yangu mwenyewe kubahatisha kile ambacho huenda kilitokea. Sikukuthamini kuliko vyote, na sikugundua kuwa kila kitu kiko chini ya udhibiti Wako. Sasa natamani kukutegemea na kukuaminia jambo hili, na kisha kushirikiana na Wewe katika utafutaji wangu unaofuata. Ikiwa nitapata kitabu hicho au la, hii itatokea kwa idhini Yako. Naomba mwongozo Wako.”

Baada ya kuomba nilikuwa na hamu ya ghafla ya kwenda kwenye chumba cha kuhifadhi kuchukua jozi ya viatu. Kwa mshangao wangu, nilipokuwa nikipiga magoti ili kuvichukua, nilipata mfuko mweupe, na wazo dhahiri likaingia akilini mwangu: Kitabu cha maneno ya Mungu kiko katika mfuko huu. Niliuchukua na nikaangalia, na ilikuwa kweli! Huku nikishangaa na kufurahi, sikuweza kujizuia kupaza sauti, “Shukrani kwa Mungu! Shukrani kwa Mungu!” Wakati huo tu ndipo niligundua kwamba ni Mungu aliyenielekeza kupata kitabu hicho. Niliona kwa kweli kuwa kila kitu kiko chini ya utawala wa Mungu, na kwamba Mungu hupanga fikira na mawazo ya watu, na kwamba hakuna kisichowezekana tunapomtegemea Mungu na kumtumainia. Nilirudisha kitabu hicho chumbani bila kupoteza wakati na kukiweka kwa uangalifu kwenye dawati langu. Jioni hiyo mume wangu aliporudi, aligundua kuwa nilikuwa nimepata kitabu cha maneno ya Mungu kilichokuwa kimefichwa katika chumba cha kuhifadhi na akataka nimkabidhi. Wakati huu, nilimtegemea Mungu kwa dhati na kumwomba anipe imani na nguvu. Nilikataa kuafikiana naye zaidi. Alipoona azma yangu, hakusihi zaidi.

Baadaye dada yule alinipa simu ya rununu ya kusikiliza tu mahubiri ambayo pia ilikuwa na maneno mengi ya Mungu yaliyokuwa yamepakuliwa; hii ilitakiwa kufanya iwe rahisi kwangu kuhudhuria mikutano na kufanya ibada zangu. Wakati mmoja nilipokuwa nikibadili mifuko, niliacha simu hiyo nyumbani kwa kutokuwa mwangalifu, na mume wangu akagundua kuwa nilikuwa nikihudhuria mikutano tena. Alinitumia ujumbe akitaka kujua, “Kwa nini bado unawasiliana nao? Kwa nini unakwenda mikutanoni kisirisiri?” Nilikasirika na kuwa na wasiwasi nilipoona ujumbe huu, lakini baadaye nikakumbuka uzoefu wangu katika kipindi cha wakati uliopita, jinsi ambavyo kila mume wangu alipojaribu kunizuia au kunionea, niliafikiana naye kila mara, nikaacha kufanya hivyo, au nikahisi hasi na dhaifu, na kwamba nilichokosa zaidi ni uwezo wa kumtegemea Mungu na kumshuhudia Mungu. Nilijua kuwa wakati huu singeshindwa na Shetani. Ningemtegemea Mungu, kumtumainia Mungu, kumshinda Shetani kupitia imani, na kuwa shahidi wa Mungu. Nilifikiria maneno ya Mungu, “Bila kujali ni wapi au wakati upi, au mazingira yako ni mabaya namna gani, Mimi nitakuonyesha kwa uwazi na moyo Wangu kufichuliwa kwako ukinitegemea Mimi kwa moyo wako; kwa njia hii utaikimbilia barabara iliyo mbele bila kupoteza njia(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 13). Kwa hivyo, nilimwomba Mungu, “Mungu! Sasa Umenichagua na Umeniruhusu nifuate nyayo Zako. Nisipofuatilia kwa nguvu zangu zote, nikisalimu amri kwa Shetani, nitapoteza nafasi yangu ya wokovu. Ee Mungu, ninatamani kukabidhi shida zangu za sasa. Hata mume wangu akiambia familia yangu au mchungaji kuhusu imani yangu katika Mwenyezi Mungu, au kitu kingine ambacho anaweza kunifanyia, nitakutii. Wakati huu, nitakutegemea ili kuwa shahidi Wako na kumwaibisha Shetani.”

Baada ya kuomba nilianza kuhisi mtulivu zaidi polepole. Nilichukua simu yangu na kumtumia majibu. “Naam, nahudhuria mikutano tena. Hebu tukae na kuwa na mazungumzo ya kweli juu ya jambo hili kesho jioni.” Mara nilipotuma ujumbe huo, bado nilihisi kuwa nilikuwa nikisafishwa: Ni kwa nini kila mara ninapotaka kufuatilia ukweli, mimi hukatizwa? Uzoefu wa Ayubu, ambao dada walishiriki nami mara nyingi kuuhusu, ulinijia akilini. Na pia nilifikiria yale ambayo Mungu alisema, “Na ni nini ambacho Mungu alifanya wakati Ayubu alipopitia mateso haya? Mungu aliangalia, na kutazama, na Akasubiri matokeo. Wakati Mungu Alipokuwa akiangalia na kutazama, Alihisi vipi? Alihisi kuwa mwenye huzuni, bila shaka(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II). Nilipima maneno ya Mungu, na nikafikiri juu ya uzoefu wa Ayubu. Aliishi maisha yake yote kumuogopa Mungu na kuepuka maovu, lakini Shetani hakuridhika kumruhusu Mungu ampate Ayubu, na kwa hivyo alimjaribu mara nyingi. Lakini wakati ule ule Shetani alikuwa akimjaribu Ayubu, Mungu alikuwa akichunguza na kutazama kila kitu, na Mungu alimpa Shetani upeo mkali: Shetani hangeweza kumuua Ayubu, na hivyo Alilinda usalama wa Ayubu. Niliweza kuona kwamba Mungu anawatunza watu, hataki tuteseke, na hataki kutuona tukishawishiwa na Shetani na kudhuriwa na Shetani. Aidha, mapenzi mema ya Mungu yalikuwamo ndani ya Yeye kumruhusu Shetani amjaribu Ayubu. Mungu alitarajia kupata ushuhuda kutoka kwa Ayubu na kukamilisha imani na utiifu wa Ayubu kwa Mungu. Je, si nilikuwamo hasa katika hali kama hiyo? Ingawa Shetani alinijaribu mara kwa mara, Mungu hakuwahi kuniacha, na Alikuwa ameniongoza hadi wakati huo. Mungu alipanga hali hizo akitumaini kwamba ningekua katika maisha, kuwa shahidi Wake, na kumwaibisha Shetani. Nilihisi tena imani zaidi katika Mungu na niliazimia kutii kile ambacho Mungu alikuwa amepanga, kusimama upande wa Mungu, na kamwe kutoafikiana tena na Shetani.

Jioni iliyofuata niliporudi nyumbani kutoka kazini, mume wangu alikuwa tayari akinisubiri. Nilipokaa chini, alisema, “Unaweza kuachana na imani yako kwa Mwenyezi Mungu?” Kisha akaanza kuongea juu ya kila aina ya uwongo juu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu ambao aliona kwenye mtandao. Jibu langu lilikuwa, “Hapana, siwezi. Unajua nini kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa kweli? Kila kitu ambacho umeona kwenye mtandao ni uvumi tu uliobunuiwa na serikali ya CCP ili kukashifu, kusingizia, na kushutumu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hakuna ulio kweli hata mmoja. CCP ni chama cha kisiasa kimkanacho Mungu ambacho kinachukia ukweli na Mungu, kwa hivyo hufanya kila liwezalo kubuni na kueneza uvumi wa aina zote ili kuwapotosha watu. Kinatumaini kuwadanganya watu ili wampinge Mungu na mwishowe waangamizwe pamoja nacho. Hio ndio nia mbaya ya serikali ya CCP. Lakini sijafanya chochote kibaya kwa kumwamini Mungu, wala sijafanya chochote kukusikitisha. Njia yangu ya imani ndio njia sahihi maishani, na nimeamua kuendelea kuitembea. Nimefikiria kiasi cha kutosha, na nimeamua kuwa unaweza kuwaita mchungaji na wahubiri, na kuwafanya wanishutumu katika mahubiri yao na kisha wanifukuze kanisani. Unaweza pia kuwapigia simu wazazi wangu na kuwafanya wanisute na kunidhalimu. Lakini bila kujali unachofanya, sitaghairi nia yangu. Sasa nimekubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na kupitia kusoma maneno ya Mungu na kupitia hali zilizopangwa na Mungu, nimekuwa na hakika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerejea. Nitaunga mkono chaguo langu bila kujali lolote.” Mume wangu alisema, “Unelewa kuwa unamsaliti Bwana, siyo? Bwana amekupa neema nyingi. Unawezaje kumsaliti?” Nikasema, “Kumwamini Mwenyezi Mungu si kumsaliti Bwana; ni kufuata nyayo za Mwanakondoo, kwa sababu Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu mmoja. Ni kwa sababu hasa nimefurahia neema ya Bwana Yesu sana ndio kwamba niliposikia habari kwamba Bwana Yesu amerudi, nilijua ni lazima nichunguze jambo hilo, na kisha nikalikubali. Bwana Yesu sasa amerudi katika mwili kunena maneno mapya, na kueleza kila kitu kuhusu kazi na mapenzi ya Mungu. Nimesikia sauti ya Mungu, kwa hivyo ninafaa kujitahidi hata zaidi katika ufuatiliaji wangu, kwenda kwenye mikutano zaidi, na kulipiza mapenzi ya Mungu kwangu.” Mwishowe mume wangu alisema, “Sawa, si kitu! Fanya unachotaka! Nilikuwa nimwambie mchungaji na kumfanya akushawishi urudi kanisani, na ningewapigia simu wazazi wako pia, lakini niliogopa kuwa wangesikitika sana kiasi kwamba wangeugua. Amini chochote unachotaka kuanzia sasa—sitahusika.”

Nilifurahi kumsikia mume wangu akisema kwamba hangezuia tena imani yangu katika Mwenyezi Mungu. Nilijua kuwa huu ulikwa mwongozo wa Mungu na kwamba moyo na mawazo ya mume wangu yalikuwa pia mikononi mwa Mungu. Maneno kama hayo yaliyotoka kinywani mwake yalikuwa kwa sababu ya utawala wa Mungu; ni Mungu ambaye alikuwa amenifungulia njia. Niliona kupitia uzoefu huu kwamba Mungu anataka moyo wangu, na ninapomtegemea, kumtumainia, na kuhatarisha kila kitu ili kumridhisha kwa kweli, ninaona matendo ya Mungu, na kwamba kila wakati Amekuwa akiniongoza kimya kimya na kunisaidia. Nilifikiri juu ya maneno ya Mungu: “Wakati wowote Shetani anampotosha mwanadamu ama anashughulika na madhara yasiyodhibitiwa, Mungu hasimami bila kazi, wala haweki kando ama kupuuza wale ambao amechagua. Yote ambayo Shetani anafanya ni wazi kabisa na yanaeleweka na Mungu. Haijalishi anachofanya Shetani, haijalishi mwenendo anaosababisha kuibuka, Mungu anajua yote ambayo Shetani anajaribu kufanya, na Mungu hawawachi wale ambao amechagua. Badala yake, bila kuvuta macho hata kidogo, kwa siri, kwa ukimya, Mungu anafanya yote yanayohitajika(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI). Nilipokuwa nikitafakari maneno haya nilihisi kuguswa sana. Nilikumbuka nilichokuwa nimepitia katika kipindi hicho cha wakati—wakati ambapo Shetani alimtumia mume wangu kunivuruga na kunitaabisha ili kunizuia kwenda mikutanoni, Mungu aliniruhusu nibaini hila za Shetani na kutoka katika uhasi wangu kupitia ushirika wa kina ndugu juu ya maneno ya Mungu; mume wangu alipoficha kitabu changu cha maneno ya Mungu na kujaribu kunizuia kumwamini Mungu, nilimtegemea na kumtumainia Mungu kwa kweli, na kisha nikashuhudia matendo ya kushangaza ya Mungu; mara nilipoamua kusimama na Mungu na nikawa tayari kuhatarisha kila kitu ili kumfuata Mungu, Shetani aliaibishwa na akajiondoa. Kupitia uzoefu wangu niliona kwamba kweli Mungu yuko upande wangu, na kwamba Alinipangia vitu kulingana na kimo changu. Mungu hakunipa mzigo ambao sikuweza kuubeba. Nilifikiria jinsi ambavyo hapo zamani, kabla ya kumpa Mungu moyo wangu kwa kweli, nilijishughulisha kila wakati na upendo wa mwili, nilitegemea njia za binadamu kuvumilia shida, na sikuthubutu kumuacha Shetani. Kama matokeo, Shetani alitumia hali yangu ya udhaifu, akitumia fursa na kunishambulia mara kwa mara, akinitesa mpaka mwisho. Lakini nilipomtegemea Mungu kwa kweli na nikawa tayari kuhatarisha kila kitu, Mungu alinifungulia njia, na Shetani akaaibishwa kwa kushindwa, akiachwa bila kimbilio. Baada ya kupitia haya yote nilipata ufahamu wa kweli juu ya uweza na ukuu wa Mungu, na vile vile tabia yangu ya uasi. Imani yangu na utiifu kwa Mungu vilikua, nilipata utambuzi juu ya ujanja wa Shetani, na nikaona asili mbaya na ya kustahili dharau ya Shetani. Chuki ya kweli kwa Shetani iliibuka ndani yangu. Ni kwa msaada wa mwongozo na mwangaza wa Mungu kwamba niliweza kuelewa yote haya. Namshukuru Mungu kwa dahti!

Nilipata mavuno mazuri kutoka kwa yale niliyoyapitia katika kipindi hicho cha muda. Wakati huo nilipitia udhaifu na uhasi, lakini mwongozo wa maneno ya Mungu na msaada na muawana wa dada zangu ulinipa imani ya kushinda majaribu na mashambulio ya Shetani, na kuendelea hadi leo. Nimeona upendo wa Mungu kupitia uzoefu wangu wa vitendo, na kwamba Mungu amekuwa akiniongoza na hajawahi kuondoka upande wangu hadi mwisho wa kila kitu. Tunapompa Mungu mioyo yetu, kumtegemea Mungu, na kumtumainia Mungu kwa kweli, tunaweza kuona matendo Yake ya kushangaza na Kuibuka kutoka kwa mateso yetu. Kuanzia leo hii na kuendelea, natamani tu kupitia kazi zaidi ya Mungu na kutafuta ufahamu wa kweli kumhusu Mungu!

Iliyotangulia: 15. Kupitia Kuelewa Siri ya Majina ya Mungu, Naenda Sambamba na Nyayo za Mwanakondoo

Inayofuata: 17. Kupenyeza Mzunguko Uliokazwa wa Shetani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

40. Kuja Nyumbani

Na Muyi, Korea ya Kusini“Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp